Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na hatari ya Ugonjwa wa Ukimwi !



Somo la Tisa
Vijana na Hatari ya ugonjwa wa ukimwi
Ukimwi uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka 1983,ambapo wagonjwa watatu waligundulika katika hospitali ya  Ndolage mkoani kagera,Mwaka 1984 wagonjwa zaidi walionekana mkoani kilimanjarommoja,na tabora wawili,1985 mikoa nane kati ya 20 iliripotiwa kuwa na wagonjwa hivyo kulikuwa na wagonjwa kati ya 404 amabao kati ya hao 322 walikua mkoani Kagera;1986mikoa yoote ya Tanzania iliripotiwa kuwa na wagonjwa hadi mwaka 2001 december wagonjwa wapatao 144,498 waliripotiwa wagonjwa hao ni wale walioripoti mahospitalini na inakisiwa kitaalamu kuwa kati ya wagonjwa (5) Watano ni mmoja tu anayeripoti hospitali,Umri wa wagonjwa hao ni kati ya 20-49,kiwango kikubwa zaidi ni 25-34 na 30-39 hivyo unaweza kuona kuwa kundi kubwa la wanaoshambuliwa ni vijana.ukimwi sasa umesambaa mara dufu zaidi na karibu kila familia imewahi kuona machungu ya ugonjwa huu Hivyo kama kanisa hatuwezi kuacha kuzungumzia  swala hili  Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo manne yafuatayo;-

  • Maana ya ugonjwa wa Ukimwi.
  • Njia kuu za maambukizi ya ukimwi.
  • Athari za ugonjwa wa ukimwi.
  • Wajibu wa kanisa katika kukabiliana na tatizo la Ukimwi.
Maana ya ugonjwa wa ukimwi.
   Neno ukimwi ni kifupi cha maneno matatu yafuatayo ambayo ni Ukosefu wa Kinga,Mwilini kwa kiingereza AIDS yaani “ A Human Immune Deficiency Syndrome”Ugonjwa huu husababishwa na  vijidudu vidogo sana kuliko bacteria ambavyo huitwa Virisi Vya Ukimwi (V.V.U) kwa kiingereza (H.I.V) yaani Human Immunodeficiency virus. Vijidudu hivi hushambulia chembechembe nyeupe zilizopo katika mwili ambazo ni kinga au askari wa mwili kwa watu wa duniani ni ugonjwa mpya lakini kwa watu wa biblia huu sio Ugonjwa mpya Magonjwa kama ukimwi yaliahidiwa katika biblia kwa watu watakaoishi kinyume na kanuni za kimungu (Kumbu 28;15,27,35,58-61),kinga ya mwili ilianza kuharibika mara tu baada ya anguko la mwanadamu katika Bustani ya Edeni,mungu alimuumba mwanadamu aishi milele lakini mungu alimuhakikishia kifo Adamu endapo angeishi kinyume na kanuni zake na kwa kutokutii kwake na kuula mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2;15-17) Ni tangu wakati huu basi kinga ya mwili wa binadamu iliharibika wanadamu walianza kuzeeka,kupatwa na magonjwa,kupunguziwa siku za kuishi kula kwa jasho kuzaa kwa uchungu na taabu za kila namna hivyo mtu awe na ukimwi au asiwe nao kufa atakufa tu,Mwili hauna tena uwezo wa kumfanya mtu asiwe na uwezo wa kupatwa na magonjwa (2Koritho 5;1-4) Mauti ni matokeo ya dhambi, na kwa kweli Mungu ataihukumu kila aina ya dhambi tuifanyayo iko ahadi ya adhabu kwa waasherati(Ebrania 13;4),hapa hatuukumu kuwa kila mtu aliye au anayeugua ukimwi ameipata kwa zinaa hapana wala wao sio wakosaji wakubwa lakini mkazo hapa ni kuwa dhambi yoyote aifanyayo mwanadamu mshahara wake ni mauti (Warumi 6;23)watu woote wanaofanya dhambi zaidi ya zinaa wanahakikishiwa kutokuurithi ufalme wa Mungu (wagalatia 5;19-21 Wakoritho 6;9-10).

Njia kuu za Maambukizi ya Ukimwi.
Njia kuu za maambukizi ya ugonjwa huu wa  Ukimwizilizofanyiwa utafiti Tangu ukimwi ulipoanza ni kama ifuatavyo kulingana na viwango vya juu mpaka vya chini
  1. Tendo la Ngono au kujamiiana
  2. Kuongezewa damu
  3. Maambuklizi ya watoto wakati wa kuzaliwa
  4. vitu vyenye ncha kali.
Hizo ndio njia kuu za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,Hata hivyo kwa mujibu wa utafiti ambao umefanywa kwa jamii kuhusu maambukizi umebaini kuwa waathirika zaidi wa ugonjwa huu ni wana ndoa wakifuatiwa na makundi mengine hizi ni takwimu za mwaka 2000 takwimu hizi ni kama ifuatavyo;-

  • Watu walio na ndoa waliongoza kwa asilimia 48%
  • Watu walioishi bila ndoa (Mabachela,Singles n.k) 32%
  • Watu waliooana na kuachana 6%
  • Watu waliotengana 5%
  • Watu ambao hawajaoa wala kuolewa lakini wanafanya ngono ni 2%.
Takwimu hizi ni sahihi Kiroho tunaweza kusema ukimwi unawashambilia zaidi watu walioko katika ndoa kwa nini huenda ni kwa sababu ya matendo ya kutokuwa waaminifu katika ndoa zetu.

Tabia ya Virusi vya ukimwi katika Picha.
                
                       Kirusi                    Chembechembe       Virusi vipya baada 

                                                               Nyeupe                 ya niezi mitatu

   Pichani juu kirusi kipya kinapoingia mwilini huishambulia chembechembe nyeupe ya uhai katika damu ambayo ni ngumu sana kushambuliwa lakini kirusi huishambulia na kuifanya chakula kasha baada ya miezi mitatu kirusi huzaliana kwa wingi zaidi na kila kimoja hutafuta chembechembe nyeupe nyingine ili kuishambulia Virusi vimekuwa vikiwasumbua wanasayansi kwani ni kidogo sana na hujibanza kwenyekinga ya mwili hivyo kupata dawa ya kukishambulia bila kuidhuru chembechembe nyeupe ni ngumu kwani huishi ndani yake,pia vina tabia ya kubadilika badilika na kinajitengenezea kinga gamba gumu,Kadiri mtu anavyofanya zinaa ndivyo anavyojiongezea maambukizi zaidi ya virusi vipya vyenye tabia mpya na kujiweka katikahatari ya kufa kwa haraka ni vizuri kujilinda kwa Mungu.

Athari za ugonjwa wa ukimwi.

Kupungua kwa wastani wa umri wa kuishi.
Kupungua kwa wastani wa umri wa kuishi ni moja ya athari zitokanazo na ukimwi,na ni swala la kimaandiko,Maandiko yanatufundisha  jinsi ambavyo mtu anaweza kuishi siku nyingi pale anapomcha Mungu (Mithali 10;27),Mungu alipunguza miaka ya kuishi kwa mwanadamu kadiri uasi ulivyokua ukiongezeka,Babu zetu tangu Adamu waliishi zaidi ya miaka mia tisa hivi 900,(Mwanzo 5;5,8,11,n.k.) Baada ya uovu kuongezeka umri wa kuishi ulipunguzwa kufikia miaka 120 (Mwanzo 6;1-3),Wakati wa Musa Mungu alimfunulia Musa kuwa amepunguza umri wa kuishi mwanadamu mpaka miaka 70 na kama ana nguvu 80 (Zaburi 90;10).Baada ya miaka michache hii ukimwi umezifanya nchi nyingi za kusini mwa sahara zikiwemo Afrika kusini,Zimbabwe,Angola n.k kuwa na wastani wa kuishi kati ya miaka 45-30 hivi.

Ongezeko la watu Tegemezi (Yatima na Wajane).
Mtu awaye yoote asiyepiga vita ukimwi haelewi analolitenda,Ukimwi umeiathiri kila familia,ukoo,na jamii,umefika wakati ambapo jukumu la kutunza Wajane na Yatima limekuwa kubwa kiasi ambacho hatutaweza kukwepa kutunza Wadogo zetu,watoto wa kaka zetu,Dada zetu,wajomba zetu,shangazi zetu,binamu zetu,mama zetu wakubwa,mama zetu wadogo, baba zetu wakubwa,Baba zetu,wadogo, n.k.Lazima tuwatunze na kuwapa elimu ya kutosha kwa kipato cha Afrika hili ni jukumu Kubwa sana na endapo hatutawapa elimu ya kutosha tutakuwa na kanisa jinga,na Taifa jinga,fgamilia jinga Jukumu la kuwatunza yatima na wajane  kibiblia ni jukumu la wakristo wa kweli (Yakobo 1;27)

Kupungua kwa watenda kazi
Ukimwi unaua wataalamu wengi,wakulima,wafanya biashara,wazalishaji viwandani,na unadhoofisha utendaji makanisani nk.Mtu mwenye ugonjwa wa ukimwi huugua mara kwa mara ,hivyo wanaweza  wasiwepo kazini mara kwa mara,hali kadhalika kanisani ,mashuleni n.k Jaribu kuwaza Mwalimu mwenye ukimwi au mwanajeshi mwenye ukimwi anawezaje kuwajibika na kulipigania taifa  Hali ya uchumi ni dhahiri pia kuwa itadidimia

Kuongezeka kwa gharama za matibabu
 (Kwa sababu ya kuugua kwa Muda mrefu) Kama tunavyofahamu tabiya na mwenendo wa ukimwi Tangu mtu anapogundulika kuwa ana virusi vya ukimwi na hasa cd4s zinapokuwa chini anatakiwa aanze tiba bila kukosa na kwa tabia ya ukimwi watu hawa huugua kwa Muda mrefu jambo hili linapelekea kuongezeka kwa gherama za matibabu na lishe.Aidha kutakuweko wimbi la kuongezeka kwa watu waliokosa Matumaini,walioathirika kisaikolojia,kusambaratika kwa familia,ukiwa,upweke,misiba na huzuni,shutuma mauaji na visasi au ulevi wa kupindukia pia kuongezeka kwa tatizo la Unyanyapaa nk .Hizi zoote ni athari za Kuwepo kwa ugonjwa wa ukimwi.

 Wajibu wa kanisa katika kukabiliana na tatizo la Ukimwi
  Ni muhimu kufahamu kuwa kanisa linawajibika na swala zima la tatizo la ukimwi Mchungaji na washirika  amabao wanadhani wako salama na wanaufurahia wokovu wakifikiri kuwa wao hawana ukimwi wanajidanganya,suluhisho la tatizo la ukimwi haliko nje ya taasisi yoyote ile wala dini yoyotre ile wala serikali yoyote Macho ya mungu yanaliangalia kanisa kama chombo chenye majibu ya kutosha kwa swala zima la ukimwi ni Biblia pekee yenye majibu ya kutosha ,matumaini ya kutosha ,kinga ya kutosha  na matibabu ya kutosha kuhusiana na swala la ukimwi Kumbuka kuwa wanaoathirika sasa wengi wao hukimbilia kanisani wakihitaji msaada wa kiroho sasa kama kanisa litakwepa wajibu huu na kujikita katika kunyanya paa wakati kanisa ndilo lenye majibu ya kimaadili,ya waliochanganyikiwa,ya waliokata tama,ya walio na wasiwasi,ya waliona mashaka na tukasimama kuhukumu na kushutumu Je watu hawa wa Mungu wakimbilie wapi? Kule Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari watu wengi walikimbilia makanisani wakifikiri wangekuwa salama lakini kwa kuwa kanisa lilikuwa limeshindwa kusimama katika nafasi yake na dhambi ya kibaguzi ilikuwa imewatafuna hukohuko walikokimbilia watu ndiko waliko uawa Ukimwi unalipa kanisa wajibu mzito sana ni wajibu ambao ni zaidi ya kuhubiri injili,Kanisa linawajibika kuwaonya watu,kufundisha ,kutoa matumaini,kufariji,kupinga vitendo vya unyanyasaji dhidi ya waathirika,kutoa jibu mbadala zaidi ya kondom ambayo ndiyo majibu ya mkato ya dunia hii,Kuwa na miujiza ya uponyaji ili kwa maombezi wagonjwa hao wapone na endapo hawatapona wajiandae kufa kishujaa wakiwa wamejaa matumaini na kuwa tayari kukabiliana mauti wakimuamini Mungu. Wakiwa na ushuhuda wa huduma juhudi na bidii ya kanisa Dhidi yao. Ni kwa msingi huu kanisa linawajibika
  1. Kutoa majibu ya Yaliyoshindikana kwa Dunia
Mungu anayo majibu ya yaliyoshindikana kwa dunia na serikali,majibu haya hayapatikani kokote isipokuwa katika neno lake kupitia kanisa,hata kama hatujasikia kokote kua Mungu anaponya ukimwi kanisa ni lazima liwe na majibu ya jinsi kama hii Kuwa Mungu anaponya Elisha hakuwahi kusikia au kusoma popote kuwa ukoma unapona lakini pale serikali iliposhindwa kutoa majibu ya uponyaji kwa ukoma Eilsha alikuwa tayari kutoa majibu ya swala lililoshindikana soma (Wafalme 5;4-14)
  1. Kondomu sio suluhisho la kujikinga na ukimwi.
Kanisa linaposimama  katika zamu yake  ni lazima lisimame  kama nabii kuonya na kuonyesha njia dunia inapoamini kuwa ,lazima mtu abakie na mpenzi mmoja muaminifu lazima tutoe majibu kuwa hakuna mtu anaweza kuwa muaminifu  bila kukutana na Yesu kristo hivyo ni lazima tumuonyeshe Kristo kuwa ni njia na kweli na uzima,Mtu kuwa na mpenzi mmoja maana yake ni lazima  awe mke halali na Mume halali Kanisa lazima lionyeshe kuwa huwezi kuwa na mpenzi mmoja muaminifu nje ya Kristo na ndoa ya kikristo,Ndoa zozote zenye kuruhusu wake zaidi ya moja kwa sasa hazina soko tena sera ya kibiblia ya mke moja mume moja inauzika kwa sasa,Dunia inaposema ikishindikana tumia kondom kanisa ni lazima lionyeshe kivitendo kupingana na dhana kwa sababu  ni lazima tujiulize kwanini ukimwi haupungui hata pamoja na kuwepo kwa matangazo ya kutosha kuhusu ukimwi na matumizi ya kondom,Kwanini uwezo wa kondom kuzuia ukimwi unapewa asilimia 70 tu,Kwanini ziwepo za viwango tofauti na bei tofauti lazima tuonyeshe jibu la kweli kuwa kondom si salama ikilinganishwa na nguvu ya utendaji wa mwili na tama zake,kimsingi kondom ziligunduliwa zamani zaidi kabla ya ukimwi kwa kusudi la kupanga uzazi kama kondom haina uwezo wa kuzuia kwa asilimia 100 ni wazi kuwa si kinga kamili

Kanisa ni lazima lisimame katika zamu yake.
    Kanisa kama nabii ni lazima lionye na kukemea na kuonyesha njia iliyo sahihi (Ezekiel 3;16-19) Lazima tuchukue tahadhari ya kutosha katika kuwashauri na kuwaandaa maharusi huku wakipimwa kabla ya ndoa,
   Kanisa kama Mchungaji lazima liwajibike kufariji Ezekiel alikuwa nabii aliyetoa maonyo sana juu ya Yuda kwenda utumwani Babeli lakini ilipotokea kuwa watu wamekwenda utumwani hakutoa tena maonyo badala yake alisimama kuwafariji,hata kama tunakemea uovu hatuwezi kuacha kuwapokea walojeruhiwa na kuendelea kuwahukumu bali tunapaswa kuwaganga(Ezekiel 34;1-10,371)
   Kanisa kama Mwalimu lazima liwafundishe watu hususani vijana kusubiri na kungoja wakati halali wa kufanya mapenzi, lazima lifundishe maadili na usafi wa ndoa ya kweli ya mke moja na mume moja waaminifu, lazima tufundishe kujali na kutokuwanyanyapaa waathirika ila wajisikie wako katika mikono salama ya wakristo
    Kanisa kama wainjilisti tunawajibu wa kuwakaribisha waathirika na kuwaonyesha njia ya halali nay a kweli ya kuishi kwa matumaini
 Mwisho kanisa ni lazima lipambanena tabia ya unyanyapaa tukumbuke kuwa wakati watu waliwatenga wenye ukoma nyakati za biblia Yesu aliwagusa (Luka 5;12-13) Wakati dunia inakataa kukaa na wenye ukimwi na kuchochea kifo cha haraka cha watu hawa ama kuwaona kuwa ni wenye dhambi sana kanisa lazima litambue kuwa wanahitaji upendo wetu,faraja,kujali na kuwa ni wakristo pekee wanao weza kuonyesha hayo. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni