Alhamisi, 4 Februari 2016

MFULULIZO WA MIJADALA KWANINI WANATOKA NJE YA NDOA 2



Kwanini wanaume sio waaminifu?. 
Kwa nini wanaume sio waaminifu? Amini usiamini sio tu katika tendo la ndoa,katika swala la kudanganya wanaume zaidi ya nusu, wanakiri kutokuwa waaminifu katika ndoa zao kwa vile wanahisi wamezarauliwa na wake zao, ni asilimia 7% tu wanaweza kufanya tendo hilo nji pasipo kutamani, kwa hiyo unaweza kuona kuwa tatizo la wanaume kutoka nje ya ndoa ni kubwa zaidi kuliko la wanawake lakini ni kwa nini ni vema tukapata sababu za kina ili tujue ni namna gani tatizo hili laweza kushughulikiwa

 vyombo vya mawasiliano kama simu vimeongeza maumivu katika mahusiano
1. Hawasikii msimsimko tena kwa wake zao
Baada ya ndoa na muda kupita kunatokea uzoefu wa nania ataanzia wapi na ataishia wapi, ukweli ni kuwa msisimko unaisha na inabaki kuwa hali ya kawaida, kila mmoja angependa kuhisi uhai wa mweziwake katika tendo, lazima ionekane kuwa kila mtu analitaka na kulifurahia katika mazingira ya Afrika wanawake walijifunza kuficha hisia zao kuhusu tendo la ndoa hawana njia mbadala, hawajitumi, hawaonekani kusisimuliwa na tendo hili, mazoea yanatoea na hali inapokuwa namna hii, mwanaume kwa kukusudia au kwa kuto kukusudia moyo unajiandika kuwa anahitaji kutafuta aina nyingine ya msisimko nje ya kile alichozoea kupata kwa mazoea katika hali hii wanawake wanashauriwa kulishabikia tendo la Ndoa, kuonyesha wanawataka waume zao wanawapenda na wajihadhari kabisa na uchawi wa kuwafananisha waume zao au kuwalinganisha na wengine ama wale waliowaona katika sinema za kingono na kwa busara kutoa maelekezo ya kile ambacho wakifanyiwa kitaleta msisimko mkubwa, badala ya kusubiri mume agundue mwenyewe.

2.    Usumbufu katika Ndoa zao
 Kwa ujumla sababu hii ndio sababu inayoweza kuwa ya msingi kwa wanaume wanaopokuwa wameamua kuoa wanakuwa na msimamo kwamba watatulia katika ndoa zao, lakini mambo yanapobadilika na mara kwa mara kukaanza kuwa na usumbufu kwa maana ya ugomvi kati yake na mke wake ugomvi unaojitokeza mara kwa mara na kukosa suluhu, hali ya kukosekana kwa furaha hujitokeza, na katika hali kama hii mume huweza kuamua kupambana ama kukimbia kwa maana ya kujiepusha na ugomvi huo na kuanza kutafauta faraja sehemu nyingine na kwa mtu mwingine, ni katika kutafuta faraja hiyo na kujihadhari na Usumbufu ndipo Mwanaume hujikuta anaanza zinaa, Kumbuka Mfalme Suleiman alisema ni afadhali kukaa katika pembe ya darini kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke  mgomvi yaani mwenye kelele (mithali 21:9) na pia alisema ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.

3.    Ugumu wa kutatua Matatizo ya ndoa 
Baadhi ya wanaume huona kama ni kazi kubwa sana kutatua matatizo ya ndoa zao, na kuona kuwa nji iliyo rahisi ni kupata mwanamke mwingine, na huko atajipatia raha na msisimko mkubwa na kujisikia kuwa mtu, kuliko kazi kubwa ya kufundisha na kuelekeza na kutatua migogoro katika ndoa, Kutoka nje inakuwa ndio zawadi kubwa wanayoweza kujipongeza hata kama watakuwa na kazi nyingi na ngumu, inaonekana ni afadhali lawama kuliko fedheha

4.    Wanaume wanapenda majaribio
Wanaume wamekuwa na ushawishi wa kimaumbile mioyoni mwao wa kutaka kufanya majaribio ya kingono, wakati wanaume wengine wanaridhika kufanya ngono na mke wao mmoja kwa muda mrefu na zaidi katika maisha yake yote, wengine wanaona hapana ni lazima wafanye majaribio ya kutosha kabala hawajaamua kutulia, wanataka kulala na wanawake wengi kadiri iwezekanavyo na mara nyingi na hivyo ahawafikiri zaidi umuhimu wa patano la ndoa na huenda wakajifikiri kuwa ni wenye nguvu katika ngono kuliko wengine

5.    Utoshelevu wa kihisia
Wakati mwanamke anapokuwa na shughuli nyingi za maisha yao, kufanya kazi kulea watoti na kuangalia ndugu jama a na marafiki au wazazi, wanaume wanabakia katika halia ya ukavu na kukosa utoshelevu lakini wanaume ni wenye kuendeshwa na hisia, wanapenda pia kupendwa kujaliwa na kushukuriwa na wangependa wake zao wawaonyeshe kuwa wanajali na kutambua kuwa wanajaribu kila liwezekanalo kuyafanya maisha kuwa mazuri, wengi wa wanaume hawapendi kukumbushwa yaliyopita ambayo nafsi zao ingependa iyasahahu, kama watalaumiwa tu nwakati wote itatokea kuwa watafanya mengineyo hata na watu wasaidizi wa kazini au Bosi zao, na wale wanaowasifia, wamaowahudumia na kuwajali nah ii ndio sababu inayowapelekea kuona ugumu na uthamani anaoupata nyumbani.

6.    Historia ya kurithi na kujifunza
Baadhi ya wanaume wana kumbukumbu za yake yaliyofanywa na wazazi wao katika ndoa, jambo hili linakuwa limewapa funzo na kuwajengea utambuzi tangu utoto kuwa kutoka nje ya ndoa ni jambo la kawaida, Hata kama inawezekana wakawa wanafahamu kwa undani kuwa wanachokifanya sio sahii, wote tunajifunza kutoka kwa wazazi wetu, na kwasababu hiyo kwa kujua au kutokujua tunapata maarifa na kuigiza kutoka kwao, kwa hiyo kutoka nje ya ndoa ni jambo ambalo wengine hujifunza kutokana na mazingira yote yanayowazunguka Marafiki, wazazi, jamaa na kila mmoja ambaye umekuwa karibu na mwenye aina hiyo ya maisha, watu hao kwa kukusudia au kwa bahati mabaya, Baadhi walikuwa na mahusiano na watu wengi huko nyuma na baadaye historia inajirudia

7.    Kulipa kisasi
Wanaume pia wanatabia ya kulipa kisasi, na kuamua kuwa na wanawake wengi, hata pale inapotokea kuwa wake zao walikuwa na hatia na wamekubalia kubadilika na kutubu baadhi ya wanaume hutumia hi kama njia ya kutokusamehe

8.    Wanahitaji kupendwa
Wanaume pia wanahitaji kupenmdwa, Mwanaume anapogundua kuwa hapendwi wanatafuta ni wapi wanapendwa na ni wapi ambapo kuna mtu atawafikiria kuwa wao ni maalumu, na matokeo yake ni kuwa ataangukia kwenye uhusiano wenye kutimiliza hisia zake na mara wakionyesha kujaliwa na kupatiwa kile ambacho hawakukipata kwa muda mrefu toka katika ndoa zao au kwa wake zao wananyoosha mikono yao hewani na kukumbatia uhusoiano mpya wa nguvu zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni