Jumanne, 26 Januari 2016

MFULULIZO WA MASOMO YAHUSUYO UTETEZI WA IMANI (APOLOGETICS) 6



MLIPUKO WA MFUMUKO WA MADHEHEBU (SECTARIAN MOVEMENTS)

Moja ya maswala ya kuzingatia ni kukumbka kuwa kumekuwako na mlipuko wa Madhehebu mengi ya kiimani katika Urkisto hata hivyo mengi ya madhehebu haya ni sect yaani madhehebu ya Uongo lakini tunawezaje kwanza kujua kuwa dhehebu Fulani ni la Uongo ukweli ni kuwa utagundua kuwa mengi ya hayo yanapotosha imani ya kweli iliyonyooka Orthodox katika theolojia zao na ili kuweza kuzibaini vema ni wazi kuwa dhehebu lolote la Kikristo lililo kinyume na Maswala Saba muhimu yafuatayo hilo liko kinyume na imani iliyonyooka ya msingi Orthodox.
§ 
 Yeyote anayepingana na Utatu
Isaya 48; 16, Mathayo 3; 17,28;19,1Timotheo 2;5
§  Yeyote anayepinga uungu wa Yesu Kristo
Yohana 1;1, 14, Isaya 7;14 Warumi 1;4
§  Yeyote anayepinga uungu wa Roho Mtakatifu.
Yohana 15;26, 16;8,13,14;17,Matendo 2;1-4
§  Yeyote anayekataa kuwa Dhambi ni hali halisi ya mwanadamu
Warumi 3; 10, 23. 14;23; 1Yohana 3;4,5;17
§  Yeyote anayekataa ukombozi kupitia Damu ya Yesu
Efeso 1;7, Wakolosai 1;20, Waebrania 10;12.
§  Yeyote anayekataa wokovu kuwa ni zawadi ya Neema ya Mungu
Efeso 2;8, Yohana 1;12,3;36
§  Yeyote anayekataa kuwa kuna hukumu baada ya kufa
Warumi 6; 23, Waebrania 9; 27,2Thesalonike 1;7,8.

SIFA ZA KAWAIDA ZA IMANI POTOFU CULTS.

Kwa kawaida yako maswala kadaa ambayo yanasaidia kuzitambua imani Potofu zifuatazo ni Alama saba zenye kuthibitisha au kutoa mwanga wa Imani potofu
1.       Maisha ya Mwanzilishi.
-          Je Ni mtu aliyejiweka mwenyewe Madarakani?
-          Je anatumia aina gani ya Jina lenye kujiinua sana Mtume? Nabii? Dr, Mwalimu mkuu au Hata Mpakwa mafuta?
-          Je ni msiri? Ni mwenye kukiri kuwa anauwezo mkubwa na nguvu za kupita kawaida au mwenyu kuona maono makubwa na ndoto au maswala Maruweruwe
-          Kama majibu ni ndivyo hiyo ni Dalili ya kuifahamu imani potofu
-          Imani nyingi potofu hudai kuwa kiongozi wao ni wa kimungu au yuko sawa na Yesu au hupewa Heshima kubwa anazostahili Masihi Yesu.
2.       Ufahamu wake kuhusu Mungu.
-          Swala linine la kujiuliza kuhusu imani hizi potofu ni namna wanavyo kiri ufahamu kuhusu Mungu je wanaaminikatika Utatu
-          Wengine humuona Mungu kama nguvu, au mtesaji au kuwa katili au ambaye sio nafsi
-          Kunaweza kuweko kwa sanamu au alama ambazo zinapewa umuhimu na heshima katika dini hiyo
-          Yesu anaweza kupewa heshima ya mwalimu tu au nabii au msemaji mzuri au moja ya watakatifu tu
-          Roho Mtakatifu hapewi nafasi ya nafisi na huonekana kama Nguvu tu au kuwa hayuko kabisa
3.       Wanaweza kuwa na Maandiko yao au ya viongozi wana na hupewa nafasi kama maandiko
-          Cults mara nyingi zinakuwa na Maandiko yao au maandiko ya viongozi wao ambayo huheshimiwa kama yako sawa na Biblia.
-          Wanaweza kuwa wanaamini kuwa kitabu chao hicho ni cha Muhimu  na cha lazima katika kutafasiri Biblia
-          Wanaweza kudai kuwa wamepewa ufunuo mpya au kweli mpya maalumu kwa ajili yao na huenda wengine hawana
-          Wanweza kusema jambo Fulani kutoka katika Biblia lakini mkazo mkubwa unakluwa katika Vitabu vyao  mfano ni Imani ya Mormonism ambao wana biblia yao inayodaiwa kuwa  ni ufunuo wa Joseph Smith ambaye  alikuwa na madai kuwa anaweka sawa injili iliyokuwa imefichwa
-          Wanaona kuwa chanzo cha maono yao ni cha kuaminiwa, ndoto na maono ni moja ya chimbuko la imani zao
4.       Wana madai kuwa wana kweli isiyopatikana popote.
-          Baadi ya imani potofu hudai kuwa wana kweli ambayo haipatikani sehemu nyingine au wana viwango vya kiroho vya juu zaidi kuliko popote au wanamjua Mungu vema zaidi kuliko wengine
-          Wanaweza pia kudai kuwa wengine wamechakachua kweli lakini wao wanayo injili kamili
-          Wanaweza kudai kuwa nje ya wao wengine ni wazushi, hakuna uhuru, ni giza  ni utumwa
-          Wana weza kuchanganya maswala ya Ukristo na ya kidunia.
5.       Kuna maswala yenye kuleta maswali
-          Mara nyingi imani potofu  zinakuwa na aina za maswala yasiyo ya kikristo yenye kuleta Maswali, wanaweza kuwa na aina Fulani ya mambo ya kuvutia sana au mapambo yenye kuvutia, au aina Fulani ya mavazi ya kuvutia sana ya kidini, au kuwa na mtu maalumu anayewaombea nabii muombezi au mtu maalumu sana
-          Wanaweza kuwa na hirizi au mapete makubwa maalumu,aina Fulani ya uchezaji na ngoma au aina Fulani za maandishi ya kichawi katika ibada zao na kwa siri maswala ya zinaa huweza kujumuishwa katika ibada
-          Wakati mwingine unaweza kuona Vongozi wao wakiwa na roho ya Uzinzi ya kupita kawaida au kuoa wake wengi
6.       Mkazo wa kutambulika kwa Dhehebu lao au kundi lao zaidi.
-          Imani potofu huwa na Tabia ya kujiona Bora  au kuona dhehebu lao kuwa Bora zaidi ya mengine
-          Wanaamuriwa kuwatii viongozi wao Bila maswalai na kutishiwa kulaanika  endapo watafanya hivyo pia kuna kutishiwa endapo utaiacha imani hiyo unaweza kutishiwa hata kifo
-          Wanaonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwasaidia  na kuwapenda wale ambao ni wanachama wapya au kuwaonyesha jinsi wao walivyo muhimu au kuwapa umuhimu Fulani
-          Wanajaribu kuthibiti kila swala la waamini wao ikiwemo ni kitu gani cha kuvaa, nani wa kuoa, na wapi pa kufanya kazi.
-          Wanachkua Muda mwingi sana katika kushuhudia na kufuatilia na wako vizuri katika eneo hilo
7.       Wokovu kwa kazi kubwa
-          Nyingi ya imani Potofu hufundisha wokovu kama unaopatikana kwa bidii za kibinadamu au kwa kushika maswala Fulani ai sheria Fulani na kwa ujumla wazo lao kuu ni wokovu kwa jitihada za kibinadamu
-          Kwa ujumla wanaweza kusema kitu Fulani hadharani lakini wanafanya kingine sirini au wako tofauti na kile wanachokisema wengi kwa mfano hujiita wakristo ingawa ukweli wanaishi tofauti na Ukristo.

KWANINI IMANI POTOFU HUFANIKIWA?
Ziko sababu kadhaa za msingi kwanini imani potofu hufanikiwa na watu wengi hujiunga au kuzikimbilia
1.       Wanatoa majibu ya mahitaji ya watu.
-          Imani nyingi potofu zinatoa majibu kwa ulimwengu huu ambao hauna majibu ya uhakika katika maswala muhimu ya Maisha wanajibu maswali muhimu mfano wewe ni nani na uko kwa sababu gani na wapi unakwenda
-          Kunapokuwa na maswali a kujiuliza kuhusu maisha wakati wote imani potouf zinakuwa na majibu  na kwa ujumla wanajua ni nini cha kujibu wanatoa majibu mepesi  na rahisi kwa mtu ambaye ulimwengu haujamridhisha katika maswala yake  kulingana na hali halisi ya wakati ulioko lakini wakati mwingine majibu yao hutokana na nguvu za giza.
2.       Wanajali wanatoa wanatia moyo wanabidii na wana mvuto wa hali ya juu
-          Wakristo wengi au Ukristo umeshindwa kuwa na hali za kujali, kutia moyo, kuwa na bidii na hata kupoteza mvuto kwa ulimwengu jambo linalopelekewa wengi kuvutiwa na imani hizi potofu zinazozukla
3.       Imani potofu zina mkazo katika Mafundisho na Semina za Neno la Mungu
-          Wanakazia kwa kiwangi kikubwa maswala ya Nidhamu kwa kila mshirika  kinyuma na inavyofanyika kwa wakristo wa kweli
-          Wana uwezo wa kugundua kuwa wengine wamepungukiwa na nini na kujaziliza ili kuwawinda wajinga pia wanaweza kusaidia katika maswala ya kusomesha  na hata kutopa elimu kubwa
4.       Kujitoa na kuhusisha/kushirikisha waamini
-          Kila muuumii hujumuishwa katika utumshi na kushirikishwa  kiasi cha kuwachukulia muda na kuwatawala kimazingira, wanazamishwa  katika mfululizo wa matukio kiasi ambacho wanaweza kukosa muda wa kujihoji kuhusu nini kinaendelea u[pande wa pili
-          Ukatili na hisia zavitisho hutumiwa kama silaha kwa wale wanaoshindwa kujishughulisha vema katka wajibu wao mfano kushindwa kuchangia, kushindwa kuleta washirika wapya, na wanakaziwa kimafundisho kiasi na kivitendo kiasi cha kufikia hatua kuwa unaposhinsdwa kutimiza jambo Fulani unaweza kudhani kuwa umefanya dhambi au unajisikia hatia.
5.       Wana mkazo wa aina yake katika maswala ya ufuatiliaji
-          Imani potofu zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa eneo la ufuatiliaji wa wale wanachama wapya, wengine wanaujuzi mkubwa sana wa kueneza vijarida  vyenye picha nzuri za kuvutia ili kuweza kukunasa na kukuingizia mafundisho yao
-          Wana ujuzi mkubwa na wepesi wa kutumia vyombo vya habari kama tv, Magazeti kaseti za mahubiri na redio na mengineyo kuliko imani zilizo sahii
-          Wana mafundisho yenye maadili mema na wanaakazia na huweza kunasa aina ku mbili za watu wale wanaoitafuta kweli na wale wanaikimbia kweli mara nyingi hujikuta wamenaswa na imani potofu.

JINSI YA KUKABILIANA NA IMANI POTOFU.
Ni muhimu kufahamu kuwa tunapaswa kuzikabili imani potofu au watu wenye imani potofu katika namna ambayo itawakomboa na kuwarejeza katika imani sahii na kuwafanya kufunguliwa toka katika imani potofu 1Petro 3; 15 Yuda 1; 23. Njia kadhaa zaweza kutumiwa katika kuhakikisha tunawarejeza
1.       Kuwaonyesha upendo.
-          Ni muhimu kuwaonyesha upendo kivitendo kwa kufanya matendo ya kikarimu dhidi yao kama kuwapa lifti, kuwatembelea, kuwasaidia swala hili litawaondolea dhana potofu kuwa nje ya kundi lao hakuna upendo na endapo itakupasa kumfuatilia mwenye jinsia tofauti ni muhimu kuwa makini muombe Mungu na uwe mwangalifu ikiwezekana nenda na mtu zaidi hii ni kwa sababu wengi wa imani potofu hawaongozwi na Roho Mtakatifu na weni hawajaokoka.
2.       Usionyeshe kuwavutia katika kanisa lako.
-          Ni muhimu kwanza kuonyesha kuvutiwa na mtu huyo na sio mtazamo wake wala usiwe na haraka ya kuonyesha kumtaka ahamie kwenye imani yako  ni muhimu wakato wote kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu
3.       Uwe hodari katika maandiko.
-          Mtu awaye yote anayetaka kujishuhulisha na kuhudumia waathirika wa imani potofu ni lazima awe hodari katika Maandiko ikiwa na maana ya ujuzi halisi wa kuitafasiri Biblia na kujua kwa haraka ni wapi kuna mtego au andiko limepindishwa  ili aweze kusaidia kuonyesha tafasiri iliyo sahii 2Timotheo 2;15.
4.       Jihadhari na mabishano.
-          Lengo lako kuu ni liwe ni kumleta mtu kwa Yesu au katika Fundisho  lililo sahii ili kuokoa nafsi na lisiwe mabishani ya kimaandiko au mijadala tu
5.       Elewa mitego ya upotofu.
-          Ni muhimu kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu maandiko na mitego inayotumiwa na imani potofu na namna wanavyoitafasiri Biblia  na misamiati yake ili kuthibitisha fundisho lao hii itakusaidia katika kuichanganua kweli
6.       Uwe katika hali ya Maombi wakati wote.
-          Ni muhimu kuwa kaika hali ya kuomba wakai wote  huku ukiwa unakemea na kuwafunga Pepo wa uongo wanaokuwa wamehusika kuwafunga watu katika imani potofu wakati wote huo unapaswa kumtegemea Roho Mtakatifu na kumuomba akuongoze ukiwafungua hao waliofungwa

BAADHI YA IMANI AMBAZO ZINASADIKIWA KUWA NI IMANI POTOFU
1.      
 IMANI POTOFU YA MORMONISM WATAKATIFU WA SIKU ZA MWISHO.
-          Ni moja ya kanisa lenye bidii katika kufanya umisheni Duniani na kama haki ingelikuwa inahesabiwa kwa kutuma wamishionari bsi wao wangestahili haki hiyo wao wametuma zaidi ya wamishionari 18,000 duniani
-          Mwanzilishi wa imani hii aliitwa Joseph Smith Jr. ambaye alizaliwa huko Sharon Vermont U.S.A. 23th December 1805, alikuwa kijana asiyesoma aliyesumbuliwa sana na wingi wa makanisa na madhehebu na alihitimisha kwa kusema hakuna hata moja kati ya hayo lililo sawa
                                                                                                                                                                      
-          Siku ya Tarehe 21 september 1823 alidai kuwa aliona malaika aliyemtaja kwa jina la “Moron” Malaika huyo alimwambia  na kumuonyesha mahali ambapo  angeona Mbao za dhahabu za Neno la Mungu  na historia ya kale ya Amerika  alidai kuwa maandishi hayo yalikuwa katika mfumo wa Kimisri ambayo aliyasoma kwa mawani za mawe alizoziita Urim na Thumim na aliweza kusoma tafasiri ya maandishi hayo kwa msaada wa malaika huyo aliyekuwa ametengwa naye kwa kioo
-          Alipokuwa na umri wa miaka 25 Smith alianzisha kanisa aliloliita “The True church The restoration of the initiated by Jesus while he was in the earth” yaani kanisa la kweli la urejesho wa kanilsa la kweli lililoanzishwa na Yesu alipokuwa Duniani.
-          Katika jimbo la Illinois Smith alijaribu kuweka na kukusanya mafundisho yake  lakini pia alituhumiwa kujihusisha na maswala yenye utata  na hivyo alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa maswala ya ubadhirifu wa fedha na kuoa wanawake wengi alikuwa na wanawake 48, baadaye vita ilitokea kati ya wafuasi wake wa kimomon na wasio wa kimomon hivyo Smith na viongozi wengine walikamatwa  na watu wenye hasira walimpiga kwa mawe na kuuawa na kaka yake Hyrum June 27 1844 hivyo wa Momon humuhesabia kuwa mfia dini
-          Mrithi wa Smith aliitwa Brigham Young aliyeongozwa na Mungu kuhamia Utah ambako alijenga mji na hekalu na kuishi huko mpaka wakati wa kufa kwake 1877 wa mormon walifikia idadi ya 150,000



Brigham Young

Kiongozi wa Pili wa Kanisa la Kristo la watatkatifu wa siku za mwisho lijulikanalo pia kama Mormonism Kiongozi huyu aliongoza wafuasi wake kuhama mwaka 1846-1847 kutoka  katikati ya Jimbo la Illinois mpaka mji wa ziwa la chumvi uitwao Utah  wakiwa chini wa maingira mapya ya kiongozi huyo kijana wakati huo Mormon walijiendeleza sana kwa kilimo na umwagiliaji  na ujenzi na kuanzisha kituo cha vijana kilichoitwa Brigham Young Academy  kwa sasa ndio chuo kikuu cha Brigham Young University  huko Provo Utah jamaa huyu alijulikana pia kwa kuoa wanawake wengi  alioa mara 27 na inaaminka kuwa alikuwa na watoto  60

2.       Maandiko matakatifu ya Moromons
-          Kanisa la Mormon Linatambua Vitabu vikuu vine kuwa ndio Vitabu vitakatifu
a.       Kitabu cha Mormon
b.      Kitabu kiitwacho The Peair of great Price
c.       Kitabu kiitwachi Docctrine and Covenants
d.      Na Biblia
-          Wanaamini kuwa Biblia ni neno la Mungu pale linapotafasiriwa tu na wao Mormons
3.       Mafundisho potofu ya Mormons
a.       Katika mafundisho yao kuhusu Mungu.
o   Kutokana na kitabu chao  cha mafundisho ya imani yao kiitwacho  the Pearl of Great Price Mormon wanatambua kuhusu Utatu wa Mungu lakini wanaamini au wanakubali kuwa kuna miungu mingine, wanaamini pia kuwa kuna wakati Mungu alikuwa mwanadamu  na hivyo kuna uwezekano wa mwanadamu wa kimormon kuja kuwa mungu
o   Smith wakati Fulani alisema “Kama mwanadamu alivyo ndivyo na Mungu alivyokua na kama Mungu alivyo mwanadamu atakuwa”



