Swali lenyewe lilikuwa namna
hii
“Kwa nini arobaini?
Mtoto akizaliwa akilazwa anatolewa nje baada ya siku 40, mtu akifa
siku ya arobaini anafanyiwa ibada, waswahili wana usemi za mwizi 40, Waisrael
walikaa nyikani kwa muda wa miaka 40, Yesu alifunga siku 40, pasaka
huadhimishwa baada ya siku 40 za mfungo,Kipindi cha Nuhu mvua ilivyesha kwa
siku 40 je Hii arobaini ina maana gani naomba nisaidie”
Maana ya namba 40.
Ni muhimu kufahamu kuwa kwanza nilipoulizwa swali hili sikufanya
Haraka kutaka kutoa majibu ya papo kwa papo kwani sikutaka kutoa majibu
nisiyoyafanyia utafiti, Ilinigharimu Muda kwani binafsi sikuwahi kujiuliza
swali kama hilo na ingawa mimi ni muhubiri sikuwahi na sipendi sana kuhubiri
kuhusu Namba au vitu ambavyo vinaweza kuwachanganya akili waamini wetu hata
hivyo swali hili limenipa uzoefu mkubwa ambao sasa naweza kushirikiana na kila
mtu mwenye mapenzi mema anayependa kujifunza.
Namba 40 Katika Biblia ni alama yenye kumaanisha kipindi cha wakati
mgumu! Wakati wa maumivu, kukata tama ya maisha, masumbufu na changamoto
mbalimbali tunazokutana nazo tunapoishi ulimwenguni, Wakati wa Nabii Nuhu mvua
ilinyesha kwa siku “40” haukuwa wakati mwepesi ulikuwa wakati wa Misiba mikubwa
kwani Ingawa Nuhu alikuwa ameokolewa na familia yake tu lakini ni ukweli
uliowazi kuwa alikuwa na huzuni kubwa kufiwa na majirani zake ndugu na jamaa
ambao huenda hawakutaka kusikiliza maonyo hivyo kimsingi ulikuwa wakati wa
majaribu, Wana wa Israel nao walipita katika jangwa refu kubwa lenye kutisha na
kukatisha tama kwani kadiri walivyokuwa wakisonga mbele matumaini ya uhai
yalikuwa yakipotea kabisa, ulikuwa ni wakati mgumu kiasi ambacho hata uhuru wa
kutoka Misri ulionekana kana kwamba hauna maana waliteseka na kupoteza
matumaini jangwa hili refu kutoka Misri hata kufika Israel liliwagharibu safari
ya mapito ya miaka “40”,Naye Masihi Mkuu Yesu Kristo wa Nazareth kabla ya
kuanza kuwahudumia watu aliongozwa na Roho wa Mungu kuelekea nyikani ili
kujaribiwa akiwa amefunga kwa siku “40” hata baada ya Pasaka kuna sikukuu
iitwayo Pentekoste huazimishwa siku 40 tangu pasaka wayahudi huadhimisha
sikukuu hiyo kwa kukaa katika vibada wakikumbuka jinsi wazee wao walivyoteseka
jangwani kwa miaka 40, Naye Yesu alipaa mbinguni baada ya kuwa amewatokea
wanafunzi wake kwa siku 40
Kwa ujumla namba 40 imekuwa sasa ikitumika kwa maeneo mbalimbali
duniani na inakubalika kama namba maalumu na wakati wote huo ikimaanisha
kipindi Fulani kigumu cha kupitia majaribu hata kama kipindi hicho sio lazima
kihesabike kama siku 40 lakini ni kipindi Fulani cha mapito na changamoto
wakati mwingine kisichohesabika au kinachohesabu kabisa siku 40 zenyewe.
Namba 40 ni uzao wa namba 5 na 8 na mara nyingi hulenga kwenye tendo
la kuhitaji Neema na kuelekea kwenye kufanywa upya, baada ya kutoka katika
mapito namba nyingine ni 4 na 10 na ni dhahiri kabisa kuwa 4 na 8 zinawakilisha
pande kuu za dunia.
Kibiblia Waisrael walipita kwenye Jangwa la kutisha na kukatisha tama
kwa miaka 40 Kumbukumbu 8;2-5, Zaburi 95: 10 Matendo 13;18,
Nabii Musa aliishi miaka 120 na Miaka 40 katika nyumba ya farao
akiyafurahia maisha ya anasa na miaka 40 Jangwani huko Midiani akiishi katika
taabu za dunia na miaka 40 akiishi kama Kiongozi wa Israel kuwapeleka Kanaani
40 mpaka alipofariki mlimani kabla ya kufika Kanaani.
Baada ya kusulubiwa Kwa masihi ilipita miaka 40 tu na mji wa
Yerusalemu uliharibiwa hivyo namba 40 bado ni moja ya namba muhimu za kibiblia
40 pia humaanisha kipindi cha mafanikio na ukombozi au raha kupumzika
mfano waamuzi walipowaokoa Waisrael kulipita wakati wa utulivu wa miaka 40- 40
hivi
Mfano
·
Chini ya Utawala wa Othiniel mwamuzi alitawala
miaka 40 Waamuzi 3;11
·
Chini ya Utawala wa Baraka mwamuzi alitawala miaka 40 Waamuzi 5;31
·
Chini ya Utawala wa Gideon mwamuzi alitawala
miaka 40 Waamuzi 8;28
·
Wakati wa Tawala zenye mafanikio pia viongozi
wengi walitawala kwa miaka 40
Mfano
- Chini ya Utawala wa Daudi, alitawala kwa miaka 40 2Samuel 5:4,
- Chini ya Utawala wa Suleman, 1Wafalme 11:42,
- Chini ya Utawala wa Yeroboam II. 2Wafalme 12:17,18, 13:3,5,7,22,25, 14:12-14,23,28,
- Chini ya Utawala wa Yehoash, 2Wafalme 12:1,
- Chini ya utawala wa Yoash 2Nyakati 24:1.
Namba 40 Kibiblia pia ilimaanisha pia
vipindi vya kunyenyekea na kuonelewa au kutokuwa na uhuru
·
Mifano ya kibiblia ni pamoja na
·
Wakati wa utawala wa wafilisti Isrel
walionewa miaka 40 Waamuzi 13;1.
·
Wakati wa utawala wa Eli wafilisti
waliwaonea sana Israel miaka 40 1Samuel; 4;18
·
Wakati wa utawala wa Sauli wafilisti
waliendelea kuwasumbua Israel miaka 40 Matendo 13 :21.
Namba 40 pia humaanisha nyakati za kusubiri au subira
·
Musa alisubiri mpaka alipokuwa mtu
mzima miaka 40 kuwaokoa watu wake Matendo 7;23
·
Pia alipaswa kusubiri wakati wa Mungu
kwa miaka 40kuwaokoa watu wake Matendo 7;30
Katika Biblia kuna Maswala yapatayo nane “8” hivi
yanayozungumzia umuhimu wa siku 40
1.
Siku 40 Musa alikuwa mlimani akipokea
sheria ya Mungu kwa watu wake Kutoka 24;18
2.
Suku 40 Musa alikuwa mlimani akiwaombea
watu wake baada ya kuwakuta wakiabudu sanamu ya ndama wa dhahabu Kumbu 9;18,25
3.
Wapelelezi walitumia siku 40
wakiwakilisha miaka 40 Hesabu 13;26,14;34.
4.
Kwa siku 40 Nabii Eliya alikuwa mlima
Horeb 1Wafalme 19;8
5.
Kwa siku 40 mji wa Ninawi ulipaswa
kutubu kwa mahubiri ya Yona kabla ya hukumu Yona 3;4
6.
Kwa siku 40 Ezekiel alilalia upande wa
kulia akitabiri Miaka 40 ya taabu ya Yuda Ezekiel 4;6
7.
Kwa siku 40 Yesu alijaribiwa na Ibilisi
akiwa amefunga Mathayo 4;2
8.
Kwa siku 40 baada ya kufufuka Yesu
aliwatokea wanafunzi wake akizungumzia maswala ya Ufalme wa Mungu Matendo 1;2.
Kwa ujumla Namba 40 imetajwa katika Biblia mara 146 na mara
zote hizo imeunganishwa na maswala ya
Majaribu, mapito na muda Fulani usiofahamika wa kipindi cha mapito au mateso.
Ni jinsi gani namba 40 inahusiana na Majaribu na wakati
mgumu?
·
Yesu alijaribiwa na Ibilisi siku 40
mchana na Usiku
·
Yesu aliwatokea wanafunzi wake kwa siku
40 baada ya kusulubiwa kufa na kufufuka
·
Baada ya miaka 40 tangu kusulubiwa kwa
Yesu Yerusalem Uliharibiwa
·
Musa aliishi miaka 40 Misri, 40
Jangwani na 40 Jagwani akiongoza wana Israel
·
Musa alikaa mlimani siku 40 usiku na
mchana akipokea sheria
·
Wapelelezi waliipaleleza kanaani kwa
siku 40
·
Eliya alitumia siku 40 katika mlima
Herob
·
Yona alihubiri kuhusu Hukumu ya Ninawi
kuwa ni baada ya siku 40
·
Kulingana na tamaduni au masimulizi ya
kale Adamu na Hawa baada ya kufanya dhambi walifunga na kujuta kwa siku 40 na
hivyo kuna uwezekano swala la 40 lilianza zamani sana na baba yetu Adam.
Kwa msingi huo kumbe basi 40 humaanisha
Subira, Uvumilivu, mapito, mateso mitihani, maombolezo, hukumu na furaha au
kustarehe
·
Mtoto anapozaliwa kunakuwa na
mchanganyiko wa Furaha na Huzuni na uvumilivu
a.
Mama anakuwa na muda wa kurejesha Afya
yake baada ya uchungu mzito wa kujifungua, huangaliwa kwa ukaribu ili yeye na
mtoto waweze kupata nguvu za kutosha kurejea katika hali ya kawaida, wakati Huu
Mume au baba anapaswa kuwa katika wakati wa Subira hawezi kumgusa mama kwani
afya haijatengemaa kwahiyo mara baada ya
mwanamke kujifungua mwanamume mwenye mke huyo hupaswa kuwa na subira na endapo
atakosa subira wengi huharibikiwa na kutoka nje ya ndoa zao hivyo nyumba nzima
huonja joto la 40
b.
Mtu anapofariki kwa kawaida watu
huingia katika maombolezo na wakati wa huzuni huu pia ni wakati wa subira
kutokana na kila mtu anapofariki huwa amefariki mtu nwa pekee na wa muhimu,
maombolezo yanapaswa kuwa siku 40, hata hivyo watu wengi sana humaliza msiba
ndani ya siku tatu, lakini siku 37 ni muhimu na zinahitaji subira na mwenedno
wenye kuheshimu kuondokewa na mtu muhimu, ndani ya siku hizo chache kama
utaonekana mwenye tabia za ajabu inaweza kuwa tafasiri mbaya katika uhusiano
wako na kifo cha marehemu kwahiyo watu huhesabu 40 tangu kuzikwa au kufa kwa
marehemu na huhitiomisha kwa Ibada za shukurani na hapo sasa familia inaweza
kuanza kufurahi na kusahau yaliyotokea
c.
Za mwizi 40 “Ni usemi wenye kumaanisha
kuna wakati wa Hukumu kwa matukio yoyote yasiyofaa kwa kuwa namba 40
inauhusiano na swala la hukumu “Ninawi baada ya siku 40 utaangamizwa!” hiyo ni
hukumu mtu mwenye tabia ya wizi iko siku Mungu atamuhukumu kwa wizi huo Mungu
ana namna yake anavyoweza kuhesabu na hatimaye kufichua au kuweka peupe maswala
yote yafanyikayo kwa siri hapa duniani kwa hiyo za mwizi arobaini sio lazima
uwe ni muda unaohesabika lakini ni siku moja ya hukumu kwa mwizhi au mtu mwenye
tabia yoyote isiyofaa kimaadili.Mungu aliwahukumu wenye kumuasi kwa kuleta mvua
wakati wa Nuhu mvua na chemichemi zilifunguka kuwahukumu watu waovu hii nayo ni
40 iko siku Mungu atahukumu uovu.
d.
Kufunga siku 40 kwa Yesu na Musa pia au
Eliya ni alama ya Unyenyekevu na kumtafuta Mungu kwa neema na Rehema zake ni
kukubali kujitesa ili kuruhusu huruma za Mungu kutujilia na ndio maana wakristo
wa zamani pia walikuwa wakifunga siku 40 Kwaresma ili kuutafuta uso wa Mungu na
kuwahudumia watu
Ni matumaini yangu
kuwa Utakuwa umafaidika na mda hii kwa maswali maoni au ushauri tafadhali acha
mchangowako chini ya mada Hii na Mungu awabariki wenu mjoli wa Bwana
Kwa mawasiliano maoni au maswali:-
Rev, Innocent Kamote.
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hakima
0718990796
0784394550
Nimelipokea neno katika wakati sahihi
JibuFutaThat's great be blessed
JibuFutaNeno limenibariki mno. Asante sana Mtumishi wa Bwana Yesu. Barikiwa mtu wa Mungu
JibuFutaAsante nimejibiwa
JibuFutaAsante sana mtumishi wa MUNGU, hakika nimeelewa vema.
JibuFutaNimebarikiwa kwa kujua maana ya namba 40
JibuFutaNimebarikiwa kwa kujua maana ya namba 40
JibuFutaKwanini Sikh za mwizi ni 40
JibuFuta🙏🙏🙏 ahsante kwa maarifa haya
JibuFutaThank you so much
JibuFutaAhsant kwa ufafanuz
JibuFutaAhsante sana kwa maelezo hayo Mungu akuzidishie neema na baraka.Nimebarikiwa na naendelea kujifunza Mtumishi wa Bwana.
JibuFutaMungu wa mbinguni akubariki nimepata somo
JibuFutaAsante kwa majibu mazuri
JibuFutaAsante eeee
JibuFutaAsante kwakufanya utafiti wa kina
JibuFutaAsnte sana kwa uchambuzi makini kweli nimepata marefu na mapana ya siku 40. Mungu akibariki
JibuFutaNaomba kufahamu namba therathini na tatu inawakilisha nini milnisaidie
JibuFuta