Waislamu wanaamini kuwa muhamad ndiye Nabii
yule.
Hoja hii
hiliigusia katika kipengele muhimu cha umuhimu wa kukabiliana na changamoto za
uislamu,Kwa mujibu wa waislamu nabii muhamad
alitabiriwa katika biblia kuwa yeye ndiye nabii yule hii inatokana na
swali ambalo Yohana aliulizwa na watu
waliotumwa na mafarisayo,swali hili lina maeneo makuu matatu ambayo ndiyo
yanayoundiwa hoja soma (Yohana 1;12-25).Maswali
hayo yaliuliza habari za Kristo,Eliya,na Nabii yule,hoja huundwa katika eneo la
Tatu la nabii yule ambapo hapo ndipo hudai kuwa nabii yule ni Muhamad ambaye
Yesu mwenyewe alimtabiri katika (Yohana
14;26), kama “ paraklete” kwa
kiyunani yaani aliyetukuzwa au Ahmad sawa na muhamad tutajadili hilo huko mbele,Nabii
huyu hudaiwa ndiye aliyetabiriwa katika (kumbukumbu
la torati 18;15,18),nabii huyu
angetoka miongoni mwa ndugu za wayahudi ambao ni waarabu,Mwandishi wa
kitabu kiitwacho uislamu katika
Biblia Ngariba Musa Fundi na Kawemba
Mohamed Ali waliamua kujichangamsha katika ukurasa wa 13 wa kitabu hicho
wakitoa madai kama hayo kwa kuthibitisha kuwa nabii huyo atakuwa kama Musa
hivyo walionyesha jinsi Musa anavyofanana na Muhamad kuliko Masihi
Musa alizaliwa akiwa na
Baba na mama sawa na Muhamad sivyo ilivyo kwa Yesu.
Musa alioa na kuzaa watoto
sawa na Muhamad Yesu hakuoa wala kuzaa.
Musa alikubalika kwa watu
na Muhamad, Yesu alikataliwa.
Musa alikuwa nabii na
kiongozi wa kisiasa kama Muhamad Yesu alikataa siasa (kufanywa mfalme).
Musa alitoa sheria na Muhamad
pia Yesu alileta neema na kweli.
Warithi wao waliiteka
kanaani,warithi wa Yesu walihubiri tu.
Musa alikufa na Muhamad na
walizikwa,Yesu alipaa mbinguni.
Hivyo nabii kama Musa kwa vyovyote ni Muhamad na si
Yesu na hivyo Biblia imemtabiri,Tunaweza kuuweka mpango huu katika jedwali kama
ifuatavyo.
Musa
|
Muhamad
|
Yesu masihi
|
Alikuwa na wazazi wote
|
Alikuwa na wazazi wote
|
Hakuwa na baba ila mama tu
|
Alioa na kuzaa watoto
|
Alioa na kuzaa watoto
|
Hakuoa wala kuzaa
|
Alikuwa nabii na kiongozi wa kisiasa
|
Alikuwa nabii na kiongozi wa kisiasa
|
Nabii lakini si kiongozi wa kisiasa
|
Alitoa sheria Torati
|
Alitoa sheria Quran
|
Alileta neema injili
|
Warithi waliiteka kanaani
|
Warithi waliiteka palestina
|
Warithi walihubiri tu
|
Alikufa na kuzikwa
|
Alikufa na kuzikwa
|
Alipaa kwenda Mbinguni
|
Namna ya
kutatua Tatizo hili.
Tukianzia na
swala la Muhamad kuwa ndiye nabii Yule kama inavyodaiwa kusemwa na Yohana
katika (Yohana 1;12-26).Ni kweli
kuwa kuna maswali matatu yanaulizwa katika mazingira ya andiko hili,Nataka
kuwakumbusha waislamu tena katika eneo hili kuwa Biblia haitafasiriwi kama
quran ambayo hujitegemea kwa kila aya,Biblia ni kitabu cha wanazuoni ni kitabu
cha wasomi huwezi kuchukua andiko na kulifasiri kama utakavyo tu , Katika moja
ya kanuni za kutafasiri biblia ambazo kwa faida ya wengi nitaziweka kwa
mukhtasari katika somo hili huko mwishoni,Kanuni inayopaswa kutumika hapa ni
kanuni ya mazingira ya kihistoria na kanuni ya kufasiri unabii, kanuni ya
mazingira ya kihistoria “Principle of
historical context” inasema ili
mtu afasiri Biblia kwa ufasaha anapaswa kujua historia ya andiko au maandiko
ili kupata maana halisi ya kile kinachozungumzwa hivyo kihistoria tujiulize ni
kwanini wayahudi waliuliza maswali yale matatu?
Kihistoria
Wayahudi walimtofautisha Nabii yule (anayetajwa katika Kumbukumbu 18;15-18) na Masihi ambaye ni mwana waDaudi(Mathayo 22;41-46), wao walifikiri nabii Yule na masihi ni watu wawili
tofauti,wakati wa Musa nabii ndiye alikuwa kiongozi,walipoanza kuwa na Mfalme Mungu alihaidi kupitia Daudi kuleta
kiongozi wa kifalme hivyo kimsingi nabii zote hizi zilimhusu Yesu Kristo Yeye
ndiye alikuwa nabii mkuu (Luka 7;16b)na
Mfalme wa wafalme(Ufunuo 19;11-16).Waislamu
hawajui historia hii na wanachanganywa zaidi kwa vile Muhamadi alivyojikinai
akitaka kujithibitisha kuwa ni nabii wa
kweli na kuwa naye alitabiriwa alishusha ay
a hii(Al-A-raaf mwinuko 7;157).
Ayah ii inadanganya waislamu na kuwafanya watafute katika kwa nguvu katika
biblia (Torati)na injili wakidhani
wataona unabii unaomhusu Muhamad,ukweli ni kuwa Yesu ndiye mwisho wa unabii na
si zaidi ya hapo kama Muhamad alitabiriwa katika biblia tungelimwamini lakini
bahati mbaya hayumo kabisa (Ebrania1;1-4)
Nabii
miongoni mwa ndugu zako kama Nilivyo mimi, Nabii mfano wako wewe. (kumbukumbu
18;15,18)
Mistari hii
hutumiwa na wanaharakati wa kiislamu
wakifikiri kuwa inamtabiri Muhamad nabii wa Waislamu,kwa bahati mbaya
kama nilivyogusia hapo awali kua Biblia au unabii hautafasiriwi kama apendavyo
mtu Fulani (2.Petro 2;20-21),Waislamu
hapa hufasiri biblia kama wapendavyo wao wenyewe,Hapa kanuni iliyokiukwa ya
kufasiri maandiko ni sheria au kanuni ya
kifungu kizima “The Principle of context”
Unaposoma maandiko ya kibiblia kanuni
hii inataka usome kifungu kizima juu na
chini pia kabla ya kunyofoa aya moja
pekee,hivyo unaposoma aya hizi kwa mfano neno “miongoni mwa Ndugu zenu” hii
haiwahusu waarabu,kifungu kinaonyesha kuwa Mungu alikuwa anazungumza na na kabila ya walawi moja kati ya kabila kumi
na mbili za Israel, hivyo maneno miongoni mwa ndugu zenu, ilihusu zile kabila
kumi na moja nyingine nje ya walawi soma
(Kumbukumbu 18;1-2) mstari wa pili
hapo utakutana na neno hili, Wala wasiwe na urithi kati ya Ndugu zao (miongoni
mwa).Hapa Mungu anawatenga walawi na zile kabila nyingine zinaitwa ndugu zao
lugha kama hii inatumika katika torati (Kumbukumbu
17;14-15) utakutana na Maneno kama haya “….Umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako”
Kwa muundo wa lugha hapo juu je unafikiri Mungu
aliwataka wayahudi wakitaka mfalme waweke mwarabu? Ambao ni ndugu wa wayahudi?
Jibu ni hapana kwani Mungu hapa anazungumza na wayahudi jamii ya walawi.
Jambo
lingine ambalo wasomaji wa Biblia wanapaswa kulitilia maanani ni kuwa manabii
walipozungumza,walizungumza katika namna kuu mbili moja na jamii ya wakati ule
(Forthtell) na jamii ya wakati ujao (Foretell),Hivyo unabii huu katika hali ya
kawaida ulimhusu nabii anayefuata baada Musa ambae alikuwa anakaribia
kufa,nabii aliyemfuata Musa kwa kawaida(Literal) alikuwa ni Yoshua ambae kwa
asili hakuwa mlawi alitokea kabila ya Yuda,hivyo Mungu alipozungumza na walawi
na kusema atainuliwa nabii miongoni mwa ndugu zenu alimaanisha kiongozi nje ya
kabila ya walawi.Hivyo nabii huyu alikuwa Yoshua na kinabii (Foretell)Alikuwa
anatabiriwa Masihi ambaye angetokea kabila ya Yuda.
Kimsingi
nabii Musa anafanana na Yesu Kristo kwa mfano tu kwani Yesu halinganishwi na
mtu,Yeye yuko juu na nibora zaidi ya Musa(Ebrania
3;1-5)
1. Musa alikuwa
Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu (Israel)kama walivyojiombea wenyewe (Kumbukumbu 18;16,Hesabu 14;11-19),aliombea
wakosaji.SasaYesu kristo ndiye
mpatanishi kati ya Myngu na wanadamu kwa ulimwengu mzima (1Timotheo 2;5).
2. Musa alimjua Mungu uso kwa uso;Musa alipataneema ya kuwa na
uhusiano na Mungu wa moja kwa moja tofauti na manabii wengine wote (Kutoka 33;11)Jambo ambalo Quran
imelikubali(An-Nisaa 4;164) na kuwa
inathibitisha ya kuwa hakuna mwanadamu aliyestahili kuongea na Mungu moja kwa
moja (Ash-shuura 42;51),Yesu alimjua Mungu uso kwa uso na alitoka kwake (Yohana 7;29,6;46).Musa alipozungumza na Mungu uso wake uliangaza (kutoka 34;29-30).,Yesu alipozungumza na
Mungu uso na mavazi yake yaliangaza kama jua (Mathayo17;2). Hatusomi popote ambapo nabii wa waislamu alipatwa na
Hali kama hii.
3. Musa
alifanya Ishara na miujiza Mikubwa.
Musa alifanya
miujiza mikubwa sana kwa jina la Mungu kule Misri kulikuwa na ishara kama
kumi,jangwani watu walilishwa kwa mana,na miujiza mingine mingi sana,hakuna
nabii yoyote atakaedai kuwa anafanana na Musa kama hana muujiza hata mmoja
unaofanana na Musa,tunajua kua Muhamad hakuwa na muujiza hata mmoja na ndio
maana wapagani wa kiarabu walimuuliza mbona huna muujiza wowote kama wa Musa ?(Al-qasas
28;48)kama Muhamad ndiye nabii aliyefananishwa na Musa mbona hakuna ishara
hata moja ya kumlinganishia na Musa? (Kmbukumbu
34;10-11).mistari hii inakazia wazi nabii atakayekuja atakavyokua kama
Musa.
4. Yesu pia
alifanya miujiza mikubwa.
Kuna habari
za miujiza mingi sana aliyoifanya Yesu alipokuwa duniani ambayo pia inafanana
na ile ya Musa wote walikuwa na nguvu dhidi ya Bahari (Kutoka 14;21,Marko 4;39) wako mana bii waliokuwa na nguvu dhidi ya
maji ya mito kama Eliye na Elisha (Yoshua
3;13,2Falme 2;14),lakini hakuna
hata mmoja aliyekuwa na nguvu dhidi ya bahari,Yesu alitembea juu ya bahari ya
galilaya na zaidi ya yoote upepo na bahari vilimtii jambo lililopelekea watu
kumuogopa sana (Mathayo 8;27).Musa
alilisha watu kwa mikate maarufu kama mana iliyonyesha kila siku juu ya
nchi,Yesu alipofanya muujiza wa kulisha watu mikate (wanaume zaidi ya 500) bila
kuhesabu wanawake na watoto woote walihisi na kuelewa wazi kuwa huyu bila shaka
ndiye nabii yule ajae ulimwenguni (Yohana
6;14) angalia mstari huu kwa makini “..
Hakika huyu ni nabii yule ajaye
ulimwenguni.”muujiza huu alioufanya ulibainisha kuwa yeye ndiye yule
aliyetabiriwa na Musa (Torati 18,15,18)
kwa msingi huu Kristo anatimiza sifa zinazo tajwa katika (Torati 34;10-11)Mitume wa Kristo walielewa wazi kuwa unabii huu ulimhusu masihi na katika mahubiri
yao mara kwa mara walinukuu mistari ile
ona (Matendo 3;22) na Stefano pia
alinukuu katika (Matendo 7;37),Pia
ni muhimu kufahamu kama Yesu alikataliwa Musa pia alikataliwa (Matendo7;27).
Jinsi maisha
ya Musa yanavyofanana na maisha ya Kristo.
Musa
|
Yesu
|
Mtoto wa kifalme kwa farao
|
Mfalme wa wafalme mbinguni
|
Mrithi wa farao
|
Mrithi wa Mungu
|
Aliishi kama mtu maalumu ikulu
|
Alikuwa
na enzi na utukufu mbinguni
|
Aliishi kama mtu dini jangwani
|
Aliishi kama mtu duni duniani
|
Mchungaji wa kondoo jangwani
|
Mchungaji
mwema wa watu woote
|
Alijinyenyekeza na kuwa mpole
|
Mnyenyekevu
na mpole
|
Alipata mateso na kuwa mbali na ndugu
|
Aliteseka
Msalabani na akiwa peke yake
|
Ni mjumbe wa agano la kale
|
Ni mjumbe wa agano la kale
|
Mpatanishi wa Israel
|
Mpatanishi
wa ulimwengu mzima
|
Aklitoa sheria
|
Alileta
Neema na kweli na uzima
|
Alifanya miujiza mingi mikubwa
|
Alifanya
miujiza mikubwa ya kushangaza
|
Alimjua Mungu uso kwa uso
|
Alikuwa
Mungu na alitoka kwa Mungu
|
Kiongozi wa Israel
|
Ni
kiongozi wa kanisa
|
Ni muhimu kufahamu
kuwa Muhamad hakutabiriwa kabisa katika torati na manabii na injili kwa kweli
kama angetabiriwa tungemwamini,sisi tunaamini maandiko sana tusingeweza
kukanusha kile ambacho tunakijua lakini hatuwezi kushuhudia uongo labda muhamad
mwenyewe angelikuwepo angetusaidia kujua kuwa ametokea wapi bahati mbaya hayuko
hai lakini Kristo yu hai leo kaburi lake liko wazi,yeye ni wa kutumainiwa na
anastahili kuabudiwa ni vema kumtukuza yule ambaye Mungu amemtukuza,Yeye ni
alfa na omega hatuoni mwingine zaidi yake.
Niwaase tu
wanaharakati wa kiislamu waachane na tabia ya kupenda kuyasingizia maandiko kwa
kutafuta kama yana mtaja muhamad ukweli ni kuwa Muhamad hayumo katika maandiko
yoyote yaani Torati,manabii na injili,yeye yumo katika Quran na khadithi tu
hatujui atokako.
Je Muhamad
ndiye Msaidizi mwingine? (Yohana 14;26).
Katika swala zima la kutafuta visingizio kuwa Muhamad
alitabiriwa katika Biblia waislam hudai kuwa Yesu alizungumza au kutabiri
habari za kuwaletea msaidizi mwingine (Mfariji)
mwingine ambaye wao hudai ni Muhamad na quran inathibitisha upotofu huo!
Madai haya
ya waislamu kuwa Muhamad ametabiriwa katika Biblia yanatokana na ahadi ya Yesu
kwa wanafunzi wake ambayo ahadi ambayo imekaririwa mara nne katika injili ya
Yohana,kuwa baada yake atakuja mwingine atakayetumwa kutoka kwa Mungu,jina lake ni mfariji(mshauri
/msaidizi) na wanadai huyo ni Muhamad nabii wao jambo
ambalo liko wazi hata kwa wakristo wa kawaida kuwa anayezungumzwa hapo ni roho
mtakatifu! Hii inatokana na waislamu kudanganyika kupitia aya katika (An- nisaa 4;157)aya hii hudai kuwa nabii wao ametabiriwa ndani ya
Torati na Injili,hebu tusome vizuri (Yohana
14;26) unasema hivi
- “….Lakini atakapokuja huyo msaidizi,huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia”
- Soma pia Aya zifuatazo (Yohana 16;7,14;16,15;26).
Waislamu
hutumia aya hizo na kuzitumia kumthibitisha Muhamad kwa madai kuwa yeye ndiye
aliuongoza ulimwengu katika kweli na kwa sababu ya matumizi ya maneno nafsi
“Yeye huyo”nk.wanahoji kuwa semi hizi zinamhusu mtu na sio Mungu,pia haimuhusu
Roho mtakatifu kwa sababu kwa sababu
yeye amekuwepo tu wakati woote na hata Daudi aliomba kuwa asiondolewe huyo (zaburi 51;11) na Yohana alijazwa tangu
utoto akiwa tumboni,(luka 1;15).
Jibu la
maswala haya ni rahisi sana ningependa kuwarudisha tena wahubiri wa kiislam
kuwa biblia haisomwi kama Quran au gazeti au kitabu kingine hii (biblia ina
kanuni zake kwanza wasome kifungu kizima (Principle
of context),Pia wazingatie kanuni ya kulinganisha (Principle of Hermonization),Hii
ni kanuni ya ushahidi wa andiko zaidi ya mawili,maandiko yote yaonyesha wazi
kuwa Yesu alikuwa ana mzungumzia Roho mtakatifu,yako mambo ambayo yanabainisha
wazi kuwa maandiko hayo hayamhusu Muhamadi ambaye alikuja karne sita baada ya
Kristo angalia vizuri habari za Roho matakatifu,Roho mtakatifu atakaa nasi hata
milele(Yohana 14;16 ).Muhamad
alikufa hayuko nasi milele,Roho mtakatifu hatatambuliwa na watu wa dunia
hii,wala kupokelewa anakaa ndani yetu (Yohana
14;17)Atatumwa kwa jina la Yesu na kutukumbusha au kutufundisha mambo ya
Kristo (Yohana 14;26).Roho mtakatifu
atamtukuza Yesu,atanena atakayoyasikia kwa Yesu,(Yohana 16;13-15).Tunasikitika kuwa Muhamad alijitikuza mwenyewe
wala hakunena yale aliyoyanena Yesu,Bali yakwake mwenyewe. Hivyo Muhamad sio
Msaidizi mwingine,kwani hakai nasi milele na Yuko kaburini amekufa Roho yuko
milele,Jana leo na milele.
Aidha wana
harakati wa Kiislamu Katika kutafuta kutetea hoja hii walikwenda kutafuta neno
wanalofikiri kwa asili linamhusu Muhamad neno hili
la asili la kiyunani ni neno “Paracklutos”
ambalo maana yake ni “Praise one”
ambalo kwa kiarabu ni Muhamad.Hata hivyo kwa asili neno hilo wamelikosea neno
linalotumiwa katika Biblia ya kiyunani ni “Paracletos”
ambalo maana yake ni Mfariji,Mshauri,au
Msaidizi ambalo hutumika kwa Roho mtakatifu na si kwa Muhamad,hivyo mkristo
uwe macho na maneno hayo yanapotumiwa na waislamu kwa lengo la upotoshaji Mungu
atupe neeema ya kuugundua uongo wao na kudumu katika kweli katika jina la Yesu.
Hiyo comparison ya yesu na Musa hazifanani kabisa jaribu kusoma upya
JibuFutaAMINA AMINA AMINA
JibuFuta