Hekalu la Mormon Huko, Utah

Salt Lake City ndio makao makuu ya Kanisa la Mormon au kanisa la watakatifu wa siku za mwisho hekalu hili lilikamilika mwaka 1893 baada ya ujenzi uliochukua miaka 40 una minara ya ghorofa zenye urefu wa mita 67 ambazo ni sawa na futi 220 kwenda juu.

b.      Katika mafundisho yao kuhusu Yesu Kristo.
o   Wanaamini kuwa Yesu alikuwa Roho kabla ya kuja kujitokeza ulimwenguni kama ilivyo kwetu pia  lakini yeye amewekwa wakfu kuwa wa kwanza kati ya wana wa kiroho wa Mungu
o   Wanafundisha kuwa Yesu alioa wanawake wawili Mary na Matha  na inaaminika kuwa ile Harusi ya kana ya Galilaya  ilikuwa ni harusi ya bwana Yesu mwenyewe
o   Wanaamini kuwa Yesu na Shetani Lucifer ni ndugu wote wanamuendea Mungu  na mipango yao ya wokovu na Lucifer alikusudia kuwafanya  watu wamuabudu Mungu, Lakini Kristo alikusudia kuonyesha  watu namna ya kumuabudu Mungu
o   Mpango wa Lucifer ukakataliwa na Mungu na mpango wa Yesu Kristo ukakubalika.
c.       Katika mafundisho kuhusu wokovu.
o   Ili mtu asamehewe dhambi anapaswa kufanya kazi kubwa  kwaajili ya wokovu wake ikiwemo kufundisha,kushika mashariti na kufuata mfumo wa makanisa kama ya kimormons
o   Lazima kujifunza namna ya kuwa Mungu wewe mwenyewe, wanaamini pia kuwa neema na shughuli vyote vinahitajika kwaajili ya  wokovu baadhi ya kazi hizo ni pamoja na kutoa zaka , kushuhudia na kubatizwa
o   Wanaamini pia kuwa mtu anaweza kubatizwa kwa niaba ya ndugu zake waliokwisha kufa wanatumia andiko la 1Koritho 15; 29 wenye kubatizwa kwaajili ya wafu.
Kumbuka!
*      Neno hilo wenye kubatizwa kwaajili ya wafu linamaanisha wale walioamini na kuwa wakristo na walikuwa wakibatizwa kwa sababu walitaka baadaye watakapokufa kukusanywa pamoja na ndugu na marafiki zao  waliokwisha kufa katika imani ya Kikristo katika maisha yajayo kama hakuna ufufuo wa wad kufanya hivyo kungelikuwa ni kazi Bure hiki ndicho Paul alichokuwa anamaanisha.
d.      Katika mafundisho kuhusu Mbingu na Jehanamu
o   Kwa Mujibu wa mafundisho yao Mormons wanaigawa mingi katika makundi makubwa matatu kwa madaraja matatu ya watu tofauti
o   Celestial – (Mbingu ya anga) hii ni mbingu ya kwanza na ni maalumu kwa watu wa imani ya kimormon
o   Terrestrial & Telestial –(Mbingu ya ardhi) hii ni kwaa ajili yaw at wa madaraja mengine  na jamii nyingine ya watu wanaobaki wataenda kwenye giza
o   Mormon wanaamini kuwa hakuna jehanamu ya moto wa milele wala hukumu ya milele hili linawavutia sana watu wanaoogopa hukumu.

IMANI POTOFU YA WASABATO SEVENTH-DAY ADVENTISM.
1.       Kuundwa kwa dhehebu la S.D.A.
-          S.D.A. ni kanisa lililoundwa katika misingi ya kurudi upesi kwa Bwana Yesu Kristo  kiini kikuu kikiwa ni unabii wa au huduma ya kinabii ya Bwana William Miller (1782-1849) ambaye alikuwa muhudumu wa Kibaptist
-          Alikuwa amejifunza elimu ya theolojia kwa kusikiliza tu lakini alikuwa mwanafunzi makini sana na hodari wa maandiko akijenga msingi kupitia kitabu cha Daniel 8;14 alielewa kuwa jioni na asubuhi 2300 ni sawa na miaka 2300 na kutoka hapo alijaribu kuweka tarehe  ya kuja kwa Masihi
-          Kutoka mwaka 457 B.K. nyakati ambazo Ezra alikuwa akilijenga Hekalu  na ujenzi wa ukuta wa Yesrusalem aliongeza  miaka 2300 na akajikuta anapata tarehe 21th March mwaka 1843 ambayo aliitangaza kuwa  ndio tarehe ya kuja kwa masihi ingawa haikutokea Bwana Miller alirudia tena kufanya mahesabu yake na kudai kuwa alikosea  na alipata tarehe nyingine 22th October 1844 ambayo hata hivyo ilipita patupu tena
-          Kosa lake lilikuwa ni kujaribu kueleza Tarehe ya kuja kwa Masihi jambo ambalo liko kinyume na Biblia inayosema kuwa kwa habari ya siku ile hakuna mtu aijuaye Marko 13; 32.
-          Baada yake uongozi ulichukuliwa na Ellen White  ambaye alisema kuwa ana madai kuwa amepewa ufunuo kuwa bwana Miller hakuwa amekosea  kwa vyovyote  kwani Kristo alikuwa anaingia katika patakatifu pa kimbinguni  tarehe ile ya October 1844 alidai kuwa kuna hema halisi kabisa huko mbinguni kama ilivyokuwa kwa Musa ambayo Kristo aliingia Patakatifu pa Patakatifu na hivyo 1844 aliingia katika  mahali hapo na kuwa atakapomaliza kazi ya kuombea wenye dhambi kwa sadaka yake ya Calvary atarudi tena duniani.
-          Mwaka 1860 ndipo imani hii ikajulikana kama S.D.A. makao yake makuu yakiwa huko Washington D.C.
-          Leo hii kuna waamini zaidi ya milioni tatu 3  wa kisabato duniani, wanafanya umisheni na waamini wake hujitoa sana ni maarufu kwa masomo ya afya na ulaji wa mboga za majani na matunda  huku wakijiepusha na ulaji nyama pombe na chain a kahawa ambavyo huaminika kuharibu afaya ya mwanadamu
2.       Maandiko maakatifu kwa wasabato
-          Wasabato wanaamini kuwa Biblia ndio mamlaka ya mwisho na ndio neno la Mungu lakini kama ilivyo kwa madhehebu mengi ya imani potofu ambao wanaamini kuwa maandiko yao ni ya muhimu sana katika kutafasiri Biblia
-          Wanaamini katika kitabi kiitwacho “The Great Controversy” (Bishano kuu) cha Bi Ellen White  kuwa kimevuviwa kama ilivyo kwa Biblia
3.       Mchepuko wa Mafundisho ya imani ya kisabato S.D.A.
-          Wasabato wanakataa kuwa kazi ya Kristo Msalabani haikamilishi kabisa swala la upatanisho wa mwanadamu
-          Mrs White alisema Kuwa damu ya bwana Yesu ina kazi ya kukutangazia na kukuombea msamaha kwa Mungu Baba  lakini dhambi za mwanadamu hubaia bado katika kitabu cha  kumbukumbu swala ambalo ni kinyume na maandiko Yohana 19;30,Waebrania 1;3,9;11-12.
-          Mrs white pia alidai kuwa na maono maalumu ambapo katika maono hayo  alidai kuwa aliona Mbao mbili za sheria  huku amri ya nne ambayo inahusiana na maswal ya sabato ikiwa inazungukwa na mwanga  na kutoka hapo sabato imekuwa ni moja yanguzo ya  imani ya muhimu sana kwa wa S.D.A.
-          Kushika sabato imekubalika kuwa ni moja ya njia muhimu sana ya kazi zinazofanya Mungu akupe rehema na wokovu
-          Kumbuka!
*      Kushika sabato ni swala linalorudisha watu katika utumwa ambao Kristo alikwisha kutuweka huru nao
*      Sabato ni agano la kudumu kati ya Israel na Yehova
*      Sabato haiwezi kushikwa ulimwenguni kote kwani ziko inchi kijiografia ambazo hazina jua kwa kipindi cha nyakati zote au huliona jua kwa muda tu aidha ziko nchi nyingine ambao huliona jua mara moja tu baada ya miezi sita na Biblia imeagiza kuwa moto usiwashe, wala taa wala kupikwa siku ya sabato katika nchi ambazo ni za baridi moto ni wa lazima na muhimu  hivyo sabato ni kwa wayahudi tu kwa wakati wake na kwa mpango wake
*      Soma Wakolosai 2;16,Warumi 6;14, 14;5-8
4.       Kuhusu Asili ya Kristo
-          Wasabato wanadai kuwa katika ubinadamu wake Kristo alichukua asili ya dhambi kama waliyonayo wanadamu wengine kusudi ajaribiwe kama tunavyojaribiwa sisi.
-          Kumbuka!
*      Kristo aliye na dhambi hangeweza kufaa kuwa mwokozi hata kidogo
*      Musa alielekeza kutoa kondoo wa dhabihu aliye mkamilifu
*      Je inawezekanaje kisicho kamili kuleta ukamilifu?
*      Soma waebrania 4;15,9;14, 2Koritho 5;21,1Petro 1;19
5.       Kuhusu wakati ujao
-          Wasabato wanaamini kuwa nafsi inalala yaani wanakuwa kama walio usingizini kati ya kifo na ufufuo
Kumbuka!
*      Ukweli ni kuwa mtu anapokufa roho yake huenda kukaa na bwana  lakini miili yao hulala udongoni  mpaka wakati wa ufufuo
*      Lakini nafsi ya mwanadamu hailali
*      Soma Wafilipi 1;21-23,Wakoritho 5;6-8 kumbuka mfano wa Lazaro na yule Tajiri
6.       Hatima ya waovu
-          Wasabato wanaamini kuwa hatima ya waovu ni kufutiliwa mbali milele na wanadai kuwa wazo la mateo ya milele halikubaliki na kuwa liko kinyume na maandiko
-          Kumbuka!
*      Bilia inasema kutakuwa na hukumu ya milele na moto wa milele na adhabu
*      Soma Mathayo 25;46, Marko 9;48,Thesalonike 1;7,9 Yuda 7.

