Jumanne, 28 Oktoba 2014

Kakajifanya Kapaka Kumbe Ni Chui


Nilipokea msichana mzuri sana wa kazi hausigeli ambaye nilimpata kupitia rafiki yangu, Huyu rafiki yangu alikuwa na uhitaji wa hausigeli kwa siku nyingio kwa hiyo alitumia watu mbalimbali ili kupata hausigeli, wakati mmoja majibu yalipokuja alipata mahausigeli watatu, kwa kuwa alijua kuwa na mimi ninahitaji alinipa na mimi mmoja kati ya hao

Binti huyu alikuwa anatokea Tanga wilayani Handeni, Alikuwa anataja vijiji tofauti tofauti kila akiulizwa kijiji anachotokea, mara Kwedizinga, kwediboma, kwedibangala, kwedibago, kwedikwazu n.k Hilo halikutusumbua kwani kuna watu wengine ni waongo mpaka wanajidanganya wenyewe.

Alianza kazi juni mwaka 2004, na hakuwa anajua kupika vyakula vingi, lakini nilijitahidi kumfundisha, pamoja na maswala ya chooni matumizi ya friji na jiko la umeme kwani kwake vilikuwa vitu vipya nilimfundisha vyote.

Kumbe mwenzangu alikuwa anajua kila kitu hadi kucheza na intaneti kwa nini sasa akaja kufanya kazi za uhausigeli hapo ndipo penye habari  Msichana huyu ambaye kweli kwa umbo alikuwa mzuri kumbe kazi yake ilikuwa ni kuajiriwa kwenye nyumba ambazo anaziona ni alihamdulilah kiuchumi, halafu baada ya muda  anaanza kuwatongoza baba wenye nyumba , tulikaa naye mwezi mmoja  na mume wangu akaniambia hapa hauna mtoto wa kazi, Awali sikumuelewa alikuwa anamaanisha nini kumbe binti huyu alishaanza kumuwangia, baadaye tulikuja kuambiwa kwamba binti huyu akimtafuta mwanaume akishindwa  huzua visa  vikubwa, alipoona mume  wangu ana msimamo  alianza visa, siku moja aliniambia kuwa angependa kuondoka kwa sababu hakuja hapo kuvunja ndoa  yangu, nilipomuuliza ana maana gani aliniambia mama wewe ni mtu mzima najua unaelewa, vitu vingine ni aibu  hata kuvisema, kwa kweli niliumia sana , Nilimwambia avumilie kidogo, Mume wangu alipokuja nilimvaa, Nilipomvaa kwamba kamtongoza hausigeli mume wangu alicheka na kusema yaani huyo naye ni wa kutongozwa?

Kama ameshindwa mbinu zake sasa ndo anataka kutuvunjia ndoa, nitamsweka ndani mwambie’Mume wangu aliniambia lakini hakunishawishi, vya kutosha, Hatimaye mume wangu aliniambia visa ambavyo huyu binti alishawahi kumfanyia ikiwemo kumfuata chumbani na kumfunulia nguo akijidai eti ameumwa na nge kwenye mapaja ili eti mume wangu ajaribu kumtoa mwiba wa nge huyo, aidha wakati mwingine alijaribu kumshika mabega  wakati mume wangu alipoingia jikoni, aidha mara nyingi alikuwa akimkalia vibaya na kumkonyeza kila wakati
Ilibidi nimfungishe virago siku hiyo hiyo, Kesho yake nilimfuata Yule rafiki yangu  na kuulizia kwa undani kuhusu binti Yule, akasema ilikuwa leo nikuulize habari za huyo binti  maana nimepata habari zake juzi tu  hadi nikashindwa kuamini nikasema nikuulize leo ili ufanye uamuzi nilibaki nimeduwaa Niliambiwa binti huyo alishavunja ndoa tatu za watu hapa dar  katika moja ya hizo alishaolewa yeye  badala ya mama mwenye nyumba  na akamfilisi kabisa mwanaume Yule na kumwacha kwa hiyo ndoa yangu ilikuwa iwe ya nne kufisadiwa  “lo kumbe kalijifanya kapaka kumbe ni chui”

Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni