Jumapili, 14 Februari 2016

Umuhimu wa Kutumia Neno la Mungu kwa Halali 4


SURA YA KWANZA KANUNI YA UTII (PRINCIPAL OF OBEDIENCE)

Ni muhimu kufahamu kuwa kuna uhusiano wa karibu kati ya kutafasiri Maandiko na utii. Jinsi gani tunalijua na kulifahamu neno la Mungu inatokana na jinsi ambavyo tunalitii shida kubwa sana ya wanadamu haiko katika kujua bali iko katika kutenda kwa mfano Wafilipi 2;14 inasema “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano” mahali hapo shida haiko katika kuelewa iko katika kutii yaani kulifanyia kazi hilo Mtafasiri mzuri wa Maandiko lazima awe analitendea kazi Neno la Mungu
I. UTII ni njia ya kufungua mlango wa Mungu kuzungumza nasi Mithali 8;17, Yohana 14;21.
A.            Mungu hufunua kweli zake kwa watu ambao wako tayari na wenye mioyo iliyopondeka
·         Kama tunaweza kutii katika kidogo tulichonacho Mungu hutufunulia makubwa kuliko hayo
A.       John 7:17: Kutii mapenzi ya Mungu kunafungua mlango mkuu zaidi wa Ujuzi wa neno la Mungu
II.     Kutokutii kunafunga mlango wa Kuifahamu kweli ya kimungu kwa upana zaidi Matth. 13:10-15, Rom 1:18-25,  5:11-14
III. Ufahamu wa mtu asiyetii unaharibika Mtu anayeishi katika maisha yasiyo na utii hafai kuwa mtafasiri bora wa Maandiko kwa kawaida dhambi na kukosa toba kwaajili ya dhambi hiyo kunachangia mtu asiwe mtafasiri mzuri wa Maandiko Mungu husikitishwa sana na mtu asiyefanya yale aliyoamuriwa kuyafanya 1Samuel 15;2210-23 Mtu anapolikataa neno la Bwana Mungu naye humkataa mtu huyo asiwe mtafasiri halali wa Neno lake, aidha tabia ya kutokulitendea kazi Neno inakufanya kudumaaa na hivyo inakuwa ngumu kufundishika kama watu wamedumaa kiroho
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania alisema ni vigumu kufundisha watu ambao wamedumaa au wasiolitendea kazi neno la Mungu au wasio na utii kwa neno la Mungu hawa watahitaji maziwa ili wakue kwani wamedumaa soma Waebrania 5;11-14, pia kuna hukumu kwa ajili ya watu wanaoijua kweli kisha wakaikandamiza kwa Matendo maovu Warumi 1;18-19, ufahamu wao hauwezi kuwa sawasawa, Warumi 1;21-22 na Warumi 1;24-25 kumbuka kuwa watu wengi walio katika imani potofu wanaufahamu wa kweli kuhusu kweli ya Mungu lakini wanaipuuzia tu  na matokeo yake watu wanashindwa kupambanua iliyo kweli na yasiyo kweli kwa sababu ya maisha yao ya uasi , Aidha watu waasi pia huishi maisha ya ukristo wa mwilini Paulo mtume alizungumza na wakristo wa Koritho na sio watu wasioamini ambao walikuwa na tatizo la kutokuelewa mambo ya kiroho kwa sababu ya tabia ya mwilini 1Koritho 3;1-3 hawa ni watu waliokuwa na wivu, Faraka na maswala ya kisiasa na kwa sababu hiyo pia walihitaji maziwa  wanafungwa na vifungo vya kuijua kweli kwa sababu wako mwilini canal Christians Mwandishi wa Zaburi akasema “mimi ninao ufahamu kuliko wazee kwa sababu nayatii mausia yako” Zaburi 119;100. Kumbe basi utii unasaidia kuwa na ufahamu wa neno la Mungu, Neno la Mungu linaweza kueleweka vema kwa namnazifuatazo
·         Ufahamu wa kawaida wa kiakili “Oida” 
·         Ufahamu wa kawaida wa kisomi au kisayansi “Ginosko” 
·         Ufahamu wa kawaida  mwepesi  “lambano” 
·         Ufahamu unaotokana na Ufunuo wa Roho wa Mungu na shuku ya kiungu “Dechomai”
Ufahamu huu unaotokana na Maneno aliyoyatumia Paulo mtume katika 1 Wakoritho  2 ; 10-16 kufunuliwa kwa Roho Mst 10,kuyajua na kuyakubali Dechomai hii humtokea mtu wa Rohoni, kutokupokea na kuona ni upuuzi hii humtokea mtu wa mwilini hivyo hawezi kufahamu. Hii ni athari ya kuto kumtii Mungu wala Roho wake kwa hivyo mtu asiyetii Hastahili kuyatafasiri Maandiko Neno hilo Dechomai humaanisha pia kupokea kwa moyo na sio kwa kichwa Ginosko, moyoni ni mahali ambapo hisia ,nia ,mawazo na misukumo huanzia hapa ndipo ambapo Roho wa Mungu huanzia kazi zake Hivyo mpokeaji kutoka kwa Mungu Dechomai pia hupokea kwa shauku hata hivyo upokeaji wa neno kati ya muumini na muumini hutofautiana kwa hivyo inahitajika Roho ya Hekima na ufahamu ili kuweza kujua vizuri kwa kufunguliwa macho ya mioyo yetu ambayo kwa hiyo sasa tunapata kujua utajiri wa utukufu na urithi wa watakatifu Efeso 1;17-18,Kolosai 1;9 kutofautiana katika kuipokea kweli kati ya muamini na muamini kunaathiriwa na mitazamo Perception watu wa Beroya walikuwa waungwana kwa sababu hii walilipokea neno kwa moyo na pia walichunguza waone kuwa Maandiko hayo ndivyo yalivyo Matendo 17;11 Hivyo hata akihubiri malaika lazima neno lake lipimwe kama ndivyo lilivyo hii ni kwa sababu mtazamo unaweza kuchangia mtu atafasiri Maandiko isivyo halali mtazamo ni moja ya vizuizi vya kutafasiri Maandiko kitaalamu unaitwa Bias Grid unakufanya usilione neno sawasawa


                     
Mtafasiri wa Maandiko                   Kizuizi cha kutafasiri a Bias grid            Neno la Mungu Biblia

Mtafasiri wa Maandiko asiye na Mtazamo sahii hawezi kulielezea vema Neno la Mungu  kwa ulinganifu sahii mpaka kizuizi kiondoke.

Hivyo anachokifanya Roho wa Mungu sio kuleta kweli mpya bali ni kusaidia kuondoa kizuizi kwa moyo wenye utii au shauku ya kutaka kujua kweli ili kuipokea kweli kwa halali na kutafasiri Maandiko kwa usahii Ufunuo huu huitwa Illumination yaani kuangaziwa kuijua kweli ya neno la Mungu

Athari za mitazamo katika kutafasiri neno la Mungu
Wote tunajua kuwa historia zetu za Nyuma zinaweza kuathiri utafasiri wa Maandiko na wakati mwingine kunaweza kukufanya usitafasiri Maandiko ipaswavyo au sawa na maana iliyokusudiwa na Mwandishi kwa mfano angalia picha hii Mwandishi alikusudia kuchora kikombe lakini unaweza kuona picha ya watu wa wili wanaokaribiana uso kwa uso
Pichani inaonekana picha ambayo Mwandishi alikusudia kuchora glasi lakini unaweza kufasiri zaidi ya glasi kwani unaweza kuona sura za watu wawili wanaokaribiaana uso kwa uso matazamo inaweza kuathiri ufasiri wa kimaandiko Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote
 
IV. Ufahamu wa Mtu mtii utaongezeka
Ni muhimu kufahamu kuwa wale wanaojua kidogo mara baada ya kuipokea kweli fulani Mungu atawapa maarifa zaidi kumbuka wakati Yesu alipozaliwa mamajusi toka mashariki walianza kuifuata nyota wakijua kua inaashiria Kuzaliwa kwa masihi hata hivyo baadaye waliweza kubaini ukweli kuwa masihi amezaliwa Bethelehemu kama yanenavyo Maandiko Mathayo 2;1-5 ni kupitia utii wao kwa Maandiko waliweza kujua kweli na hatimaye kumuona masihi kumpenda kwetu Mungu ni lazima kuambatane na utii makuhani wa kiyahudi walifahamu kuwa masihi azaliwa wapi lakini hawakuwa na utii hivyo kumuona masihi aliyezaliwa kwao halikuwa tukio la mvuto Mtu asiyetii aweza hata kuelekeza neno lakini kwake lisifanye kazi.

SURA YA PILI KANUNI YA UVUVIO (INSPIRARION)
Mwaka wa 303 BK mtawala wa kirumi Diocletian aliamuru Biblia zitiwe moto katika ufalme wake hii iliwasumbua sana wakristo lakini leo Biblia imetefasiriwa katika lugha zipatazo 2000 na mamilioni ya nakala zinapatikana kote ulimwenguni, kuteseka kwa Biblia kulitokana na watu wenye mashaka nayo kuwa ni neno la Mungu au imetungwa tu watu hawa hawakuwa wanaamini kuwa Biblia ina pumzi ya Mungu yaani imevuviwa
Mtu yoyote anayetaka kuingia katika kazi ya kuitafasiri Biblia lazima aamini kuwa imevuviwa ni lazima ieleweke kuwa Biblia imeletwa kwetu kupitia uvuvio na ndio maana unaweza kuifikiria kuwa ni wazo la mtu mmoja ijapokuwa ukweli unabaki kuwa iliandikwa na waandishi wapatao 40 hivi walioishi nyakati tofauti kwa Elimu na nyadhifa tofauti na majukumu na matazamo tofauti lakini inabeba mamlaka kubwa moja na wazo la ukombozi moja na ndio mamlaka ya mwisho ya kufaa kwa watu wa Mungu
Maana ya uvuvio
Neno uvuvio maana yake ni Pumzi ya Mungu Hivyo tunaposema Biblia imevuviwa maana yake ina Pumzi ya uhai wa Mungu 1Timotheo 3;16  neno hilo Pumzi kwa kiyunani ni Theopneutos” ambalo halijatumika mahali popote katika Biblia na wala halitumiki katika Maandiko yoyote ya kiyunani zaidi ya hapa katika Timotheo nane hilo maana yake  Limetolewa na Roho wa Mungu” kwa hiyo linamaanisha pia  ni zao la mwisho ambalo Mungu anazungumza na mwanadamu
Uvuvio ni mchakato ambapo Mungu alipilizia Pumzi yake kupitia waandishi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kuwawezesha watu hao kuandika kile alichokikusudia  kuwafikia wanadamu Bila kukosea hivyo haikuwa wanaandika kwa mapenzi yao bali Roho wa Mungu aliwasukuma kufanya hivyo 2Petro 1;20-21Awali ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama apendavyo mtu mwenyewe.Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

ROHO MTAKATIFU NDIYE ALIYEVUVIA MAANDIKO
     Maandiko yaani Biblia ni kazi ya Mungu na Roho Mtakatifu ndiye muhusika mkuu wa usimamizi wa kazi ya maandiko

Umuhimu wa maandiko
     Neno la Mungu lililoandikwa lilihitajika kwa ajili ya wokovu kwa sababu tunahitaji ujuzi na kweli za wokovu wetu ambao msingi wake ni katika kufa na kufufuka kwake Yesu Kristo kwani hatuwezi kujiokoa wenyewe kupitia matendo yetu mema na mawazo yetu mazuri
     Mungu ni Mungu aliyetamani kujifunua kwa wanandamu yeye mwenyewe na ili kazi yake anayoifanya iweze kujulikana kwa miaka na miaka mpaka wakati huu tulionao leo  watu wanahitaji nakala ya yale Mungu aliyokuwa na ambayo anatenda.Kwa hivyo neno la Mungu ndio njia pekee ambayo kwa hiyo tunaweza kujua na kuelewa na kuamini kweli kuhusu Mungu na mpango wake kwa wanadamu na hivyo neno lazima lienezwe Warumi 10;13-17.

Matendo ya Roho Mtakatifu na Neno lililovuviwa
     2Petro 1;20-21Manabii ambao waliandika neno la Mungu waliongozwa na Roho Mtakatifu walitii na kukubali kuubeba mpango wake kwa wanadamu wengi walijitambulisha kwa jumbe zao kuwa zinatoka kwa Mungu Neno kama Neno la Bwana likanijia limetajwa mara 3,800 katika Biblia hii ikijumuisha neno asema Bwana wa majeshi Roho aliwaongoza katika njia ya moja kwa moja akiwapa wao neno la Mungu
Matendo mengine yalifanywa na watu katika agano la kale kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mfano
·         Gideoni alipiga tarumbeta baada ya kujiwa na Roho wa Mungu Waamuzi 6;34
·         Samsoni alimchana mwana simba vipande baada ya kujiwa na Roho Mtakatifu Waamuzi 14;4
·         Sauli aligeuzwa kuwa mtu mwingine na aliweza kutabiri baada ya kujiwa na Roho wa Mungu 1Samuel 10;6
·         Wanafunzi walinena kwa lugha baada ya Roho Mtakatifu kuja juu yao Matendo 24; 10;46 19;6.
·         Roho alivuvia watu kuandika Neno la Mungu- wengi walioandika neno la Mungu hawakufanya hivyo kwa mapenzi yao walifanya hivyo kwa kuwa Mungu Roho Mtakatifu aliwataka kufanya hivyo
·         Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kutuangazia au kutufunulia neno la Mungu kusudi tulielewe vema,Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza waandishi kuandika neno la Mungu hufanya kazi ya kumuangazia au kumpa ufunuo mtu anayelisoma neno la Mungu akiwa na Moyo uliovunjika na kutaka kujua humpa ufahamu.tafasiri na namna ya kulitumia neno hilo kwa usahii kusoma pekee hakuwezi kusaidia kupata ufahamu kuhusu kweli za kimaandiko 1 Koritho 2;14 Mungu hakumtoa Roho Mtakatifu kwa kusudi tu la kuongoza waandishi bali pia kwa kusudi la kuangazia  neno la Mungu kwetu ili kutimiza kusudi ambalo Mungu amelikusudia liweze kutimizwa hivyo kuangaziwa au ufunuo hutusaidia katika kuyaelewa maandiko,kutafasiri na kuyatumia.

Asili ya uvuvio
     Ni nini maana ya neno uvuvio? Kwa bahati mbaya  si makanisa yote yanakubaliana na wazo la uvuvio. Kwa miaka mingi sana kumekuweko na hoja mbalimbali na mawazo mabalimbali yatolewayo kuhusu uvuvio wakati mwingine yana ukweli lakini yanakuwa magumu kuelezeka.
A: Mawazo mbalimbali yasiyo sahii sana kuhusu uvuvio
     Uvuvio Asili au Ufahamu wa kupita kawaida intuition theory
Wao huamini kuwa uvuvio ni tendo la kawaida la uwezo wa kufahamu ulio juu ya viwango vya kawaida wao huamini ni uwezo wa kawaida wa binadamu kuwa kwa uwezo wa asili anakuwa na viwango vya juu vya ufahamu ambapo huweza kupata kweli za rohoni.
Udhaifu wa wazo hili
     Hufanya uvuvio wa kibiblia uwe hauna tofauti na maandiko yoyote ya kawaida yaliyoandikwa kwa viwango vya juu kama yale ya akina Shake speare na nyimbo kuu za kanisa, Hii inachanganya kati ya kazi za Roho mtakatifu aktika kuvuvia na kuangazia au kufunulia,Kuangazia hakuhusiani na kuleta kweli mpya bali kuielewa kweli ambayo tayari imekwisha funuliwa katika neno
     Uvuvio wa baadhi ya maandiko tu Partial inspirations theory
Wao huamini kuwa Mungu alitoa uwezo uliohitajika na wa kuaminika katika kulileta neno la Kweli la Mungu kwa waandishi walioamriwa kuandika kwa hivyo iliwafanya wasikosee katika baadhi ya mambo ya imani lakini si katika mambo mengine mfano waliweza kukosea katika maswala ya kihistoria na kisayansi
     Uvuvio wa mawazo na sio maneno
 Wao huamini kuwa Mungu alivuvia wazo la ufunuo fulani lakini aliwaachia wanadamu hao kuamua kuwa watayaandika vipi. Dhana ya wazo hili si sahii ni vigumu kufikiri wazo kisha ukaandika tofauti,wazo linaweza kutafasiriwa vizuri kwa maneno hivyo tunaamini kuwa maneno yalivuviwa na sio swala la mawazo.
     Uvuvio  Huria
Hawa huamini kuwa Biblia ina maneno ya Mungu hii ina maana kwamba pia yako maneno ya kawaida ya watu ambayo yamechanganyika, wanaamini kuwa ni kitabu hasa cha kidini lakini kuna Historia,Habari,vizazi,mashairi ya kimapenzi,mipangilio na mambo yasiyopangiliwa wala kujali mtiririko maalumu au kamili. Dhana hii  inataka kuhatarisha kwani ina maana kuwa waandishi walijiamulia tu wapi waandike wapi ni uvuvio wapi hawakuvuviwa wapi Mungu anazungumza na wapi mwanadamu anaweka mkono wake

     Uvuvio wa Imla
Hawa huamini  kuwa manabii walipopokea uvuvio wa kuandika waliandika moja kwa moja kile ambacho Mungu alikuwa akikisema hii inamaanisha wao walikuwa kama kalamu tu,Roho aliwavaa kiasi ambacho hawakuwa na uhuru wao wenyewe isipokuwa kuandika kile Mungu anachokusudia  kwa hivyo huamini kuwa kila neno lilitoka moja kwa moja kwa Mungu na hivyo wao walifanya kazi kama mashine tu Dhana hii siyo sahii kwani Mungu alitumia watu na sio mashine au vifaa,Mungu hakuwafanya wasiwe na ubinadamu wao hivyo si kila kitu waliandika si kama bomba la kupitishia moja kwa moja kile Mungu alichokisema lakini waliandika kile ambacho Mungu alikuwa akikiweka katika mioyo yao 

B; Mawazo Mbalimabli sahii kuhusu uvuvio
·          Uvuvio shirikishi-Uvuvio lilikuwa tendo la Roho Mtakatifu kwa waandishi akifanya kazi pamoja nao na kazi yao ilikuwa ni kusikiliza na kutii na kuandika
·         Uvuvio ulikuwa ni muongozo wa Roho mtakatifu kwa waandishi akiwaongoza katika kuchagua nini cha kuandika na maneno ya kuandika
·         Roho mtakatifu aliwalinda waandishi kutoka katika kukosea na kuruka uvuvio huu ulihusu kile kilichoandikwa na haikuwa lazima yawe mawazo au fikra
·         Mungu aliwafanya waandishi kuwa wafanya kazi pamoja naye  akitumia misamiati yao,mitindo yao ya uandishi na uzoefu wao katika kuzipeleka kweli
·         Maandiko yamevuviwa kwa sababu ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakartifu kupitia waandishi yeye aliwaongoza katika kazi nzima ya uandishi ili kwamba kweli ya Mungu iweze kunukuliwa katika Biblia kama neno kamili la Mungu
      C; Kweli halisi
·         Uvuvio ni msingi wa kuaminika kwa Biblia na hapa tunaizungumzia Biblia yoote
·         Biblia nzima kwani imevuviwa ni sahihi haina makosa na ni halisi haijatiwa mkono
·         Ni sahii katika maswala yoote ya kihistoria au kisayansi na maadili na maswala ya mafundisho kwa wanadamu
·         Ukweli huu ni kwa maandiko yoote katika Biblia bila kuwekea mipaka baadhi ya mafundisho yake
D; Tafasiri sahii
·         Neno lina mawazo mbalimbali kuhusu Mungu,Kristo,Msalaba,Ufufuo na ubatizo wa Roho Mtakatifu
·         Ina nukuu halisi na tafasiri sahii kuhusu kweli nyingi
·         Ndiyo inayotupa ukweli na muongozo sahii kwa ajili yetu
       E; Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli na nguvu.
·         Mungu ni Mungu mkamilifu na mnyoofu katika njia zake
·         Yesu ni Kweli
·         Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli
·         Kila kinachozungumzwa katika maandiko kuhusu Mungu,Yesu na Roho Mtakatifu  ni cha kweli Biblia inatuambia kweli zote zinazomuhusu Kristo na Mungu na kile ambacho Yesu alisema kuhusu Roho Mtakatifu ni halisi Roho anabeba ushahidi huo
Mamlaka Ya Roho Mtakatifu
     Uvuvio unaifanya Biblia kuwa kitabu pekee ambacho ni muongozo wa kweli wa imani na maisha

Mamlaka ya Biblia
     Imefungwa pamoja na mwanadamu inajua mawazo yake ,dhamiri yake moyo wake na matakwa yake na inamuongoza katika imani sahihi, aidha Biblia ina njia sahii na muongozo sahii Roho aliivuvia  na analitumia neno kuwa muongozo wa maisha yetu,Jukumu letu ni kulisoma, kulitafakari na kulitendea kazi Roho pekee anajua mapenzi kamili ya Mungu na kwa msingi huo anajua ni namna gani atuongoze na amechagua maandiko yawe Muongozo wetu kwa kuyavuvia.

Andiko huua
     Ukitumia akili zako tu kutaka kuyafahamu maandiko utaharibikiwa wengi wanaofuata yaliyoandikwa tu bila msaada waRoho Mtakatifu wameishia katika ufarisayo uliokithiri au uhuru usio na mipaka
Msingi wa Kumtegemea Roho katika Kuyafahamu maandiko
     Yesu aliyajua maandiko na alifahamu kuwa yanaongoza lakini alitaka watu wayafahamu kwa usahii kwa hivyo alileta tafasiri sahihi kwa matumizi ya neno,Roho Mtakatifu anayajua maandiko na hutusaidia kuichunguza Biblia kupata muongozo unaohitajika,Hivyo basi tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu katika kuielewa Biblia vema na kuitii,Tunahitaji kufikiri zaidi ya andiko moja kuelewa lipi jema na lipi baya

Roho Mtakatifu hutumia neno.
     Baadhi ya watu hujaribu kumfuata Roho Mtakatifu bila kukubaliana na neno au mamlaka ya Biblia. Kifaa kikuu Roho Mtakatifu anachokitumia katika kutuongoza ni maandiko yaani Biblia, Neno la Mungu pia huitwa upanga wa Roho kwa hivyo basi Neno ni silaha ya pekee ya Roho Mtakatifu ni kupitia neno na Roho Mtakatifu sisi nasi tunaweza kuwa nyenzo yake Roho husimama na neno na hajipingi mwenyewe

Biblia ni nakala iliyovuviwa
Makanisa yote ya Kiinjili yanakubali kuwa Biblia imevuviwa yote ingawaje inachohitaji ni matumizi mazuri au kuitumia kwa halali 2Timotheo 2;15, hii ni kwa sababu Biblia ina nakala sio tu maneno ya Mungu  na mitume na malaika lakini pia kuna maneno ya  shetani wazushi,na hata mapepo,Aidha Mungu aliona anukuu matukio yote yatakayomfaa mwanadamu mafanikio yake na kushindwa kwake ufunuo kwa mwanadamu na uongo wa wanadamu waandishi wa biblia walivuviwa kuweka nakala zote hizo ili kwamba Mungu atusaidie kuelewa nini kilizungumzwa Kwa mfano Petro alisema Hata kama wote watakukana mimi sitakukana  kamwe Mathayo 26;33 usemi huu umevuviwa jibu ni ndio na sio ndio ni kwa sababu Roho alimvuvia mathayo kuliweka  kwa ajili yetu ili kwamba tujifunze kupitia makosa ya Petro kwa hivyo Mathayo 26;33 imevuviwa na  ni kweli Petro alisema ingawaje Petro mwenyewe hakuwa amevuviwa kusema hayo alichokisema ni uongo  Yesu alitaka kumsaidia Petro kuhusu ujasiri wake na kujiamini katika kile alichokisema  lakini Petro  hakuweza kuona  kiburi cha kujiamini kwake alichokuwa nacho kwa hivyo kunukuliwa kwa usemi huu wa petro  kumevuviwa ingawaje usemi wenyewe ni uongo

Kuvuviwa kunaifanya Biblia yote iwe
·         Inafaa kwa Mafundisho na kusahihisha  na kumfanya mtu wa Mungu awe kamili apate kukamilishwa kwa kutenda kila tendo jema 2Timotheo 3;16
·         Inafaa kwa huduma Warumi 15;4 hii ikiwemo agano la kale
·         Inafaa kwa mafundisho na kwa matumizi ya mtu binafsi
Pamoja na sababu hizo za msingi hapo juu na ujuzi kuwa neno la Mungu klimeviviwa bado hatuwezi kutumika kila andiko vyovyo te tutakavyo maandiko yana faa kwa mafundisho lakini pia si kila andiko linafaa kwa mafundisho hivyo tunapaswa kuwa makini katika matumizi ya maandiko kwa mfano Nyaraka nyingi ziliandikwa kwa kusudi la kufundisha lakini ukitoa salamu,maswala binafsi ya waandishi,na tamaduni zisizoweza kuhamishika kwetu mengi ya yanayobaki hutusaidia kwa ajili ya mafundisho na tunapata mafundisho mengi katika nyaraka kwa kuwa hutafasiri injili kwetu
1Petro 5;14, Salimianeni kwa Busu takatifu kwanini hatuwezi kujenga fudnisho katika andiko hili?

Injili na kitabu cha matendo viliandikwa kwa kusudi la kutupa sisi historia kuliko mafundisho ingawaje yako mafundisho tunayoweza kuyapata kutoka katika yale aliyoyafundisha Yesu na mitume ingawaje bado inatupasa kuwa makini ili tusitunge mafundisho yaliyolalia kwenye historia
Kwa mfano huwezi kuweka Fundisho katika Marko 11;2, kuhusu kumfungua mwana punda asiyepandwa bado pia Mathayo 10;9,Yohana 21;18 Matendo 4;32-33 karibu maandiko yote hayo hapo juu hayajajirudia na hivyo huwezi kutengeneza fundisho

                                     
Angalia Mtu anayetumia andiko moja lenye utata kufanya fundisho hawezi kuwa salama kama anayetumia maandiko yenye ushahidi huyo anakuwa kama aliyekalia stuli yenye miguu minne ukitumia nadiko moja imekula kwako! na nirahizi kuanguka lakini ukikalia ya miguu minne uko salama


 KUNOA UPANGA
 
KANUNI YA KUFAHAMU HISTORIA YA ANDIKO (CONTEXT)

A.      Ni ni maana ya historia ya andiko?
Neno kufahamu historia ya andiko limetokana na neno la kilatini Context ambalo ni muungano wa Maneno mawili “Con” na “Textus” ambalo maana yake ni weave together yaani kukusanya pamoja maana ya kila andiko au mstari aya kulingana na historia yake ya nyuma na mazingira ya kawaida
Historia ya andiko yaani Historical context inahusu mambo ya muhimu na msingi kuhusu mazingira ambayo kwayo andiko linatokea kwa msingi huo ili mtu aweze kuwa mtafasiri mzuri wa andiko au Maandiko anapaswa kuijua historia ya Maandiko hayo aelewe mambo muhimu ya msingi yafuatayo
·         Mwandishi na wakati au tarehe ya uandishi
·         Watu aliokuwa akiwaandikia ni akina nani
·         Tamaduni zao zilikuwaje na desturi zao zilikuwaje
·         Mwandishi alikuwa akishughulikia tatizo gani
Huwezi kumchunguza kanga na kumuelewa kupitia unyoya wake mmoja tu itakupasa kuwa na kanga mzima ili kuweza kumuelewa vema kwa msingi huo huwezi kulielewa vizuri andiko bila kujua limetokea katika historia gani

B.      Namna ya kuchunguza Historia ya andiko
Kwa ujumla tunasema kuwa kutafasiri Vitabu vya Nyaraka ndio swala gumu zaidi kuliko kutafasiri vitabu vya Injili na kitabu cha Matendo ya mitume kwa msingi huo tutaangalia zaidi namna ya kutafasiri nyaraka ingawaje pia huko mbele tutashughulikia swala la kutafasiri Unabii kwani nalo pia ni swala gumu, Ni muhimu kufahamu kuwa kuna hatua kuu tatu za kuchunguza historia ya andiko na swala hili sio jepesi ni swala gumu mambo ya msingi unayopaswa kujiuliza ni pamoja na
1.       Jiulize kuhusu Mwandishi
·         Ni nani
·         Aliandika lini
2.       Jiulize kuhusu walengwa waandikiwa
·         Ni akina nani?
·         Walioishi katika mji gani na mji huo ulikuaje?
·         Walikuwa watu wa jamii gani wayahudi au mataifa na hali zao zilikuwa za namna gani matajiri au masikini
·         Wana uhusiano gani na Mwandishi
3.       Chunguza ni tatizo gani Mwandishi alikuwa anajaribu kulitatua kupitia kitabu chake
·         Tatizo siku zote litakusaidia kujua kiini cha Mwandishi na kitaakisi waraka mzima au kitabu husika
Kwa mfano ni namna gani tunaweza kujua historia ya Maandiko katika 1Wakoritho?
1.       Kuhusu Mwandishi
·         Alikuwa ni nani jibu ni Paulo mtume
·         Aliandika 1Koritho kati ya Mwaka wa 56 B.K hii ni baada ya Kuweko pale Efeso kwa miaka mitatu Matendo 20;31 Ikorotho 16;5-8
2.       Walengwa wa waraka huu ni
·         Wale waliomwamini Mungu huko Koritho
·         Koritho ulikuwa mji wa bandari katika bahari ya mediteranian na ni mji uliokuwa unakaliwa na jamii ya wapagani na ulikuwa maarufu kwa kuabudu miungu na tabia za uasherati na uchafu wa kingono.
·         Hali ya mji wa koritho ulikuwa ni mchanganyiko wa wayahudi wachache na wayunani wengi 1Korittho 6;9-11,8;10,12;13 na watu wake walipenda Hekima na maarifa 1;18-2;5,4;10,8;1-13 na walikuwa watu wa kujivuna sana
·         Mwandishi ndiye aliyewahubiri injili Matendo 18;1-18
3.       Matatizo aliyokuwa akijaribu kuyatatua Mwandishi kupitia kitabu chake ni
Ø  Kulikuwa na Faraka na migawanyiko 1Koritho 1;10-4;21
Ø  Kulikuwa na zinaa isiyokuwa ya kawaida 5;1-13
Ø  Kulikuwa na maswala ya wakristo Kushitakiana mahakamani 6;1-11
Ø  Kulikuwa na matatizo ya uasherati watu walikua wakifanya zinaa 6;1-11
Ø  Kulikuwa na tabia mbaya katika maswala ya ndoa 7;1-24
Ø  Kulikuwa na tatizo kuhusu wanawali 7;25-40
Ø  Kulikuwa na tatizo la vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu 8;1-11;1
Ø  Kulikuwa na tatizo la wanawake kutokuvaa Vilemba 11;2-16
Ø  Kulikuwa na matumizi mabaya ya meza ya bwana 11;17-34
Ø  Kulikuwa na matumizi mabaya ya karama za rohoni 12;1-14;40
Ø  Kulikuwa na mafundisho potofu kuhusu Ufufuo 15;1-58
Ø  Swala la kuwasaidia masikini huko Yerusalem 16;1-11

Wapenzi Biblia ni neno la Mungu tunapaswa kulisoma na kulitii wako watu wanaosema kuwa unahitaji kuisoma na kuitii tu na wala usiitafasiri hii ni sawa lakini ni uongo kwani kila mtu hutafasiri kwa asili kile anachokisoma unaposoma andiko unajaribu kujua kuwa Mwandishi alikuwa anamaanisha nini? Kule kujiuliza ili uweze kuelewa ndio kutafasiri kwenyewe
Biblia ni neno la Mungu limetolewa kwa wanadamu katika nyakati tofauti kwa historia tofauti kwa kuwa Mungu amechagua kuzungumzia na wanadamu kwa Neno lake alizungumza na mwanadamu halisi lakini kwa wakati halisi, kwa Matukio halisi, kwa historia halisi kwa hivyo lazima litafasiriwe kwani neno limekuja kwa tamaduni tofauti na vizazi tofauti na ndio maana ndani ya Biblia kuna Mashairi, Mithali, Nyakati, Mifano, Hadithi, Sheria, Unabii, Nyaraka, injili na maswala ya Ufunuo.
Mungu alikusudia tuelewe katika lugha zetu na mazingira yetu
Na anazungumza nasi kwa namna mbalimbali katika nyaraka utagundua kuwa nyaraka nyingi ni  OCCASIONAL yaani zimetokana na Matukio fulani kwa asili kwa hivyo ziliandikwa kwa sababu ya msukumo fulani aidha kutoka kwa walengwa au Mwandishi kwa hivyo ni lazima ujue
·         Kwanza Historia  ya wakati ule ilikuwaje There and then
·         Tatizo au mazingira na kujiuliza Mwandishi alimaanisha nini alipokuwa akijibu hoja za wakati ule then and there
·         Kile alichokuwa akikijibu Mwandishi ni neno la Mungu kwa watu wa wakati ule na kwa wahusika halisi wa wakati ule
·         Je wakati huu sasa Mungu ansema nini nasi? Here and Now kwa hivyo leo tunatumiaje lile neno katika wakati wetu hapa ndipo Hermeneutics inapotenda kazi
Kama hili halina umuhimu basi Hebu jaribu kuwaza wale wafanya kazi katika Mathayo 20;1-16 waliolipwa Dinari kama mshahara wa kutwa wa kazi  je leo hii tutalipwaje kwa Siku  kwa hivyo ni muhimu kujua Historia ya kila kitabu na sababu kwanini kiliandikwa
Tafasiri kwa kuzingatia pia mazingira ya aya husika Literal context
Mazingira ya andiko au aya ni mazingira ambayo yanalizunguka andiko unalotaka kulifasiri mara nyingi Maandiko hayo huwa na Vifungu vya Maneno na sura kwa hivyo kumbuka kuwa vifungu ni sehemu ya sura na sura ni sehemu ya kitabu na kitabu ni sehemu ya Biblia kwa msingi huo unapolichukua andiko tu na lifasiri bila kuzingatia mazingira yake unaweza kusababisha madhara ni kama kunyofoa uzi katika gauni unaweza kuharibu vyote gauni na nyuzi pia kwa sababu vyote kwa pamoja ndio hufanya gauni.
Andiko linapochukuliwa pekee nje ya mazingira husika ni silaha ya shetani na ameitumia kudanganyia wakristo wengi angalia Mathayo 4;5-6 hapa shetani aliitumia Zaburi ya 91;11-12ambayo inasema hivi “Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao atakuinua juu, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
 Sasa kuna namna tano za kuchunguza mazingira ya andiko
1.       Jiulize kuwa andiko unalolisoma limetokea kitabu gani na nini somo kuu la kitabu hicho
2.       Jiulize andiko unalolitumia linatoka kifungu gani?
·         Ni Maandiko mangapi kifungu hicho kinayaweka pamoja?
·         Chini ya kifungo hicho kuna somo gani?
·         Je kile unachotaka kukihubiri ndicho kinaelezwa na vifungu hivyo?au na wazo zima la kitabu?
3.       Jiulize pia kuhusu vifungu vidogo katika mazingira ya andiko husika
·         Kuna hali gani au ahadi gani
·         Kuna tatizo au suluhisho lielezee
·         Kama kuna mfano nini maana kuu ya mfano huo
4.       Fupisha kifungu kizima kwa Maneno yako mwenyewe katika sentensi moja kwa kila kifungo
5.       Jiulize mtu anapoyatumia Maandiko hayo je kuna
·         Maneno halisi ya andiko husika eleza
·         Mwandishi alimaanisha nini katika migawanyo husika
·         Kitabu kilimaanisha nini
Mfano sasa Zaburi ya 91; 11-12
Zaburi nyingine zina waandishi na zina Matukio fulani lakini Zaburi ya 91 hijulikani Mwandishi hivyo tutaendelea
1.       Kiini kikuu cha zaburi ni Kusifu na kumuabudu Mungu
2.       Zaburi hii ina mistari yake inatoka katika kifungo cha mstari wa 1-16
·         Zaburi 91;1-16
·         Somo ni kuhusu ulinzi wa Mungu
·         Wazo zima la kitabu ni kumsifu Mungu na zaburi hii inasisitiza  sababu maalaumu za kumsifu Mungu
3.       Mazingira ya andiko husika yako hivi
·         Kuna ahadi lakini ina neno kama kwa hivyo kuna ahadi za ulinzi wa Mungu lakini kama mtu ataendelea kukaa na Mungu
·         Tatizo lililoko ni hatari katika maisha kuna nyoka, mitego, wapiga mishale lakini suluhisho lake ni ulinzi wa Mungu Zaburi 91;1-2,9
·         Kuna mfano wa kuku anavyofunika vifaranga vyake vifaranga hupata pa kukimbilia lakini kama tukikaa kwake tunayo makimbilio
4.       Kwa ufupi wale wanao mwamini Mungu na kukaa ndani yake hawataogopa wakati wa mabaya Bwana atakuwa ulinzi wao na kimbilio lao
5.       Maneno halisi ya andiko husika
·         Shetani aliruka neno kukulinda katika njia zako zote
·         Mwandishi alimaanisha katika mapito yetu yote hivyo kujirusha kutoka katika kinara cha hekalu sio kulindwa katika mapito yetu yote
·         Kusudi kuu la kitabu ni kumsifu Mungu je unafikiri kujirusha kutoka katika kinara ndio kusudi la kitabu?
·         Kwa hivyo shetani hakutumia Maandiko kwa halali na hivyo alitaka kumtia Yesu katika mazingira ya kumjaribu Mungu.



KANUNI YA KUCHUNGUZA MAANA YA ANDIKO NA MAMBO YALIYOMO NDANI YAKE (CONTENT)
A.      Umuhimu wa kuchunguza kilichomo ndani ya andiko unalolitafasiri
Kanuni ya kuchunguza maana ya andiko na kile kilichomo ni kanuni ya msingi sana wakati wa Yesu Kristo Duniani mwishoni mwa huduma yake aliwahi kukaririwa vibaya na wanafunzi wake na uongo ukawa duniani kwa karibu zaidi ya miaka 40 hivi uongo huo ulivumishwa kutokana na Yohana 21;21-23 ambapo inasemekana kuwa baadhi ya wanafunzi walifikiri kuwa Yesu alimwambia Yohana ya kuwa hatakufa maandiko haya husema hivi;- ” Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamwuliza Yesu, “Bwana na huyu je?’’ Yesu akamjibu, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!’’ Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba,“Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, imekupasaje wewe?’’
       Hatuna shaka kuwa wanafunzi walikuwa watu waaminifu hata pamoja na kusambaza uvumi kuwa Yohana hatakufa lakini uaminifu pekee hautoshi katika kuzuia uongo usisambae kwa msingi huo Maandiko yasipotafasiriwa kwa kuzingatia kanuni zake uaminifu pekee pia hautoshi kuzuia kuenea kwa uongo
     Wasomi wanaamini kuwa injili ya Yohana ndiyo ya mwisho kuandikwa na iliandikwa baada ya miaka 40 hivi na ndipo Yohana alipoweza kuitumia nafasi hiyo kuelezea kweli kuwa Yesu hakumaanisha kuwa yeye hatokufa kwa hivyo unaweza kuona athari ya uongo wa dhambi ya kutafasiri Maandiko vibaya inavyoweza kuchukua miaka na kuleta athari mbalimbali kwa msingi huo basi ni lazima mtafasiri wa Maandiko azingatie nini kimo ndani ya andiko analotaka kulitafasiri
B.      Chunguza mamneno yaliyomo ndani ya andiko unalotaka kulihubiri
Kwa kawaida kuna sheria kuu tatu za kuweka akilini kila unapotaka kutafasiri Maandiko hapa tunamaanisha ni lazima utafute maana ya kila neno unalokutana nalo katika sentensi husika na uchunguzi lina uhusiano gani na mangineyo hii itatusaidia tusiharibu mambo kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa nyakati za kanisa la kwanza waliovumisha kuwa Yohana hatokufa kwa sababu walitafasiri vibaya alichokisema Bwana Yesu.
1.       Chunguza Neno unalojua kuwa hulijui
      Unaposoma Maandiko unaweza kukutana na neno ambalo hulijui hii peke yake ni kama Tahadhari inayokuambia kuwa hakuna daraja mbele na hivyo unapoendelea na safari basi utapata ajali Simama na zingatia kwanza kutafuta maana ya neno usillolijua liangalie linasomeka vipi katika matoleo mengine ya Biblia au fuatilia katika Kamusi unapojaribu kuliruka neno ambalo hujalifahamu basi nakuhakikishia kuwa utatafasiri vibaya Maandiko
2.       Chunguza Neno unalofikiri kuwa unalijua
     Wakati mwingine kuna neno ambalo unadhani kuwa unalijua kabisa pia unapaswa kulichunguza  kwa sababu kuna uwezekano ukawa hulijui au limetumika tofauti na unavyofikiri kwa mfano wote tunajua neno Imani vema si ndivyo sasa jiulize limetumikaje katika Warumi 14; 23 na Wagalatia 1;23 Hapo utagundua kuwa neno imani lile unalolijua hapo limetumika vinginevyo kati ya Warumi na Wagalatia
3.       Jiulize swali linalokusukuma kutafasiri Maandiko na kisha tumia kile ulichogundua
     Je umewahi kusoma kifungo cha Maneno kisha ukajikuta unakirudia tena kwa sababu ulikuwa hujafikiri? Kumbe inawezekana mtu kusoma kisha asielewe? Msomi mzuri wakati wote hujiuliza swali kuwa jambo hili lina maana gani? Kisha husoma tena ili kuona kama umeelewa vizuri
Kwa mfano sasa Tuchunguze Yohana 21;21-23
Yesu alisema nini? Kimsingi alikuwa akimweleza Petro kile ambacho kingempata mwishoni mwa huduma yake na kumtabiria mauti yake itakavyokuwa lakini kama ilivyo desturi ya wanadamu tunapenda sana kujua na mambo ya wengine Hivyo Petro aliuliza Je kuhusu Yohana itakuwaje? Yesu hakutaka kumpa Petro faida ya kujua maswala ya wengine hivyo alimjibu Hata kama au hata ikiwa nataka huyu aishi hata nitakaporudi wewe inakuhusu nini? Kimsingi Yesu alivunja moyo hali ya kupenda kujua mambo ya wengine au mipango ya Mungu juu ya mtu mwingine wewe pokea kile Mungu alichokujalia na sio kutafuta mwisho wa wengine utakuwaje? Unaona Kumbe Maandiko yasiposomwa vema yanaweza kupotosha maana iliyokusudiwa

Chukua mazoezi fuatilia maana za meneno haya
-          Mwanzo 30;14 Tunguja
-          Wagalatia 4;6 Abba
-          Mathayo 25;14-30 Talanta
-          Marko 5;41 Talitha koumi
-          Marko 7;34 Ephatha
-          Marko 15;34 Eloi, Eloi lama Sabachatani?
Ni muhimu sana Kufahamu kile unachotaka kukihubiri  kwani kuna tofauti ya kusoma na kufahamu au kusikia na kufahamu Maroko 7;14 Yesu alisema  “Nisikieni nyote na Kufahamu” kusikia na kufahamu ni maswala mawili tofauti wote tunajua kuwa katika mazingira haya ndipo Yesu alipotakasa vyakula Vyote na tunajua kuwa Petro alisikia lakini je alielewa alifahamu? Matendo 10;9-16 Petro hakuweza kufahamu kile Yesu alikisema katika Marko 7;14-19.

Mfano mwingine;-
    Watu wengi wamehubiri kuhusu njaa iliyoikumba Samaria 2Wafalme 6; 25 ambapo Biblia inasema hivi
“Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama wakauhusuru hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya Fedha na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya Fedha” watu wengi wamehubiri kuwa mavi ya njiwa yaliuzwa je umawahi kujiuliza kuwa ni katika tamaduni gani watu hula mavi ya njiwa? Neno mavi ya njiwa ni neno geni lazima ujiulize lina maana gani kabla ya kuhubiri!
Kibaba cha mavi ya njiwa Biblia ya RSV Revised Standard Version inasema fourth part of a Kab of doves dung
Biblia ya NIV New International Version inasema a Cab of seeds ambapo kwa lugha nyepesi kumbe Biblia inazungu mzia robo ya kibakuli cha mbegu RSV na NIV ni Kibakuli cha mbegu kibakuli hicho cha mbegu ndio kiliitwa Kibaba cha mavi ya njiwa kwa msingi huo unaweza kuona kuwa kutokuzingatia Maneno ndani ya kile unachokisoma kunaweza kabisa kusababisha upotofu wa maana halisi iliyokusudiwa
      Mathayo 24;28 “ Kwakuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai” Yesu alisema mfano huu au usemi huu katika mazingira ya unabii unaohusu kuja kwake mara ya pili duniani kwamba kimsingi ujio wa Yesu mara ya pili duniani hautakuwa wa kificho kwani utaambatana na kuuawa kwa maadui wa masihi na taifa la Israel jeshi hilo la mpinga Kristo watauawa kwa maelfu yao na kukosa wa kuwazika kwa hivyo miili yao itakuwa chakula cha tai ni katika mazingira kama hayo Yesu anatamka neno kwa kuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapo kutanika tai.unaona!
          Mathayo 11;12 ‘Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka”Nyakati za Kristo na Yohana mbatizaji kulikuwako na makundi ya wana mapinduzi waliojulikana kama Zealots au mazerote hawa walikuwa na nia ya kuleta mapinduzi ili kuhakikisha kuwa Israel inajitawala na kuwa na ufalme wao wenyewe kwa nia ya kijeshi walikuwa na Shauku kubwa wivu mkuu Yesu alimtumia shauku waliyokuwa nayo wana mapinduzi hao na kuioanisha na mtu yeyote yule anayetaka kupata ufalme wa Mungu kwamba hata kama ni kwa gharama ya kimapinduzi ufalme upatikane watu wenye shauku hiyo wanaweza kupata ufalme wa Mungu.
Nyenzo za kuzingatia
Kama tulivyoona kuwa kumbe basi ili mtu aweze kuwa Mtafasiri mzuri wa Maandiko katika viwango vya juu anahitaji Nyenzo za viwango vya juu vitakavyoweza kumsaidia na nyingi ya nyenzo hizo ziko nje ya Biblia yenyewe hii ina maana gani ninakukumbusha ya kuwa unahitaji kuwa na Matoleo mabalimbali ya Biblia,unahitaji Kamusi za Biblia,unahitaji mafafanuzi Commentary nzuri za Biblia,na nyenzo nyingine zitakazoweza kukusaidia katika usomaji wako wa Biblia na pia ni muhimu kuisoma Biblia yenyewe kitabu kwa kitabu kila mara kwani nayo ni silaha nzuri lakini zaidi sana tafuta Biblia inayosadikiwa kuwa na tafasiri nzuri ziko nyingi lakini inatakiwa ile inayotafasiri maana iliyokusudiwa katika Lugha halisia kinyume cha hapo basi lazima ukubali kujifunza Lugha ya kiyunani na kiibrania zitakusaidia katika kujisomea moja kwa moja na kupata maana halisi zilizokusudiwa

              Kumbuka!  Msomi mzuri wakati wote hujiuliza swali kuwa jambo hili lina maana gani?
    

KANUNI YA KUCHUKUA ANDIKO KAMA LILIVYO RAHISISHA.(SIMPLICITY)
 Kanuni hii inahusu kutafasiri andiko kwa kurahisisha kama lilivyo bila kujaribu kutafuta maana kwamba hili ni fumbo au bila kujali lugha iliyotumika kuwa ni ya namna gani Kanuni hii inaruhusiwa kwa sababu Mungu alikusudia Maandiko yaweze kueleweka kwa kila Mtu na Mungu anataka ajifunue kwa watu hivyo alitupa Biblia kwa msingi huo kusudi la Biblia liko wazi na ni kuweka wazi kweli zote na sio kuwachanganya watu wala Maandiko sio mkusanyiko wa mafumbo na siri ni ujumbe wa Mungu kwa watu wake kwa hivyo unapoitafasiri Biblia tafuta maana nyepesi ya asili na itumie lakini yako mambo ya msingi unapaswa kuyazingatia
1.       Kuhusu Lugha ya kawaida
Lugha ya kawaida iko wazi katika maisha yetu ya kila siku wala hatuna mafumbo katika maisha yetu ya kila siku kila kitu kikowazi na kimenyooka angalia kwa mfano katika Maandiko haya Matendo 20;7-12
Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka usiku wa manane. Kwenye chumba cha ghorofani walikokuwa wamekutania kilikuwa na taa nyingi. Kijana mmoja jina lake Eutiko, aliyekuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akiendelea kuhubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa. Paulo akashuka chini, akajitupa juu ya yule kijana na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, uzima wake bado umo ndani yake.” Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea mpaka mapambazuko, akaondoka. Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.”
Katika kifungo kama hiki lugha ni ya kawaida na hakuna mafumbo yoyote kwa msingi huo ni dhambi kuanza kufikiri kuwa kuna mafumbo usianze kufikiri kuwa kuna maana ya Neno usiku, ghorofa, na dirisha na Eutiko mwenyewe ukafikiri kuwa kukaa karibu na dirisha ni mkristo kukaa karibu na dhambi kusinzia ni kutokuwa makini na mafundisho na hatimaye anguko likatokea na kifo cha kiroho hapohapo! Hii haitakuwa maana sahii ya Maandiko haya kwani yako wazi hivyo ulitakiwa kuchukua maana Rahisi tu Rahisisha!
Ni muhimu kufahamu kuwa katika maisha ya kawaida mafumbo hayatumiki sana kwa mfano kama mtu ametoka Tanzania akaruka na ndege kwenda Ulaya akaivuka bahari ya Hindi anapotoa taarifa hiyo mtu huyu haimaanishi kuwa anazungumza fumbo wala haimaanishi kuwa amekwenda katika inchi ya ahadi kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa si mara zote basi Biblia inamaanisha mafumbo wakati mwingi na sehemu nyingi iko wazi kabisa
Tahadhari
Msingi wa kanuni hii ni kulinda kile ambacho kimewahi kutokea miaka mingi kabla ya Kuzaliwa kwa Masihi walikuweko watu waliopenda kutafasiri Maandiko kiroho “Spiritualizing of a text” na katika historia ya aknisa jamii hizi zilikuweko watu hao ambao hupenda kutafasiri Maandiko Kiroho walitumia njia iitwayo “allegory”njia hizi zilikuja kusaidika baada ya wasomi kama Martin Luther na John Calvin ambao walisisitiza kuwa maana ya Maandiko ni wazi kabisa kuwa ni ile iliyokusudiwa na andiko kwa hivyo Mtindo wa kutafasirti Maandiko kiroho ni moja ya dhambi mbaya za watafasiri wa Maandiko hii ni hatari sana kwa sababu unapokataa maana halisi iliyokusudiwa na andiko unakataa neno la Mungu na unapohubiri maswala hayo unahubiri kisicho neno la Mungu kwa hivyo unahubiri vitu vya kufikirika tu na hivyo Baraka za Mungu nje ya neno lake haziwezi kumiminika kwetu
Angalia mfaono wa andiko hili siku Yesu alipoingia Yerusalem kwa shangwe Mathayo 21;5 Biblia inasema “Mwambieni Binti Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda punda, juu ya mwanapunda, mtoto wa punda.’

