Jumatatu, 29 Februari 2016

Dada akaagiza tena Bwana!


Napenda watu wengine wajifunze kutokaa na uzoefu wangu na ndio maana naelezea kisa hiki najua wale wanaonifahamu watajua kwamba ni mimi, naomba hawa wachukulie kuwa nasimulia ili wengine wajifunze siyo kwa sababu nyingine, Mwaka 1996 nilikuwa nafanya kazi katika duka la vipuri vya magari lililokuwa eneo la msimbazi jijini Dar es Salaam, ukweli ni kwamba nilikuwa natengeneza pesa sana kwenye duka hili  zilikuwa ni fedha za wizi, labda ndio maana duka lenyewe halikudumu kwani lilifungwa mwaka 1996.

  
Nilikodolewa Mijimachi kila kona ya bar na Disco kwa kujifanya ninano kumbe ulofa tu!


Kwa hiyo baada ya duka kufungwa nikawa sina kazi, kwa sababu nilikuwa mtu wa matumizi sana, sikutaka kujishughulisha ghafla nilitaka kulinda hadhi na heshima yangu, kwa hiyo niliendelea na matanuzi yangu  nakumbuka ilikuwa juni 1997  yaliponikuta maswaiba haya 

Siku hiyo nilikwenda kwenye ukumbi mmoja maarufu wakati ule hapa Dar nasema wakati ule kwa sababu ndio ulikuwa unafunguliwa, nilikwenda pale kwa kupewa ofa ya kuingia ukumbini na rafiki yangu mmoja , aliniambia atanikatia tiketi  halafu maswala ya vinywaji ningejua mwenyewe, Nilikubali. Ni kweli baada ya kuingia ukumbini akamchukua bibi yake wakaenda kukaa kivyao, nilikuwa na shilingi 1000 mfukoni ambapo ningeweza kunywa bia kama mbili kwa wakati ule kwenye ukumbi kama ule, wakati naanza kunywa  bia niliyokuwa nimeagiza akaja msichana mmoja  ambaye awali sikuwa nimemtabua, baada ya kunisalimu kwa kunitaja nilimtambua  alikuwa ni msichana ambaye wakati nawika kwa fedha  niliwahi kufanya naye mapenzi, kwa bahati mbaya alisafiri kwenda Mauritius kwa kaka yake, haki ya Mungu leo nataka nikunywe hadi ukimbie nina hamu na pombe yako na mwili wako alisema, kabla sijajibu alimwita muhudumu  na kuagiza pombe kali nilijua kuwa ile oda moja tu ilihitaji 1000, nilijichangamsha na kujifaragua  lakini moyo wangu ulikwenda mbio nikianza kufikiria deni  la hiyo pombe nikiwa nafikiri aliagiza nyama choma, mazungumzo yalikuwa makali sana, huku binti Yule akinisanifu kwamba ninazo, nilijisikia vibaya ila sikuweza kusema, kufika saa sita usiku alikuwa amekunywa na kula kiasi cha shilingi 9000 mfukoni nilikuwa na 1000, bili ililetwa nilijua sina hela lakini ajabu sikusema hivyo, nilitulia huku nikitafakari, ingawa akili haikufanya kazi, baadaye kidogo  muhudumu alirudi kuchukua malipo. Alikuta sahani ya kuwekea hela iko tupu, aliondoka baadaye kidogo alirudi tena na kukuta sahani iko tupu haina kitu.

Aliuliza kwa upole ni nani anatakiwa kulipa , naomba malipo kwani namaliza shifti nilimwambia Yule mwanamke mwambie anayekupokea aje  nitamlipa yeye, Yule muhudumu alisema inanibidi nikamilishe hesabu ndipo niondoke, nilinyamaza halafu Yule msichana alianza kupayuka, alianza kunitukana na kunisimanga kwamba najifanya nina kitu wakati nimechoka, alinitukana hadi matusi ya nguoni, ilibidi watu waache burudani zao watupe macho na masikio kule kwetu na wengine walifika kabisa pale kwenye vurugu akiwemo na meneja wa ukumbi, kama unavyojua tena mitanzania kwa umbeya!

Nitalipa mimi achaneni na huyu bwege aende zake Pamoja na kuwa alikuwa amelewa nilijua alikuwa ananikomoa, nilitoka nje ya ukumbi kama aliyenyeshewa Nilikuja kugundua kuwa ile ilikuwa ni njama ya yule rafiki yangu aliyenipa ofa kunikomesha kujifanya bado nina pesa wakati nawapa shida wengine, ingawa haikuwa njia ya kiungwana kunifundisha lakini nashukuru kwani tangu wakati ule hadi leo maisha yangu sio ya kujionyesha bali naishi kama mimi. Cheki ulivyokodoa mimacho ishi kama Mungu alivyokujalia acha kujiinua!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni