Jumanne, 26 Januari 2016

SOMO; JINSI YA KUSHINDA MIGANDAMIZO AU MSONGO WA MAWAZO (DEPRESSION OR STRESS)


MJENZI:  Mchungaji Innocent Kamote
     Moja ya matatizo makubwa na yanayokuwa kwa kasi siku hadi siku na hususani siku hizi ni tatizo la migandamizo (depression) Hili ni tatizo la kisaikolojia na kiroho pia. Tatizo hili linapopita kiasi huweza kupelekea mwanamke au Mwanamume kujiua, na kwa vijana ambao uwezo wao wa kuhimili mihemko ni wa kasi zaidi wengi huweza kujidhuru, kumbuka kuwa wengi wa watu wanaofikia ngazi ya kujiua  wenyewe  wakati mwingine hufanya hivyo kwa sababu ya migandamizo depression hali ya migandamizo hii wakati mwingine haielezeki lakini huweza kujumuishwa hali za kukata tamaa, kukosa furaha au faraja na, kuvunjika moyo,kufiwa na mpendwa mwanao, mkeo, mumeo au ndugu na rafiki, kujiona duni, kukosa rafiki, kusalitiwa, kupoteza tumaini ndani ya ndoa, kuudhiwa na jamaa waliokaribu, kusalitiwa, talaka, ndoa iliyovunjika, au kuchoshwa na vikao vya upatanishim kazi nyingi na maudhi, kukosa furaha kuwa na huzuni na kujisikia hali nzito sisi kama wanadamu wakati mwingine hufikia hatua ya kuwa na hali kama hizo Zaburi 34;17-19 inasema hivi:-

“17. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. 18. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. 19. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

Unaona watakatifu waliotutangulia pia walipitia Matatizo haya waliovunjika moyo, na waliopondeka roho hii ni lugha ya zamani inayozungumzia stress na depression wakati huu biblia inazungumzia kuvunjika Moyo Broken hearted na roho iliyopondeka crushed in spirit


Ø  Tatizo hili kwa mujibu wa wanasaikolojia ni tatizo la ngazi ya juu sana ya maumivu ya moyo wa mwanadamu au tatizo la akili la kibinadamu, Tatizo hili wakati mwingine linaweza kumpata mtu kwa sababu ameshindwa kuipokea taarifa mbaya nzito kama kupoteza mchumba, kufiwa na uliyempenda, na inapofikia ngazi ya akili za mwanadamu kushindwa kulibeba tatizo hilo mwanadamu huweza hata kupoteza maisha au kupata ugonjwa wa kiharusi stroke mfano 1Samuel 4;12-22

 “12. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake.             13. Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. 14. Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. 15. Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona.    16. Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?        
17. Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.         18. Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini.        
19. Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.      20. Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. 21. Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe. 22. Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.

Unaona si kila mtu duniani anaweza kuvumilia taarifa ngumu na mbaya kama hizo, Moyo ulioshambuliwa na roho iliyopondwapondwa huweza huweza kusababisha Mauti! Wako wengi wanalia kwa sababu ya matatizo mbalimbali duniani ni Ngumu sana

Ø  Inahitajika Mungu kuingilia kati wakati mwingine ili mtu ashinde migandamizo hii katika maisha, wakati mwingine shetani huruhusu migandamizo hii kwa kutushambulia kwa matatizo mengi ili kutupata na kufanikiwa kutuua kimwili na kiroho au hata kimafanikio
Ø  Daudi mtu wa Mungu ni moja ya watu waliopitia tatizo la migandamizo kwa zaidi ya miaka 25 ya maisha yake, Mfalme Sauli alikuwa anataka kumuua, aliishi mbali na ndugu zake  pamoja na kuwa Mungu alikuwa amempaka mafuta lakini alikutana na matatizo mengi mbali na nyumbani, mbali na marafiki, uchumi duni watu duni wenye madeni kwa ujumla aliishi kama yatima na wakati mwingine matatizo yenye kutatanisha 1Samuel 30;3-8
Ø  Hatujui wewe unapitia migandamizo ya aina gani pengine mchumba wako amevunja uhusiano nawewe, Mumeo anaweza kuwa sio muaminifu au amekuacha, watoto wanaweza kuwa sio watii, ndugu na jamaa hawakuoni kuwa wa maana na wakati mwingine hata ndugu zako wa Kanisani wako kinyume nawewe, umezungukwa na taarifa mbaya kila mahali, unahangahika tu na unashindwa ni wapi pa kusimamia inakuumiza lakini huna jinsi, maisha hayaonyeshi kufanikiwa unachokipata hakitoshelezi mahitaji yako kibinadamu kila ukipiga akili inakataa, malengo yako na ndoto zako katika maisha hazionekani kuwa na mafanikio je unafanya nini kukabiliana na hali hizi wakati mwingine unalia kitandani unatembeatembea na huoni faraja yoyote hali yako ni ngumu unahitaji kushinda mgandamizo huo wa mawazo kwani maisha yako yanathamani sana wala usifikie hatua ya kujiombea kufa au kutamka heri nife!
Ø  Migandamizo mingine inatokana na mitatizo sugu katika ndoa wengine wanajuta wanasema heri nisingeolewa au heri nisingeoa matarajio na matumaini uliyoweka kwa mwenzi wako picha yake imekuwa kinyume na ndoto zako, sasa umekata tamaa, wengine wametamani kufa au wapenzi wao wafe au wamepoteza uaminifu ili kutafuta faraja nje ni matatizo matupu ni maumivu juu ya maumivu upweke wako haujaondoka kamwe nyumba imekuwa kama kituo cha polisi huna rafiki nyumbani hali hizi zote zinasababisha moyo kupondeka na roho kuumia unahitaji uponyaji.
JINSI YA KUSHINDA MIGANDAMIZO
·         Samehe wote walio kinyume na wewe 1Samuel 24;1-6, Jifunze kuwa Komandoo wa kusamehe na sio wa kulipiza kisasi usiwe kama Van dame alisema “No retreat no Surrender” hata kama kuna uonevu wa kupita kawaida Mungu na atupe uvumilivu na uwezo wa kusamehe Yesu aliweza kusamehe waliomtesa Msalabani, Stephano aliweza kusamehe walimpiga kwa mawe unahitaji Kusamehe ili uchungu uondoke Moyoni mwako linaweza kuwa jambo gumu lakini uliomba Roho Mtakatifu atakuwezesha.
·         omba toba kwa Mungu Zaburi 38;4 toba ni jambo la msingi sana sisi sote tunakosea, yeye asiyekosea huyo ni mtu mkamilifu, tunapokosea lazima tukimbilie toba, omba radhi kwa Mungu Mungu ataondoa uchungu mioyoni mwetu
·         Lia kwa machozi ya furaha na kupiga kelele za shangwe kumsifu Mungu Ayubu 1;20-22,Marko 14;26,matendo 16;25, kisaikolojia kulia kunaleta nafuu, usipolia jeraha la moyo linaweza kuwa kubwa hivyo ni vema ukalia, ukimaliza imba zaburi, sikiliza nyimbo za kwaya na neon la Mungu furahi na kama unaweza kucheza mpira nenda furahi na uponyaji wa Bwana utachukua nafasi
·         Jitie nguvu katika Bwana na kuomba na kuutafuta uso wake 1Samuel 30;6-8 mtwike yeye fadhaa zako maana anajishughulisha nazo 1Petro 5;6-7 soma neno la Mungu hususani zaburi
Kuna wakati hutapata mtu wa kukutia moyo hata kidogo, huu ni wakati wa kujitia nguvu katika Bwana, tumia upweke kujiimarisha kwa Bwana na kuomba manabii wengi waliishi katika migandamizo lakini waliamua kutafakari, kukaa peke yao kuomba na kukesha na Mungu akashughulika na matatizo yao
Kumbuka Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote. Ni imani yangu kuwa Umejengeka na bwana amekuganga ikiwa yako mambo zaidi maswali au ushauri nipigie simu 0718990796 nitaomba pamoja nawe na kukushauri

Maana Msingi mwingine hakuna  mtu awezaye kuuweka isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo –

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote

+255784394550
+255718990796
Box. 100 Muheza, Tanga

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni