Alhamisi, 11 Februari 2016

UFAHAMU KUHUSU MANABII WADOGO (STUDIES IN MINOR PROPHETS)



UFAHAMU KUHUSU MANABII WADOGO, STUDIES IN MINOR PROPHETS

UTANGULIZI;

-Moja ya majukumu makubwa ambayo Taifa la Israel lilipewa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanalishika agano la Mungu walilokabidhiwa katika mlima wa Sinai.
-Unapo gusia tu kuhusu Historia ya Taifa la Israel ni lazima utakutana na vitu muhimu vitatu vifuatavyo;-

*      Habari kuhusu Mungu wa Israel
*      Historia ya Israel na uhusiano wake na Mungu
*      Historia ya kinabii na jinsi Mungu anavyo jishughulisha na wanadamu woote kupitia Taifa la Israel.

-Historia ya kinabii inatengeneza daraja muhimu kati ya Mungu na watu wake na kozi hii Ufahamu kuhusu Manabii wadogo inagusa maeneo muhimu ya kinabii kuanzia kati ya mwaka 853 k.k. Mpaka karibu na wakati wa uongozi wa Nehemiah mwaka 425 k.k, Manabii waliifanya kazi kwa Nguvu na ujasiri katika wakati mgumu Mungu alipowaita watu hao, Kazi kubwa ikiwa ni kuwaonya watu kumrudia Mungu na kulitunza agano lake kwa usalama wao.

-Mungu aliwatumia Manabii kushughulikia Maswala ya dini na siasa na maadili katika siku zao ambazo hazikutofautiana na siku zetu, kulikuwa na hofu za njaa,vita,Mmomonyoko wa maadili na imani potofu zikiwemo ibada mbaya za mabaali,unafiki, kutokuamini na ukengeufu vilitawala
-Mungu wakti huu aliwatuma Manabii kama sauti yake kwa watu wake ili kufundisha, kuhubiri na kuwakumbusha watu agano la Mungu na jinsi wanavyopaswa kuwajibika kwa ajili ya Mungu .Ni katika hali kama hii hii Mungu anataka kuwatumia watu wenye huduma za kitume, kinabii, kiinjilisti, kichungaji na kiualimu kama mashahidi na sauti ya kutoa mwito kwa watu wa Mungu kuishi kwa ajili ya Mungu na kuepuka maangamizi

ASILI YA HUDUMA YA KINABII.
-Moja ya sababu za kuwako kwa huduma ya kinabii ilikuwa ni kuhakikisha agano la mungu alilolitoa katika mlima wa Sinai linashikwa agano hili liliitwa pia sheria ya Musa Mosaic Covenant au Sinaitic Covenant
-Jukumu hili linaonekana kuwa mwanzoni walipewa makuhani yaani kufanya kazi ya kufundisha ,kuhubiri na kulisimamia agano lakini kadiri siku zilivyokwenda inaonekana kuwa makuhani walishindwa kulitimiza Jukumu lao kwa uaminifu na hivyo huduma ya kinabii ililzimika ichukue nafasi ili kusimamia agano na viwango vya maadili mungu alivyovitaka kidini,kisiasa na kimaadili. Kumbukumbu 18; 9-22.
-Huduma ya kinabii ilikuwa ni ya muhimu ili kuwalinda na uharibifu ukiwemo ule wa mataifa yaliyowazunguka, mataifa yaliyoizunguka Israel yalikuwa na uovu na hivyo huduma hii ilikuwa muhimu ili kuwalinada na wapiga ramli,ili kutofautisha kazi za Mungu na za wachawi hivyo Manabii walionya wasiotii na kufundisha ,kuhubiri, na kutahadharisha kuhusu kuwepo kwa Manabii wa uongo
-Manabii pia waliifanya kazi ya Mungu kwa kusimama mahali palipobomoka kati ya Mungu na wanadamu ili kuwapatanisha 
-Manabii pia waliifanya kazi ya kuwandaa watu kwa ajili ya ujio wa masihi yaani Nabii mkuu atakayetimiza vema  na kwa ukamilifu shughuli za kinabii huyu ni Yesu Kristo
         
Mlima wa Sinai eneo ambalo hutumika kuteremka kutoka mlimani hapa ndipo mahali Mungu alisema na wana wa Israel na kuwapa amri na sheria zake Kupitia Musa Mtumishi wake Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote

JINSI MANABII WALIVYOPATIKANA;-
-Kabla ya Nabii Samuel kulikuwa na makundi makuu mawili ya Manabii
*      Manabii wanenaji wa kale Old oral Prophets –Hawa ni wale waliohubiri kuonya na kufundisha au kutia moyo bila jumbe zao kuandikwa hawa ni kama vile Abraham Mwanzo 20;7, Henoko, Nuhu, Habili, Isaka, Yakobo na Yusufu, wengine ni Miriam  na Debora Manabii wa kike Waamuzi 4;4.
*      Manabii waandishi wa kale – Hawa ni wale wa zamani lakini waliandika Vitabu na kati yao ni Ayubu,Musa na Yoshua
*      Hao woote hapo juu upatikanaji wao ulimuhusu Mungu moja kwa moja.
-Wakati wa Nabii Samuel
*      Uapatikanaji wa Mnabii ulikuwa kitu cha wazi kabisa kwani Samuel alianzisha chuo cha wana wa Mnabii au Manabii wanafunzi. Hawa hawakuwa watoto wa Manabii bali walikuwa wanafunzi wa vyuo vya kinabii Mfano wa vyuo vya Biblia leo 1Samuel 10;5-13,2Falme 2;1-7 katika wakati huu pia kulikuwa na Manabii wanenaji wasio wa kale sasa na Manabii waandishi  wasio wa kale.
*      Mnabii wanenaji baada ya Samuel Latter oral Prophets ni pamoja na wale waliifanya kazi wakati wa serikali ya umoja yaani Gadi, Nathan, Sadoki, na heman walioitwa pia waonaji.aida Ahija alikuwa Nabii wakati wa serikali ya umoja katika wakati wa Suleimani na sehemu wakati wa utawala wa Yeroboamu huko samaria wengi wa Manabii wanenaji waliifanya kazi kabla ya Manabii waandishi mpaka wakati wa Obadia na Yoel mwaka 2852-796 k.k.
*      Manabii wanenaji uande wa Isarael ni pamoja na Iddo 2Nyakati 9;29,Shemaya, Azaria,hanani,Yehu.Eliya na Elisha aida kunauwezekano kuwa wengine waliandika lakini Vitabu vyao havikupita katika kanuni ya Waebrania
*      Manabii wanenaji upande wa Yuda  ni pamoja na  Mtu wa Mungu alitajwa hivyo tu katika 2nyakati 25;5-16,mikaya na Zekaria aliyeuawa.
*      Manabii waandishi baada ya Samuel walifikia jumla yao 16 yaani kati ya hao wanne Manabii wakubwa Isaya, Yeremia, Ezekiel na Daniel. 12 ni Manabii wadogo yaani kuanzia na Hosea mpaka Malaki

SIFA ZA MANABII
§  Waliitwa na Mungu na walikuwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu 2Petro 1;21 Kutoka 4;16,Torati 18;18
§  Waliitwa Manabii Neno Nabii maana yake ni “Navi” au “Nabi” kwa kiibrania ambalo maana yake ni Msemaji kwa niaba ya Mungu au mwenye kusema kwa mamlaka ya Mungu
§  Waliitwa watu wa Mungu “MTU WA MUNGU” hii ni kwa sababu walijitoa kwa Mungu kwa asilimia mia moja “Total Committed”  waliifanya kazi wakati wa uharibifu na Mmomonyoko mkubwa wa kimaadili walikataliwa na kuteswa lakini hawakukata tamaa.
§  Walitoa ujumbe bila hofu au kujali uso wa Mtu
§  Walitabiri mambo yajayo mengi yakimuhusu Masihi
§  Walikuwa ni kama walinzi Ezekiel 3;17,33;7
§  Zamani waliitwa waonaji, walikuwa ni wahubiri wa haki 2Petro 2;5 na pia waliitwa mdomo wa Yehova yaani wasemaji kwa niaba ya Mungu Kutoka 4;16.

JINSI YA KUPIMA AU KUMTAMBUA NABII WA KWELI
Ø  Nabii wa kweli alipozungumza unabii uliotimia au alitakiwa kutumia ili kuthibitisha kuwa ni Bwana amemtuma  Torati 18;21-22 Japokuwa ni muhimu kufahamu kuwa unabii wakati mwingine huweza kuwa wa muda mrefu au unaweza kubadilika kutokana na mazingira  mfano ule wa Yona watu walipotubui Mungu alihairisha hukumu  au inaweza kukawia kwa hukumu 1Falme 21;29
Ø  Unabiii wa kweli nilazima ukubaliane na Maandiko Matakatifu yaani Biblia Wagalatia 1;6-9 Torati 13;1-5 Marko 7;8
Ø  Lazima unabii wa kweli umuinue Kristo
Ø  Maisha ya Nabii yawe na viwango vinavyokubalika kibiblia Mathayo 7;15-20 Ampende Mungu na sio Fedha Mika 3;5,11
Ø  Atakuwa ni mtii kwa Viongozi wa kanisa katika Bwana 1Koritho 14;26-33
Ø  Je unabii wake unakusudia kulijenga kanisa  au kubomoa? 1Koritho 14;26-33
Ø  Atakuwa ameitwa na Mungu kuifanya kazi hiyo au kuwa na wito maalumu Yeremia 23;21.
Ø  Atakuwa anasukumwa na Roho Mtakatifu. 2Petro 1;20-21
Ø  Zamani Manabii walithibitisha kile walichokisema kwa kuhitimisha na Maneno asema Bwana wa Majeshi n.k. Amosi 3;8 unabii lazima upimwe au kupambanuliwa kwa sababu ya utendaji wa Roho tatu ya Kimungu,kibinadamu na ya shetani. Hivyo lazima ujaribiwe.

SURA YA KWANZA: WAKATI WA UTAWALA WA ASHURU YA ZAMANI MANABII WASIOJULIKANA TAREHE

1UTANGULIZI KUHUSU MANABII WADOGO
*      Mungu aliwatuma Manabii hao kwa paned zote mbili Yuda na Israel
*      Kwa ujumla walihudumu kati ya Mwaka wa 760 – 625 k.k kwa upande waufalme wa kaskazini na mwaka wa 760-43 kwa upande wa ufalme wa kusini yaani Yuda
*      Manabii waliotumwa kaskazini yaani kwa Israel ni pamoja na Amosi,Hosea ambao walikuwa ni raia wa ufalme wa kusini lakini walitumwa kufanya unabii huko kaskazini
*      Manabii waliotumwa kwa mataifa mengine ni pamoja na Obadia kwa ajili ya Edomu, Yona kwaajili ya Ninawi na Nahumu pia kwa ajili ya Ninawi
*      Manabiii waliotumwa kwa ajili ya Yuda ni pamoja na Yoeli, Mika Zefania na Habakuki
*      Manabii wengine waliotumwa baada ya utumwa wa babeli ni pamoja na Haggai,Zekaria na malaki na hivyo kufanya jumla ya Manabii kuwa kumi na mbili

       

Ramani ya Israel Kuonyesha shughuli za Manabii na maeneo ya huduma zao Nyakati za Biblia na wakati wa Israel na Yuda Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote

UCHAMBUZI WA MANABII WADOGO;
OBADIA MTUMISHI WA MUNGU NABII WA HAKI
Mwandishi wa kitabu cha Obadia.
A.     MWANDISHI NI NABII OBADIA MWENYEWE
-          Jina lake maana yake ni mtumishi wa Mungu sawa na “Abdullah” la kiarabu
-          Ni maarufu kama nabii wa haki
-          Kitabu chake hakina nukuu yoyote kuhusu yeye kazi yake  na wito wake
-          Tunajua kuwa alikuwa ni Nabii aliyetumwa huko Edomu kusini mashariki ya Yordani
-          Kitabu chake ndio kifupi kuliko vyote katika agano la kale
-          Tareha ya uandishi inakadiriwa kuwa mwaka wa 586 k.k.
-          Obadia haelezi ni lini alipata maono  na ingawaje ni kutokana na yale anayoelezea unaweza  kuhisi kuwa huenda ni baada ya anguko la Yerusalem
B.     UPEKEE WA KITABU CHA OBADIA
-          Ni kitabu cha pekee katika ujumbe wake na urefu wake
-          Ni kifupi kuliko vyote katika Agano la kale na kinabeba Tangazo na hukumu nzito kuhusu dhambi
-          Ujumbe wa Obadia kimsingi uliihusu Edomu wana wa Esau  ingawa aligusia na kurejezwa tena kwa Wayahudi ambako kutatimia kwa ukamilifu atakapokuwa anarudi Kristo baada ya dhiki ile kuu
C.     HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA OBADIA
-          Mwanzo 25;21-34,27;32-33 Hesabu 20;14-21, 2samuel 8;11-14-14, 2Nyakati 20;1-24,21;8-16
-          Ili kukifahamu kitabu cha Obadia Vizuri msomaji anapaswa kurudi nyuma na kuangalia maisha ya Mapacha wa Isaka yaani Yakobo na Esau
-          Mashindano yao yalianza tangu tumboni mwa mama yao na yaliendelea kwa karne nyingi katika ya vizazi vyao Mwanzo 25;21-34 watoto wote walikuwa na wazazi wacha Mungu na haki sawa ingawaje Esau alikuwa na shauku kwa mambo ya mwilini zaidi wakati Yakobo alikuwa na shauku ya mambo ya kiroho licha ya kuwa mwenye dhambi alikuwa na shauku katika Mungu na ahadi zake Waebrania 12;16 inasema Esau hakuwa mcha Mungu
-          Mungu aliona tabia zao hata kabla ya Kuzaliwa Mwanzo 25;23 Tabia tofauti na mitazamo Tofauti iliwapelekea vijana hao katika muelekeo Tofauti kidini, kiuchumi, na kimafanikio.
-          Upendeleo ulionyeshwa na kila mzazi ulichangia katika kuelekea kwenye migogoro wao
-          Baraka ambazo Isaka baba yao alikusudia kumpa Esau na zikaibiwa na Yakobo zilipelekea Chuki kubwa ya Esau dhidi ya Nduguye, Esau aliapa kuwa atamuua Yakobo na hii ilipelekea Yakobo kukimbia mpaka Padan- aram kwa mjomba wake Labani
-          Esau alitunza kisasi hicho kwa miaka 20 hivi mpaka wakati Yakobo  alipokuwa anarudi na Esau alituma kikosi cha askari 400 kumuua Lakini kwa neema ya Mungu, Mungu aliingilia kati na  wakapatana
-          Ingawa Esau na kizazi chake chote hawakuweza kuushinda uchungu waliokuwa nao dhidi ya Yakobo na kizazi chake
-          Miaka 300 baadaye kwa ajili ya uchungu na chuki Edomu haikuwaruhusu Israel kupita katikati yao walipokuwa wakitoka Misri Hesabu 20;14-21.
-          Mwaka 1042 k.k yaani kama miaka 700 hivi baadaye Daudi alizipiga nchi jirani na kupanua mipaka ya Israel na kuwafanya wana wa Esau yaani Edomu kulipa kodi yaani kutimiza unabii kuwa Esau angemtumikia Yakobo.
-          Wakati wa utawala wa Yehoramu Edomu waliasi 2Falme 8;20-22 na miaka 146 ilipita ndipo Edomu wakiungana na Waamoni na Wamoabu waliivamia Yuda wakati wa utawala wa Yehoshafati lakini Mungu alimpa Yuda ushindi.
-          Mwaka wa 586 k.k Edomu walifurahia ilipoanguka Yerusalem Zaburi 137;7 Ezekiel 35;15
-          Inaonekana kuwa baada ya Waedomu kushirikiana na Wakaldayo waliruhusiwa kukaa kusini mwa Israel baada ya wayahudi kuchukuliwa mateka huko Babeli
-          Walifanikiwa sana, lakini Makabayo baadae aliwashinda na kuwalazimisha kushika sheria za kiyahudi na baadaye wayunani na Warumi walipotawala waliliita eneo hilo Idumeya
-          Inasemekana kwamba Mfalme Herode mkuu anatokea katika jamii hiyo na eneo hilo
-          Baada ya mwaka wa 70 B.K Waedomu walimezwa na waarabu na wametoweka leo hawako kama Taifa au kabila.
D.     MISTARI YA MUHIMU
-          Msatari wa 3-4
-          15
-          17
-          21
E.     MIGAWANYO YA KITABU CHA OBADIA
-          Kuanguka kwa Edomu Mstari wa 1-16
-          Kuhuishwa kwa Israel Mstari wa 17-21
F.      UCHAMBUZI
*      Hukumu ya Mungu dhidi ya Edomu mstari wa 1-14.
-          Unabii unahusu kuanguka kwa Edomu  mstari wa kwanza unaonyesha kuwa kile Mwandishi aliandika sio mawazo yake lakini Mungu alikuwa amemfunulia “Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana” hii inaweza kuhusu  Obadia kusikia kutoka kwa Mungu kabla ya kuandika na huenda Yeremia na Ezekiel pia walipokea ujumbe kama huo.
-          Mjumbe aliyetumwa inaweza kuwa Malaika au Roho wa Bwana aliyetumwa kuyachochea mataifa  kuinuka dhidi ya Edom


G.    HALI YA EDOMU
-          Walikuwa na kiburi Mstari wa 2-4 walijiinua kwa sababu walikuwa na eneo lisiloweza kuvamiwa na mafanikio ya kijeshi na kisiasa waliyokuwa nayo iliwapelekea Kujiamini na kuacha kumtumaini Mungu Zaburi 127;1 Bwana asipoulinda mji aulindaye akesha bure.

                 
Mabaki ya mji wa wa Petra ambao ulikuwa chini ya serikali ya Edomu kama ngome zake zinavyoonekana leo Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.

-          Ingawa mji wao ulikuwa jangwani lakini mataifa mengi yaliionea wivu Edomu kwani walikuwa matajiri  wa visima vya maji na mabonde mazuri
-          Walikuwa na madini ya chuma na shaba na njia kuu za kibiashara  hata kwa njia ya bahari  hivyo utajiri wao pia ulichangia kiburi walichokuwa nacho Mstari wa 5,-6.
-          Edomu waliifanya biashara na Syria, Ashuru, India, Misri, Arabuni na Afrika
-          Mstari wa 5-6 unaonekana katika maono ya Obadia  kwamba wangepoteza utajiri wao moja ya mji wao mzuri ungetekwa  na huu ni mji wa Petra kiyunani au Sela kiibrania ambalo jina hilo maana yake ni mwamba,
-          Ilikuwa ni ngome kabambe isiyoweza kuanguka, tajiri na yenye kuzungukwa na mawe kila upande Linganisha Edom na ushauri unaotolewa katika 1Timotheo 6;1-19 hasa 17.
-          Kumbuka maagizo ya Mungu kwa Israel walipokuwa wakitoka Misri katika Kumbukumbu 2;4-5 na 23;7 na kitendo cha Waedom Hesabu 20;14-21 lakini pamoja na hayo chuki yao iliendelea Zaburi 137;7 na kulingana na  Ezekiel 35;1-11 Kitendo cha Edomu kilitokana na chuki na wivu wa kale  Galatia 6;7wenye uchungu.
-          Kumbuka!
           Mungu atayahukumu au huukumu mataifa kulingana na jinsi yanavyoshughulika na watu wengine na hususani watu wake aliowachagua Edomu walihukumiwa kutokana na tendo lao la kuwa kinyume na wanaoteseka katika Mathayo 25;31-46 Yesu alifundisha kuwa tuwasaidie wale wanaoteseka au wenye uhitaji kama wakimbizi, wathirika, masikini na wenye vita sasa ukilinganisha Matendo ya Edomu na Mathayo 5;43-45 na 1Yohana 3;15-18 tunajifunza kanuni za kuwapenda maadui zetu na chuki zinatufanya kuwa wauaji mbele ya macho ya Mungu kama hatia iliyowapata Edomu.
H.    SIKU YA BWANA MSTARI WA 15-17. 
Kwa ujumla hii inazungumzia swala la siku ya hukumu ya Mungu dhidi ya Maadui zake, Pia hutumiwa na Manabii kuelezea matukio ya mwisho wa dunia ambayo hujumuisha
·         Kunyakuliwa kwa kanisa
·         Dhiki kuu
·         Vita vya Armageddon
·         Kurudi kwa Yesu mara ya pili katika utukufu
·         Kuokolewa kwa Israel
·         Hukumu ya mataifa
·         Utawala wa Yesu Kristo wa miaka 1000 duniani
              Kwa ajili ya Edomu siku ya Bwana ilimaanisha siku ya hukumu ya Edomu kwa ajili ya uchungu dhidi ya Ndugu zao
-          Kiburi kingine cha Edomu ilikuwa ni rafiki zao Mstari wa 7 Waarabu walikuwa ndio rafiki wa karibu wa Waedomu  na walijiunga nao katika kuishambulia Yuda Zaburi 83;5-6 pia rafiki zao Waamini, Wamoabu, na wengine waliifanya biashara nao hawa waliwageuka
-          Kiburi cha kisiasa Mstari wa 8-9 Waliwategemea wenye Hekima, Viongozi wao wa kisiasa washauri na majeshi wataalamu wa Vita wa mlima Seiri  walijulikana sana kwa Hekima na maarifa ya ulimwengu inasemekana watu Rafiki wa karibu wa Ayubu mwenye Hekima Elifazi Mtemani alitokea Temani  ambazo ni sehemu za Edomu Linganisha msatari wa 9 na  Ayubu 2;11. Hekima ya kibinadamu inaweza kutumiwa kwa ajili ya Mungu na kwa utukufu wake kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa salama Yakobo 1;5 Ingawaje maarifa na Hekima pasipo Mungu  haiwezi kusaidia katika kuikwepa hukumu yake.
-          Kiburi kilichotokana na nguvu za kijeshi mstari wa 9; na kuwa na makomandoo wa kivita  mashujaa watemani vilitilia hofu mataifa mengine Yeremia 49;16 walijitumainia katika hali hiyo lakini ilitabiriwa kuwa askari wake wangechinjwa na watu wangeachwa bila ya ulinzi
-          Sababu kuu za Maangamizi ya Edomu ni Mstari wa 10-14.

*      Uasi dhidi ya Ndugu zao
*      Kusimama peke yao kujitenga kiburi cha Kujiamini
*      Kufurahia maangamizi ya ndugu zao
*      Kuwadharau ndugu zao na kuwasengenya siku ya taabu zao
*      Kufurahia utajiri na mali za ndugu zao na Kuwashambuilia mateka waliosalia.


YOELI: NABII WA PENTECOSTE

A.     MWANDISHI WA KITABU CHA YOELI
Ø  Mwandishi ni Yoel baadhi ya wasomi wanaamini alikuwa mwana wa Samuel (Samuel 8;1-2.) lakini Maandiko yanamtaja kama mwana wa Pethuel yaani uaminifu wa Mungu ingawa hatuna taarifa alizaliwa wapi na historia yake si kubwa sana ingawa inaonekana ya kuwa alikuwa kuhani Yoel 1;13-14,2;1 na 14-17.
Ø  Jina lake maana yake ni Yehova ni Mungu wasomi wengi wanaamini kuwa alikuwa kuhani hii labda huenda inatokana na kujishughulisha kwake zaidi na maswala ya hekalu na kushughulikia na majukumu ya kikuhani  1;13-14, 2;1, 14-17.Na mkazo wake katika kitabu chake chote unawafanya wasomi kuamini hivyo.
Ø  Inaonekana pia kuwa alikuwa anaishi Yudea na ni maarufu sana kama Nabii wa Pentekoste.Kwa sababu ya kuzungumzia swala la ujio wa Roho Mtakatifu katika Yoel 2; 28.


B.     TAREHE YA UANDISHI.
Ø  Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Yoel Haijulikani hasa ni lini Baadhi wanaamini kuwa huenda kiliandikwa wakati wa baada ya Uhamisho wa Babel kwa sababu Yoel hajawataja waashuru wala wakaldayo wala maswala ya kuabudu sanamu.
Ø  Ingawaje baadhi ya wasomi wanaamini kuwa uchanganuzi wa wadudu kama tunutu, Madumadu n.k ni Lugha ya mafumbo inayohusiana na uvamizi wa majeshi ya kigeni hivyo kama hivyo ndivyo Basi tarehe ya uandishi inaweza kuwa ni kabla ya utumwa na moja ya jambo linalothibitisha kuwa hakikuandikwa wakati wa utumwa ni kwa sababu kinagusia maswala ya ukuhani na hekalu hivyo kunauwezekano kikawa kimeandikwa 830 k.k. kwani hekalu liliharibiwa mwaka wa 586 k.k.
C.      HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA YOEL 2Falme 11; 1-12;3.
Ø  Ukweli kuwa Yoeli anashughulika na makuhani zaidi na sio wafalme unashuhudia ya kuwa kitabu huenda kiliandikwa wakati wa Yehoiada kuhani mkuu ambaye ni mtu mkubwa aliyechaguliwa kusimamia maongozi kwa sababu mfalme alikuwa mtoto hivyo Yoel hajazungumzia maswala ya mfalme katika kitabu chake.
Ø  Malkia wa Yuda Athalia alikuwa amewaongoza watu katika kuabudu mabaali. Lakini Yehoiada aliwaongoza kurudi kwa Mungu Na huduma ya Nabii Yoel ilichangia kuwarudisha watu kwa Mungu
Ø  Athalia alikuwa mtoto wa mchawi malikia Yezebeli aliyeolewa na Ahabu na aliolewa na Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Athalia aliwaongoza Yehoramu na Yuda kuenda mbali na Mungu kuabudu baali na kufanya dhambi nyingine Yehoramu aliwaua nduguze 6 ili kujihakikishia anabaki kwenye kiti cha kifalme na alipokufa mwanae Ahazia akawa Mfalme Badala yake, Athalia alimchochea Ahazia katika kuabudu miungu na baada ya mwaka mmoja aliuawa na Athalia alitawala na kutoa amri kuuawa kwa watoto woote wa Ahazia yaani wajukuu wake na warithi wa kiti cha ufalme.
Ø  Dada wa Ahazia alikuwa ni mke wa kuhani mkuu Yehoiada na kwa neema ya Mungu aliweza kumuokoa moja ya wana wadogo aliyeitwa  Yoashi na kwa kuwa alikuwa na umri mdogo  miaka 7 Yehoiada aliongoza makuhani na wazee wa Yuda kisiasa kufanya mapinduzi na kumfanya Yoashi kuwa mfalme na Athalia akauawa.
Ø  Yehoiada aliendelea kusaidia kuongoza mpaka Yoashi alipofikia Umri wa kuweza kutawala.
D.     UPEKEE WA KITABU CHA YOEL NA UJUMBE WAKE
a.       Yoeli alisisitiza kuhusu Siku ya Bwana, majukumu ya makuhani ambao ni muhimili wa dini na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mapigo yanayohusiana na nzige ni vitu maalumu sana katika kitabu hiki.
b.       Kitabu chote kialenga katika siku ya Bwana, huku Yoeli akitumia mifano ya Nzige kuwaonya dhidi ya hukumu ya Mungu itakavyokua isipokuwa kama watatubu. Jambo hili ingawaje linaenda zaidi ya hali halisi ya siku hizo kwani pia inazungumzia juu ya dhiki ile kuu siku za mwisho ambapo hasira ya Mungu itashuka ulimwenguni.
                

Nzige (Locust) Moja ya wadudu waharibifu wakubwa wa mazao kwa mujibu wa Yoel ni miongoni mwa Majeshi ambayo Mungu angeyatumia kuwashambulia watu wasipotubu uovu wao Picha na Maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.

E.     MSTARI WA MSINGI AU MISTARI YA MUHIMU

Yoeli 2;1   - Siku ya Bwana inakuja
Yoel 2;13. -  Rarueni mioyo yenu
Yoel 2;28  - Nami nitawamwagia watu wangu Roho yangu
Yoel 3;10  - Yeye aliye dhaifu na aseme mimi ni Hodari

F.      MGAWANYO WA KITABU
Kitabu cha Yoeli kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
a.       Nabii anazungumza 1;2-2;17
b.       Mungu anazungumza 2;18-3;21

G.    MCHANGANUO WA KITABU CHA YOELI
·         Hukumu na toba Yoel 1;1-2;27
Yoeli anatoa kwanza sababu za ujumbe 1;1, Neno la Bwana lilimjia, mara nyingi kile ambacho Bwana aliwapa Manabii walitakiwa kuwaambia watu na Mungu alizungumza wazi kulingana na mazingira yao nini cha kukifanya  ili waepuke hukumu zake na kufurahia Baraka zake zaidi
·         Mapigo ya Nzige 1;2-0
Mapigo ya nzige kulikuwa kitu cha kawaida katika mazingira yale lakini nzige hawa anaozungumza Yoel ni wa Tofauti na hawajawahi kuonekana mstari 2-3 ilikuwa ni kitu ambacho wazazi wangewasimulia kizazi kijacho cha watoto wao, kule kuonyesha kuwa wazazi hawatasahahu ni wazi kuwa watu wanapomuacha Mungu kwa hakika hukumu ya Mungu huwa inakuja juu yao bila mzaha, 2-4, Mstari wanne unaashiria labda vipindi vinne vya uvamizi wa nzige au hatua zao za kukua
·         Baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa adhabu ya aina hii ya nzige inawakilisha falme nne zilizoigandamiza Yuda na Israel kwa miaka mingi
Ø  Tunutu – wanawakilisha Babeli
Ø  Nzige – wanawakilisha Waajemi na Waamedi
Ø  Parare - wanawakilisha Wayunani
Ø  Madumadu -   wanawakilisha Warumi.
Hata hivyo baadhi ya wanatheolojia wanasema hawa walikuwa ni wadudu halisi na hawakuwakilisha falme yoyote I; 4 na 2;25-26
H.    WITO WA KUTUBU 1;2-2;17
Ø  Yoeli aliwaita watu woote kutubu kuanzia na Viongozi 1;2,3,14, 2;15-16 na wote walioishi juu ya nchi 1;2,3,14, Watoto wachanga na wanyonyao 2;16, Walevi 1;5 wakulima na watunzaji wa mizabibu 1;11 makuhani 1;13,14,2;15,2;1,15,17.bwana harusi na bibi harusi 2;16,8 walitakiwa kuomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mume wa ujana wake, walitakiwa kufunga na kuomba na kuitakasa siku ya bwana  hili lilikuwa linadhihirisha nini watu wanatakiwa kukifanya ili kuepuka hukumu ya Mungu
Ø  Yoeli aliwahakikishia watu kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na huruma na neema na si mwepesi wa hasira  na  kuwa hughairi mabaya
Ø  Uamsho lazima uanze na Viongozi wa kidini  hivyo makuhani waliagizwa kuomboleza kati ya patakatifu na madhabahu
I.       KUREJESHWA KWA BARAKA ZA MUNGU 2;18-27
Ø  Yoeli 2;18-27 Inatoa majibu ya Mungu kwa maombi ya Nabii, makuhani na watu wote, toba ya kweli inapofanyika Mungu Huiheshimu na kuikubali, hivyo Mungu alihaidi kuwaondolea Mbali nzige na kuwa angerejesha mazao na mavuno yangepatikana, miti ya matunda ingezaa na mashamba yangezalisha mavuno mengi
Ø  Baadhi ya wasomi wanatafasiri kuwa Yoel 2;20  jeshi la kaskazini kuwa kama ni Ashuru lakini mstari wa 25 unaweka wazi kuwa Mungu anamaanisha ni nzige halisi
Ø  Ingawaje namna atakavyo wafukuza nzige hao kungewatia moyo  watu wake kumuamini kwa wokovu dhidi ya majeshi ya wageni
Ø  Yoeli 2;21-27 inakazia maswala ya kiroho na Baraka ambazo zingewajilia watu wa Mungu,Baraka hizo za kimwili na kiroho zingeipata Yuda kama wataamua kumgeukia Mungu na hii pia iliwakilisha Baraka ambazo zingewapata kwa kumuamini Yesu wakati wa miaka 1000 ya Utawala wake duniani.
J.      SIKU ZA MWISHO 2;28-3;21
Ø  Kwa Maneno Hata itakuwa baada ya hayo 2;28 Nabii alimaanisha kuhusu wakati ujao mbali kutakuwa na utembeleo maalumu na hukumu
A.      Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu 2;28-29
Ø  Watu woote wa Mungu wangejazwa Roho Mtakatifu na kuna makundi sita yanatajwa kama ambao wangetembelewa na Roho Mtakatifu Wana wenu, binti zenu, vijana, wazee wanaume na wanawake.
Ø  Hiki alicho kitabiri Yoeli kilitimia kuanzia siku ya Pentecost Matendo 2;17-18 Petro aliitumia tafasiri ya siku za mwisho na kuendelea kwa kawaida siku za mwisho zilianza na Kuzaliwa kwa kanisa  siku ya Pentecost na kuendelea katika kipindi chote cha kanisa, Mungu aliwajaza watu wa chache Roho wake kwa kusudi maalumu lakini sasa anasema kwa watu woote kila mtu atakuwa na sehemu katika utumishi wa kazi yake Sehemu hii pia ya unabii wa Yoeli unaeleza nini kitatokea kutokana na kumwagwa huko kwa Roho wa Mungu, watu watatabiri, wataota ndoto, na kuona maono
Ø  Ishara hizi zoote zinafunua ushahidi wa Agano la kale  Mungu angaeendelea katika namna kama hiyo iliyokuwa wazi wakati wa Agano la kale  kujifunua mwenyewe lakini kwa upana zaidi katika Agano jipya
B.      Dhiki kuu 2;30-32.
Ø  Ishara na maajabu yanayotajwa katika mstari wa 30-32 yatatukia mwisho wa  kipindi  cha kanisa, Danieli alisema kutakuwa na kipindi cha dhiki ambayo haijawahi kuweko tangu kuumbwa kwa ulimwengu  lakini katika wakati huo watu wako kila atakayeonekana jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima wataokolewa Daniel 12;1, Tunaona katika Ufunuo 6;12-14 kile ambacho Yoel alitabiri lakini kwa undani zaidi
Ø  Tetemeko kuu jua kutiwa Giza na kuwa jeusi mwezi kuwa mwekundu kama damu lakini wale watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.
C.      Hukumu ya Mataifa 3;1-16 Isaya 2.
Ø  Mwishoni mwa dhiki ile kuu kutakuwa na hukumu kubwa kwa kuanziwa na vita vya Armageddon watu wa Mungu watakapokuwa wamepatwa na maangamizo makubwa mwishoni wataliitia jina la Bwana kwa wokovu 5;15
Ø  Maombi ya Israel wakati huu yatakuwa  watelemshe mashujaa wako ee Bwana Yoel 3;11 na Isaya 64;1
Ø  Yesu atakuja na watakatifu wake na jeshi la malaika  na atamshughulikia mpinga Kristo na Israel watakapomuona watatubu na kumtambua kama Bwana na mwokozi wao, Kisha hukumu ya mataifa itachukua nafasi yake na mataifa yoote yatahukumiwa katika msingi wa namna wanavyoshughulika na Israel na kanisa.
D.      Utawala wa Yesu Kristo wa Miaka 1000. 3;17-21 Isaya 35
Ø  Ujumbe wa Yoeli unamalizikia na Baraka kubwa iliyohaidiwa kwa watu wa Mungu
o   Bwana atakuwa kimbilio lao na Ngome yao kuu sana 3;16
o   Bwana atakaa katika Sayuni 17,21
o   Yerusalemu watakuwa watakatifu na haitovamiwa tena mstari wa 17
o   Israel itapata chemuchemu za maji na nchi itakuwa yenye kuzalisha sana mstari wa 18 na Yuda itadumu milele mstari wa 20. Mungu atawasamehe Israel Mstari wa 21.


YONA: MMISHIONARI MZALENDO
A.      UTANGULIZI
Ø  Je umewahi kusikia habari za Mwinjilisti ambaye amekasirika kwa sababu wenye dhambi aliowahubiri wametubu na kuokolewa? Yona ni miongoni mwao
Ø  Yeye anaitwa Nabii  asiyetii au Mmishionari Mzalendo yeye alikuwa na uchungu dhidi ya watu ambao Mungu alikuwa amemtuma akawahudumie, alikuwa mbishi muasi na mwenye ubinafsi wa hali ya juu alikosa upendo na huruma na kama ungekuwa wewe na mimi Tusingelimtuma Yona kuwa Nabii
Ø  Jina lake Yona ni la kiibrania ambalo maana yake ni “Njiwa” Ni mwana wa Amittai  ambaye maana yake ni kweli ya Mungu kutoka Gath-Hepher ambayo ni kana ya wakati wa Agano jipya  na ilikuwa karibu na Nazareth mahali alipokulia Bwana Yesu
Ø  Kitabu kinahusu kufanya umisheni katika nchi ngeni na Mungu anamtumia Nabii asiyependa kufanya umisheni wa kigeni kukiandika, Kitabu kinatufundisha jinsi Mungu anavyojihusisha na mataifa mengine pia na kuwa hana upendeleo.
B.      MWANDISHI 
Ø  Wanatheolojia wengi wanaamini kuwa huenda kitabu kiliandikwa kati ya 780- 753 K.K  mapema wakati wa utawala wa Yeroboamu wa pili 
Ø  Kuna uwezekano kuwa alianza huduma yake wakati wa Nabii Elisha mwishoni kwani kulingana na Tamaduni za Israel inasemekana kuwa ndiye mtoto wa mwanamke mjane wa Sarepter ambaye Eliya alimfufua kutoka kwa wafu tarahe kamili inakisiwa ya uandishi kuwa 780 K.K.
Ø  Yesu alinukuu Matukio ya Yona katika Mathayo 12; 39-41 Jambo linalothibitisha kuwa kitabu chake kimevuviwa na sio hadithi tu kama watu wengine wanavyofikiri Yona pia anatajwa katika 2Falme 14;23-25 kama mtu anayetambuliwa kuwa alikuwa Nabii katika ufalme wa kaskazini wakati wa Yeroboamu wa pili mwaka 792-753 K.K.
C.      HISTORIA YA WAASHURU WALENGWA.
Ø  Watu wa Ashuru walijulikana sana kwa ukatili wao baadhi ya watu waliochukuliwa mateka na wafalme wa kiashuru waliwekwa katika visanduku vidogo vya chuma na misumari  na kupelekwa nje ya mji wa Ninawi mji wao mkuu
Ø  Visanduku hivyo vilikuwa vidogo kiasi ambacho mtu hakuweza kukaa wala kusimamia waashuru waliwaua wafungwa wengi kwa kuwakata miguu kila siku mguu moja na siku nyingine mguu mmoja ili kuwafanya wasikie maumivu makali
Ø  Wengine walilazimishwa kuwachinja rafiki zao waliowafahamu zamani watu wengi waliona ni afadhali kujiua kuliko kuwa kwenye mikono ya waninawi Nahumu 3;19
Ø  Wanawake waja wazito waliwapasua tumboni ili kuona ni jinsi gani kitoto kinakaa ndani ya tumbo la mama zao.
Ø  Inawezekana hii ndio ilikuwa sababu iliyomfanya Yona kuchagua kufa kuliko kuwahubuiri watu hawa katili aliokuwa amesikia habari zao na huenda pia Yona alifahamu kuwa wangetumiwa na Mungu kuwaadhibu wa Israel. kwani mnamo mwaka wa 722 K.K. yaani miaka 38 baada ya mahubiri ya Yona Waashuru waliivamia Israel na kuwachukua mateka huko Ashuru
D.      UPEKEE WA KITABU CHA YONA
Ø  Kitabu cha Yona ni Tofauti na Vitabu vingine vya kinabii kwa sababu ya maswala ya msingi yafuatayo;-
1.       Kimeandikwa katika mtindo wa kihistoria kuliko Vitabu vingine vya kinabii ingawa kina kweli nyingi ambazo zinaweza kuwa ni changamoto kubwa na kweli kuu ambazo zaweza kufanya kazi katika maisha yetu leo.
2.       Matendo ya Mungu kwa asili katika kitabu hiki kina kweli kuu kuhusu Mungu kwa asili hii inafundisha wazi kabisa kuwa Mungu yuko kila mahali na ni vigumu kukimbia au kujificha mbali na uso wake Zaburi 139;7-12, kinafundisha pia kuwa Mungu ni Bwana wa Historia, mataifa na Viumbe vyote na kuwa anahukumu kila jamii inapokosea na anaweza kutumia asili kwa mfano alimtumia upepo, samaki mkubwa mmea wa mtango, mnyoo Jua n.k. katika kukamilisha mpango wake kwa Yona kwenda ninawi.
3.       Kitabu hiki kipekee sana kinasisistiza Umisheni  na kufunua Upendo wa Mungu na mpango wa Mungu wa wokovu sio kwa wayahudi pekee bali kwa watu wote wa mataifa Yoote Matendo 10;34-35
4.       Unabii unaotegemea Conditional natural Prophecy Yona alitangaza kuwa Ninawi utaharibiwa katika siku arobaini lakini haukuharibiwa mji kwa sababu watu walitubu Yeremia 18;7-10
E.       MGAWANYO
Ø  Yona kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
1.       Wito wa kwanza na upinzani wa Nabii sura ya 1-2
2.       Wito wa mara ya pili na Manung’uniko ya Nabii 3-4
F.       MSTARI MKUU AU MISTARI YA MSINGI
Ø  2;9 Wokovu unatoka kwa Bwana
Ø  3;9 Nani ajuaye ya kuwa Mungu ataghairi na kusamehe
Ø  4;2 Najua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma si mwepesi wa hasira u mwingi wa rehema  nawe wagahiri mabaya.
G.       MCHANGANUO WA KITABU CHA YONA
Kukimbia wito wa Mungu sura ya 1-2.
Ø  Yona hakuwa na mshaka kuhusu nini Mungu alikuwa anataka kukifanyaalipokea ujumbe kwa Mungu kabla na hivyo alifahamu sauti ya Mungu lakni kile ambacho mungu alikuwa amemtuma kilikuwa kimemshagaza kumbuka wakati Mungu alipomwambia Petro aende kwa Kornelio Matendo 10;1-29
Ø  Ninawi ulikuwa mji wa kipagani na mji mkuu wa Ashuru Utawala ambao ulikuwa ni adui mkubwa wa Israel kwa miaka  Mungu alisema uovu wao umepanda juu mbele zangu Mwanzo 18;25 Kwa hivyo yona aliitwa kwenda kuhubiri dhidi ya Ninawi lakini yona hakutaka kulitimiza Jukumu hilo hivyo alikimbia kwenda mbali ingawa alijua wazi kuwa Mungu yuko mahali kote 
Ø  Kumbuka Ninawi ilikuwa karibu kuluiko alikokuwa anakimbilia yaani Trshishi ambayo inaaminika kuwa ni sehemu za Hispania ya leo  Mbali sana kutoka Yaffa
Ø  Kilichofuata ni adhabu kwa ajili ya kutokutii kwa Yona lakini kwa upande mwinginie ni Rehema za Mungu ni upendo wake kumrejeza Yona katika hali ya utii Waebrania 2;10-11.Mungu alituma upepo mkali na mabaharia walifikiri kuwa meli ingevunjika.
Ø  Katika hali hizo zote za dhuruba Yona alikuwa amelala usingizi na hakuwa anajua nini kinaendelea 1;6 matoleo mengine ya Biblia kama Septuagint inasema alikuwa anakoroma
Ø  Yona alipoamsahwa alitoa ushuhuda wa ajabu kuwa anamwabudu “Mungu wa mbingu aliyeumba bahari na nchi kavu …. Na ya kuwa ninakimbia mbele zake” jambo la kushangaza ni kuwa zaidi ya kuasi kwake Yona alikuwa anashuhudia kuhusu Mungu wa kweli na kabla ya kutupwa watu hao waliomba sasa si kwa miungu yao bali kwa Mungu wa Yona 1;14 walitoa sadaka na kuweka nadhiri kwa Mungu huyo huenda waliahidi kumtumikia Ushuhuda wa Yona ulileta matokeo na watu walitubu ingawaje yeye alikuwa akielezea kukimbia kwake
Ø  Yona aliyatoa maisha yake kwa hiyari yake mwenyewe ili wale walikuwa kwenye meli waweze kuokolewa 1;12
Ø  Huenda Yona alijua wazi kuwa kama Ninawi watatubu Mungu atawasamehe na kuwaokoa lakini la kushangaza Yona mwenyewe hakuwa tayari kutubu na badala yake alikuwa tayari kufa kuliko kwenda Ninawi hii inaonyesha jinsi ambavyo kuna hatari katika kuasi mapenzi ya Mungu na na jinsi chuki dhidi ya wengine inavyoweza kutenda kazi ndani ya mtu.
H.      KUHIFADHIWA NA KUOKOLEWA.
Ø  Mungu hakuwa amemsahau mtumishi wake na bado alikuwa na mpango naye na huduma yake kwa ajili ya watu wa Ninawi aliandaa samaki mkubwa Nyangumi na kummeza Yona baadhi ya matoleo ya Biblia yanasema Mungu akaandaa au akachagua samaki mkubwa hii inaonyesha uweza wa Mungu dhidi ya mambo ya asili kuwa Mungu aweza kuyatumia mazingira au Viumbe katika kutimiza mpango wake,wengine wana fikiri kuwa labda swala la kumezwa na nyangumi ni hadithi lakini kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu, Mungu aliandaa samaki mkubwa hii imerudiwa mara nne katika kitabu cha Yona
Ø  MAOMBI KWA AJILI YA WOKOVU.
Yona alifanya maombi na kujiuhukumu mwenyewe ndani ya samaki, lakini Mungu kwa huruma yake na Neema wakati mwingine anaruhusu sisi kupitia hukumu zake ili kwamba tumlilie yeye na kumtegemea yeye na kwa wakati huu sasa Yona alikuwa tayari kwenda Ninawi na kumtii Bwana  alithibitisha kujitoa kwake kwa Mungu na  Furaha ikaujaza moyo wake.
I.         KUTII WITO WA MUNGU MARA YA PILI.
-          Hakuna ajuaye ya kuwa Samaki alimpeleka wapi Yona huenda alimtapika huko Ninawi hata hivyo hili si la muhimu hapa la muhimu ni kuwa Yona alikubali wito wakati, Mungu alipomtuma mara ya pili.
-          Watu wengine hukataa wito wa Mungu na hawapati nafasi ya pili ya kumtumikia Mungu wengine hufikiri ya kuwa huenda Mungu hata watumia tena,Yona alitii neno la Bwana lilipomjia mara ya pili na alikwenda Ninawi
-          Inakisiwa watu wapatao 600,000. Waliishi Ninawi na vitongoji vyake ilimgharimu siku tatu Yona kuihubiri Ninawi ingawa alipewa siku 39. Ujumbe wake ulikuwa katika siku tatu ninawi utaangamia, kwa mujibu wa Luka 11;30  tunajua kuwa huenda Yona alimtumia uzoefu wake wa kumkimbia Mungu na kuokolewa na hii ilikuwa ishara kwa watu wa ninawi kutubu mji mzima na kumrudia Mungu
J.       KUMFAHAMU MUNGU NA MTAZAMO WAKE SURA YA NNE
-          Mwinjilisti anakasirika kwa sababu wenye dhambi wametubu  hiki nacho ni kioja ni wazi kuwa alijua kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na ya kuwa atawasamehe waninawi na ndio maana alikimbia wala hakutaka waninawi waokolewe
-          Wakati waninawi wanatubu kwa kufunga, Yona alikuwa anajijengea kibanda cha mapumziko kwa ajili yake nje ya mji akisubiri kwa tumaini kuwa Mungu atawaangamiza na siku arobaini zikapita patupu!
-          Yona alikasirika alikuwa na tatizo Kiburi,Ubinafsi na kukosa upendo alijihusisha sana na heshima yake kama Nabii ametabiri na Mungu ataitimiza unabii wake alikuwa tayari kufa kuliko kurudi Israel na kusimulia kuwa mahubiri yake yamewafanya Waninawi watubu na kuokolewa
-          Mungu ana namna yake anavyoweza kuyaangalia mambo na kutuonyesha makosa yetu na kutufundisha mtazamo wake aliandaa mtango kumpa Yona kivuli  na Nabii wake mwenye hasira akapumzika kisha akaandaa mnyoo upepo na jua kali vikaharibu kile kivuli Yona akakasirika zaidi
-          Kumbuka kuwa mungu alimuuliza yona unaona vema kukasirika hatupaswi kulaumu kile mungu anachokifanya Yona alijibu kuwa anafanya vema kukasirika hata kufa Hasira husumbua watu wengi na husababisha kifo au kupooza Srtokes
-          Mungu alikuwa akimfundisha Yona na sisi kuwa Yeye ni mwingi wa Rehema  Yona alifurahia faraja zake na starehe zake  kuliko maisha ya watu 120,000 watoto wachanga na wanyonyao Mungu aliwajali wao kwani anaupenda ulimwengu mzima Yohana 3;16.


SURA YA PILI: WAKATI WA UTAWALA WA ASHURU NA MANABII WA KARIBU NA ISAYA
AMOSI: NABII WA UTAKATIFU
A.      UTANGULIZI
-          Amosi alikuwa miongoni mwa wanamapinduzi wakubwa katika Isarael huduma yake ilifanyika kipindi ambacho Israel walikuwa wameharibika vibaya  na walikuwa katika wakati wa mafanikio na starehe ambazo ziliwafanya Israel  kuishi maisha ya dhambi
-          Jina lake maana yake ni “Mbeba mzigo” alikuwa na mzigo wa kutimiza agizo Mungu alilokuwa amempa kulitangaza neno la bwana wakati wa ukengeufu mkubwa wa Israel alizaliwa katika kijiji kiitwacho Tekoa miles 12 hivi kutoka Yerusalem
-          Alikuwa Mchungaji wa Kondoo na mtunzaji wa miti ya mikuyu hakuwa Nabii aliyesomea  7;14 lakini alikuwa mnenaji Hodari “Great orator”Asili ndiyo ilikuwa shule yake na anga ubao wake 5;8 Neno lake linaonyesha historia yeke 3;8
-          Amosi alikuwa mtu wa Yuda ingawa alitumwa kwa Ufalme wa Israel
Pichani Juu wachungaji wakichunga kondoo katika uwanda wa mashamba ya ngano huko Tekoa mahali alikotokea Nabii Amosi Tekoa iko mail 12 hivi kutoka Yerusalemu katika tawala za Yuda Picha kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote 

B.     TAREHE YA UIANDISHI.
-          Kitabu kiliandikwa mwaka wa 755 K.K. wakati wa utawala wa Yeroboamu II mfalme wa Isarael na Uzziah Mfalme wa Yuda


C.     WASIFU WAKE.
-          Amosi alikuwa Mnyenyekevu na wala hakijaribu kuficha maisha yake ya huko nyuma 7;14
-          Alikuwa na Hekima  katika kupeleka kwake ujumbe alimtumia misamiati amabayo ilikuwa wazi na ya kivitendo
-          Alikuwa mtu Imara thabiti alikataa kugeuzwa na Amazia kuhani mwakilishi wa Yeroboamu huko Betheli 7; 10-17.
D.     HISTORIA YA WALENGWA.
-          Wakati huu Israel walikuwa wanaishi maisha ya anasa na mafanikio makubwa sana hata hivyo baadhi ya matajiri waliupata kutokana na dhuluma
*      Masikini walikandamizwa Amosi 5;7,11
*      Mahakimu au Waamuzi walikuwa wakipokea Rushwa Amosi 5;12
*      Wafanya Biashara hawakutumia mizani za halali Amosi 8;5-6
*      Wenye haki waliuzwa utumwani amosi 2;7
*      Kulikuwa na uashaerati usio wa kawaida hata Baba na Mtoto waliweza kutembea na mwanamke mmoja Amosi 2;7.
*      Waliwakataza Manabii kuhubiri Amosi 2;7.
*      Watu walioishi maisha ya Stareha na anasa Amosi 6;1
*      Uasi wa kidini ulitawala Amosi 4;4-5, 5;21-23
-          Utawala ambao ungeiangamiza Israel ingawa haujaelezwa ni Ashuru.

E.     WAZO KUU NA MISTARI YA MSINGI.
-          Wazo kuu katika kitabu hiki ni Samaria Inavuna hukumu,amosi alikuwa  ni Nabii wa kwanza kutamka anguko la Samaria au Israel ambalo lilitimia miaka 40 baadaye ujumbe wake ulikuwa hukumu ya Mungu kwa sababu ya Kukosekana kwa haki katika jamii
-          Mstari mkuu au wa msingi ni
-          Amosi 3;3 Je wawili waweza kutembea Pamoja isipokuwa wamepatana?
-          Amosi 4;11-12 “Jiandae kukutana na bwana Mungu wako”
-          Amosi 6;1 ole wao wanaostareha katika Sayuni
F.      MGAWANYIKO WA KITABU CHA AMOSI.
-          Hukumu ya mataifa sura ya 1-2
-          Hukumu ya Israel sura ya 3-6
-          Uchanganuzi wa hukumu 7-9;10
-          Ahadi ya kurejeshwa upya 9; 11-15.
G.     MCHANGANUO WA KITABU CHA AMOSI
-           Kabla ya kutangaza hukumu  dhidi ya Yuda na Israel Nabii anachagua mataqifa kama sita hivi  ambayo pia aliyatangazia hukumu ya Mungu
-          Matatu kati ya hayo ni Dameski Syria,Gaza kwa wafilisti na Tiro ambao hawa hawakuwa na uhusiano wa kindugu na Israel bna yuda
-          Mataifa mengine matatu ambao walikuwa na uhusiano wa kidugu na Israel na Yuda ni Edomu, Ammoni na Moabu.
-          Kila tamko la hukumu kwa mataifa ya jirani na Israel na Yuda ilianza na “Haya ndiyo asemayo Bwana kwa makosa matatu naam kwa makosa manne sitazuia adhabu….”
-          Mtindo huu unamaanisha maovu yaliyopita kiasi na ya kuwa maovu hayo yaliongezeka mwaka kwa mwaka
-          Amosi ndiye mwanzilishi wa mtindo wa kuliita taifa kupitia jina la mji mkuu wake mfano anapoizungumzia Yuda anaitaja kama Yerusalem na Israel kama samaria.