 Watu wanao tafasiri kiroho wanaweza kudhani kuwa Punda anawakilisha Gari basi au shangingi lakini Punda hawakilishi chochote hapa ametajwa punda kwa sababu Yesu alimpanda hapa! Hakuna neno la ndani lililojificha kuhusu Punda hapa! Msingi wa andiko hili ni kutimizwa kwa agano la kale kuhusu unabii wa Yesu kumpanda Punda kwa hivyo andiko hilo halihitaji ufafanuzi wowote linatakiwa lichukuliwe kwa maana rahisi na ya kawaida

Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa tunachukua maana rahisi ya kawaida katika Maandiko ambayo yako kawaida ambayo yakitafasiriwa kawaida yanaleta maana hii haimaanishi kuwa hakuna Maandiko yasiyohitaji kujua maana yake yako na tunayashughulikia sehemu ifuatayo

Ufahamu kuhusu Lugha za Mafumbo

Hapo juu tumesisistiza kuhusu kuichukulia Biblia katika maana ya kawaida na rahisi lakini ni muhimu kuzingatia pia kuwa iko mistari ambayo huwezi kuichukulia kirahisi kwani ni lazima ufahamu kuwa iko katika lugha za kifumbo kama tulivyoona kuwa mtu anaweza kutafasiri fumbo katika eneo ambalo linapaswa kuchukuliwa kirahisi na kikawaida hali kadhalika mtu huweza kufanya makosa kwa kutokuzingatia lugha hizi za mafumbo
 Kwa mfano nikodemo hakuweza kumwelewa Yesu pale alipochukulia Maneno ya Yesu kuhusu Kuzaliwa mara ya pili kama tafasiri rahisi na ya kawaida na kumbe Yesu hapa alimtumia lugha ya fumbo Yohana 3;3-4

 “Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.’’ Nikodemo akauliza, “Awezeje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? ‘‘Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”

  Hapo Nikodemo alitaka kutumia namna rahisi na ya kawaida kutafasiri alilolisema Yesu lakini Yesu alimtumia Fumbo
Mwanamke msamaria pia alifanya kama Nikodemo alichukua Maneno ya Yesu kama kawaida na katika namna rahisi kumbe Yesu alizungumza Lugha ya fumbo Yohana 4;10-11

“Yesu akajibu akamwambia, ‘‘Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba Yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.’’Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, Wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?”

Hapa pia Mwanamke msamaria alichukua Maneno ya Bwana Yesu katika namna ya kawaida hakujua kuwa Yesu alizungumza lugha ya Fumbo

Kumbe basi baadhi ya Maandiko ni wazi kuwa yako wazi na unaweza kuyachukulia kwa urahisi na kwa njia ya kawaida lakini mengine ni mafumbo na unapaswa kuyatafasiri
Inasemekana nyakati za Martin Luther mzozo wa kitheolojia ulitokea kuhusu andiko la kula mwili wa Yesu na kunywa damu yake Mathayo 26;26  kwa sababu Lutha alikua akikazia swala la kuchukua andiko kama lilivyo walimletea kisu Mezani  ili ajikate naye waweze kuliwa kumbe si kila andiko linapaswa kuchukuliwa kama lilivyo Hebu angalia Maandiko yafuatayo na jiulize kama yangechukuliwa kama yalivuyo leo tunagekuwa na wakristo wa namna gani?

1.       Mathayo 5;29 jicho lako lakuume likikukosesha ling’oe………………..
2.       Mathayo 5;30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha………………

Aina mbali mbali za Lugha za Mafumbo

 Kuna aina mbalimbali za Lugha za mafumbo zinzotumika katika Biblia inasemekana ziko lugha za mafumbo zilizotumika katika Biblia zaidi ya 200 pamoja na mifano yake ipatayo 800 lugha hizo za mafumbo ni kama vile kama vile
·         Mifano na fumbo la maneno  (Parable and allegories)
·         Ulinganisho unaotumia maneno  kama,  na na ulinganishi usiotumia neno kama na (Similes and Metaphors)
·         Maneno ya kuongoza chumvi (Hyperboles)
·         Maneno ya kuhuisha au kukipa kitu au mnyama uhai au ubinadamu ( Personification)
·         Kumliganisha Mungu na mwanadamu (Antropomorphism)
·         Jina moja kwa niaba ya linguine (Metonymy)
·         Sehemu moja kwa jambo lote au Sehemu nzima kwa sehemu (synecdoche)
·         Kuzungumza kinyume cha uhalisia ( Irony)
·         Lugha za mficho  inayotumika badala ya neno chafu Figurative language au (Euphemism )
·         Misamiati au Maneno magumu au Mithali na misemo


A.      MIFANO NA FUMBO LA MANENO  (PARABLE AND ALLEGORIES)
Moja ya njia kubwa sana alizotumia Yesu kufundishia ni stori na mifano hizi ni hadithi fupi ambazo kwa kawaida hubeba maana moja ya kiroho au somo moja maalumu ndani ya hadithi hizo kunauchambuzi unaotolewa kwa kusudi tu la kufikisha ukweli uluiokusudiwa, kwa mfano katika mfano wa msamaria kuna ukweli mmoja tu katika mfano huo Yesu alikuwa akijibu swalai Jirani yangu ni nani? Kuna mambo mengi ndani ya mfano huo ambayo hayapaswi kuchambuliwa  na katika fumbo la Maneno Allegories au kisa kilichofichwa kuna weza kukawako na kweli nyingi mafano ni Yohana 10,  “Yesu anaposema Mimi ndimi Mchungaji mwema” hapa unaweza kupata mambo mengi kuhusu Mchungaji,kondoo, mwivi, mgeni, kukodisha, mbwa mwitu, Tunawezaje kujua kuwa huu ni mafano na haya ni fumbo la Maneno mara nyingi utaweza kuona kuwa Yesu mwenyewe alitafasiri maana aliyoikusudia na kama hukufanya hivyo basi tunapaswa kuchukua kama mfano au lugha ya mafumbo hata hivyo tutashughulikia swala hili katika kanuni maalumu ya kutafasiri mifano huko mbele

B.      ULINGANISHO UNAOTUMIA MANENO  KAMA,  NA NA ULINGANISHI USIOTUMIA NENO KAMA NA (SIMILES AND METAPHORS)
1.       Similes ni mifano ya ulinganisho inayotumia neno kama au na moja kwa moja neno simile limetoka katika kilatini  lnye maana ya kufanana au kama  kwa mfano “anatenda kama nguruwe” huu ni mfano wa moja kwa moja wa ulinganisho wa Maneno similes mingi ya mifano ya yesu pia iko katika lugha za ulinganifu Mfano ni
·         Luka 10;3 “…Nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu”
·         Marko 4;31 “…..Ni kama punje ya haradali…..”
·         Mathayo 24;27 “……kama vile umeme utokavyo mashariki…”
·         Kutoka 16;14 “……Kidogo kama sikitu juu ya nchi”
                 Kwa msingi huo ulinganishio wa Maneno unaotumia neno kama au na huitwa similes na kwa mchoro wa     mfano huonekana namna hii

 Na
Ufalme wa Mbinguni umefana na

                        umefanana                                   na                                                    chachu                               
                                                     

2.       Metaphors ni ulinganisho wa Maneno wa moja kwa moja usio na kiungo kama na au kama kwa mfano Mungu ni Mwamba wangu, Bwana ni ngome yangu, au  ngao yangu au wokovu wangu Zaburi ya 18;2. Au Yesu anaposema Mimi ni mkate wa uzima Yohana 6;35
Yesu alimtumia Maneno haya pia katika kufundisha kwa mfano Maneno kama ninyi ni chumvi ya ulimwengu,au ninyi ni Nuru ya ulimwengu kwa msingi huo Metaphors hazina kiunganishi katikati bali ni neno la moja kwa moja lakini la ulinaganifu

                          Ninyi                                          ni                           Nuru Ya Ulimwengu                                      

Ni muhimu kufahamu kuwa pia uko ulinganifu ulio kuinyume au ulinganifu unaokanusha ambao pia hutumika katika Maneno kadhaa ya kibiblia kwa mfano Hesabu 23;19 unaosema Mungu si mtu aseme uongo wala si mwanadamu ajute

     
                                    
                                           Ulinganifu ulio kinyume Mungu si Mtu hata aseme uongo Hes 23;19

C.      MANENO YA KUONGOZA CHUMVI (HYPERBOLES)
Lugha ya kutia chumvi ni lugha ya kukuza au kukazia au kuonyesha msisistizo wa jambo fulani muhimu kwa mafano Yesu alipowaambia mafarisayao Rnyi wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia Mathayo 23;24 hii ilikuwa ni lugha ya kusisitiza hapa yesu alikuwa akiwakosoa tabia yao ya kusisitiza mambo madogo ya sheria huku wakisahau mambo muhimu ya sheria ambayo ni Haki, Rehema na uaminifu kwa kutumia lugha ya mficho na ya kutia chumvi ukweli ulifika mahali pake kwani ni kweli mtu aweza kuchuja mbu wakati wa kunywa maji lakini kimsingi hakuna mtu awezaye kumeza ngamia unaona!
Maandiko mengine ambayo ni yenye Maneno ya kukazia au kuonyesha msisitizo au kutia chumvi ni pamoja na

·         Mathayo 19;24…..Ni rahisi kwa Ngamia kupenya katika Tundu ya sindano
·         Mathayo 16;26…..itamsaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote na kisha kuipotyeza nafsi yake
·         Zaburi 6;6………..Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu
·         Zaburi 79;3………Wala hapakuwa na mzishi au hapakuwa na wa kumzika mwingine
·         Yohana 21;15……Ulimwengu usingelitosha kwa vitabu
·         Wagalatia 4;15…..ngelinipa macho yenu

D.      MANENO YA KUHUISHA AU KUKIPA KITU AU MNYAMA UHAI AU UBINADAMU( PERSONIFICATION)
Uhuishaji ni tendo la kukipa kitu siku au mnyama ubinadamu. Hali hii hutokea pale mnyama au mahali au kitu au kitendo,vitu vinapoelezwa vikiwa na sifa kama ya binadamu halisi
Kwa mfano
·         Tamaa ikiisha chukua mimba huzaa dhambi Yakobo 1;15
·         Kwanini (Yuda) unataka kupigwa tena? Isaya 1;5
·         Ingawaje dhami zenu zinatushuhudia Yeremia 14;7
·         Milima na vilima vitaimba nyimbo Isaya 55;12
·         Acha Kesho ijisumbukie yenyewe Matahyo 6;34

E.       KUMLIGANISHA MUNGU NA MWANADAMU (ANTROPOMORPHISM)
Kwa kawaida Lugha kubwa inayotumika kumuelezea Mungu katika Biblia ni ile inayompa Mungu hali ya ubinadamu ingawaje Mungu sio mwanadamu ni Roho na haonekani Mungu amepewa tabia hisia na vitenzi vinavyofanana na mwanadamu penginepo ili wanadamu waweze kuelewa katika akili za kawaida za kibinadamu Kolosai 1;15 Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.na 1Timotheo 1;17. Kwa msingi huo utaweza kuona kuwa

·         Mungu anapewa uso,kutoka 33;23
·         na anapewa macho 2Nyakati 7;16
·         anapewa masikio zaburi 31;2
·         kinywa 1falme 8;24
·         Mikono Isaya 52;10

F.       JINA MOJA KWA NIABA YA LINGINE (METONYMY)
Hii ni njia iliyotumika kuelezea kwa kuataja jina moja lenye kumaanishwa kwa niaba ya wengine kwa mfano Badala ya kusema serikali ya Marekani waandishi wa habari wanaweza kusema ikulu ya Marekani au badala ya Urusi imesema wanaweza kusema Moscow imesema au badala ya Tanzania imesema unaweza kusema Dare es Salaam imesema; jambo hilo kitaalamu huitwa Metonymy ambalo maana yake Meta kubadili na Onoma maana yake jina  kwa msingi huo katika Biblia utaweza kuona wakati mwingine nenoYakobo likitumika kwa Israel nzima au wayunani likitumika kwa ajili ya mataifa mengine nje ya wayahudi
Hili linaweza kuonekana katika vifungu vya mfano vifuatavyo

·         Wapenzi wangu msiiamini kila roho bali zijaribuni 1Yohana 4;1 hapa anamaanisha mafundisho yatokayo kwa Mungu au kwa roho nyingine
·         Isaka ataharibiwa Amosi 7;9
·         Wanao Musa na Manabii na wawasikilize wao Luka 16;29
·         Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu Yohana 3;16
·         Tukilitizamia tumaini lenye Baraka Tito 2;13
·         Kwakuwa pale hazina yako iliko ndipo na moyo wako Matahayo 6;21
·         Upumbavu wa Mungu 1koritho 1;21,25

G.      SEHEMU MOJA KWA JAMBO LOTE AU SEHEMU NZIMA KWA SEHEMU (SYNECDOCHE)

Ni muhimu kufahamu pia kuwa abiblia hutimia lugha ya mficho ambapo sehemu moja huwakilisha sehemu nzima hii hutokea pale kitu kinapozungumzwa kwa sehemu na kumbe kinyume chake kinazungumzwa kwa ujumla wake hali ndio huitwa synecdoche mifano ya sehemu moja kuwakilisha sehemu nzima ni kama hii ifuatayo;-

·         Baraka humkalia mwenye haki kichwani Mithali 10;6 – kichwa hapa huwakilisha mtu kamili
·         Jinsi ilivyo mazuri miguu yake aletaye habari njema Isaya 52;7 miguu huwakilisha huyo atangazaye
·         Nafsi zaburi 103;1 nafsi huwakilisha mtu mzma au mtu kamili
·         Jicho 1Koritho 2;9 hapa jicho humwakilisha mwanadamu kamili
·         Heri mtu Zaburi 1;1 hapa inawakilisha wanadamu wote ingawaje anatajwa mtu
·         Sheria Yakobo 2;10 ikimaanisha Agano la kale
·         Agano la kwanza Waebrania 9;1 ikimaanisha agano la kale
·         Sheria na Manabii ikimaanisha agano lote la kale Mathayo 7;12
Kwsa msingi huo utaweza kuona kuwa wakati mwingine wana ikiwakilisha wanadamu wote au baba zetu ikimaanisha wazazi wetu wa kale waliopita au Yoeli 2;28 inaposema nitawamwagiwa watu wangu  au kila mwenye mwili si wakati wote humaanisha hivyo wakati mwingine inaweza kumaanisha wayahudi na mataifa wale watakao mwamini au 1Timotheo 2;4 ambaye anataka watu wote waokolewe hii humaanisha ingawa Mungu anataka watu wote waokolewe bado ni wale tu wanaokubali mpango wake katika maisha yao ndio wanaookolewa kwa hivyo Synedoche humaanisha “sehemu kwa lote au lote kwa sehemu

H.      KUZUNGUMZA KINYUME CHA UHALISIA ( IRONY)
Hii ni hali ya kuzungumzia jambo kinyume na uhalisia kwa mfano mtu wakati wa baridi kali anaweza kusema mzee vipi joto la leo nawe ukajibu joto leo mzee kali sana hii inamaanisha kuwa mnazungumza kwa kujmaanisha lakini kinyume na hali halisi ya tukio husika kwani uhalisi unabaki kuwa kuna joto sana halii hii huitwa Irony kitaalamu mifano halisi ya kibiblia ambayo inaonyesha maeneo ambayo misemo hii ilitumika baadhi ni kama
·         Ayubu 12;2 hakika ninyi ndio watu na bila shaka Hekima itakufa na ninyi
·         Mwanzo 3;22 Bwana Mungu akasema Basi huyumtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima  akala akaishi milele hapa Mungu hakuwa anamaanisha kuwa sasa ni hakika kuwa mwanadamu amekuwa kama Mungu kimsingi mwanadamu aliumbwa akiwa kama Mungu na kwa kula matunda aliasi na alipoteza hali ya kuwa kama mungu  hivyo hapa Mungu anasikitishwa na kile kilichotokea na anatumia msemo huu uitwao Iron
·         Ezekiel 20;39 Enendeni mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja Mungu hapendezwi na kuabudu sanamu wala hajaruhusu ila ana akisi dhambi za Israel hivyo anazungumza kwa kutumia Iron
·         2Wafalme 8;10 Enenda ukamwambie utapona  nabii anatumia Iron kwani Mungu alimwambia mfalme kuwa atakufa wala hatapona
·         1Wafalme 22; 15 Ahabu anaambiwa aende vitani na kushinda lakini uhalisia ni kuwa atakufa
·         2samuel 6;20Mfalme wa Israel alikuwa mtukufu leo kumbe alikuwa akimsanifu
·         Mathayo 23;32 Kijazeni basi kikombe cha baba zenu hapa Kristo alikuwa akikazia dhambi ambayo ingefanya na kizazi kilichomsulubisha ambayo kimsingi hata baba zao hawakuwahi kuifanya ingawa waliwakataa Manabii wengi lakini kwa kitendo cha wao kumkataa masihi wanawazidi hata baba zao na kuti miliza ile chuki yao dhidi ya Manabii Yesu hakuwa anasisistiza waifanye dhambi hiyo bali alitaka kuonyesha ni jini gani wako mbali na Mungu zaidi ya baba zao

I.         LUGHA ZA MFICHO  INAYOTUMIKA BADALA YA NENO CHAFU FIGURATIVE LANGUAGE AU (EUPHEMISM )
Lugha za mficho ziko karibu katika kila utamaduni ambapo watu huweza kutumia Lugha hizo kwa ajili ya kuficha mambo fulani kama Ngono au kwenda choo kujisaidia n.k kwa mfano mtu anaweza kutumia neno mzigo akimaanisha ngono Paulo mtume alimtumia Lugha ya mficho katika 1Wakoritho 7; 1 akikataza zinaa na uasherati alisema “….Ni heri mwanamume asimguse Mwanamke” hivyo hapo haimaanishi kuwa Mwanamume asioe lakini wasizini au kufanya uasherati
Miano mingine ya lugha za mficho ni kama
·         Waamuzi 3;24 kujifunika miguu ni kunya lugha inayotumika kufunika neno hilo Euphemism
·         Malaki 2;16 kufunika nguo kwa udhalimu ni kunyimia tedno la ndoa
·         2Samuel 13;14 akamlazimisha akalala naye maana yake akambaka
·         Amosi 4;6 Nami nimewapa ninyi usafi wa meno neno hili linamaanisha njaa na sio kupigwa mswaki
·         Mwanzo 31;35 nimeshikwa na mambo ya kike maana yake yuko mwezini
·         Mwanzo 32;25 alimgusa panapo uvungu wa paja lake ukateguka, alimvunja Mapumbu

J.        MISAMIATI AU MANENO MAGUMU AU MITHALI NA MISEMO
Watu wengi wanaposikia au kuzungumzia kuhusu kutafasiri Maandiko haraka watafikiri swala la kushughulikia ni misamiati hilo huwa katika akili za watu wengi na linaweza kuonekana kama swala jepesi tu wanaweza kutafuta neno la kiingereza lenye maana sawa na ile ya kiebrania na kiyunani lakini Ili mtu aweze kuwa na tafasiri nzuri lazima atafute Neno sahii lililotumika na hii husaidia sana katika kupata maana sahii ingawaje pia swala la kutafasiri linaweza kuwa Gumu zaidi kwa sababu ya kukosekana Maneno ambatano na neno husika ingawaje kujua neno lililotumika au msamiati uliotumika katika lugha ya asili itakusaidia kupata kweli za kibiblia katika njia iliyo nyepesi zaidi
·         Zingatia matoleo mbalimbali ya Biblia
·         Zingatia mchezo wa Maneno hasa katika Vitabu vya mashairi mara nyingu hauingiliani
·         Zingatia maswala ya Jinsia kunawakati mji au nchi inaweza kupewa jina la kike au mwanaume akawakilisha watu wote au wa jinsia zote

KUUSHIKA UPANGA VIZURI
KANUNI YA MIZANI, ULINGANIFU, USHAHIDI WA MAANDIKO MENGINE (HARMONY)
Moja ya maswala ya hatari sana katika kujipatia tafasiri zisizo halalai za kimaandiko ni kutengeneza fundisho katika andiko moja hii ni sawa na wale jamaa ambao mmoja aliamua kukalia kiti kimoja na mwingine alikalia kiti cha miguu minne yula wa miguu minne alikaa salama kuliko yule wa mguu moja unapotumia andiko moja kutengeneza fundisho hauwezi kupata mlingano sahii wa kimaandiko na ni hatari kwani unaweza kupata mafundisho yasiyo sahii
Kwa mfano angalia aya zifuatazo ikiwa zitafanywa fundisho nini kinaweza kutokea
·         Msihubiri kwa mataifa bali kwa wayahudi tu Mathayo 10;5 - 6
·         Msichukue Fedha safarini wala viatu Mathayo 10; 9-10
·         Hubirini juu ya nyumba Mathayo 10 ;27
·         Hubiri na kufundisha ukiwa katika boti au mtumbwi Marko 4;1
·         Kumfuata Yesu lazima kuambatane na kuwachukia ndugu Luka 14 26
·         Yey achinjaye Ng’ombe ni sawa na yeye auwaye mtu Isaya 66;3
·         Kumfanyia mtu maombezi mbali na watu Marko 8;23
Kwa msingi huo tunaweza kuona kuwa tayari tumepata picha kuwa kutumia andiko moja kutendeneza fundisho si halali katika kanuni za kufasiri Maandiko na hivyo awaye yote atakayetegemea andiko moja kwa fundisho amekalia kiti chenya mguu moja hawezi kuwa salama andiko lazima liwe na masahidi wawili au watatu ili lithibitike, hii haina maana kuwa mtu aliyekalia kiti cha miguu minne yuko salama pia hapana kunauwezekano pia Maandiko yakawa mengi lakini ikawa sio yaliyolingana  hata kama una Maandiko mengi yanayounga mkono fundisho lako ni muhimu kufahamu kuwa tunahitaji Biblia nzima ikubalianae na kile unachotaka kukihubiri kwani tumepewa Biblia nzima na sio manenno machache tu  kwa msingi huo mtafasiri wa Maandiko hapaswi kudharau kile au andiko lililo kinyume na kile anachotaka kukifundisha kwa hivyo Maandiko mengi bado hayakupi kuwa salama japo unaweza kupumua kuliko yule wa andiko moja lakini hii sio taa ya kukuruhusu kuendelea mbele bado unahitaji kuwa makini ili iwe hivyo zingatia mambo ya msingi yafuatayo

  weka Mzigo nyuma ya Punda usiweke mzigo mbele ya Punda

1.       Usiweke mzigo mbele ya Punda.
Tumeitwa kuhubiri. Lakini tutahubiri nini ? Je tujiamulie tu kile tunachotaka kukihubiri? Hapana Mungu amekataza Tumeitwa kuihubiri Biblia lakini ni eneo gani la Biblia tunaweza kulihubiri? Je ni Maandiko yanayotuvutia tu? Au tuchague ile mistari tunayoijua sana Mpaka hapo tutakuwa hatujaitendea haki Biblia Hatuamui sisi kile tunachopaswa kukihubiri kisha tukaamua kutafuta katika Biblia kuunga mkono kile tunachofikiri halii ndio dhambi ya kuweka Mzigo mbele ya Punda ili ausukume
Ni muhimu kwanza kwenda kwenye Biblia yenyewe na kuisoma tena na tena na kuijuifunza inasema nini kisha hubiri kile Biblia inachosema katika hali hii utakuwa na amani na Mungu mafundisho mengi leo sio kile Biblia inachokisema bali ni kile watu wanasema na kwa msingi huu kuna mafundisho mengi ya uongo duniani watu wengi hawalihubiri neno badala yake wanaangalia nini kimo mioyoni mwao kisha wanakwenda katika Maandiko na kuyasingizia au kutafuta kuungwa mkono kwa mawazo yao
Muhubiri maarufu William Branham aliumba usiku na mchana na kupata Ufunuo kutoka kwa Mungu na kupata wazo kuwa hakuna utatu isipokuwa ni Yesu pekee na alipata wazo kuwa Yesu ndiye Baba na ndiye Roho na ndipo alipoanzisha imani iitwayo Jesus Only pia alikwenda katika Maandiko na kutafuta kusapoti mawazo yake na akaktuta andiko alilolidhani kuwa linaunga mkono mawazo yake Yohana 14;9 Branham alipuuzia kuwa katika sura ileile kuna Maandiko ambayo yako kinyume na mawazo yake au Ufunuo wake
·         Mna mwamini mungu niaminini na mimi Yohana 14;1
·         Nitamuomba baba sio nitajiomba mwenyewe Yohana 14;16
·         Yeye anipendaye mimi  atapendwa na baba yangu  Yohana 14;21
·         Nasi tutakuja kwake na kufanya makazi ndani yake Yohana 14;23
·         Maneno niliyowaambia si yangu bali Yohana 14;24
·         Lakini huyo Roho ambaye baba atampeleka Yohana 14;25-26
·         Baba ni mkuu kuliko mimi je mtu anawezaje kuwa mkuu kuliko yeye mwenyewe? Yohana 14;28
                               
Unapopuuzia kile kinachosemwa na Biblia nzima na kukaa katika andiko moja na kutengeneza Fundisho au kutafuta Biblia iunge mkono mawazo yako ni sawa na kuweka mzigo mbele ya Punda usiweke mzigo mbele ya Punda Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote Mwandishi wa somo
2.       Kumbuka kusema kuwa Imeandikwa pia
Mathayo 4;5-7 “Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na kumweka juu ya mnara mrefu mwembamba wa hekalu, akamwambia, “Kama Wewe ndiye Mwana wa Mungu jitupe chini, kwa kuwa imeandikwa,
“Atakuagizia malaika zake nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’ Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’

Kumbuka kuwa si kila wakati mtu akiinukuu Biblia ndio anahubiri kweli haisaidii kunukuu Maandiko pekee, Baadhi ya watu wanaitafasiri vibaya Buiblia kwa bahati mbaya Lakini wengine ni Mbwa mwitu wakali katika mavazi ya kondoo kumbuka Shetani pia alisema “Imeandikwa” alinukuu mstari au aya hii kwa kusudi la kumkosesha Bwana Yesu Neno la Mungu litakuwa ni taa ya miguu yetu pale tu linapotafasiriwa kwa halali na kwa ulinganifu na Maandiko mengine

Yesu hakupambana na shetani kuhusu andiko alilolitumia wala hakukanusha kuwa wako malaika ambao wanatulinda, lakini Yesu alimshinda adui kwa kutumia kanuni ya ulinganifu alimwambia kuwa “Pia imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako”kwa kufanya hivyo aliweka ulinganifu wa andiko kwa andiko jingine ,Hiii inafanyika pale andiko linapotumika kwa kusudi la kudhuru badala ya kusaidia,Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili unaweza kukata huku na huku kwa mfano hebu tuangalie Maandiko yanayohitaji kufanyiwa ulinganifu ili kupata ukweli halisi wa kibiblia

A.      Swali: Kama Yesu hakuja kuleta amani duniani kwanini malaika waliimba amani duniani?
Luka 2;14 “Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”
Imeandikwa pia
Mathayo 10;34” Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.

Namna ya kuweka ulinganifu;
 Yesu alikuja kuleta amani Duniani kwa watu wote wanaomkubali lakini pia kwa wale wanaomkataa hakuja kuleta amani kwao kwa msingi huo kumpokea Mfalme wa amani kunaweza kuwafanya wasiomwamini kutuchukia kabisa.

B.      Swali:  Je Yesu alikuja kuleta hukumu?
Yohana 9;39 “Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.’’
Likini pia imeandikwa
Yohana 12;47 Mimi simhukumu mtu ye yote anayesikia maneno Yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
Namna ya kuweka ilinganifu
Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea na sio kuuhukumu kwa dhambi zao ingawaje wale walio mkataa watahukumiwa

C.      Swali: Kama Roho anatufundisha je hatuhitaji waalimu?
1Yohana 2;27 Kwa habari yenu ninyi, Mafuta yale mliyoyapokea kutoka Kwake yanakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu ye yote kuwafundisha. Lakini kama vile mafuta yale yanavyo wafundisha kuhusu mambo hayo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama yanavyowafundisha kaeni ndani Yake.
Lakini imeandikwa pia
Efeso 4;11 “Naye alitoa wengine kuwa Mitume,wengine kuwa Manabii,na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”

Namna ya kuweka ulinganifu
Mafuta ya Roho Mtakatifu yanamfundisha mwamini kweli nyingi na hivyo haupaswai kupuuziwa lakini kuheshimika kwani ni njia ya pekee ya kufundishwa na Mungu mwenyewe, kwa hivyo hatuhitaji mwalimu anayeweza kudai kuwa ana Ufunuo au ameangaziwa siri fulani kwa ajili yetu Lakini Mungu pia ameweka waalimu kama zawadi kwa kanisa ili kulikamilisha na kuwakataa ni kumkataa Mungu
D.      Kama Mungu anaweza kufanya miujiza mikubwa kwanini wakati mwingine anaacha watumishi wake wanaugua?
Matendo 19;11 “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida…”
Lakini pia imeandikwa
2Timotheo 4;20 “…..Trofimo nimemwacha huko Mileto Hawezi (Mgonjwa)

Namna ya kuweka ulinganifu
Mungu anaponya wagonjwa hii ni wazi kabisa katika neno lake hususani Agano jipya Lakini kuna wakati ambapo hata maombi ya mitume wakubwa waliotumiwa sana na Mungu hayakuweza kuponya wagonjwa katika wakati huu Tunaendelea kuamini kuwa Mungu ni mponyaji lakini ni lazima tukubali kuwa si kila wakati Mungu anaponya kwa sababu zake ambazo hatuwezi kuzieleza
E.       Kama Mungu akiwa upande wetu hakuna wakuwa kinyume nasi kwanini wakristo huuawa?
Warumi 8;31 “…Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliyejuu yetu”?
Lakini pia imeandikwa
Warumi 8;36 “…Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa”
Namna ya kuweka ulinganifu
Kunawakati walinzi 16 walishindwa kumlinda Petro Gerezani Matedno 12 kuna wakati ambapo Mungu aliacha Paulo mtume kupigwa mawe Matedno 14 mungu anaweza kuruhusu mpigwe bakora,mburuzwe na kutiwa Gerezani lakini pia anaweza kuleta tetemeko kubwa na milango ya gereza ikafunguka Matedno 16 ili Mungu abaki kuwa Mungu tumewekewa si kumwamini tu bali na kuteswa kwa ajili yake Wafilipi 1;29.
Kwa msingi huu basi kumbe tunajifunza kuwa andiko moja likiachwa bila ulinganifu wa Maandiko mengine linakuwa dhaifu kama ilivyo kwa Nyuzi moja ya kamaba ya katani inakuwa dhaifu inapoachwa pekee kuliko inaposokotwa pamoja na kundi la nyuzi nyingine ndipo linapokuwa imara kwa hivyo kanuni ya kubalance au mizani ya Maandiko ni muhimu katika kujifunza na kupata kweli ya kuifahamu Biblia si kila wakati mtu anapopatwa na mabaya au kukosa Fedha au kulala na njaa ni kuwa hana imani kunawakati utaamini na kuokolewa na kuna wakati utaamini na utakufa angalia mifano mingine ya kumizanisha Maandiko kupata kweli
F.       Kwaimani watu waliokolewa na kwaimani watu walikufa
Waebrania11;32-35a “Basi niseme nini zaidi? Sina wakati wa kusema habari za Gideoni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii, ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitekeleza haki, walipokea ahadi za Mungu, walifunga vinywa vya simba, walizima makali ya miali ya moto, waliepuka kuuawa kwa upanga, udhaifu wao ukageuka kuwa nguvu, walikuwa hodari vitani wakayashinda majeshi ya wageni na kuyafukuza. Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa.

 Lakini pia imeandikwa
Waebrania 11; 35b-39a “Lakini wengine waliteswa nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo ulio bora zaidi. Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyonyoro na kutiwa gerezani. Walipigwa kwa mawe, walipasuliwa vipande viwili kwa msumemo, waliuawa kwa upanga, walizunguka-zunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, waliteswa na kutendwa mabaya, watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika mapango na katika mahandaki ardhini. Hawa wote walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao,
Namna ya kuweka ulinaganifu
Wakati mwingine Imani inatuwezehs kuhamisha milima na wakati mwingine inatuwezesha kuipanda milima Ayubu akasema tupate mema kwa Mungu tusipatwe na mabaya Ayubu 2;10

G.      Je ni kweli Yesu alisema tuwachukie ndugu zetu?
Luka 14;26 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake na mama yake na mke wake na wanawe na ndugu zake  naam na hata nafi yake mwenyewe hawezi kuwa Mwanafunzi wangu.”
Lakini pia imeandikwa
Mathayo 10;37 “Ampendaye baba yake au mama yake kuliko mimi hanistahiliwala ampendaye mwana au binti kuliko mimi hanistahili’
Namna ya kuweka ulinganifu
Maandiko yana tabia pia ya kujitafasiri yenyewe kwa yenyewe hivyo wakati mwingine kwa kutumia Maandiko sambamba yaani Cross reference inakusaidia kupata majibu kwa msingi huo neno kuchukia katika injili ya luka lilipaswa kutumika kupenda ndugu zaidi yangu.

H.      Kwa msingi huo kila ahadi ya Mungu pia inapaswa kuchukuliwa kwa ulinganifu
·         Amehaidi kutuokoa lakini lazima tujitie nidhamu kuiutunza wokovu
·         Amehaidi mbingu lakini pia ameahidi hukumu
·         Amehaidi kukubalika lakini pia ameahidi kukataliwa
·         Ameahidi ushindi lakini pia ameahidi mateso
·         Amehaidi kuzaa sana matunda lakini pia ameahidi kukata tawi lisilozaa matunda
·         Ameahidi furaha lakini pia ameahidi dhiki
     Kumbe ahadi za Mungu zinajumuisha wakati mzuri na wakati mgumu


KANUNI YA UHUSIANO WA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA (COVENANTS)
Mtafasiri wa Maandiko anapaswa kuuelewa uhusiano ulioko kati ya ukristo na agano la kale au uhusiano ulioko kati ya Agano jipya na la kale. Agano la kale lina sheria zipatazo 600, Je mkristo anapaswa kuzishika hizo zote? Kama tunapaswa kuzishika zote, Je itawezekanaje pasipokuweko hekalu?. Na madhabahu za wanyama za kuteketeza? Na kama hali tuhusu kwanini ni sehemu ya Biblia? Na kama hatuko chini ya sheria kwanini Yesu alisema ‘Msidhani ya kuwa nimekuja kuitangua torati na Manabii, Sikuja kuitangua bali kuikamilisha” Mathayo 5;17
Biblia yetu imegawanyika katika makundi makuu mawili agano la kale na agano jipya sisi wakristo tuko chini ya agano jipya na waisrael walikuwa chini ya agano la kale kwa mukhtasari agano la kale lina mambo muhimu yafuatayo
Ø  Kuumbwa kwa ulimwengu na vitu vyote
Ø  Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu baba yao wote waishio kwa imani
Ø  Kutoka kwa wana wa Israel huko Misri
Ø  Kupewa Sheria , Mungu aliagiza yale Israel walipaswa kuyatimiza
Ø  Kuhangaika katika jangwa
Ø  Kuingia kanaani na kuimiliki nchi ya kanaani
Ø  Kipindi cha Waamuzi
Ø  Kipindi cha Wafalme  na manabii
Ø  Mashairi
Ø  Kupelekwa utumwani na kurudi kutoka utumwani
Mungu ametupa Agano la kale hata kama hatuko chini ya agano la kale kwa msingi huo ni muhimu kwetu kujifunza Muongozo wa kuelewa uhusiano wa Ukristo na agano la kale
1.       Agano la kale (Sheria ) ni sehemu ya Agano
Agano ni mapatano ya pande mbili husika huku zikimuhusisha Mungu katika agano kuna majukumu ambayo kila upande unapaswa kuyatimiza, Leo hii tunaona watu wanapouziana Ardhi wakiandikishana hiki kinasaidia kutujulisha kuwa muuzaji amesema nini na mnunuzi amesema nini yale waliyokubaliana huonekana katika mkataba wote watapaswa kukubaliana na mkataba wao  au inaweza isiwe lazima, Agano la kale ni mkataba wa Mungu na Waisrael ni agano na ndani yake Mungu amewapa amri zaidi ya mia sita 600 kama wakizishika Mungu angewabariki na kuwalinda sheria hizi ziko kati ya Kutoka 20 mpaka Kumbukumbu la torati 33.
2.       Agano la kale sio agano letu
Agano la kele ni agano la Mungu na Waisrael limekalia katika mamia ya sheria na linahusu uchinjaji wa wanyama na utoaji wa sadaka za kuteketezwa za kila mwaka  wakristo hawako chini ya sheria hii ya kale tunaweza kuliona hilo wazi  katika Maandiko yafuatayo.
·         Warumi 6; 14 - Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
·         Yohana 1; 16-17 - Kutokana na ukamilifu Wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.
·         Wagalatia 5; 4 Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.
Yesu hakuja kuitangua Torati lakini alikuja kulitimiza na agano ambalo lilikuwa limekamilishwa au limamaliza kazi yake ya Ufunuo, Yeye alikuja kutuhesabia haki inayozidi haki ile ya mafarisayo haki itokanayo na neema na sio kwa sheria au Matendo ya sheria, haki itokanayo na imani kupitia sadaka aliyoitoa yeye msalabani iliyochukua nafasi ya zile za wanyama za agano la kale Warumi 10;4 Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye”.

3.       Maagizo mengi katika agano la kale hayakurudiwa katika agano jipya
Agano la kale limegawanyika katika maeneo makuu matatu ya sheria yaani sheria za Kimaadili Moral law, Sheria za kidini Ceremonial law na sheria za kisiasa au za kiraia Civil laws, kundi lililo kubwa zaidi ni la sheria za Kidini hizi hupatikana kwa wingi katika walawi na sehemu kadhaa za kitabu cha kutoka, Hesabu, na Kumbukumbu la torati hizi sheria za kidini kwa ujumla zinamuhusu Mungu hizi zinawajulisha wayahudi Mungu anatarajia nini kutoka kwao  pamoja na kumuabudu namna gani watengeneze hema vipimo gani vitumike sanduku liweje madini gani yatumika n.k. wajisafisha wakati gani na waabudu vipi sheria hizo zinafanya kazi kwa Raia wa zamani wa Isarael pekee na hakuna hata moja imerudiwa katika Agano jipya, leo hii vyakula vyote vimetakaswa 1Timotheo 4;1-5, Maswala ya Hekalu, Sadaka za kuteketezwa na ukuhani vimeondolewa milele Yesu amekuwa kuhani wetu mkuu
Kwa nini tunasema sheria za kidini ziliwahusu waisarael kwa Mungu?

Waebrania 10;1-10 “Kwa kuwa Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena, kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani alisema,“Dhabihu na sadaka hukuzitaka, bali mwili uliniandalia, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo. Ndipo niliposema,‘Tazama niko hapa, kama nilivyoandikiwa katika kitabu, Nimekuja kufanya mapenzi Yako, Ee Mungu.’ ” Kwanza alisema,“Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).Kisha akasema “Tazama niko hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi Yako.” Aondoa lile agano la kwanza ili kuimarisha la pili. Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu”.
Sheria za kidini za agano la kale hazikurudiwa katika agano jipya ,agano la kale sio tu lina sheria za kidini bali pia lina sheria za kiraia na kimaadili ambazo hizi zinahusu uhusiano ulioko kati aya mwanadamu na mwanadamu mwenzake hizi zinajibu maswala ya matatizo yajitokezayo siku kwa siku Israel wanapoishi kwa pamoja  sheria hizi ni kama vile nini kifanyike Ng”ombe anapoua mtu,Mtoto anapomshutumu baba yake,mwizi anapokamatwa,Mtu anapofanya zinaa sheria za kiraia na kimaadili zilikuwa zikitoa majibu ya matatizo kama haya  kwa msingi huo chini ya agano Jipya Je Mungu anatutaka tukaangalie sheria zile za kale zinasema nini na kuzitenda? Jibu ni la hasha Leo hatumpigi mtu mawe anapofanya zinaa au anapokuwa amemtukana mzazi wake hatuko chini ya sheria yoyote au hata moja ya agano la kale.

Mtafasiri mzuri wa Maandiko atatofautisha sheria za kidini na za kiraia na wakristo hawako chini ya hizo


4.       Sheria za kimaadili za Agano la kale zimerudiwa au zimefanywa upya katika agano jipya

Tumekwisha kusema kuwa Yesu hakuja kuitangua Torati bali kulitimiza lakini zingati mstari wa 19 katika Mathayo 5; 19 unaosema Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.
Hapa Kristo anazungumza na wale walio wa Ufalme wa mbinguni wafahamu kuwa nyingi ya sheria za agano la kale zinakubaliana na mfumo wa agano jipya kwa maana hii Nyuma ya kila sheria kuna kanuni ya msingi ya kuizingatia Hivyo wakristo wanapaswa kuishi kwa kanuni hizo Yesu hapa alienda mbele zaidi ya sheria  ambapo Nyuma ya kosa la mtu kuua kuna chuki hii ni dhambi Mathayo 5;21-24,Nyuma ya sheria ya zinaa kuna tamaa isiyoweza kuzuiliwa hii ni dhambi Matahayo 5;27-30 nyuma ya sheria ya kuapa kuna kanuni ya kuwa mkweli Mathayo 33-37
Sheria hizi zimetolewa kwa kusudi la kukwepa maswala ya kulipizana klisasi kama jino kwa jino au jicho kwa jicho kwa msingi huo Yesu alitupa kanuni za msingi za kutusaidia kimaadili kuweza kuishi kwa kanuni zilizo juu ya  sheria
·         Uhusiano wetu na Mungu katika agano jipya haujengwi na uwezo wetu wa kuishika sheria Tito 2;11-12
·         Wakati wa agano la kale sheria ziliandikwa katika jiwe katika agano jipya zinaandikwa katika moyo Waebrania 8;8-10.
·         Tunatimiza sheria yote kwa Roho ya upendo na sio kwa ulazima wa sheria Matahayo 22;36-40,Warumi 13;8-10
·         Jinsi gani mkristo anaitimiza sheria ya agano la kale Kumpenda Mungu na kumpenda jirani yake

5.       Agano la kale sio amri ya  Mungu kwetu lakini ni njia ya kujifunza kwetu
Biblia imejaa amri nyingi na mifano amabayo kwayo Mungu anataka tujifunze na kutii Binafsi kwa mfano Mungu alimuamuru Nuhu kuijenga safina ya mti wa Mvinje Mwanzo 6;14 ingawaje alitaka sisi tujifunze kuhusu amri zake  hatarajii kuwa na sisi tutaanza kujenga safina tunajifunza nini hapa?
Agano la kale ni neno la Mungu kwetu lakini sio Amri ya Mungu kwetu
Ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu ni endelevu na hujifunua kwetu hatua kwa hatua watu wa agano la kale walimfahamu Mungu kwa kiasi kidoko kuliko ambacho sisis tunamfahamu walimfahamu kwa mbali lakini sisi tumepewa Roho wake Waebrania 12;18
Agano jipya Bora zaidi katika kumfunua Mungu kwetu kuliko katika agano la kale lakini tunalihitaji agano la kale ili kulielewa agano jipya kwani agano jipya lina nukuu zaidi ya 1100 kutoka agano la kale hatu wezi kuelewa misemo kama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu bila kuwa na ufahamu wa agano la kale kwa msingi huo agano la kale nui neno la Mungu kwetu ingawaje hatuko chini ya agano hilo bali agano jipya
Ona mfano wa matumizi yake 1Koritho 9;9-10 “Kwa maana imeandikwa katika sheria ya Musa? “Usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ng’ombe? .Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Hakika yameandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu mtu anapolima na mwingine akapura nafaka, wote wanapaswa kufanya hivyo wakiwa na tumaini la kushiriki mavuno.”
Kwa msingi huo kuna mengi ya kujifunza kutoka katika agano la kale na moja ya somo muhimu tunalojifunza ni hitaji letu la kuwa na agano jipya ambapo haki hupatikana kwa imani na sio kwa kuishika sheria shera ni mwalimu mzuri wa kutuonyesha hitaji letu kwa neema ya Mungu Wagalatia 3; 23-25 “Kabla imani haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate tuhesabiwa haki kwa imani. Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.
6.       Ahadi katika agano jipya ni tofauti na Ni bora zaidi kuliko  ahadi katika agano la kale
Agano la kale ni patano la Mungu na wana wa Israel aliwaahidi inchi ya maziwa na asali hii ilikuwa ni nchi yenye mipaka maalumu kabisa na hata leo nchi hii inajulikana kama Israel kuingia katika inchi hii kulimaanisha vita vya kisiasa kwa sababu kulikuwa na mataifa mengine yaliyokuwa yanaitawala nchi hiyo na wakati mwingine Mungu aliwatia hofu maadui ili Israeal wawashinde
Wakati wa agano la kale Israel ilikuwa chini ya utawala wa Mungu kazi yao ilikuwa ni kutimiza sheria 600 na Mungu angefanya sehemu yake kuwapa ushindi na kuwalinda na kuwabariki kuna ahadi nyingi ambazo Mungu alizifanya kwa wana wa Isarael wakati wa agano la kale kumbuka kuwa tumesema agano la kale sio agano letu wala kanisa halipaswi kuzishika sheria 600 za agano la kale swali linakuja je kanisa linaweza kudfai kuwa ahadi za agano la kale zina lihusu? Au zinawahusu Israel tu? Jibu Ni ndio na hapana Hebu msomaji (uwe mvumilivu)
A.      Ndio ahadi hizo zinalihusu kanisa leo
Hakuna taifa ambalo leo ni kanisa na hakuna kanisa ambalo leo ni taifa Mungu anshughulika na mataifa mengi  leo na kanisa lililoko chini ya agano jipya hii ni tofauti kabisa na alivyokuwa akishughulika na Israel wakati wa agano la kale  kwa hivyo hawezi kwa mfano kututia mikononi mwa wamidian au wafilisti au amaleki,kwa sababu eti hqatushiki sheria 600,wala Mungu hajaliahidi kanisa kuwa adui yako atakimbia mbele yako Kumbukumbu 28;7 bali kinyuma na hayo Yesu amehaidi kuwa watatutesa watatusaliti na kutuchukia kwa sababu ya imani yetu angalia yaliyompata Paulo 2Koritho 11;24-27 “Mara tano nimechapwa viboko arobaini kasoro kimoja na Wayahudi. Mara tatu nalichapwa kwa fimbo, mara moja nalipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa. Katika safari za mara kwa mara, hatari za kwenye mito, hatari za wanyang'anyi, hatari kutoka kwa watu wangu wenyewe, hatari kutoka kwa watu Mataifa, hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi, ninajua kukaa njaa na kuona kiu, nimekaa mara nyingi bila chakula, nimesikia baridi na kuwa uchi”.
 Maadui wa Paulo hawakukimbia na badala yake walimuandama mji kwa mji wala Paulo hakusema kuwa imeadnikwa adui zako watakuja kwa njia moja na watatawanyika kwa njia saba, hakuwa mtakatifu wa agano la kale alikuwa mtakatifu wa agano jipya kwa hiyo hakuweza kunukuu ahadi za agano lililokuwa limepitwa na wakati Waebrania 8;13

 Angalia kisa hiki
Kijana mmoja alikuwa na wachumba wawili mmoja anaitwa Kanuni na mwingine anaitwa Neema kwa msingi huo kijana alikuwa anasumbuka atamuoa nani? Kadi ya kina dada hawa wawili,Kanuni alikuwa mzuri sana na wa kuvutia lakini alikuwa mwanamke wa gharama sana na ingekugharimu kufanya kazi sana ili kumuoa na jamaa alijua kuwa anaweza lakini kanuni ni mlalamishi sana anapokosewa na atanungu”nika sana ukimkosea na baba yake alikuwa tayari kumsaidia kijana yule lakini akishindwa kumfanya Kanuni kuwa na Furaha Kanuni pamoja na baba yake waliahidi kumlaumu milele, tunapokuja kwa Neema naye ni msichana mzuri wa kuvutia wala si wa gharama sana naye anafaa kuwa mke mzuri ni mchangamfu na hana maswala ya kunung’unika na huitaji kufanya kazi sana ili kumpata haukumu mtu anapokosewa wala baba yake hana mpango wa kukuhukumu unaposhindwa kutimiza ndoto zako kwake na wataendelea kukupenda, wewe unajua kuwa ni dhambi kuoa wake wengi je uwewe kama kijana yule ungemuoa nani?

Wakristo wameamua kumuoa Neema na sio kanuni kwa sababu haturuhusiwi kuwaoa wote na kwa msingo huo hatuwezi kuweka tumaini letu kwa ahadi za agano la kale yaani kanuni kwa sababu sio mke wetu kwa sababu tumemuoa neema tunatarajia ahadi zote tulizoahiadiana na neema ,tutafurahia kile anachotupa na hatutatafuta mke mwingine na huo ndio utakuwa uaminifu

B.      Hapana ahadi zile za kale si kwa ajili yetu
Kwa namna nyingine agano jipya ni bora zaidi kuliko agano la kale Waebrania 8;6 ,Mungu hakupendezwa na wale walioshindwa kushika amri zake 600 kwa hivyo aliwatupilia mbali Waebrania 8;9 Mungu ameamua kutukubali sisi kwa imani kupitia Yesu Kristo aliwaahidi wao mchi ya kanaani bali sisi ametuahidi mbingu, aliwaahidi wao kuwa atawashindia dhidi ya adui zao bali ametuahidi sisi mkuwa kama kondoo wa Kuchinjwa katika maisha sisi ni zaidi ya washindi Warumi 8;36-37 na Warumi 8;17-18.
Kumbuka
·         Agano la kale ni sehemu ya agano
·         Agano la kale sio agano letu
·         Maagizo mengi katika agano la kale hayakurudiwa katika agano jipya
·         Sheria za kimaadili za Agano la kale zimerudiwa au zimefanywa upya katika agano jipya
·         Agano la kale sio amri ya  Mungu kwetu lakini ni njia ya kujifunza kwetu
·         Ahadi katika agano jipya ni tofauti na Ni bora zaidi kuliko  ahadi katika agano la kale


KANUNI YA YALIYOTIMIZWA AU YASIYOTIMIZWA KATIKA UFALME WA MUNGU (KINGDOM)
Mtafasiri wa Maandiko ni lazima atofautishe yaliyotimizwa na yasiyotimizwa katika mtazamo wa maswala ya ufalme wa Mungu, Unapozungumzia ufalme unazungumzia serikali au ulimwengu wenye Mfalme Yesu alipokuwa akifundisha kuomba alisema tuombe Ufalme wako uje mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni

Swali sasa ufalme wa Mungu uko wapi? Je umekwisha kuja ? kwanini Yesu aliwafundisha wanafunzi kuomba kuwa ufalme wako uje?Mungu anatawala wapi?na yatafanyika wapi?Je mapenzi ya Mungu yanaweza kutimizwa kwa ukamilifu Duniani kama mbinguni? Kama ufalme wa Mungu hauko hapa kwa ukamilifu wake utakuja lini? Haya ndio maswala tutakayoshughulika nayo katika sura hii

Biblia inazungumza mengi kuhusu ufalme wa Mungu na kwa msingi huo tunapaswa kujibu maswali matatu kuhusu ufalme wa Mungu

1.       Ufalme wa Mungu ulianza lini Duniani?
Tunaweza kusema kuwa Mungu aliitawala dunia akiwa mbali nayo tangu wakati wa uumbaji, aliweka mipaka ya bahari na aliahiza mahusiano ya jua na mwezi na nchi aliamuru wanadamu ndege na wanyama na samaki kuzaliana na kuongezeka na kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka malaki Mungu amekuwa akiwasiliana na ulimwengu kwa hivyo kuna mtazamo wenye kuchanganya kuhusu utawala wa Mungu duniani ulianza lini kwa kuwa katika Shughuli zake
Kwanini ni ngumu kujua kuwa ulianza lini?

Mtahayo 8;11-12 Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni. Lakini warithi wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa na kulia na kusaga meno.’’
2.       Kuna uhusiano gani kati ya ufalme wa Mungu na ufalme wa Mbinguni
Unaposoma kwa makini uhusiano wa ufalme wa Mungu na ufalme wa Mbinguniutagundua kuwa hakuna tofauti na ni kitu kimoja  hii ni kwa sababu ilikuwa desturi katika wakati wa Yesu watu kutumia neno Mbinguni kumwakilisha Mungu kwa hivyo neno mbinguni na Mungu huingiliana katika Biblia
Mifano
·         Mathayo 8;11 – Ufalme wa Mbinguni
·         Luka 13;28-29 – Ufalme wa Mungu
·         Mathayo 11;11 - Ufalme wa Mbinguni
·         Luka 7;28  - Ufalme wa Mungu
·         Mathayo 13;11 - Ufalme wa Mbinguni
·         Marko 4;11  - Ufalme wa Mungu
·         Luka 8;10  - Ufalme wa Mungu
·         Mathayo 13;31 - Ufalme wa Mbinguni
·         Marko 4;30-31 - Ufalme wa Mungu
·         Luka 13;18-19 - Ufalme wa Mungu
Mathayo alimtumia sana neno ufalme wa Mbinguni kwa sababu aliwalenga wayahudi ambao walikuwa hawapendi kumtaja Mungu moja kwa moja kwa kuwa kwao si vizuri kulityaja bure jina la bwana Mungu wako
3.       Ni kwa njia ipi ufalme wa Mungu tayari na yapi bado hayajatimia
Tumegusia awali kuwa ufalme wa Mbinguni ni utawala ambao unatakiwa kuwa na mfalme na ufalme wa Mungu ulikuja na Kristo Yesu hivyo tayari umekwisha anza ingawaje haujatimia kabisa hapa duniani kama sasa umekwisha anza kujifunza Hermeneutics lakini bado hujamaliza kozi hii tutayajuaje ni kwa kutumia chati hii ifuatayo

 CHATI YA UFALME WA MUNGU

Swala husika
Tayari limetimia
Bado halijatimia
1.        Wokovu.
Wakristo wamesamehewa na wanaikulia neema
Wakristo watakamilishwa kufikia kiwango cha utimilifu wa Kristo Efeso 4;13
2.        Maarifa
Tunafahamu kwa sehemu 1Koritho 13;9-12 kwa jinsi ya fumbo
Kisha tutajua kama ninavyojuliwa sana 1Koritho 13;12
3.        Thawabu
Tunayo furaha,amani,upendo,kibali,uhakika,na kujaliwa au kutunzwa
Tazama ninakuja haraka na ujira wangu mkononi kumlipa kila mtu sawasawa na Matendo yake Ufunuo 22;12
4.        Afya
Kwa ujumla tuna afya njema,maombi ya imani yanaponya wagonjwa Yakobo 5;14-15 Mungu ametupa pia madaktari,na madawa ya aina mbalimbali
Hakutakuwa na kifo wala kilio wala maombolezo kwakuwa mambo ya kale yamekwisha pita Ufunuo 22;5
5.        Utajiri
Mungu hukutana na mahitaji yetu lakini sio na tamaa zetu tukitafuta kwanza ufalme wakeMathayo 6;33 wafilipi 4;19
Tutaona na kugusa hazina zote za baba yetu katika ufalme ambao umetunzwa kwa ajili yetu mbinguni Luka 12;32-34
6.        Mateso
Mateso yetu ni ya kipimo na ya muda mungu haruhusu tujaribiwe kupita tuwezavyo 1Koritho 10;13,2Timotheo 2;12,21Petro2;19-23,4;19
Atafua kila chozi, hakutajkuwako kifo wala maombolezo wala kilio wala maumivu mambo yote ya kale yataopita  Ufunuo 21;4
7.        Ulinzi
Wakatimwingine miujiza ya kulindwa inatokea lakini Mungu si kila wakati hufanya hivyo,wakati mwingine huruhusu waizi,ajali na mateso
Kila silaha itakayofanyika kinyume nawe haitafanikiwa Isaya 54;17
8.        Hukumu ya watakatifu
Watakatifu huadhibiwa kwa sehemu  na kuhukumiwa Yohana 15;2!Koritho11;30,Waebrania 12;5-6
Kwani wote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu Kristo ili kila moja apokee kwa yote aliyoifanya alipokuwa katika mwili kama ni mema au mabaya
9.        Hukumu ya waovu
Wenye dhambi hupokea sehemu ya malipo ya dhambi wametengwa kwa muda na Mungu na kuteseka kwa muda kama matokeo ya dhambi zao Efeso 2;1,1Timotheo 5;24
Wafu watafufuliwa na wenye dhambi watahukumiwa sawa na matedno yao na kila ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa katika kitabu cha uzima atatupwa katika ziwa liwakalo moto Ufunuo 20;12,21;8
10.     Hukumu ya Ibilisi
Shetani ametupwa kutoka mbinguni waamini hufurahi kwa ushindi huo kwa sehemu luka 10;18-19
Shetani atatupwa katika ziwa la moto na kuteswa huko usiku na mchana Ufunuo 21;10
11.     Mapenzi ya Mungu
Yanakubalika na watu wachache wengi huyapinga Mathayo 6;18;141Timotheo 2;3-4
Kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri ya kuwa Yesu ni Bwana kwa utukufu wa Mungu baba Wafilipi 2;10-11 Ufunuo 21;1-4

Mtafasiri mzuri wa Biblia anapofundisha maswala yoyote ya ufalme wa Mungu anapaswa kuzingatia yapi yamekwisha kutumia katika ufalme wa Mungu na yapi bado ili asichanganye mambo na ndipo atakuwa amelitendea haki neno la Mungu jambo hili ni muhimu kulizingatia katika eneo hili la ufalme wa Mungu


KUUSHIKA UPANGA KWA UANGALIFU
KANUNI YA KUTAFASIRI MASWALA YA MIFANO (PARABLES)
Katika kanuni ya kutafasiri mifano mtafasiri wa Maandiko anapaswa kuzingatia maswala ya kihistoria pamoja na kukumbuka kuwa kuna somo moja tu katika kila mfano na pia kuweza kuondoa alama ndogondogo zinazo tumika ndani ya mifano hiyo. Katika somo lililopita kuhusu mambo yaliyo tayari na ambayo badi katika ufalme wa Mungu Wayahudi walitarajia kuwa ufalme ungekuja mara moja na ghafla na kuonekana Yesu alijaribu sana kurekebisha dhana hii na hivyo mafundisho mengi aliyoyatoa kuhusu ufalme wa Mungu aliyatoa kwa njia ya mifano, kwa msingi huo maswala ya ufalme yaliyo tayari na yasiyo tayari yatakuwa yakijitokeza ndani ya somo la mifano
A.       Asili ya mifano
Katika eneo huili tutajifunza n amna ya kutafasiri mifano ingawaje kwanza tutapaswa kujifunza nini maana ya mifano, kwa nini Yesu aliitumia mifano na jinsi watu walivyoitumia vibaya mifano
Neno mifano linaweza kutumika katika maana pana na maana ya kawaida  katika nmna pana mifano ni pamoja na Mithali,vitendawili,hadithi,stori nefu na fupi,vijihadithi vya kusadikika na ulinganifu wa mambo lakini katika somo hili tutaitafasiri mifano katika namna isiyo pana ambapo maana yake ni  Hadithi rahisi fupi zenye maana fulani za kiroho
B.       Kwanini Yesu alizungumza kwa mifano
Kama tulivyoona kuwa Yesu alimtumia mifano sana katika mafundisho yake na ziko sababu kama nne hivi zilizopelekea Yesu kufundisha kwa kutumia mifano
1.       Alitumia mifano kwa ajili ya usalama wake
Mafundisho yake yalikuwa ni tishio kwa wengi katika nyakati zake alihukumu maisha na mafundisho yasiyo sahii ya mafarisayo na masadukayo aliwatia changamoto na ilionekana kama wanapoteza nafasi yao na heshima zao kwa watu kwa msingi huo waliamua kumfuatilia ili wapate kumshitaki kwa Maneno au kuatfuta namna ya kukosoa na kupingana naye  aidha Viongozi wa kisiasa kama Herode waliona kuwa Yesu alikuwa kiongozi tishio kwa usalama wao na kwa serikali ya kirumi kwa hivyo walimuona ni hatari kwa hivyo alipotumia mifano na hadithi fupi zenye maana fulani za kiroho maadui zake walikosa jambo la kumshitaki kwa msingi huo matumizi ya mifano ilikuwa njia nzuri ya kujilinda na kuwa salama  wakatambua ya kuwa amewasema wao kwa njia ya mifano marko 12;12 lakini huwezi kuthibitisha
2.       Alifundisha kwa mifgano ili kuwasilisha kweli
Mara nyingi ni rahisi kujifunza kwa kulinganisha mambo kitu kipya kinapowasilishwa katika namna ambayo inalingana na kitu kinachofahamika  tunajifunza kwa urahisi na kukumbuka vizuri na hii ndio maana pamoja na kuwa Yesu alimtumia mifano bado leo mtu akiwasaidia wengine tunamuita Msamaria mwema hata kama hatoki samaria  kwa hivyo mifano hufanya kweli ya Mungu kuweza kuzama ndani kwa urahisi na kukumbukwa  mwalimu yeyote mzuri hutimia mifano kama mjezi mzuri znavyotumia kichapio kujenga matofali karibu theluthi ya mafundisho yote ya Bwana Yesu katika injili zote tatu zifananazo Synoptic gospel ni mifano.
3.       Alifundisha kwa Mifano kwa sababu mifano inafanya kweli iweze kupenya katika mioyo ya watu
Kwa kawaida watu hujilinda wasiumizwe na neno ambalo huwachoma na mtu akijua kuwa unamkosoa ni rahisi kufunga moyo wake ili kupingana au kujilinda na kukosolewa hili ni jambo la kawaida katika maisha ya kibinadamu  lakini inasemekana kuwa watu wengi sana wanapenda Stori kwa msingi huo unapotumia mifano kweli hufika ndani ya mtu bila kuleta madara mfano anagaluia alichokifanya nathani alipokwenda kuonya dhambi ya Daudi 2 Samuel 12;1-4 Daudi aliamua kumuhukumu mtu huyo aliyetenda jambo lile na kumbe alikuwa akijihukumu mwenyewe kwa hivyo ili mtu asijilinde afungue moyo stori zinafaa kupenyeza ukweli
4.       Yesu alimtumia mifano kama njia ya hukumu
Matahayo 13;10-15,
Wanafunzi wake wakamwendea wakamwuliza,“Kwa nini unasema na watu kwa mifano?’’ Akawajibu, “Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao sivyo. Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele, lakini yule asiye na kitu, hata kile alichonacho atanyang'anywa. Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano: ‘‘Ingawa wanatazama, hawaoni, wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi. Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema: ‘‘‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, wakageuka, nami nikawaponya.’
Yesu alimtumia mifano kama njia ya hukumu ilikuwa ni kama Password au kufuli maalumu la kuifunga kweli na ni watu wenye shsuku ya dhati tu ambao wangeweza kuzigundua kweli za ufalme wa Mungu na mtu aliye puuzia angetoka akiwa mtupu matahayo 13;12-13, wayahudi walikuwa wameifanya mioyo yao kuwa migumu  na walifunga masikio  na mcho yao ili wasiwasikilize manabii  Kwa msingi huo Yesu hakutaka kuwaongezea kitu wale waliokuwa wameikataa kweli na hivyo aliificha kweli katika mifano  kama sehemu ya hukumu kwa ajili ya kuasi kwao
C.      Jinsi mifano ilivyotumika vibaya
Kwa Muda mrefu mifano imetumika vibaya au imatafasiriwa visivyo halali kuliko Maandiko mengine yoyote ukiondoa kitabu cha Ufunuo,wakati fulani katika historia ya kanisa mifano ilikuwa ikitafasiriwa kirohoroho Allegorizing hii ni njia mbaya na sio halali ki hermeneutics tunapo ruhusu kila kieneo cha mfano kutumika kuwakilisha kitu kingine  hapo ndipo tunapokuwa hatuhubiri tena neno la Mungu wala hatufundishi tena neno la Mungu  kwani tunakuwa tuko mbali na maana iliyokuwa imekusudiwa na Mwandishi na tunakuwa tumeongoza katika kile ambacho Mungu hakukikusudia  na huo sio uaminifu kwa kusudi ambalo hata Bwana Yesu mwenyewe alikuwa amelikusudia kupitia mfano huo katika karne ya kwanza Augustino alijaribu kutafasiri mfano wa msamaria mwema kirohoroho na hivi ndivyo alivyofundisha
*      Mtu moja aliyekuwa anatoka Yerusalemu kwenda Yeriko ni mwanadamu
*      Yerusalemu ndio mji wa mbinguni wa amani ambapo Adamu alianguka
*      Yeriko inawakilisha kurudi nyuma
*      Wevi wanawakilisha Shetani na mapepo
*      Kumpiga inawakilisha kumshinda katika dhambi
*      Kumuachia inawakilisha kufa kiroho
*      Kupita kwa mlawi kunawakilisha huduma ya kikuhani ya agano la kale
*      Msamaria anamwakilisha Kristo
*      Kumfunga majeraha kunawakilisha kusamehe dhambi zake
*      Kumpaka mafuta kunawakilisha faraja ya Roho
*      Kumpeleka kwa watunzaji ni kumuachia kwa kanisa
Ingawaje mfano umefafanuliwa kwa namna ya kusisimua sana hiki sicho Yesu alichokuwa amekikusudia kukisema kwa kuwa sasa tunajua kwanini Yesu alimtumia mifano na tunajua kwanini si vema kuinyambulisha kwa mtindo huo ni muhimu basi kwa kila mtafasiri wa Biblia kujifunza namna ya kuitafasiri mifano kwa halali

Jinsi ya kutafasiri mifano
Kuna hatua kubwa tatu za jinsi ya kuitafasiri mifano kwa usahii
1.       Tafuta historia ya mazingira ya mfano
2.       Tambua maana ya mafumbo na malengo katika mfano
3.       Tambua kuwa kuna somo moja kubwa ambao mfano huo unalenga kufundisha
TAFUTA HISTORIA YA MAZINGIRA YA MFANO
Ni muhimu kukumbuka historia ya mazingira ya mfano yaani mazingira ya asili ya eneo ambalo mfano umetolewa kwa hivyo ni muhimu kila wakati kujiuliza mazingira ya kihistoria ya mfano, jiulize Yesu alikuwa akamwambia nani mfano huo na kwanini Yesu alimtumia mfano huo kwa mfano kwa habari ya mfano huu wa msamaria
1.       Yesu alikuwa akamwambia nani mfano huo?
Jibu alikuwa akijibu swali la mwalimu wa sheria Luka 10; 25-30
2.       Kwanini Yesu alitoa mfano wa Msamaria?
Jibu kwa sababu mwalimu wa sheria alimjaribu Yesu Luka 10; 25, mwalimu huyu pia alikuwa akijaribu kujitafutia haki yeye mwenyewe kwa hivyo aliuliza Jirani yangu ni nani? Luka 10; 29 Kwa msingi huo Yesu alimtumia mfano kujibu swali la mwana sheria na kujaribu kuweka wazi tabia yake ya kujihesabia haki jinsi ilivyo tofauti na mtazamo wa Mungu
TAMBUA MAANA YA MAFUMBO NA MALENGO KATIKA MFANO
 Katika ulimwengu huu tulio nao kuna milima na vilima watu hawapendi kutoa kipaumbele kuangalia vilima kwa sababu ni vidogo na ni vya kawaida watu huangalia mlima zaidi kwa sababu ni mikubwa na ni nadra milima ina mvuto maalumu kwetu kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa katika mifano kuna vilima na milima mifano ina fafanuzi nyingi ambayo ni sawa na vilima fafanuzi hizo katika mifano kwa kawaida havina maana wala haviwakilishi kweli fulani ya aina yoyote, Lakini kwa njia nyingine Mifano ina maana kuu mbili au tatu kuu ambazo ni mambo ya msingi ya mlima wenyewe kwa mfano katika mfano huu wa msamaria kuna pints kama tatu za msingi zinazosaidia kuuelewa mfano wenyewe
·         Mtu aliyejeruhiwa anawakilisha mtu mwenye mahitaji
·         Msamaria anawakilisha jirani wa kweli anayejali
·         Kuhani na mlawi wanawakilisha majirani wasio jali
Ndani ya mfano huu pia kuna vilima vingi kama Yerusalem, Yeriko njiani, punda, mtunzaji, malipo n.k , lakini hivi sio vya maana viko kwa ajili ya kujenga mfano na hivyo ukijaribu kuanza kuvitfasiri vinaweza kutupeleka mbali katika kuifasiri mifano kwa halali kwa msingi huo tofautisha vilima na mlima kama sheria kuu ya kukuongoza kutafasiri mifano ukikumbuka kuwa kunaweza kuwako points mbili au tatu za kukusaidia kupata kweli ya mfano husika
TAMBUA KUWA KUNA SOMO MOJA KUBWA AMBAO MFANO HUO UNALENGA KUFUNDISHA
Yesu alitoa mifano ili kuwakilisha ukweli moja kuu kwa msingi huo unapaswa uweze kuelezea katika sentensi moja tu maana ya mfano, kwa mafano kwa swala la mfano wa msamaria  somo  “Jirani wa kweli”  usijaribu kutengeneza maana zaidi ya moja ya katika mfano wahubiri wote wazuri na waalimu wazuri wa neno la Mungu hutimia mifano ili kukazia kweli katika mfano wanaotumia mara nyingi mfano moja hutumika kukazia kweli moja na sio vinginevyo kwa msingi huo unapoigundua kweli moja tu amabayo mafano huo unafundisha usijaribu kuiharibu Elimu yako ua Hermeneutics kwa kutafuta maana nyingine Taifa lina mji  mkuu mmoja tu  na mifano ina kweli moja tu inayowakilishwa
KUTAFASIRI NA KUITUMIA MIFANO
Kuna tofauti kubwa kati ya kutafasiri na kutumia mifano ktafasiri ni kufanya kazi ya kutafuta maana na baada ya kutafuta maana unatakiwa uitumie kwa hivyo baada ya kuwa umepata maana kwa mfano wa mfano wa msamaria unapaswa kuitumia kwa watu kwa kuwahamasiha kwamba washufghulike na watu wenye mahitaji kumbuka Yesu alipomaliza kutoa mfano alisema “ Enenda ukatende vivyo hivyo” kwa msingi huo si vema kuwapita watu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo utakuwa umeitendea haki mifano Yesu aliyokuwa akiifundisha

KANUNI YA KUTAFASIRI MASWALA YA UNABII (PROPHECY)
Kutafasiri unabii kunahitaji uwe mnyenyekevu huku ukizingatia Historia ya mazingira, lugha za mafumbo na sheria ya kujirudia kwa unabii Multiple Fulfillment kutafasiri unabii na vifungu vinavyohusu unabii ndio moja ya sehemu ngumu sana katika kuilewa Biblia
A.       Huduma za Manabii  na wajibu wa nabii
Nabii alikuwa ni mnenaji kwa niaba ya Mungu ilikuwa ni sauti ya Mungu, wao walisubiri mpaka neno la Mungu lilipokuja kwao kisha walisimama na kusema kwa mamlaka Asema Bwana wa majeshi, Kusudi kubwa la unabii wakati wote  ilikuwa ni kuwasaidia watu wa Mungu kumjua Mungu na kuyajua mapenzi yake  waliifanya hivyo kwa kutabiri  na kwa kufundisha , moja ya mifano ya kutabiri au kuelezea mambo yajayo ni Isaya 9;6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto Mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa begeni mwake naye ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa amani “ Isaya alitoa unabii huu nyuma ya miaka karibu au zaidi ya 750 hivi lakini anasema kwa ajili yetu kwa hivyo wakati mwingine waandishi wa Biblia walizungumza  wakati ujao kama wakati ulioko ndani ya Agano la kale kuna nabii nyingi sana  kama zile za
·         Kuelekea urtumwani kwa watu wa Mungu, kuokolewa kwao ,kurudi na kutawanywa kwao duniani
·         Kuzaliwa , kuteseka , kufa na kufufuka kwa Masihi,kuja kwake mara ya pili na ufalme wake milele
Kadhalika katika agano jipya kuna nabii nyingi za nyakati zile na nayakati zijazo kwa mfano Njaa ya Yerusalem, kukamatwa na kufungwa kwa Paulo, kubomolewa kwa Yerusalem na nayakati za mwisho kwa msingi huo aidha nabii alitabiri katika agano la kale au jipya kusudi linabaki lilelile kuwa ni kuwasaidia watu kumjua Mungu na kuyajua mapenzi yake kwa hivyo huduma ya kinabii ilihusisha kufundisha na kutabiri yaani kulisema neno la Mungu kwa jamii iliyokuweko na itakayokuja.
B.       Chunguza mazingira ya kihistoria ya unabii
Hatuna Vitabu vya unabii kutoka kwa Ibrahimu aliyeishi miaka 1800 K.K mpaka kwa Daudi aliyeishi miaka 1000 K.K Vitabu karibu 16 vyote vya kinabii katika agano la kale viliandikwa kati ya miaka 750 – 460 hivi miaka hii ilifunikwa na maswala ya kisiasa,vita,uchumi na mamabadiliko katika jamii na kulikuwa na hali za kutokumcha Mungu na kulivunja agano la Mungu alilowapa kupitia Musa mtumishi  wake  watu walikuwa wakiongezeka na mipaka ilikuwa ikibadilika kwa msingi huo Mungu aliwainua Manabii kuwakumbusha Israel agano lake .
Sasa basi ilikuvielewa Vitabu vya kinabii vyote 16 vya agano la kale inakupasa kujua historia ya mazingira ya unabii ulikotolewa jiulize maswali muhimu yafuiatayo
1.       Unabii ulitolewa kwa nani Israel au Yuda?
2.       Unabii ulitolewa wakati gani? Kabla au baada ya kupelekwa utumwani?
3.       Kwa nini unabii ulitolewa ni kwa ajili ya kuwataka watubu au kuwatia moyo? Baada ya kujiuliza maswali ya muhimu kama hayo ndipo sasa unaweza kujua vema mazingira ya unabii yalikuwa ya jinsi gani?
C.      Chunguza Lugha za mafumbo ndni ya unabii
Tulizungumza awali kuwa ikiwezekana kila kifungo cha Maandiko kitafasiriwe kama kilivyo kwa njia rahisi na ya kawaida  Lakini kwa maswala ya unabii wakati mwingine ni lazima upambanue mafumbo Vitabu vingi vya kinabii kama Ezekiel,Daniel na Zekaria vina utajiri wa mafumbo na katika agano jipya kitabu cha Ufunuo wa Yohana  nacho kina lugha nyingi za mafumbo tunapaswa kuyaelewa vema kwa mfano hebu angalia mafumbo yaliyoko katika Ufunuo wa Yohana na maana zake kama yalivyoainishwa na moja ya wasomi
·         Nyota saba 1; 16 zinawakilisha malaika saba 1; 20
·         Taa yenye vinara saba 1; 13 inawakilisha makanisa Saba 1; 20
·         Mana iliyofichwa 2; 17 inawakilisha utukufu wa Yesu Kristo Kutoka 16; 33-34.Waebrania 9; 4
·         Nyota ya asubuhi 2; 28 inawakilisha kurudi kwa Yesu kabla ya kuja kutawala Ufunuo 22; 16,2Petro 1; 19
·         Ufunguo wa Daudi 3; 7 unawakilisha nguvu ya kufunga na kufungua Isaya 22; 22
·         Taa Saba za moto roho Saba za Mungu 4; 5
·         Wenye uhai 4; 7 wanawakilisha tabia ya Mungu na macho saba yanawakilisha Ufunuo kamili wa Roho wa Mungu 5;6
·         Chetezo cha dhahabu kinawakilisha Maombi ya watakatifu 5; 8
·         Farasi na wapanda farasi 6;1 zinawakilisha mpangilio wa matukio ya takayoendelea wakati wa dhiki kuu
·         Nyota iliyoanguka 9; 1 inawakilisha Shetani 9; 11
·         Nyota za mbinguni 12;4 inawakilisha malaika walioanguka 12;9
·         Mwanamke na mtoto 12;1-2 inawakilisha Israel na Kristo 12;5-6
·         Shetani anatajwa kama dragoni kama nyoka wa zamani na shetani 12;9,20;2
·         Nyakati na nayakati na Nusu ya nyakati 12;14 ni sawa na siku 1260 12;6
·         Myama kutoka Baharini 13;1-10 mtawala ajaye kutoka ulimwenguni na tawala zake
·         Mnyama kutoka katika inchi 13;11-17 Nabii wa uongo 19;20
·         Kahaba  17;1 unaelezwa kama mji mkubwa 17;18kama babeli mkubwa 17;5 kama aketiywe juu ya vilima 17;9, inatafasiriwa kama wakristo waliorudi nyuma
·         Maji 17;1inawakilisha watu wa ulimwengu huu17;15
·         Pembe 17;12 falme kumi zinazoambatana na yule mnyama  na mengineyo mengi .
Jambo la muhimu tunaloliona hapa ni kuwa wakati mwingine Biblia inatabiya ya kutafasiri yenyewe lugha zile za kimafumbo  kwa mfano Yohana mwenyewe anatuambia kuwa Zile nyota saba ni  malaika saba 1;16, na 1;20 kwa msingi huo pale inapotokea kuwa maana imetolewa na mwandishi mwenyewe tunaweza kuhubiri kwa ujasiri na kwa furaha  lakini wakati mwingine historia itatusaidia namna ya kuweza kutafasiri mafumbo hayo kwa mfano wa ile ndoto ya nebuchadneza  ambapo tunajifunza falme zilizofuata baada ya Babeli lakini pale unapokutana na mafumbo magumu usiyoyafahamu basi haya ni mambo ya msingi ya kuzingatia
1.       Tafasiri katika hali ya kawaida na rahisi mfano Mika 5;2 Masihi atazaliwa Bethelehemu hili liko wazi
2.       Tafasiri kwa kuzingatia kuwa kuna lugha za mafumbo kwa mfano Malaki alitabiri kuja kwa matangulizi wa masihi na alimtaja kuwa ni Eliya  Malaki 4;5-6  Lakini nabii aliyetokea kumtangulia masihi alikuwa Yohana Mbatizaji Yohana 1;21 na Kristo alikubaliana nalo Yohana 17;10-13 Yohana mwenyewe alisema mimi siye Eliya Lakini Yesu alisema ndiye
3.       Chunguza na kufahamu kuwa unabii una tabia ya kutumia zaidi ya mara moja kwa mfano Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa Isaya 9;6 Ni kweli mtoto Yesu alizaliwa kwa ajili yetu lakini wakati huu uweza wa kifalme haukuwa Begani mwake mpaka ajapo mara ya pili kwa hiyo sehemu ya unabii umetimia na sehemu bado na mara nyingi Manabii walipotabiri kuhusu kuja kwa Yesu hawakutofautisha ni ujio upi wa kwanza au wa pili hii ni kwa sababu inasemekana wao waliona ujio wa Yesu kama mlima mmoja kumbe kulikuwa na milima miwili




Nabii
                                             Mlima wa Kalivari                                 Mlima wa mizeituni


                                            Mathayo 27; 33                                           Zekaria 14;4


                                                 Zaidi ya miaka 2000

       Idadi ya milima inategemea ni wapi wewe umesimama Manabii wengi walizungumza nabii za kuja kwa masihi kama kitu kimoja sawa na mtu aliyekuwa anaona mlima mmoja kumbe iko milima miwili Kielelezo kwaniaba ya Maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote Home Bible library 2010 Mwalimu wa somo hili

D.      Onyesha roho ya unyenyekevu unaposoma na kutafasiri unabii
Kuna wakati kijana mmoja alijidai kuwa ana majibu yote kwa habari ya maswala ya unabii na alipofundisha kila kitu alionekana akihitimisha kwa kusema asema Bwana wa majeshi na hakutaka hata kidogo mijadala wala kukosolewa na akamwambia mtu mmoja aliyekuwa akimkosoa kuwa nikisema hauko sahihi maana yake hauko sahii kijana huyu alifikia hata kuweka tarehe ya April 2 kuwa ndiyo ilikuwa tarehe sahii kwa ujio wa masihi kwa mujibu wa kitabu cha Daniel alichokuwa akikifundisha , siku moja usiku aliota ndoto akiwa yuko mbinguni na aliona mambo mazuri ya ajabu na mziki mzuri pamoja na kumuona Bwana Yesu akiwa ameketi katika kiti chake cha Enzi kwa unyenyekevu sana na mara akasikia mtu akimshika katika bega na kumwambia ndugu umekuwa ukifundisha maswala ya unabii ambao hata mimi Yesu mwenyewe sijawahi kuwatuma Manabii wafanye hayo je unaweza kunielezea kwa ufupi kile unachokifundisha kabla sijakuruhusu kurudi duniani kisha jamaa alistuka na kumbe ilikuwa ndoto Tangu wakati huu ndugu huyu alijifunza kuwa mnyenyekevu na kuwa na tabia ya kuwasikiliza na wengine
Kwa ujumla katika Eneo hili tumejifunza maswala ya muhimu Matano
1.       Kutafuta historia ya Unabii
2.       Kutambua lugha ya mficho iliyotumika katika unabii
3.       Kuamua kama unabii huu unapaswa kutafasiriwa kwa urahisi na kawaida au kama fumbo
4.       Kukumbuka kuwa unabii una tabia ya kutumia zaidi yamara moja
5.       Kuwa na tabia ya unyenyekevu unapotafasiri maswala ya unabii

MAMBO YA MSINGI YA KUYAZINGATIA KATIKA KUTAKA KUIFAHAMU BIBLIA NA KUITAFASIRI KWA HALALI.
Soma Biblia kwa kujiuliza maswali Mtafasiri mzuri wa Biblia anapaswa kusoma Biblia kwanza kwa kujiuliza maswali ili baadaye afanye kazi ya kuyajibu na kuyachanganua ili kutafasiri Biblia kwa halali Kuna maswali mengi ya kujiuliza Mtu anapokuwa anaisoma Biblia miongoni mwa mambo ambayo unaweza kujiuliza ni pamoja na
·         Kwa nini Daudi alikwenda kuwasaidia wafilisti? 1Samuel 27;1-7
·         Tarshishi iko wapi na kwanini Yona alitaka kwenda huko? Yona 1;3
·         Inakuwaje Yesu alikasirika na kuwatoa nje wababdilisha Fedha kipi kilikuwa si sahii Mathayo 21;12-13
·         Kwa nini mwanamke msamaria Alisha ngaa Yesu kuzungumzia naye Yohana 4
·         Je Viongozi wa kiyahudi walimtisha Pilato alipotaka kumwacha Yesu huru? Yohana 19;12-13
·         Mwiba wa Paulo ulikuwa ni nini? 2Koritho 12,7-9
·         Kwanini Daudi alibaki Yerusalemu wakati majeshi yake yalipokuwa yamekwenmda vitani ? 2samuel 11;1
·         Je ni kweli Ezekiel alitabiri kuwa urusi itaivamia Israel? Ezekiel 38-39
·         Sanamu aliyoiona Nebukadreza katika ndoto ilikuwa ina maana gani Daniel 2
·         Ni nini Ishara ya mti wa mtini katika Matahyo 24;34
·         Kwanini Yesu anatumia siku za Nuhu kuoanisha na kuja kwake mara ya pili?Matahyo 24;37-39
·         Je wale waliotiwa muhuri yaani 144000 ni akina nani huko mbinguni Ufunuo 7
·         Kwa maana gani Yakobo alizaliwa akiwa amesmhika Esai kisigino?Mwanzo 25;26
·         Yesu alikuwa ana maana gani kusema atalijenga kanisa lake juu ya Petro Mathayo 16;18
·         Mwandishi wa zaburi anasema Mungu yuko kila mahali hatya kuzimu ana maana gani? Zaburi 139;8
·         Je Yesu aliweka kiwango cha kusamehe tunapokuwa tumekosewa na wenzetu? Mathayo  18;22
·         Kwa Nini Mungu ambaye aliupenda ulimwengu wote aseme nimempenda Yakobo lakini nimemchukia Esae?Malaki 1;2-3
·         Kwanini Ni rahisi kwa ngamia kuopenya katika tundu ya sindano? Luka 18;23-25
·         Je Yesu aliposema ombeni lolote kwa jina langu je tunaweza kuomba jambo Baya? Yohana 14;14
·         Inakuwaje watu wa kila taifa walikuwako Yerusalemu siku ya Pentekoste? Matedno 2;5
·         Kwanini jina Nyota ya alfajiri lilitumika kwa shetani na pia linatumika kwa Yesu? Isaya 14;12
·         Kwanini Yohana alimtumia namba 666 kama alama ya mpinga Kristo? Ufunuo 13;18
·         Kwanini Adamu na Hawa hawakufa mara baada ya kutokumtii Mungu Mwanzo 2;15-17
·         Je kaini aliwekwa alama ya namna Gani? Mwanzo 4;3-4
·         Kaini alioa mke kutoka wapi? Mwanzo 4;17
·         Kwanini Mababa kabla ya Gharika walioishi miaka mingi sana ? Mwanzo 5
·         Hao wanefili ni akina nani Mwanzo 6;1-4
·         Je Gharika ilikuwa ya ulimwengu mzima? Kama ndio wanyama walifikaje kwenye visiwa?
·         Kwanini Kanaani alilaaniwa wakati dhambi ilikuwa ya baba yake? Mwanzo 9;25-27
·         Kama Esau alimsamehe Yakobo na alikuwa na amani naye kwanini alikuja kumpokea na watu wa vita 400 Mwanzo 32;6
·         Kwanini Mungu aliruhusu Yefta kuweka nadhiri ngumu na kumtoa mwanae sadaka ya kuteketezwa? Waamuzi 11
·         Nini kilipelekea Isarel kuhitaji mfalme Mwanadamu kama Mungu alikuwa Mfalme wao? 1Samuel 8
·         Kwanini Mungu alimchagua Sauli nkisha akamkataa je si alifanya makosa kwa kumchagua kisha akabadili mawazo? 1Samuel 10-12
·         Je Elisha alikuwa mara mbili zaidi ya Eliya 2Wafalme 2;9-14.
·         Kwanini Mungu aliruhusu Ayubu kuteseka huku anajua kuwa alikuwa mwenye haki Ayubu 2;3,6
·         Je inawezekana mtu aliyeokoka akapoteza wokovu Waebrania 6;4-12
·         Kama kunywa ni dhambi kwanini Yesu mwenyewe alitengeneza Divai? Yohana  2;1-11,1Timotheop 5;23
·         Paulo anafundisha kuwa wanawake wawatii waume zao jambo hili lina maana gani? Efeso 5;22-33
·         Kwa namna Gani Yakobo na Ayubu wanasema walimuona Mungu na Yohana anasema hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu wakati wowote  hili lina maana Gani
·         Kama Paulo hakuruhusu wanawake kuwa na mamlaka juu ya wanaumeKanisani kwanini wanasimikwa leo?
Maswala ya msingi ya kuyazingatia wakati wa kutafasiri Maandiko
·         Kumbuka kutafasiri kama ilivyoandikwa ni moja ya njia nzuri ya kutafasiri kwa usahii
·         Usitafasiri mafumbo katika hali ya kawaida
·         Acha Maandiko yajitafasiri Yenyewe
·         Usijenge fundisho katika mstari wenye utata au ulio mgumu
·         Achilia fundisho lililo sahii lisaidie kujua kile kisichoeleweka
·         Tafasiri yoyote ya Maandiko itokane na Maandiko
·         Usitumie andiko gumu kutafasiri andiko gumu
·         Unapokutana na majina ya ukoo fulani lazima ujiulize kusudi lake
·         Usitumie maswala ya kihistoria kujenga fundisho
·         Usipindishe ukweli wa Maandiko kwa ajili ya kukwepa hitimisho lisilo pendeza
·         Usitafasiri mafumbo kupitiliza au kupita kiasi chake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni