Jumatatu, 30 Machi 2015

Ufahamu Kuhusu Yesu Kristo (Christology)


UTANGULIZI: 
Katika moja ya kazi zilizongumu kitheolojia ni kumwelezea kibinafsi Yesu Kristo huu ni mzigo mkubwa mno, Wasomo wengi sana wamekubali kwa haraka kuwa kuna mipaka ya kibinadamu inayotosheleza kabisa kuwafanya wasimuelezee Kristo katika namna inayofaa na inapofikia hatua ya kutaka kumweleza inakuwa ni Shughuli ngumu, Hasa pale inapokupasa kumuelezea mtu huyu mwenye utukufu mkubwa unaozidi kawaida zaidi sana katika uhusiano wake wa kazi nzima ya ukombozi wa wanadamu tuliokuwa tumepotea,Kwa msingi huo Basi ingawaje hatuwezi kuelezea au kujibu kila kitu kumhusu Yesu Kristo lakini kujifunza kuhusu Yesu  Kristo kazi zake ndio msingi wa Mambo yote ya kitheolojia na ndio kiini cha Biblia nzima kutoka Mwanzo hata Ufunuo, Kwa msingi huo kusudi la somo hili ni kukuhabarisha swala zima kuhusu Yesu Kristo kama anavyelezwa Kibiblia na kujaribu kufafanua maeneo magumu ili kuyaelezea upate kumfahamu Bwana Yesu katika upana wake.

Vitabu vingi sana vimeandikwa kumuhusu Bwana Yesu lakini kozi hii au somo hili limeandaliwa ili kukupa wewe kuelewa ukweli wa kitheolojia kumuhusu Yesu ili awe rafiki wa karibu sana unayeweza kufahamiana naye Vizuri na utaona jinsi Mungu alivyofunua Neno lake la ukombozi wa mwanadamu na kulitimiza kupitia Yesu Kristo maswala ambayo yatakusaidia si tu kumuelewa bali pia kumueleza Vema kwa wengine

Kuzaliwa kwake kunaadhimishwa dunia nzima na kifo chake na habari za kufufguka kwake zinzsimuliwa na kuutikisa ulimwengu mzima na kila anga Huyu Ni nani? Swali kama hili litakuwa linajaribiwa kujibiwa katika somo hili ,Mapema katika maisha yake Bwana alipokuwa anakaribia mwisho wa Maisha ya kidunia aliuliza swali kama Hili Watu husema kuwa mwana wa Adamu ni nani? Wanafunzi walijaribu kutoa maoni mbalimbali kumhusu, wengine walisema Huyo ni Eliya, au Yohana mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu au moja ya Manabii wa kale na kadhalika swali liligeuka kwa wanafunzi wenyewe Je ninyi nanyi mwaninena mimi kama nani? Ni Petro pekee aliweza kujibu Kuwa “wewe ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai”na hata hivyo Yesu alimwambia Petro kuwa Damu na nyama havikukufunulia hili Bali baba yangu aliye mbinguni, Kumbe tunawezakuwa tumeokolewa,tumemtumikia Mungu na kutembea naye Lakini tukiwa bado hatuja mfahamu, ndio hii inaonekana wazi pale wanafunzi wengine wanapokuwa kimya na kushindwa kujibu swali lile na Hata huyu aliyejibu alijibu kwa msaada wa Mungu hili lina tupa picha ya kwamba Kujibu kuwa Yesu Kristo ni nani sio swala dogo na kumbe linahitaji Mwangaza maalumu kutoka kwa Mungu. Swali hili linabakia kwetu leo na wanadamu wengi wanajaribu kulijibu Lakini jibu halisi tunalipata kutoka katika Biblia hususani agano jipya ambalo limeandikwa na watu waliomjua Vema na kwa msaada wa Roho Mtakatifu walihesabu mambo yote kuwa kama mavi ili kumtumikia Kristo hawa walimuelewa Vema ni imani yangu kuwa Bwana atampa neema kila mmoja wetu kuweza kujua Mungu na Kumjua Yesu Kristo kupitia kozi hii sala hii ni Muhimu kabla ya kuendelea
“Eee Nafsi yangu umfahamu Mungu wangu,Eee ngome yangu uufunulie moyo wangu ee Roho wa Mungu wangu Uufunulie moyo wangu kwa damu yangu na kwa akili zangu siwezi kumjua mwokozi wangu, lakini kwa kiu yangu Mungu ukajifunue kwangu nimjue mwana wa Mungu wangu Yesu Kristo mwokozi wangu wewe ndiwe kimbilio langu sikuzote maishani mwangu jufunue moyoni mwangu ”

UFAHAMU KUHUSU KRISTO (CHRISTOLOGY)
Neno Christology lina asili ya Kiyunani na ni muunganiko wa Maneno mawili Christ ambalo maana Yake Kristo na o logy au logos  ambalo maana yake ni Elimu au ufahamu kuhusu, kwa msingi huo basi Christology maana yeke Ni Elimu kuhusu Kristo au ufahamu kuhusu Kristo katika somo hili tunajifunza kwa undani kile ambacho Biblia inakifundisha kuhusu Yesu Kristo kwa msingi huo tunajifunza  kwa undani na kwa mpangilio kuhusu utu wa Yesu Kristo Milele wakati uliopita ulioko na kazi zake za wakati ujao somo hili litakusaidia wewe kama Mwanafunzi wa Biblia kuweza kukanusha dhana zozote zisizo sahii kuhusu Kristo zitolewazo na watu wenye kuipinga imani yetu , ndani ya somo kuna mambo mengi kuhusu Yesu na tutayajifunza kwa makini ili kupata Ufunuo wa kimaandiko wa kutosha kuhusu Kristo na kuitetea imani,tutamuona Yesu katika Agano la kale na kumfahamu anavyozungumzwa katika agano jipya lakini kusudi la somo hasa ni Kujua kuwa Maandiko yanasema nini kuhusu Yesu Kristo somo hili ni la kitheolojia zaidi Theology ni Elimu kuhusu Mungu Theo ni Mungu o logy au logos ni Elimu au ufahamu kwa msingi huo kwa kuwa Yesu ni Mungu si kitu rahisi sana kueleweka kirahisi inahitajika neema maalumu ya kiungu ili kujua somo hili vizuri na ni maombi yangu kuwa Mungu atatusaidia kumfahamu Bwana vema.
Somo hili ni tofauti na somo la Maisha ya Yesu Kristo ambalo huzungumzia Yesu na maisha yake na kazi zake kama zinavopatikana katika injili, ambapo utajifunza mafundisho yake mifano n.k somo hili la ufahamu kuhusu Kristo lina lengo la kumjua Kristo mwenyewe kuliko kuelezea alifanya nini? Kwa msingi huo tofauti ya Masomo haya tunaweza kuiweka hivi
Life of Christ (Maisha ya Kristo) tunajibiwa kuwa Yesu Kristo alifanya nini?
Christology (Ufahamu kuhusu Kristo) tunajibiwa kuwa Yesu Kristo ni nani?
Mwanafunzi atakapomaliza somo hili angalau awe na uwezo wa kufanya mambo ya msingi na ya muhimu yafuatayo;-
1.      Kujua kwa usahii na kufundisha  kwa usahii Yesu Kristo ni nani na kupinga dhana potofu
2.      Kujua mawazo ya wasomi mabimbali na michango yao waliyochangia kuhusu Yesu Kristo
3.      Kuweka uwiano wa ufahamu kuhusu Kristo na Shughuli za wokovu na utatu wa Mungu katika imani yetu na mafundisho ya kibiblia
4.      Kutambua na kufundisha kwa ujasiri maswala mengi kumhusu Yesu Kristo na kazi zake kuanzia agano la kale na mpaka jipya
5.      Kujua ukweli mbalimbali kuhusu Kristo, kama Kuzaliwa kwake na Bikira na faida zake, Kuteseka kufa na kufufuka na uhusiano wake na mpango wa Mungu
6.      Kufundisha ukweli wa kibiblia kuhusu uungu wa Yesu na ubinadamu wake kupitia incarnation yaani tendo la Mungu kuutwaa mwili wa kibinadamu
7.      Kufahamu vema na kwa undani na kufurahia tendo la Kristo kuutwaa mwili na kuwako duniani na faida zilizopatikana kwa matendo yake kufa na kufufuka kwake
8.      Kutumia mafundisho sahii na mahubiri sahii tunapomzungumzia Kristo katika huduma zetu
9.      Kufundisha na kuhubiri kwa usahii maana ya kurudi kwa Yesu mara ya pili na huduma yake ya baadaye ya kimbinguni

MITAZAMO MBALIMBALI KUHUSU UFAHAMU KUHUSU KRISTO (CHRISTOLOGY)

Swala kuhusu Yesu kristo lilichanganya wasomo wengi sana katika ulimwengu wa kitheolojia na hivyo iko mitazamo mbalimbali ya kimafundisho kuhusu Yesu Kristo ambayo ni muhimu kuipitia pia kabla ya kujifunza kuwa Yesu Kristo ni nani jamaa hawa waliokuwako enzi hizo waliamini hivi kuhusu Yesu
*      Ebonites Waebonait
Hili lilikuwa kundi la wakristo wenye msimamo mkali wa kiyahudi (Extreme Judaizing Christianity) hawa walifundisha kuwa ni mwana wa Mariamu na Yusufu na aliitimiza Sheria ya Musa kwa ukamilifu kiasi kwamba Mungu alimchagua awe masihi na walikataa kabisa kuwa yeye ni Mungu, hivyo pamoja na kukubali wazi kuwa alizaliwa na Bikira waliona kuamini katika uungu wa Yesu ni kwenda kinyume kabisa na imani ya kuwa Mungu ni mmoja tu (monotheism)

*      Gnosticism Wanostiki

Hawa waliamini kuwa kila kitu pamoja na mwili ni kiovu tu isipokuwa roho na kwa msingi huo basi Mungu hawezi kukaa katika mwili na hivyo wao hudai kuwa Kristo alikuja juu ya mwili wa Yesu wakati wa Ubatizo na kuondoka Muda Mfupi kabla ya Yesu kufia msalabani kwa msingi huo imani hii ilienea sana wakati wa Nyakati za kanisa la kwanza na hivyo mitume walipambana na mafundisho ya aina hii katika Wakolosai,wathesalonike na 1Yohana  na ufunuo vinagusia Kuweko kwa mafundisho hayo 1Yohana 4;1-3 Wapenzi, msiamini kila roho,bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.

*      Arians Waariyani

Jamii hii ilitokana na mwana theolojia maarufu wa karne ya nne aliyeitwa Arius wa Alexandria huko Misri Yeye alikuja na hoja ya kuwa ingawa Yesu anaitwa Mungu au amepewa heshima ya kuitwa Mungu  Hakuwa Mungu kwa asili wala hakuwa Mungu tangu milele bali alikuwa mzaliwa wa kwanza aliumbwa kabla ya vitu vingine Ufunuo 3;14c “… Mwanzo wa kuumba kwa Mungu” kwa hivyo yeye alikuwa wa kwanza kuumbwa na alishiriki kazi ya uumbaji kwa hivyo Kristo hakuwa Mungu kamili wala mwanadamu kamili Marko 13;32, Yohana 5;19,14;28 na 1Korotho 15;28 mistari hiyo aliitumia kuunga mkono hoja zake imani hii ilipingwa vikali wakati wa baraza la Nikea lililofanyika mwaka 325 na kuitangaza imani hii kuwa potofu

*      Nestorians Wanestori

Mwana theolojia huyu alikataa dhana ya kuwa na asili mbili na kudai kuwa haiwezekani uungu na ubinadamu kukaa katika hali moja inawezekana je mtu akawa Mungu na huku akawa mwanadamu? Dhana hii haikuingia kichwani mwake

*      Apollinarians Waapolonari

Mafundisho ya huyu bwana yalikuwa na lengo la kuharibu kabisa ubinadamu wa Yesu Kristo kwa kweli Baraza la Constantinople lililofanyika mwaka 381 AD lilihukumu mawazo ya waapolonari na kuyatangaza kuwa ni mafundisho potofu
*      Eutychians Waeutiko
Jamaa hawa walipinga hali ya Kuweko kwa asili mbili za Yesu na kudai kuwa kulikuwa na asili moja tu na hivyo Yesu alikuwa Mungu tu na hata alipokuwa katika mwili, mwili wake ulikuwa Mungu dhana hii ilikuja kupingwa vikali na baraza la Chalcedon mwaka wa 451 na kulihukumu fundisho hilo kuwa ni potofu

*      Mawazo ya wa Orthodox 

Waorthodox maana yake wenye imani sahii hawa walifundisha kuwa Yesu Kristo ni mmoja bali ana namna mbili za asili Ni Binadamu kamili na ni Mungu kamili hii iliungwa mkono katika baraza la Chalcedon mwaka wa 451 AD wakiliwekea msimamo mkali hata leo
Mambo kama haya yanatupelekea sisi kuwa tayari kujifunza kwa makini habari kuhusu Yesu Kristo ili tuweze kuelewa vema kile ambacho Biblia inakisema kumhusu jambo hili litatusaidia kumjua vema Kristo na siri hii ya ajabu kumhusu

SURA YA KWANZA; KUWEKO KWA YESU KRISTO KABLA YA ULIMWENGU

Yesu Kristo ni nani?

Yesu Kristo ni muungano wa majina mawili Yesu Kristo. Jina Yesu ni jina lenye asili ya kiyunani ambalo kwa asili limetokana na jina la Kiebrania Yoshua ['Wv¢/hy“ , [~'vŸu/hy“, au WvyE,   ambalo maana yake Yahweh anaokoa, jina linalobebwa na moja ya Viongozi maarufu katika agano la kale Yoshua, hili lilikuwa jina la kawaida miongoni mwa majina ya kiebrania na nyakati za ulimwengu wa agano jipya  na ili kulitofautisha na majina hayo ya kawaida Jina YESU KRISTO lilitumika na wakati mwingine lilijumuishwa na eneo alilokulia Nazareth na ndio maana angalau katika mistari ya Mwanzo ya vitabu vya injili jina hili liliwekwa na ingawa hawarudii kila wakati ndani ya vitabu hivyo lakini kule kuliweka mwanzoni ilimaanisha kuwa ni Yesu yupi wanaye mzungu mzia Mathayo 1;1,Marko 1;1 na 9 kuonyesha kuwa wanamzungumzia Yesu Kristo wa Nazareth, Ingawaje si kila wakati watayaunganisha majina hayo yote sehemu nyingine jina Yesu pekee hutumika lakini katika msisitizo wa mistari ile ya msingi katika kitabu cha Matendo ya mitume wanalitumia jina hilo kwa kuchanganya
Katika Mathayo 1; 21 Uthamani wa jina la Yesu unaonekana kuwekewa wazi zaidi kwanza si jina ambalo lilichaguliwa na mwanadamu ni jina ambalo Mungu mwenyewe alimchagua lakini linaonekana linatoka katika mzizi uleule wa maswala ya wokovu “Maana yeye ndiye atakayewaokoa watu watu wake na dhambi zao” na ni baadaye baada ya kazi ya ukombozi wa Msalabani ndipo dhana ya jina hili ilifahamika wazi zaidi
Kwa habari ya jina linguine Kristo hili ni la muhimu kwani ndilo linalo mtofautisha Yesu na wanadamu wengine wanaotumia jina hilo. Kuna makristo wengi wa uongo lakini yuko Yesu Kristo mmoja tu wa kweli jina hili linawakilisha jina la kiebrania Masihi j'yvim;, ambalo maana yake ni mpakwa mafuta lakini limekuja kutumika zaidi kwa Mpakwa mafuta mmoja tu ambaye alikuja kwa ajili ya kuutimiza unabii katika agano jipya kwa msingi huo jina hili linapounganishwa Yesu Kristo ndipo tunapopata maswala mengi ya kitheolojia ya kujifunza kumuhusu Yesu Kristo, kwa hivyo hatupaswi kufikiri tu kuhusu Historia ya Yesu Kristo bali na kweli zinazobebwa na msingi katika jina hilo.

Asili ya Yesu Kristo
Swali letu bado linabaki palepale kuwa Yesu Kristo ni nani kumbuka kuwa hapo juu tulikuwa tunafafanua maana ya Jina Yesu Kristo lakini ili tumfahamu Bwana Yesu inatupasa kujua majina yake jinsi anavyojulikana na kutumika lakini lazima tujue asili yake

Kristo Yesu Kuweko kabla ya ulimwengu kuumbwa

     Yesu Kristo aliishi duniani takribani miaka 2000 hivi iliyopita lakini kwa asili alikuwako kabla ya ulimwengu kuwako kimsingi Yeye hakuwa mwanadamu wa kawaida au nabii tu au kama mtumishi yeyote wa Mungu  yeye ni zaidi ya kawaida  hivi leo Yesu Kristo anawafuasi wengi zaidi kuliko kiongozi yeyote duniani na hutajwa mara milioni kwa siku tu habari zake zimeandikwa katika Vitabu vingi vinavyoelezea Maisha au Matendo yake  kuliko mtu awaye yote duniani, amehubiriwa katika mamilioni ya jumbe amenukuliwa na Viongozi, wasomi, wasio wasomi, wanasayansi.wana historia na vyombo vingi vya habari kuliko mtu yeyote zaidi ya yote mafundisho yake Yamebadili maisha ya watu wengi kwa karne nyingi na jina lake limetumika kuponya na kufanya miujiza mingi zaidi na ni mwenye sifa nyingi zaidi kuliko mtu awaye yote duniani
Kwa msingi huo basi ni muhimu sana kujua habari zake kwa kina na mapana na marefu na kwa utafiti wa kibiblia au kitheolojia unaonyesha  maisha ya Kristo hayakuanzia duniani mara baada ya Kuzaliwa na Mariam bali inaonekana kuwa alikuwako katika ulimwengu wa roho kabla ya kudhihirika ulimwenguni humu na kujulikana na watu hata leo

·         Yohana 8;56-58   “…. Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona Abrahamu?’’ Yesu akawaambia, ‘‘Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko. Hii ni kauli ya Yesu Kristo mwenyewe akijitambulisha kuwa alikuwako kabla ya Ibrahimu jambo hili ni moja ya misingi inayoonyesha kuwa Kuzaliwa kwake haukuwa ndio Mwanzo wa maisha yake.
·         Yesu Kristo alikuwako Tangu milele, milele ni muda mrefu usio na Mwanzo wala mwisho, malaika,wanyama ,pepo na kadhalika ni viumbe tu  na viliumbwa na Mungu na havina sifa ya kuwako tangu milele mwenye sifa ya kuwako tangu milele ni Mungu peke yake, tunawezaje kulijua hili Biblia inatufundisha katika Yohana 1;1,14 “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 14Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.Ushahidi huu mwingine wa kimaandiko unathibitisha ya kuwa Yesu alikuwako tangu milele
·          Wakolosai 1;15-18 Kristo anaelezwa kuwa amekuwako kabla ya vitu vyote kuwako ni wazi kuwa si tu kuwa Yesu aliumba vitu vyote na kuwa kila kilichoumbwa kiliumbwa kwa ajili yake lakini amekuwako kabla ya vitu vyote naye ndiye Mwanzo ni wazi tu kwamba kuja kwake duniani na kuutwaa mwili kulikuwa kwa ajili ya kusudi linguine la ukombozi wa mwanadamu lakini Yesu  alikuwa ana asili ya Uungu
·         Wafilipi 2;5-8Iuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu. Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu. Naye akiwa na umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! Andiko hili linasaidia kuweka wazi habari za Kristo kwamba yeye alikuwa sana na Mungu na alikuja duniani katika mfumo wa Kuzaliwa tu na alijinyenyekeza sana
·         Hakuna andiko lolote linalothibitisha kuwa Yesu ni kiumbe au aliumbwa hapana Kwa kweli hana Mwanzo wa siku zake wala mwisho wa siku zake Waebrania 7;3Hana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, kama Mwana wa Mungu, yeye adumu kuhani milele.na Waebrania 13;8 inasema Yesu Kristo ni Yeye yule jana, leo na hata milele. Unaweza kuona pia Ufunuo 1;8,17-18 maandiko yanathibitisha kuwa Yesu ni wa milele
·         Penginepo inaweza kuonekana kana kwamba labda waandishi tunataka kumfagilia Yesu na kumtukuza sna kuliko anavyopaswa kutukuzwa na hivyo tunampa sifa hii lakini Yesu mwenyewe anasema Maneno haya katika Yohana 17; 4-5 “Mimi nimekutukuza Duniani hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye, Na sasa Baba unitukuze mimi pamoja nawe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Unaona!  hii ni wazi katika Maandiko kuwa Yesu alikuwako kabla ya ulimwengu kuwako alikuwako tangu milele
·         Nabii Mika aliyeishi miaka 750 hivi kabla ya Kristo ni moja ya Manabii waliotabiri mji atakaozaliwa masihi kuwa ni Bethelehemu lakini pamoja na hayo anaonyesha kuwa mtawala huyo ana asili ya milele Mika 5;2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.’’
·         Yohana mbatizaji amabaye ni Nabii aliyetangulia kumuelezea Kristo au kumtambulisha Kristo kwa dunia alieleza kuwa asili ya Kristo sio Duniani ni juu Yohana 3;31 “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia, naye anena  mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni, yu juu ya yote.” Sio tu yuko juu ya Yote lakini ametoka mbinguni.

Majina aliyopewa Yesu Kristo alipokuwa Duniani

Ni muhimu kufahamu kuwa Swali yesu Kristo ni nani halitoshi kujibiwa tu na kwamba alikuwako kabla ya ulimwengu kuwako kwani hii inaweza kuwachanganya wanadamu lakini namna watu walivyomueleza na majina anavyopewa au aliyopewa akiwa duniani na heshima anazopewa katika Maandiko ni msaada mkubwa katika kulijibu swali Yesu ni nani?

1.      Yesu anaitwa mwana wa Mungu
Wako watu ambao wanakubali kuwa Yesu ni moja ya mitume wa Mungu lakini wanakataa kuwa si mwana wa Mungu, Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu ni mtu mkuu zaidi aliyepata kuishi lakini wanakataa kuwa yeye ni Mungu huku wakiamini kuwa amepewa heshima ya kuwa juu ya malaika na kuwa chini au msaidizi wa Mungu lakini sio Mungu. Kila mtu anaweza kuwa na jibu  lake kuhusu Yesu lakini Biblia pekee inayo majibu sahii kuwa Yesu ni nani nasi tutaiangalia Biblia kuwa inatuambia nini?
 Yesu Kristo kama mwana wa Mungu Neno mwana wa linamaanisha asili kama ni Mwana damu maana yake ni aliyezaliwa na mwanadamu na Mwana wa Mungu maana yake aliyezaliwa kutokana na Mungu, Yesu anapoitwa mwana wa Mungu maana yake ana asili ya Mungu wala yeye haitwi mwana wa Mungu katika dhana ile ya mwana wa Mungu kama inayotajwa kwa malaikaAyubu 2;1 ,Adamu.Israel na wanadamu wa kawaida Yeye anatajwa kama mwana wa Mungu katika namna ya pekee sana
·         Malaika huitwa wana wa Mungu (Created sons of God) Ayubu 1,;6,2;1-3,8;7,Zaburi 89;7,Daniel3;25) wana wa mungu kwa kuumbwa
·         Adamu aliitwa mwana wa Mungu Luka 3;38 (Created son of God) kwa kuumbwa
·         Wakristo huitwa wana wa Mungu Yohana 1;12,Warumi 3;14,19,9;26 (adopted sons of God)
·         Wana wa Israel wanaoitwa wana wa Mungu (Elected sons of God) kwa kuchaguliwa
·         Yesu anaitwa mwana Pekee wa Mungu Yohana 1;1, 3;16,Matahyo3;17,17;5 (Monogyny means of the same nature) yaani wa asili moja na Mungu kwa msingi huo Yesu alipojitambulisha kwa kumuita Mungu baba yake wayahudi walielewa Yesu alikuwa akimaanisha ana asili moja na Mungu au yuko sawa na Mungu Yohana 5;17-18 Yesu akawajibu, “Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi. Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumwua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba Yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.ni Muhimu pia kufahamu kuwa katika ulimwengu wa tawala za kifalme kama mtawala mranyingi hufuata ukoo na hivyo mtoto wa kifalme Prince huwa na heshima sawa na ile ya Mfalme kwa msingi huo Kristo ni mwana wa kifalme He is the Prince

Yesu anasema nini kwa habari ya nafsi yake?
            Akiwa kijana mdogo tu hivi mwenye umri kati ya miaka 12 Yesu alikuwa na ufahamu wa kutosha kujihusu kwanza alijitambua kama Mwana wa Mungu kwa kumuita Baba yangu Luka 2; 49 Yesu akawaambia, “Kwa nini kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba Yangu?” hii ni wazi kuwa mapema sana alitambua kuwa Yeye ni mwana wa Mungu aliwezaje kujua jambo kama hili mapema sana katika umri mdogo kama huo? Hii inabaki kuwa siri kwetu
            Alipokuwa akibatizwa katika mto wa Yordani Yesu aliisikia sauti ya Baba yake ikithibitisha Mbele ya watu kuwa Yeye ni mwana wake mpedwa anayependezwa naye Mathayo 3; 17Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.’’
              Mapema kabisa Shetani alipokuwa akimjaribu Yesu kule Jangwani alitambua kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu Mathayo 4; 3Mjaribu akamjia na kumwambia, “Kama Wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.’’
               Yesu alimsifia Petro kuwa aliweza kumtambua kuwa yeye ni mwana wa Mungu kwa kuwezeshwa na Mungu baada ya Petro kwa uweza wa Mungu kugundua kuwa Yesu alikuwa ni mwana wa Mungu Mathayo 16;15-17 “Akawauliza, ‘‘Je, ninyi, mnasema mimi ni nani?’’Simoni Petro akamjibu,  “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.’’ Naye Yesu akamwambia, ‘‘Heri wewe, Simoni mwana wa Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. Usemi huu wa Kristo unathibitisha kuwa yeye mwenyewe alijitambua kuwa ni mwana wa Mungu.
              Jambo linguine la kushangaza kabisa lilijitokeza Pale Yesu alipokuwa hukumuni mbele ya kuhani mkuu ambapo angeweza kuepuka hukumu ya kifo kama tu angekubali kuwa Yeye sio mwana wa Mungu lakini akiulizwa kwa kuapishwa aseme kama kweli yeye ni mwana wa Mungu Hivi ndivyo ilivyokuwa Mathayo 26;62 - 65 “Kisha Kuhani Mkuu akasimama na kumwambia Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi wa namna gani hawa watu wauletao dhidi yako?” Lakini Yesu alikuwa kimya. Ndipo Kuhani Mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai, tuambie ikiwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.” Yesu akajibu,“Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu na akija juu ya mawingu ya mbinguni.’’

Semi za Yesu zinazomweka katika ngazi ya uungu au mwana wa Mungu
·         Alieleza wazi kuwa anatenda kazi kama baba yake wa Mbinguni Yohana 16;28
·         Alieleza kuwa ametumwa na baba yake Yohana 20;21
·         Alikiri kuwa ana ushirika na Mungu Mathayo 11;27 Yohana 17;25
·         Alikiri kuwa amekuja kumfunua Baba  aliye ndani yake Yohana 14;9-11
·         Alionyesha ya kuwa yuko mahali kote Mathayo 18;20
·         Alionyesha mamlaka ya kusamehe dhambi marko 2;5-10
·         Alionyesha ya kuwa ana mamlaka ya kuhukumu na kuamua mwisho wa mwanadamu Yohana 5;22,Mathayo 25;31-46
·         Alionyesha kuwa anahitajika kupendwa zaidi kuliko chochote sawa na Mungu Mathayo 10;37,luka 14;25-33
Hizi nisemi za Yesu mwenyewe zinazodhihirisha kuwa yeye ni mwana au Mungu Kwa msingi huo hatumsingizii Yesu kuwa ni mwanqa wa Mungu yeye mwenyewe amethibitisha mara kadha na kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa yesu alikuwa ni mwana wa pekee wa Mungu na kwakuwa hakuwahi kutenda dhambi hakuwa na sababu ya kutuongopea
  
Jinsi mamlaka aliyokuwa nayo inavyomtambulisha 

Katika mafundisho yake  Bwana Yesu hautaweza kuona Maneno yenye mashaka kama “kwa maoni yangu” au “inawezekana”  au “nafikiri…”n.k wayahudi wenyewe waliomsikia walisema  alizungumza kwa mamlaka ya kuonyesha ndiye Mungu mwenyewe hili lilidhihirika kwa wazi kabisa kwa mfano katika hutubva yake ya mlimani na neno la Mungu alilolifundisha aliweka wazi kabisa kuwa lilikuwa neno lake pia matumizi ya Neno amini nawaambieni Mathayo 7;24,Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.na Mathayo 7;28-29 “ Yesu alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.Mathayo 6;38-39 Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia, semi hizi zenye mamlaka ambazo ni tofauti hata na za manabii waliosema asema Bwana wa majeshi zinadhihirisha kuwa Kristo alikuwa na mamlaka ya kiungu

Maisha yake ya kutokutenda dhambi.
Hakuna mwalimu yeyote aliyeweza au anayeweza kuwaambia watu watubu na kuishi maisha ya haki anayeweza kuepuka kuwa hana dhambi au mapungufu katika wanadamu wote Yakobo 3;1-2Sisi sote tunajikwaa katika mambo mengi. Ikiwa mtu ye yote hakosei kamwe katika yale anayosema, yeye ni mkamilifu, naye anaweza kuuzuia pia na mwili wake wote.  ni Yesu pekee ambaye aliishi bila kufanya dhambi na kwa Maneno na kwa Matendo yeye pekee alikuwa na ujuzi wa ndani sana kuhusu ubaya wa dhambi wakla dhambi haijawahi kuukaribia hata moyo wake na kwa ujasiri kabisa huku akiwa mnyenyekevu aliwauliza wayahudi kuwa ni nani anishuhudiaye kuwa nina dhambi? Yohana 8;46 “Je, kuna ye yote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa nina dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? Kwa msingi huo hakuna mwanadamu aliye mkamilifu ila Mungu peke yake na hivyo kwa uwezo wa Yesu kuishi duniani Bila kufanya dhambi ni utambulisho ulio wazi kuwa Yeye alikuwa na asili tofauti na kibinadamu.

Ushuhuda wa wanafunzi wake
Wayahudi hawajawahi kufanya makosa ya kufikiri hata siku moja kuwa Musa ni mwana wa Mungu na wala wanafunzi wa Yesu hawakuwahi kufikiri kubatiza watu kwa jina la Baba na Musa na Roho Mtakatifu sawa na Matahayo 28;19 na sababu kubwa ni kwamba Musa hajawahi kusema kuwa yeye ana ushirika na Mungu au ametoka kwa Mungu, Badala yake wanafunzi wa Yesu walumuhubiri Yesu walifanmya miujiza kwa jina lake na walimuabudu wao walikuwa na uelewa tofauti na jamii nyingine za watu
·         Walimuhusisha na kazi ya Uumbaji na hivyo Yesu ni Muumba Yohanma 1;1;3
·         Thomasi alimuabudu na kutamka Maneno Bwana wangu na Mungu wangu Yohana 20;28
·         Petro ambaye alikula naye na kutembea naye katika mitaa mbalimbali ya Israel  alieleza wazi kuwa Yesu yuko mkono wa Kuume wa Mungu Matedno 2;33,36 na ya kuwa huyu ndio njia ya pekee ya wokovu Matendo 4;12 ndiye anayesamehe dhambi  Matendo 5;31 na ndiye atakayehukumu wafu Matendo 10;42 na alimuabudu katika waraka wake kwa kumpa yeye utukufu hata milele 1Petro 3;18
·         Hatuna habari kuwa Paulo aliwahi kumuona Yesu katika mwili ingawa amewahi kumuona baada ya ufufuko wake akiwa ametukuzwa lakini katika namna ya kushangaza Paulo ambaye alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu tangu utoto wake alimtambua Yesu kama Mungu mkuu Tito 2;13 “Tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu,Mungu mkuu na mwokozi wetu;anamtambua kama ukamilifu wote wa Mungu wakolosai 2;9 muumba wa vitu vyote wakolosai 1;17 na kulijumuisha jina lake katika Maombi 1Koritho 1;2 na Matendo 7;59 na kuyatumia majina ya Baba na Roho pamoja na la Bwana Yesu katika salamu za neema
·         Nyakati za kanisa la kwanza hakuikuwa na ubishi kuwa Yesu ni Mungu na wakristo wote walimuabudu na waandioshi wa kipagani wa karne ya kwanza waliandika hivi kuwa wakristo wanamuabudu kiongozi mkubwa sana aliyesulubiwa huko Israel  na wengine walisema wanaimab wimbo wa kumopa sifa Yesu kama wanampa Mungu kwa hiyo wapagani walijua kuwa watu wa karne ya kwanza walimuabudu Bwana Yesu
·         Wanafunzi wa Yesu walikuwa wayahudi na ndio waliotuletea habari za Kristo kumbuka ni ngumu sana kwa myahudi aliyejifunza sheria Tangu utoto kuabudu miungu au kumpa mtu sifa ya Mungu kwa msingi huo sisi tumepokea habari hizi njema kutoka kwao na wokovu watoka kwa wayahudi Yohana 4;22“Ninyi (Wasamaria) mnaabudu msichokijua. Sisi (Wayahudi) tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi.
·         Imani ya Nikea mababa walipokuwa wakitengeneza ukiri wa imani yetu waliemndelea kumuheshimu Yesu kama Mungu “Twamwamini Yesu Kristo mwana wa pekee wa Mungu mwana wa azli wa baba,wenye uungu moja na Baba,mwana wa azli asiyeuumbwa,Mungu kutoka katika Mungu Nuru kutoka katika Nuru …..”
2.      Yesu anaitwa Neno la Mungu
Mwana damu anapozungumza Maneno ndipo anapoweza kujiweka wazi mwenyewe ama kueleweka anapowasiliana na wengine na kwa Maneno anaweka wazi hisia zake na mawazo yake kujulikana na anatoa amri na kuonyesha mapenzi yake na hivyo tunaweza kumjua au kumfahamu na kujua nguvu zake uwezo wake wa ufahamu na matakwa yake. Mungu naye amejifunua kwetu kupitia mwana wake Waebrania 1;1-3 kwa msingi huo yeye ni neno la Mungu na mtu akijiuliza swali Mungu yukoje jibu ni kuwa yuko kama Kristo Yeye ni neno ni wazo la Mungu Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu asiyeonekana

3.      Yesu ni Bwana
Jina hili Bwana ni moja ya majina yanayotumika kuweka wazi kuwa Yesu Kristo ni Mungu, ametukuka na ni mtawala wa Ulimwengu wote Jina Bwana linapotumika Kabla ya jina husika huwa linawakilisha dhana ya uungu hii ilikuwa wazi kwa wayahudi na wayunani,Jina Bwana kwa kiyunani ni “Kurios” ambalo hutumika sawa na Yehova katika tafasiri ya kiyunani ya agano la kale kwa msingu huo kwa wayahudi unaposema “Bwana Yesu” ilikuwa wazi kwamaba huyo ni Mungu, sote tunakumbuka kuwa mtawala wa kirumi Kaisari alipotawala alitaka pia kuabudiwa  alitaka kuitwa Bwana Kaisari ambalo ni sawa na kusema kuwa Kaisari ni Bwana na mataifa walielewa madai ya Mtawala huyo na kwa sababu hizi wakristo waliteswa sana kwa sababu hawakutaka kumtambua Kaisari kuwa ni Bwana Badala ya Yesu
·         Jina Bwana katikaagano la kale Septuagint lilitumika kumaanisha mambo makuu matatu
a.       Bwana maana yake kuwa sawa na Mungu Yehova
b.      Mrithi wa Mungu adonai
c.       Heshima ya kibinadamu inayotolewa kwa Mungu Yoshua 3;11,Zaburi 97;5
·         Katika agano jipya tunaona maana zinazo fanana na hizo zikielekezwa kwa Yesu
a.       katika hali ya heshima kubwa na unyenyekevu mkuu Mathayo 8;2,,20;33
b.      katika kuonyesha mamlaka na nguvu za kitawala Mathayo 21;3,24;42
c.       Katika mamlaka iliyo kuu sawa na Mungu Marko 12;36-37,Luka 2;11,3;4,Filipi 2;111Koritho 12;3.
4.      Yesu ni mwana wa Adamu.
Kwa mujibu wa matumizi ya Maneno ya kiebrania: “Neno mwana wa” huwa linahusu uhusiano au ushiriki  mfano wana wa Ufalme Mayhayo 8;12 ni wale wanaoshiriki katika kweli na Baraka za ufalme wa Mungu au washirika wa ufalme wa Mungu, au neno Mwana wa Amani Luka 10;6 maana yake mwenye kuonyesha ushiriki au kumiliki Amani, au neno mwana mpotevu Yohana 17;12 Ni mwenye kushiriki au kushirikiana na upotevu, Kwa msingu huo Kristo anapoitwa mwana wa adamu maana yake ni mwenye kusushiriki ubinadamu,au mwenye kuushiriki udhaifu wa wanadamu wasio na msaada Neno hili lilitunmiwa na Mungu sana karibu mara “80” katika Ezekiel kuonyesha udhaifu wa Ezekiel aliyekuwa mwanadamu Hesabu 23;19,Ayubu 16;21,25;6 Linapotumika kwa Yesu Kristo lina maana ya mwenye kuushiriki Ubinadamu kwa ubora,Yesu alipotumia jina hili mwana wa adamu yaani mwanadamu angeweza kuleta hoja kuwa ndio tunajua kuwa wewe ni mwanadamu sasa kuna haja gani tena ya wewe kutangaza kuwa u mwanadamu? Hivyo katika midomo ya Yesu hii ilikuwa ina maana ya Mwenye asili ya Mbinguni au uungu anashiriki Ubinadamu na hii inakamilisha ule unabii Mungu pamoja nasi Mathayo 1;23, Kwa msingi huo jina hili linatumika kuonyesha maswala kadhaa kumhusu Yesu Duniani
·         Linaonyesha maisha ya Kristo duniani Marko 2;10
·         Linaonyesha kuwa ni mwana wa Mungu pia ni mwana wa adamu anashiriki uungu na ana shiriki ubinadamu
·         Yohana 5;17-18 Kwa msingi huo Mtu aliposema kuwa Yeye ni mwana wa Mungu maana yake anashiriki uungu na hivyo yuko sawa na Mungu Maandiko hayakanushi kuwa Yesu ni Mungu Wafilipi 2;5-7
·         Baadhi ya wanatheolojia walijaribu kufikiri kuwa neno mwana wa pekee “Monogyny  ni kuwa labada aliumbwa lakini neno hili maana yeke mwenye asili moja na Mungu Yohana 1;14,18kuitwa kwake mwana wa adamu kunakuja tu kwa sababu
1.      Alishiriki ubinadamu kwa Kuzaliwa hapa duniani Mathayo 2;1-2,1;21,Yohana 18;37
2.      Alifufuka toka kwa wafu Matendo 13;33
·         Muhubiri mashuhuri John Wesley  anachangia vizuri wazo lake juu ya Matendo 13;33 ambayo yanaleta msaada wa kitheolojia anasema Yesu aliitwa mwana wa Mungu tangu milele hivyo hakuwa mwana wa Mungu baada ya kufufuka wala hakujiita mwana wa Mungu baada ya kufufuka hata katika eneo ambalo Paulo anaeleza hivyo Warumi 1;4 Yesu ni wa aina moja na Mungu Baba tangu milele
·         Wasomi wengine wanahoji kwanini Yesu anaitwa mzaliwa wa Kwanza kama ni Mungu?
Ni kweli kuwa watu wengi wamefikiri na kudhani kuwa Yesu aliumbwa kwa sababu ya neno mzaliwa wa kwanza kutumika kwake kwa hivyo ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu ndio kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu kisha akashirikishwa katika uumbaji na Mungu mwenyewe, ni muhimu kufahamu kuwa kwa wayahudi Neno mzaliwa wa kwanza halikumaanisha kuwa alizaliwa au kuumbwa kwanza kabla ya viumbe vingine Neno mzaliwa wa kwanza linapotumika kwa wayahudi humaanisha Heshima kubwa au heshima maalumu kuliko wengine Neno mzaliwa wa Kwanza katika kiyunani ni “Prototokos
Prototokos ambalo maana yake ni “Wa kwanza katika cheo” kwa msingi huo kwa Waebrania mzaliwa wa kwanza ni cheo na kinaweza kuhama kutoka kwa mkubwa na kwenda kwa mdogo kwa mfano Esau na Yakobo Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza lakini aliokiuza cheo hicho kwa Yakobo na haki ya mzaliwa wa kwanza ikampata Yakobo 

5.      Yesu ni Kristo
Yesu pia anaitwa Kristo Neno Kristo maana yake mwenye kutiwa mafuta ili awe kuhani, au nabii au mfalme na hujitokeza mara ya kwanza kwa ufafanuzi katika  1Samuel 2;10 na mafafanuzi chini ya Biblia ya Kiswahili Neno hilo Kristo kwa kiebrania ni Masihi au mpakwa mafuta  kwa msingi huo mtu alipochaguliwa na Mungu kufanya kazi fulani kati ya hizo alitiwa mafuta kama ishara ya Kuchaguliwa na Mungu na hivyo mtu huyo angekuwa anamwakilisha Mungu katika ngazi aliyowekwa ,kupakwa mafuta kuliambatana na hali halisi ya kiroho ili kwamba mpakwa mafuta huyo awe mpakwa mafuta halisi katika kuishi kwake,2Samuel 1;14 1Samuel 10;1,6,16;13.Kwa hivyo anapopewa Yesu Kristo ambaye ndiye masihi mkuu ni kwa ajili ya kumwakilisha Mungu na kufanya kazi Ya nabii, mafalme na kuhani wa kipekee sana kwani wote waliopakwa mafuta kwa ngazi hizo walikuwa na mapungufu Yesu alitabiriwa maalumu kama masihi halisi na ndio maana jina Kristo kwa Yesu ni maalumu sana Isaya 11;1-3,61;1 Yeye kama mwana wa Daudi pia wakati huo huo anagekuwa mwana wa Mungu akiwa na sifa za Mungu Isaya 9;6-7,Yeremia 23;6 na tofauti na Daudi yeye utawala wake ni wa milele na wa ulimwengu mzima na yeye ndiye tumainai la Israel
     Nyakati za Agano la kale mtu alipochaguliwa kushika wadhifa wa viti vile vyenye kutiwa mafuta aliwekwa mafuta hayo kama kuteuliwa au kutawazwa rasmi kuwa mfalme mpaka mafuta alitakiwa kutangaza wazi sababu za kumpaka mafuta mtu huyo Yesu alitangazwa wazi pale Yordani kuwa mwana wa Mungu 1Samuel 10;1 Marko 1;11, 9;7,Luka 3;22 

6.      Yesu ni mwana wa Daudi
Yesu Kristo kuitwa mwana wa Daudi haina tofauti na ile ya kuitwa Masihi hii ni kwa sababu masihi alittabiriwa kuwa mwana wa Daudi ni kwa sababu ya uaminifu wa Daudi mungu alimuahidi kuwa atampa kiti cha ufalme milele au hatakosa mtu wa kutawala katika kiti chake cha enzi milele 2Samuel 7;16 kwa hivyo hilo lilikuwa agano la milele la Mungu kwa Daudi na kwa msingi huo tangu wakati huo watu walikuwa wakitazamia kutokea kwa kiongozi wa aina hiyo si hivyo tu bali manabii pia walikuwa wakiwakumbusha watu juu ya ujio wa kiongozi wa jinsi hiyo ambaye ni mwana wa Daudi  ambaye atakuwa mfalme mkuu Yeremia 30;9,23;5Ezekiel 34;23,Isaya 55;3-4,Zaburi 89;34-37, Isaya 11;1

 KRISTO YESU NDANI YA AGANO LA KALE.
Kwa kuwa tunakubali kuwa Yesu alikuwako tangu milele na pia kabla ya uumbaji ni muhimu kufahamu kuwa alihusika kutenda kazi ndani ya agano la kale katika namna iliyofichika Indirect katika namna isiyokuwa ya kawaida alijulikana kama malaika wa Bwana Hii ni kwa sababu zifuatazo
·         Wengi tunafahamu kuwa malaika hawakubali kuabudiwa au kusujudiwa  na hii iko wazi hata kama malaika huyo ni malaika mkuu Ufunuo 19;10,22;8-9 kwa kawaida heshima ya kuabudiwa hupelekwa kwa Mungu tu na kwa msingi huo malaika wanajua kuwa heshima ya kuabudiwa na kusujudiwa ni heshima ya Mungu pekee na katika utii na unyenyekevu walio nao  wao hawakubali kuipokea ibada hata kidogo
·         Malaika wa Bwana anayetajwa katika agano la kale  na ambaye ameonekana kuipokea ibada ana sifa zifananazo na zile za Kristo
*      Anaitwa Mungu wa Ibarahimu Isaka na Yakobo kutoka 3;2-6
*      Huapa kwa nafsi yake Mwanzo 16;7
*      Huongea kwa mamlaka kamili kama Mungu Waamuzi 2;1
*      Ana uwezo wa kusamehe au kutokusamehe dhambi na jina la Mungu liko ndani yake Kutoka 23;20-23
*      Anakubali kusujudiwa na ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Bwana Yoshua 5;13-15
*      Ana uwezo wa kubariki na walipomuona walimuona kama Mungu Mwanzo 32;30,48-16
*      Hajaumbwa na ana sifa nyingine nyingi.
·         Ni kwa sababu hizo wanatheolojia wengi wameshindwa kuepuka kuhitimisha kwa kusema kuwa huenda malaika huyu ni Masihi mwana wa Mungu na mwokozi wa ulimwengu na hivyo huitimisha kwa kusema huyu ni Yesu Kristo mwenyewe akiwa kazini nyakati za Agano la kale kabla ya Kuzaliwa duniani maalumu (Incarnation) kwa hivyo hii ni wazi kuwa Yesu alikuwa akafanya kazi katika agano la kale katika namna hii na kwa Ufunuo mdogo aliokuwa nao Nebukadreza kumhusu Masihi mwana wa Mungu Yeye alisema huyu ni mafano wa mwana wa Miungu Daniel 3;22-25 Kama Mungu Kristo alitenda kazi na Mungu baba yake Bega kwa bega Mwalimu wa somo hili Mchungaji Innocent Kamote anahitimisha kwa kuwasaidia wanafunzi kugundua utendaji wa utatu kwa migawanyo ya kazi zao kwa Mukhutasari huu kwamba popote pale utakapoona kazi hizi zinafanyika basi moja ya nafsi ya Mungu inahusika sana na swala hilo japokuwa wote hufanya kazi pamoja lakini hizi huwatambulisha zaidi
*      Kazi ya Mipango na majira au Muda ni kazi ya Mungu Baba
*      Kazi ya ukombozi na wokovu Shughuli zozote zinazo husiana na ukombozi au wokovu na uponyaji ni kazi za Mungu Mwana Yesu Kristo
*      Kazi zozote zinazohusiana na maongozi au kuweka Viongozi au kuongoza ni kazi za Roho Mtakatifu
Aidha ndani ya agano la kale Kristo sasa anapewa majina ambayo yanadhiohirisha kazi nzima ya ukombozi aliyokuwa akiifanya kwa mfano sasa kila utakapoona kazi za ukombozi zikifanyika zinafunua utendaji wa Yesu Kristo ulio wazi katika agano la kale chukulia sasa mfano jina
Yehova
Biblia ya kiingereza ya KJV inatafasiri jina hilo Yehova kama Bwana na Adonai Jina Bwana lilitumika Badala ya jina Yehova {JHVH} kwa sababu wayahudi waliliheshimu sana jina hili na kuogopa hata kulitaja sasa unapofuatilia kwa makini jina Hili Yehova utagundua kuwa halina tofauti na kazi atakazo zifanya Kristo mwenyewe katika ulimwengu wa agano jipya angalia kwa mfano katika unabii wa Zekaria 12;1-10 “Hili ni neno la BWANA kuhusu Israeli. BWANA, Yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: ‘‘Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye kwa uenda wazimu,’’ asema BWANA. Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu BWANA Mwenye Nguvu ni Mungu wao.’ “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake. “BWANA atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. Katika siku hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa BWANA akiwatangulia. Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia Yerusalemu. “Nami nitamiminia roho ya neema na maombi juu ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma, nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.” Kwa msingi huo Zekaria anatumia neno Bwana ambalo ni mbadala wa Yehova lakini kazi hii kinabii ni ya Yesu kwa msingi huo utaona kuwa kazi za ukombozi ni za Yesu na jina la Yehova hutumika pamoja na shughuli za wokovu au ukombozi.

Elohim

Jina Elohim limetumika mara nyingi sana katika agano la kale kiasi kuwa baadhi ya wasomi hulitafasiri maana yake ni Mwenye nguvu au wa kuogopwa  jina hili kwa asili ni jina linalowakilisha wingi kwa msingi huo wasomi huamini kuwa jina hili lilikuwa likihusisha utatu mzima wa Mungu hata ingawaje jina hilo hutumiwa  wakati mwingine kama kumaanisha maana moja


Adonai

Adonai ni jina lililotumika kwa Mungu ambalo lilitafasiriwa pia kama Bwana katika agano la kale kuonyehs ubwana wake au uwezo wake wa kiutawala, kumiliki na pia linatumika kuonyesha mabwana wa kibinadamu

Muonekano wa Yesu Kristo katika agano la kale (Theophany)

Muonekano wa Yesu Kristo katika agano la kale katika matedno fulani ya muda mfupi kitheolojia unaitwa Theophany katika hali kama hizi Yesu alijitokeza kama malaika wa Bwana  laki tofauti na malaika wengine malaika huyu alikuwa akikubali ibada  neno malaika maana yake ni mjumbe malaika wa Bwana pia Ni malaika wa Yehova huyu alitokea katika Matukio kadhaa na akakubali kuabudiwa
*      Alimtokea Musa kutoka 3
*      Aliwatembelea Israel kutoka 19
*      Musa na Haruni na Nadabu na wakuu sabini wa wana wa Israel walimuona katika namna ya kibinadamu  Kutoka 24;9-11,kutoka 33;17-33
*      Alitambuklika kama malaika wa bwana au wa Mungu Mwanzo 16;13,Kutoka 3;2,5-7
*      Alimtokea hajiri Mwanzo 16;7-13
*      Sehemu nyingine katika agano la kale malaika huyu anakotokea ni pamoja na Mwanzo 22;11-18, 24;7, 40, 31;11,32;24-32, 48;15-16, Hosea12;4, Kutoka 3;2.13, 21, 14;19, 23;20-23, 32;34,33;2, Hesabu 20;16,22,22-35, Waamuzi 2;1-4,5;23,6;11,13;3-23, Samuel 14;17-20, Muhubiri 5;6, Isaya 37,63, Zekaria 1;9,2;3,3;1-10,4;1-7,5;5-10,6;4-5,12;8.
*      Aidha ni muhimu kukumbuka kuwa Yesu Kristo anatajwa kama mwokozi katika agano la kale  wanatheolojia hutimia unabii wa Maandiko kama Ayubu 19;25 na Mwanzo 3;15 na maeneo mengi yanayohusiana na kazi za ukombozi kuonyesha Yesu kuwa ni mwokozi kupitia agano la kale Yeye anaonekana kama Mowkozi kwa umoja,kwa watu binafsi na kwa siku zijazo.

KRISTO YESU KATIKA ALAMA VIVULI TYPOLOGY
Typology ni Elimu inayohusu Picha au kiwakilishi au mfano au kivuli cha kitu fulani halisi kitakachokuja kwa lugha za kinabii hii inahusisha tukio la uhakika la kihistoria linaloweza kusimamia kama mfano wa kweli fulani za kiroho kwa msingi huu ndani ya agano la kale kuna mifano zaidi ya 50 hivi inayomwakilisha Kristo au iliyokuwa ikitoa Picha ya uhalisi wa Yesu Kristo katika uhalisia wa kutimiza unabii huo Mifano hii inaweza kujumuisha watu, Matukio,vitu,sherehe za kidini, ibada na kadhalika
Umuhimu wa typology
·         Zinatusaidia kuelewa kwani uhalisi kuwa kazi ya ukombozi na wokovu halikuwa swala lililozuka tu bali lilikuwa katika mpango wa mMngu.
·         Zinatusaidia sana katika kuelewa kazi ya Kristo ya wokovu na kutupa picha iliyo wazi ya sifa zake,kazi na tabia
·         Zinatusaidia katika kuwasilisha kweli za kibiblia kwa mafundisho au mahubiri kumuhusu Yesu Kristo
·         Zinawakilisha kweli halisi zijazo kumuhusu Kristo.
Mifano ya watu Typical Person
o   Adamu  - ni kiongozi wa uumbaji wa kwanza wenye anguko, Yesu ni kiongozi wa utii unaoleta utu mpya Mwanzo 2;7,1Koritho
o   Habili –mchungaji wa kweli aliyetoa dhabihu ya damu yenye kukubalika na Mungu  katika utii
o   Haruni - aliwekwa na Mungu kuwa kuhani Waebrania 5;4 kama Kristo Waebrania 8;6
o   Musa – alichaguliwa kufanya kazi ya ukombozi kutoka 3;7-10;Matendo 7;25 wote walikataliwa na ndugu zao kutoka 2;11-15 Yohana 1;11Matendo 7;23-28;18;5-6
o   Malkizedeki- Kuhani mkuu wa Mungu Mwanzo 14,Zaburi 110;4 Kristo ni kuhani mkuu milele kwa mfano wa Melkizedeki maana ya jina hilo ni uhalisia wa jina na tabia za Kristo na ukuhani wao ulitoka nje ya kabila ya Lawi Waebrania 5;6,6;20,7;12,21
o   Boazi Kinsman redeemer- Kinsman redeemer maana yake ni Mkombozi ambaye kwa mujibu wa agano la kale na tamaduni za wakati ule kama mtu alifiwa na mume na mume alikuwa na ndugu ndugu huyo aliyekaribu alitakiwa kufanya kazi ya ukombozi ya kumkomboa na kumuoa Mwanamke aliyeachwa hali ya ujane ili kumuinulia nduguye uzao Walawi 25;48-49,Ruthu 3;12 Waebrania 2;14-15 Kristo alifanyika kwa njia ya kufanyika mwanadamu na kutukomboa na kulipa gharama Walawi 25-27, Warumi 3;24-26,1Petro 1;18-19,Wagalatia 3;13
o   Yoshua- jina lake maana yake Yohova anaokoa ni jina sawa na la Yesu aliwapa raha ya kanaani Waisrael Yesu atatoa raha ya mbinguni Waebrania 7;19-29
o   Yusufu- alisalitiwa na ndugu zake na baadaye kuja kuwa mtawala wao Yesu alisalitiwa na wayahudi nduguze na baadaye atakuja kuwa mtawala wao,walinyang’anywa mavazi Mwanzo 37;23,Mathayo 27;35,waliuzwa kwa Fedha Mwanzo 37;2814-15.
o   Isaka – wote ni wana wa pekee Yohana 3;16;Waebrania 11;17 maisha yote ya Isaka  yanaonyesha mfano ulio kamili  zaidi wa nafasi na kazi ya Kristo kuliko wote waliotangulia alibeba kuni ili kutolewa sadaka juu ya kuni hizo, alibeba Msalaba ili kutolewa sadaka juu ya Msalaba huo
o   Daudi – Mchungaji na mfalme Kristo ndiye Mchungaji mwema kwa mamlaka kama ya Daudi
o   Benjamin kwa jina lake – majina yote mawili ya Benjamin huonyesha  mateso ya Yesu Kristo na utukufu utakaofuata aliitwa jina Bennon yaani mwana wa huzuni kutoka kwa mamaye Rahel na Yakobo alimpa jina Benjamin maana yake mwana wa mkono wangu wa kuume
o   Yona – alikuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine, pia alikaa katika tumbo la nyangumi kwa siku tatu na umisheni katika jamii ngeni
o   Samsoni – Alitiwa mikononi mwa wenye dhambi na nduguze, hakuheshimika, lakini aliheshimika baada ya kufa alikufa akiwa ametanua mikono yake katika Nguzo mbili
o   Esta – alikuwa Tayari kufa kwa ajili ya taifa lake, alijitoa sadaka kwa mfalme ili awakomboe ndugu zake
o   Abrahamu – rafiki wa Mungu Isaya 41;8 na Mathayo 17;5
Mifano ya vitu Typical things
o   Kondoo aliyechukua nafasi ya Isaka – Mwanzo 22;13,Isaya 53;6,1Korithians 15;3
o   Ngazi aliyoiona Yakobo Mwanzo 28;12, Yohana 14;6
o   Manna Kutoka 16;14,15,Yohana 6;31-63
o   Mwamba wa Herobu kutoka 17;6,1Koritho 10;4 na Yohana 7;37-39
o   Hema ya kukutania Kutoka 40;33,34,Kolosai 2;9
o   Sanduku la agano Kutoka 25;16,Zaburi 40;7,8,Yohana 15;10,Luka 22;20
o   Kiti cha rehema Kutoka 25;21,22,Warumi 3;25,Waebrania 4;16
o   Pazia la hema na hekalu Kutoka 40;21,2Nyakati 3;14 Waebrania 10;9,-10
o   Madhabahu ya kufukizia uvumba ya dhahabu kutoka 40;26,27 Waebrania 13;15
o   Meza ya mikate ya wonyesho Kutoka 25;23-30 Yohana 6;48
o   Taa ya vinara saba kutoka 25;31,Yohana 8;12
o   Madhabahu ya shaba Kutoka 27;1-2Waebrania 13;10
o   Nyoka wa shaba  Hesabu 21;9 Yohana 3;14,15
o   Miji ya makimbilio Hesabu 35;6 Waebrania 6;18
Mifano ya sikukuu typical feast
o   Malimbuko Walawi 23;10-11 1Koritho 15;20
o   Sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi na jioni Kutoka 29;38-39 Yohana 1;29
o   Siku ya upatanishi walawi 16;15-34,Waebrania 9;11-13
o   Sadaka ya dhambi walawi 14;6,7 waebrania 13;11-13
o   Sadaka ya amani walawi 3;1-2 Efeso 2;14-18
o   Pasaka 1Koritho 5;7 1Petro 1;15-19
Mifano ya kimatukio typical events
o   Kuvikwa vazi kwa Adamu na Hawa  Mwanzo 3;21
o   Nuhu kuhifadhiwa katika safina 2Petro 2;5,9
o   Ukombozi wa wana wa Israel kutoka Misri kielelezo cha kazi ya ukombozi wa Kristo
o   Kuingia kanaani ni mfano kielelezo cha kuingia mbinguni halisi itakavyokua

KRISTO YESU KATIKA UNABII WA AGANO LA KALE
Yesu Kristo alitabiriwa katika maisha Shughuli kazi na utendaji wa aina mbalimbali kuhusu maisha yake katika agano la kale hata kabla ya Kuzaliwa kwake yako maeneo mengi yaliyotabiriwa kumhusu masihi Yesu jambo hili ndilo lililopelekea wayahudi kuwa na mtazamo wa kumtazamia masihi Yesu Kristo

Unabii kuhusu Mtangulizi wa masihi
Masihi alitabiriwa kutanguliwa na mtangulizi na ambaye angepiga kelele nyikani kuwa watu watengeneze njia huyu alikuwa Yohana mbatizaji na unabii ulitimizwa
Ø  Isaya 40;3-5 Luka 3;2-6 Isaya 40;9-10 Mathayo 3;1-3
Ø  Malaki 3;1,Malaki 4;5 Marko 1;2-3,Luka 7;24-27Mathayo 11 ;10,13-14 Luka 1;17
Ø  Ezekiel 29;21 Luka 1;68-69,76-79

Unabii kuhusu ukoo wa masihi na Nafsi ya Masihi
Ø  Ni uzao wa mwanamke Mwanzo 3;15,Galatia 4;4
Ø  Ni mwana wa Daudi Mathayo 1;1,Yohana 7;42
Ø  Amekuwako tangu milele  Mika 5;2
Ø  Ni Mungu mwenye nguvu Isaya 9;6-7
Unabii kuhusu Kuzaliwa kwake 

Ø  Atazaliwa Bethelehemu Mika 5;2,Mathayo 2;1-6
Ø  Kuzaliwa na Bikira Isaya 7;14
Ø  Ndiye atakaye miliki Mwanzo 49;10
Ø  Ni Mtawala aliyepakwa mafuta Daniel 9; 25

Unabii kupakwa kwake mafuta
Ø  Utawala wake ni wa milele na milele  Zaburi 102;25-27,Waebrania 1;8-12
Ø  Roho wa Bwana atakuwa juu yake Isaya 61 ; 1-3 Luka 4;16-21,Yohana 3;34
Ø  Ni chipukizi katika shina la Yese Roho atakua juu yake Isaya 11;1-4, 42;1.Luka 3;21-22,

Unabii kuhusu huduma yake
Ø  Kiongozi toka miongoni mwao Yeremia 30;21,Marko 6;1-4
Ø  Huduma  atakayoifanya Isaya 61;1-4,Mathayo 4;17,Marko 1;14-15,Luka 4;17-21
Ø  Miji itakayofaidika na huduma ya masihi  Luka 9;1-2,Mathayo 4;12-17
Ø  Kufundisha kwake kwa mifano Zaburi 78;2-4, Mathayo 13;34-35
Ø  Kushangiliwa na wanafunzi na watu na watoto Zaburi 8;2, Mathayo 21;15
Ø  Kufukuza watu Hekaluni wivu wa Bwana Zaburi 69;9,119;139 Yohana 2;13-17

Unabii kuhusu kifo chake  
Ø  Nitampiga Mchungaji wa kondoo na kondoo watatawanyika Zekaria 13;7, Yohana 10;11,15
Ø  Kuinuliwa kwake msalabani Yohana 3;14,12;32
Ø  Mateso yake, kujitoa kwake kwa ajili yetu, kuchukua dhambi zetu kupatwa na adhabu itakayoleta amani yetu Isaya 53.Zaburi 22
Ø  Masihi kukatiliwa mbali Daniel 9;26

Unabii kuhusu kufufuka kwake
Ø  Nafsi yake haitaachwa kuzimu, Zaburi 16;8-10
Ø  Nafsi yake haitaachwa kaburini, Zaburi 30; 3, 41;10
Ø  Nafsi yake haitaachwa katika nguvu za kaburi Zaburi 49;15

Unabii kuhusu kupaa kwake
Ø  Kukaa kwake mkono wa kuume wa Mungu Zaburi 16;10-11
Ø  Kupaa kwake juu na kutoa vipawa Zaburi 68;18

Unabii kuhusu Ufalme wake
Ø  Utakua ufalme wa amani Isaya 9;6-7,
Ø  Utakua ufalme wa milele 2Samuel 7;16-17,Luka 1;32-33
Ø  Fimbo ya ufalme haitaondoka katika Yuda Mwanzo 49;10 Ufunuo 19;15-16
Ø  Adui zake wote watawekwa chini ya miguu yake Zaburi 110;1 Matendo 2;34-35
Ø  Atalijenga hekalu la Bwana Zekaria 6;12,9;9-10
Ø  Ufalme wake hautaondoshwa Daniel 7;14

SURA YA PILI; YESU KRISTO KATIKA MWILI WA KIBINADAMU

KRISTO YESU KUUTWAA MWILI

Kristo Yesu kuwa katika mwili wa kibinadamu tendo hili kitheolojia huitwa Incarnation  dhana hii imekuja kutokana na ukweli kuwa ukiichunguza injili kweli hii inadhihirika wazi kuwa Yesu alikuwa Mungu na aliamua kuchukua asili ya kibinadamu ili kwamba apate kuwakomboa wanadamu huku alipokuwa mwanadamu hakuutumia uwezo wake wa kiungu bali aliishi kama mwanadamu wa kawaida Tendo la kiumbe cha kiroho  kuutwaa mwili wa kibinadamu huitwa Incarnation kwa msingi huo basi Yesu alikuwa Mungu kamili na Mwanadamu kamili tendo hili linaungika mkono kama sehemu ya utatu wa Mungu kwamba nafsi moja ya Mungu ilichukua umbile la kibinadamu kwa ajili ya kutimiza Makusudi fulani maalumu neno akafanyika mwili Mathayo 1;20, Luka 1;35, Yohana 1;13-14, Matendo2;30, Warumi 8;3, Wagalatia 4;4, Wafilipi 2;7
     Swala hili katika karne ya kumi na tisa katikati lilichukua sura mpya ya aina mpya ya ufahamu kuhusu Kristo na kuundwa kwa fundisho maalumu lililoitwa Doctrine of Kenosis au kenotic Theory fundisho hili lilipata kibali miongoni mwa jamii ya kilutheri na baadhi ya waprotestant  na hivyo kulileta kanisa pamoja mwanzilishi wa fundisho hili au mgunduzi wa fundisho hili aliitendea haki nafsi ya Yesu kuwa Ni mwanadamu halisi na pia ni Mungu halisi isipokuwa Yesu alijinyenyekeza na kujitoa sadaka kuwa mwanadamu
Neno kenosis hutumika katika maana kuu mbili ya kwanza ni self limitation yaani hii ni hali ya kujiwekea mipaka kujidhili au kujishusha na kujiondoa katika uhalisia na kuweka kando tabia za kiungu na kutumia uanadamu wake hali hii Ina faida kwetu kama zinavoonekana chini.
Faida za Yesu kuutwaa mwili wa kibinadamu Incarnation?
  • Alimshinda yeye aliyekuwa na nguvu za mauti shetani.na kuziharibu kazi zake 1Yohana 3;8;Waebrania 2;14
  • Alizuhubiri roho zilizokuwa kifungoni (1Petro 3;18-19), neno linalotumika katika Petro kuhusu kuzihubiri roho zilizokuwa kifungoni katika biblia ya kiyunani ni “Kerussen” ambalo maana yake ni kutangaza announce na sio kuhubiri kule tunakofikiri au tulikozoea.
  • Kwa kuuvaa mwili amefaa kuwa kuhani mkuu mwenye rehema na mwaminifu katika mambo ya Mungu (Waebrania 2;17-18).Yeye anawajua wanadamu na anamjua Mungu hivyo yu afaa kuwa kuhani mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu.kwa kuwa anawajua wote kwa asili
  • Alijaribiwa sawa na sisi katika mambo yoote bila kufanya dhambi na kwa sababu ya ukamilifu wake tunaweza kuyategemea maombi yake, msaada wake na tunapata ujasiri wa kumuendea maana anatujua vizuri,mara nyingi tumewaeleza wanadamu shida zetu na hisia zetu na wakaishia kutuumiza zaidi kuhani anayefaa zaidi na mtu wa kumueleza shida zetu na hisia zetu ni Yesu Kristo pekee yake.
  • Aliweza kuzichukua dhambi za wanadamu na kufanya upatanishi kwa Mungu na kumfanya awe hakimu wa haki utawahukumuje wanadamu huku wewe hujawahi kuonja uanadamu?
  • Aliweza kufanya matayarisho ya kuja kwake mara ya pili Waebrania 9;28

MWANADAMU YESU KRISTO
Ubinadamu wa Yesu Kristo
1.      Kuzaliwa kupitia kwa Bikira.
Unapozungumzia Yesu kama mwana wa Adamu yaani Mungu anayeshiriki ubinadamu lazima kwanza utafikiri juu ya Kuzaliwa kwake na Bikira.maandiko yanafundisha kuwa Yesu alizaliwa kwa Muujiza katika tumbo la Mariamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wala sikwa uwezo wa kibinadamu Mathayo 1; 18, 20, 24-25 Luka 1; 35, 3; 23 ni nini maana ya tukio hili la Yesu kuizaliwa na Bikira kuna mafundisho makuu kama matatu tuyapatayo kupitia Tendo la Yesu Kuzaliwa kwa njia hii
1.      Kuonyesha kuwa Wokovu unatokana na Mungu mwenyewe kama Mungu alivyoahidi kupitia uzao wa mwanamke Mwanzo 3;15.Wokovu ni matokeo ya kazi ya Mungu na sio ya wanadamu ni kwa miujiza wa kiungu ndipo tunapata wokovu kwa msingi huo tendo hili ni wazi kabisa kuwa kazi ya ukombozi ni juhudi ya Mungu  kwa hivyo alizaliwa chini ya sheria ili awaokoe wale walio chini ya sheria na kufanywa wana wa Mungu Wagalatia 4;4-5
2.      Kunaonyesha Muungano sasa wa asili ya uungu na asili ya ubinadamu na hii ndio maana neno Mungu alimtumia mwana wake hutumika Yohana 3;16,Wagalatia 4;4 Hapa ndipo Yesu alichukua Ubinadamu na ili aje ulimwenguni kama mwanadamu na ingekuwa ni vigumu kwetu kuamini kuwa Yesu ni mwanadamu kamili kama angelikuja moja kwa moja kutoka Mbinguni na sio hivyo tu bali ilibidi achukue asili ya Adamu na pia ingekuwa ni vigumu ketu kuamini kuwa Yesu ametoka kwa Mungu kama kwa upande mwingine angeruhusu Yesu Kuzaliwa na wazazi wa kibinadamu wawili kwa msingi huo kwa kuwa wokovu ni kazi kamili ya Mungu ilibidi asili mbili ziungane kwa hivyo tunampata Yesu Mwanadamu kamili na Mungu kamili kwa msingi huo Mungu katika Hekima yake aliamua kufanya hivi hivyo tunaamini Yesu alikuwa Mungu kwa sababu kutungwa kwake katika tumbo la Mariam ni kazi ya Roho Mtakatifu na Kuzaliwa kwake na mariam kunatupa uhakika kuwa ni mwanadamu
3.      Kitendo hiki pia ndicho kinachomfanya Yesu Kristo kama mwanadamu kamili pia lakini asiye na dhambi, wanadamu wote wana asili ya Dhambi na tuna hatia na hatuko sawa kimaadili kwa sababu ya Baba yetu wa kwanza Adamu Kwa msingi huo kwa kuwa kua na ukweli kuhusu Yesu kutokuwa na baba wa kidunia  kuna mfanya Bwana Yesu asiwe na asili kama ile tuliyo nayo sisi ya dhambi na hii ndio maana Yesu huitwa mwana wa Mungu Luka 1;35 kwa msingi huo miujiza huu unamfanya Yesu asiwe na asili ya dhambi ya Adamu huku akiwa mwanadamu na kwa kule kuwa mwana wa Mariam Yesu hakuweza kuchukua asili ya dhambi kwa sababu Roho wa Mungu aliingilia kati Kuzaliwa kwa Kristo na pia kulinda asili ya ubinadamu ya dhambi ndani ya Mariamu isiweze kuleta athari kwa Yesu Kristo rejea Luka 1;35
2.      Udhaifu wa kibinadamu na Mipaka ya kibinadamu
a.       Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu. Ukweli kuwa Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu kama tulio nao sisi  unaonekana katika Maandiko yenyewe ,
·         Alizaliwa kama wanadamu wengine yaani kwa miezi kamili tisa tumboni Luka 2;6-7,
·         Alikuwa na kuongezeka katika kimo  Luka 2;40
·         Alikua kiakili yaani katika Hekima, kimo  na maadili na yaani akiwapendeza Mungu na wanadamu Luka 2;52
·         Wakati mwingine alichoka kama wanadamu wengine  Yohana 4;6
·         Aliona kiu kama watu wengine Yohana 19;28
·         Alisikia njaa na kutamani kula Mathayo 4;2
·         Alikuwa dhaifu baada ya kufunga kwa siku kadhaa Mathayo 4;11
·         Alichoka Baada ya kupigwa mijeledi na hatimaye kushindwa kuubeba nsalaba na kuhitaji kusaididwa Luka 23;46
·         Alikufa kama wanadamu wengine wawezavyo kufa pale msalabani Yesu alikufa Luka 23;46
·         Alikuwa na mifupa na majeraha baada ya kufufuka kuonyesha alikuwa mwanadamu Luka 24;39
·         Walimpa samaki wa kuo9kwa na alikula mbele yao Luka 24;42,30,Yohana 20;17,20,27,21;9,13.
·         Kisha Bwana Yesu alipaa kwenda mbuinguni huku wakimshuhudia Matendo 1;9
Mistari yoote hiyo hapo juu inatuthibitishia kuwa Yesu alikuwa na mwili wa Kibinadamu na hivyo alikuwa mwanadamu kamili akiwa na nyama na mifupa na ule ukweli kuwa alipaa mbinguni akiwa na mwili huu wa kibinadamu ni wazi kuwa Yesu ameendelea kuwa na mwili wa kibinadamu hata huko mbinguni mwili huu haukubadilika hata baada ya kufufuka isipokuwa ulikuwa katika hali ya kutokuharibika tena na kuwa mwili wa kimilele ambao ni mortal
b.      Yesu alikuwa na akili za kibinadamu. Ukweli kuwa Yesu alikuwa katika kimo na Hekima unatuthibitishia kuwa alikuwa na akili za kibinadamu Luka 2;52, alijifunza kama wanadamu wengine Luka 2;46,alijifunza kula,kutembea.kusoma na kuandika na kuwatii wazazi Waebrania 5;8 hali hizi zote za kujifunza zilikuwa ni za kibinadamu na akiwa na akiliza kibinadamu kama wanadamu wengine hakuweza kujua siku atakayo rudi duniani mara ya pili Marko 13;32
c.       Yesu alikuwa na Nafsi ya kibinadamu na hisia za kibinadamu, tunaona dalili nyingi za kuonyesha kuwa Yesu alikuwa na Nafsi au roho ya kibinadamu
·         Alifadhaika rohoni Yohana 12;27
·         Alisikitikia usaliti Yohana 13;21 neno la kiyunani kufadhaika linasomeka Tarasso
Tarasso Neno ambalo hutumika kwa wanadamu wanapokuwa katika hali ya kuteseka au kufadhaishwa na kukabiliwa na hali ya hatari.
·         Alisikia huzuni kiasi cha kufa Mathayo 26;38
·         Alistaajabia imani ya akida Mathayo 8;10
·         Alilia wakati wa msiba wa Lazaro Yohana 11;35
·         Alimlilia Mungu amtoe katika wafu Waebrania 5;7
Lakini pamoja na haya yote hukufanya dhambi bali alijifuza kuwa mtii Waebrania 5;8-9 4;15 ukweli kuwa alijaribiwa sawa na sisi katika mambo yote ni wazi kuwa alikuwa na Nafsi ya kibinadamu na hisia ya kibinadamu
d.      Watu waliokuwa karibu naye walimuona kama mwanadamu wa kawaida Mathayo 4;23-25 Yesu alifanya miujiza mingi sana lakini alipokuja kwao Nazarethi watu hawakumpokea  kwani walimjua na kuona kuwa alikuwa mtu wa kawaida Mathayo 13;53-58 maandiko haya yanafunua kuwa wale watu walipomuona yesu majirani zake eneo alilokulia akitengeneza fanicha na ndugu zake wakijulikana wao walimuona Yesu kuwa Binadamu wa kawaida
·         Walimuona kama mwana wa Seremala Mathayo 13;55
·         Walimfahamu yeye mwenyewe kama Seremala marko 6;3
·         Alikuwa wa kawaida hata wakamuuliza amepata wapi haya Mathayo 13;56
·         Hata ndugu zake walimuona wa kawaida kiasi cha kutomuamini Yohana 7;5
Kwamaaana hii Yesu alikuwa wa kawaida kiasi kuwa wale walipomuona akikua katika yao kwa muda wa miaka 30 kabla ya kuanza huduma walimuona mtu wa kawaida mwema tu na sio vinginevyo
e.       Yesu Kristo hakutenda dhambi
Ingwaje mafundisho ya kibiblia pia huonyesha ya kuwa Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida lakini yanatuhakikishia kuwa yeye hukufanya dhambi na hii ndio tofauti yake na wanadamu wengine ni wazi kuwa wanadamu wote hutenda dhambi lakini sivyo ilivyo kwa Yesu
·         Alikuwa na Hekima na alimpendeza Mungu na wanadamu Luka 2;40
·         Shetani alimshawishi ili atedne dhambi na alishindwa Luka 4;13
·         Wayahudi walishindwa kushuhudia kuwa alitenda dhambi Yohana 8;46
·         Semi zake zinathibitisha kuwa aliishi maisha ya ushindi alisema mimi ni Nuru ya ulimwengu Yohana 8;12
·         Alighakikisha kuwa wakato wote anafanya mapenzi ya baba yake Yohana 8;29
·         Alizishika amri zote za baba yake Yohana 18;38
·         Aliitwa mtakatifu mwenye haki Matendo 2;27,3;14,4;30,7;52,13;35
·         Mitume walishuhudia kuwa asiyejua dhambi 2koritho 5;21
·         Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anasema kuwa yeye alijaribiwa katika mambo yote bila kufanya dhambi Waebrania 4;15-16
·         Ni kuhani mkuu aliye mtakatifu Waebrania 7;26
·         Ni mwanakondoo asiye na waa 1Petro 1;19
·         Hukufanya dhambi wala kunena uovu 1Petro 2;22
·         Ni mwenye haki aliyekufa kwa ajili ya wasio haki 1Petro 3;18 1Yohana 2;1
·         Ndani yake hakuna dhambi 1Yohana 3;5
Je Yesu angeweza kutenda dhambi?
Kuna mijadala ya kitheolojia kuhusu Yesu kama angeweza kutenda dhambi au la na hii huzaa makundi maalumu mkauu mawili kundi la kwanza husema ndio Yesu asingeweza kufanya dhambi na kundi jingine linasema kama asingeweza kutenda dhambi gasi hakukuwa na sababu za kujaribiwa au majaribu yake hayakuwa majaribu ya kweli utakijaribu vipi kitu amabacho unajua kuwa hakiwezi kufanya dhambi? katika kulijibvu swala hili vema ni lazima kwanza kusema hivi
1.      Maandiko yanaonyesha kuwa Yesu hakutenda dhambi hii ieleweke hivyo kuwa hakutenda dhambi
2.      Maandiko yanaonyesha wazi kuwa kweli Yesu alijaribiwa na kuwa majaribu haya yalikuwa halisi kabisa Luka 4;2 na kama tunayaamini maaandiko basi nilazima tukubali wazi kuwa majaribu ya Yesu yalikuwa majaribu halisi na alijaribiwa kila eneo Waebrania 4;15 kwa hivyo swala la kusema kuwa majaribu ya Yesu hayakuwa dhahiri ni wazi kuwa ni hitimisho lisilo la kimaandiko na la uongo
3.      Lazima pia tukubali wazi kuwa Mungu hajaribiwi kwa uovu sawa na Yakobo 1;13 na kama hivyo ndivyo basi je kwanini kama Yesu ni Mungu anajaribiwa?ndio Yesu ni Mungu lakini pia ni mwanadamu na hakuna Maandiko yanayothibitisha kuwa Yesu hajaribiwi kwa uovu kama yesu angekuwa na asili ya kibinadamu inayosuimama mpeke yake kama ile ya adamu basi kulikuwa na uwezekano ulio halisi wa Yesu kufanya dhambi, lakini kwa kuwa Yesu alikuwa na asili zote mbili kwa wakati huu basi uwezekano wa kutotenda dhambi kwa Kristo ulikuweko na katika hali kama hii basi Yesu angetenda dhambi basi pia ilikuwa ni wazi kuwa Mungu ametenda dhambi
4.      Kwa msingi huu tunapo jiulize je Yesu angeweza kutenda dhambi jibu ni moja tu hangeweza kutenda dhambi lakini swali linaweza kubakia Je majaribu yake yalikuwa halisi
5.      Jibu ni kuwa kama Yesu angekubali kugeuza mawe kuwa mkate wote tunajua kuwa utendaji wa Yesu wa miujiza ulikuwa ni sehemu yake ya kazi za kiungu hivyo angefanya hivyo basi angekuwa ameitumia sehemu yake ya uungu na kukana ubinadamu na hivyo angekuwa ameanguka kama Adamu tu
Umuhimu wa Yesu kuwa mwanadamu
a.       Kwa ajili ya kutufundisha utii uliotimia
b.      Kwa ajili ya kuwa sadaka halisi ya ukombozi wa dhambi zetu
c.       Ili awe mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu
d.      Kutimiza kusudi la Mungu la asili la mwanadamu kuutawala uumbaji
e.       Kuwa mafano wa kuigwa wa maisha ya mwanadamu
f.       Kuwa sehemu ya miili yetu itakayokombolewa
g.       Ili kusudi aweze kuchukuliana nasi kama kuhani mkuu
Yesu ataendelea kuwa Mwanadamu?
Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu hakuacha kuwa mwadamu hata baada ya kufufuka katika wafu alikuwa akiwatokea wanafunzi wake akiwa na alama za misumari kuonyesha mwili wake uliojeruhiwa kwa kusulubiwa Yohana 20;25-27 alikuwa na mifupa na nyama Luka 24;39 alikula chakula Luka 24;41-42 na hata baada ya kufufuka alipokuwa akipaa Malaika waliahidi kuwa kama alivyopaa ndivyo atakavyokujqa  matedno 1;11 Stefano alisisitiza kua alimuona  ameketi mkono wa kuume wa Mungu Matedno 7;56  alimtokea Paulo huko dameski matedno 9;5 na alitokea wengine wengi kwa jinsi hiyo Ikorotho 9;1 ,15;8 na katika Ufunuo Yohana anamuona kama mwana wa kuibinadamu Ufunuo 1;13 pamoja na kuwa alikuwa amefunikwa na utukufu  mwingi kiasi cha kumfanya Yohana kuanguka kumsujudia Ufunuo 1;13-17 Yeye mwenyewe alihaidi kuwa siku moja atakula na kunywa pamoja na wanafunzi wake katika ufalme wake Mathayo 26;29 Ufunuo 19;9 hii ni wazi kuwa Yesu ataendelea kuwa mungu mwanadamu milele.
MAISHA YA YESU KRISTO DUNIANI
Hatutakuwa tena na Muda wa kutosha kujadili kuhusu Kuzaliwa kwa masihi maana hilo tumeligusa katika maeneo mengi ya kutosha katika eneo hili tutazungumzia  zaidi wajibu alio kuwa nao au ofisi za Kristo yesu alipokuwa duniani , Nyakati za agano la kale kulikuwa na ofisi kuu tatu amabazo zilikuwa ni ofisi zenye kufanya kazi ya upatanishi kati uya Mungu na wanadamu hawa wal;ikuwa wafalme makuhani na amanabii Yesu kama Mpatanishi mkamilifu nawa pekee alikuwa na ofisi hizo zote tatu kwa wakati moja (1Timotheo 2;5) Yeye alikuwa nabii, Kuhani na mafalme na alitimiza nyadhifa hizo katika maisha yake duniani kwa namna hii tunayoichambua chini
Kristo Yesu kama Nabii
Yesu Kristo kama Nabii ni wazi kuwa Manabii katika agano la akle waliifanya kazi ya kumwakilisha Mungu na kusema kwa niaba ya Mungu  wakifunua mapenzi yake kwa wakati uliopo na wa baadaye nao walitabiri wazi kuwa Masihi pia atakuwa nabii mkuu mwenye kusubiriwa kwa hamu na Israel wote  Isaya 42;1 na Warumi 15;8 na ndivyo Yesu alivyochukuliwa katika injili Marko 6;15,Yohana 4;14,9;17marko 6;4 1;27 kote huku anachukuliwa kama nabii Yesu kama Nabii alifanya mambo ya msingi yafuatayo
a.      Alihubiri wokovu mara nyingi katika Israel ilipotokea kuwa Viongozi wa kisiasa na makuhani na wengine wamefikia mahali pa kushindwa kujua nini cha kukifanya Ndipo nabii hutokea na kuonyesha njia kuwa hili ndilo jamabo la kufanya au kufuata Yesu alikuja katika wakati kama huo watu wakiwa katika hali ya kukosa amani na kutokujua nini cha kukifanya  na kuwaonyesha njia  aidha wale waliokataa njia na kutaka kufanya mapinduzi kwa njia zao Yesu alikwisha kuwaonya kama nabii kuwa nini kingewapata Luka 19;41-44 na Mathayo 26;52 mwaka wa 70 Ad. Hivi walijaribu kujitafutia uhuru tofauti na ujumbe wa Kristo na hivyo damu nyingi ilimwagika na matokeo yake walitawanywa duniani
b.      Yesu alitangaza ufalme wa Mungu Manabii wote waliopita walikuwa wakiwakumbusha watu yaliyo wajibu wao kwa sheria za Mungu hii ina maana ya kujitia katika utawala wa Mungu yaani ufalme wake  Yesu alihubiri watu watubu kwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia Mathayo 4;17 na alimtumia muda mwingi kufafanua namna ufalme huo unavyofanya kazi
c.       Alitabiri mambo yajayo Unabii hautegemeani na kanuni za kakwaida za kihistoria wenyewe unakwenda kutokana na mpango wa Mungu kwani yeye anajua mwisho kabla ya Mwanzo Mathayo 24-25 ni mfano wa Matukio ya kinabii amabayo Yesu alitabiri na pia anaendelea na kazi hii ya unabii hata baada ya kupaa kwake kupitia mwili wake yaani kanisa Yohana 14;26;16;13 hii hainja maana kuwa wakristo wanapaswa kuongezea katika Maandiko ya kinabii hapana lakini ziko karama za kinabii 1Koritho 12;0 lakini unabii huo unapimwa kulingana na Maandiko na unabii huo lazima uwe kwa kusudi la kujenga 1koritho 14;3
Kristo Yesu kama Kuhani
Kristo Yesu kama kuhani alitimiza mambo makuu ya msingi yafuatayo
·         Alifaa katika ofisi ya ukuhani Waebrania 1;3-6
·         Aliwekwa na Mungu kuwa kuhani Waebrania 5;1-10
·         Alikuwa na ukuhani bora zaidi kuliko ukuhani ule wa Haruni Waebrania 5;6,10
·         Alifanya kazi zote za ukuhani Waebrania 7;23-28,9;11-28,10;5
·         Ukuhani wake ni wa milele usio na kikomo
Kristo Yesu kama Kuhani
·         Yesu Kristo alikuwa ni kuhani mafalme na nabii na kwakuwa na ofisi hizi zote kumemfanay awe kiongozi mkamilifu kwa mfano wa Melkizedeki Mwanzo 14;18-19 waebrania 7;1-3, na kwa mujibu wa agano la kale masihi alitabiriwa kuwa mfaqlme mkuu wa uzao wa Daudi Isaya 11;1-9 zaburi 72 na Yesu alikubali kuwa yeye ndiye mfalme huyo mbele ya Pilato Yohana 18;36
·         Baada ya Ufufuo Yesu alikiri kuwa mamlaka yote Mbinguni na duniani amepewa yeye Mathayo 28;18, hivyo kupitiqa Ufufuo Yesu alivikwa taji na kuketishwa katika kiti cha enzi cha Mungu na baba byake Ufunuo 3;21,sawa na Waefeso 1;20-22 haya yote ni sahii katika mtazamo wa Mungu lakini kwa wanadamu bado wengi hawajatambua kuwa yeye ni mafalme ingawa amekwisha kupakwa mafuta kuwa mafalme Matendo 2;30Yohana 1;11,19;15
Kristo Yesu kama Mwalimu mkuu
Ni wazi pia kuwa Yesu Kristo alikuwa mwalimu mwema na mwenye mafanikio makubwa kuliko waaalimu wote duniani aliyefanikiwa sana alikuwa “Rabi”
·         Amekuwa na mafundisho Bora zaidi kuliko mtu awaye yote
·         Mafundisho yake yanauwezo mkubwa wa kubadili maisha ya watu kwa karne nyingi
·         Alimtumia njia bora zaidi za ufundishaji ikiwamo mifano na hadithi alieleweka kwa wasomi na wajinga
·         Amepata matokeo mazuri kuliko yeyeote katika historia ya dunia mwenye kuweza kubadilisha maisha ya watu na wanafunzi wake kupitia neno lake
·         Alikuwa na sifa zote kuu tano za mwalimu mwema, aliwapenda wanafunzi wake Mathayo 9;35,marko 6;34,aliwajua wanafunzi wake  na wanadamu Yohana 2;24-25 alilijua vizuri somo lake na kile alichokuwa akikifundisha Luka 2;42-47,52, Mathayo 7;28-29 alijua namna za njia za kufundisha na kuzitumia aliongoza alishirikisha alidhibiti na kuweka mipango
·         Aliishi kile alichokuwa akikifundisha matedno 1;1 1Koritho 1;11 mwalimu mwema anaishi kile anachokifundisha

KAZI ZA YESU KRISTO DUNIANI

MATESO YA YESU KRISTO NA KIFO CHAKE
Yesu Kristo alifanya kazi nyingi sana lakini kazi moja ya mughimu ilikamilishwa klatika kifo chake cha mateso pale msalabani ambapo aliklufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu Mathayo 1;21, Yohana 1;29 hii ni kazi iliyoleta upatanishi wa wanadamu kwa Mungu na pia kufufuka kwake na kupaa kwake Mbinguni kunawakilisha utendaji endelevu wa kazi nyingine anazo zifanya Kristo huko anatuombea kama kuhani Warumi 8;34,4;25,5;10
Kufa kwa Yesu Msalabani
a.      Umuhimu wa kifo cha Yesu Msalabani
Kiini kikubwa cha injili na mafundisho yote ya agano jipya kinaweza kuhitimishwa kwa neno Kristo alikufa kwa ajili yetu 1Koritho 15;3, Martin Luther alisema hii ndiyo tofauti kati ya ukristio na imqani nyingine zote duniani  na kiini cha uprotestant ni katika fundisho la akzi ya msalabani hivyo kuelewa fundisho sahii la Msalaba ni huruma za Mungu kwa wanadamu ili wapate Msamaha
b.      Maana ya kifo cha Kristo msalabani
Kuna uhusiano wa Muumba na uumbaji wake yaani mwanadamu ambaye aliumbwa na Mungu wana mahusiano lakini mahusiano hayo yaliharibika na hivyo kulihitajika upatanishi kwa njia ya damu ya mwadamu mwenye kumtii Mungu kwa asilimia zote asiye na doa mwenye ujuzi kumhusu Mungu na mwanadamu ili afanye upatanishi kwani kwa juhudi za kibinadamu ni muhimu kufahamu kuwa mwanadamu hawezi kamwe kufuta historia yake kuhusu dhambi na hatia wala kuiondoa au kuizuia na hivyo ilikuwa ni lazima Kristo mwenye sifa za kiungu na kibinadamu afe kwa ajili ya kazi ya kuwapatanisha wanadamu kwa Mungu Yohana 1;35
c.       Yesu aliteseka na alikufa pale msalabani

Mazingira ya kifo cha Msalabani kwa Yesu.
    Yako madai kutoka kwa wanaharakati wa kiislamu kuwa Yesu alikuwa na afya nzuri na ndio maana aliweza kufunga siku arobaini na kutembea kwa miguu sehemu mbalimbali, na kutokana na mazingira ya hukumu ya kifo cha msalabani kilikuwa ni kifo cha polepole isingekuwa rahisi Yesu kufa msalabani mapema na ushahidi ni kwa wale wahalifu wengine waliolazimika kukatwa miguu ili wafe mapema.
      Nataka kuwajibu waislamu hoja hii kwa ufupi kuwa wahalifu wale wengine wawili walibeba misalaba yao na kwenda kusulubiwa moja kwa moja bila mateso ya aina yoyote mbadala. Lakini kwa Bwana Yesu yeye alikamatwa Mapema alfajiri katika siku hii hatuambiwi kama alihudumiwa kwa chakula au la? lakini bila shaka wafungwa wale wengine walihudumiwa gerezani kama kawaida, akiwa hajala kitu alianza kuteswa (Mathayo 26;67),Tunaambiwa kuwa alipigwa makonde na makofi,hatuambiwi ni kwa kiasi gani,Pia tunaambiwa kuwa alipigwa mijeledi ambayo kwa mujibu wa Historia Enzi za Warumi, Mtuhumiwa
alivuliwa nguo zote na kuwambwa kwenye nguzo au kuinamishwa kwenye nguzo fupi na kufungwa mikono yake na kuchapwa na kifaa maalumu,Kifaa hiki cha kuchapia yaani mjeledi kilikuwa ni kifaa chenye Mpini mfupi wa mbao ambapomikanda kumi na mbili ya ngozi iliambatanishwa ikiwa na vipande vya chuma au mifupa iliyofungwa kama shanga kwenye kila mkanda,vipigo vilifanywa na wanaume wawili mmoja upande huu na mwingine upande huu,Kipigo hicho kilipelekea nyama ya mwili kupurwa au ku katwa katwa kiasi cha kuweza kuathiri mishipa ya fahamu,vena na ateri na hata kuumiza viungo vya ndani vya vya tumbo na wakati mwingine vilitoka nje jambo hili pekee lilifanya watuhumiwa wengi kufa  wakati wa kupigwa mijeledi,Mijeledi ilikuwa inaharibu kabisa sura ya Mtu ukweli ilikuwa ni adhabu yenye kutisha sana,Inawezekana kabisa kushindwa kwa Yesu kuubeba msalaba wake na kuanguka mara tatu na hatimaye kusaidiwa na Simon mkirene kulitokana na kuchoshwa na kipigo cha mijeledi alichopata (Math 27;32,                        ),Achilia mbali kule kusimikwa kwa taji la miiba kama mfano wa taji kichwani ambapo kulitoboa maeneo ya kichwa na mishipa,kubeba ule msalaba,Na baadae kugongomelewa masumari mazito ya chuma yenye umbo la mraba miguuni na kusimamishwa na kuchuruzika madamu kwa masaa masaa tkribani sita hivi,misuli inavutwa Ngozi inaharibika,huku kukiwa na dhihaka na matusi na shutuma ili kuteswa kiakili katika hali kama hii hata kama ulikuwa unalia huwezi kulia tena  ni rahisi kuhisi kuwa Mungu amekuacha! Acha kiu ya maji ambayo kwa mateso kama haya mtu alalamika kua ana kiu maana yake kutokana na kumwagika kwa damu nyingi akiomba maji akinywa anakufa(Yohana 19;28).hivyo kuomba maji kwa  Yesu kunaashiria alikuwa amefikia hatua ya kukata roho na kwakweli ALIKUFA!. Mateso haya kwa kweli yalichangia Yesu kufa mapema kuliko wale wengine.
       Pamoja na mateso hayo yoote aliyoyapata Masihi ambayo yalichangia kufa kwake mapema kabla ya wale wawili,Inashngaza eti kuona wahubiri wa kiislamu wanakosa shukurani na kugundua Upendo mkuu aliokuwa nao Yesu kwa ajili ya ulimwengu na wao pia  badala yake wandhihaki kazi hii ya huruma kwa wanadamu na wanafanya jitihada za kuipinga kazi hii kwa makusudi hii ndio shukurani wanayomlipa Mungu kuupinga msalaba jaribu kuwaza ni hukumu gani itawapata watu wa jinsi kama hii kwa kushindwa kumuamini Yesu na kushikamana na marehemu Muhamad na kusahau kuwa mateso ya Kristo yalikuwa ni kwa ajili yao.
    (Isaya 53;2b-5). “…Yeye hana umbo wala uzuri, Na tumuonapo hana uzuri hata tumtamani, Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko; Nakama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu,Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu, Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,amepigwa na Mungu na Kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu. Alichubuliwa kwa Maovu yetu, Adhabu ya amani Yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona….”
           
                                             Pichani Mchoro kuonyesha jinsi Yesu alivyopigwa mijeledi

Isaya nabii alitabiri vema na kuonyesha wazi kuwa ni kifo cha namna gani Masihi angekufa soma aya hizo hapo juu za unabii wa Isaya kumhusu masihi, Hivi karibuni wataalamu wa biblia walifanya utafiti wa kutosha kuhusu Mateso yaliyompata Masihi na kujaribu kuyaigiza katika filamu iitwayo “The passion of Christ”Tunaweza kusema kuwa lile kilichoigizwa katika filamu ile ni sahihi kabisa na kuna uwezekano kuwa mateso hayo yalikuwa zaidi ya kile kilichoigizwa,Lakini lile wazo la nabii Isaya limeweza kufikiwa kwa aslimia zaidi ya themanini!
                                   
 Pichani juu ni muigizaji maarufu wa filamu “The passion of the Christ” akiigiza kwa karibu sana aina ya Mateso aliyoyapata kristo ndugu huyu amejipatia sifa kubwa kwa uigizaji unaokaribiana na kile Biblia inachosema.(Picha na  Maelezo Na Rev. Innocent Samuel Kamote Mwandishi wa somo hili. 2007.)

KUFUFUKA KWA YESU KRISTO
Ufufuko wa Yesu Kristo  ni miujiza mkubwa sana kwa ukristo  miujiza mingine yote katika injili ingekuwa haina maana kama miujiza huu haungelifanyika  na kwa sababu hii imani yetu ya ukristo inasimamama katika kufufuka kwake Yesu Kristo
·         Kifochake kisingekuwa kinafaa kwa upatanishi
·         Ukristo ungekuwa ni uongo  na wahubiri wangekuwa wamehubiri makosa
·         Lakini ashukurtiwe Mungu kuwa Yesu Kristo amefufuka na kuna ushahidi mwingi katika Maandiko lakini muda usingeweza kutosheleza kuyapitia 1Koritho 15;14-20
·         Uko ushahidi wa Maandiko kadhaa ya kinabii na yaliyotimizwa kuhusu kufufuka kwa Yesu zaburi 16;8-10,zaburi 30,3,41;10 marko 16;6-7matedno 2;27-31,13;33-35,zaburi 49;15,Hosea 6;2,118;17,Mathayo 28;5-7,Luka 24;36-48 Yohana 20;19,24-29 !koritho 15;17,20,Wafilipi 3;21

     Pichani juu ni kaburi alilozikwa Bwana Yesu kisha akafufuka,liko wazi hata leo,Watu wengi huenda mahali hapo kwa shughuli za kutalii tu .Eneo hili huitwa Garden Tomb,Yaani Bustani ya Kaburi,Mungu amepatunza mahali hapa hata leo hii ili watu wapate kusadiki kuwa Yesu yu hai.Picha na Maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote,

Kupaa kwa Yesu Kristo
·         Kupaa kwake mbinguni kulikuja kwa sababu wakati wake ulikuwa umewadia 
            Kule mbinguni Yesu ametukuka sana
·         Aliridi kule alikokuwa Yohana 17;5 ni bwana na matawala mwenye mamlaka yote
·         Ushahidi wa kimaandiko kuwa Yesu alipaa zaburi 16;10-11,Marko 16;19,Yohana 20;16-17.Mathayo 28;9 , 1Koritho 15;4, Zaburi 68;18, Luka 24;50-51 Matendo 1;9-11Zaburi 24;1-10, Efeso 4;8, Yohana 6;62,7;33,13;33,14;28-29, Zaburi 118;17-20, Waebrania 4;14,9;24
·         Kupaa kwake kumemuwezesha kufanya kazi ya kutuombea na kuandaa makao

SURA YA TATU; WAKATI HUU NA KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI
Kazi za sasa za Yesu Kristo
Ule ukweli kwamba Yesu alipaa mbinguni ambao umethibitishwa katika injili na Matendo ya mitume na nyaraka ni wazi kuwa kuna kazi anazozifanya Yesu kwa sasa, Yesu aliacha ulimwenfu huu na kurudi kwa baba yake kwa wakati alirudi katika ulimwengu amabao kwamba alikuweko kama alivyokuja kwa njia ya miujiza wa kimungu pia alipaa kwa miujiza wa kiungu tedno hili linatufundisha mambo kadhaa yafuatayo
A.     Yesu ametukuzwa Mno
Yesu kupaa mbinguni zinatumika lugha mbili kuu kwanza alipaa mbinguni na pili akachukuliwa juu mbinguni Lugha hizi zinatumika  kwanza kuonyesha kuwa ilikuwa ni kwa mapenzi yake yeye mwenyewe alipaa na pili ilikuwa ni mapenzi ya baba yake yeye kupaa si kuwa mbingu kilikuwa ni kitu kipya kwake lakini ametukuzwa kwa maana ya kuwa amerudi katika utukufu ule aliokuwa nao kwanza Yohana 17;5 si hivyo tu bali akiwa ametimiza Jukumu kubwa la kiungu la kumkomboa mwanadamu Waebrania 12;2 jambo amabalo limeleta furaha kubwa sana mbinguni na ni kwa ajili ya furaha hii tunasema Kristo ametukuzwa mno huko mbinguni, Kristo alirudi katika hali ya matumizi ya mamlaka kamili ya kiungu yote ya mbinguni na duniani Mathayo 28;18,Efeso 1;20-23,1Petro 3;22,Wafilipi 2;9-11,Ufunuo 5;12
B.     Yesu amekuwa Bwana juu ya yote
Kwa kupaa kwake Mbinguni amekuwa kichwa cha kila Mwanadamu 1Koritho 11;2,amekuwa juu ya falme na mamlaka kolosai 2;10 amekuwa juu ya mamlaka zote zisizoonekana 1Petro 3;22,Warumi 14;9 na Wafilipi 2;10-11 huko anamiliki ubwana wa ulimwengu mzima na Mungu ameweka kila kitu chini ya miguu yake  na pia amekuwa Kichwa cha kanisa
C.     Yesu anaandaa makao
Kujitenga kwa Yesu Kristo na kanisa lake kulikotokea baada ya kupaa kwake sio mwisho wa kila kitu au sio kwa kudumu  lakini huko qanaandaa makao ili kwamba kule atatkakokuwako na watumishi wake wawezekuweko Yohana 12;26 na pia anakuwa kama Bwana harusi ambaye yuko kwenye maandalizi ya kuja kumchukua bibi harusi ambaye ni kanisa
D.     Yesu anafanya kazi za kikuhani
Kwa kuopaa kwake Mbinguni Yesu Kristo kama kuhani mkuu ameingia patakatifu pa kimbinguni ili kutuombea na kufanya upatanishi wa dhambi kwa ajili yetu yeye sasa ndiye mpatanishi pekee kati ya Mungu na wanadamu 1Timotheo 2;5, Kutuomea ni kazi muhimu sana anayoifanya Kristo huko mbinguni Warumi 8;34 kwa msingi huo hata kupaa kwake mbinguni ni kwa ajili yetu ,Shetani ni mshitaki wetu kwa msingi huo tunapotenda dhambi hupeleka hoja za kuonyesha madai kuwa hatufai tena kwa Mungu lakini kwa ushirikiano wetu na Kuhani mkuu tunapomueleza kwa njia ya Toba yeyey hufanya upatanishi kwa kutuombea anagalia 1Yohana 2;1-2 “Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki. Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.”
E.      Yesu Kristo anakuwa na sifa  ya kuwako mahali kote kwa wakati mmoja
Alipokuwa duniani Yesu Kristo alikuwa na mipaka ya kibinadamu iliyomlazimu Kuweko kule Israel tu Yohana 14;12 Yeye anapokuwa Mbinguni kwa baba sasa anaweza Kuweko mahali kote kwa wakati mmoja Omnipresent kwa hivyo kwa kupaa kwake sio tu amepewa Nguvu zote lakini amekuwa na uwezo wa Kuweko mahali kote Mathayo 28;18,20

KAZI ZA BAADAYE ZA YESU KRISTO
Kristo Yesu atakuja tena Fundisho kuhusu kuja tena kwa Yesu Kristo limetajwa mara 300 hivi katika agano jipya pekee, Paulo mtume pekee amahitimisha katika nyaraka zake mara 50 hivi akitaja kuhusu kuja kwa Yesu mara ya pili duniani, kuja kwake mara ya pili kuetajwa mara 80 hivi na kumerudiwa kwa uwazi kzaidi katika Wathesalonike 1&2 Mathayo 24, na Marko 13 ni vitabu vinavyowekwa wakfu kwa habari ya kuja kwake mara ya pili kuja kwa Yesu mara ya pili kimegawanyika katika sehemu kuu mbili
1.      Kunyakuliwa kwa kanisa Rapture au Parousia “ Parousia
2.      Kuja mara ya pili duniani Revelation
Kunyakuliwa kwa kanisa Rapture.
·         Kristo atakapokuja kwa ajili ya kanisa hatakanyaga ardhi ataishia hewani au mawinguni na kulinyakua kanisa yaani watu wake wanaomcha yeye kutoka kila pembe ya dunia na dhehebu
·         Ujio huu ni wa ghafla kama mwivi na si kila jicho litamuona swala hili litafanyika kabla ya gharika kwa mujibu wa imani Orthodox hata hivyo wako watu wengine wanaoamini tofautina hivyo kufanya Kuweko kwa dhana kama nne hivi za ungakuo amabazo ni
1.      Kunyakuliwa baada ya dhiki (PostTribulation View)
2.      Kunyakuliwa wakati wa dhiki au katikati ya dhiki (Midtribulation view)
3.      Kunyakuliwa kwa awamu (Partialtribulation View)
4.      Kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu (Pretibulation view)
·         WaOthodox wenye imani sahii wana amini kuwa kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki ile kuu kwani ndicho tunachosubiri kwa sasa 1Thesalonike 4; 13-18,5;1-7, 1Koritho 15;52, tukio la unyakuo litakuwa la ghafla ni kama kufumba na kufumbua ,litaambatana na kufufuliwa kwa wafu watakatifu na kuungana na watakatifu walio hai watakaobadilishwa mioyo na kumlaki Kristo mawinguni  na tutakuwa naye mawinguni na kupewa tahwabu na kusha kualikwa kwenye karamu ya mwana kondoo Baada ya kupewa taji za haki huku duniani dhiki kuu itakuwa ikiendelea na mwishoni ndipo Kristo atarudi na watatkatifu wake duniani hapo itakuwa dhahiri na sio kwa wizi
Kuja Mara ya pili kwa Yesu duniani Revelation
Hili ni tukio litakalokuwa waziwazi kwani kila jicho litamuona Kristo atarudi na kukanyaga ardhi mahali pale alipopaa kwenda mbinguni katika mlima ule wa mizeituni tukio hili ni la Kristo kuja na watakatifu wake kwa ajili ya utawala wa miaka 1000 hapa duniani kuja kwake huku kutaambatana na kuuawa kwa Mpinga Kristo na nabii wa uongo pia kutiwa kifungoni kwa Ibilisi miaka 1000 ufunuo 19; 20 ujio huu utakuwa na sifa nyingi kama zifuatazo
·         Utakuwa ni halisi Kriosto mwenyewe ataonekana  Yohana 14;3,Matendo 1;10-11,1Thesalonike 4;16,Ufunuo 1;7 Zekaria 14;4
·         Haitakuwa kwa wizi itakuwa waziwazi Waebrania 9;28,Wafilipi 3;20,Zekaria 12;10
·         Itakuwa kwa utukufu mkubwa sana Mathayo 16;27,2Thesalonike 1;7-9,Kolosai 3;4Mathayo 25;31
                                      
Mahali hapa ndipo ambapo Inasadikiwa Yesu alipaa kwenda Mbinguni Pale Yerusalemu katika mlima wa mizeituni,mahali hapa Yesu aliacha nyayo zake na zimetunzwa kitaalamu hata leo kachumba haka katikamlima wa mizeituni ndiko kanakotunza nyayo hizo za mwisho Yesu alipopaa kwenda Mbinguni atakaporuidi atakuja katika mlima huu wa mizeituni Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya  Mchungaji Innocent Samuel Kamote.
Siku ya kurudi kwa Yesu
Wako watu waejaribu kuweka sawa hesabu zao kujaribu kujua kuwa Yesu anakuja lini  lakini waliaibika vinaya kwani Maandiko yanaeleza kuwa siku ya kuja kwake imeficha katika Hekima ya mungu  Mathayo 24;36-42,Marko 13;21,22, hakuna mtu ajuaye siku ya kuja kwa Bwana kimsingi hata mitume waliokuwa na mafunuo makubwa hawajawahi kujidfai kuwa wanajua kuwa Yesu anakuja lini lakini tumepewa dalili za kuja kwake ikiwa Hata Yesu kama Mwanadamu na Nabii mkuu alisema haijui siku hiyo kujifanya unaijua siku hiyo ni kiburi cha wazi cha kujifanya unajua kuliko mitume siku hiyo itakuwa ghafla 1Koritho 15;52,Mathayo 24;27 na haitategemewa 2Petro 3;4Mathayo 24;48-51Ufunuo 16;15
Kristo alitoa dalili nyingi sana za ujio wake hizi ndio za muhimu kwetu kuziangalia na kujiandaa mioyoni mwetu
*      Injli itahubiriwa kwa mataifa yote kuwa ushuhuda Luka 19;11-27Mathayo 24;14
*      Atachelewa kiasi ambacho kanmisa watashangaa kwanini amechelewa Luka 18;1-8
*      Wengine watajiandaa na wengine watapuuzia na kukata tamaa Luka 12;45Mathayo 25;19,6
*      Hakuna ajuaye siku wala saa atakayokuja mwana wa Adamu Mathayo 24;36,42,50
*      Atakuja ghafla na kuhukumu watumishi wake kulingana na kazi zao Mathayo 25;19 na 2Koritho 5;10
*      Watu watakuwa wakila na kunywa wakioa nakuolewa kama siku za Nuhu Mathayo 24;37-39 na siku za sodoma Luka 17;28,29
*      Atakuja kwa utukufu mkubwa na nguvu na hukumu kuja kuutawala ulimwengu na mataifa yote ya Dunia Mathayo 25;31-46
Makusudi ya kuja kwake
1.      Kwa ajili ya kanisa lake atawanyakua kabla ya ujio kamili wa kuja kuitawala dunia
2.      Kwa ajili ya mpinga Kristo  kumuhukumu kwa ajili ya uovu dhidi ya Israel na ulimwengu na dini potofu pia kujitukuza kwake juu kama Mungu na kwa ajili ya mateso makubwa jkwa wanadamu na hasa wale wanaoamini katika Mungu wa kweli 1Yohana 4;3,2;18,2;22,2Thesalonike 2;3Ufunuo 13;1,Daniel 7;8,25,Ufunuo 13;16-17,17;1-15
3.      Kwa ajili ya kuhukumu mataifa ,kila taifa la dunia litahukumiwa  na kila mtu atawajibika kwa mfalme wa wafalme Daniel 2;44,Mika 4;1,Isaya 49;22-23,Yeremia 23;5,Luka 1;32,Zekaria 14;9,Isaya 24;23,Ufunuo 11;15
4.      Kwa ajili ya kutwawala dunia miaka 1000 wakati wa millennium Zaburi 2;7-9,72,Isaya 11;1-9 Ufunuo 20;6.

YESU KRISTO KATIKA MITAZAMO TOFAUTI YA KITHEOLOJIA
Ziko dhana mbalimbali ambazo muda susingeweza kutosha za watu na wanatheolojia mbalimbali kumhusu Yesu Kristo ni muhimu kuwa na ufahamu na kujua namna na jinsi ya kuitetea imani yako baada ya kuwa umejifunza mafundisho haya ya muhimu kuhusu Yesu Kristo
*      Wako wanaoamini kuwa Yesu akishindwa kama watu wengine pale alipokubali kusulubiwa Msalabani  kwa msingi huo tunaweza kujifunza kutoka kwake maisha safi aliyoishi na wema wake lakini tendo la kukubali kudhalilishwa msalabani ni kushindwa vibaya kwa Yesu
*      Wako wengine wanamuona kama mwana siasa,mwana jamii na mwanauchumi
*      Wengine wanamuona mwanadamu wa kawaida tu aliyewahi kuishi duniani au mwana Filosofia au rabi mkubwa aliyepata kutokea katika Israel ambaye wengine walimkubali na wengine walimkataa
*      Apolonarianism hii ni jamii iliyotokana na Apolliaris ambaye alikuwa ni Askofu wa Laodekia kati ya mwaka 361 Yeye alifundisha kwamba Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu lakini akili za kiungu na roho ya kiungu hivyo Kristo alikuwa na mwili wa kibinadamu na akili za kiungu na roho ya                                                                 kiungu



                                                           

                 Mwili wa kibinadamu                                                     akili na roho za Kimungu

*      Nestorianism  hawa walifundisha kuwa kuna aina mbili za utu wa Yesu Kristo zilizo tofauti Kristo wa kimwili na Kristo wa kiroho kwa hivyo Yesu alikuwa Mwanadamu na pia alikuwa Mungu  fundisho hili liko tofauti na mtazamo wa kibiblia kumhusu Yesu Kristo ambao humuona Yesu kuwa ni nafsi moja kamili
Mwanadamu  Kristo
Mungu Kristo
 


          
           Imani ya wanestorian Kristo ni nfsi mbili Mwanadamu na Mungu

*      Monophyisitism au Eutychianism  walifundisha kuwa Kristo ni mwenye asili moja  kwa msingi huo asili ya kiungu iliungana na asili ya kibinadamu na kufanuya asili mpya moja

 


                             Asili Mpya






                                                                                           Asili ya kimungu


              Asili ya kibinadamu

Eutychianism wana amini kuwa Yesu ni muungano wa asili mbili uliozaa asili mpya.



SURA YA NNE; UUNGU WA YESU KRISTO
Kwa kumalizia somo letu la Christology ni muhimu kwetu kuhitimisha kwa kusema kuwa Yesu sio tu alikuwa mwanadamu kamili lakini pia ni Mungu kamili ingwa hakuna andiko linalothibitisha moja kwa moja lakini neno lile Incarnation limetumiwa na kanisa kwa Muda mrefu kuonyesha wazi kuwa Yesu ni mwanadamu na ni Mungu au ni Mungu katika mwili tunaweza kugundua kuwa Yesu ni mungu kwanza kwa kuangalia mambo ya msingi yafuatayo

Ana sifa zote ambazo kwa kawaida ni sifa za Mungu peke yake

1.      Ni mwenye nguvu zote His Omnipotence (He is all Poweful).
    Sifa hii ya kuwa na nguvu zote sio ya kibinadamu ni sifa ya Mungu tu viko vitu vingi duniani vina nguvu hata shetani ana nguvu ,miungu ina nguvu,mapepo na wachawi wana nguvu na vitu mbalimbali vina nguvu lakini havina nguvu zote Yesu alitabiriwa kuwa na nguvu zote na alitimiza sifa ya kuwa na nguvu zote, Zaburi 110;3,Nahumu 1;3,Luka 4;14-15,8;54-55,Isaya 40 ;10,Waefeso 1;20-23,Isaya 50;2-3,mathayo 28;18,Ayubu 42;2,Mwanzo 18;14 Mathayo 19;26,zaburi 107;25,Mathayo 8;26-29.

2.      Ni mwenye kujua yote His Omniscience (He is all Knows).
    Hakuna mwanadamu mwenye kujua yote sifa ya kujua yote ni sifa ya Mungu pekee lakini Maandiko yanamuonyesha Yesu kuwa anajua yote unaweza kuulizwa kwanini Yesu alipoulizwa siku ya kuja kwake alisema siku ya kuja kwake hakuna aijuaye? Yesu alijibu kwanza kama mwanadamu, lakini siku ya kuja kwa bwana Mungu katika Hekima yake aliamua kuifanya kuwa siri na hatupaswi kuhoji kwa nini lakini kama Yesu alikuwa haijui siku hii angewezaje kutupa dalili za kuja kwake kama mtu anaweza kukupa dalili kamili za ujio wake ni wazi alikuwa anajua siku ya kuja kwake kama Mungu, aida ifahamike pia kuwa nilisema mwanzoni katika somo hili Nafsi zote za Mungu zina wajibu wake Mungu baba hushughulika na majira na nyakati na mipango na kwa sababu hizo Yesu kila mara alikwepa kujibu maswali yanayohusiana na majira na nyakati au mipango Mathayo 24;36,Matendo 1;6-7, Yesu majukumu yake ni ya ukombozi na wokovu, na Roho majukumu yake ni maongozi na nguvu kwa msingi huu basi hayo hayamaanishi kuwa yesu hajui yote Yesu anajua yote Mithali 8;14,Isaya 11;2,Mathayo 9;4,12;25,Luka 6;8,22;10-13,Yohana 6;64,18;4,Ayubu 37;16,Zaburi 145;5 1Yohana 3;20 kolosai 2;3Mithali 15;3,Yohana 1;48,zaburi 139;2-4,Yohana 4;16-19,28-29,Yeremia 17;9-10,Yohana 2;24-25.
3.      Yuko kila mahali kwa wakati mmoja His Omnipresence (He is Everywhere in one time).
Hakuna mwanadamu mwenye sifa ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja wala malaika ghata shetani mwenyewe hana uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja bali huzungukazunguka, Kristo alipokuwa Duniani hakuwa na uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja kwa sababu alikuwa mwanadamu lakini kwa kupaa kwake mbinguni na kuirudia enzi ameweza kuwa na sifa ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja hii ni sifa ya Mungu pekee na Yesu alikuwa nayo Zaburi139;7-10,Mathayo 18;20,Yeremia 23;23-24, Mathayo 28;20,Ufunuo 21;2,3,10,22-23, Mika 5;2Yohana 14;20,1;1Kolosai 1;1

4.      Yesu ni wa milele He is eternal 

Waebrania 13;8, Ufunuo 1;17, Ni muhimu kufahamu kuwa viumbe vyote vina Mwanzo na vina mwisho hata shetani ana mwisho kwani atatupwa jehanamu ya moto lakini sivyo ilivyo kwa Yesu Kristo yeye amekuwako tangu milele Yohana 1;1 sifa ya umilele ni ya kimungu pekee na siyo ya kibinadamu wala malaika kwani wao walikuwa na mwanzo Mungu hana Mwanzo wala mwisho yeye yuko siku zote milele nyuma na milele mbele Mika 5;2, Yeye ni alfa na omega Ufunuo 1;11

5.      Yesu Kristo habadiliki He is Unchangeble
Waebrania 13;8 pia humaanisha kuwa yesu ni yeye yule jana leo na hata milele si kuwa andiko hili linaonyesha kuwa Yesu ni wa milele lakini pia linaonyesha tabia ya Mungu ya kutokubadilika badiliko  Mungu alipojifunua kwa Musa na Musa kumuuliza jina lako ni nani Yeye alijibu mimi Niko ambaye Niko  maana yake ni kuwa atakuwa kama atakavyokuwa au yeye ambaye kweli yuko kutoka 3;15 hii ni sifa ya Mungu wanadamu hubadilika badiliko hata malaika walibadilika na kuacha kumtii Mungu wakawa mapepo kwa msingi huu tabia ya kubaki kuwa mkeli na ya Mungu pekee na Yesu anayao.

Anauwezo wa kusamehe dhambi
Kwa kawaida mwanadamu anapotenda dhambi huwa hamkosei mwanadamu mwenzake tu hayta pale inapotokea kuwa kosa hilo amelifanya kwa mwanadamu mwenzake lakini kama Mungu alikataza kosa hilo lisifanyike kwa wanadamu wenzake unakuwa umemkosea Mungu Daudi alionyesha wazi kuwa alimkosea Mungu pekee Zaburi 51; 4 “ Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya uovu mbele ya  macho yako” Kwa msingi huo dhambi hutendwa kumuelekea Mungu peke yake na hivyo kama tunahitaji Msamaha lazima Msamaha huo utoke kwa Mungu pekee soma Mathayo 6;12a “utusamehe makosa yetu” hii ni sehemu ya sala ya bwana kumuomba Mungu atusamehe kwa msingi huo Msamaha wa dhambi hutolewa na Mungu tu na wayahudi walilielewa hilo Vizuri Luka 5;18-24 Ni wazi kuwa mwenye uwezo wa kusamehe dhambi ni Mungu pekee Yesu husamehe dhambi hii inamaanisha kuwa yeye ni Mungu

Anakubali kuabudiwa
Wanafunzi wa Yesu walikuwa ni wayahudi na wayahudi walikuwa waeonywa kuwa wasiabudu kitu kingine chochote isipokuwa Bwana Mungu wako peke yake hii hata Kristo mwenyewe alisema Pale shetani alipotaka ibada kutoka kwake Luka 4;5-8 lakini katika namna ya kushangaza Yesu alikubali kusujudiwa na kuabudiwa hii ni wazi kuwa alikuwa Mungu
·         Alisujudiwa na kuabudiwa na mamajusi Mathayo 2;10-12 pia walitoa matoleo
·         Alisujudiwa na wenye ukoma Mathayo 8;1
·         Alisujudiwa na mapepo yaliyokuwa ndani ya mgersi Marko 5;1-15
·         Thomasi alimkiri kuwa Ni bwana na Mungu Yohana 20;26-29
·         Alisujudiwa na kuabudiwa na wanafunzi wake Mathayo 28;9,16-20
·         Anaabudiwa na malaika wote Ufunuo 14;1-5

Kristo ni Mungu kamili
Kwa ujumla agano jipya katika Maandiko mengi sana limemuita Yesu kuwa ni Mungu  au Bwana kwa mamia ya aya na kwa majina mengine mengi yanayoonyesha uungu wakeuemi wake maisha na matedno yake yote yanaonyesha uungu wake  na kuwa Yeye alikuwa Mungu kweli au Mungu wa kweli  wakolosai 1;19 inasema hivi Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote wa Mungu ukaye Biblia nyingine za Kiswahili zimeruka neno hilo Mungu  na ujio wake duniani ni kwa ajili yetu ili kuwa Mungu akae au apatane na sisi na kurudisha uhusiano wake kwetu ili kutimiza unabii ya kuwa yeye ni Immanuel uyaani Mungu pamoja nasi Mathayo 1;23 ‘Tazama bikira atachuikua mimba naye atazaa mwana  nao watamwita jina lake Immauel yaani Mungu pamoja nasi’Paulo mtume alimwita Yesu Mungu mkuu na mwokovu wetu Tito 2;13 kwa msingi huo ni muhimu kuhitimisha somo hili kwa kusema kuwa Yesu ni Mungu!
Na kama tunakubali kuwa Yesu ni Mungu basi ni muhimu kulikumbuka hili kuwa hatuwezi kumfahamu Mungu kwa asilimia 100 tukiwa na akili hizi za kibinadamu kwani Mungu ni mkubwa kuliko akili zetu take care!
somo na Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!

Maoni 1 :