Maana ya Ufunuo.
Neno Ufunuo kwa kiingereza ni Reveletion au Disclosure au
Apokalupsis kwa kiyunani Apokalupsis Maana yake ni Mungu kujiweka wazi, au kujifunua kupitia
uumbaji wake, Historia, Dhamiri ya mwanadamu na Maandiko kwa msingi huo
linapotumiwa katika maandiko hutumiwa kwa maana mbalimbali tofauti na hakuna
maana maalumu, Maneno makuu mawili ya kiyunani hutumika katika Biblia yaani
Apokalupsis na Faneroun fanerou'n ambalo maana yake ni yaliyo
juu ya uweza wa kibinadamu, au yaliyo zaidi ya kufunuliwa, ni kupitia maneno
haya makuu mawili ndio tunapata maana ya neno Ufunuo ambao kwa maneno ya
kufupisha tunaweza kusema ni kuwekwa wazi kwa Maswala ambayo mwanzoni yalikuwa
hayajawekwa wazi.
Kitheolojia ufunuo unaweza
kuzungumziwa katika maana kuu mbili ufunuo wa Mungu wa Ujumla General or Naturral Reveletion na Special Reveletion. Ufunuo wa ujumla wa
Mungu ni ushahidi wa kuweko kwa Mungu kwa wanadamu wote waliojuu ya uso wa
Inchi kupitia uumbaji, Historia na dhamiri ya mwanadamu. Jambo hili linaweza
kuthibitishwa na Maandiko kama Zaburi ya 19;1 Mbingu zahubiri utukufu wa Mungu
na anga latangaza kazi ya mikono yake, Matendo 14;8-18,17:16-34, Warumi
1;18-32,2;12-16 na mistari mingine mingi. Dhana hii inakubalika na baadhi ya
wakatoliki na waprotestant kwamba ni ya ufunuo wa ujumla ambao unamthibitishia
mwanadamu kuwa Mungu yuko bila kuhusisha maswala ya imani bali kwa kujihoji
Reasoning, wakati ufunuo maalum ni ule unaotokana na msaada wa Mungu ambao
hupatikana kwa imani na uzoefu tu kupitia maneno ya Mungu. Ufunuo huo wa ujumla
hauna msaada katika kumuwezesha mwanadamu kuokoka lakini kumfanya asiwe na
udhuru kuwa hakuna Mungu.
Kwa ujumla ufunuo wa asili au
ufunuo wa ujumla umejengwa katika misingi ya jumla ya kuthibitisha tu kuwa
Mungu yupo lakini ni ufunuo usiotosheleza kwa habari ya kuleta wokovu lakini
angalau unaweza kumsaidia mwanadamu kuwa na ufahamu huo kwa kuanzia,
inasemekana kuwa hata wale wanaofikia hatua hii kwa namna Fulani wanajua hayo
kupitia imani ingawaje eneo kubwa ni kwa kutumia akili, wakati dhana ya Ufunuo
unaotokana na Mungu inajifunua kupitia Historia ya matukio ya kweli ya wokovu
na ufunuo utokanao na ujuzi halali wa maandiko.
Baadhi ya wasomi huamii kuwa
ufunuo Haufanani wala hauko sawa wakati wote na wanaamini kuwa hata Biblia
yenyewe ni Matokeo ya ufunuo na ni nukuu za mafuno kwa watu waliokuwa
wakijaribu kumtafuta Mungu na wakajaribu kumuelezea kwa ufahamu wao kupitia
kazi za namna alivyojifunua kwa hiyo wao huamini kuwa ufunuo hutokea wakati Mungu anapojifunua yeye
mwenyewe kwa mtu na mtu huyo anapoitikia mwitikio wa Imani katika Kristo kwa
hiyo Biblia kwao ni kiongozi tu wa uzoefu huo wa kimafunuo lakini yenyewe sio
ufunuo kamili.
Maana
ya ufunuo kwa Mtazamo wa Kibiblia.
Hatima ya ufunuo wa aina
yoyote ile Bado ni makusudi ya Mungu kutuleta kwake ili tupate kumfahamu yeye,
Mungu kujifunua kwa mwanadamu hakutegemeani na mfumo au kanuni maalumu au mfumo
Fulani wa kimafundisho msingi wa kwanza ni mtu Binafsi kukutana na Mungu na
hivyo kibiblia hata kukutana na kumfahamu Mungu wa kweli ni ufunuo hii ni kwa
sababu .
§ Mwanadamu kuwa na ujinga wa
kutokumfahamu Mungu ni sawa na Ujinga wa kutokujifahamu yeye mwenyewe hivyo
kama mtu hamjui Mungu hawezi kujijua yeye mwenyewe.
§ Mwanadamu ana hatia anayotembea
nayo inayomuhukumu kuwa amemkosea Mungu na hivyo ufunuo wa kweli katika kristo sio
tu unampa maarifa bali unamkamilisha katika utakatifu na rehema na msamaha wa
Mungu
Ufunuo wa Kibiblia ni ufunuo wa Mungu na matendo yake ya
kweli kihistoria, Mungu alikamilisha mpango wake wa kumuokoa mwanadamu na
mpango huo ulikamilishwa katika Yesu Kristo. Kwa msingi huo Hakuna Yesu Kristo
wa Imani tu Lakini Pia tunaye Yesu Kristo wa Historia kwa hiyo “hakuna imani katika Kristo kama hakuna
Kristo katika Historia”, Kwa hiyo Historia ya Kibiblia ni historia ya kile
ambacho Mungu amesema na kutenda Mika 6;5 na Kristo ndiye ukamilifu wa Historia.
Agano la kale ni ufunuo uliokuwa unategemea kuja kwa Yesu
Kristo na Agano jipya ni ufunuo unaoakisi na kuthibitisha ukweli wa ujio wa
kristo. Kwa msingi huo kufanyika mwili kwa Bwana Yesu ndio ufunuo kamili
wa Mungu na ndio kiini cha Injili Warumi 1;3,16, 1Wakoritho 15;1-4, Wagalatia
4;4, Waebrania 1;1,2, Ni wazi kuwa Mungu alijifunua kwa wanadamu kuhusu mpango
huo wa wokovu kwa njia nyingi na kwa namna mbalimbali Waebrania 1;1-2
kwa hiyo ingawa ufunuo wa Mungu umekuja katika mwana wake kwa ukamilifu lakini
Mungu alijifunua kwa njia
mbalimbali kwa hiyo uko ukweli kuwa Mungu amejifunua pia kwa wanadamu kwa njia
ya uumbaji, Historia na dhamiri ya mwanadamu yaani ufunuo wa jumla.
Ufunuo wa Kibiblia maana yeke ni ufunuo katika neno lake ni
mkusanyiko wa matendo ya Mungu aliyoyatenda na kusema akiwasiliana na wanadamu
katika njia maalumu na ujumbe wa agano jipya ni tafasiri ya matendo yake ufunuo
huo wote wa agano la kale na agano jipya umefungwa katika tukio kuu la Ukombozi
wa mwanadamu, Paulo anaonyesha kuwa Hata agano la kale lilikuwa likizungumzia
tukio hilo la ukombozi wa mwanadamu 1Koritho 15;3-4 ni wazi kuwa wakati huu
alipokuwa akinukuu maneno kama yanenavyo maandiko alikuwa akimaanisha Agano la
kale kwamba nalo lilikuwa linaona kwa mbali ukombozi ukikamilisha katika kifo
na kufufuka kwa Bwana Yesu kwa hiyo Historia ya wokovu Kerygma katika agano
jipya ni muendelezo wa kazi ya ufunuo ulioanza katika agano la kale hivyo neno
la Mungu ni ufunuo wa wokovu kwa maana ya agano la kale na agano jipya.
Kwa msingi huo Ufunuo wote wa matukio yaliyopita,
yaliyopo na yajayo yanakamilishwa katika tukio moja la Kufufuka kwa Bwana Yesu
na hivyo Mungu amajifunua kwa msingi wa maswala yajayo kwa kiwango cha juu
katika kristo na kwa mujibu wa Waebrania 1;2 kufanyika Mwili kwa Kristo
kunakamilisha maswala ya ufunuo wa tulikotoka tuliko na tuendako ufunuo huo
sasa unakuja kwa wanadamu kupitia neno lake yaani Biblia kwa hiyo Biblia sio tu
muelekeo wa Ufunuo lakini yenyewe ni Ufunuo kamili
Ili ufunuo uweze kueleweka unapaswa
kueleweka kwa kupitia kweli kuu Tatu
§ Mfunuaji ambaye kwa uwazi ni Mungu
§ Njia ya ufunuo ambayo ni maandiko
na katika maandiko haya tunaambiwa kuwa Mungu alijifunua kwa Njia mbalimbali
ambazo ni maono, Ndoto, usingizi mzito, Urim na thumim, kura, Muonekano wake
mwenyewe akijidhihirisha theophanies, kupitia malaika, mazungumzo ya kiungu,
historia na matukio na neno la Mungu au Kristo Yesu mwenyewe.
§ Mwisho Mpokeaji yaani mwanadamu
ambaye amejiweka katika utayari wa kupokea na kushuhudia
Biblia hata hivyo ni matokeo matukio ya
ufunuo wa Mungu ambapo anadhihirisha mpango wake wa ukombozi wa mwanadamu kupitia
Yesu Kristo Katika neno Mungu anawasiliana na mwanadamu aliyeanguka ingawa
uwazi kabisa wa ufunuo huo huja kwa muitikio wa imani wa kazi zilizofanyika
lakini mwitikio huo hauwi wa aina binaamu mwenyewe kwa matakwa yake bali ni
kazi kamili ya zawadi na msaada wa Roho Mtakatifu kazi hiyo ya ndani ya moyo wa
mwanadamu inayompa uwezo wa kupokea ufunuo huo huitwa illumination au Estimoium kwamba
mtu anaweza kukulia katika maandiko na kufunzwa katika maandiko lakini neno la
Mungu likawa halijafunuliwa kwake 1Samuel 3;7 kwa hiyo ingawa Mungu alizungumza
na Samuel zaidi ya mara tatu lakini halikuwa neno la Mungu kwake ni mpaka mara
ya nne ndipo Samuel alipoweza kuelewa na neno la Mungu likawa neno la Mungu
kwake, Ni mpaka mtu awe na uwezo wa kusikia na kupokea kwa moyo ndipo kweli ya Mungu inapokuwa yake
1Thesalonike 2;13.
Mamlaka kubwa ya maandiko inatokana na
kuvuviwa kwake na hivyo lafaa kwa mafundisho, kwa konya na kusahihisha na kutoa
mafunzo ili kuwakamilisha watu wa Mungu 2Timotheo 3;16-17 kwa hiyo Biblia ni ya
kimungu au ni ya Mungu kwaasili ingawa Mungu aliwatumia wanadamu kuiandika na
waliandika ujumbe kamili kutoka kwa Mungu lakini uelewa kamili wa uvuvio huo
lazima upokelewe katika mtazamo sahii wa Ufunuo kwa msingi huo awaye yote
anayeisoma Biblia anapaswa kujua kwanza msomaji alikuwa anakusudia nini kwa
wasomaji wake wakati huo, kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa mtu anapoisoma Biblia
kwanza anapaswa kusikiliza baada ya kuelewa ujumbe uliokuwa ukizungumzwa na
ujumbe kwa asili ulihusu nini ndipo unapaswa kujiuliza jinsi ujumbe huo
unavyomuhusu kwa wakati alionao lakini hii ni hatua ya pili.
Ufunuo ni lazima utofautishe na maswala
mawili Uvuvio (Inspiration) na
kuangaziwa (illumination). Ufunuo ni
mawasiliano ya taarifa kutoka kwa Mungu kumjia mwanadamu aliye katika hali ya
anguko ili ajue kile ambacho Mungu anakisema au anakifanya kwaajili yake,
Uvuvio unahusika na swala la Roho wa Mungu kuwatumia wanadamu kuandika kwa
mamlaka yale aliyokusudia wanadamu wawe nayo katika neno lake, lakini ingawa
maandiko yote yamevuviwa sio maandiko yote ni ufunuo ila tunaweza kuzungumza
kwa ujumla wake tu kuwa maandiko ni ufunuo kamili wa Mungu kwaajili ya
kuwasaidia wanadamu kumjua na kwaajili ya utukufu wa Mungu.
Kuangaziwa yani illumination ni kazi ya Roho Mtakatifu kumuwezesha msomaji wa neno
la Mungu kuwa na uwezo wa kuelewa maandiko akisaidiwa na Roho Mtakatifu
1Koritho 2; 13-14 kwa hiyo katika ufunuo Mungu anafunua kweli zilizokuwa
zimejificha lakini katika kuangaziwa iilumination aliyeamini anawezeshwa
kuelewa. Kwa hiyo Ufunuo ni Namna alivyowasilisha, Uvuvio ni jinsi
alivyowasilisha na kuangaziwa ni kwanini aliwasilisha hii inakuja kwa msaada wa
Roho wa Mungu.
KITABU
CHA UFUNUO WA YOHANA
Neno ufunuo kama tulivyogusia awali ni neno linalotokana
na lugha ya asili ya Kiyunani Apokavluyi
yaani Apocalypse ambalo maana
yake ni Kuweka wazi au kufunua kwa msingi huo kitabu hiki kiliitwa The
Apocalypse of John na sawa na neno hilo la Kiswahili Ufuno wa Yohana, hiki ni
kitabu cha Mwisho katika mfululizo wa Vitabu vya Agano jipya, ni kitabu cha kipekee
sana ukilinganisha na Vitabu vingine kwa ujumla, pekee katika Agano jipya ndio
kitabu ambacho kinafanana kwa nguvu na Vitabu vya unabii kama Ezekiel, Daniel
na Zekaria na kama ilivyo kwa Vitabu hivyo mwandishi alikuwa na kundi la watu
waliokuwa wakizungukwa na mateso na dhiki, Ufunuo ulikuwa ni waraka kwa
wakristo wa nyakati za karne ya kwanza, wakati wakristo wakiwa wametengana na dini
ya kiyahudi na wakiwa wanatambuliwa kama kundi linalojitegemea kwa Serikali ya
Kirumi.kwa hivyo kitabu cha ufunuo ni kitabu cha maswala yaliyokuweko na zaidi
sana maswala yajayo it is an escatological book.
UFAHAMU
KUHUSU KITABU CHA UFUNUO.
1.
Ufahamu
kuhusu Historia ya kitabu cha ufunuo
§ Historia
§ Jamii
§ Dini
2.
Umoja
§ Mwandishi
§ Tarehe
ya uandishi
§ Mahali
§ Makusudi
§ Muda
§ Malengo
3.
Kupitishwa
kwenye kanuni
§ Kutambuliwa
kwa kitabu cha Ufunuo.
§ Msimamo
wa kanisa la Magharibi.
§ Msimamo
wa kanisa la Mashariki.
§ Kukubalika
kwa ujumla.
§ Jinsi
ya kutafasiri litabu cha Ufunuo.
§ Theolojia
katika kitabu cha Ufunuo.
§ Mgawanyo
kamili.
Ufahamu
kuhusu Historia ya kitabu cha ufunuo
Historia.
Mazingira ya Kitabu cha ufunuo
yanachukua eneo la utawala wa Rumi ya zamani katika jimbo la Asia ndogo Asia minor, kulikuwa na uzushi wa kila aina
ambao ulikuwa umefunika mazingira hayo pamoja na imani Potofu na Kanisa
lilikuwa linapitia changamoto za Udunia na theolojia za kidunia kuingia katika
imani, Ibada za sanamu, lakini pia kulikuwa na mafanikio makubwa sana ya kiuchumi,
kulikuwa na majengo makubwa ya Miungu, waabudu, na watengenezaji wakubwa wa
sanamu, utoaji wa sadaka kwa miungu, pamoja na hayo watawala wakubwa kama Nero
(AD 54-68) na Domitian (AD 81-96) walikuwa waefikia kiwango kikubwa cha madai
ya kutaka kuabudiwa na hivyo kuharibu aina nyingine za imani, Wakristo walikuwa
wakikataa kuabudu wanadamu jambo lilolosukuma kuingia katika mateso na
kudhalilishwa kwa hali ya juu kutokana na imani yao.
Jamii.
Msukumo wa dini hizi jamii na aina ya
siasa na matukio tofauti tofauti yalisukuma na kuzalisha kanisa la kikristo
kuwa na maamuzi magumu, na ili kanisa liendelee kuweko na kujitambua au
kutambulika kama kanisa liliamua kuwa na msimamo, Mwandishi wa kitabu cha
ufunuo alikuwa ametengwa na jamii kwaajili ya Imani na haishangazi kuona
maandiko yake yakifunua uharibifu mkubwa wa utawala wa kirumi, tabia zao mavazi
yao na hulka ya ukahaba mavazi yao mekundu na ya rangi ya dhambarau tabia ya
mauaji mfano nikamwona mwanamke amelewa kwa damu ya mashahidi wa Yesu Ufunuo
17;6 ingawa maneno ya unabii yanaweza yakahusu nyakati nyingine lakini unapata
picha ya mazingira ya wakati ule na kanisa na hali zake.
Dini.
Utengano mkubwa wa Ukristo na Dini ya
kiyahudi ulikuwa mpana mara baada ya anguko la Yerusalemu mwaka wa 70 AD.
Wakati ule Kanisa na sinagogi la kiyahudi walianza kuwa na muelekeo tofauti
Fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani nje ya matendo ya sheria lilikuwa ni kama
upanga kwa wanasheria wa kiyahudi (Orthodox
Judaism) na waamini wa Kikristo na kuharibiwa kwa hekalu mwaka wa 70
kuliharibu kabisa hata uhusiano mwembamba uliokuweko kati ya wayahudi na
wakristo na kuharibika kwa uhusiano na kulaumiana na kushitakiana ndiko
kulikopelekea kuweko kwa lugha kama Sinagogi la shetani Ufunuo 3;9 na matokeo
yalikuwa ni kuachana kabisa kwa dini hizi mbili. Ndani ya kanisa kwenyewe kulikuweko
matatizo ambayo yanaakisi katika barua zile kwa makanisa yale saba ya asia
ndogo. Upendo ulikuwa umepoa, mmomonyoko wa kimaadili, Mafundisho potofu ambayo
yalichochewa na waalimu wa uongo, kuongezeka kwa anasa na starehe na kadhalika
Ufunuo ni kitabu ambacho pia kilikuwa kinajaribu kuamsha hisia za kumpenda
Bwana na kuwapa maonyo wasomaji na kuwaandaa kwa ajili ya ujio wa Yesu Kristo
na Hukumu ya mwisho pia kutia moyo kuwa hatimaye Mungu atakomesha siku moja
uovu na huzuni na kiburi cha ulimwengu na amani ya kweli itatawala dunia.
Umoja.
Mwanatheolojia R.H.Charles
ambaye ameandika Commentary kubwa inayohisika na maswala ya Ufunuo kwa undani
sana anachangia kuwa Mwandishi alikufa alipokuwa amekamilisha kuandika ufunuo 1
- 20;-3 katika kazi yake na shughuli ya umaliziaji iliwekwa katika mfululizo wa
kazi zake na mwanafunzi wake mmoja mwenye akili kwa kufuata utaratibu alioubuni
kuwa utahitimisha sawia mawazo yeke. Charles anaeleza kuwa Kitabu cha ufunuo
kimepangiliwa katika mfumo wa mawazo yanayobebana kwa ufasaha jambo linaloleta
umoja mpangilio na mtindo unaoonyesha umoja. Maono yote kwa ujumla yamelenga
katika kiti cha enzi cha Mungu kama chanzo cha maono hayo na kwa vyovyote vile
inaonekana kabisa kuwa mpangilio wake unatoka katika chanzo kimoja namna mawazo
yanavyojegwa na tabia ya usafi wa maono yenyewe unadhihirisha wazi kuwa
muandishi alikuwa Patmo utumwani na kuwa ujenzi wa mawazo ya ndani utangulizi
wa kila waraka ulioandikwa kwa makanisa yale saba unalenga katika maono yele
aliyoyaona mwandishi kuhusu Kristo na namna anavyohitimisha kwa ahadi ni wazi
kuwa ahadi izo zilikuwa zinalenga ule mji mtakatifu wa Mungu ambao anahitimisha
nao aidha mpangilio wa matukio na hatua za hukumu kutoka moja hata nyingine
utaratibu wa kufunguliwa kwa muhuri na
ufafanuzi wae toka sura ya 5-mpaka – ya 20 hata kama kuna muingiliano Fulani
haviaharibu umoja wa uandishi huo wa msingi wa uhalisia kuwa kitabu hiki kina
umoja na kuwa kimeandikwa na mtu mmoja.
Mwandishi.
Mwandishi najaitambulisha kamaYohana
amejiita Mtumwa wa Yesu Kristo ndugu wa wote wenye kuushiriki mateso na ufalme
na subira ya Kristo Ufunuo 1; 1, 9 maono anayoyawakilisha kwenye kitabu hiki
alionekana kuyapokea akiwa huko Patmo ambako alipelekwa utumwani kwaajili ya
Jina la Yesu au imani ya Kikristo alifahamika kwa makanisa mengi ya Asia ndogo
na aliwekwa katika daraja la Manabii Ufunuo 22:6, 9, 19, huyu ndiye mwandishi
aliyeandika kitabu cha Ufunuo
Simulizi za kijadi zinaeleza kuwa
mwandishi ni Yohana mwana wa Zebedayo ambaye pia ni mwandishi wa injili ya
Yohana na nyaraka tatu zilizoitwa kwa jina lake Mwanatheolojia
§ Justin
Martyr aliyeishi AD 150 alisema hivi Ufunuo umeandikwa na mtu mmoja miongoni
mwetu ambaye jina lake aliitwa Yohana mmoja wa mitume wa Yesu Kristo.
§ Irenaeus
Askofu wa Lyons alithibitisha kwa nakala nyingi zilizokuwa tayari kama ushuhuda
kutoka kwa watu waliomuona Yohana Uso kwa uso
§ Tertulian
aliyeishi AD 200 alielezea Ufunuo kama kitabu kilichoandikwa na Yohana na
alimtambua Yohana ambaye alikuwa moja wa mitume wa Bwana
§ Origen
AD 225 alichangia kuwa mwandishi ni Yohana mpaka karne ya pili na ya tatu
Ufunuo wa Yohana kilianza kukubaliwa na makanisa na wasomi kama huko Alexandria
§ Ufafanuzi
wenye kuonyesha mlengo mkubwa kabisa wa kuwa Yohana ndiye mwandishi ulitolewa
na Dionysius wa Alexandria ambaye alikubaliana na mawazo mengi ya kijadi au
masimulizi ya kijadi kwamba Yohana ndiye mwandishi alisema kuwa Ufunuo
unajikiri wazi kuwa Yohana ndiye mwandishi wakati injili na nyaraka zake
hazifanyi hivyo alisema misamiati na muundo wa Lugha na maarifa una nguvu za
kuthibitisha kuwa Yohana ndiye mwandishi ingawa wengine wanahoji kuwa kitabu
hiki kiliandikwa kwa mpangilo wa grama nzuri na fasaha za kiyunani jambo
linalotia shaka kama Yohana Mwebrania ndiye aliyeandika.
§ Eusebius
akifuata nyayo za Dionysius alihoji mamlaka ya kitabu cha ufunuo alichangia
kuwa ni kweli kuwa Injili na nyaraka za Yohana hazikuwa na majina lakini
zilithibitishwa kuwa zake na wale waliomjua na kuzipokea nyaraka zile alisema zenyewe zinabeba ushahidi kuwa ni neno
la Mungu na zinashuhudia wazi kuwa ziliandikwa na mtu ambaye alimuona Yesu kwa
jicho lake Yohana 1;14, 21;24, ni wazi kuwa hata kama ufunuo kinataja jina la
Yohana anayedhaniwa siye mwana wa Zebedayo lakini kuna maelezo yaliyo wazi
katika Ufunuo 1;2 kuwa aliyeandika alimshuhudia Yesu wazi wazi kwa kumuona. Kwa
msingi huo hata kama mtindo wa uandishi unaweza usikubaliane haimaanishi kuwa
basi mwandishi wa injili na zile nyaraka siye mwandishi wa Ufunuo.
§ Mabadiliko
ya misamiati wa uandishi katika nyaraka na injili tofautia na ufunuo unaweza
ukachangiwa na maswala kadhaa kwa nini kuna tofauti kubwa Injili imenukuu habari
za Yesu na ni wazi kuwa habari za Bwana Yesu mwana wa Zebedayo aliandika
akikumbuka matukio ya siku nyingi wakati Yesu alipoishi duniani tena katika
mtazamo wa Kikristo wakati ufunuo kiliandikwa mwandishi akiwa katika hali ya
migandamizo Stress tena mwandishi akiwa utumwani au gerezani na kumbuka
alichokuwa anakiandika ni maono. Injili iliuwa ikishughulikia mazingira yaliyokuwa
sahii ya amani na mwandishi alikuwa akishuhudia wazi yaani iliandikwa katika
mazingira ya maisha ya kawaida, Lakini ufunuo umejaa maono, ishara vitu vigeni
watu wageni, viumbe vigeni na mazingira ambayo yalizingirwa na uwepo wa
kimungu, lakini pamoja na hayo bado kuna kufanana kukubwa kwa matukio ya ufuno
na uandishi wa Yohana
§ Alimuita
Yesu kwa namna ileile aliyozoea kumuita Neno la Mungu Yohana 1;1 Ufunuo 19;13.
§ Alimuita
mwanakondoo Yohana 1;29 Ufunuo 5;6
§ Mchungaji
Yohana 10;11 Ufunuo 7;17
§ Anavyomzungumzia
shetani ni kwa namna ileile Yohana 8; 44, 27, 14; 30, Ufunuo 2; 10, 12; 9, 20; 2,
7, 10.
§ Kisha
msisitizo wa Kifo cha Yesu Kristo Yohana 12;32 na Ufunuo 1; 5, 5; 6
Kufanana
huko sio lazima kuwe sawasawa lakini kunathibitisha wazi kuwa tunaweza
kuhitimisha kwa kusema kuwa maandiko haya ya Ufunuo ni wazi kuwa ni wa Yohana
mwana wa Zebedayo. ni wazi uwa kitabu hiki kiliheshimika sana na makanisa ya
Asia ndogo ambayo kihistoria walimjua Yohana vema kwa hivyo hakuna shaka kuwa
Mwandishi ni Yohana mwana wa Zebedayo aliyekuwa Mtume wa Bwana Yesu. na kuna
uwezekano kuwa labda injili ya Yohana iliwekwa sawa kiasi Fulani na msaidizi
wake aliyehitimisha mchango wa mwisho katika Yohana 21; 24-25.
Yohana
mwana wa Ngurumo Mtume wa upendo
Ni wazi kuwa kulingana na mapokeo na
vyanzo vyote vinavyopatikana vinathibitisha wazi kuwa Yohana alikuwa ndiye
mtume pekee aliyekufa kifo cha kawaida na bila shaka kuwa huyu ndiye mwandishi
wa kitabu cha ufunuo
§ Yohana
huyu alikuwa ni ndugu yake na Yakobo wana wa Zebedayo, ingawa wao mara kwa mara
wanatajwa pamoja Yohana anafahamika
zaidi kutokana na maandiko yake na yakobo inaeleweka wazi kuwa alikufa mapema
sana mongoni mwa mitumeYeye aliitwa na Yesu toka kuwa mvuvi wa kawaida kuwa
mvuvi wa watu na pamoja na nduguye waliitwa na Bwana wana wa ngurumo hii
inawezekana kutokana na tabia zao za ukali Luka 9;54
§ Yeye na ndyguye wakati Fulani walikuja na ombi la
ajabu kutaka kuketi upande wa kuume na kushoto Marko 10;35-37
§ Mapema
katika utumishi wa Yesu Yohana aliwakilisha shitaka la kukemewa kwa mtu
aliyekuwa anatoa pepo lakini hafuatani na wao Marko 9;38 ni wazi kuwa Kristo
aliwakemea mara kwa mara katika makosa yao hayo yote
§ Kwaajili
ya unyenyekevu uliojengeka baadaye ni wazi kuwa ilikuwa mara chache sana
kujitaja jina lake katika ijnili yake badala yake alijiita mwanafunzi
aliyependwa sana na Yesu Yohana 13; 23, 19, 26, 20; 2, 21; 17, 20. Mwana huyu
wa ngurumo alikuwa amekwisha kujifunza kuachana na mambo ya ukuu na kuwa mwana
wa upendo aligundua kuwa Upendo sio maneno bali ni matyendo, la muhimu sio cheo
bali ni uwepo wa Mungu
§ Aliwaasa
watu aliowaita watoto wake kupenda kwa matendo na sio kwa maneno 1Yohana 3;18
alikuwa ameacha kabisa tabia ya kuwa kimbelembele na kutaka kuwa wa kwanza na
sasa anakemea hata watu wenye tabia kama ile 3Yohana 9
§ Hata
ingawa alikuwa sasa amezeeka sana moto wa injili ulikuwa ukiwaka ndani yake
alihesabu mateso ya uzeeni kuwa ushuhuda wa Yesu Ufunuo 1;9 mateso na shida
alizozipata huko patmo halikuwa jambo la muhimu kulieleza zaidi ya kile
alichoagizwa na Kristo
§ Ni
wazi kabisa kuwa kila mmoja ana maswala ya kujifunza kutoka kwa Yohana
mabadiliko yake kutoka tabia ya ngurumo mpaka kuwa mtume wa upendo,
kutokujihusisha na kusimulia mapito na badala yake kile ambacho Yesu alikuwa
amemuagiza, mzigo wa kulitia moyo kanisa kuliko kutaka kutiwa moyo yeye
mwenyewe, kuwa katika roho siku ya bwana hata pamoja na kuwa katika mazingira
magumu kunaonyesha jinsi alivyotoa kipaumbele kwa maswala ya ibada
Tarehe
ya uandishi
Kuna hisia kubwa tatu kuhusu tarahe ya
uandishi wa kitabu cha ufunuo wa Yohana kulingana na mitazamo tofauti tofauti
§
Epiphanius aliandika mnamo katika karne ya Tatu
kuwa Yohana aliandika kitabu chake cha ufunuo mara baada ya kurudi kutoka Patmo
wakati wa utawala wa Claudius mwaka 41-54 lakini tarahe hii haikubaliki kwani
ni mapema sana makanisa mengi ya asia ndogo yalikuwa hayajaanzishwa wakati huu
nah alia ya uhasama kati ya ukristo na serikali ya Rumi pia ilikuwa
haijachachamaa, inchi ilikuwa haijaendelea katika ngazi ambayo kibabu
kinaonyesha kwa misingi huo kuna
uwezekano kabisa kuwa Epiphanius alikuwa akizungumzia Nerp ambaye pia aliitwa
Claudius.
§
Mjadala kuhusu kuandikwa kwa kitabu hiki wakati
wa utawala wa Nero umejengeka saa AD 54-68 kutokana na kuweko kwa alama maarufu
katika kitabu cha ufunuo yaani 666 kwa kuzijumuisha pamoja namba hizi unapata
thamani ya namba za herufi NERON KESAR kwa kiebrania jumla ya namba hizo
zilitambuka kumaanisha hilo.Maswala mawili yanaweza kuhusishwa kinyuma na dhana
hii, kwamba kuna Herufi nyingi sana ambazo zikijumuishwa zinaweza kuleta idadi
kama hiyo na pili kwa jamaii ya Asia ndogo ingekuwa vigumu kwao kuwahusisha na matumizi ya herufi za Kiibrania
§ Tangazo
la kuweko kwa Milima inayomsaidia Mwanamke katika ufunuo 17 imekuwa ikitumiwa
pia kumaanisha wakati wa Nero, vile vichwa saba ni milima saba anayoikalia hupo
na mwingine hajaja bado naye atakapokuja
imempasa kukaa muda mchache na Yule mnyama aliyekuwako naye hayuko yeye ndiye
wa nane naye ni mmoja wa wale saba naye anaenda kwa uharibifu Ufunuo 17;9-11
§
Kama tukio hili linahusishwa na kupeana
madaraka kwa watawala wa kirumi wafalemwa kwanza wa Kirumi ni pamoja na Julius
Caesar, Caesar Augustus,Tiberius, Caligula na Claudius na kama hao watano
wamekwisha kuanguka wasita ni Nero na hapo ndipo kitabu cha Ufuno kilipoandikwa
yaani wakati wa utawala wa kaisari Nero. Tafasiri
hii sio uhakikisho wa ukweli kuwa wafalme
hao hawatupi uhakika kuwa kwa sabau hatujui ni yupi anahesabika kama wa kwanza
Augustus au la kama ni Augusto basi Nero anahesabika kama mfalme wa tano na kwa
kweli Nero hakutawala muda mrefu sana kiasi cha kuwa wa muhimu katika utawala
huo na hivyo Vespecian anakuwa wa sita na Tito anakuwa wa saba na Domitian
anakuwa wa nane lakini kitabu kinaashiria kuwa ulikuwa wakati wa ukatili mkubwa
wa Nero lakini makanisa ya asa yalikuwa hayajafikia kiwango cha mafanikio
makubwa wakati wa Nero.
§
Kwa mujibu wa maelezo ya jadi ufunuo ni
kitabu kilichoandikwa wakati wa Utawala wa Domitian kwa mujibu wa ushuhuda wa
Irenaeus, Clement wa Alexandria pia alikubali swala hilo na ni kweli kuwa
katika wakati huo makanisa ya Asia yalifikia kilele kikubwa cha mafanikio na
huu ulikuwa wakati wa utawala wa Domitian na huyu alikuwa na madai ya
kuabudiwa kama Dominus et dues akiwa
anatajwa kama mnyama aliyekuwa na nguvu kubwa ya kisiasa Ufunuo 13;15 na
inakubaliwa kuwa jumla ya namba ya mnyama huyo inamuhusu Domitian yaani 666
ambaye kwa idadi ya herufi za jina lake Domitian yaani A[utokrator] KAI[sar]
DOMET [ianos] SEB[astos] GER[manikos].kwa
kujumlisha idadi ya hesabu ya herufi zake kwa kiyunani unapata jumla ya namba
hiyo 666 na kwa kuwa idadi hii inakubalika sambamba na jina la Domitian
haliwezi kuthibitishwa inakenda sambamba na kukubalka pia kwa jina la Nero .
Mahali
§ Kisiwa
cha Patmos mahali ambapo maono yalipokelewa na kuna uwezekano kuwa yalinukuliwa
pale au baadaye huko Efeso, Patmos ni kisiwa kilichoko juu ya mwamba katika
Bahai ya Aegean (Aegean Sea) katika ukanda wa bahari ya Asia ndogo, lilikuwa ni
eneo la koloni la warumi, mahali hapo wafungwa wa kisiasa walipelekwa wakilazimishwa kufanya kazi ngumu na kuchimba
madini, Yohana alisisitiza kuwa alikuwa huko Patmo kwaajil ya neno la Mungu na
ushuhuda wa Yesu Kristo Ufunuo 1;9, aidha mafunuo hayo yaliandikwa hukohuko
Patmo au vinginevyo ni wazi kuwa kulikuwa na muda mfupi sana tangu kupokelewa
na kuandikwa kwa maono hayo na kwa namna yoyote ile yanaakisi lugha na mazingira
ya Kirumi, na jimbo la Asia ambako kwa
wakati huo mwandishi ndiko alikotokea na alikoishi.
§ Patmo
kwa kiyunani Pavtmo ni kisiwa klichoko pwani ya Asia ndogo kama maili 35 kusini
magharibi mwa kisiwa cha Mileto ni kisiwa chenye miamba na milima na kima ukubwa
unaokisiwa kama Maili kumi kwa sita na kina ukavu na baridi kali kwa sifa zake
na ni mahali palipotumiwa na Warumi kama eneo la Mateso inaaminika kuwa miaka
ya zamani wa Italy walikiitakisiwa hiki Palmosa wakimaanisha kisiwa chenye
Mitende kwa hiyo inaaminika kuwa zamani kilikuwa na Miti ambayo ilkatwa na
hatimaye kukiacha kisiwa hiki kikiwa kikavu na kuna uwezekano kuwa hakuna maji.
§ Ni
katika kisiwa hiki ndio Yohana alipelekwa kuadhibiwa na Mtawala wa wakati huo
Domitian na hapo ndipo alipopokea yale maono na kuyaandika Ufunuo 1;9-11
§ Historia
ya kisiwa hiki Ilibadilika mnamo miaka ya 1088 wakati mtawa Christodulos
alipojenga Ngome ya kitawa ya Mtakatifu Yohana katika eneo ambalo zamani
kulikuwa na Hekalu la Artemi na miaka ilivyokwenda watawa waliishi hapo na
kujifunza maswala kadhaa na kulima pia kuliwekwa( Library) Maktaba Patmos
ilikuwa mahali pa kazi za Wayunani wa Ki Othodox lakini 1453 walitafuta msaada
kwa Papa wa rumi kwaajili ya usaidiwa dhidi ya waturuki kwenye Karne ya 16
kikawa chini ya waturuki lakini waliachiwa wajiongoze na kuendesha mambo yao
chni ya sultani.Mwaka 1832 kisiwa kiliangukia katika utawala wa waturuki na
baada ya 1912 kilirejeshwa kwa Warumi na ilipofika 1947 kilikabidhiwa kwa
Wayunani au Ugiriki hata leo.
Makusudi
§
Makanisa ambayo viongozi wake wametajwa katika
kitabu cha ufunuo yalikuwa yameunganishwa na barabara inayoelekea upande wa
Kaskazini kupitia pwani ya Efeso mpaka Pargamo kupitia Smyrna. Kutoka Pargamo
kuna njia nyingine inayoelekea kusini zaidi bara na kugusa miji ya Thyatira,
Sardis, Philadelphia na Laodikia na kisha njia inarudi nyuma kuelekea Efeso,
Kama mjumbe angelipewa Barua au ujumbe angeweza kukamilisha mzunguko huo kwa
urahisi, Efeso ndio ulikuwa mji mkubwa mtukufu wa Hekalu kubwa la artemis na
Huko Pergamo ndiko kulikokuwa na madhabahu kubwa ya Zeus, Thyatira ulikuwa mji
wa kilimo na utengenezaji wa nguo.
Muda
§ Utawala wa Domitian ulianza kwa usumbufu mkubwa,
Uharibifu wa Pompeii na Herculaneum na mauaji ya kikatili ya uchunaji ngozi ya
Vesuvius mwaka 79AD. Ikifuatiwa na matukio mabaya yaliyoipiga Rumi kwa magonjwa
na uasi katika mji mpaka 81AD wakati Domitian akiingia madarakani, Alipoingia
madarakani aliamuru kuabudiwa na alijiita kwa Kilatin Dominus et Deus yaani
Domitian ni Bwana na Mungu yeye alikuwa mtawala wa kwanza kujilinganisha na Mungu,
ingawa wengine walitaka kuabudiwa na walikuwa wakipokea Ibada hata kwa
kulazimishwa, Domitian alijitangaza kuwa
Mungu na mama yake Domitia kuwa mungumke fedha yake ilikuwa na alama ya mwezi
na mtotoaliyeketi katika njia ya kuzunguka dunia pamoja na sayari kwaajili ya
kumkumbuka mwanae aliyefariki akiwa mdogo mwaka 83AD.
§
Heshima
yote ambayo alikuwa anastahili kupewa mwokozi Yesu Kristo ilidaiwa kupewa
Domitian, Domitian alikuwa muuaji, alimuua mwana wa dada yake Titus Flavius
Clemens na alimuua mke wake, Domitilla inasemekana kuwa Clemens alikuwa Mkristo
na Domitilla alikuwa akifuata tamaduni za kiyahudi kwa siri, huku yeye aliamini
kuwa hakuna Mungu “Atheism” Eusebius anaeleza kuwa Domitian alijistawisha mwenyewe
kama mrithi wa Nero kwa ukatili na mwenye kustahili kama Mungu, ni mfalme wa
pili kuinua kiwango cha mauaji na mateso kinyume nasi.... Eusebius alikuwa
akimnukuu Hegesippus aliyekuwa akishuhudia ushuhuda wa Yohana alipokuwa amerudi
Efeso baada ya kuachiliwa wakati wa utawala wa Nero mwaka 96.
Malengo
§
Kitabu cha
ufunuo kiliandikwa kwa makanisa yaliyokuwa yamefunikwa na tishio la mateso kwa
lazima, kulikuwa na tishio la maafisa waliokuwa wakipita huko na huko kutoa
vitisho na kwa sababu ya aina ya mapito waliyokuwa wakiyapitia walihitaji
kutiwa moyo ili waendelee na kusimama imara katika imani na kuwaonya dhidi ya
uadui kutoka nje na ndani, na mafundisho potofu yenye ukengeufu, kwa hiyo
pamoja na hali halisi iliyokuweko ndipo sa maswala haya yanajitokeza katika
kitabu cha ufunuo.
§
Kanisa linatiwa
moyo nakuelekezwa katika kutazamia ujio wa Yesu na kuwa atakuja kuwahukumu
maadui na kuliokoa kanisa maswala ambayo yanajitokeza Ufuno 2;5, 16, 25,
3;3,11, 20 na msisitizo wa maneno tazama naja upesi 3;11, 22;7, 12, 20 kwa hiyo
maandalizi ya ujio wa Kristo mara ya pili ni msingi wa kitabu cha ufunuo.
KUPITISHWA
KWENYE KANUNI
§
Utambuzi
wa mapema. Kulingana na ushahidi uliokuweko mwanzoni kitabu cha ufunuo
hakikukubaliwa na makanisa yote mwanzoni kilikuwa kinafikiriwa kuwa ni swala la
mauzauza tu allusions kutoka kwa wachungaji wa Hermas 140AD, lakini
haikuendelea kusadikiwa hivyo kwani Kutokana na Mwanahistoria Jerome Melito ya
Sardis AD 160-190 aliandika katika michango yake akisimulia kuhusu Justin
Martyr AD 135 alihibitisha kuwa kimeandikwa na Yohana mmoja wa wanafunzi wa
Bwana Yesu, Irenaeus aliyekuwa Askofu wa Lyons alikubali kuwa kitabu hiki kina
asili ya utume na kinakubalika
§
Kanisa la
magharibi Kanisa la Alexandria walikuwa wataalamu wa maswala ya kinabii na Clement
alikikubali kuwa ni maandiko na wanafunzi wake ama Origen alikikubali ingawa
Dionysius wa Alexandria alikataa kuwa sio cha Yohana ingawa alikuwa anajua kuwa
kimekubaliwa na makanisa, katika kanuni ya kanisa la Roman iliyopitishwa na
Muratorian Fragment AD.170 walikijumuisha kama moja ya Vitabu na mwanatheolojia
Hippolytus (190-235) alikinukuu mara nyingi, kanisa la Cathage ambalo lna asili
ya Rumi pia walikkubali, Tertullian(190-220) alinukuu sura 18 kati ya 22
zilizokuweko, kanisa la maghari la karne
ya 2 kwa ujumla walikubali kitabu cha
ufunuo, ni sauti mbili tu kama ya marcion aliyekuwa na mipaka yake
aliyojiwekea kwani alikuwa myahudi na
Alogi ambaye alipinga kazi za Epiphanius na Irenaeus na hakuunga mkono kazi
yoyote au wazo lolote linalohusiana na unabii lakini mpaka karne ya tatu
kilikuwa kimekubalika kabisa katika kanuni.
§
Kanisa la
mashariki walikuwa kwa namna Fulani kama maadui wakubwa wa Ufunuo hii
huenda ilichangiwa na kutiwa shaka na Dionysus Askofu wa Alexandria ambaye
alikitilia mashaka, pia Eusebius 260-340 alifuata muongozo huo, yeye
hakukiorodhesha kabisa kitabu hiki inawezekana hili pia lilichangiwa na kuweko
kwa Ofisi ya Papa na tafasiri yake kuhusu millennium,Ushawishi wa Eusebius ulikuwa
na nguvu, naye Cyril wa Yerusalem AD 315- 386 alikataza watu wa kanisa kukisoma
kitabu cha ufunuo hadharani au madhabahuni na alikikataza kutumika hata kwa
kujitoa binafsi, Baadaye makanisa ya Asia ndogo hayakujumuisha kitabu hiki kwa
vile hakikuorodheshwa na mkutano wa Kanuni wa Synod wa Laodekia AD 360 wala
katika katiba ya mitume wala katika orodha ya Gregory Nazianzus, Naye thoodore
wa Mopsuestia AD 340-428 alikikikataa kitabu cha ufuno akiambatanisha na waraka
wa kikatoliki aliongoza kanisa la ki Nestorian pamoja na shule ya Antiokia,
Mpaka katika karne ya 4 na 6 ndipo hatimaye kitabu cha ufunuo kilikubalika na
kanisa la mashariki, Andrew wa Kaisaria huko Kapadokia aliandika mafafanuzi ya
kitabu hicho na Leontius ambaye alikuwa Msomi huko Yerusalem alisema ni kitabu
cha mwisho kukubalika na kupita katika kanuni ya Vitabu vya agano jipya.
§
Kukubalika
kwa ujumla.
Kukubalika
kwa ujumla kwa kitabu cha ufunuo kulitambuliwa rasmi baada ya barua ya Festal
wa Athanasuis kunasadikiwa kutoka Alexandria mwaka 367, na mkutano wa Damasine
Council wa 382 na mkutano wa Carthage wa 397 na cheti maalumu cha kuvitambua
Vitabu na maandiko ya agano jipya kwa wa magharibi, na huko mashaiki msimamo wa
kanisa ulitolewa kwa uthabiti mnamo karne ya pili na mamlaka yake kutambuliwa
baadaye.
Jinsi ya Kutafasiri Kitabu cha Ufunuo.
Ni muhimu
kufahamu kuwa kutafasiri kitabu cha ufunuo ni swala Gumu kwa namna Fulani na
hakuna tafasiri mbili zinazoweza kukubaliana sawasawa hii ni kwa sababu
zinazungumzwa ishara na lugha za mafumbo na kuna wingi wa Maruweruwe Illusions
maswala ambayo wakati mwingne ni vigumu kujua hatima yake, Kwa ujumla kuna
shule kuu nne za kutafasiri kitabu hiki
1. Preterit: Unabii huu ulitimizwa wakati wa Kanisa
la kwanza lilipopitia katika
mateso
yaliyoendeshwa na Warumi. Wengine
wanaamini kuwa unabii ulitimizwa mwaka 70 BK wakati Yerusalemu ulipoangamizwa.
2. Historicit: Nabii hizi
zinahusiana na watu na matukio mbalimbali yaliyotokea huko nyuma – km. Napoleon na kuinuka kwa Uislam.
3. Idealist: Matukio yanaelezea mifano ya kiroho
kuhusiana na mapambano kati ya Mungu na shetani uovu na haki.
4. Futurist: Nabii hizi zinahusiana na matukio
halisi yatakayotokea siku zijazo ili kukamilisha mpango wa Mungu. Ni wazi kuwa
sisi tunaofuatilia makala haya tunaamini katika mfumo huu wa tafasiri za kitabu
cha ufunuo kwani ndivyo tunavyoamini.
MAMBO MUHIMU:
Kitabu
cha Ufunuo ni cha aina ya Apokrifa, hivyo:-
§
Kinatumia
ishara na mifano kutoa ukweli
§
Malaika
wanaoelezea matukio
§
Kinaonyesha
ushindi wa Mungu juu ya shetani.
KANUNI ZA KUTAFSIRI NA MAANA ZAKE:
Kanuni Na. 1 - Acha Maandiko yatafsiri
yenyewe – Eze. 12:1-16
Kanuni Na. 2 – Tumia mwonekano wa unabii –
mf. Lk. 4:16-21; Isa. 61:1,2
Kanuni Na .3 – Tambua kutumia mara mbili kwa
andiko la unabii
Kanuni Na. 4 – Elewa matumizi ya ishara na
mifano.
Aina za mifano Mfano Maana:
Namba moja Mungu
Mbili Kuhakikishwa
Tatu Utatu
Nne Dunia
Sita Mwanadamu,
uovu
Saba Utimilifu
wa Mungu
Kumi Kukamilika
kwa siasa
Kumi
na mbili Mwisho wa
kukamilisha
Wanyama Mwanakondoo Yesu
Farasi Uwezo wa
Kijeshi
Wanyama Mpinga Kristo na
nabii wa uongo
Vyura Mapepo
wachafu
Silaha Yesu
Rangi Nyeupe Utakatifu
Nyekundu Damu vitani
Nyeusi Baa la Tauni
Zambarau Anasa za Kifalme
Kijani Burudisho
Kijivujivu Mauti.
Theolojia
katika kitabu cha Ufunuo.
Ingawa maswala ya ufunuo hayatiliwi mkazo
katika Theolojia ni muhimu kufahamu kuwa kitabu cha Ufunuo kina magfundisho
yaliyowazi yenye kukazia kuhusu maswala yajayo au matukio ya mwisho wa dunia
Escatology ni wazi kuwa tunaona katika maono haya hatima ya baadaye ya kanisa
katika mpango wa Mungu na juu ya maswala yajayo
Kitabu hiki kwanza kinatuonyesha jinsi
Mungu alivyo mwenyezi na kuwa ni Bwana juu ya yote ni wazi kuwa kiini cha
kitabu hiki ni kiti cha enzi cha Mungu kitabu hiki kinatukumbusha kuwa Mungu ni
Mwenyezi ni mkuu kuliko ufalme uwao wote ukiwamo ule wa Rumi, nguvu zake ziko
juu kuliko hata taifa lenye kutisha na ndie mwamuzi wa jinsi gani, lina na
wakati gani atahukumu na kuwa anajua namna ya kushughulika na wanadamu walio
waovu na kila uasi wa aina binadamu yeye ni mwenyezi 4:8; 11:17;
15:3; 16:7, 14; 19:6, 15; 21:22 na ni muumba wa kila kitu 4:11; 14:7 na
muhukumu wa wanadamu 20:11-15).
Utatu wa Mungu umegusiwa katika ufunuo 1;
4-5 ambako kuna mazungumzo juu ya yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja,
Roh saba zitokazo katika kiti cha enzi cha Mungu na Yesu kristo ni wazi kabisa
kuwa kitheolojia kuna utatu hapa na swala hili linajitokeza katika kitabukizima
ingawa si katika namna ambayo inaorodheshwa pamoja kila wakat kwa hiyo kitabu
kizima kinamfunuo yeye Kristo Ufunuo 1;1.
Katika kitabu cha Ufunuo kuna somo kuu la
Ufahamu kuhusu kristo Christology, kuna Historia ya sifa za Kristo za kipekee
Ni samba wa kabila la Yuda Ufunuo 5;5, alikuwa na mitume kumi na wawili 21;14
alisulubiwa huko Yerusalemu 11;8 na alifufuka kutoka kwa wafu 1;5,18,
ametukuzwa 3;21 na ana sifa zote zilizoorodheshwa katika sura ya kwanza.
Ana mamlaka dhidi ya Historia 5;6-12 ndio
ufunguo muhimu wa kitabu hiki, ni Kondoo aliyechinjwa kwa sadaka 5;6 kama samba
wa Yuda ni Mrithi wa kiti cha Enzi cha Daudi 5;5 ni mwana wa Adamu aliyeshinda,
atokeaye juu ya mawingu kukamilisha mavuno ya ulimwengu 14;15 Anaitwa Neno la
Mungu 19;13 ni mlinzi wa kanisa 1;12-20 na muhukumu wa mwisho wa ulimwengu
11;15 na ndiye Nuru ya mji ule uja 21;23.
Kazi za Roho Mtakatifu zinaorodheshwa
ingawa mkazo katika kushughulika na mtu mmoja mmoja haukaziwi sana,
anawakilishwa kama Roho saba za Mungu Ufunuo 1;4 ndiye aliyetengeneza mazingira
mpokeaji kupokea maono 1:10; 4:2; 17:3; 21:10. Inagwa
matumizi ya neno roho yanaonekana kutumia neno Pnuvmati kumaanisha hali ya hisia alizokuwa akizipata muona maonao
kuliko kuhusu nafsi lakini Roho yuko pamoja na Bibi harusi wa Yesu kristo na
anahusika katika amri ya kuja na kunywa maji ya uzima ufunuo 22;17.
Hali ya mwanadamu mbele za mungu inawekwa wazi, wanadamu
wamejitenga na ungu wanamuhofu 6;16, 17 na mawindo wazi ya pepo wachafu 9:4;
13:3, 14; 17:8 na hatimaye watahukumiwa kwa matendo yao Ufunuo 20;12-13, Wokovu
unahakikishwa kwa waamini 7;3 mwisho wa walioamini na wasioamini unawekwa wazi
kuwa waasi ni katika ziwa la moto 21;8 na waliokombolewa kwenye miwa Mungu
22;14.
Pia kuna theolojia ya hali za kiroho ambazo waamini
wanapaswa kuwa nazo na zisizopaswa kuwa ambazo zinaelezwa kwa wingi katika
kitabu hiki sura ya 1-3 mwanzoni, mfano uvumilivu wakati wa mateso, upendo kwa
Yesu, uaminifu n.k vinakaziwa katika kitabu hiki.
Ulimwengu wa kiroho wa kishetani unawekwa wazi huku
shetani na mapepo yakitajwa sawa na sifa zao 9;4-11 ni wazi pia kitabu cha
ufunuo knaweka wazi kuwa mgogoro tulionao kati yetu na shetani ni wa kiroho na
ni vita na uwa ulianzia mbinguni na kuja
duniani 12;7, hatinma yeke inawekwa wazi kuwa hatimaye atahukumiwa 12;9 na
Mungu atashinda na shetani atatupwa katika ziwa la Moto 20;1-3,10. Na kongozi
wa kisiasa aliye kiyume na maswala ya Mungu anayetajwa kama mnyama hatimaye
ataharibiwa Ufunuo 13.
Swala la malaika nalo limazungumzwa kwa uapana sana katika
kitabu cha ufunuo kuliko kitabu kingine chochote katika agano jipya kwa mafano
kwa kila kanisa moja kna malaika na pia
wametajwa Karibu katika kila sehemu ya kitabu hikikuwa ni watumishi wa Mungu
5:2; 7:2, 3; 8:2; 10:1; 12:7; 14:6, 8, 9, 17; 15:1; 17:1; 18:1, 21; 19:17;
20:1; 21:9; 22:8 viumbe vyeye uhai Ufunuo 4;6-8 vinafanana na maserafi wa Isaya
6 na ni wazi kuwa vi viumbe maalumu sana
na pia tunawekewa wazi kuwa malaika na mapepo ni viumbe walio katika namna
moja ya maumbile ya kiroho wakigawanywa kuwa wema na waovu Ufunuo 12;7
Ni wazi kuwa msingi na makazo wa Kitabu hiki ni mambo
yajayo na mafundisho yote yanakubaliana na mpango wa Munu katika historia 2:7,
10, 17, 28; 3:5, 12, 20 eneo jingine linahusika na maswala ambayo hayaa budi
kuja upesi na kutimia sifa za Mungu zinawekwa wazi,mpango wake wa uumbaji
unawekwa wazi,umbaji mpya unawekwa wazi,kazi za Yesu za wokovu zinawekwa wazi,
kazi za uovu zinawekwa wazi hali ya baadaye ya watu waliokombolewa zinawekwa
wazi sura ya 19-22 hili ni lengo la ki-
eschatological
Mgawanyo kamili
Ingawa kitabu cha ufunuo kinaonekana kuwa
ni maono lakini kimekaa katika mgawanyo mzuri na mapangilo mzuri unaofaa ambao
unaweza kugawanywa katika maeneo makuu sita. Kupitia kukazia neno nalikuwa
katika roho kila moja ya matukio haya katika kitabu hiki yanashughulika na
tukio maalumu la kiufunuo. Kristo ndio ufunguo mkubwa wa kitabu cha ufunuo na
ni wa muhimu kuliko mpangilio ingawa kuna muendelezo wa matukio kutoka mwanzo
ambao unaweza kuorodheshwa kwa namna ifuatayo.
Utangulizi
Ufunuo 1;1-18.
§ Jina
: Ni Ufunuo wa Yesu Kristo 1,a
§ Waliotumiwa:
Yesu,Yohana na malaika 1b-2
§ Baraka;
Kwa kila asomaye ,na wao wayasikiao, kuyashika3
§ Salaam;
kwa makanisa saba,kutoka kwa Yohana na Yesu Kristo 4-7
§ Utambulisho
mkuu Yesu ni Alfa na Omega 8
§ Mamlaka
ya kuandika kitabu; 9-11.
Mambo
yale uliyoyaona Yesu kristo aliyetukuzwa 1;12-18
§ Agizo
la kuandiki kitabu cha ufunuo 19-20
Mambo
yale yaliyoko Maagizo kwa makanisa saba 2;1-3;1-22.
§ Kwa
kanisa lilioko Efeso 2;1-7
§ Kwa
kanisa lilioko Smyrna 2;8-11
§ Kwa
kanisa lilioko Pergamo ;2;12-17
§ Kwa
kanisa lilioko Thyatira2;18-29
§ Kwa
kanisa lilioko Sardis3;1-6
§ Kwa
kanisa lilioko Philadelphia3;7-13
§ Kwa
kanisa lilioko Laodicea 3;14-22
Mambo
yatakayokuwa baada ya hayo 4;1-16;21.
§ Hali
halisi ya Kiti cha enzi cha hukumu naheshima na ibada huko mbinguni 4;1-11
§ Kitabu
cha hukumu cha mwana kondoo 5;1-14
Kufunguliwa
kwa Muhuri saba 6;1-8;5
§ Muhuri
wa kwanza Farasi mweupe Ushindi wa mpinga Kristo na utawala 6;1-2.
§ Muhuri
wa pili Farasi mwekundu vita 6;3-4
§ Muhuri
wa tatu Farasi mweusi njaa 6;5-6
§ Muhuri
wa nne Farasi wa kijivu kifo 6;7-8
§ Muhuri
wa tano Nafsi chini ya madhabahu waliofia dini 6;9-11
§ Muhuri
wa sita Hasira za mwana kondoo mapigo mazito kwa dunia 6;12-17
§ Muhuri
wa saba ukimya matayarishio ya tarumbeta
saba 8;1-5
Kupigwa
kwa tarumbeta saba 8;6-11;19
§ Hukumu
dhidi ya nchi 8;6-7
§ Hukumu
dhidi ya bahari 8;8-9
§ Hukumu
dhidi ya mito 8;10-11
§ Hukumu
dhidi ya mbingu 8;12
§ Hukumu
dhidi ya wanadamu ole kuu tatu 8;13
§ Hukumu
dhidi ya wanadamu wakaao ju ya inchi 9;1-11
§ Kutangazwa
kwa Ole kuu 9;12
§ Kufunguliwa
kwa malaika wanne waovu zaidi 9;13-21
§ Malaika
na Muona maono 10;1-11;14
§ Kitabu
kidogo 10;1-11
§ Kupimwa
kwa hekalu 11;1-13
§ Kutangazwa
kwa ole ya tatu 11;14
§ Kupigwa
kwa tarumbeta ya saba 11;17-19
Ishara
kuu 12;1-16;21
§ Mwanamke,
mtoto wa kiume na Yule joka 12;1-17
§ Mnyama
kutoka baharini 13;1-10
§ Mnyaka
kutoka katika inchi 13;11-18
§ Mwana
kondoo katika mlima sayuni 14;1-5
§ Malaika
wa Habari njema 14;6-13
Kutangazwa
kwa injili
Kuanguka
kwa Babel
Kutangazwa
kwa heri ya wafu waliobarikiwa
§ Mvunaji
katika mawingu 14;14-16
§ Kushughulikiwa
kwa mzabibu wa dunia 14;17-20.
Kumwagwa
kwa vitasa saba vya mapigo 15;1-16-16;21
§ Wimbo
wa Musa na mwanakondoo 15;1-4
§ Kufunguliwa
kwa Hekalu na hema ya mbinguni 15;5-16;1.
§ Kumiminwa
kwa kiatsa cha kwanza majipu mabaya 16;2
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha pili bahari kuwa damu 16;3
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha tatu mito na maziwa kuwa damu 16;4-7
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha nne jua kuunguza wanadamu 16;8-9
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha giza kwa ufalme wa mpinga kristo 16;10-11
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha kukauka kwa mto frati na vita vya Armageddon 16;12-16
§ Kumiminwa
kwa kitasa cha saba Tetemoko la inchi 16;17-21
Ushindi
wa Yesu Kristo 17;1-21;8
§ Hukumu
dhidi ya Babel 17;1-18;24
§ Hukumu
dhidi ya tamaduni 17;1-18
§ Hukumu
dhidi ya mji 18 ;1-24
§ Muitikio
huko mbinguni 19;1-10
§ Kushindwa
vibaya kwa wakuu wa uovu 19;11-20;24
§ Ushindi
wa Yesu Kristo 19;11-16
§ Kuharibiwa
kwa mpinga kristo 19;17-21
§ Kufungwa
kwa shetani 20;1-3
§ Utawala
wa miaka 1000 Millennal reign 20;4-6
§ Kuharibiwa
kwa shetan 20;7-10
§ Hukumu
ya mwisho 20;11-14
§ Yerusalemu
mpya 21;1-8
Yesu
katika mji wa Mungu 21;9-22;5
§ Kutokea
kwa mji 21;9-21
§ Mwangaza
wa mji ule 21;22-23
§ Wakazi
wa mji ule 21;24-27
§ Mandhari
ya mji ule 22 ;1-5
§ Mausia
ya Kristo 22;6-21
Mstari
wa Msingi ni
§ Ufunuo
1;19 Basi Uyaandike mambo hayo uliyoyaona
nayo yaliyopo na yale yatakayokuwa baada ya hayo
UCHAMBUZI WA KITABU CHA UFUNUO
KITABU CHA UFUNUO:
Lengo
la 1: Taja mambo matano yanayoelezea
chanzo cha Ufunuo katika sura ya 1:-
Mambo
matano yaliyodhihirishwa katika sura ya 1 ni:-
- Ufunuo wa Yesu Kristo 1:1
- Ujumbe huu uliwasilishwa kwa Yohana kupitia Yesu Kristo, malaika na maono – 1:1,10-18
- Ujumbe huo uliletwa kwa Yohana – 1:1,4,9,2
- Alipewa ujumbe huu akiwa mfungwa katika kisiwa cha Patmo
- Walengwa wa ujumbe yalikuwa makanisa saba katika Jimbo la Asia ndogo.
Kitabu
hiki kiliandikwa wakati wa utawala wa Domitian aliyetaka watu wamwabudu kama
Mungu. Amri hii ilileta matatizo na
mateso kwa wakristo. Hivyo kitabu hiki kiliandika
katika mazingira haya.
M A K U S U D I:
Lengo
la 2: Eleza kusudi la kuandikwa kwa
kitabu hiki Kusudi la kuandikwa kitabu hiki liko katika sehemu tatu:-
- Nyaraka zilizoandikwa zilikuwa za kukemea makanisa yaliyoridhia dhambi bila kuikemea.
- Kutokana na mateso ya Domitian aliyetaka kuabudiwa – kitabu hiki kiliandika kuwatia moyo kuvumilia mateso na kuwa waaminifu hadi kufa.
- Kiliandikwa kwa ajili ya Kanisa la Kizazi chake ili kuwaonyesha waamini juu ya mapambano waliyo nayo dhidi ya majeshi ya shetani. Jinsi kuja kwa pili kwa Yesu Kristo kutakavyokomesha utawala mwovu wa mpinga Kristo.
M H U S I K A:
Lengo
la 3 : Eleza mhusika mkuu
linazungumzwaje:
§ Mtiririko wa kitabu cha Ufunuo ni kuelezea
kuja mara ya pili kwa Yesu Kristo (Ufu.1:7).
Mhusika Mkuu katika kitabu cha Ufunuo ni Yesu Kristo mwenyewe. Yale aliyokwishafanya, anayofanya sasa na
yale atakayofanya baadaye.
MWANDISHI NA TAREHE:
Lengo
la 4: Orodhesha ushahidi wa Uandishi na Tarehe ya Kitabu cha Ufunuo:
§
Kitabu
hiki kiliandikwa na Yohana Mtume wakati wa utawala wa Kaisari Domitian mnamo
mwaka kati ya 91-96 BK. Ushahidi
tunaopata ni matumizi ya maneno “Logos” “Nikao” na “Ekkenteo” (kushinda na
kuchoma). Pia ushuhuda wa Viongozi wa
mwanzo wa kanisa kama Justin Martyr unathibitisha kuwa mtume Yohana aliandika,
ushahidi wa ndani ya kitabu unahusiana na kuwa kifungoni kisiwani Patmo huko
Asia ya Kati.
SEHEMU KUU ZA KITABU:
Lengo
la 5: Eleza sehemu kuu za Kitabu.Katika Ufu.
1:19 Yesu mwenyewe anaelezea:-
- Utangulizi – 1:1-8
- Yale uliyaona 1:9-20
- Nayo yaliyopo 2-3
- Yatakayokuwepo baadaye – 4:1-22:6
Kanisa
katika Utukufu – 4:1-5:14
Dhiki
Kuu – 6:1- 19:21
Miaka
elfu -20:1-6
Gogu na Magogu – 20:7-10
Kiti
cheupe 2:11-15
Mambo
yote mapya – 21:1-22:6
§ Hitimisho - 22:7-21
§ Maelezo
ya Zaidi:
§ Ni maelezo ya kina kuhusiana na jambo
lililokwisha elezwa tayari.
§ Sura ya 7- Wayahudi 144000 na waliovikwa
mavazi meupe.
§ Sura ya10 - Malaika mwenye nguvu mwenye
Gombo au kitabu
§ Sura 11:1-14 – Mashahidi wawili
§ Sura ya 12 - Mwanamke, mtoto na Joka
§ Sura ya 13 - Wanyama wawili
§ Sura ya 14 - 144,000 (Israeli), mwisho wa
Injili kuhubiriwa, Tangazo la Kuangushwa kwa Babeli, mavuno ya mwisho na
shinikizo.
§ Sura ya 17 - Wanyama wawili na kahaba mkuu
§ Sura ya 18
- Babeli
MASWALI:
- Chanzo cha Ufunuo ni kipi?
- Taja makusudi matatu ya kitabu cha Ufunuo
- Nani mhusika Mkuu wa kitabu hiki?
- Taja sehemu kuu za kitabu hiki.
YALE YOHANA ALIYAONA: KRISTO ALIYETUKUZWA;
CHANZO NA KUSUDI LA UFUNUO:
Lengo
la 1: Eleza chanzo cha Kitabu cha Ufunuo
na ujumbe wake. Chanzo cha ujumbe wa kitabu ni Mungu akiwa na lengo la kuifunua
kweli kwa watumishi wa Mungu. Hivyo
kitaeleweka kwa watu wake kwa sababu wanayo hekima kutoka kwa Mungu.
EN TACHEI:
Lengo
la 2: Eleza maana ya neno “upesi” - Ufu.
1:1Yesu alimtuma malaika wake
kumwonyesha Yohana mambo ambayo hayana budi kuja upesi – neno upesi linatokana
na neno la Kigriki “En Tachei” “En tachei" likiwa na maana “mara moja “ upesi, ghafla, wakati wowote.
MAANA YA “MALAIKA”:
Neno au jina malaika lina asili ya
kiyunani ambayo ina maana pana kadhaa
jina hilo kwa kiingereza ni Angel
ambalo limetokana na jina la kiyunani Angelos
(Angelos)ambalo
lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) ambalo pia maana
yake ni mjumbe wa Mungu lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa
kumaanisha maswala kadhaa yafuatayo;-
§
Neno hili angelos lilitumika pia kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa” na matumizi kama
hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika
Matendo 12;15 ambapo wanafunzi walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga
mlango hii ni kwa sababu kimsingi wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na
isingeliwezekana kutoka gerezani na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama
vile hii ni kwa sababu walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa
Yakobo pamoja na kuwa waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro
kuweza kuwa hai. Jambo lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa
kama malaika kwa msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia
ilimaanisha wazi kutumiwa kama neno malaika.
§
Neno malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe wa Mungu aliye mwanadamu” mfano
katika ufunuo 2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu
inakisiwa kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani wajumbe
ambao wanabeba gombo la chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa
ambayo Yohana alikuwa akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa
na ufunuo 1;11, ambapo agizo linaonyesha
kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo ukayapeleke kwa hayo makanisa
saba Efeso, na Simirna, na Pergamo na Thiatira, na Sard na Filadelfia
na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano wale waliopeleka
magombo hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa inamaanisha viongozi
wa kila kanisa ambao husimamia makanisa
na huwasomea watu maandiko kama ilivyokuwa wakati wa matumizi ya
masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza kazi ya kiongozi ilikuwa ni
kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo walikuwa ni watu wanaowajibika
kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo viongozi hao pia waliitwa malaika
yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha
viumbe wa kiroho wa Mungu ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa
yale na imani hii ina mzizi katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa
malaika wa kila eneo, na pia kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya
mbinguni hapa duniani.
Lengo
la 3: Eleza njia mbali mbali za Kibiblia
kuhusiana na neno “Malaika” na Ujumbe alioonyeshwa Yohana (Ufu.1:2)
Ufu. 1:1 unaonyesha kuwa neno“malaika” lina
maana ya mpeleka habari (tarishi). Hii inaonyesha kuwa Yesu Kristo alifunuliwa
kwa Yohana na malaika. Katika Biblia
kuna malaika wa aina mbili: Wajumbe wa kimwili na wa Ki-Mungu. Huyu malaika alitoa ujumbe kwa kutumia ishara
na mifano. Mambo mawili yaliyofunuliwa
ni Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.
HERI SABA ZILIZOMO KATIKA UFUNUO
(1:3-5)
Hizi ni baraka
za Mungu kwa watu watakaotenda mambo Fulani.
Lengo
la 4 : Orodhesha Heri hizo.
§ Ufu. 1:3 - “Heri asomaye na wao wayasikiao
maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyoandikwa..”
§ Ufu. 14:13 -Heri wafu wafao katika Bwana,
tangu sasa wapate kupumzika.
§ Ufu. 16:15 - Heri akeshaye na kuyatunza
mavazi yake asiende uchi..”
§
Ufu.
19:9 - Heri walioalikwa karamu ya Arusi
ya Mwanakondoo
§
Ufu.20:
6 - Heri na Mtakatifu ni yeye aliye na
sehemu katika ufufuo wa Kwanza
§
Ufu.
22:7 - Heri yeye ashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
§
Ufu.
22:14 – Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa Uzima.
ROHO SABA ZA MUNGU – Ufu. 1:4
Lengo
la 5: Onyesha Roho saba ni nini?
§
Roho Saba
za Mungu maana yake ni ukamilifu wa huduma ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa la
Mungu.Ufunuo 4.5, Ufunuo 5;6 ni wazi kuwa utendaji Huu na Ufafanuzi huu kuhusu
Roho Mtakatifu haumaanishi kuwa Roho wa Mungu amegawanyika lakini unawaklisha
Utendaji mkamilifu wa Roho wa Mungu Isaya aliweka wazi Ukamilifu huu mapema ona
katika Isaya 11;1-3Roho anatajwa kama, Roho ya Bwana, Roho ya Hekima, Roho ya
Ufahamu, Roho ya Usahauri, Roho ya uweza, Roho ya Maarifa, Roho ya kumcha
Bwana.
AINA TATU ZA KUJITAMBULISHA KWA YESU – 1:5,6
Lengo
la 6: Eleza jinsi Yesu anavyojitambulisha.
(a)
Yesu ni
Shahidi mwaminifu
(b)
Mzaliwa
kwa Kwanza wa walio hai
(c)
Mkuu wa
Wafalme wa dunia.
ALFA NA OMEGA –1:8
Lengo
la 7: Eleza sababu inayomfanya Yesu
aitwe Alfa na Omega. Yesu anaitwa Alfa na Omega kwa sababu herufi za Kiyunani
zinaelezea kuwa katika yeye Mungu Baba aliumba vitu vyote na katika yeye Baba
ataleta mwisho wa kila kitu.Yeye ni mwanzo wa kila kitu yeye ni wa kwanza na wa
mwisho yeye ni kila kitu A & Z.
NENO TAZAMA – 1:7
Lengo
la 8: Eleza maana tofauti za neno Tazama, katika kifungu hiki lina maana ya:
Kuona kwa macho ya kimwili
Kuelewa au kufahamu
Kushangaa na kujiuliza.
SIKU YA BWANA - 1:10
Lengo
la 9 : Eleza maana ya siku ya Bwana.
§ Katika mstari huu una maana siku ya kwanza
ya juma, Jumapili. Yohana alikuwa katika roho siku hiyo.
§ Nalikuwa katika
Roho siku ya Bwana Yohana 20;1,19;26.Mdo 20;7 1Koritho 16;2
§ Yohana
anatufundisha kitu cha ajabu sana kwani ingawa alikuwa ametengwa mbali na watu
Imani na mazingira aliweza kuwa katika roho siku ya bwana, ni wazi kuwa liko
bishano la kuhusu siku ya kuabudu ukweli siku hii ilikuwa ni siku ya jumapili
siku ambayo Bwana Yesu alifufuka
§ Katika kitabu
hiki utendaji wa Yesu unaashiria wazi kuwa
alikuwa amekusudia kabisa siku hii iwe maalumu kwaajili ya kuabudu, kuna
matukio kadhaa yaliyojitokeza katika siku hii ya kwanza ya juma ambayo ni
matukio ya kushangaza yanayoashiria kuwa Bwana aliikusudia itumike kwa makusudi
ya kuabudu pia
Bwana alifufuka kutoka kwa wafu siku ya kwanza ya juma
Mathayo 28;1,Marko 16;2,Luka 24;1 neno mia
la kiyunani lilitumika katika mistari hii kumaanisha siku aliyofufuka Bwana
Aliwatokea wanafunzi wake
mara mbili katika siku hiyo ya
kwanza ya juma Yohana 20;19,26
Ujio wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ulitokea siku
ya kwanza ya juma hili tunalijua kutokana na Walawi 23;15-16.Hata ilipotimia
siku ya Pentekoste...Roho Mtakatifu akaja Matendo 2;1.
Kuna dalili nyingi kuwa wanafunzi wa nyakati za kanisa la
kwanza waliiadhimisha siku hii hata ingawa uko ushahidi kuwa walikuwa
wakikutana kila siku kwaajili ya kuabudu Matendo 2;46 lakini ni wazi katika
maandiko kuwa siku hii baadaye ilikuwa maalumu
Paulo alifundisha wazi kabisa umuhimu wa siku ya Bwana akiwataka wakoritho
kujiandaa kumtolea Mungu katika siku hiyo 1Wakoritho 16;2
Mtakatifu Ignatio aliandika hivi, Tukiwa hatushiki tena sabato bali tukiishi kulimgana na siku
ya bwana ambayo ndiyo nuru yetu
alipofufuka
Justin Martyr alipokuwa akiandika utetezi wake wa imani
kwa mtawala wa Rumi aliandika hivi
”Jumapili ndiyo siku ambayo sisi tunakusanyika wote pamoja kwa sababu
ndiyo siku ya kwanza ya juma
Katika mkusanyiko wa mafundisho yaitwayo mafundisho ya
mitume yaliyokusanywa mwaka 105 B.K.
twaona taarifa kuwa mitume waliiamuru siku hii kuwa na ibada ya pamoja , na
ushirika na kusomwa maandiko kwa sababu ni siku aliyofufuka Bwana
Eusobio mwandishi aliyeheshimika wa Historia ya Kanisa
tangu Kristo hadi Kostantino aliandika
Tangu mwanzo wakristo walikusanyika kwehye siku ya kwanza ya juma
Historia ya sabato
Mungu alukuwa na sabato yake katika Mwanzo 2;2-3 hii ni
sabato ya Mungu na hakuna mahali pengine
yeye amewahi kushika nyingine tangu wakati huo
Sabato nyingine ni ya kiyahudi Mungu aliwapa wao tu na
sio wenine Mwanzo 7;4-10,8;10-12, Sabato
ya kiyahudi ilitajwa kwa mara ya kwanza katika Kutoka 16;21-30 hii iliwahusu
waisrael tu na sio mataifa mengine wala sio kwa Wakristo Kutoka 31;13-17 hii ni
Ishara ya Mungu kwa wana wa Israel tu milele Wagal;atia 3;19 torati na mabnabii
vilifanya kazi hata wakati wa Yohana batizaji lakini Tangu wakati huo Habari za
ufalme hutangazwa Luka 16;16.
Sabato ilikuwa ni kivuli tu cha maswala ya ujio wa Kristo
wakolosai 2;7 kwa hiyo siku ya bwana haina uhusiano wowote na uvumi kuwa ni
alama ya mnyama ufunuo 13
Jambo la mwisho la kuzingatia ni kuwa siku sio jambo la
msingi sana katika swala la kuabudu ingawa wote tunajua kuwa jumapili ni siku
ya bwana na kuwa imekubalika itumike na wakristo wote kwa kusudi la kuabudu
lakini kama wengine wanaweza kuabudu siku nyingine yoyote kuabudu kulingana na
mazingira husika hii isitufanye kufungwa na fundisho la kuabudu katika siku
fulani Warumi 14;5-9.
SAUTI, AMRI NA MAONO – 1:10-16
Lengo
la 10: Elezea Yesu aliyeonwa na
Yohana.Yohana alimwona Yesu katika Utukufu wake mkubwa mmno.
§
Vazi
lililofika miguuni - Ukuu wa Yesu kama nabii, kuhani na mfalme.
§
Kichwa
na nywele zake - Utakatifu,, hekima na
Umilele wa Yesu
§
Macho
kama mwali wa moto- Anajua yote
§
Miguu
kama shaba iliyosuguliwa - Hukumu ya
Yesu kwa watu
§
Sauti
ya majimaji - Mamlaka na nguvu za Yesu
§
Mkono
wake wa kuume - Kujali,
msaada na kudhibiti kwa Yesu
§
Upanga
utokao kinywani - Neno lenye mamlaka ya Yesu
§
Uso
kama jua katika nguvu zake – Utukufu, Ukuu na Utakatifu wake.
MAUTI NA KUZIMU - 1:17,18
Lengo
la 11 : Eleza neno “Paradiso”, jadili mahali ilipo.
§
Kufuatana
na Maandiko, Paradiso ni mahali pa kuwafariji watakatifu waliokufa. Wakati wa Agano la Kale paliitwa kifuani pa
Ibrahimu huko kuzimu. Yesu alipokufa na
kufufuka Paradiso ilihamishwa mbinguni.
Hivyo kuzimu Sheol HB au Hades GK ni mahali wanapokwenda waovu
wanaokufa.
NYOTA NA VINARA VYA TAA - Ufu. 1:19,20
Lengo
la 12: Elezea maana ya nyota na Vinara.
§
Nyota Saba
na malaika saba ikiwa na maana ya wachungaji wa Makanisa. Vinara Saba ni
makanisa saba (Mst.20) ambayo yamewekwa kuwa nuru ya kumfunua Yesu Kristo kwa
watu. Yesu yupo katikati ya vinara
kuonyesha uwepo wa Mungu upo ndani ya kanisa na wachungaji wapo mikononi mwake.
MASWALI:
1.
Neno “ Malaika” lina maana gani katika Ufunuo.
2.
Orodhesha
heri zilizomo katika Ufunuo
3.
Siku ya
Bwana inayotajwa Ufu.1:10 ni ipi?
4.
Nini
maana ya Alfa na Omega – Ufu.1:8.
MAMBO YALE YALIYOPO, YESU NA MAKANISA
SABA;
kabla
Kristo hajaanza kuhusika na hukumu kwa ulimwengu anaanza kuhukumu watu wake
yaani kanisa 1Petro 4;17, Ezekiel 9;6 Kila aunaposoma habari za makanisa haya
saba utaweza kuona kuwa makanisa haya saba yanapita katika hukumu ya bwana ni
wazi kuwa makanisa haya uiyaangalia kwa undani ni makanisa ya mahali pamoja
lakini pia ni mtu mmojammoja binafsi ni wazi kabisa kuwa watakatifu
watahukumiwa kwa hukumu yao maalumu na kuwa hawatahukumiwa pamoja na dunia katika
eneo hili sasa tutakuwa tukiyaangalia makanisa yale saba na nyaraka zake na
uchambuzi wake kutoka Ufunuo 2;1-3;22.
Makusudi makuu ya Nyaraka zile.
§
Makanisa
yale saba yalikuwa ni makanisa halisi na yalikuwa na matatizo halisia
yaliyoatakiwa kushughulikiwa kichungaji na kuonywa na kuongozwa na Mkuu wa
kanisa ambaye ni Bwana Yesu mwenyewe
§
Makanisa
yale saba pia huwakilisha nyakati saba za kihistoria katika kanisa tangu wakati
wa kanisal la kwanza siku ya pentekoste hata wakati wa kuja kwa
bwana , haya pia yanaweza kuwa makanisa au madhehebu ambayo yana mapungufu
mbalimbali na baraka mbalimbali sambamba na hali ya yale makanisa saba,
makanisa hayo pia yanawakilisha Roho za kinabii 19;10.
o
Apostolic Church 33-100 Kanisa la
wakati wa Mitume kanisa lenye shughuli.
o
Persecuted Church 100-113 kanisa la
Karne ya kwanza lililoteseka
o
Imperial Church 313- 476 Kanisa
la kpindi cha lililopata ushindi na kanisa lililokosea
o
Medieval Church 476-1453 kanisa lililopoa kipindi cha
giza kanisa lenye tatizo
o
Reformed Church 1453-1648 kanisa la kimapinduzi kanisa lililotazama nyuma
o
Morden church 1648-1970 kanisa la leo kanisa la
kiinjilisti
o Morden charismatic church 1970 mpaka leo. Kanisa lenye mafanikio
§
Makanisa
haya saba yanawakilisha pia kujihusisha na mtu mmoja mmoja utaweza kuona lugha
kama Yeye aliye na sikio na asikiye Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa
Ufunuo 2; 7, 11, 17, 29, 3;6, 13, 22. Kwa msingi huo wakristo waweza kupokea
halia za kutiwa moyo, kuonywa na kujengwa kupitia ujumbe huu wa makanisa yale
saba 2Timotheo 3; 16.
Yaliyomo kwa Mukhtasari katika makanisa yale
Saba.
Lengo
la 1: Orodhesha mambo yaliyomo katika barua zilizoandikwa kwa. Makanisa Saba:
- Salamu kwa Kiongozi wa kila Kanisa.
- Tabia na hali za Yesu Kristo.
- Yale Yesu anayajua kwa kila Kanisa
- Yale anayoyafurahia katika kila Kanisa isipokuwa Laodekia
- Yale Yesu aliyakosoa na kukemea katika kila Kanisa isipokuwa Smirna na Filedefia.
- Ahadi kwa kila Kanisa
- Ushauri kwa kila Kanisa kusikia ujumbe
- Ahadi kwa washindi
N.B: Jumbe kwa Makanisa saba inaelezea hali ya
Kiroho iliyokuwemo ndani ya Makanisa hayo.
Hali hiyo inalingana na Makanisa ya vizazi vyote.
BARUA KWA KANISA LA EFESO: Kanisa lenye shughuli
bila Upendo Ufunuo 2;1-7.
Lengo
la 2: Eleza Historia na hali ya Kanisa
la Efeso.
§
Efeso
ulikuwa mji na bandari wenye ibada za sanamu uliozungukwa na mashamba mazuri.
§
Ulikuwa
ni mi wenye maswala ya dini za kipagani Animism hekalu la Mungu Artemis
lilisimamishwa katika mji huu na lilikuwa kubwa na zuri kiasi cha kuingizwa
katika moja ya maajabu saba ya kale ya Dunuia.
§
Artemis
alikuwa ni mungu aliyehusika na maswala ya Uzazi alikuwa ni mungu mke
aliyeaminika kuwa alishuka kutoka mbinuni Matendo 19; 35 na wayeyusha vyuma
walitengeneza sanamu za mungu huyo na kuziuza.
- Kanisa lilianzishwa na Paulo katika safari ya tatu ya Utume. Watu wengi waliokolewa na kuchoma uchawi wao na Vitabu vya uchawi na uganga Mdo.19:1-41. Paulo alifanya kazi Efeso kwa muda wa miaka 3 , Mdo. 20:31
- Baadaye Kanisa hili alilisimamia Timotheo ili kukemea mafundisho potofu yaliyoletwa na baadhi ya waamini 1Tim. 1:3.
- Kanisa lilisifiwa na Yesu kwa mambo matano mazuri:-
§
Bidii,
uvumilivu, kutovumilia uovu, kuwajaribu wajiitao mitume, kuchukia mafundisho ya
wanikolao.Wanikolao yalikuwa ni mafundisho ya watu waliosemekana kuwa waliamini
kuwa “Woman is For social not a Personal” Hivyo walibadilishana wanawake na
walikubaliana na maswala ya Uasherati na Uzinzi, na walikula vyakula
vilivyotolewa sadaka kwa sanamu Kristo alichukizwa na aina iyo ya mafundisho a
aliikataa tena na tena katika Mstari wa 6 na wa 15.
§
Hawakuchoka
katika subira ya Kristo na walifundisha mafundisho sahii Mstari wa 3,6.
- Lilikemea kwa kupoteza upendo wa kwanza; hivyo lilikuwa katika hatari ya kutengwa. Kanisa ni lazima lifanye uinjilisti likiongozwa na upendo wa Kristo.
Fundisho: Uhusiano wetu na Yesu uwe wa kwanza kuliko
vitu vyote, mfano Mke, watoto, kazi, nk.
BARUA KWA KANISA LA SMIRNA Kanisa lililoteswa
–2:8-11
Lengo
la 3: Eleza hali na mistari ya Kanisa la
Smirna.
§
Mji huu
wa Smirna ulichukua jina kutokana na manukato yaitwayo Myrrh.ambayo yalikuwa ni manukato maalumu kwaajili ya kuandaa
mazishi ya mtu aliyekufa manukato ya aina hii ndiyo yaliletwa na mamajusi kwa
zawadi kwa Bwana Yesu kama unabii wa maziko yake, Smirna Ulikuwa mji mzuri na ajiri katika Asia ya Kati
§
Ulikuwa
na Wayahudi wenye nguvu na wapinzani wa Injili. Kanisa hili katika Historia ya
kanisa wakati wa mateso hayo liliongozwa na Mchungaji aliyeitwa Polokapo ambaye
alichaguliwa na Yohana kuwa Askofu wa Kanisa la Smirna Mchungaji huyo huenda
alitiwa nguvu na waraka huu kwani wakati
aliposhkwa na kufikishwa mbele ya liwali na kuonywa kuwa alitakiwa tu kumkana
na kumlaani Kristo ili kupata nafasi ya kuachiwa Huru asiliwe na simba, Yeye
aliitunza Imani na alisema “Miaka themanini na sita nimemtumikia Kristo naye
hajanitendea lolote Isipokuwa mema Nitawezaje basi kumlaani Bwana wangu na
Mwokozi?” kwaajili ya maneno hayao alichomwa mto akiwa hai. Kumbuka maneno yale
Uwe mwaminifu hata kufa name nitakupa taji ya Uzima Mstari wa 10.
§
Kanisa
lilikuwa na watu maskini na wenye kupitia mateso. Wayahudi walikuwa wanawatukana Wakristo.
Tunajifunza kuwa Yesu anajua watu wake wako wapi na wanapitia halia gani na
uwezo wao wa kuvumilia Mstari wa 8-9
§
Yeye
anayetia moyo naye aliteseka na hatimaye alishinda anawatia moyo kuwa waaminifu
na kutokuogopa.Yesu anaonya kuwa baadhi yao watatupwa gerezani wawe waaminifu
mpaka kufa.
Fundisho: Yesu Kristo anajua majaribu tunayopitia,
anataka tuwe waaminifu na atatupa taji ya uzima.
BARUA KWA KANISA LA PERGAMO Kanisa lillokosea – 2:12-17
Lengo
la 4: Eleza hali na Historia ya Kanisa.
§
Mji wa
Pergamo ulikuwa makao makuu ya kisiasa na dini katika Asia ya Kati. Ndipo palikuwa pa kwanza kuanzisha kumwabudu
Kaisari (kiti cha enzi cha shetani).
§
Ulikuwa
mji wenye kuabudu miungu miungu kama Zeus na Athena iliabudiwa pia na likuwa
mji wenye madawa au tiba za aina mbalimbali mungu Nyoka Asclepius aliyehudumiwa
na makuhani alihusika na tiba, mji huu ulikuwa na maktaba kubwa yenye Vitabu
200,000 ulikuwa ni mi wenye kujaa maswala ya dini za kienyeji,zinaa, Falsafa na
maswala ya elimu.
§
Yesu
anajitambulisha kwa kuwa na upanga mkali maana yake anakosoa mafundisho potofu
kulikuwa na makosa mawili ya kimafundisho,
a.
Fundisho
la Balaam Mst 14 Hesabu 24;25-25;13 2Petro 2;15,16 Yuda1; 11-12 balaamu
alishawishi watu kuabudu miungu na kujihusisha na uasherati wakati wa agano la
kale na kuwakosesha watu wa Mungu
b.
Fundisho
la Wanikolai Nicolaitans Mst 6,15 ni kundi lilofundisha kuwa hawapaswi kufungwa
na sheria ya aina yoyote wako huru mbali na utumwa wa aina yoyote ilikuwa ni
fundisho lisilojali maadili na mafundisho
hawakujali ni aina gani ya watu wanajiunga na kanisa walisema “Washinde
watu ili uwatawale” wakatoliki walipoanza kanisa walichukua baadhi ya
mafundisho ya wanikolai inasemekana hata kubadilishana wanawake ilikuwa Riksa
ili kudumisha upendo wa ndugu.
§
Yesu
analikosoa kwa kuwavumilia watu wenye Imani potofu.(Mafundisho ya Ballam –
ibada ya sanamu na uzinzi- mafundisho ya Wanikolao uhuru usio na mipaka na
zinaa).
§
Kanisa
linasifiwa kwa uaminifu na kushikilia Imani. Na anamtaja mmoja ya watu
waliokuwa waaminifu na kuuawa kwaajili ya ushuhuda wa Yesu Antipas Mst 13
§
Endapo
watashinda wanaahidiwa
i.
Mana
iliyofichwa na jiwe jeupe
ii.
Mana
iliyofichwa ni Chakula cha kiroho na jiwe jeupe ni kinyume cha jiwe jeusi ambalo humaanisha
hukumu ambayo mtu huukumiwa na kutaabika waklati jiwe jeupe ni kwa maisha ya
raha na maisha marefu
Fundisho: Lazima waamini wasipinge imani potofu na
mafundisho potofu.
BARUA KWA KANISA LA THIATIRA Kanisa lenye Tatizo
–2:18-29
Lengo
la 5: Eleza hali na Historia ya Kanisa:
§
Kanisa
lilikuwa katika mji wa viwanda vya nguo vya zambarau. Lydia alitokea hapa,Mji
huu ulikuwa ni mji wa kibiashara , kilimo na eneo maarufu au zuri kwa ulinzi na
Usalama na kulikuwa na sifa za kiusalama
na nguvu ya kijeshi nuo za rangi ya zambarau zilitengenezwa hapa Kumbuka matendo
16;14
§
Yesu
anajitambulisha kama mwana wa Mungu akitokea katika utukufu wa Kiungu macho
kama mwali wa moto na miguu kama shaba iliyosuguliwa sana juu ya maadui wake
§
Yesu
alilisifu Kanisa kwa mambo manne – (upendo, imani, huduma, subira)
§
Yesu
analikosoa Kanisa kwa kumridhia Mwanamke nabii wa uongo mwenye tabia za
Yezebeli. Mstari wa 20,Yezebeli alikuwa mwanamke aliyeongoza taifa la Israel
katika ukengeufu mkubwa 1Wafalme 16;29-34, alistawisha uasherati, uabudu
sanamu, upagani, kumbua kuwa chachu kidogo huchachusha Donge zima 1Koritho 5;9.
§
Wakristo
waaminifu watatawala mataifa na wanahaidiwa nyota ya alsubuhi.
Fundisho: Yesu anachukia Kanisa likifumbia macho walimu
wa uongoYesu anaahidi kuwashughulikia wote wafundishao uongo.
BARUA KWA KANISA LA SARDI Kanisa lililotazama nyuma
- 3:1-6
Lengo
la 6: Elezea Historia na hali ya Kanisa:
§
Mji wa
Sardi ulikuwa juu ya mlima kama kiasi cha futi 1000 juu katika njia kuu ya
biashara. Ulikuwa na ngome imara ya
kijeshi na tajiri, uliojengwa na Kaisari
Tiberia.Raia walikuwa na usalama wa uhakika wakiamin kuwa mji wao ni wenye
nguvuna ni vigumu kwa maadui kuuweza ni mi uliokuwa tajiri wenye kujulikana kwa
vito vya thamani nguo n.k. mji huu ulikuwa umewekwa wakfu kwa mungu Artemis
hivyo kulikuwa na ibada za kipagani
§
Yesu
anajitambulisha kuwa anazo hizo Roho saba, kuonyesha kuwa anafahamu matendo
ndani ya Kanisa. Watumishi wanawajibika kwake.
§
Kanisa
linakemewa kwa kuonekana kwa jina liko hai, lakini ukweli limekufa.
§
Baadhi
ya waamini yaani mabaki walikuwa safi, Mungu siku zote ana mabaki watu
waaminifu.
Fundisho: Kanisa linatakiwa kuwa hai Kiroho.
BARUA KWA KANISA LA FILEDEFIA Kanisa lililohubiri
injili – 3:7-13
Lengo
la 7: Eleza Historia na hali ya Kanisa
- Kanisa lilikuwa katika mji uliojengwa na mfalme Pergamo. Ulichukua jina la mjenzi Akalus Phidadefia. Lilikuwa ni eneo lenye matetemeko makubwa ya nchi. Ulikuwa mji uliojawa na wanafalsafa,watu wa dini na zinaa, pia uliitwa mji wa ndugu wapendanao,Mfalme anawapenda ndugu zake hii ndio maana ya Philadelphus Filadelfia
- Mji ulikuwa unakabiliwa na matetemeko na makao ya ibada ya kipagani. Uliitwa Athens ndogo.
- Kanisa la mahali hapa lilikuwa na nguvu katika maswala ya kuhubiri injili na watu waliipokea injili na watu walikuwa waaminifu
- Yesu analihaidi mlango uliofunguliwa.
- Yesu analisifia Kanisa kwa mambo matatu.
- Linazo nguvu kidogo
- Limetunza Neno lake
- Hawakulikana jina la Yesu.
- Yesu analiahidi mambo manne:
- Atawafanya kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu
- Ataandika jina jipya la Mungu juu yao
- Ataandika juu yao jina la mji wa Mungu
- Ataandika juu yao jina lako jipya.
Fundisho. Kanisa linapaswa kuendelea kuhubiri
injili.
BARUA KWA KANISA LA LAODEKIA kanisa lenye mafanikio ya kimwili– 3:14-22
Lengo
la 8: Eleza historia na hali ya Kanisa.
- Kanisa lilikuwa katika mji tajiri kwa viwanda, nguo na maziwa, madawa na mabenki.
- Mji huu uliopewa jina la malkia Laodekia mke wa mfalme Antioch ii aliyeitwa Laoduce ulikuwa na bomba la maji lililokuwa likisambaza maji kutoka katika chemichemi za maji ya moto kama miles 6 kutoka kusini mwa mji, maji hayo ambayo wanawake walipoyachota walifika nayo nyumbani yakiwa yamepoa au kuwa na uvuguvugu.
- Jina Laodekia maana yake Popular Judgement au Popular Approval ikimaanisha kukubalika na watu, au kugfahamika sana, Kanisa la mahali hapa lilikuwa limetajirika katika maswala ya fedha na uchumi lakini kiroho walikuwa masikini,vipofu na uchi
- Kanisa halina sifa njema Yesu analikemea kwa tabia ya uvuguvugu iliyo nayo na kulishauri kutubu.
- Walifikiri kuwa wanaweza kujitosheleza, na Yesu alikuwa amefungiwa nje, ni wazi kuwa kanisa la Laodikia linawakilisha kanisa la siku za mwisho kihistoria ambalo litakumbwa na ukengeufu mkubwa , pamoja na kuwa na mafaniko ya kiuchumi na utajiri wa vitu
§
Fundisho: Yesu
hapendi mtu vuguvugu anataka mtu aamue kumfuata yeye au hapana.kuwa moto au
kuwa vuguvugu.
HALI TATU ZA KIROHO:
1.
Hali
ya moto - Mwamini mwaminifu
aliyejitoa kikamilifu kwa Bwana. Ameokolewa na anamfuata Yesu Kristo kwa kila
neno.
2.
Hali
ya uvuguvugu –Ni mtu
aliyeokolewa lakini hajafikia kiwango cha Kristo na Injili yake, Anashika
baadhi ya mambo ya Mungu.
3. Hali ya Ubaridi - Mtu anaishi kama
ulimwengu hana hamu ya mambo ya kiroho
na Mungu.
MASWALI:
- Orodhesha sifa zilizotolewa na Yesu kwa kila Kanisa.
- Orodhesha udhaifu unaotolewa kwa kila Kanisa.
MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO BAADA YA HAYO:
·
KUNYAKULIWA KWA KANISA
·
KITI CHA ENZI CHA MUNGU
·
WAZEE ISHIRINI NA NNE
·
WENYE UHAI WANNE
·
KITABU CHENYE MUHURI SABA.
SEHEMU YA 3: MAENDELEO YA MATUKIO KATIKA
SIKU YA MWISHO: KANISA NA DHIKI KUU:
MAANA YA USEMI “BAADA YA HAYO” – 4:1.
Lengo
la 1: Eleza maana ya usemi huu:
§ Usemi huu unatokana na neno la Kigriki “Meta
tauta” Metatauta likiwa na maana ya yale yatakayotokea baada ya kipindi cha Kanisa.
§ Ni wazi kuwa sura ya nne mstari wa kwanza
unazungumzia maswala yatakayo kuwa sio tu baada ya Yohana kupelekwa katika
maono mengine zaidi bali kunyakuliwa kwa kanisa na maandalizi kwaajili ya dhiki
kuu.
§ Ni wazi pia kuwa tendo la kunyakuliwa kwa
Yohana mwenyewe katikia ulimwengu wa kiroho na kuwa mbinguni kunawakilisha wazi
kunyakuliwa kwa kanisa ili aonyeshwe maswala ambayo kanisa litayashuhudia
wakiwa pamoja na Mungu mbinguni.Neno kanisa limetajwa mara 19 katika sura za
nyuma na halitajwi tena baada ya hapo
hii ikiwa na maana wazi kabisa kuwa kanisa litatengwa na dhiki kuu kwani Yesu
atalinyakua mapema
§ Ujio huu wa Kristo kulinyakua kanisa utakuwa
wa aina yeke na utawashangaza wengi kwa sababu kuu mbili
i.
Jinsi
atakavokuja na kulinyakua kanisa
ii.
Namna
anavyoishi hata sasa kuwa alikufa na sasa yu hai.
§ Wayahudi wengi walikuwa wamechanganya unabii
huu wa kuja kwa Yesu mara ya pili na ule ujio wa kwanza wao hawakona sana ule
ujio wake wa kwanza bali huu wa pili
§ Na hata leo wengi wanapuuzia swala la
kunyakuliwa kwa kanisa wakiupuuzia unabii huu ambao utajitokeza mapema kidogo
kabla ya ujio huo wa mara ya pili.
Tofauti ya Kunyakuliwa kwa Kanisa na ujio wa Yesu mara ya pili.
Kunyakuliwa
kwa kanisa
|
Ujio
wa yesi Kristo mara ya pili duniani
|
§
Itakuwa
ni mawinguni kama mwivi
|
§
Ni
duniani kila jicho litamuona
|
§
Ni
maalumu kwaajili ya kanisa
|
§
Yesu
na kanisa lake Kwa ajili ya ulimwengu
|
§
Kwaajili
ya kufarji na hukumu ya watakatifu
|
§
Kwaajili
ya kuhukumu ulimwengu na kutawala
|
§
Atanyakua
watu wake 1Koritho 15;51-58,1Thes 4;13-18
|
§
Kila
jicho litamuona Ufunuo 3;3,16;15
|
§
mawinguni
|
§
Duniani
mlima wa mizeituni.
|
§ Kristo atakuja mawinguni kwaajili ya
watakatifu atakuja kama mwivi
§ Mara ya pili anarudi duniani na watakatifu
kuitawala dunia
§ Uthibitisho wa kibiblia kuhusu unyakuo
Luka 21;34, 1Koritho 15;51,52
Makusudi ya kunyakuliwa kwa kanisa
Moja
ya kusudi kubwa la kunyakuliwa kwa kanisa ni pamoja na hukumu ya watakatifu na
baadaye kutolewa kwa taji za thawabu za aina mbalimbali kulingana na kazi
aifanyayo kila mtu, Yesu atakaa juu ya kiti cha hukumu kiitwacho Bema kwa kiyunani yaani mahali
palipoinuka Kama jukwaa wakaapo au akaapo Mgeni rasmi kwaajili ya kumtunuku washindi
wa medal mbalimbali baada ya ushindi katika michezo,Bema inafanana na kiti cha
hukumu na ni hukumu lakini hukumu isiyo na madhara, Wakati
wa “Bema” kazi ya kila mtu
aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia Mungu itajaribiwa kwa moto ili ipate
kufahamika thawabu ipi atakayopata (I Wakoritho 3: 13- 15). Ikiwa kazi
aliyoifanya mtu ni ya thamani kama dhahabu, fedha au mawe ya thamani,
itakapopitishwa katika moto, itazidi kung’aa na wengine wote watashangilia
pamoja na malaika. Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ilikuwa duni itakapopitishwa
katika moto itateketea kama miti, majani au manyasi, na itakuwa nia aibu ingawa
mtu ataendelea kuweko mbinguni, atakuwa kama mhalifu msalabani, bila kuwa na
taji yoyote.
Hukumu
ni nini?
Mjadala kuhusu Hukumu ni
mjadala mpana sana Neno hukumu au Judgement katika kiingereza na Kiswahili lina
maana kubwa kama ilivyo katika kiyunani pia wayunani wana maneno makuu mawili
yanayotumika kuzungumzia hukumu liko neno Krima
“Krima"
Na pia neno lingine ni Krino “Krino"
neno lile Krima la kiyunani lina maana ya kufanyiwa sawa na ulivyofanyaau
kuadhibu, na neno la pili Krino lina maana ya Kufikiri nini kinafaa, kutoa
uamuzi baada ya kufikiri kwa kina, kuamua au kutoa uamuzi wa mwisho. Neno Krima linaweza kutumika katika maeneo yote yanayohusu mwanadamu
aliyeokoka kwa wanadamu wenzake mfano usilipe ubaya kwa ubaya, au usiadhibu au
hukumu ya adhabu Warumi 8; 1. na
neno Krino linaweza kutumika katika
mtazamo wa uamuzi wa Mungu kwa ujumla tunaweza kufafanua neno hukumu katika
mitazamo zaidi ya kumi.
1.
Hukumu ni uamuzi unaokuja mwishoni na
kutangazwa mahakamani baada ya kusikilizwa kwa kesi Legal verdict
2.
Hukumu ni Tangazo la deni, wajibu,
cheti, au barua inayomwajibisha mtu kwaajili ya jambo Fulani Obligation resulting from verdict.
3.
Hukumu ni uamuzi wa Hakimu au jaji ni uamuzi wa haki unaotolewa kama hitimisho la
kukata mjadala na uamuzi huo hufikiriwa kuwa ndio wa mwisho Decision of Judge
4.
Ni mawazo yanayotengeneza uamuzi ili
kuondoa swala lenye utata au linaloleta mijadala Decision on disputed matter
5.
Ni uwezo wa kutengeneza wazo
linalokubalika na kuingia akilini na kutenda sawa na kilichotegemewa au
kisichotegemewa kwa jambo lililoleta utata.Discernment
of good sense.
6.
Wazo litolewao baada ya kufikiri kwa
kina snap judgement/Opinion
7.
Makadirio yanayofanyika baada ya
uchunguzi au yanayofanyika kutegemeana na uchunguzi estimate based on Observation.
8.
Kutoa mapendekezo juu ya jambo Fulani Judging of Something
9.
Malipo ya uamuzi wa kimungu unaotokana
na wajibu au matendo au tabia Divine
Punishment.
10.
Ni tendo la kutoa taarifa au uamuzi
unaokubalika kiakili, ulio sawa unaoeleweka au usioeleweka sawasawa na jambo
Fulani Act of making statement.
Kwa msingi huo
tunapozungumzia hukumu ni muhimu kufahamu kuwa tunazungumzia jambo pan asana na
tunapozunghumzia hukumu ya watakatifu neno linaloweza kutumika ni Krino na sio
Krima Kristo atakaposimama katika Kiti cha hukumu kiitwacho Bema atakua
anafanya hukumu iitwayo Krino ni hukumu isiyo na madhara lakini itashangaza
sana watu kwa kuwa inafanywa na Mungu mwenyewe katika mtazamo wake na usio wa
kibinadamu.
1.
TAJI
ISIYOHARIBIKA (INCORRUPTIBLE CROWN) 1 KORITHO 9: 23- 25, 2 TIMOTHEO 2: 4- 6.
Taji hii watapewa watakatifu ambao walifanya mambo
yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine. Walijizua yote
katika utoaji wao kwa ajili ya Injili, walijizuia yote katika maombi yao kwa
ajili ya Injili na pia walitumia vyote walivyo navyo, muda, ujuzi vipawa cheo
chao, uwezo wao wote n.k kukishiriki Injili pamoja na wengine.
2.
TAJI
YA KUJIONEA FAHARI ( CROWN OF REJOICING) 1 WATHESALONIKE 2: 19, DANIEL 12: 3
Taji hii inaitwa taji ya
kujionea fahari kwa sababu watakaoipata taji hii watang’ara kama nyota tofauti
na wengine watakavyong’ara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko yaw engine. Mng’ao
wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale
waliowaleta watu wengi kwa Kristo kutokana na kushudia kwao au kuhubiri Injili.
Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya mtu kwa mtu au
vinginevyo na wakawaongoza mahali ambapo watakuzwa kwa mafundisho na kuwa
watenda haki.
3.
TAJI
YA UZIMA (CROWN OF LIFE) UFUNUO 2: 10.
Taji hii ni kwa wale
waliopita katika mateso au mitihani mikubwa ya maudhi na kuchikiwa kwa ajili ya
Kristo na wakashinda. Hawakupenda maisha yao kufa (Yakobo 1: 2, Ufunuo 12: 11.
Mathayo 5: 11- 12, Waebrania 11: 24- 26, Zaburi 129: 2)
4.
TAJI
YA HAKI (CROWN OF RIGHTEOUSNESS) 2 TIMOTHEO 4: 6- 8.
(a)
Taji hii ni kwa wale waliopenda
kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Wakati wote moyoni walisema “Amina na uje Bwana
Yesu” Walikuwa katika utakatifu wakati wote. Kila neno walilojifunza
walilitendea wokovu kidogo, hivyo hivyo mpaka alipokua Yesu akawakuta katika
hali ya kutubu.
(b)
Taji hii watapewa wale ambao wanachukua
muda wao kuwafundisha watoto wachanga wengi wa kiroho mpaka wanakua. Namna yoyote
ya kumsaidia mtu kujifunza, itakupa thawabu hii – kumuazima au kumpa vitabu au
kaseti za mafunzisho mwenzio, kumpa nauli ili aende kwenye mafundisho ,
kazi ya kudumu kanisani- kubeba watoto
au kufanya lolote ili watu wawe na raha ya kujifunza n.k
(c)
Taji hii watapewa wale ambao
wanawahudumia mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji, na Waalimu ili wapate
urahisi wa kuzifanya kazi zao.
MLANGO UKAFUNGUKA MBINGUNI – 4:2
Lengo
la 2: Eleza juu ya maoni ya kuwa tendo la Yohana kuchukuliwa toka duniani
kupitia mlango uliofunguliwa kwenda mbinguni kunahusiana na unyakuo wa Kanisa.
§
Yohana
alisikia sauti ya Yesu Kristo, Yohana anaambiwa “panda hata huku” mara
moja. Mambo yanabadilika mbinguni.
§
Kunyakuliwa
kwa Yohana 4:1-2 kunaonekana kuwakilisha kunyakuliwa Kanisa kabla ya dhiki
Kuu. Hii inadhihirisha ya kuwa Kanisa
litaondolewa kabla ya dhiki kuu.
§
Pia
neno Kanisa halitumiki baada ya sura ya 3 hadi 22.
UPEKEE WA DHIKI KUU:
Lengo
la 3: Eleza kwa nini dhiki kuu ni jambo la pekee katika historia ya Binadamu
duniani.
§ Dhiki kuu ni tukio la pekee katika historia
katika dunia, kwa sababu ni dhiki pekee ambayo inaitwa siku kubwa ya hasira ya
Mungu.
§ Hakujawahi kuweko wala haitajuja iweko dhiki
iliyo kuu kama hiyo katika Historia ya dunia
UNYAKUO WA KANISA –(1Thess. 4:11-13)
Lengo
la 4: Eleza mambo yatakayotokea wakati wa kunyakuliwa Kanisa.
§
Tunaamini
Kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki kuu, kwa sababu hatusomi neno lolote
“Kanisa” kutoka Ufu. 4:1-22. Hivyo Kanisa halitapitia katika dhiki kuu (1Thes.
5:9). Mambo mawili yatatokea wakati Yesu
anakuja kwa mwaliko mkuu kutoka mbinguni- Baragumu Italia:
(a)
Kwanza, wafu waliolala katika Kristo watafufuliwa.
(b)
Pili,
walio hai watabadilishwa na kunyakuliwa pamoja na wafu waliofufuliwa kumlaki
Bwana hewani.
N.B: Yesu
ataleta roho za waliokuwa katika Bwana pamoja naye ili kuungana na Miili
iliyofufuliwa.
MANENO YANAYOTUMIWA KATIKA KUJA KWA YESU:
Lengo
la 5: Eleza maana ya maneno ya Kigriki yanayotumiwa, maneno ni:
§
HARPADZO -
Kunyakua kwa nguvu
§
EPIPHANELA - Mng’ao
§
PAROUSIA -
Kuja mwenyewe.
MAJADILIANO YA MWASWALI MATATU KUHUSIANA NA SIKU ZA MWISHO (Mt.
24:3)
§
Mathayo
haelezi jinsi Yesu alivyojibu maswali, Bali Luka anaelezea majibu. Siku za mwisho zitaambatana na usaliti,
wakristo wa uongo, chuki na mateso kwa waamini.
Pamoja na kurudi nyuma kwa watu, Injili itahubiriwa duniani pote.
§
Yesu
alielezea matukio ambayo yangetokea mara moja na yale yangetokea baada ya muda
mrefu katika taifa la Wayahudi hasa kuangamizwa kwa hekalu na mji wa
Yerusalemu. Alieleza.
§
Anaelezea
na dalili zitakazoonyesha kuja kwake.
Mt. 24:2-14 – Yesu anaelezea mambo yatakayotokea kabla ya Kanisa
kunyakuliwa:-
Manabii
na wakristo wa uongo watakaowadanganya watu wengi.
Kuongezeka
kwa vita, njaa na matetemeko yatakuwa mwanzo wa utungu.
Mateso
yataongezeka zaidi kwa waamini na wengi wao wataacha imani.
Vurugu,
uhalifu na kuasi sheria za Mungu kutaongezeka.
Injili ya Kristo itahubiriwa duniani pote.
§ Mt. 24:42-44 - Hakuna ajuaye saa ya Yesu
kuja kunyakua Kanisa. Siku itakuja ghafla kwa waamini na wasioamini.
§ Mt. 24:15-28 - Yesu anaelezea matukio yatakayotokea
wakati wa kipindi cha dhiki ambayo waliookoka wakati huo watayaona kabla ya
Yesu kurudi mara ya pili.
Chukizo
la uharibifu lililonenwa na nabii Danieli
Kutokea
kwa manabii na wakristo wa uongo watakaowadanganya hata wateule.
Taabu
na dhiki kubwa
Jua na
Mwezi kutiwa giza na nyota kuanguka.
Yesu
atarudi mara ya pili.
§
Mt.
25:1-13 – Mfano wa Wanawali Kumi:
Huu
mfano unaonyesha unyakuo utawajia ghafla waamini waaminifu na wasio waaminifu. Yesu
anatuasa kuwa hatangojea kanisa lote lijiandae.Hivyo kila mwamini anatakiwa
kujiandaa kwa kuishi maisha matakatifu na kuwa na Uwepo wa Roho Mtakatifu.
§
Mt.
25:14-30 - Mfano wa
Talanta:
Hapa
Yesu anatueleza kanuni muhimu zitakazoamua nafasi ya mwamini katika ufalme wa
mbinguni. Nafasi na thawabu zitategemea
jinsi ulivyojitoa kwa Bwana na Ufalme wake.
§
Mt. 25:31-46 – Hukumu ya Kondoo na Mbuzi:
Kondoo -ni watu waliookoka na wako hai wakati wa dhiki
kuu.
Mbuzi – ni watu waovu waliosalia wakati wa dhiki kuu.
§ Hukumu
inahusiana na :-
Kutenganishwa
kwa watu waliookolewa na watu waovu.
Na
matendo ya upendo na huruma kwa wale walioteseka kwa ajili ya Yesu.
Waovu
watatupwa katika ziwa la moto na wenye haki watakuwa raia katika ufalme wa
Mungu.
ANAYEZUIA NA MPINGA KRISTO:
Lengo
la 6: Mtambue anayezuia uovu na mpinga Kristo:
§
Walimu
wa uongo wamekuwa wanawaambia Wathesalonike kuwa siku ya Bwana imekwisha
pita. Hivyo waliamini kuwa wameachwa.
§
Mambo
mawili ambayo lazima yatokee kabla ya dhiki kuu:
o Uasi mkuu utatokea
o Mpinga Kristo atatokea.
§
Roho
Mtakatifu akitenda kazi kupitia Kanisa ndiye anazuia uasi na Mpinga Kristo.
§
Mwovu
atakuja katika mamlaka kwa njia ya udanganyifu na kufanya miujiza. Hivyo watu wengi watampokea kwa sababu ya
kukataa kweli.
§
Jinsi
tunavyoendelea mwisho wa nyakati uasi na uovu unaongezeka. Utafikia kilele wakati wa mpinga Kristo.
MASWALI:-
1. Kunyakuliwa kwa Yohana kwenda mbinguni
kunawakilisha nini?
2. Taja mambo mawili yatakayotokea wakati wa
kunyakuliwa kwa Kanisa.
3. Katika waraka wa Wathesalonike Paulo
anasema yupo azuiaye kutokea kwa mpinga
Kristo. Huyo ni
nani?
4. Ni mambo
gani Yesu anaelezea katika sura zifuatazo:-
(a)
Mt.
24:4-14
(b)
Mt.
24:42-44
(c)
Mt.
24:15-28
MWENYE KITI CHA ENZI MBINGUNI –
4:3
Lengo
la 1 : Mtambue mwenye kiti cha Enzi mbinguni.
Mwenye Kiti cha
Enzi mbinguni ni Mungu mwenyezi. Anayeishi katika utukufu akiwa amezungukwa na
viumbe vinavyomwabuudu. Upinde wa mvua
ulikizunguka Kiti unaonyesha Ahadi za Mungu.
MAELEZO KUHUSIANA NA WAZEE ISHIRINI NA NNE - Ufu. 4:4
Lengo la 2: Elezea na kuwatambua wazee Ishirini na
Nne (Ufu. 4:4)
Wazee wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu
vichwani mwao wanaonyesha ni watu waliokombolewa kwa sababu wao wametajwa kwa
mara ya kwanza katika Ufunuo 4;4, 10 na kisha tena katika 5;8,14 na niwazi kuwa
popote wanapotajwa wanawakilisha watakatifu wa agano jipya walionyakuliwa na
sio malaika jina linalotumiwa kuwaita wazee hao kwa kiyunani ni Presbuteros ambalo kwa akawaida
halitumiwi kuzungumzia malaika :-
§ Mavazi meupe ni
kwa ajili ya watu waliokombolewa Ufunuo 5;11-14.
§ Taji za dhahabu
wanapewa waliokombolewa baada ya kumshinda shetani-3:3
§
Kufuatana
na Ufu.21:12-14 – ukuta wa Yerusalemu una milango 12 yenye majina ya makabila
12 ya Israeli na misingi 12 yenye majina ya mitume 12.
§
Hakuna
katika Biblia ambapo malaika hutajwa kama wazee.
§
Kutokana
na Ebr. 11:39,40 na Ufu. 21:12-14 inaonekana wazee hao huwakilisha watakatifu
wa Agano la Kale na A/Jipya.
VITAMBUE VIUMBE HAI WANNE – 4:6-11
Lengo
la 3: Eleza viumbe.
§ Viumbe hai wanne vipo kwa ajili ya kusifu Mungu
mwenyezi. Inawezekana viumbe hivi vinawakilisha viumbe wote. Viumbe vyote
vitaleta utukufu na heshima mbinguni wakati vitakapokombolewa kutoka katika
laana.Neno la kiyunani linalotumika kuwataja viumbe hao ni “Zoa” ambalo linaweza kutafasiriwa kama Mnyama, au walio hai, au
viumbe na ni tofauti na neno lile mnyama linalotumika katika maeneo mengine
kama Ufunuo 13;18, 14;9-11, 15;2, 16;10 viumbe hawa ni wa kipekee na ni tofauti
sana na wengine kama Makerubi, Maserafi na ni tofauti na wale wazee na
wanaonekana kufanya huduma maalumu sana licha ya viumbe hao kuhisiwa kuwa
wanawakilisha falme za wanyama wote yaani wa kufugwa wa porini wa angani n.k
pia huisiwa kuwakilisha mfumo wa injili zile nne katika kumuelezea Yesu Kristo.
UFUNGUO
|
MATHAYO
|
MARKO
|
LUKA
|
YOHANA
|
WASOMAJI
|
WAYAHUDU
|
WARUMI
|
WAYUNANI
|
KANISA
|
INJLI
YA
|
UFALME
|
MATENDO
|
HEKIMA
|
UFUNUO
|
KIINI
|
YESU NI MFALME WA WAYAHUDI
|
YESU NI MTUMISHI MWAMINIFU WA MUNGU
|
YESU NI MWANA WA ADAMU
|
YESU NI MWANA WA MUNGU
|
ISHARA
YA
|
SIMBA ishara ya nguvu na ufalme na UBWANA UFALME WA YESU
|
NG’OMBE alama ya utumishi uvumilivu na unyenyekevu
UTUMISHI WA YESU
|
MWANADAMU
Ishara ya Hekima ufahamu na utii
UANADAMU WA YESU
|
TAI Ishara ya ujasiri uungu asili ya mbinguni
UUNGU WA YESU
|
KITABU KILICHOTIWA MHURI - Ufu. 5:1.
Lengo
la 4: Eleza maana ya kitabu hiki.
§
Kitabu
hiki kina umuhimu sana kwa sababu kina ufunuo wa Mungu kuhusiana na mambo
yatakayokabili dunia na mwanadamu katika siku zijazo. Kinaelezea jinsi watu
watakavyohukumiwa, ushindi wa Mungu na watu wake juu ya uovu. Kila muhuri
unapovunjwa jambo hutokea.
YESU KRISTO MWANAKONDOO ANAYESIFIWA – 5:6-14
Lengo
la 5: Eleza maana ya Mwanakondoo aliyechinjwa.
§
Kristo
anaonekana kuwa ni Mwanakodnoo aliyechinjwa.
Hii inaonyesha kujitoa kwake pale msalabani (Kalvari) Kwa ajili ya
dhambi za watu. Ni kitambulisho cha
kustahili, nguvu, mamlaka na ushindi wa Yesu juu ya msalaba.
§
Pembe Saba
zinaonyesha nguvu na uwezo wa mtawala.
KUFUNGULIWA KWA MIHURI SITA – 6:1-17.
Lengo la 6: Taja vitu vinavyotokea baada ya
kufungua mihuri sita.
§ Watu wengi wasioamini kuwa Kanisa litapitia
katika dhiki kuu wanaamini kuwa kufunguliwa kwa mihuri ni mwanzo wa dhiki kuu.
§ Mhuri wa Kwanza- Mpanda farasi mweupe mwenye uta kinywani ni Mpinga Kristo.
Ufunuo 6;1-2 Daniel 7;8,23, 26, 8;8-10,20-25, 11;35-45,Wathesalonike
2;1-12 Ufunuo 13;1-18, 17;10-16. Mpinga Kristo ni kiongozi atakayekuwa na
usahawishi mkubwa kwa dunia kama mtu mwenye majibu ya matatizo ya kiuchumi, kisiasa,
na kijamii Yeye atakapotokea atakuwa na nguvu ya kuzishawishi serikali kwa
pamoja na kueleta jibu la amani kwa
Dunia anaonekana kuja katika farasi mweupe ili kumuigiza Kristo lakini Yeye
siye mfalme wa amani hata kidogo lakini mpango wake ni kuiondoa amani yote
iliokuwa imesalia Yesu atakuja akiwa amepanda farasi mweupe lakini Hatakuwa na
uta alama ya kivita kama aliyokuja nayo mtu huyu Ufunuo 19;11-21 mpinga Kristo kuwa na uta ni
Ishara ya uovu ona Zaburi 46;9 na Yeremia 49;35
§ Mhuri wa Pili- Farasi mwekundu anawakilisha vita na vifo vya kutisha.
Ufunuo 6;3-4 Mathayo 24;6-7 ni wazi kuwa hii ni hatua ya kujidhihirisha
kwa moyo wa mpinga Kristo kwani kuja na Farasi mweupe kulikuwa na maana ya
amani lakini amani hiyo sio ya kudumu
roho ya ukatili ya kushindana na kushinda inajifunua ni wazi kuwa dunia
itashuhudia umwagikaji mkubwa wa Damu ambao ni wa kutisha sana Farasi huyu
atakuwa na nguvu ya kuiondoa amani duniani watu watauana hii itakuwa hali
ambayo haijawahi kutokea au kuonekana duniani vinginevyo isingelipewa nafasi ya
kuwamo katika dhiki hii kuu
§ Mhuri wa Tatu- Farasi mweusi unaonyesha njaa na ukame wa kutisha.
Ufunuo 6;5,6, Mathayo 24;7. Maandiko yanapozungumza juu ya tukio la
kupimwa kwa mkate au shayiri au nafaka ni wazi kuwa inazungumzia njaa ona
2Wafalme 7;1 na Ezekiel 4;10-17 ni wazi kabisa kuwa wakati wa dhiki ile
kutatukia njaa halisi ambayo haijawahi kutukia katika Historia ya njaa duniani
njaa ya aina yoyote ambayo umewahi kuisikia au kuishuhudia ni mfano tu wa njaa
kuu itakayoikumba dunia ya wakati wa dhiki kuu
§ Mhuri wa Nne - Farasi wa kijivu akiwakilisha
vita, njaa, tauni na hayawani Mauti na Kuzimu
Ufunuo 6; 7-8. Mathayo 24;7 ni wazi kuwa Tatizo linaendelea kuwa kubwa
farasi huyu anawakilisha mauti na kuzimu huku vita , njaa na mengineyo
yakiwakilisha aina za vifo vitakavyotokea wakati wa dhiki ile kuu ni wazi kuwa
Robo ya watu watakufa vitani kwa upanga, njaa
ama kukosekana kwa chakula na
kuuawa na wanyama au hayawani wa inchi kwani njaa hii itawasumbua na wanyama wa
mwituni ambao kwaajili ya kujikimu hawataogopa kuingia katika makazi ya
watu na kujipatia kitoweo hili
halipendezi lakiini limeruhusiwa kwaajili ya kutimiza hukumu kubwa ya Mungu
dhidi ya wanadamu wanaoikataa neema . Kumbuka kuwa muhuri hizi nne zitakuwa
zikimwagwa kwa robo ya dunia ya wakati huo na sio ulimwengu mzima tunaoufahamu
§ Mhuri wa Tano - Watakatifu waliouawa wakiwa mbele ya Kiti cha Enzi. (chini ya
madhabahu)
Ufunu 6;9-11,Mathayo 24;8-28 Ni wazi kuwa maono haya yanaonyesha kuwa
kuna watakatifu kadhaa ambao wataokolewa au roho zao kupokelewa mbinguni hata
hivyo hili sio jambo la kutia moyo hata kidogo,Hawa ni watu ambao wataokolewa
kwaajili ya kuuawa kwaajili ya Neno la Mungu na Ushuhuda wao watakuwa
wamegharimika kwa kiwango cha kutisha sana , ni wazi kuwa roho zao zitalia
kwaajili ya kisasi cha adui na watesi wao ni wazi kuwa ni gharama kwa mkristo
kutarajia wokovu wakati wa dhiki kuu
§ Mhuri wa Sita - Tetemeko kubwa linalotikisa ulimwengu mzima Hasira ya mwanakondoo.
Ufunuo 6;12-17 Mathayo 24;29,30. Muhuri huu unaonyesha jinsi Kristo
alivyo na nguvu kuu na kuwa Yeye ni mtawala juu ya yote na kuwa watu wote
wanatambua nguvu na mamlaka kubwa aliyonayo na wanatambua ghadhabu aliyonayo
mwana kondoo na kutafuta kujisitiri ingawa wanamtambua kama mwana kondoo wakati
huu ni kwa sababu tu ya hofu kubwa waliyonayo lakini ni wazi kuwa wao
walimpinga kwa muda mrefu na sasa wanalazimika tu kumuogopa mwanadamu hata
akiwa na nguvu kubwa sana ni dhaifu sana mbele za Mungu.
MASWALI:
1.
Je, Wazee Ishirina na nne ni akina nani?
2.
Taja matukio yanayotokea kila muhuri unapofunguliwa. (Ufu. 6:1-17)
MATUKIO KATIKATI YA DHIKI KUU NA KUENDELEA: Ufunuo
7;1-17
Lengo
la 1: Eleza matukio – dhiki kuu hadi mbingu mpya.
§
Kufungua
mihuri saba na Baragumu saba miaka 3 na nusu ya kwanza.
§
Vitasa
saba katika miaka 3 na nusu ya mwisho
§
Ufufuo
wa Watakatifu
§
Utawala
wa miaka 1,000
§
Hukumu
ya mbele ya Kiti Cheupe.
§
Mbingu
mpya na nchi mpya.
MALAIKA WANNE NA MALAIKA ANAYETIA MUHURI – 7:1-3
Lengo
la 2: Eleza sababu za kutiwa muhuri wa 144,000.
Malaika wanne wanazuia upepo, na kuidhuru
nchi. Malaika mwingine anatokea kwa
ajili ya kuwatia muhuri watumishi wa Mungu.
Lengo la kutiwa muhuri 144,000 ni kuwapa ulinzi wakati wa hukumu inapotolewa
ili kwamba majeshi ya pepo waovu yasiwadhuru.Swala hili linafanyika kati ya
muhuri ule wa sita na kabla kidogo ya muhuri ule wa saba kusudi ikiwa ni kuwalinda wateule au mabaki
katika Israel.
WATU 144,000 - 7:4.
Lengo
la 3: Eleza ni akina nani 144,000 kutoka makabila kumi na mbili.
§
Hawa ni
Wayahudi watakaomwamini Kristo wakati dhiki kuu kutoka kabila 12 za
Israeli. Muhuri vipajini pao ni
kuonyesha kuwa ni mali ya Mungu na watalindwa na Mungu kutokana na hukumu yake.
144,000 –WATAMBULIWA – 7:5-8.
Lengo
la 4: Eleza sababu zinazofanya makabila mengine yameondolewa:
§
Majina
ya Dani na Efraimu hayamo katika orodha ya makabila ya Israeli. Hii inawezekana kwa sababu makabila haya
yaliongoza taifa katika ibada za sanamu na uasi.
MKUTANO MKUBWA WA WALIOVAA MAVAZI MEUPE - 7:9-17.
Lengo
la 5: Eleza umuhimu wa watu hawa
waliovaa nguo nyeupe (Ufu.7)
§
Hawa ni
watu walioamini wakati wa dhiki kuu. Wametoka katika kabila za duniani. Watanyakuliwa mwishoni mwa dhiki kuu na
kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo. Ukweli
huu unaonyesha watu wataokolewa wakati wa dhiki kuu.
Wazee 24
|
Mkutano Mkubwa
|
Wameketi Vitini
|
Wamesimama mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu
|
Wana Taji
|
Hawana Taji
|
Wana vinubi na vyelezo
|
Wameshika matawi ya mitende.
|
MALAIKA ALIYE NA CHETEZO CHA DHAHABU – 8:3,4
Lengo la 6 : Eleza ni nani malaika mwenye chetezo.
§ Muhuri wa Saba
unafunguliwa kunakuwa na ukimya. Hapa
haijulikani maana yake. Malaika aliye na
chetezo ni Yesu Kristo kwa sababu katika A/Kale, makuhani peke yao walifukiza
uvumba kuwaombea watu. Katika A/Jipya
Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu, mpatanishi kati ya Mungu na watu.
TARUMBETA au
BARAGUMU SITA - 8:6-9:21
Lengo la 7: Eleza ni matukio gani yatakayotokea
wakati wa kupigwa tarumbeta Sita.
§ Tarumbeta ya 1 –
Mvua ya mawe, moto, Damu Ufunuo 8;7.
Theluthi 1 ya miti na mimea ya nchi itateketea, bila shaka swala hili
litaongeza njaa ambayo ilikuweko tangu kufunguliwa kwa Muhuri zile
§ Tarumbeta ya 2
– Mlima unaowaka Ufunuo 8;8-9
Theluthi1 ya bahari kuwa damu na viumbe na meli Kuangamizwa, Bla shaka
mlima huo wa moto ni kitu kama kimondo kiytakachoupwa juu ya bahari na theluthi
ya viumbe vya baharini vitauawa na hivyo asili nyingine ya vitoweo au chakula
kupungua, Biashara zitaathiriwa kwa kiwango kikubwa hasa kutokana na theluthi ya
merikebu hukumu hii inatukumbusha hukumu ile iliyokuwa juu ya Inchi ya Misri
wakati wa Nabii Musa.
§ Tarumbeta ya 3 –
Pakanga , maji machungu Ufunuo 8;10-11
Theluthi 1 ya mito na chemchemi zitaathirika na watu wengi kufa hii ni
kutokana na kuanguka kwa nyota hii iitwayo pakanga mpinga Kristo pamoja na
nguvu zake zote alizonazo atashindwa kutoa msaada wakati watu watakapokuwa wanaangamia kwa kunywa maji machungu.
§ Tarumbeta ya 4 –
Giza kuu Ufunuo 8;12
Theluthi 1 ya jua ikapigwa, na 1 ya Mwezi na 1 ya nyota ili Theluthi
itiwe giza ni wazi kuwa taa za ulimwenguni hazitakuwa na uwezo wa kudhibiti
aina ile ya giza ambayo Mungu ataipiga kwa Dunia pigo hili pia latukumbusha
uweza wa Mungu uliokuwa juu ya Nchi ya Misri ambayo nayo ilipigwa kwa Giza zito
wakati wa siku za Nabii Musa.
§ Tarumbea ya 5 – Nzige wanaotesa Ufunuo 9; 1-12.
Majeshi ya pepo waovu kutesa watu wasio na muhuri wa Mungu kwa miezi
mitano.inaonekana wazi kuwa Nyota inayotajwa katika mstari wa Kwanza ni malaika
ambaye alipewa funguo za kuzimu Hatuwezi kusema kuwa alikuwa ni malaika wa
upande wa shetani kwani angewafungulia viumbe hao ili kuwatumia kwa maanufaa ya
Ibilisi, lakini ni wakati wa kuruhusiwa kwa viumbe hao ambao watatesa na
kuumiza watu hususani wale ambao hawana muhuri ya Mungu katika vipaji vyao,
nzige hao wenye kutisha hata hivyo hawana mamlaka ya kuua isipokuwa kuumiza
§ Tarumbeta ya 6 –
theluthi ya watu kuuawa Ufunuo 9; 13-15.
Malaika wanne walifunguliwa na kuuwa theluthi 1 ya watu bila
shaka ni miongoni mwa malaika wale walioanguka
nguvu zao zinazidi zile za wale nzige kwani wao licha ya kudhuru pia
wanaua kwa moto moshi na kiberiti na
kuuma kama nyoka wao wanaonekana kuwa viongozi wa jeshi la wapanda farasi
wanaotajwa Mstari wa 16-19 wapanda farasi wapatao 200,000,000. Hata hivyo jambo
la kushangaza ni kuwa pamoja na mapigo hayo wanadamu waliosalia hawakuwa tayari
kutubu dhambi zao Mastari wa 20-21 hii haina tofauti na wakati wa mapigo kule
Misri ambapo moyo wa farao na watu wake ulikuwa mgumu.
§ Malaika
mwenye nguvu Ufunuo 10;1-11;14
Lengo la 1
: Eleza ushahidi unaoweza kukusaidia kujua huyu malaika ni nani.
§
Ushahidi
unatuonyesha kuwa huyu malaika mwenye nguvu ni Yesu ni huu ufuatao:-
§
Mwonekano
wake ni sawa na Yesu wa Ufunuo - 1:13-15
§
Kiapo
chake anachoapa.Hakuna katika Biblia malaika aliyeapa.
§ Sauti yake kama simba aungurumapo.Biblia
(Yoel. 3:16) inasema Bwana anaunguruma kama simba (Hosea 11:10, 11; Amosi 3:8)
Usemi wa malaika “hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufu.10:6-7). Una maana kuwa yale yaliyokusudiwa hukumu juu
ya uovu lazima utekelezwe.
Ni wazi
kuwa malaika huyu mwenye nguvu ni Yesu Kristo mwenyewe kule kuvikwa winu
kunatukumbusha lile tukio katika mlima wa ugeuko Marko 9;7 na pia wakati
alipokuwa anapaa juu Matendo 1;9 pia ziko semi za Bwana mwenyewe akihusisha
kurudi kwake na mawingu Mathayo 24;30 na nguvu na utukufu Yeye alisema Tangu
sasa mtamwona mwana wa adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni Mathayo 26;64 pia
usemi ule Tazama yu aja na mawingu Ufunuo 1;7
Ushahidi
mwinne ya kuwa malaika huyu mwenye nguvu ni Bwana ni kuonekana upinde wa mvua
ukiwa umemzungukakama alivyoona mapema Yohana katika Ufunuo 4;3 na ndivyo
ilivyo kwa malaika huyu mwenye nguvu, pia inatukumbusha kuwa huyu ni Mungu
mwenye kutunza maagano
Uso
wake ulikuwa kama jua na miguu yake kaa nguzo ya moto hii ni sawa na kile
alichokiona Yohana katika ufunuo 1;14-16 Yohana alipona mng’ao huo alianguka
kama ilivyokuwa kwa Sauli wa Tarso malaika huyu alikuwa na kitabu kidogo
ambacho yohana alikiona katika Ufunuo 5;1-4 ambacho kilimtia wasiwasi na baada ya ufafanuzi tumaini Ufunuo
5;5-7,6;1. Ni wazi kuwa alikuwa Kristo mwenyewe mwana kondoo
Hakuna
uthibitisho wa malaika ambaye alitumwa na Mungu na akaambatanisha kiapo,
kuunguruma kwake kama simba ni wazi katika maandiko kulimaanisha Bwana mwenyewe
Yoel 3;16,Hesea 11;10-11,Amosi 3;8. Ngurumo saba zilitokea wakati malaika huo
alipotoa kilio cha Kwanza
§
YOHANA
ATUMWA KUTOA UNABII - Ufu.10:8-11
Lengo la 2: Eleza maana ya Yohana kula
kitabu kidogo.
Kitabu hicho alichokula Yohana kilikuwa na
ujumbe uliokuwa unaeleza kukamilisha kusudi la Mungu kwa watu duniani. Kilielezea mambo yatakayotokea.Kujua ujumbe
kulikuwa kutamu kama asali, bali baadaye kulisababisha uchungu ndani ya moyo wa
Yohana. Hivyo Mungu anamwagiza akahubiri
ujumbe huo ili watakaomwamini wapate uzima wa milele na wasioamini wapate
kuhukumiwa.
MAELEZO ZAIDI KABLA YA BARAGUMU YA SABA –
Ufu.11:1-14
Lengo la 3:
Eleza maana ya kupimwa kwa hekalu na mahusiano yake ni miezi 42.
1.
Kulipima
Hekalu – 11:1,2:
Kupimwa kwa hekalu na madhabahu na kuhesabiwa kwa wanaoabudu
kunamaanisha kuwa Wayahudi watajenga hekalu lao. Kutokana na Agano lao na mpinga Kristo
watakuwa na uhuru wa kuabudu. Katikati
ya dhiki kuu mpinga Kristo atavunja agano na kulinajisi hekalu. Kipindi cha miezi 42 ambacho ni miaka 3 na
nusu mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa, mpinga Kristo atawatesa
na kuwaua Wayahudi waaminifu. Mwisho wa
miaka 3 na nusu utakamilisha mwisho wa kipindi cha mataifa.
2.
Mashahidi
wawili - 11:3-14
Lengo la 4:
Eleza kusudi la Mashahidi wawili, uwezo wao, matokeo ya ushuhuda wao na
ni akina nani.
Mashahidi
wawili watatokea ambao watahubiri Injili kwa uwezo mkubwa huku wakileta hukumu
na mapigo kwa wale wanaowapinga.
Watahubiri Injili kwa muda wa siku 1260.
Baada ya kumaliza ushuhuda watauawa na mpinga Kristo ambaye atakuwa
amepona jeraha lake. Miili yao italazwa
mitaani na kushuhudiwa na watu kwa njia ya Televisheni. Baada ya siku tatu,na nusu watafufuliwa na
kupaa, matokeo yake kutakuwa na tetemeko kubwa la ardhi litakaloua watu 7000.
Mashahidi wanadhaniwa na wanatheolojia kuwa
ni Henoko na Eliya kwa sababu hawakuonja mauti walitwaliwa mbinguni.
Sifa
za mashahidi wa nyakati za dhiki kuu.
Mwanzo 5;24, Zekaria 4;10-14 Malaki 4;5-6
Waebrania 11;5 Kuna hisia za watu watatu wanaokisiwa kuwa mashahidi wa siku za
nyakati za dhiki kuu watu hao ni pamoja na Eliya,Henoko na Musa hata hivyo
kulingana na sifa za kimaandiko wanaokisiwa wanapaswa kuzifikia ni pamoja na
Mashahidi
hao watatokea mbinguni Mstari wanne 4
Watapewa
nguvu za kupita kawaida ambazo wasingeweza kuwa nazo na sio lazima wawe
wamekuwa nazo katika wakati uliopita Mstari 3-10
Watahubiri
na kufanya unabii kwa miaka mitatu na nusu wakiwa wamevikwa magunia Mstari wa 3
Wao
ndiyo ile mizeituni miwili na vile vinara mbele za Mungu wa mbinguni mstari wa
nne
Wao ni
lazima wawe ambao hawajawahi kufa na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara
moja na baada ya kufa ni hukumu Waebrania 9;27
Wao
watauawa katika barabara na kukaa hapo kwa siku tatu na nusu ndipo
watanyakuliwa Mstari wa 7-12.
§ Kazi kubwa n ya mashahidi hawa ni kuionyesha
dunia hii iliyoharibika uweza na nguvu za Mungu, hakua mtu atakayeweza kuwazuia
wala kuwaua mpaka watimize huduma yao
§ Baada ya kukamilisha kazi mnyama atokaye kuzimu atafanya vita nao na
kuwashinda na kuwaua
§ Maadui wa Mungu watafurahi na miili yao
itaachwa bila kuzikwa juu kwa siku tatu ili kuwaaminisha watu kuwa wamekufa
kwelikweli na watasheherekea na kupeana zawadi
§ Hata hivyo furaha yao itakuwa ya muda mfupi
kwani watafufuliwa na kisha kunyakuliwa juu ni wazi kuwa kupitia huduma yao
watu wengi mmno wataokolewa wakati wa dhiki kuu.
Fundisho:
Mtumishi wa Mungu ataondolewa ikiwa amemaliza kazi.
§
Tarumbeta
ya 7 – shetani anafukuzwa Ufunuo 11;15.
Sauti kutoka mbinguni kuwa ufalme ni wa
Mungu bara gumu hii inalia katikati yaq kipindi cha dhiki kuu au katikati ya
juma la sabini la nabii Daniel chini ya baragumu hii kuna matukio kadhaa
yanajitokeza
KUPIGWA KWA BARAGUMU YA SABA - 11:15-19
Lengo la 5: Eleza mkazo wa baragumu lasaba.
Mkazo wa baragumu ya saba ni tangazo la kuwa
falme za ulimwengu zimekuwa ufalme wa Yesu Kristo. Pia inaonyesha kuwa hukumu inakaribia
kumalizika, “kufunguliwa kwa Hekalu la Mungu mbinguni na sanduku la agano
kuonekana hekaluni mwake”, ina maa lengo la agano ambalo ni ahadi ya ufalme
linakaribia kutimizwa. Mungu anatunza
ahadi ya neno lake. Matetemeko ni dalili ya kuja kwa mwisho.
MWANAMKE NA JOKA.
MWANAMKE
ALIYEVIKWA JUA – 12:1-6,13-16.
Lengo la 6: Eleza na kumtambua huyu mwanamke
aliyevikwa jua na elezea na Kukimbia kwake:
Ishara 1: Mwanamke
huyu ni taifa la Israeli lenye makabila kumi na mbili ambamo Masihi anatokea kwake.Mwanzo
27;9-11,Isaya 54;5-10,Yeremia 3;1-14,Hosea 2;14-23,3;4-5,Mika 5;3 Zekaria
12;10,Warumi 11;25-27 Mathayo 24;15-22. Ni wazi kuwa mwanamke huyu sio kanisa
hata kidogo, Mtoto mwanamume ni wale wayahudi 144,000hawa wanaitwa wazaliwa wa
kwanza kwa Mungu na mwana kondoo
Ishara 2: Joka
lenye vichwa saba na taji maana yake ni shetani katika nguvu zake. Nyoka
mbinguni ni malaika waasi aliofukuzwa nao kutoka mbinguni. Mtoto aliyenyakuliwa ni Yesu Kristo
aliyezaliwa na kufufuliwa na kupaa kwenda mbinguni. Naye atatawala mataifa. Mwanamke alikimbia
maana yake katikati ya dhiki kuu Israeli wanakimbia kutoka Utawala wa mateso ya
mpinga Kristo. Israeli atakimbilia
Perta huko katika nchi Ya
Yordan, na kuhifadhiwa kwa muda wa miaka 3 na nusu. Hawa Waisraeli ni Uzao utakaosumbuliwa (Ufu.
12:13-17)
Mabaki ya mji wa wa Petra Kiyunani au Sela
Kiibrania ambao ulikuwa chini ya serikali ya Edomu kama ngome zake
zinavyoonekana leo huko ng’ambo yam to Yordani inaaminika kuwa ni katika mji
huu Israel wengi watakimbilia huko na
kujificha Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.
MASWALI:
1.
Ni ushahidi gani unaotuonyesha kuwa huyu malaika ni Yesu
Kristo?
(a)
________________________
(b)
________________________
(c)
________________________
2.
Nini
matokeo ya ujumbe wa mashahidi wawili (11:3-14)
3.
Baragumu
ya saba inaashiria nini?
4.
Taja ishara zilizomo katika Ufu. 12:12.
JOKA NA VIBARAKA VYAKE. 12:3-4.,7,9,13;2-4 16;12,20;2.
Lengo
la 1: Mtambue joka na shughuli zake.
Huyu anajulikana kama shetani, joka la
zamani la Ibilisi. Majina yana maana
gani?:-
§
Joka la
zamani – mdanganyifu – Mwa. 3:1-13
§
Ibilisi
- Mjaribu, mwenye hila, mpingaji – Mt. 4:1; Efe. 6:11;
§
Shetani
- mshitaki – 1Pet 5:8; Zek 3:1
VITA MBINGUNI - Ufu. 12:7-12;
17:7-18
Lengo
la 2: Eleza vita hivyo mbinguni.
§
Wakati
wa dhiki kuu hakutakuwa na mapambano ya kiroho duniani tu, bali hata mbinguni
kutakuwa na vita mbinguni. Shetani na
malaika zake watapigana na Mungu na malaika.
Shetani atatupwa chini na kutoruhusiwa mbinguni. Akiwa na hasira na
akijua ana muda mchache anafanya vita na Waisraeli waaminifu walioko Israeli
wanashindwa na kutetewa na Mungu.Hivyo anawaudhi mabaki wa uzao ambao Wayahudi
waliotawanyika duniani waliomwamini Yesu Kristo.
MNYAMA ALIYETOKA BAHARINI MPINGA KRISTO – 13:1-10
Lengo
la 3: Elezea asili yake, chanzo cha
nguvu za mnyama.
§ Huyu mnyama ni mtumishi wa shetani, ni
mwanadamu aliyetoka katika watu wa dunia.
Baadhi ya wanatheolojia wanasema ni falme saba ambazo zimesumbua taifa
la Israeli yaani-Misri, Syria, Babeli, Umedi na Uajemi, Ugriki na Rumi. Pembe kumi ni viongozi kumi watakaotawala
pamoja na mpinga Kristo kwa muda mfupi.
§ Atatawala kwa nguvu na mamlaka kwa muda wa
miezi 42. Atakapofufuka au kupona jeraha lake atataka watu wote wamwabudu. Atawatesa na kuwaua watakatifu wengi. Kutokana
na uwezo aliopewa shetani atawaunganisha watu kupigana na Mungu.
§ Ni wazi kabisa kuwa mnayama huyu ndiye mpinga Kristodamiel
7;8,11,20-25,8;23-27,11;36-45,2Thesalonike2;7-8,Isaya 14;4-17,Mathayo
24;15,Ufunuo 13;1-10,17;8,11. Huyu atakuwa ni mwanadamu kabisa ambaye ata kuwa
ameasi na kujitoa kabisa kwa shetani ni mwana wa upotevu 2Wathesalonike 2;3
hata pamoja na nguvu atakazo kuwa nazo ufalme wake hauta kuwa ni wa dunia yote
yeye atahusika na eneo la Rumi ya kale
atazitiisha nchi za Uyunani,uturuki na Misri kati ya zile dola kumi za
Rumi iliyofufuka na nyingine zinzjitolea
tu kwake Daniel 7;8 Makao makuu ya kwanza ya Mpinga Kristo yatakuwa Babel na
kisha atahamia Yerusalem kulingana na Isaya 14;4-11
MNYAMA KUTOKA KATIKA NCHI NABII WA UONGO - 13:11 -18
Lengo
la 4 : Elezea kuhusiana na mnyama wa
pili.
§
Huyu
mnyama anaonekana kama mwana-kondoo, lakini anasema kama joka. Hii ina maana atajidai mpole, mwenye upendo
na kujali, lakini tabia yake ni ya kishetani.
Huyu ataanzisha kanisa la uongo ambalo litamwabudu mpinga Kristo. Atafanya miujiza minngi na kuwafanya watu
wamwabudu mpinga Kristo. Watauwawa wale watakaopinga amri hiyo na kuwa
waaminifu kwa Yesu Kristo.
NAMBA, JINA NA ALAMA YAKE – 13:16-18
Lengo
la 5: Jadili alama ya mnyama na umuhimu
wake.
§ Ili kuwadhibiti wamwabudu mpinga Kristo
atatumia silaha ya kiuchumi. Wote
wanaotaka kununua na kuuza wawe na namba au jina la mpinga Kristo pajini pa uso
au mkononi. Hivyo namba hiyo itawafanya
watu wamkubali au wampinge mpinga Kristo – wasomi wengi wanahangaika kutafuta
jina la mpinga Kristo lakini wanapingana.
§ Alama – Ufunuo 13;16 alama hii itakuwa
halisi inayoweza kuonekamna kwa urahisi katika mkono wa kuume au kwenye paji la
uso
§ Jina – Ufunuo 13;17 kuwa na jina la mnyama
inawezekana kabisa kuwa ni kuwa na kitambulisho maalumu chenye saini yake
ambacho kitahitajika kwa ajili ya huduma mbalimbali gharama ya kitambulisho hicho
itakuwa nibei ya nafsi na roho na kuwa kila atakayepokea atalazimika kuapa na
kuwa mwaminifu kumuabudu mpina kristo
§ Hesabu yake – Ufunuo 13;18 alama yake ni
sita ,sita ,sita 666 hii ikimaanisha kuwa ni uthibitisho kuwa yeye ni mwanadamu
mwanadamu mwanadamu kupokea chapa hii ni sawa na kukubali kumuabudu Ufunuo 14;9-10. Jipu baya litamwagwa kwa wale
watakaoipokea lama hiyo na mfululizo wa kumwagwa kwa vitasa utaanza
KAHABA MKUU - 17:1-6
Lengo
la 6: Elezea kweli mbili kuhusu kahaba na mambo yake katika siku ya mwisho.
§ Huyu kahaba anawakilisha dini zote za
uongo. Katika Biblia kahaba ni mtu
anayemwasi Mungu na kuabudu miungu mingine.
Hivyo kahaba huyu ataikana Imani na Injili ya Yesu Kristo. Hili ni kanisa
la uongo litakalomsaidia Kristo kupata madaraka. Litashiriki katika kuwatesa watakatifu. Dini na siasa itatumika kutawala
mataifa. Baadaye mwishoni mpinga kristo
atalichukia hili kanisa la uongo. Hivyo
ataiangamiza tasisi hii.
UNABII WA SIKU ZA MWISHO - Dan. 9:24
Mambo sita yatakayokamilishwa katika majuma sabini
ni:-
§
Kumaliza
makosa
§
Kukomesha
dhambi
§
Kusamehe
uovu
§
Kuleta
haki ya milele
§
Kutia
muhuri maono na unabii
§ Kupaka mafuta
mahali patakatifu kabisa.
1. MWANAKONDOO NA 144,000 juu ya mlima sayuni – 14:1-5
Lengo
la 7: Zitambue kweli kuhusiana na
utambulisho na tabia za 144,000:
§
Hali ya
144,000 ni wasafi kiroho, wamekombolewa kutoka duniani wameandikwa vipajini
mwao jina la Baba na wanamfuata Bwana.Hawa ni watakatifu ambao hawakujinajisi
na uchafu wa dhambi na ibada ya mpinga Kristo wala hawajawahi kusema uongo.Hawa
ndio watakao uimba wimbo wa Mwanakondoo.Watakuwa wamechaguliwa miongoni mwa
watakatifu walionyakuliwa kwenda mbinguni kabla ya dhiki kuu.
2. TANGAZO LA MALAIKA WATATU – 14:6-13
Lengo
la 8: Jadili kwa kifupi yaliyomo katika matangazo
ya malaika watatu.
§
Malaika
wa kwanza anawataka watu wote duniani wamche Mungu kwa sababu saa ya hukumu
imefika.
§
Malaika
wa pili, anatangaza kuanguka kwa Babeli – yaani mifumo ya siasa, dini na uchumi
ya dunia imefika kikomo.
§
Malaika
wa tatu, anawaonya watu wanaokubali kupokea chapa watateswa katika ziwa la moto
milele.
§
Wale
watakaokufa katika Bwana watakuwa heri, kwani watapumzika taabu zao (mateso na
kwenda kwa Bwana).
3. MAVUNO YA DUNIA - 14:14-20
Lengo
la 9: Eleza mahusiano ya mavuno na shinikizo la divai.
§
Mavuno
haya yanahusiana na hukumu. Mavuno ya
zabibu ni dunia na shinikizo la divai linahusiana na ghadhabu ya hukumu ya
Mungu, itakayowafikia wakazi wa dunia.
Ni umwagikaji wa damu wa kutisha.
MASWALI:
1.
Nini
maana ya majina haya:
(a)
Joka la
zamani ________________________
(b)
Ibilisi
________________________________
(c)
Shetani
______________________________
2.
Mpina Kristo atakapotoka atafanya nini?
3.
Nabii wa uongo atamsaidiaje mpinga Kristo?
4.
Kahaba
mkuu ni nani?
5.
Namba
ya mnyama 666 itatumikaje?
6.
Nini tabia
za 144,000 walio pamoja na mwanakondoo? (Uf. 14:1-5)
MATUKIO YA MWISHO WA DHIKI KUU:
MAANDALIZI YA VITASA SABA.
1.
ISHARA KUU YA TATU –Ufu. 15:1-8
Lengo
la 1: Itambue ishara kuu ya tatu. Eleza
umuhimu wake.
§
Ishara
kuu inayotolewa hapa ni ya malaika wenye vitasa saba ambayo ni mapigo ya
mwisho. Ishara mbili zingine ni:
Mwanamke aliyevikwa jua (Ufu.12:1) na Joka kubwa jekundu lenye pembe kumi na
vichwa saba (Ufu. 12:3). Ishara kuu ya
tatu ni ya muhimu kwa sababu inahitimisha hasira na hukumu ya Mungu.
2.
KUMWAGWA
KWA VITASA VYA GHADHABU YA MUNGU – 16:1-21
Lengo
la 2: Eleza vitasa saba vinawakilisha nini na athari juu ya wanadhamu:
§ Kitasa 1: Madonda
mabaya na majipu ya kuumiza yawapata wanadamu walio na Alama ya mpinga Kristo.
16;2 ni pigo linalowahusu wale tu waliopokea alama ya Yule myama na sio kwa
dunia nzima
§ Kitasa 2: Viumbe
hai vyote baharini vinakufa.16;3
§ Kitasa 3: Mito
na chimchemi za maji zageuka damu 16;4
§ Kitasa 4: Jua
likawaunguza wanadamu 16;8-9
§ Kitasa 5: Giza
kubwa juu ya utawala wa mpinga Kristo 16;10-11
§ Kitasa 6: Vita
vya Harmagedonia.16;12
§ Kitasa 7: Ngurumo
na tetemeko Babeli na miji ya mataifa yaangushwa. Visiwa na milima ikatoweka,
mvua ya mawe kubwa ilinyesha. 16;17-21
Matokeo ya mapigo haya watu waliendelea na
mioyo migumu na kumtukana Mungu.
KAHABA MKUU (Babel ya siri) – 17:1-18
§
Kahaba
mkuu ni mji ule mkuu ulio na mamlaka juu ya wafalme wote. Hii itakuwa ni Kanisa la uongo ambalo
litakuwa na nguvu ya ushawishi kwa viongozi mbalimbali duniani, katika miaka 3
na nusu ya mwanzo ya dhiki kuu itamsaidia mpinga Kristo ili kupata
madaraka. Lakini mpinga Kristo
atakapopata nguvu na kufufuka au kupona jeraha lake atafanya hila ya
kumwangamiza. Wakati wa kipindi cha
miaka 3 na nusu ya mwisho mpinga Kristo atataka kuabudiwa na wote. Hili kanisa la uongo litashiriki katika
kuwaua watakatifu watakaopingana naye.
PEMBE KUMI - 17:10-15
Lengo
la 3: Elezea juu ya pembe kumi:
§
Mstari wa 10 unazungumzia wafalme saba, watano wameanguka na mmoja
bado. Watu wanaamini kuwa ni falme za
Misri, Ashuru, Babeli, Uajemi na Umedi, Ugriki iliyokuwa bado kuanguka ni
Rumi. Wa saba unakuja ni jumuiya ya
mataifa kumi. Mpinga Kristo atakuwa ni
mfalme wa nane. Pembe kumi ni mataifa
kumi yenye nguvu za kisiasa na watamsaidia mpinga Kristo na kupingana na Yesu
Kristo.
KUANGUKA KWA BABELI NA MIFUMO YA KISIASA NA KIUCHUMI:
HUKUMU YA BABELI - 18:1-24
§
Mji wa
kisiasa na kiuchumu wa Babeli unatafsiriwa na wasomo kuwa unawezekana ni mji
halisi ambao ni makao makuu ya mpinga Kristo.
Pia unafikiriwa kuwa ni mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa mwanadamu.
§
Maangamizi
ya Babeli yanaonyesha kuanguka mifumo ya kisiasa na kiuchumi iliyotokea katika
historia yote ya mwanadamu kama tulivyosoma katika Dan. 2 na 7, lazima mifumo
ya falme za dunia hii kubatilishwa na kuondolewa ili ufalme wa Kristo uje.
§
Mungu
ndiye suluhisho la matatizo yote ya kijamii na kiuchumi ambayo yamesababishwa
na dhambi ya mwanadamu.
§
Mifumo
ya kidunia na mpinga Kristo wataangamizwa.
KUJA MARA YA PILI KWA YESU:
SHUKRANI KWA AJILI YA HUKUMU JUU YA
BABELI.-Ufu. 19:1-5
Lengo
la 4: Wataje wale wanaotoa sifa kwa
Mungu mbinguni na kiini cha sifa zao.
§
Wale
wanaotoa sifa na shukrani ni umati wa watu wengi, wazee ishirini na nne na
viumbe hai wane – Mungu anawatia moyo.
§
Kiini
cha sifa kwa wale wanaomsifu Mungu mbinguni ni
Kuangusha
uasi wa shetani na hukumu ya haki ya Mungu
Tabia
na asili ya Mungu chanzo cha ukombozi.
Kuanzishwa
kwa ufalme wa Mungu katika historia ya mwanadamu.
HARUSI YA MWANA-KONDOO – 19:6-10
Lengoo
la 5: Elezea karamu ya harusi ya Mwanakondoo na vazi la Bibi Harusi
§
Karamu
ya Harusi ya Mwanakondoo inatangazwa katika Maandiko, ila haielezwi kwa undani.
Ni
wakati wa kuunganika kwa Yesu Kristo na watu wake
Itafanyika katika wakati ambao Mungu amefanya
Wale tu
walioalikwa watahudhuria Harusi hiyo, wale waliookolewa.
Mavazi ya Bibi Harusi ni matendo mema ya watakatifu. Kukaa na kumtii Yesu Kristo.
KUFUNULIWA KWA MASIHI - 19:11-21
Lengo
la 6: Elezea wajibu wa Masihi aliyepanda farasi mweupe.
§
Yesu
Kristo ni wakala wa ghadhabu ya Mungu na tumaini la waamini. Yesu anamwaga hukumu juu ya waovu, lakini
wakati huo ni chanzo cha faraja na utukufu kwa watu wake wanaoshuhudia utawala
wa haki. Yesu anakuja mara ya pili
pamoja na watakatifu wake. Anakuja akiwa
mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, Anakuja akiwa jemadari kuanzisha kweli
na haki, kuhukumu mataifa na kufanya vita dhidi ya uovu.
Kuwatawala
kwa fimbo ya chuma – maana yake kuwaangamiza mataifa.
Anakanyaga
shinikizo la mvinyo – maana yake hukumu ya kutisha.
KARAMU YA MUNGU - 19:17-18
Lengo
la 7: Elezea karamu ya Mungu.
§
Hii ina
mahusiano na vita ya Har-Magedonia,
Mungu atawaangamiza watu waovu wengi wakati wa vita hivyo kiasi kwamba
watahitajiwa ndege wala nyama wengi ili kusafisha uwanja wa vita. Hii ni kwa sababu itakuwa vigumu kuzika watu.
HUKUMU YA MPINGA KRISTO NA NABII WA UONGO – 19:19-21
Lengo
la 8: Elezea hukumu ya wanyama wawili waovu.
§
Mpinga
Kristo atakusanya majeshi yake ili apigane na Bwana Yesu na majeshi yake.
§
Majeshi
ya mpinga Kristo yatashindwa vibaya, mpinga Kristo na Nabii wa uongo watatekwa
na kutupwa ziwa la moto.
§
Majeshi
au watu waliopigana wakiongozwa na mpinga Kristo waliuawa.
MASWALI:
1.
Taja
matukio yanayotokea wakati wa vitasa saba
2.
Kuanguka
kwa Babeli kuna maanisha nini?
3.
Nani
watakuwepo katika karamu ya Harusi ya Mwana kondoo?
4.
Nini
hatma ya mwisho ya mpinga Kristo na nabii wa uongo?
UFALME WA KRISTO WA MIAKA ELFU NA ULIMWENGU UJAO:
MIAKA ELFU:
KUFUNGWA KWA SHETANI – 20:1-3
Lengo
la 1: Orodhesha mojawapo ya hali ya
kiroho itakayokuwepo wakati Wa miaka elfu. Kwa nini kutakuwa na mafanikio?
§
Mojawapo
ya hali ya kiroho ambayo itakuwepo wakati wa utawala wa miaka elfu ni ya
kutokuwepo kwa udanganyifu hapa duniani.
Hii ni kutokana na kufungwa kwa shetani huko kuzimu kwa kipindi chote
cha miaka elfu.
UFUFUO WA KWANZA – 20:4-6
Lengo
la 2: Taja watakaohusika katika ufufuo
wa kwanza.
§
Kwanza
kuna watakatifu watakaofufuliwa kabla ya dhiki kuu. Pili ni kundi la waamini
watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu ili kutawala pamoja na Kristo. Hawa ndio walioteswa na kuuawa wakati wa
dhiki kuu. Watashiriki katika kutawala
pamoja na Kristo.
MAONI MBALI MBALI KUHUSIANA NA MILLENIA:
Lengo
la 3: Eleza maana ya Millenia na kueleza maoni mbali mbali.
Neno
Millenia linatokana na lugha ya Kilatini likiwa na maana ya miaka 1,000. Sasa
kuna maoni mbali mbali kuhusiana na millennia, nayo ni:-
- Post Millenialism - Yesu atakuja wakati ulimwengu umejiandaa Kumpokea
§
Amillenialism - Hakutakuwa ufalme wa miaka elfu wakati wa
kurudi kwa Yesu mara ya pili.
§
Premillenialism - Ulimwengu utakabiliwa na utawala wa
Masihi- Yesu wa kipindi cha miaka elfu wakati Yesu atakaporudi mara ya pili (Ufu.20) unasema kurudi kwa
Yesu mara ya pili kutafuatiwa na kufungwa
kwa shetani kuzimu na ufufuo wa wenye
haki ambao watatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu.
HALI KATIKA UTAWALA WA MIAKA
ELFU:
Lengo
la 4: Eleza hali na maisha yatakayokuwepo wakati wa millennia.Mambo haya
yatakuwepo katika kipindi hiki:-
Mwana simba atakaa pamoja na mwana kondoo kwa amani wakati wa utawala wa Yesu
Kristo Duniani.
§
Amani
duniani pote hapatakuwepo na vita wala jujifunza vita (Zab. 46:9; Isa. 2:4;
9:6-7; Mika 4:3-4)
§
Maendeleo
makubwa ya kiuchumi – (Isa. 65:21-24; Amo.9:13-15; Mika 4:4-5)
§
Haki
itatawala (Isa. 11:13-15; Yer. 23:5)
§
Watu
wote watamjua Bwana (Isa.11:9; Habak.2:14; Zek.8:21-23)
§
Wanyama
waondolewa ukali, watakula majani (Isa. 11:6-9; 65:25)
§
Nchi
itarudishwa hali yake ya kwanza na kuzaa sana (Isa. 35:1,2; Amo. 9:13-15;
Eze.36:8-12)
§
Maisha
marefu (Isa.65:20-22)
§
Mabadiliko
ya dunia ya kupokea mwanga wa jua na Mwezi (Isa.30:26)
Lengo
la 5: Taja wakazi wa ufalme wa miaka
elfu.
§
Kutakuwa
na aina mbili ya watu: Kwanza watakatifu waliokuja na Yesu ambao watatawala
pamoja na Kristo. Pili, ni watu wenye
miili hii ya kawaida ambao walikuwa waaminifu wakati wa dhiki kuu na wale
watakaozaliwa wakati wa miaka elfu . (Mt. 25).
BAADA YA MIAKA ELFU.
UASI
WA MWISHO WA SHETANI - Ufu. 20:7-10
Lengo
la 6: Eleza sababu za shetani
kufunguliwa na matokeo yake.
§
Shetani
atafunguliwa kutoka gerezani baada ya miaka elfu ili awajaribu watu waliozaliwa
wakati wa millennia. Hii itawkuwa nafasi
yao ya kuchagua kumtii mungu au shetani.
Watu wengi watamfuata shetani na kuizingira kambi ya watakatifu. Kabla ya kuishambulia kambi, moto utashuka
kutoka mbinguni na kuwangamiza. Shetani atatupwa katika ziwa la moto.
HUKUMU YA MWISHO MBELE YA KITI CHEUPE- 20:11-15
Lengo
la 7: Eleza kweli kuhusiana na hukumu ya
mwisho.
Katika
wakati huu watu wote waovu watafufuliwa na kusimama mbele ya kiti cheupe ili
kuhukumiwa.
- Mtu asiyeandikwa jina katika kitabu cha Uzima atahukumiwa.
- Wote waliomkataa Yesu na wokovu wake watatupa katika ziwa la moto wa milele
- Mauti na kuzimu zilitupwa katika ziwa la moto.
Jehanam
ni moto mkali usiozimika kamwe, tanuru la moto ambako watu watasaga meno na
kuomboleza. Pia hii ndio mauti ya pili
(Mt. 22:13; 25:30; 13:42,50; Mk. 9:43)
MPANGO MPYA - Ufu. 21-22
1.
MBINGU
MPYA NA NCHI MPYA – Ufu. 21.
Lengo
la 8: Eleza maana hasa ya mbingu mpya na nchi mpya.
§
Kulingana
na somo hili ina maana ya kuwa mbingu na nchi ya sasa zitaondolewa. Baada ya kuja mbingu mpya na nchi mpya (Isa.
51:6; 2Pet.3:7,10-12). Nchi ya sasa
inaondolewa kwa sababu imechakazwa na kunajisiwa na dhambi. Nchi mpya haina bahari.
2.
YERUSALEMU MPYA – 21:2-22:5
Lengo
la 9: Eleza jinsi mji ulivyo:
- Mji huu unaitwa ni Bibi Harusi kwa sababu Mungu atakaa pamoja na watu wake.
- Mji una milango 12 ambayo inawakilisha taifa la Israeli. Pia una misingi 12 ambayo inawakilisha kanisa. Hii ni kuonyesha umoja wa watakatifu wa A/Kale na A/Jipya.
- Mji ni mraba wenye mapana, marefu na wimo sawa wa maili 1,500. Ukionyesha kuwa utakuwa na makao ya kutosha ya watakatifu wote wa vizazi vyote. Pia mji unajawa na utukufu na utakatifu wa Mungu.
- Mji hauna hekalu kwa sababu Mungu na Mwanakondoo ndio hekalu lake.
- Hakuna usiku katika mji huo
- Barabara zake ni za dhahabu.
- Kulingana na Wanatheolojia, mji huu utakaliwa na watakatifu wote kabla ya dhiki kuu.- yaani walionyakuliwa kabla ya dhiki kuu na wale watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu.
- Nchi mpya itakaliwa na watu wote ambao waliishi katika ufalme wa miaka elfu na walimkataa ibilisi na ushawishi wote. Inasemekana watakuwa mataifa wanaongozwa na wafalme. Wafalme hao wataenda Yerusalemu kumtukuza Mungu kwa yale anayofanya katika nchi mpya (Ufu. 21:24-26)
- Wakazi wa mji wa Yerusalemu ni washindi waliovumilia taabu na adha mbali mbali
- Hawa hawataingia katika nchi hiyo:
- Waoga ambao wanaogopa kumkiri na kumfuata Yesu Kristo Aliye hai (Mk. 8:35; 1Thess. 2:4)
- Wasioamini – hawa ni pamoja na wakristo ambao wameanguka dhambini.
- Waamini wote wanaosema wanamfuata Yesu, lakini wanaishi katika dhambi (1Kor. 6:9,10; Efe. 5:5-7; Gal. 5:19-21)
- Hawa wote watatupwa katika ziwa la moto
- Watakatifu watamwona uso wake – hili ndilo lengo la historia ya ukombozi. Watamwona Yesu Mwanakondoo kwani wataishi naye. (Mt. 5:8; 1Yh. 3:2)
- Mti wa Uzima ambao ni halisi unaonyesha mfano wa Roho Mtakatifu na Uzima, baraka na nguvu za kiroho zitokazo kwa Mungu. (Isa. 44:3; Yn. 7:37-39).
HITIMISHO - 22:6-21
Lengo
la 10: Eleza mambo muhimu yaliyomo
katika Hitimisho;
1.
Anathibitisha
kuwa unabii huu ni wa kweli kwa sababu
umetolewa na Bwana wa roho za Manabii ambaye aliwaongoza Manabii kunena
2.
Yesu
anasema anakuja upesi na amebarikiwa yule atakayezingatia Unabii huu.
3.
Kila
mtu atapokea kulingana alivyotenda hapa duniani.
4.
Baraka
ni kwa wale wanaoshika amri zake ambao watapewa haki ya kuuendea mti wa uzima
na kuingia mji wa Yerusalemu mpya.
5.
Watu
waovu wanaosema uongo na wauaji watatupwa katika ziwa la moto wa milele
6.
Roho
Mtakatifu na Bibi Harusi (Kanisa) wanafanya kazi ya kuwaalika watu kupokea Neno
la wokovu.
7.
Kuna
hukumu juu ya watu ambao wanachagua sehemu Fulani na kuziacha zingine katika
unabii huu. Hivyo hivyo kwa wale
wanaongezea mawazo yao juu ya Neno.
8.
Yohana
anaitikia kuwa uje Bwana hii inamaanisha:
(a)
Wakristo
wa kweli wanaomba na wanahamu ya kurudi kwa Bwana kwani ndipo ukombozi wetu
utakamilika.
(b)
Siku ya
kurudi Yesu imekaribia ambapo atarudi katika utukufu wake.Je, mpendwa uko
tayari kunyakuliwa?
MASWALI:
1.
Taja
matukio mbali mbali yatakayotokea kabla ya Yesu Kristo kutawala?
2.
Eleza
maana ya millennia kuhusiana na maoni ya:
(a)
Post
millennialism _______________________
(b)
Amillennialism
__________________________
(c)
Premillennialism
________________________
3.
Mambo
gani yatakuwepo wakati wa utawala wa Kristo wa miaka elfu moja?
4.
Jehanam
ni nini?
5.
Eleza
kwa kifupi kuhusiana na mbingu mpya na nchi mpya.
Barikiwa sana mtumishi wa Mungu.
JibuFutasijaelewa kuhusu siku ya Bwana nahitaji ufafanuzi
JibuFutanahitaji ufafanuzi wa vitabu vingine zaidi
JibuFutaTo g
JibuFutaShalom mtumishi kwanza mimi na shukuru saaaana kwakazi kubwa na mda wako ambao umeutumia ili nasisi tunufaike kwa ikikitabu nilikuwa nimesha angaika saana namna yakufahamu ichi kitabu kupita pita kwangu kwenye mitandao njo roho moja ikinielezeya suulize kwanza kwenye google oluone kama utapata unacho tafuta mimi kuuliza tu nikaona kitabu kizima na tafsiri yote kwaujumla inajitokeza nakushukuru sana tena sana Mungu wangu akunariki mimi napatikana congo uvira naitwa baraka elisha ila ningependa kufahamu mengi kupitia vitabu vingine
JibuFutaWhatsapp namba zangu izi +2438130
O5825