Yako madai ya baadhi ya wanaharakati wa kiislamu
wanaodai kuwa Eti bwana Yesu alikuwa Muislamu kwa madai kuwa alikuwa akiingia
katika Masinagogi (yaani misikiti ya wayahudi) Luka 4;16,Pia kwa sababu alikuwa anaomba akiwa anasujudia (Mathayo 26;38-44) Maandiko haya kwa
waislamu ndio kigezo kikuu cha kuwa Yesu ni mwislamu.Madai haya ni ya ajabu
sana kwani yanapingana na ile kweli iliyomo katika quran na Khadithi za
Kiislamu Kulazimisha kuwa Yesu alikuwa muislamu kunaanza kutufanya tukubali
kuwa Qurani ni kweli kuwa si kitabu kinachoongoza katika kweli kwani ni Qurani
yenyewe ndiyo inayosema kuwa Muhamad aliamuriwa awe wa kwanza miongoni mwa
waliosilimu soma (Surat al-anaam 6;14)……. “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu……”
ayah ii inathibitisha wazi kuwa Muislamu wa kwanza katika wanaume aliyesilimu
alikuwa Muhamadi mwenyewe, aidha katika
kitabu cha cha historia ya Maisha ya nabii muhamad uk 18 kifungu cha
pili cha shekh Abdulla Saleh Farsy kinasema ….Basi Mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke akimaanishwa bi khadija
unaona sasa linakuwa jambo la kushangaza kuona wana mujahidini wakipingana na
maulamaa wao au wanazuoni wenzao au hata quran aidha wanaharakati hawa wa
kiislamu kumbe wanataka kutuambia kuwa wayahudi nao ni waislamu? Na kama hivyo
ndivyo je quran inafundisha nini kuhusu wayahudi? Soma Surat al
maida-5;51 inasema hivi….. “Enyi
mlioamini msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa rafiki zenu (wa kuwapa siri
zenu) wao kwa wao ni marafiki.Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki nao basi
huyo atakuwa pamoja nao na hakika allah hawaongozi watu madhalimu….” Qurani
inaonyesha kuwa Hakuna uhusiano wa waislamu na wayahudi wala wakristo Yesu
alikuwa Myahudi na hivyo kuingia katika msikiti wa wayahudi ilikuwa ni desturi
yao. Je muhindu akiingia kwenye msikiti wa wahindu ni mwislamu kwa sababu hiyo?
Musa na Harun pia hawakuwa waislamu wala hawakuanzisha Dini
Tukumbuke kuwa Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea hivyo ilikuwa ni
lazima aingie kwenye majengo ya watu waliopotea ili apate kuwafundisha Luka 4;17-30, hata hivyo mara nyingi
watu hao wa kenye masinagogi walijaa ghadhabu na walimtoa nje ya mji
wakimpeleka katika ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa wapate kumtupa
chini.Luka 19;45-47 Yesu aliingia
katika Hekaluni akaanza kuwatoa nje wale waliokuwa wakifanya biashara
akawaambia imeandikwa nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala lakini ninyi
mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi naye akawa akifundisha kila siku hekaluni
je alikuwa dini gani? Aidha ikumbukwe
pia kuwa Paulo mtume pia aliingia katika masinagogi hayo Matendo 17;1-2 na pia ilikuwa ni desturi yake je wanaharakati wa
kiislamu wanataka kutuambia kuwa Paulo naye pia alikuwa mwislamu? Kwa kuwa tu
aliingia katika sinagogi? Mbona huwa hawadai kuwa Paulo mtume ni mwislamu?
Aidha ni Muhimu kukumbuka kuwa mafundisho ya bwana Yesu yalikuwa yakipingana
vikali na watu wa Masinagogi Yesu alikemea tabia zao za kupiga panda watoapo
sadaka yaani walikuwa wanafiki Mathayo
6;2.,aliwakemea kwa kupenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na
katika pande za njia ili waonekane na watu hii nayo ilikuwa tabia ya kinafiki (Mathayo 6;5-15) aidha Bwana Yesu
alifundisha kusali kwa kupitia sala ya bwana Baba yetu uliye mbinguni………. Jambo ambalo waislamu hawalifuati
kabisa,Mwishoni watu wa masinagogi walimfukuza Yesu kabisa wakiwa wamejaa ghadhabu
ikiwa Yesu alikuwa mwislamu mwenzao iweje walimfukuza? Quran inasema Wanafiki wamejenga msikiti wa kuleta udhia na
kutia nguvu ukafiri……… Hivyo aya hii inathibitisha kwamba misikiti ni ya watu
wanafiki,Pia quran inayataja Masinagogi
kuwa ni nyumba tofauti na Misikiti ona Surat
al-hajj 22;40 Ambao wametolewa majumba (mjini)mwao pasipo haki ila kwa
sababu wanasema mola wetu ni mwenyezi
mungu na kama mwenyezi Mungu asingali wakinga watu baadhi yao kwa wengine bila
shaka yangalivunjwa MAHEKALU (Swaamiu) na MAKANISA (Wabiya-unw) na nyumba
nyingine za ibada MASINAGOGI (Wasalawatunw) na MISIKITI (Masaajidu) ambamo jina
la mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi…….. jambo linalo shangaza ni kuwa Qurani
inataja masinagogi tofauti na misikiti kulikoni basi kama sinagogi ni msikiti?
Biblia
haitufundishi kuwa Yesu alikuwa Mwislamu inatuambia Yesu ni mwana wa Mungu soma
(Mathayo 3;16-17,Yohana 17;1,8;54,)aidha
Tunafundishwa kuwa Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa katika Mathayo 16;18 anasema “Nitalijenga
kanisa langu wala milango ya kuzimu
haitalishinda”Yesu aliyasema hayo kabla Muhamad hajazaliwa wala uislamu
haujaanza aidha ufunuo wa Yohana sura ya pili yoote Yesu anazungumza na kanisa na anatofautisha
na sinagogi. Hivyo Kanisa limeanzishwa na Bwana. Maadui wakubwa wa waislamu ni
mayahudi Surat al maida 5;82 na Yesu
alikuwa myahudi leo Mujahidina wanasemaje Yesu alikuwa Mwislamu? Na Quran
inasema maadui zao ni wayahudi na biblia inasema Yesu alikuwa Myahudi soma (Yohana 4;9).
Unaona una matongotongo
JibuFutaMuhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.
JibuFutaMuhammad aliposema kuwa ni wa kwanza alikua nakusudia wa kwanza kwa umma wake na sio wa kwanza kwa umma zote usikurupuke.
JibuFutaUnaona una matongotongo
JibuFutawe kafir muhammad ndio wa kwanza kusilim. hiyo haya kwamba ndionwa kwanza kwa uma mbona hujatoa.
JibuFutaacha ujinga. elimu hiyo fundisha msikitini maana ndiko utaposema uongo ili mjifurahishe.
ukija huku sema ukweli tunataka andiko kama sisi tulivyotoa. na kwanza hata muhammad mwenyeww hakusilim maana hakuna haya aliyokubali.
ndio maana wa kwanza kusilim akawa bi adija. muislam wa kwanza duniani sasa wewe leta mdomo badala ya andiko. mti mzima kutumia hisia badala ya akili ni hatari
mambo ni mengi muhimu ni kuacha dhambi.
JibuFutaAcha ujinga ww mkiristo Soma vizuri fatilia Mambo kwaundani
JibuFutaUkifatilia vitabu kwa kuvisoma vizuri uislam utaachana nao literally,..maana utagundua uislamu umejaa uongo mtupu.
JibuFutaMimi sio msomi nataka kuelewa nikiulizwa yesu nimungu au Mwana Wa mungu nijibu nini ?
Futa