A.      HUKUMU DHIDI YA DAMESKI SYRIA 1;3-5
-           Dameski ulikuwa ni mji mkuu wa Syria na hapa Syria inatangqaziwa hukumu kwa sababu ya kulitendea vibaya Gileadi Gileadi ulikuwa mji wa kale wa kabila ya nusu ya Manase ambao walibaki ng’ambo ya Yordani watu walipokuja kuitamalaki inchi ya mkanaani,
-          Dameski waliwachukuwa watumwa au mateka kwa vyombo vya chuma na kuwaburu za kama mtu avunaye ngano mungu anahaidi kushusha moto na kuwateketeza
B.      HUKUMU DHIDI YA GAZA 1;6-8
-          Gaza ulikuwa mji mkuu wa wafilisti  kusini magharibi ya Yerusalem,Dhambi yao ilikuwa ni kusafirisha watumwa waliwachukuwa watu walioishi vijijini  hususani waisreal na kuwauza huko edomu kama watumwa
-          Mungu anaahidi kuwaletea hukumu ya kuwateketeza kwa Moto na kuuchoma mji na majumba yake
C.      HUKUMU DHIDI YA TIRO 1;9-10
-          Tiro iko kaskazini mwa pwani ya Israel na mji uliokuwa kutuo kikuuu cha bahari au bandari Isaya ,Yeremia na Ezekiel waliitangazia hukumu maalumu ulikuwa mji mkuu sana wa kibiashara  na kajhba mkuu wa wakati ule
-          Inaonekana waliwachukuwa watu fualni kabila nzima huenda Waisrael na kuwatia mikononi mwa Edomu hivyo dhambi yao ilikuwa ni kufanya biashara ya utumwa na Edomu na walisahau agano la undugu huenda hili lilikuwa ni agqano walilolifanya Daudi na Hiramu katika 2samuel 5;11
-          Hukumu yao ni moto na kuharibiwa majumba yake na ni kweli Nebukadneza alijaribu kuuteka tiro lakini si kwa mafanikio sana na mwishoni  uliharibiwa vibaya na Alexander mkuu.
D.      HUKUMU DHIDI YA EDOMU 1;11-12
-          Hwa walikuwa ni uzao wa Esau pacha wa Yakobo na walioishi kusini mwa bahari iliyokufa  sehemu iliyoitwa araba, wao wanahukumiwa kwa Matendo yasiyo ya kindugu,alimtumia upanga na mateso hawakuwa na huruma na walikuwa na kisasi cha hasira kwa siku nyingi na wanatangaziwa hukumu nya moto juu ya temmani na Borsa  miongoni mwa miji yao mikubwa na kuiteketeza.
E.       HUKUMU DHIDI YA WAAMONI 1;13-14
-          Waamoni na wamoabu ni Watoto,wajukuu wa Lutu waliozaliwa kutokana na zinaa ya baba na watoto wake wa kike  Mwazno 19;30-38
-          Wao wanahukumiwa kwa sabau ya ukatili wao kwa Gileadi ,waliwapasua wanawake wenye mimba wa Gileadi wanatangaziwa hukumu dhidi ya mji wao mkuu  Raba au Raboth-ammoni
-          Inaaminika kuwa huko ndiko Daudi alikoagiza Yoabu kuhakikisha Uria anauwa vitani 2Samuel 11.
F.       HUKUMU DHIDI YA WAMOABU 2;1-3
-          Hawa walikuwa na kosa la kuichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu  hata ikawa chokaa inaonekana hawakumpata akiwa hai hivyo kwa hasira walilipa kisasi kwa mifupa ya mfalme Isaya 15;5,16;11 Yeremia 48;36
-          Wamoabu walihukumiwa kwa moto ,na kuuawa kwa Viongozi ,Waamuzi na watu wakuu
-          Mungu anafuatilia sio tu mataifa wanavyolifanyia taifa la watu wake bali hata kila taifa linavyolifanyia lingine.
G.      HUKUMU DHIDI YA YUDA 2;4-5
-          Tofauti na mataifa haya mengine ya kidunia sita Nabii anaigeukia Yuda ambao ni ufalme wa kusini lakini hawa wanahukumiwa kwa kutokishika Sheria ya Mungu hivyo wao wanahukumiwa kwa maswala ya kidini yaani walikengeika na kuiacha Shetia ya Bwana
-          Waliishi kama watu wa dunia  nao watahukumiwa kwa moto na majumba yao kuteketezwa
H.      HUKUMU DHIDI YA ISRAEL 3;1-6
-          Pamoja na matangazo yoote hayo ya hukumu mungu alikuwa akiilenga Israel wao ndio wanaoonekana kuwa na dhambi nyingi zaidi kuliko mataifa mengine mlomlongo wa msururu wa dhambi kwa Israel ni mkuu sana  walionea masuikini,waliwauza watu wenye haki ,waliabudu sanamu,waliifanya biashara ya utumwa, waliwafanya wanadhiri kuvunja nadhiri zao na kulitii unajisi jina la bwana
-          Amosi aliorodhesha dhambi nyingi za Israel kuliko za mataifa mengine huenda ili kuonyesha hatia kubwa waliyokuwa nayo na pia kwa sababu alikuwa akiihubiri Israel na kuwaonyesha uhakika ya kuwa Mungu angewahukumu wao.
-          Mungu anaihukumu Israel na kuwatangazia hukumu hivyo akisisitiza katika matangazo makuu matatu yoote yakianzia na neno lisikieni 3;1,4;1,5;1 na katika 3;3 anauliza je wawili waweza kutembea Pamoja isipokuwa wamepatana? Mungu alikuwa anahoji anawezaje kutembea na Israel na kukubaliana nao huku wanatembea dhambini
-          Amosdi alimtumia hata mifano kama simba na mawindo,Mtego na tarumbeta  ili kuwaaamsha Israel kutoka katika usingizi wa maovu na starehe
-          Mungu hawezi kutuma hukumu kwanza kabla hajaifunua siri hiyo kwa watumishi wake Manabii amosi 3;8
-          Israela walikuwa wameingia katika ile dhambi ya kuabudu miungu 1Falme 12;25-33 na dhambi za starehe 3;15
-          Katika Sura ya 4 amosi aliendelea na ujumbe wake wa hukumu aliwaita Israel Ng’ombe za bashani Bashani palijulikana sana kwa  utajiri wa mifugo na mafuta na wanyama waliolishwa vizuri sana  Kumbukumbu 32;14-15, Wanawake matajiri waliokuwa wabinafsi waliitwa ng’ombe za bashani walijali maswala yao ya starehe na anasa na waliwatia moyo waume zao kujitajirisha na kuwaonea masikini 4;4 inaonekana kulikuwa na shughuli nyinfgi za kiibada na za kidini lakini  hakukuwa na kujitoa kwa kweli kwa Mungu
-          Mungu alihaidi kuwatumia Mapigo makuu matano  4;6-11 yaani njaa ,ukavu dhuruba,nzige,magonjwa
-          4;6 Lugha ya kimafumbi inatumika “Euphenism language” nimewapa usafi wa meno maana yake njaa. 4;12 wanaambiwa wajitayarishe kukutana na Mungu.
-          Katika sura ya 5 nabii anaomboleza kwa ajili ya dhambi ya Israel, wako watu ambao hudhani kuwa kuudhuria kwao ibada ni kwa muhimu zaidi au kunaweza kuwapa kibali kwa mungu na kusahu wajibu wa kujitoa kwake
H.    UFAFANUZI WA HUKUMU AMOSI 7;-9;10
a.       Eneo hili lina ufafanuzi wa hukumu tano ambazo Mungu alimuonyesha Amosi katika maono
i.        Nzige- Mungu wakati mwingine hutimia majanga ya asili  katika kuhukumu amosi aliomba kwa niaba ya taifa likasamehewa pigo hilo 7;1-3
ii.   Moto Mungu alikusudia uteketeze na kuangamiza lakini pia amosi alimuomba    Mungu asamehe na ikawa hivyo  7;4-5
iii.      Timazi kilikuwa kipimo cha kuonyesha kuwa wamepotoka kiasi gani Bwana alimuonyesha amosi na wakati huu ikawa ndio mwisho wa kusamehewa mungu ana kipimo chake kwa ajili ya maisha yetu
iv.      Kikapu cha mavuno ya wakati wa hari 8;1-3 kuonyesha kuwa wanvuna kile walichokipanda
V. Kuvunjwa kwa madhabahu 9;1-10 huku ni kuharibiwa kwa hekalu lililokuwako huko Betheli kwa ufalme wa kaskazini
·         Amazia ambaye alikuwa ni kuhani mkuu kwa upane wa Betheli 7;10-17 alishutumu Amosi na kumshutumu kuwa amafanya uongo fitina juu ya Israel na hivyo hawawezi kustahimili Maneno yake na Amosi alisisitiza kuwa wito wake ni kutoka kwa Mungu
I.  AHADI YA KUREJEZWA TENA 9;11-15.
- Amosi anamalizia kitabu chake kwa ahadi ya kurejezwa tena kwa Israel
- Kwamba watatawanywa hukona huko kati ya mataifa lakini mabaki watarejezwa
- Nchi itastawi na hawataweza kutawanywa tena 9;11-15





HOSEA: NABII WA UPENDO

A.       Mwandishi wa kitabu cha Hosea.
-          Alikuwa Nabii kwa Israel katika Dakika za mwishoni kabla kidogo sana Israel kuanguka katika mikono ya waashuru mwaka 722 K.K
-          Ni Nabii maarufu kama Nabii wa Upendo na uaminifu jina lake Hosea ni la Kiebrania Hoshea ambalo maana yake ni wokovu au msaada,jina kama Yoshua na Yesu yanatokea katika mzizi wa jina kama hilo.
-          Ni wazi kuwa Hosea alikuwa Mwiisrael alizungumza kama ndugu na aliyataja mataifa kama Lebanon,Tabori, Bethel na Samaria
-          Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa alikuwa na asili ya ukuhani kutokana na kutaja kwake maswala mengi yanayohusiana na ukuhani
-          Alikuwa na Mambo mengi ya kukatisha tamaa aliyokutana nayo katika familia yake, Huduma na hali halisi ya Taifa lake.
-          Hosea anazungumza na kuonyesha kwa nguvu upendo wa Mungu kwa Israel licha ya kuwa na uovu mwingi, Dhuluma, mateso, udanganyifu, Rushwa, kukosa uvumilivu, ulevi na maisha ya anasa, Mungu aliwataka warejee kwake.
B.       Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Hosea.
Inakisiwa kuwa kati ya Mwaka wa 750-725 wakati wa utawala wa Uzzia, Jothamu, Ahazi na Hezekia Mfalme wa Yuda na Yeroboamu ii mfalme wa Israel Inaonekana Nabii ananukuu Wafalme wa upande wa Yuda kwa sababu kwanza alikuwa anaamini kuwa walikuwa wafalme wa kweli na warithi halisi wa kiti cha enzi cha Daudi pili wafalme wengi wa Israel waliomfuta Yeroboamu wa ii walioishi muda mfupi sana na kuuawa hivyo huenda majina mengi yangeorodheshwa mfano ni orodha hii ifuatayo;-                            

                                                    Utawala wa wafalme wa Israel 2Falme 14-18

Yeroboamu
Miaka 41
2  Falme 14;23-29
Alikufa
Zekaria
Miezi 6
               15;8-12
Aliuawa
Shalumu
Mwezi 1
               15;13-15
Aliuawa
Manahemu
Miaka 10
               15;16-22
Alikufa
Pekaiya
Miaka 2
               15;23-26
Aliuawa
Peka
Miaka 20
               15;27-31
Aliuawa
Hoshea
Miaka 9
               17;1-41
Alifungwa.

                                    Mwisho wa utawala wa Israel wakachukuliwa utumwani Ashuru

-          Watu wa Israel walikuwa wamekataa kurudi kwa Mungu Pamoja na mahubiri ya Nabii Amosi na matokeo hali ilizidi kuwa mbaya
-          Badala ya kumrudia Mungu watu waliendelea kuwa waasi huku wakiwaua wafalme wakifanya mapinduzi kwa mapinduzi Mafalme Tiglath – Pileser wa Ashuru aliishinda mashariki ya kati na kupanua mipaka yake mpaka Misri na mataifa yoote  yaliyotawaliwa yalitakiwa kulipa kodi kwa waashuru
-          Syria na Israel waliamua kuishambulia Yuda kwa sababu walikataa kuungana nao katika kuasi kulipa kodi kwa Ashuru
-          Hivyo Mfale Hoshea aligoma kulipa kodi na akaomba msaada Misri kuungana nae katika kujitoa chini ya utawala wa Waashuru jambo hili lilisababisha uvamizi wa majeshi ya waashuru huko Israel na kuwahamisha ambapo Hoshea mfalme aliwekwa kizuizini.
C.       DHAMBI YA ISRAEL ZILIKUWA  SURA YA  4-10
*      Kukosa maarifa ya kumjua Mungu Hosea 4;6,11
*      Kiburi 5;5
*      Kutokuridhika 6;4
*      Udunia na kuwa kama mataifa  7;8
*      Rushwa 9;9
*      Kurudi nyuma 11;7
*      Kuabudu sanamu 13; 2,4;11-12.
D.      Upekee wa kitabu cha Hosea na ujumbe wake
-          Hosea ni mojawapo ya kitabu kirefu ukilinganisha na vingine katika Manabii wadogo na kinakaribiana kidogo na cha Zekaria
-          Ujumbe wake unawezekana ulitolewa kwa muda mrefu kiasi kwani kitabu kinaonyesha Upendo wa Mungu kwa Taifa lisilo na uaminifu la Israel na kinatumia maisha ya Mwandishi yaani Nabii Hosea kama mfano hai wa jinsi Mungu anavyojisikia kuhusu watu wake
-          Hosea anaonya  juu ya hukumu inayokuja ambayo inaweza kuepukika kwa kumrudia Mungu tu
E.       Mstari mkuu na mistari ya Msingi.
-          Kiini kikuu cha kitabu hiki ni Pendo la Mungu kwa Israel na hukumu dhidi ya dhambi
2; 19, 4;1, 4;6, 6;6, 7;8, 8;7.
F.       Mgawanyo wa kitabu cha Hosea
-          Zinaa ya Israel ilikuwa ni kukosa uaminifu kwa Mungu sura ya 1-3
-          Hoja za kinabii kutokumcha Mungu na hukumu ijayo isiyoepukika 4-13
-          Kuamini kwa Israel na kusamehewa sura ya 14;
G.      Mchanganuo wa kitabu cha Hosea
a.       Familia ya Hosea na Israel sura 1-3
i.                     Mungu alimuagiza Hosea kuoa mwanamke kahaba hata hivyo kuna mjadala wa kitheolojia kuhusu ukahaba wa mke wa Hosea kuwa ulikuwa ni ukahaba wa aina ipi Zinaa au kuabudu miungu ambako nako kuliambatana na ibada za zinaa? Katika Israel wazinzi walipigwa mawe je ni zinaa ya aina gani?
ii.                    Mungu alitaka kuwafundisha Israel kitu  kwani walikuwa wazinzi kiroho na Hosea alikuwa ndio somo lenyewe
iii.                  Mungu huihesabu tabia ya kuabudu miungu kama zinaa ya kiroho na kwa kuwa Hosea alikuwa mwaminifu kwa mkewe Gomeri ambaye Yeye hakuwa mwaminifu ndivyo na Mungu alivyokuwa mwaminifu kwa Israel.
iv.                  Hosea aliwaita wanawe majina yaliyokuwa yakiashiria unabii.
1.       Yezreel jina hili lilikuwa na maana ya kuwa Mungu “ametawanya au Muangu atapanda” hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha watu wa mji wa Yezreel juu ya mauaji yaliyofanyika Yehu alipokuwa mfalme,Yehu aliagizwa na Mungu kuwashughulikia watoto wa Ahabu lakini aliwashughulikia zaidi ya kiwango kwa sababu ya ubinafsi aliwaua watoto70 wa Ahabu huko Yezreel, Mungu alimwambia Yehu kuwa wanawe kizazi cha nne watamiliki kiti cha enzi, Yeroboamu wa pili alikuwa ni uzao wa tatu na Zekaria mwane ndipo unabii ulikuja kutimia 2Falme 10;30,1-8,Zekaria alitawala miezi sita tu kisha akauawa
2.       Lakini hata Hivyo Yezreel walikuwa na ujumbe mzuri pia  kuwa Mungu hupanda 1;45 yaani pamoja na kuwa wana wa Israel walichukuliwa mateka utumwani Mungu angewarejeza tena katika inchi yao
3.       Lo-Ruhama 1;6-7 mtoto mwingine wa Hosea jina hili maana yake Hakuna rehema
4.       Lo-Ammi maana yake sio watu wangu 1;8-9 majina haya mawili yanatufundisha na kuwakumbusha wana wa Israel na Gomeri juu ya dhambi zao na jinsi walivyolivunja agano lao na Mungu
v.                    Kwa mujibu wa sheria ya Musa wazinzi walitakiwa kuuawa kwa mawe lakini Hosea alimpenda mkewe na Mungu aliipenda Israel hivyo Gomeri na Israel walikuwa wanapewa Muda ili kwamba waweze kubadilika lakini haikuwezekana na hivyo talaka iliwakumba wote
vi.                  Mwishowe Hosea aliamua kumrudia tena mkewe na Mungu alikusudia kuwarejeza tena Israel matukio haya yana mambo ya kutufundisha sisi wa kizazi hiki cha leo
vii.                 Kwa ufupi sura ya 1-3 Inazungumzia maisha ya kielelezo ya Nabii Hosea ambaye anamwakilisha Mungu  Hosea alimuoa mwanamke kahaba anayefanya zinaa kwa sababu hatosheki na mume mmoja hatosheki ashiki zake ni Malaya anafanya zinaa pia kwa ajili ya kupata faida mapato, Huyo ni Gomeri mke wa Hosea anayeiwakilisha Israel, Baada ya kuwa amezaa watoto watatu alimwachia Hosea watoto hao na kwenda kuishi na mwanaume mwingine, wanaume wengine wakamgombea na ikalazimu wamuuze mnadani ndipo Hosea akamnunua  kwa upendo akamrudisha nyumbani.
b.       Ujumbe wa Nabii Sura ya 4-14
i.                     Kuanzia sura ya nne hadi ya 14 Nabii analeta mashtaka ya Mungu kwa wana wa Israel
1.       Anaonyesha jinsi ambavyo hakuna rehema, Hakuna kweli, hakuna kumjua wala kumjali Mungu katika Israel
2.       Kwa kusudi walijiingiza katika Ibada za sanamu na kuabudu miungu mingine
3.       Nabii anatoa wito wa kutubu lakini Israel wanakataa na kuendelea na dhambi zao
ii.                    Kwa kukataa kwao kutubu Nabii analeta ujumbe wa adhabu kwao anaitabiria Samaria kuanguka na Yuda pia wataadhibiwa
iii.                  Mwisho Nabii anatabiri kurejezwa upya kwa Yuda na Israel kuwa taifa moja na nchi moja na kuwa baadae watamtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao bila shaka huu uatakuwa wakati wa utawala wa miaka 1000 ya Kristo Duniani.

MIKA: NABII WA MASIHI
A.      Mwandishi
-          Mwandishi wa kitabu cha Mika ni Mika mwenyewe
-          Jina lake maana yake ni “Nani aliye kama Mungu” yeye alitokea Moresheth-Gath mji mdogo kusini magharibi mwa Yerusalem kilomita zipatazo 40 kwa hiyo Tekoa alikoishi Amosi ni Kilomita 27 hivi kutoka kijiji cha Mika
-          Kuna uwezekano ya kuwa Mika ameitembelea Yerusalem mara nyingi na huko aliona jinsi dhambi ilivyosababisha vilio kwa masikini
-          Katika mahubiri yake alikemea dhuluma ya Yerusalem kwa jamii alikemea sana kama Amosi alivyokemea  huko kaskazini
-          Alijulikana kama bingwa wa kuwatetea masikini au Nabii wa uongozi wa haki yaani Nabii wa Masihi alihubiri kabla na baada ya anguko la Samaria huduma yake inakisiwa kuchukua muda wa miaka kati ya  735-700 K.K. kabla kidogo ya Israel kuchukuliwa utumwani na wakati huu Isaya na Hosea walikuwa Manabii sambamba naye Mika alishughulika sana na watu, Isaya alishughulika na Wafalme.
B.      Historia ya hali halisi ya Yuda.
-          Yuda ilikuwa na wakati wa amani na starehe wakati wa utawala wa Yothamu na hivyo watu walijenga ngome na majumba ya kifahari “Kasri” lakini uovu ulikuwa uimepamba moto
-          Wakati wa utawala wa Ahazia Yuda walilazimishwa kulipa kodi kwa Waashuru na kwakweli ulikuwa mzigo mzito sana kwao na hivyo matajiri walichukua mali za masikini
-          Na mpaka wakati wa Hezekia mfalme Yerusalemu ilikuwa ni kitanda cha moto kisicholalika kwa ajili ya uovu, rushwa utapeli na ufisadi- dhuluma
C.      Upekee wa ujumbe na Kitabu cha Mika.
-          Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu anguko la Yerusalemu na kuchukuliwa utumwani BABELI watu watakuwa walishangazwa kwani Babeli wakati huo ilikuwa bado hata haijajulikana wala kuwadola yenye nguvu Mika 4; 10.
-          Manabii wengi walitabiri pia kuja kwa Masihi akiwemo Isaya lakini Mika alitabiri mpaka mahali atakapozaliwa kuwa ni Bethelehemu Mika 5;5 Mathayo 2;6
-          Mwanzoni Mika alikazia kuhusu utakatifu wa Mungu dhidi ya hali ya uovu wa watu wake, kwani utakatifu wa Mungu unataka utakatifu kwa watu wake, Mika alisisitiza juu ya kumcha Mungu na mahusiano yaliyo mazuri Mika anahitimisha kitabu chake kwa kuonyesha tabia ya Mungu katika Mika 6;8 na kitabu chote kwa ujumla tunaona juu ya tumaini la ujio wa Masihi
-          Na ingawaje atazaliwa Bethelehemu alikuwako tangu milele Mika 5;2 Mika anamwelezea Masihi na kuwa atatawala watu wake Israel kama Mchungaji na kuwalisha  na hii itatimia atakapokuja mara ya pili duniani.
D.      Mstari wa Msingi
-          Mika 5;2 “Lakini wewe Eeh Bethelehemu Efrata uliye mdogo miongoni mwa Yuda….”
-          Mika 6;8 “Amekuonyesha yaliyo mema…”
E.       Mgawanyo wa kitabu cha Mika
-          Hukumu na haki Sura 1-3
-          Mtawala na mabaki Sura ya 4-5
-          Matakwa na kurejezwa upya Sura 6-7
F.       Uchanganuzi wa kitabu cha Mika.
a.       Hukumu na haki Sura ya 1-3.
-          Soma kwa kulinganisha Mika 1;1, Amosi 1;1 na Obadia 1;1. Manabii hawa woote walipokea ujumbe wao kupitia maono waliyopewa na Mungu
-          Mika hakuwa na mafundisho yoyote kuhusu nini cha kusema, maono ya maangamizi yalimjia na akajazwa Roho Mtakatifu na kupewa Maneno ya kusema Mika 1;1,3;8.
-          Alisisitiza  Umuhimu wa ujumbe wake kwa kuuelekeza kwa watu wote 1;2 alimuona Bwana anashuka kwa hukumu akitembelea mahali pa juu  na milima ikiyeyuka chini ya miguu yake na bonde likagawanyika
-          Kumbuka kuwa Biblia inazungumza kwa mafumbo na wakati mwingine waziwazi mahali pa juu huweza kumaanisha Kiburi au milimani ambako ibada za sanamu zilikuwa zikifanyika 1; 6, 3; 12.
-          Unaposoma Mika 1;3-4 na kulinganisha na 2Petro 3;10-15 na Ufunuo 21;1-5 utagundua kuwa hizi ni nabii mbili kwa Mfululizo yaani
i.                     Kuanguka kwa Samaria na Yerusalemu na
ii.                    Kufanywa upya kwa ulimwengu kwa moto
-          Woote Mika na Petro walisisitiza utakatifu katika mtazamo wa kuja kwa Bwana, na kuyeyuka kwa milima kwa uhalisi kunaweza kuwa wakati wa ujio wa pili.
-          Mika alifanya huduma miaka 13 kabla ya Ashuru kuivamia Samaria na aliishi akaona sehemu ya unabii wake ikitimia. Mika alionyeshwa namna samaria itakavyo haribiwa  na Ashuru 1;6-7                              
Bethelehemu mahali ambapo wachungaji waliwasikia malaika akiwapa ujumbe wa Kuzaliwa kwa masihi na kisha kundi la malaika wakaimba Ndivyo panavyoonekana leo ni katika mji huu Yesu Masihi alizaliwa Kama alivyotabiri Mika 5;2 miaka 730 K.K, Picha na maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Rev.Innocent Kamote

-          Mika alimtumia baadhi ya Maneno kwa baadhi ya miji ambayo ingetekwa na kufanyiwa uharibifu alimtumia mtindo wa Maneno kama au kinyume cha jina halisi la mji kuonyesha kile ambacho kingewapata Mika 1;10-14.
-          Beth- le –afra   nyumba ya vumbi
-          Beth eseli - kuondolea tegemeo
-          Moroth -kuondoa Tegemeo
-          Lakishi - mikanda inayofungwa kwa farasi
-          Moresheth – gath zawadi ya kuagia
-          Akzibu- kijito kidanganyacho wafalme
-          Maresha -  kumilikiwa
-          Zaanani -hutotembea
G.      Hukumu kwa Viongozi pamoja na watu 2-3.
-          Mungu aliamini kuwa Viongozi watasimamia ugawanyaji wa ardhi  kwa familia na kuwa urithi wao wa kudumu lakini kwa sababu ya umasikini familia nyingi zililazimika kuuza mali zao ardhi na ilitakiwa mwaka wa jubilee ambao uliazimishwa kila baada ya miaka 50 ardhi zirudishwe lakini watu wenye tamaa walipanga namna ya kuzidi kuwa matajiri kwa kuendelea kumiliki mali za wengine 2;1-2.Mungu anaitikia mipango yao kwa mpango wake 3-4,Pia tunaona sheria ya kuvuna na kupenda ikifanya kazi soma 2;1;3; 2;2,4;2;2,4-5, 2;8,10, 2;9-10.
-          Hata hivyo bado Mungu alikuwa na mpango na watu wake yaani wokovu kwa wale watakaomfuata 2;12-13 Mungu angewasaidia mabaki ya watu wake huko utumwani na angewarudisha katika nchi yao na ya kuwa Masihi atahusika katika kuwaweka huru watu kutoka katika utumwa wa dhambi Mika 2;13
-          Manabii wa uongo walijaribu kumpinga Mika  na ujumbe wake  wakimuonya kuwa asihubiri mambo hayo 2;6, Linganisha na Amosi 7;10-17 Jaribu kubwa walilokuwa nao Manabii hao katika siku zao ilikuwa ni kuhubiri kile watu wanachokitaka watu ili walipwe na kulishwa 3,5,11 kama watajisahau katika hali hii wataanguka katika giza kubwa la kiroho  alisema Mika 3;6-7
-          Katika sura ya tatu hukumu ya Viongozi  inaonyesha pia tunatakiwa kuwa Viongozi wa aina gani  Viongozi katika Israel walipenda uovu, walijitumikia wenyewe ubinafsi,  na hawakuwa na huruma juu ya watu wengine  3;3. Lakini Mika alikuwa amejazwa nguvu na Roho Mtakatifu 3;8 Matendo 1;8
H.      Unabii kuhusu Utukufu sura ya 4-7
Utawala wa Masihi 4-5
-          Tunamshukuru Mungu kwa kuwepo kwa ufalme wake katika maisha ya mioyo ya watu wake lakini tunatazamia ya kuwa siku moja Kristo atatawala katika ulimwengu huu pale Yerusalemu
-          Mataifa hayatapigana tena na wala hawatajifunza vita tena  4;3
-          Mika 4-5 pia inatuambia baadhi ya matukio yatakayokuwako ambayo yatatukia kabla ya utawala wenye utukufu wa masihi.
-          Katika 4;9-10 Mika anatabiri kuchukuliwa mateka  utumwani Babeli na kurejezwa tena
-          Mika 5;1 si ajabu ni  unabii unaojirudia  kwa ufalme wa Yuda na kwa ajili ya Masihi kwa kupigwa Mathayo 26;67,27;30 wakati mstari wa 2 unaonyesha masihi atazaliwa wapi na ya kuwa ni mtawala wa kimungu na mwenye kudumu milele.
I.         Furaha baada ya mateso Mika 6-7.
-          Sura mbili za mwisho zinaonyesha Israel wakiwa katika kipimo cha Mungu, Mungu aliwaita na kuwahoji kwanini wamemuacha wakati amewaonyesha upendo na wema kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
-          Israel walifikiri kuwa wanaweza kumpendeza Mungu kwa sadaka zao  6;6-7
-          Mika 6;8 inaeleza kile ambacho Mungu anakitaka kwa mwanadamu yaani Haki, Upendo, Rehema na kutembea kwa Unyenyekevu na Mungu  kwa maana nyingine kulitii neno lake Yakobo 1;22
-          Mungu aliwashitaki Israel kwa ajili ya dhambi ya uongo, uasi, ibada za sanamu, rushwa, uhaini, 6;10-12;16 17;2-6 na hukumu yake ni anguko 6;16
-          Mika 7;18-20 inatoa suluhisho kwa Israel na ni Pendo la Mungu katika kuwasamehe dhambi zao
SURA YA TATU: WAKATI WA UTAWALA WA BABELI MANABII WA KARIBU NA YEREMIA
8 ZEPHANIAH: NABII WA HUKUMU YA ULIMWENGU

A.      Mwandishi wa kitabu cha Zefania na Tarehe ya uandishi
§  Jina zefania maana yake ni “Yehova amemficha
§  Zefania huenda alizaliwa wakati wa Mfalme Manase na inawezekana ni wakati ambapo mfale huyo aliijaza Yerusalemu kwa Damu ya watu wasio na Hatia kwani aliwauwa watu wengi wa Mungu 2Falme 21;16
§  Inawezekana kuwa wazazi wake walimwamini Mungu juu ya ulinzi wa mtoto wao na hivyo kumpa jina Zefania yaani Mungu amemficha
§  Alikuwa ni moja ya vijukuu vya Hezekia kwa ule ukweli kwamba anatoka katika familia ya kifalme na ndugu wa mfalme Yosia hii iliweza kusaidia kufanya ujumbe wake kusikiwa vema siku zote Mungu pia huitumia historia ya mtu kwa utukufu wake ili kuwafikia ndugu na jamaa
§  Inaaminika kwamba Nyumbani kwao ni Yerusalem kwa sababu alifahamu hali halisi ya pale 1;4 Yeye ni maarufu sana kama Muhubiri wa utakatifu au Mwinjilisti anayewakwa
§  Tarehe ya uandishi wa kitabu chake huenda  ni kati ya Mwaka wa 630-625 K.K
B.      Historia ya Nyuma ya mambo 2Falme 21-23,2Nyakati 30-35.
§  Bwana alimtumia Isaya Mika na Hezekia kujaribu kuigeuza Yuda kwa Mungu na hivyo Israel walipokwenda utumwani Yuda ilihifadhiwa
§  Hezekia alifanya kila jitihada kuangamiza ibada za sanamu lakini Mwanae Manase alirejeza kila kitu ambacho baba yake alikiangamiza ,Alijenga tena madhabahu mahali pa juu na madhabahu za miungu ya kipagani miungu kama Kemoshi, miliconi, Baali na Ashera
§  Alimpa hata mtoto wake jina Ammoni kwa ajili ya miungu ya Misri, Mungu alimtia nidhamu kwa kumuachia achukuliwe utumwani na kufungwa huko  Ashuru 2Nyakati 33;1-12 na baadaye Mungu akamrudisha tena katika ufalme na alijaribu kufanya masahihisho kwa uovu alioufanya ingawaje ibada za sanamu alizozianzisha ziliendelea na kukua wakati wa utawala wa mwanae aliyemrithi ambaye alivitiamoyo kuendelea
§  Yosia mwana wa Ammoni  alikuwa mfale mwema  na Zefania alihudumu wakati wa utawala wake  na huenda alimsaidia kufanya mabadiliko huu ulikuwa ni wakati ambapo waashuru wanaanza kuanguka kama taifa kubwa na Babeli ilikuwa inaanza kupata nguvu kumbuka kuwa Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu kuinuka kwa Babeli
C.      Upekee wa kitabu na ujumbe.
§  Zefania alianza kitabu chake kwa ujumbe wa kutosha kuhusu siku ya bwana na wakati wa hukumu ya mataifa yote Sehemu ya ujumbe wake  ilianza kutimia kuhusu Yuda kuaharibiwa lakini hukumu ilihairishwa mpaka wakati wa Yosia alipofariki kwa kuwa alikuwa mwema na alikuwa na watu waliomgeukia Mungu
§  Zaidi ya hayo unabii utatimizwa wakati wa Dhiki kuu na mwisho ni hukumu ya dunia kuhukumiwa kwa moto
§  Zefania kutabiri kwake kuhusu hukumu ya ulimwengu ilikuwa ni dalili wazi za kuonyesha Mungu ni Bwana wa mataifa yote na kuwa yeye ndiye atawalaye Dunia
D.      Mistari ya Msingi ni
-          1;7 1;14, 2;3.
E.       Siku ya hukumu na Maangamizi 1;1-3;8
1.       Hukumu ya ulimwengu woote 1;1-3,14-18
-          Kiini cha kitabu ni 1;2-3, Na neno siku ya bwana ni wakati wa hukumu
-          Ulimwengu mzima na kila kiumbe kimeathiriwa na dhambi 1;3
-          Kwa ajili ya Yuda Mungu atalitumia  jeshi la Babeli 1;14-18 na siku ya Bwana kwao ilikuwa karibu 1;14 Lakini Paulo anaizungumzia wakati ujao 1Thesalonie 5;2-3
-          Kumbuka matukio ya siku ya Bwana kama yanavyo changauliwa katika kuwa itakuwa ni siku ya;-
a.       Uchungu na kilio 1;14
b.       Kulia kwa mashujaa 1;14
c.        Hasira 1;15
d.       Mgandamizo na kutisha 1;15
e.       Taabu na ukiwa 1;15
f.         Giza na utusitusi 1;15
g.       Mawingu na weusi 1;15
h.       Tarumbeta na kilio cha vita 1;16
i.         Damu kumwagika 1;17
j.         Moto na wivu wake 1;18
k.        Mwanadamu na mnyama kufutiliwa mbali 1;2-3
l.         Dunia nzima kuyeyuka 1;18
m.      Mwisho wa kustukiza kwa ulimwengu 1;18
Kumbuka dalili tatu za mwisho katika k,l,m zitatimia katika mwisho ule uliozungumzwa na Paulo
F.       Hukumu dhidi ya Yuda 1;4-2;3
-          Mashitaka makuu ya Yuda katika kitabu cha Zefania ni kuhusu kuabudu miungu ya uongo
-          Mwanadamu ameumbwa na Mungu kwa kusudi la kuabudu lakini shetani hujaribu kumuharibu mwanadamu kutoka katika kusudi hilo na kuwageuza kuabudu vitu vingine
-          Watu walidai kuwa wanamwabudu Mungu lakini pia waliabudu miungu
-          2falme 23 watu wa Yuda waliabudu kila kitu kinachohusiana na dini za uongo ambayo iliangamizwa na Yosia na wala hawakuogopa 1;18 Mungu aliingiwa na Wivu na hasira yake ikawaka
-          2;1-3 Nabii aliwakumbusha kuwa kama kuna tumaini lolote basi linapatikana katika unyenyekevu na haki na ndipo watu waweza kufaidika katika  katika siku ya hasira ya Bwana.
G.      Hukumu dhidi ya mataifa 2;14-15
-          Hukumu ya Mungu ilikuwa inakuja si kwa Yuda tu bali na kwa mataifa mengine Nebukadreza angeivamia Yuda na mataifa mengine na kustawisha utawala wake Amosi na Zefania walitabiri na ilikuwa inakaribia kutumia
      
        Hukumu ya Mungu kwa mataifa zefania 2;4-15na Amosi 1;6-2;3


Taifa
Hatia
Adhabu
Zefania
Amosi
Ufilisti
Kuchukua mateka na kuuza
Kuharibiwa na ardhi yao kupewa mabaki ya yuda
2;4-7
1;6-8

Moabu

   Na
 Amoni
Ukatili kwa watu wa Mungu,kiburi na kuwacheka
Kuuawa katika vita,kuchukuliwa mateka,kama sodoma na Gomora na ardhi itakuwa kwa mabaki wa Mungu
2;8-11
1;13-2;3
Kushi
Haikuelezwa
Kuuawa kwa upanga
2;12

Ashuru
Kiburi na majivuno
Ninawi uabaki ukiwa na kuchukiwa na watu wote
2;13-15


H.      Hukumu dhidi ya Yerusalemu 3;1-7
-          Katika eneo hili Nabii anawageukia watu wa Yuda na Viongozi huko Yerusalem
-          Wao walikuwa wanawajibika kwa hali ya Taifa na walihukumiwa kutokana na maswala makuu matatu Kugandamiza watu, Uasi na unajisi 3;1 soma 3;1-7
-          Hukumu hizi zingewahusu Viongozi wengi walio madarakani leo
I.         Siku ya wokovu na Furaha 3;8-20
-          Baada ya ujumbe mzito  wa hukumu Zefania anamalizia ujumbe wake  kwa ushindi wa kurejezwa upya wakati wa millennium
-          Ni kweli kuwa hasira zake zitamwagwa lakini 3;8 mabaki kutoka mataifa mbalimbali wataokolewa na kutakaswa 3;9-10
-          Bwana ambaye aliwahukumu atawarudisha nyuma adui zao katika Msalaba na atakuwa pamoja nao 3;15 Bwana ataifanya Israel sifa na furaha.

NAHUMU: NABII WA KUANGUKA KWA NINAWI
A.      Mwandishi wa kitabu cha Nahumu
-          Nahumu maana yake ni mwenye kufariji
-          Hakuna linalofahamika kuhusu wazazi wake au historia yake wala mafunzo yake lakini ukweli unabaki kuwa kwa kuwa ujumbe wake unahusu hukumu  ni wazi kuwa ulitolewa wakati mfupi  kabla ya Uamsho mkubwa uliokuja wakati wa Yosia 627-621
-          Nahumu anajulikana kama Nabii wa kisasi au Nabii wa kuanguka kwa Ninawi  kinakisiwa kuwa kiliandikwa 621 K.K. katika mwaka wa 18  wa Yosia mfalme wa Yuda na kabla ya anguko la Ninawi la mwaka 612 K.K
-          Nahumu anajiita mwekloshi 1;1 na Ekloshi yenyewe Haijulikani iko upane gani ila kuna wanaodhani kuwa  ni kijiji kidogo mashariki ya mto Tigrisi sio mbali kutoka Ninawi na wengine wanafikiri kuwa ni kijiji kidogo huko Galilaya karibu na Kapernaumu jina Kapernaumu maana yake ni kijiji cha Nahumu
B.       Kiini cha kitabu
-          Kiini cha ujumbe wa kitabu hiki ni anguko la Ninawi katika Septuagint kitabu hiki kimewekwa mara tu baada ya kitabu cha Yona  ikifikiriwa kuwa ni ukamilisho wa kitabu cha Yona
C.      Historia ya nyuma ya mambo
-          Ninawi ulikuwa ni mji mkuu wa waashuru
-          Kwa karne nyingi waashuru waliwaonea sana watu wa mashariki ya kati na kumuka ukatili waliokuwa nao katika kitabu cha Yona na angalia Isaya 37
-          Lakini kwa huruma zake Mungu alimtumia Yona Ninawi na watu walitubu na kuokolewa hata hivyo baada ya Muda watu walirudi katika njia zao za uovu vilevile
D.      Mistari ya msingi
-          1;3    - Bwana si mwepesi wa hasira lakini ana nguvu
-          2;13 – Niko kinyume nawe asema Bwana
-          1;7 – Bwana ni mwema kimbilio wakati wa Taabu
-          1;15 – Angalia huko milimani miguu yake yeye aletaye habari njema
E.       Uchanganuzi
-          Hasira ya Bwana 1;1-8 Kuna Maneno sita ya nguvu katika Nahumu  yanayoelezea hisia za Mungu  na majibu yake kwa waninawi Wivu, Kisasi, Hasira, Ukali, Ghadhabu, Kumwagwa  Nahumu 1;6. Ingawa nahumu amesema wazi kuwa mungu ni mwingi wa huruma 1;7 na hivyo rehema zake na upendo wake humfanya asihukumu kwa haraka dhidi yao wamtendao mabaya  lakini wakati unakuja ambapo hulazimika kuadhibu maovu
-          Hasira ya Mungu ni Tofauti na ya wanadamu ya wanadamu huchanganyika chuki kwa waliomuuzi na mwanadamu hawezi kujizuia katika hasira yake  yenye ubinafsi, Hasira ya mungu  haina haraka wala ubinafsi, au isiyozuilika kama ya wanadamu 1;3, haki yake na kisasi chake kiko katika kanini ya kupenda na kuvuna wanadamu na mataifa yote yatavuna kile walichokipanda.
-          Wivu wa mungu ni wa haki unasukumwa na upendo wake kwa watu  na unakusudia kuwalinda kutoka kwao wanapojaribu kuwapeleka watu wake mbali na yeye na furaha aliyoikusudia kwao kumbuka alivyomwambia “Sauli Mbaona waniudhi”
-          Kabla ya hasira za mungu milima ilitetemeka  na vilima viliyeyuka na nchi ilitetemeka 1;6
F.       Upekee wa kitabu cha Nahumu na ujumbe wake
-          Nahumu ndiye Nabii pekee anayeuita ujumbe wake kitabu 1;1
-          Nahumu kama Yona na Obadia wanashughulika na  mataifa adui  waliozionea Israel na Yuda
-          Yona aliwahubiri waninawi huko ninawi lakini Nahumu aliizungumzia Ninawi kwa Yuda hivyo ujumbe wake ulikuwa ni faraja kwa Yuda juu ya ukombozi toka kwa adui zao na watesi wao na hakuna mashitaka kuhusu yuda wala wito wa toba
-          Nahumu kinasisitiza Anguko la Ninawi na kinakazia juu ya Hasira takatifu ya Mungu dhidi ya dhambi
-          Kumbuka kuwa ujumbe wa Ninawi kwa Yuda haukutokana na chuki binafsi za Nahumu kwa adui zao Lakini mungu alimpa ili kuthibitisha agano lake dhidi ya Yuda na kuwakumbusha kuwa Mungu atawapigania dhidi ya adui zao Kumbukumbu 28;1,7.
G.      Mgawanyo
-          1  Anguko la Ninawi linatangazwa sura ya 11;1-15
-          2 Anguko la Ninawi lina changanuliwa sura ya 2;1-13
-          3 Anguko la ninawi  linathibitishwa Sura ya 3;1-19


HABAKUKI: NABII ALIYECHANGANYIKIWA AU MWENYE MASWALI

A.      Mwandishi wa Kitabu cha Habakuki
-          Aliyeandika kitabu hiki anajitambulisha kama Nabii Habakuk i(1:1 ; 3: 1). Hakuna maelezo mengine ya ziada kuhusu maisha ya binafsi au ya familia ya huyu mwandishi yaliyopo po pote katika Maandiko. Alikuwa nabii wa Yuda na inajulikana kutokana na zaburi yake (sura ya tatu) na kwenye maelekezo kwa mkuu wa waimbaji (3:19) kwamba alikuwa wa kabila la Lawi, mmoja wa waimbaji wa hekaluni. Habakuki maana yake Kumbatia
-          .Kitabu cha Habakuki kimeandikwa kwa mtindo wa mazungumzo kati ya Mungu na Nabii.
-          Habakuki aliona kwamba viongozi wa Yuda walikuwa wanawaonea maskini, kwa hiyo aliuliza swali kwamba ni kwa nini Mungu anawaruhusu watu hawa waovu kustawi.
-          Mungu alipomwambia kwamba Wakaldayo wangekuja kuwaadhibu Yuda, Habakuki aliumia zaidi. Hakuelewa ni kwa jinsi gani Mungu angeweza kuwatumia Wakaldayo ambao walikuwa waovu kuliko Wayahudi waovu, ili kutekeleza hukumu dhidi ya watu walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu. Jibu la Mungu lilikuwa kwamba wenye haki wangeishi kwa imani kwa Mungu na kwamba walikuwa na uhakika kwamba Mungu alikuwa anafanya lililo sahihi. Mungu alimwambia Habakuki kwamba punde si punde Wakaldayo wangehukumiwa na kwamba hatimaye haki ingeshinda kwa ajili ya watu wa Mungu. Habakuki anamalizia kitabu kwa zaburi ya sifa.
B.      Kiini Cha kitabu cha Habakuki.
-          Mungu anavyotumia waovu kuadhibu watu wake wanapotenda uovu kwa nia ya kuwarudisha ili wamrudie, lakini hao waovu wakiisha kutimiza kusudi la Mungu, wao huadhibiwa zaidi.
-          Yuda walitenda dhambi ikiwa ni pamoja na kuabudu sanamu, lakini Mungu anatumia Wakaldayo walio waovu zaidi kuwaadhibu na hatimaye Mungu anawaadhibu Wakaldayo.
-           Ilimshangaza Habakuki kuona waovu wakistawi huku wakiendelea kutenda dhambi nyingi wala Mungu hawaadhibu upesi! Habakuki anaelezea imani yake katika mamlaka ya Mungu na katika uhakika kwamba Mungu ana haki katika njia Zake zote.
-           Ufunuo wa Mungu kwa wenye haki na nia Yake ya kuiangamiza Babeli iliyokuwa ovu iliamsha wimbo wa sifa wa kinabii na ahadi kuhusuwokovu katika Sayuni (3:1-19)
C.      Kusudi
-          Kuonyesha kwamba bado Mungu anaitawala dunia hata kama tunaona kwamba uovu unashamiri na ya kwamba iko siku Mungu atauhukumu na kuadhibu huo uovu hatimye kuuangamiza kabisa usiwepo tena.
D.      Wahusika Wakuu
-          Habakuki, Wababeli.
E.       Tarehe
-          Kitabu hiki hakikuwekewa tarehe, lakini bila shaka kilikuwa kipindi cha Wakaldayo.
-           1.Hekalu bado limesimama (2 :20) na huduma ya uimbaji inafanyika (3 :19),
-          2. Kuinuka kwa Wakaldayo kuwa dola inayotisha miongoni mwa mataifa kunatokea wakati wa kizazi hicho (1 :5,6) na kuchinjwa kwa mataifa na Wakaldayo tayari kulishaanza
-          (1 :6,7).Wakaldayo walijulikana na Wayahudi muda mrefu kwa kuyashinda mataifa mengine hadi kuongoza katika dola za ulimwengu wakati wa kuanguka kwa Ninawi 612 K.K. au 606 K.K. na kwa ushindi wao juu ya Wamisri huko Kerkemishi mwaka 605 K.K.
F.       Mgawanyo
-          Swali la Habakuki na jibu la Mungu. (1 :1-11)
-          Swali la pili la Habakuki na jibu la Mungu. (1 :12-2 :20)
-          Maombi ya Habakuki. (3 :1-19)
                                                          
Hekalu lililokarabatiwa wakati wa Herode na kutumiwa Na Yesu na wanafunzi wake kama linavyoonekana katika Nyumba za mfano za kale hii ilitiza kwa sehemu unabii  utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko ule wa kwanza kama alivyotia Moyo Nabii Haggai na Zekaria Picha na maelezo kwa hisani ya Mwalimu wa somo Rev.Innocent Kamote Home Bible library 2007


SURA YA NNE: MANABII WA BAADA YA UTUMWA NA WA KARIBU NA EZRA /NEHEMIA
HAGGAI: MTIA MOYO WA UJENZI WA HEKALU
A.      Mwandishi
-          Hagai ni moja ya vitabu vitatu vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya uhamisho ambavyo ni Hagai, Zekaria na Malaki.
-          Hagai anatajwa kwa jina mara mbili katika kitabu cha Ezra (Ezr 5:1,6:14) kama “mjumbe wa Bwana” (1: 13). Inawezekana alikuwa mmoja wa wale waliorudi kutoka uhamishoni waliorudi Yerusalemu, walioweza kulikumbuka hekalu la Solomoni lilivyokuwa kabla halijaharibiwa na majeshi ya Nebukadneza mwaka 586 K.K. (2:3). Hagai na Zekaria ndio waliowatia moyo wale watu waliorudi kutoka uhamishoni kujenga upya hekalu.
-          Ilikuwa ni mnamo mwaka 538 K.K., miaka kumi na minane ilikuwa imepita tangu Dario alipopitisha amri kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni. Watu walikuwa bado wanashughulika kujenga nyumba zao, hivyo ujenzi wa hekalu la Mungu ulikuwa bado haujakamilika.
-          Kundi la kwanza la Wayahudi lililorudi Yerusalemu liliweka msingi wa hekalu jipya.mnamo mwaka 536 K.K.wakiwa na furaha na matumaini makubwa (Ezr 3:8-10).
-          Hata hivyo Wasamaria na majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa wafanya kazi hata ikafanya ujenzi huo usimame mwaka 534 K.K..
-          Watu waliacha ujenzi wa hekalu, wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Ujumbe wa Hagai ulikuwa kwamba ni wakati wa kujenga nyumba ya Mungu. Hagai akiwa amefuatana na Zekaria (taz.utangulizi wa kitabu cha Zekaria), yeye alianza kumhimiza Zerubabeli na watu wote kuanza tena kujenga nyumba ya BWANA. Chini ya uongozi wa Zerubabeli mtawala na Yoshua kuhani mkuu na kule kuhimiza kwa Nabii Hagai hekalu lilijengwa mnamo 520 K.K. Miaka minane baadaye hekalu lilimalizika kujengwa na kuwekwa wakfu (ling.Ezr 4-6).
B.      Kiini cha ujumbe wa Haggai

-         Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu Wake ndani yake.

-          Kuwahimiza watu kujenga upya hekalu la BWANA na kuwahamasiaha kuyatengeneza maisha yao upya na Mungu ili waweze kupata baraka Zake.
C.      Historia ya nyuma ya mambo
-          Hekalu la Yerusalemu lilibomolewa mnamo mwaka 586 K.K. Mwaka wa 538 K.K,
-          Mfalme Koreshi wa Uajemi alitoa amri Wayahudi warudi ili kujenga upya mji wa Yerusalemu na hekalu.Mwaka 536 K.K.walianza kujenga hekalu lakini ilikuwa vigumu kumalizia kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwa Wasamaria na mataifa ya jirani.
-          Kupitia huduma ya Hagai Zekaria na Yoshua, mwaka 520 K.K., walianza kujenga tena hekalu.Miaka minane baadaye kazi hiyo ya ujenzi wa hekalu ilimalizika.

                           
   Mabaki ya ikulu ya Mfalme Dario Mmedi /Mmuajemi ni katika utawala wake ndipo Nabii Haggai aliandika kitabu chake cha kuhamasisha ujenzi wa Nyumba ya bwana makazi haya ya iliyokuwa ikulu yako mahali paitwapo Persepolis Nyakati za Leo Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya mwalimu Innocent KamoteMchungaji.
D.      Tarehe  ya uandishi
-          Tarehe ya kuandikwa kwa kitabu kwa hiki ni ya uhakika, yaani, mwaka wa pili wa Mfalme Dario wa Uajemi (mwaka 520 K.K. (1:1).
-          Mpangilio wa kihistoria ni wa muhimu sana ili kuuelewa ujumbe wa kitabu hiki. Mnamo mwaka 538 K.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi alitoa amri ikiwaruhusu Wayahudi waaliokuwa uhamishoni kurudi nchini mwao ili kuujenga upya Yerusalemu na hekalu katika kutimiza unabii wa Isaya na wa Yeremia (Isa45:1,3; Yer 25:11-12; 29:10-14) na maombezi ya Danieli (Dan 9).
E.       Wahusika Wakuu
-          Hagai, Zerubabel, Yoshua.
F.       Mgawanyo
-          Wito wa kujenga hekalu. (1:1-15)
-          Matumaini ya hekalu jipya. (2:1-9)
-          Baraka zilizoahidiwa. (2:10-19)
-          Ushindi wa mwisho wa Mungu. (2:20-23)

ZECHARIA: NABII WA MAONO KUHUSU MASIHI;
A.      Mwandishi
-          Zekaria alianza huduma yake mnamo mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa Dario (520 K.K.), miezi miwili baada ya ujumbe wa kwanza wa Hagai. Maana ya jina Zekaria ni “BWANA amekumbuka.”
-          Haijulikani kwa uhakika Zekaria aliendelea kufanya huduma hiyo kwa muda gani.Kwa kadiri ionekanavyo alikuwa kijana (2:4) wakati alipoanza huduma yake.
-           Ido, ambaye ni babu yake (Zek 1:1) alikuwa miongoni mwa wale waliorudi kutoka uhamishoni mwaka 538 K.K.
-          Katika ujumbe wake wa kwanza (1:1-6) Zekaria anawaonya watu ambao ndio kwanza tu walikuwa wameanza kujenga upya hekalu kwamba inawapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia manabii na kudumisha uhusiano wa muhimu na Mungu, wasije wakaharakisha hukumu ya Mungu.
-          Mfululizo wa maono ya usiku (1:7-6:8) yanatia moyo wajenzi ule wakati mgumu katika hatua ya kukata tamaa.
-          Ule utaratibu wa ujenzi ulikuwa umesababisha maafisa wa Kiajemi kufanya uchunguzi na kuandika taarifa ya malalamiko kwa Dario (Ezr 5-6). Huenda Wayahudi walikuwa wakingojea hukumu ya Dario wakati Zekaria akitoa ujumbe wake uliowekewa msingi katika haya maono ya usiku. Mtazamo wa jumla wa mfululizo wa maono haya manane yanawahakikishia wajenzi kwamba Mungu anao mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli. Miaka miwili baadaye, (518 K.K.) suala la kutia katika matendo kutii kufunga liliibuka (7:1-8:23). Zekaria kwa mara nyingine anaangaliza watu kwamba njia ya kudumisha uhusiano sahihi na Mungu ni utii. Kule kufunga ili tu kwamba mtu amefunga ni ubatili.Utaratibu wa kushika sheria kamwe hauwezi kutumika kama njia mbadala ya kuonyesha upendo wa Mungu katika maisha ya kila siku. Sehemu ya mwisho ya ujumbe wa Zekaria (9-14) haukuonyeshwa tarehe. Uwezekano mkubwa ni kwamba ulitolewa baadaye, huenda mnamo mwaka 480 K.K. Hapa mkazo uko katika mpango wa maendeleo wa muda mrefu ukionyesha kusimamishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa tabia ya unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisreli watamtambua Yeye “Yule waliomchoma mkuki” (Zek.12:10) na wataibuka na ushindi. Ndipo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana wa Majeshi.

B.      Kiini cha kitabu cha Zekaria
-          Zekaria anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita mwito wa utii.
-          Anaonyesha jinsi ambavyo watu wanaweza kufanya mambo Si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho Yangu ”asema.( 4:6)..
-           Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masihi.
C.      Historia ya Nyuma ya mambo
-          Huu ujumbe wa mwanzoni unafuatiliwa na maono ambayo yaliwatia moyo wajenzi ambao Zekaria aliwatia moyo kwa kuwaambia kwamba Mungu alikuwa na mpango mrefu kwa ajili ya Israeli.
-          Katika sura ya 7 na 8 Zekaria aliwataka watu wamtii Mungu, hii ikiwa ni njia ya kila mtu kumjali na kumhurumia mwenzake. Mungu alitaka utii kwao katika kuhusiana naye.
-          Sura ya 9 mpaka 14 inazungumzia habari za miezi inayokuja, hukumu ya mwisho na kukua kwa muda mrefu kwa ufalme wa mwisho.
D.      Mahali
-          Yerusalemu
E.       Tarehe
-          520-470 K.K.
F.       Wahusika
-          Hagai, Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.

G.      Mgawanyo

-          Wito wa kuwa watiifu. (1:1-6)
-          Maono. (1:7-6:15)
-          Hukumu dhidi ya maadui wa Israeli. (9:1-8)

MALACHI: NABII WA SIKU ZA UAMSHO
A.       Mwandishi
-          Malaki aliishi katika nusu ya pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo, baada ya ujenzi wa hekalu kumalizika. Malaki ambalo ni neno la Kiebrania ‘‘Malaki’’ kama lilivyo kwenye Kiswahili, maana yake ‘‘Mjumbe wangu.’’. Jina hili ni kifupi cha ‘‘Malakia’’ ambalo maana yake ni ‘‘Mjumbe wa Bwana‘’ (1:1).
-          Jina hili la kitabu limetumika vivyo hivyo kwenye maandiko ya Kiebrania na Kiyunani likionyesha kwamba hili likuwa jina la nabii ambaye ujumbe wake umenukuliwa humu. Hakuna habari nyingine zo zote za kibinafsi zinazofahamika za huyu nabii. Maisha ya kidini ya Wayahudi yalikuwa mabaya :
-           Walikuwa wamekengeuka, wakawa wameoa wanawake wa mataifa mengine, wakaacha kutoa zaka (fungu la kumi) na dhabihu ambayo na sehemu ya Mungu, hata wakawa wamemwacha Mungu, hali ambayo ilifanana sana na ile iliyokuwepo wakati wa Nehemia (444-432 K.K.).
B.      Kiini cha ujumbe wa kitabu cha Malaki
-          Masikitiko makubwa ya Malaki ni uhusiano kati ya Waisraeli na Mungu haukuwa kama ulivyopaswa uwe. Walimwacha Mungu na kumdharau, wala hawakumheshimu inavyostahili, wakashindwa kufuata yale Mungu aliyowaagiza. Matokeo yake hukumu ikawa inawangoja, lakini watu wanaomcha Mungu wamehakikishiwa kuwa wameandikwa kwenye kitabu cha Mungu, nao watafuhia wokovu wa Mungu milele.
C.      Kusudi
-          Kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao, kwa kuwakumbusha upendo wa Mungu (1:1-5) na pia kwamba adhabu yake iko karibu (2:17; 3:13)

D.      Mchanganuo wa kitabu cha malaki
-          Kitabu hiki kinaonyesha kuwa:(1)Hekalu lilijengwa tena (516/515 K.K.), dhabihu na sikukuu zilirudishwa. (2)Ufahamu wa jumla wa sheria ulirudishwa tena na Ezra (kama 457-455 K.K. ; tazama Ezra 7 :10, 14, 25-26) na (3).Kurudi nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea miongoni mwa makuhani na mwa watu pia (kama mwaka 433K.K.). Kutokana na hali hii hali ya kiroho na upuzi Malaki anaouzungumzia kwa karibu vilifanana sana n aile hali aliyoikuta Nehemia aliporudi kutoka uhamishoni Uajemi (kama 433-425 K.K.) ili kuwa mtawala wa Yerusalemu (ling. 13 :4-30).
E.       Mahali
-          Yerusalemu. Malaki, Hagai na Zekaria walikuwa manabii katika Yuda (Ufalme wa kusini) baada ya watu kurudi kutoka uhamishoni.. Hagai na Zakaria waliwakemea watu kwa kutokumalizia ujenzi wa hekalu. Malaki alipambana nao kwa sababu walipuuzia hekalu na kutokumjali Mungu.
F.       Tarehe
-          Yale yaliyomo kwenye kitabu hiki yanaonyesha kwamba huduma ya Malaki ilikuwa kwenye utendaji mnamo sehemu ya pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo. Hekalu lilikuwa tayari limeshajengwa tena upya. Kutokana na wakati alioishi Malaki na yale yaliyomo kwenye kitabu hiki, inawezekana kiliandikwa 557- 525 K.K.
G.      Wahusika wakuu
-          Malaki na makuhani
H.       Mgawanyo
-          Upendo wa Mungu kwa Israeli. (1:1-5)
-          Israeli yamtukana Mungu. (1:6-2:16)
-          Hukumu ya Mungu na ahadi yake. (2:17-4:6)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni