Jumapili, 31 Januari 2016

NIKAMSANIFU MTU MFUPI MWEUSI.



Mwaka 1997 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza pale chuo kikuu cha Dar es Salaam, nilikuwa nimefanyiwa mpango wa ajira na jamaa yangu mmoja kwenye kampuni moja jijini Dar na nikawa nimefanikiwa, Baada ya mipango ya hapa na pale  na kunifagilia sana kama wanavyosema watu wa mjini nilifanikiwa kupata barua ya ajira  kama afisa uhusiano kwenye kampuni moja ambayo haikuwa kubwa  sana wakati ule ingawa sasa hivi imeshakuwa, Nilipata barua iliyonitaka kuanza kazi wiki inayofuata kwa kweli nilifurahi sana , lakini kitu kibaya kwangu ni kuwa sikuwa na adabu na kile kiburi cha watoto wa kidato cha pili  siyo cha mtu aliyemaliza chuo kikuu  bado kilikuwa kinayawala kwangu.

Usimdharau Mtu awaye yote kwa sababu ya Mtazamo wa nje tu Mungu huangalia kwa namna tofauti


Siku ya kuripoti kazini iliwadia ambapo niliamka mapema sana na kujiandaa. Nilikuwa naishi mabibo External kwa wazazi wangu wakati huo, Niliondoka nyumbani saa 12 asubuhi nikiwa na uhakika kuwa nitafika mjini Posta  kabla ya saa mbili asubuhi muda wa kuripoti ofisini, Nilipanda basi hadi  ambapo nilipanda basi linguine , tulisafiri hadi pale Shekilango ambapo gari Fulani ilipoteza muelekeo likataka kuivaa daladala niliyokuwemo, ilibidi mwenye gari lile linguine kusimama na daladala yetu pia ilisimama, Abiria wa daladala walishuka na wa lile gari linguine aina ya Prado nao walishuka , mimi nikawa wa kwanza, kuwaendea wale wenye gari nyingine ambao walikuwa watatu, mmoja wao mwembamba kiasi na mwenginemfupi mweusi sana aliyekuwa ndiye msemaji, Hakuwa anasema chochote zaidi ya kuomba radhi kwa unyenyekevu kuwa gari lao lilikuwa limepata tatizo la usukani. Mimi nilipandisha  sana huku nikitumia maneno ya kingereza kuwaambia kwamba hawajastaarabika , nilimwambia Yule aliyekuwa msemaji wao kwamba ndio maana  amekuwa mweusi na kafupi sana kwa sababu ya ujeuri, Yule jamaa alisema ni sawa ninavyonena, hata hivyo dereva wa daladala yetu alikuwa mstaarabu aliwaunga mkono jamaa wale  akisema anaelewa aina hozo za tatizo na akaomba abiria tupande garini  na kuondoka  niliwageukia wale jamaa na kuwaambia “You are just luck guys” nikimaanisha kwamba wana bahati sana

Ndani ya basi nikazidi kusema kama kinanda , baadhi ya abiria wenye tabia kama mimi wakaniunga mkno , abiria wengine hawakuniunga mkno, ingawa hawakusema  hivyo, bali ile tazama yao  niliijua tu sikujali. Nilifika Posta mapema na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ambayo nilitakiwa kuanza kazi, iliandikwa kwenye barua kwamba nimuone mkurugenzi mkuu kabla sijaenda kwa menenja  kupangiwa majukumu yangu ya awali. Ilipotimu saa mbili niliomba kuingia kwa mkurugenzi ambapo niliruhusiwa, niliingia nikijua kuwa nitapokea zinga la sifa kwa kuchaguliwa kwangu kujiunga na kampuni ile , haikuwa hivyo ndugu yangu, pale mbele ya kiti alikuweko bwana mmoja unaweza kuhisi ni nani ? alikuwa ni mtu mfupi mweusi sana. Sikuwa na akili ya samli kwani nilimtambua mara moja kuwa , Naye hakuwa boga kwani aliponitazama tu alitabasamu Halafu alisema karibu afisa uhusiano kasha alinyoosha mkono wake  kutaka tusalimiane, nilikuwa natetemeka naye alijua dhahiri, karibu kaa alisema bila shaka unajua shughuli za kampuni yetu, kila saa na kila siku utakuwa unapambana na wateja wakorofi unadhani utaweza kuwavumilia? Aliuliza nilijua alikuwa ananisanifu tu nilisema ndiyo nitaweza 

Halafu aliniuliza je ukiwa kazini akatokea mtu mwenye gari alafu akjataka kukugonga kwa bahatri mbaya.. no tuseme ukiwa kwenye daladala likatokea gari linguine likataka kuigonga ile daladala utafanyaje? Nilinyamaza kwa muda kisha Nitamwacha dereva azungumze na mwenzake wajue watakavyomalizana wenyewe’ kwa nini hiyo ilikushinda leo asubuhi? Badala ya kuwa abiria ukawa dereva?

Nilitamani kuona jambo Fulani linatokea ili mahojiano yale yaishe ni kweli jambo lile lilitokea  Yule mkurugenzi ambaye ni Yule bwana niliyemkashifu pale shekilango aliniomba ile barua ya ajira, aliichukua na kuichanachana, halafgu aliniambia  potea nisikuone hapa ofisini hata mara moja, nilitaka kufanya jambo Fulani kama kupambana naye ili nimfunze adabu  jamaa naona alijua aliinua simu kuita mlinzi nilitoka kwa haraka  nikiwa nimeshukwa uso,”kweli aushikaye upanga ataangamia kwa upanga” leo hii ndio nasema habari hizi kwani hata ndugu zangu sikuwaambia sababu za kukosa kibarua kile

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni