Jumatano, 20 Mei 2015

Familia Chini Ya Uvamizi (Family Under Siege)


Nyakati hizi tulizo nazo ni nyakati za mwisho sana, Biblia inaziita nyakati hizi kama nyakati za hatari “2Timotheo 3:1-5”Katika nyakati hizi za mwisho moja ya matatizo makubwa sana yatakayosumbua ulimwengu ni pamoja na matatizo ya kifamilia, ni muhimu kufahamu kuwa nshetani atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa anazishambulia familia kwa kadiri awezavyo ili kuwavuruga wanadamu na kuharibu mpango na makusudi ya Mungu. Tutajifunza somo hili FAMILIA CHINI YA UVAMIZI kwakuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-


  • ·         Familia ni Mpango wa MUngu.
  • ·         Uvamizi Katika Familia (Family Under Siege).
  • ·         Jinsi ya Kuilinda na kuiponya Familia.

Familia ni Mpango wa Mungu

Kabla hatujaanza kuangalia kwa undani kuhusu uvamizi katika familia ; ni muhimu kwa kila mmoja kuwa na ufahamu kuwa Familia ni Mpango wa Mungu, kutokana na vipingmizi mbalimbali tunavyokutana navyo wanadamu tunaweza kufikiri kuwa labda sio mpango wa Mungu kwangu au kwetu kuwa na familia, lakini ni muhimu kuyajua maandiko ambayo yanatukumbusha kuwa familia ni Mpango wa Mungu.

       Kaini akimuua Habili Nduguye

1.       Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu ndiyi aliyemuumba Mwanadamu Mwanzo 1:26-27
2.       Mungu alimuumba mwanadamu ili awe na uhusiano Mwanzo 2:18
3.       Mungu alimuumba Mwanadamu ili awe na uhusiano naye Mwanzo 3:8
4.       Mungu alikusudia mwanadamu awe na Hisia kali dhidi ya jamii yake Mathayo 19:4-6
5.       Mungu alikusudia Jamii iongezeke Mwanzo 1:28, Zaburi 27:3-5
6.       Mungu alikusudia watoto walelewe na familia na sio mitaani 1Timotheo 5:8
7.       Mungu alikusudia Familia iwe ndio shule ya kwanza ya kujifunza uadilifu Mwanzo 18:17-19
Hata hivyo kwa kufahamu kuwa familia ni taasisi muhimu, shetani amekuwa akizishambulia familia na kuziweka chini ya ulizni wake kwa kujua kua akifanya hivyo ataharibu Jamii, taasisi. Kanisa, taifa na ulimwengu kwa ujumla!

Uvamizi Katika Familia

Tunapozungumzia uvamizi katika Familia tunazungumzia Kiswahili cha zamani KUHUSURU kwa kiingereza SIEGE. Kuhusuru ni uvamizi unaofanywa na jeshi katika vita za zamani ili kuwabana watu walioko mjini kwa muda mrefu wasiweze kutoka au kuingia mpaka wadhoofike na hatimaye kuwangamiza kabisa kwa urahisi!

SIEGE  - “According to Oxford Advanced Learners dictionary is  A military Operation in which an army tries to capture a town by surrounding it and stopping the supply of food etc to the people”
Shetani makusudio yake kwa familia ni mabaya, analeta mashambulizi na kuzibana familia kila kona ili kuleta uharibifu mkubwa,
Shetani katika karne hii amafanikiwa kuharibu familia kiasi ambacho miaka michache ijayo kutakuwa na hali mbaya zaidi

Amefanikiwa
·         Kuwafanya wazazi kuwa mbali na watoto wao
·         Amefanikiwa kuharibu utawala na Mamlaka katika familia kupitia Usawa na haki
·         Amefanikiwa kuwafanya wanaume kwa wanawake kuwa na pilikapilika za kutafuta maisha
·         Misuguano katika maswala ya fedha
·         Amefanikiwa kuwafanya watoto wengi sana waishi mitaani na kukosa malezi
·         Amefanikiwa kuwaangamiza wengine mapema kwa kusababisha n utoaji wa mimba
·         Ameingiza utasa na ugumba katika familia nyingi kinyume na Baraka za Mungu
·         Amefanikiwa kuwafanya watoto wengi wasitii, ameleta magonjwa,Hofu, kutokuaminiana,ubinafsi, choyo, umimi,  na kukosa uaminifu
Shetani katika mpango wake huo amekusudia kuharibu mpango wote wa Mungu kabisa na kuwa kinyume na familia Biblia inatukumbusha kuwa tutapoyaona hayo hatupaswi kufikiri kuwa ni kitu Kigeni 1Petro 4:12 Biblia imejaa mifano mingi ya watu ambao shetani alizivuruga familia zao hata pamoja na kuwa walikuwa watu wa Mungu!
-          Familia ya kwanza ilikuwa ya wana wa Mungu mwenyewe Adamu na Eva wao walikuwa wa kwanza kumuasi Mungu ambaye alikuwa ni Baba yao
-          Adamu na Eva walikuwa na watoto wao wa pekee Kaini na Habil lakini walijaa wivu na kuchukiana na kaini aliamua kumua nduguye?
-          Nuhu alikuwa Mtu wa haki alikuwa na wana watatu Hamue, Japhet na Shemu Lakini Hamu alimvinjia Heshima Baba Yake
-          Ibarahimu alikuwa na Ishmael na Isaka lakini Ishamel alimnyanyasa na kumdhihaki nduguye
-          Lutu alizaa na Binti zake
-          Isaka alimpenda Esau Rebeka akampenda Yakobo na kusababisha mgawanyiko katika familia
-          Esau na Yakobo walifanyiana mambo ya hiyana na Esau alikusudia kumuua nduguye
-          Reuben alimkosea Heshima Baba Yake, Pia wana wa Isarael walitaka kumuua Yusufu Ndugu yao na kuamua kumuuza huko Misri
-          Musa, Mkewe alishambuliwa na wifi yake na shemeji yake yaani Miriam na Haruni
-          Daudi alikuwa shujaa lakini hakuwa shujaa wa kuilinda familia yake aliidekeza na kushindwa kusimamia uadilifu katika familia
Huu ni Uvamizi katika Familia, hali ni mbaya leo ziko familia zinagombania Urithi, Mali na kadhalika, watu hawajifunzi kuwa na vyao, ziko familia nyingine watu wanaombea mpaka maiti, au watu wanaapizana usiisogelee maiti yangu, au uaduia kati ya ndugu na ndugu, watoto wasiotii, leo hii wengine wazazi wanawaogopa watoto wao hufu na wasiwasi umeingia katika Familia hakuna kuaminiana magomvi na Vitimvi, Tendo la Ndoa baya, watu wananyimana, hii yote ni Uvamizi katika Familia! Ni namna Gani tunaweza kupata Uponyaji?

Jinsi ya Kuilinda na kuiponya familia

Kwa kuwa Familia ni Mpango wa Mungu hii ndio zawadi yetu ya Kwanza na ni Mungu ndiye aliyetuchagulia
1.       Ni lazima Mamlaka na Utawala katika Familia Ukawa chini ya Baba Mwanzo 3:16
2.       Lazima watoto wajitiishe chini ya wazazi wao Kutoka 20:12, Efeso 6:1
3.       Lazima Wazai wawafundishe watoto wao njia za Mungu Kumukumbu 6:6-7 Mithali 22:6
4.       Lazima wakubwa wote nyumbani wawe mfano na kielelezo cha kuigwa 2Nyakati 26:3-4
5.       Tuache kujifikiri kuwa tunaweza kuwa na akili kumshinda Mungu ni lazima tulifuate neno lake huu ndio Muongozo wake unaoweza kutusaidia
6.       Mpinge Ibilisi na wala msimpe nafasi, Kemea kila unachokiona sio cha kawaida, Mafno haiwezekani Binti mdogo miaka 9 akaanza kuota maziwa ni lazima ujiulize ya nini? Ni mapema sana
7.       Kemea na kuwa na maombi maalumu ya kifamilia na kama mnaweza kuwa na Ibada za Kifamilia anzisha Ibada
8.       Kuwa na Muda na Familia yako, Mumeo au Mkeo na zungumza naye kwa Lugha njema na tuwaheshimu wazazi wetu na kuwatunza.
9.       Pinga sheria mbaya zinazopitishwa na mataifa makubwa mfano ndoa za jinsia Moja, Haki za utoaji wa Mimba , haki za watoto na wanawake, ni lazima zipimwe kwa neno la Mungu kwanza pamoja na mila na tamaduni zetu zilizo nzuri.
Mungu amekupa wajibu wa Kuilinda na kuitetea Familia yako itetee, ukiyajua Hayo Heri wewe Ukiyatenda
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote.

Maoni 1 :

  1. Ni moja ya somo muhimu sana pata nafasi ya kulipitioa kwa Biblia utaelewa mapenzi ya MUngu hususani katika nyakati hizi tulizo nazo!

    JibuFuta