IMANI POTOFU YA MASHAHIDI WA YEHOVA JEHOVAS WITNESSES
1.       Kuundwa kwa Mashahidi wa Yehova.
-          Mashahidi wa Yehova pia huitwa Russelism, au Mnara wa Mlinzi (Watch tower) au Millennial Dawn.
-          Ni dhehebu lililoanzishwa na Charles Taze Russell 1852-1916 huko Pennsylvania U.S.A. akiwa kijana mnamo mwaka 1870 huku akiwa hana mafunzo ya kutosha kuhusu theolojia  alianzisha Darasa la Biblia ambapo waamini wake walimfanya kuwa mchungaji, mwaka 1896 aliandka pamphlets mbalimbali
-          Alikuwa na woga mkubwa sana kuhusu Jehanamu ya moto  mpaka alipokutana na mafundisho a wasabato kuhusu kuja kwa Yesu Kristo na akachukua baadhi ya mafundisho yao
-          Mwaka 1896 alianzisha Mnara wa mlinzi taasisi inayohusika na uandishi wa Tracts na maandiko mengineyo aidha 1908 alihamishia makao yake makuu Brooklyn New York
-          Mengi ya maandishi yake yalikusanywa katika makundi saba seven Volumes yaitwayo Kusoma maandiko, alikubaliana na mafundisho ya kisabato kuwa Kristo aliwasili Hekaluni 1914
-          Russel alikuwa mtu mwenye majivuno makubwa sana akiyasifia maandiko yake kuwa ni ya hali ya juu kama ilivyo kwa maandiko ya Paulo mtume, Martin Luther na Wycliffe na kuna wakati alidai kuwa ni afadhali kuchagua maandiko yake kwanza kasha Biblia baadaye
-          Mkewe alimshutumu na kuomba talaka mwaka 1913 kwa sababu ya zinaa, kiburi na kupenda kutawala alishutumiwa pia na magazeti kuwa ni mwenye hila aliwahi kuai mahakamani kuwa anajua kiyunani na alipoombwa kutambua herufi alishindwa
-          Alifariki mnamo mwaka 1916 akiwa ndani ya treni huko Texas
-          Mwaka 1917 mwanasheria na jaji msaidizi J.F. Rutherford 1870-1942 alikuwa mrithi na kionozi wa kundi alijipa mamlaka kubwa sana kiasi cha kumfukuza yeyote ambaye angehoji maswali kumuhusu na mnamo mwaka 1930 aliliita kundi lake Mahsahidi wa Yehova kutokana na andiko la Isaya 43;10.
-          Rutherford alikufa kwa ugonjwa wa kansa huko San Diego Califonia January 8th 1942 baada ya kifo chake waruth wao hawakuwa maarufu kwa jamii isipokuwa maandiko yao yakawa maarufu na kusambazwa zaidi
-          Mashahidi wa Yehova wanakataa dhana ya kupiga kura, kupiga saluti, kuheshimu bendera, kuimba wimbo wa taifa, na kutumikia Jeshi pia hupinga swala la kuongezewa au kuongeza mtu damu.
-          Mtazamo wao kuhusu Kristo wanamuona kama kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu ambaye baadaye alishirikishwa na Yehova katika uumbaji na hivyo Yesu sio Mungu na kuwa hakuna utatu, Roho Mtakatifu kwao ni nguvu za Mungu tu na sio nafsi
2.       Imani yao kuhusu maswala yajayo.
-          Walitabiri kuwa ulimwengu ungefikia mwisho mnamo mwaka 1914,1918,1920,1925 na 1941 na pale inapotokea kuwa mwisho haukufika walijaribu kuweka vema hesabu zao walijumuisha miaka 6,000 ya uumbaji na kupata (4026.B.K.) na walitabiri kuwa Yesu atakuja mara ya pili 1975 B.K.
-          Kwa sasa wanaazamia vita vya Harmageddon na ufufuo wa watu 144,000 ambao ni mahshidi waliotiwa muhuri huko mbinguni mwaka 1914 kama wafalme  na makuhani
-          Kama ilivyo kwa S.D.A. wanaamini kuwa nafsi inalala na wanakanusha kuweko kwa jehanamu ya moto na kuwa hakuna hukumu ya waovu zaid ya kufa milele wanaona ni jambo lisiloingia akilini kuwa Munu mwenye upendo kuruhusu wanadamu awapendao kuingia katika moto wa milele.
3.      Kama ilivyo kwa imani nyingine potofu wao pia hutumia maandiko mengi sana kama ushahidi wa mafundisho yao.
-          Mashahidi wa Yehova wanasahau kuwa ni upendo wa Mungu ulioruhusu Yesu kuteseka na kufa msalabani
-          No wazi pia kulingana na haki ya Mungu wazo la Jehanamu ya moto halipingani na haki a Mungu,
-          Mungu amempa kila mwanadamu utashi na anaweza kuchagua uzima wa milele au mauti ya milele ingawaje uamuzi huo unaweza kufanyika katika wakati huu wa sasa tukiwa hai Waebrania 9; 29.
-          Mashahidi wa Yehova ni wainjilisti wa chini kwa chini hufanya kazi kwa kushuhudia nyumba kwa nyuba ni ni Hodari sana katika maandiko mpaka kwenye miaka ya 1900 walikuwa na waamini zaidi ya milioni tatu duniani.
4.       Mafundisho ya Mashahidi wa Yehova kinyume na Utatu wa Mungu
-          Mashahidi wa Yehova wanapingana kabisa na fundisho kuwa kuna Mungu watatu katika umoja  yaani Mungu baba na Mwana na Roho Mtakatifu  na kuwa wote watatu wana nguvu sawa umoja na kuwa ni wa milele Katika kitabu chao kiitwacho Let God be true  cha Brooklyn kinajenga hoja kali kuhusu utatu kama ifuatavyo
-          Shetani ndiye mwanzilishi wa fundiso la Utatu wanadai kuwa fundisho hilo halikuanzishwa na Yesu wala wanafunzi wa Yesu wa mapema, huu ni mpango wa ibilisi ili kwamba mtu akitaka kumjua Mungu wa kweli na kumtumikia aweze kujikuta ana wakati mgumu wa kumpenda na kumuabudu Mungu ambaye ni mgumu kueleweka huu ni mkakati wa shetani kutaka kuwapoteza watu wengi wenye mioyo ya kumcha Mungu kuwa na ukweli halisi kuhusu Yehova Mungu na Mwana wake Yesu Kristo kwanini kwa sababu hakuna utatu!
-          Jaribio lolote la kujifunza kuhusu Utatu wa Mungu linaishia katika kuchanganya akili za watu na kuharibun hata maana ya andiko la Yohana1;1-2 badala ya kurahisisha uwazi wa andiko hili inapelekea kuwachanganya watu
-          Je ni kweli kuna Utatu? Mungu Yehova ni utatu? Hapana Yehova Baba ni Mungu mmoja wa pekee Yohana 17;3 Marko 12;29 Yesu ni mzaliwa wa kwanza na anatioishwa chini ya Baba 1Koritho 11;3 Baba ni mkuu kuliko mwana Yohana 14;28
-          Roho Mtakatifu (roho takatifu) sio nafsi ni Nguvu ya utendaji wa Mung  Mwanzo 1;2, Matendo 2;18
-          Hakuna kitabu chochote kati ya 39 vilivyokubalika katika agano la kale wala 27 vya agano jipya vinavyounga mkono au kufundisha kwa uwazi kabisa fundisho la utatu ni wazi kuwa kibiblia na kihistoria fundisho kuhusu utatu halikuweko wala halikujulikana na hata kwa karne kadhaa baadaye.
5.       Mafundisho ya mashahidi wa Yehova kinyume na uungu wa Yesu Kristo.
-          Maandiko yanamzungumzia mwana wa mungu Neno kama mungu (m ndogo) na sio  (M kubwa)  Ni mungu mwenye nguvu  lakini sio Mungu mwenye nguvu zote katika kitabu chao kiitwacho The Truth Shall make You Free cha Brooklyn kinafundisha hivyo kwa msisitizomkubwa
-          Kwa maana nyingine wanamaanisha kuwa Yesu  ndiye kiumbe pekee kilichoumbwa na Mungu moja kwa moja  Biblia inaonyesha kuwa yuko Mungu mmoja na ni mkuu kuliko mwana  mwana yeye ni mzaliwa wa kwanza , ni mwana wa pekee na aliumbwa na Mungu ana mwanzo na hoja ya kuwa Baba ni mkuu kuliko mwana iko wazi na ni rahisi kueleweka  na hiki ndicho Biblia inachokifundisha
-          Uwazi kuwa alikuja duniani akiwa ametumwa na Mungu ni uwazi ulio wazi kuwa  hayuko swan a Mungu lakini ni mdogo na ndio maana haishangazi kuona Yohana akisema Hapo mwanzo kulikuwako Neno naye neno alikuwa kwa Mungu ingawa wakati huo huo huyo Neno ni mungu (m ndogo)
-          Ni wazi kuwa Yesu alikuwa na Mungu huko mbinguni lakini hilo halimaanishi kuwa alikuwa sawa na Mungu huko ni wazi kuwa Biblia inatoa picha kuwa Yesu aliumbwa wakati Fulani akiwa kiumbe wa kiroho kama ilivyo kwa malaika wa Mungu kwa hiyo sio Yesu au malaika ambao waliwahi kuweko kabla ya kuumbwa.
6.       Mafundisho ya mashahidi wa Yehova kinyume na uungu wa Roho Mtakatifu.
-          Roho takatifu ni nguvu zisizoonekana za utendaji wa Mungu ambayo hutembea kwa watumishi wake wanaotenda mapenzi yake
-          Kama tulivyoona ni makosa kumfanya roho takatifu kuwa ni nafis wakati hiyo sio nafsi  hili ni jambo ambalo liko wazi katika maandiko kuwa roho takatifu ni nguvu tu ya utendaji wa Mungu  katika kukamilisha makusudi yake ni nguvu inayodhibitiwa na ungu na huitumia kama apendavyo hii ni nguvu tu kama ulivo umeme.
-          Nguvu hiyo haiwezi kuwa Mungu wala kuwa sawa na Mungu.



IMANI POTOFU YA CHRISTIAN SCIENCE
Christian Science ni imani inayoweka msingi wake wa maishja na mafundisho ya Yesu Kristo pamoja na maswala ya uponyaji kama inavyoainishwa katika Agano jipya, kulingana na mwanzilishi wa imani hiyo Mary Baker Eddy anasema Christian Science imetokana na usomaji wa Biblia wa Muda mrefu , Eddy anaamini kuwa Mungu ni Mungu wa Upendo  na ni mwenye nguvu zote  na ni baba wa watu wote  na hivyo swala hilo lilimpa maswali kuhusu kuweko kwa maovu na uhalisia wake  na uhusiano ulioko katika maisha ya mwanadamu
Eddy alizaliwa huko  Bow, New Hampshire, mwaka 1821  wazazi wake walikuwa watu walijitoa sana kwa Mungu. Alichangia kwa kiasi kikubwa kutoka katika maumivu yake ya ghafla yaliyomtea sana mwaka 1866 aliandika kitabu kiitwacho  glimpse of the great fact” Kweli kuu kwa Ufupi  yaani kinachozungumzia maisha na Roho (Mungu)aliamini kuwa maisha ya kiroho ndio msingi wa maisha halisi tunayoyaona  Eddy alitumia miaka 45 ya maisha yake yaliyosalia  kufanya utafiti wa uhakika wa ufahamu na matumizi yake ingawa wakati wote wa uatafiti wake aliamini kuwa wokovu unajumuisha utiii kwa amri za Bwana Yesu hususani ya kuponywa wagonjwa sio kwa muujiza wa kuingilia sheria ya asili bali kwa utendaji wa nguvu za Mungu unaoonekana katika sheria ya asili ya Kiroho.

Mary Baker Eddy
Eddy alifundisha wanafunzi wake kuwa kupitia maombi wanaweza kujiweka wenyewe katika ahsria ya kiroho na kuweza kuondoa magonjwa na masumbufu yote ya aina binadamu na ndio maana watu wa imani hii huomba zaidi kuliko kuliko kutegemea madawa katika uponyaji wa magonjwa. Na inapotokea muamini wa imani hii anahitaji msaada maombi yao hugeukia kwa muombaji maalumu ambaye amajisajili kuweko wakati wote akijishughulisha na maombi kwaajili ya uponyaji baahi ya hao waombaji pia ni waalimu wenye mamlaka katika kanisa wanaofundisha wanafunzi wao kanuni za sayansi ya Kikristo “Christian Science”.
Mwaka 1875 Eddy alichapisha kitabu chake cha kwanza kuhusu Sayansi na Afya  na baadaye toleo la Sayansi na Afya na ufunguo wa kimaandiko mwaka 1881, miaka miwili baadaye baada ya kuanzisha kanisa  alikwenda Boston,Massachusetts. wanachama wa kanisa lake waliongezeka kwa kasi  na akakamilisha ujenzi wa kanisa lake 1895 na majengo mengine makubwa yaliyokamilika 1906 mpaka Eddy anafariki kulikuwa na makanisa 1190 ya jamii yake, Hata kufikia 1911 kanisa lake lilienea sehemu za Marekani na ulimwenguni na katika inchi 72 za kiprotestant.
Mwaka 1892, Eddy  alitambua kanisa la Boston na kubakia hapo na likatambuliwa kama kanisa mama la makanisa ya Christian Science kanisa hili huongozwa na Bodi ya wakurugenzi wakiliangalia kanisa tokea hapo makao makuu na makanisa mengine ya kawaida huhesabika kama matawi  kila kanisa hujiongoza ingawa ni lazima kufuata mfumo wa kanisa mama
Mafundisho na ibada zinafuata kanuni zilizowekwa na mwanzilishi, kitabu cha msingi ni kile cha Sayansi na afya kilichoandikwa mara kadhaa na Eddy
Mafundisho na imani ya Christian Science.
-          Wanaamini kuwa wazo la Mwanzo 2;7 kuwa ni la uongo na ni la kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hakuumbwa kwa mavumbi kwani udogo ni kitu kisicho na uhai na mwanadamu ni kiumbe chenye uhai hivyo dhana hiyo sio ya kweli
-          Wazo la utatu wa Mungu ni wazo la wanadamu ambao hufikiri kuwa mwanadamu pia ni utau
-          Wakristo wanaoamini katika mari ya kwanza ni wale wanaoamini katikia Mungu mmoja kama wayahudi na kuwa wanatambua pia kuwa Yesu sio Mungu kama ilivyo kwa wayahudi
-          Wanaamini kuwa Yesu Kristo ni Muungano wa nafsi mbili Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mungu
-          Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu, Mungu ni kanuni, kweli, maisha, upendo, ufahamu. Maarifa, hekima, akili nafsi.
-          Hakuna dhambi ila kuna mawazo tu kuwa kuna dhambi ni mawazo ya maruweruwe ni mawazo yasiyo sahiimbingu I utawala wa maswala ya kiroho tu ni sayansi ya ujuzi wa kiungu
-          Mwanadamu alishaokoka tangu milele
-          Maombi hayawezi kumbadilisha Mungu, wala kuumba kitu kipya,ila yanainua imani kwamba dhambi imeondolewa maombi yenye kelele hayana msingi wowote lakini maombi ya kimyakimya ndio yenye matokeo.
-          Mwenye dhambi hujitengenezea jehanamu yake mwenyewe kwa uovu wake na mwema hujitengenezea mbingu yake kwa wema wake mwenyewe kwa hiyo maswala ya kuweko kwa jehanamu ni ya wale wanaofikiri kuweko kwa mwili
-          Shetani maana yake ni makosa,uovu,kinyume cha kweli, kuamini katika dhambi,magonjwa, kifo na tama za mwili
-          Wanaamini maswala Saba kuhusu Mungu.
*      Mungu anakumbuka
*      Mungu anasema
*      Mungu anasikia ,anaona  na anaumba
*      Mungu anajua, ana akili
*      Mungu atahukumu ulimwengu
*      Mungu Roho.
*      Mungu ana utashi
-          Wanaamini kuwa wagonjwa hawaponywi kwa kutamka kuwa hakuna magonjwa bali kwa kujua kuwa hakuna magonjwa Christian science hawaamini katika miujiza kwani Eddy anaamini kuwa magonjwa,dhambi na kifo sio vitu vya kweli  mawazo tu ambao watu wameingiziwa na kuamini kuwa viko lakini haviko
-          Mungu ni kanuni tu za kiroho
-          Yesu sio Mungu
-          Maandiko yanaweza kukosea
-          Mungu hana umbile lolote maalumu umbile alilo nalo ni lile analopewa na wanadamuu tu kwa akili zao za kibinadamu
-          Sayansi ndiyo inayoleta kweli kwenye mwanga .na amani katikam ulimwengu kwani pasipo watu wenye kufikiri na wenye akili huu ulimwengu utakuja kuzimia.

IMANI POTOFU YA JESUS ONLY
-          Mwanzilishi wa imani hii ni mwinjilisti William Branham ni mwinjilisti aliyekuwa na upako  wa kupita kawaiada katika maswala ya uponyaji alikuwa ni mtu aliyejiamini sana  na alifikia hatua ya kutokumuamini mtu zaidi ya Yeye mwenyewe
-          Alijikuta akiamini kuwa yeye pekee ndiye aliyeangaziwa  alipinga sana mafundisho kuhusu Utatu jambo ambalo kanisa limeamini kwa zaidi ya miaka 1900 na alisema awaye yote anayepingana naye amekosea  matokeo yake kulitokea faraka na kutokuelewana
-          Alidai kuwa anaufunuo kuwa watu walitakiwa kulitumia jina la Yesu tu kana inavyoonekana kaika kitabu cha Matendo wakati wa ubatizo
-          Alidai kuwa Yesu ndiye Mungu baba, Mwana na Roho Mtakatifu, walidai kuwa wale wanaodai utatu wanaamini katika utamaduni wa mapokeo kuhusu miungu mitatu
Kumbuka!
-          Mungu yu Utatu Baba, mwana na Roho Mtakatifu na Baba sio mwana na mwana sio Roho Mtakatifu waebrania katika lugha ya asili walipomtaja Mungu walitumia Neno Elohim ambalo kwa ujumla liko katika wingi ingawa linatumika katika umoja.
-          Waamini wa imani hii wanakazia zaidi katika kanuni ya ubatizo iliyoko katika matendo ambayo hukazia “wakabatizwa kwa jina la Yesu” pia hukazia kuwa jina hilo ltamkwapo kwa mtu hata kama hajabatizwa au kuokoka  anakuwa mwamini
-          Kwa ujumla ni makosa sana kuamini hivi je namna gani mtu kutamka jina la Yesu tu anakuwa amepokea wokovu? Pia ni muhimu kuahamu kuwa hakuna wakati ambapo risto amekiri kuwa yeye ni baba na baba ni yeye au Roho
-          Kama ilivyo kwa imani nyingine potofu Jesus Only wana maandiko yao wanayoyatumia lakini ukiyachunguza kitaalamu yametafasiriwa nje ya kanuni za Hermeneutics somo lihusulo kanuni za kutafasiri maandiko na kuyatumia kwa halali
-          Uanzilishi wake pia ulikuwa katika misingi a kugawanya wau na kuwapotosha na wanaamini kuwa badhi a mababa wa kanisa kuwa ndio waanzilishi wa imani yao na mafundisho yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni