Alhamisi, 11 Februari 2016

Wokovu ni nini?



Wokovu ni nini?
Neno wokovu kwa asili lina maana ya kuwekwa huru, neno linalotumika kuelezea kuhusu wokovu lina asili ya kiyunani “Soteria”Kwa kiingereza “Deliverance” ambalo maana yake ni kuwekwa huru, kuokolewa hatarini, kulindwa na hatari, kusamehewa dhambi na kuponywa magonjwa yako yote na kufutiwa hatia yote, ni kuondolewa katika hali ya hofu, kulindwa na maadui zako, kusitiriwa, na kushindiwa vita, Kuondolewa hali ya aibu,n.k. Kazi hizi zote hufanywa na Mungu kwa kiebrania neno wokovu linachanganuliwa  kwa maneno Yeshu’ah” “Yesa” na  tesu’ah  sawa na jina Yesu. Ambayo kwa ujumla yana maana ileile kama ya kiyunani pia liko neno la kiyunani Sozo ambalo pia lina maana ya kuokoa, kutoa katika migandamizo au utumwa au kuokoa na hatari.

     Katika mtazamo wa agano jipya wokovu maana yake ni Kazi nzima aliyoifanya Bwana Yesu katika kumkomboa mwanadamu aliyepotea na kumrejesha kwa Mungu, ni kazi ya Mungu mwana kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini na kurejesha uhusiano uliovunjika kati ya mwanadamu na Mungu hii ndio kazi iliyomleta Kristo kufanya Luka 19; 10 Biblia inasema;-

Kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea


Mkazo mkubwa katika agano jipya kuhusu wokovu ni katika kusamehewa dhambi na uhusiano wetu na Mungu kurejeshwa kama ilivyokuwa kwa Zakayo kwa hiyo Kusamehewa na Mungu hakuhitaji juhudi zetu kwani kazi nzima ya wokovu ni mpango wa Mungu mwenyewe na hufanya kwa wale anaotaka mwenyewe kwa neema wala sio kwa juhudi ya mtu au matendo Fulani ya kumshawishi na kumpendeza yeye akionyesha wazi jinsi kazi ya wokovu ni ya upendo na neema ya Mungu Paulo anawafundisha Waefeso hivi;-

“Waefeso 2;8-9 “ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa (Yaani zawadi) cha Mungu wala sio kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu.”

Kwa msingi huo kumbe wokovu hautokani na juhudi za kibinadamu kuupata ni neema ya Mungu neema hii katika Kiebrania hutumika neno Hen na kwa kiyunani  ni Charis ambayo maana yake ni upendeleo pasipo kustahili, kukubalika, ni  kutakiwa mapenzi mema ni wema unaoleta upendeleo kwa mwenye dhambi asiyestahili. kwa hiyo neno hili lina maana ya kuwa Wokovu ni Bure, unatokana na upendo wa Mungu unakufanya uwe mbali na hasira ya Mungu, unakufanya usijihukumu, unakufanya usilipizwe kisasi wala kuufanyia kazi ni upendeleo wa Mungu tu pasipo kazi yoyote. Ndio maana wengi wetu siku ile tulipookoka hatukuhitaji kufunga na kuomba sana, hatukuhitaji kusali sana au kuungama sana hatukufanya bidii ya aina yoyote huenda tulisikia tu injili na tulipoikubali kutoka moyoni tayari Mungu akatukubali tukabadilishwa maisha yetu,tukaondolewa hatia zote, tukajawa na furaha, tukaumbiwa kiu ya kutaka kumpendeza yeye, kumuomba yeye, kumuabudu yeye, kumtumikia yeye kwa sababu ni yeye aliyekuwa akitutafuta wala sio sisi ilikuwa ni zawadi ya bure wala hatukuhitaji kuilipia  ni wema wa Mungu tu usiotokana na historia yetu kuwa huko nyuma tulifanya nini wema huu wa Mungu ndio neema na neema hii ni kubwa sana kwa wanadamu wote lakini kwa waliokolewa ni neema maalumu isiyo ya kawaida.


Aina za Neema.
 Kuna aina kuu mbili za neema
·         Neema ya kawaida Common grace huu ni wema wa Mungu ulio juu ya wanadamu wote bila kujali wanafanya nini au wanamuabudu nani wana dhambi au la  neema hii inaweza kuwafanya wanadamu kuwa wema, kuishi kwa haki kwa utaratibu katika jamii, jamii kupewa mvua, majira na nyakati, chakula na furaha, mavazi na mafanikio mengineyo pamoja na elimu hii ni neema ya kawaida na haina uhusiano wowote na wokovu kwa hiyo neema hii haitoshi kumfanya mtu aokoke ni neema njema inayoweza kusaidia mwanadamu kuitikia neema ya Mungu ya wokovu Neema hii imesababisha watu kuwa na maarifa ya kutengeneza silaha, kufuga wanyama, kuwa na maarifa ya kitabibu na wagonjwa kupona mahospitalini wanapotibiwa, au kukimbizwa hospitali, kuvumbua madawa na tiba za maswala mbalimbali, kuokolewa na ajali mbalimbali na matukio mengine mengi yanayodhihirisha wema wa Mungu kwa viumbe wake wote bila ya upendeleo hii ni neema ya kawaida Common grace.
·         Neema maalumu Special Grace  hii ni neema maalumu inayowezesha kumleta mtu kwa Yesu Yohana 6;44 neema hii inakuja juu ya mtu na kumfanya mtu huyo kugeuzwa nia yake, kuwekwa huru mbali na dhambi, hii ni neema maalumu ya Mungu ni neema inayokuja kupitia Kristo Yesu Yohana 1;17, hii haimaanishi kuwa kabla ya Kristo watu hawakuokolewa hapana watakatifu waliotutangulia waliokolewa lakini Kristo ndio ufunuo kamili wa neema hii ya wokovu neno neema limetajwa mara 38 katika Agano la kale na mara 128 katika Agano jipya na limefafanuliwa kama upendeleo au kibali mara 64 katika Agano la kale na mara 6 katika agano jipya  kwa kawaida neno hili huunganishwa pamoja na Mungu  katika shughuli nzima ya kusamehe na kughairi hukumu au mabaya  mfano soma  Yona 4;2 na Nehemia 9;17

Yona 4;2 Biblia inasema “ Akamwomba Bwana akasema  Nakuomba ee Bwana sivyo hivyo nilivyosema  hapo nilipokuwa katika inchi yangu? Hii ndio sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejawa huruma, si mwepesi wa hasira u mwingi wa rehema nawe waghairi mabaya”

Nehemia 9;17 Biblia inasema “….. Lakini wewe u Mungu mwenye huruma nyingi mwenye neema, mwenye huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema basi hukuwacha”

Kumbe basi katika neema ya Mungu kuna Rehema, Kuepushwa na hasira, kuhurumiwa, na kusamehewa kutoka katika kupatwa na mabaya kwa sababu ya hukumu ya Mungu.Mungu anatamani kumuokoa kila mtu 2Petro 3;9 , lakini  ni wale wenye kuitikia neema hii kwa kuiamini injili na kukiri kuwa Yesu ni Bwana neema hii humshukia na kufanya kitu cha tofauti kabisa katika maisha ya huyo aliyempokea Bwana Yesu ikiwa ni pamoja na kumfundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia na kutufanya kuishi kwa kiasi na haki  na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa.

Tito 2;11-12 Biblia inasema hivi kuhusu kazi ya neema hii maalumu “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa nayo yatufundisha kuukataa ubaya na tamaa za kidunia  tupate kuishi kwa kiasi na haki na utauwa  katika ulimwengu huu wa sasa.

Kumbuka kuwa moja ya kazi ya neema hii maalumu ni kuwaelekeza walioamini  kuwa na uamuzi sahii wa kuzikataa hisia zisizo za kimungu na anasa za kidunia  na kuyaona mambo ya ulimwengu wa sasa kuwa chukizo na inatupa nguvu za kuishi maisha sahii yenye kumcha Mungu, kwa msingi huo mpaka hapo unaweza kukubaliana nami kuwa kuna maswala kadhaa ambayo mtu anapookoka tu anaweza kujua kuwa si mema au mema Moja kwamoja tu kabla ya kujifunza maswala mengine mpaka wakati huu neema ya Mungu inapofanya kazi wokovu unakuwa haujaharibiwa na uko salama yaani hadi hapo mtu huyo anakuwa huru kutoka katika kongwa la dhambi na amani ya Mungu Shalom humfunika.

Wajibu wa mwanadamu katika kuitikia neema maalumu ya Mungu ya wokovu.
Ni muhimu kufahamu ndugu msomaji kuwa pamoja na neema hii maalumu ya Mungu kutolewa bure mwanadamu anawajibika kuwa tayari kupokea zawadi hii ya neema bure Kuna usemi wa zamani wa Kiswahili na hata lugha nyingine kuwa “unaweza kumpeleka Punda kisimani kwa kusudi la kumnywesha maji lakini asinywe” maana yake ni kuwa ni mapenzi ya Mungu watu waokolewe watu wote kama biblia isemavyo katika 1Timotheo 2;1-5

“Basi kabla ya mambo yote nataka dua na sala na maombezi na shukurani zifanyike kwaajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na usatahivu, Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu mwokozi wetu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli.”

Lakini sio kila mmoja anaweza kuokoka kwa sababu Mungu hamlazimishi mtu hivyo watu wengi hukataa wenyewe neema ya Mungu na hivyo kuukosa wokovu na hivyo Mungu anahuzunishwa, Sasa ili mwanadamu aweze kupokea upendeleo huo wenye zawadi za wokovu anapaswa kukubali lakini anakubali namna gani anakubali kupitia hatua muhimu zifuatazo na ambazo hatimaye Mungu huzijibu kwa kufanya mambo kadhaa ambayo hukamilisha wokovu wa mtu huyo anayekubali
1.      Toba ni Muhimu kwa ajili ya kupokea Neema ya wokovu.
Neno Toba “repentance” ni kuhuzunika moyo kwa mujibu wa Biblia ya Kiebrania neno Sigh hutumika ambalo maana yake ni kuhuzunika moyo, kujuta, kughairi, kuomboleza au kuwa na mpango mpya Tunaweza kuona asili ya neno hili katika Mwanzo 6;6-7 Biblia inasema hivi “Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika moyo Bwana akasema nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba  usoni pa nchi mwanadamu na mnyama na kitambaacho na ndege wa angani kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya” kwa msingi huo basi neno kutubu kwa kiibrania ni kuhuzunika na kughairi mpango Fulani uliokuwa nao kwa hiyo kimsingi toba ni lazima iwe na mfuatano wa kuhuzunika moyo na kuchukua hatua madhubuti. Kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili. Kama ulikuwa unafanya jambo Fulani lazima ughairi Kutoka 32; 14, 1Samuel 15; 11

Neno toba Katika Biblia ya kiyunani linatumika neno Metanoeo au metanoia au metamelomai ambalo maana yake ni kuwa na hisia nyingine, au kuhuzunika na kuchukua hatua ni kubadilika hivyo toba ni kuhuzunika na kubadilika au kuhuzunika na kuchukua hatua mfano Mathayo 21: 28-31 Biblia inasema hivi
“Lakini mwaonaje mtu mmoja alikuwa na wana wawili, akamwendea yule wa kwanza  akasema mwanangu nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu, Akajibu akasema naenda Bwana  asiende, Akamwendea Yule wa pili akasema vilevile, Naye akajibu akasema Sitaki baadaye akatubu akaenda , Je katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia ni Yule wa pili…”
Bila shaka ni wazi kabisa kuwa katika mfano huu wa Bwana Yesu alikuwa akionyesha ni nani ametubu toba ya kweli kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili ni sawa na mwana aliyekubali kua atakwenda shambani lakini hakuenda,Yuda alihuzunika alipokuwa amemsaliti Bwana Yesu alifanya vema kuhuzunika  lakini hakufanya mapinduzi dhidi ya huzuni yake Bali aliamua kwenda kujiua hii haikuwa toba kamili, Toba ya kweli hujumuisha kuhuzunika na kubadilika kimtazamo na toba hii ya kweli itapelekea maisha yako kuwa yenye furaha hutakuwa mtumwa wa huzuni tena utawekwa huru kutoka kongwa la huzuni.
Toba ni kama pembe tatu inahusisha pande kuu tatu ili iweze kukamilika na pande hizo kuu tatu zinapokuwa zimekamilika ndipo tunapoweza kusema kuwa hiyo ni Toba kwa hiyo toba inahusisha .Ufahamu (Akili), hisia na utashi au uamuzi.



                                                                                        Ufahamu
               
 Toba
 
Hisia                                                     Uamuzi /ukiri

Ufahamu. (Intellectual aspect)
Ili mtu aweze kufikia toba anapaswa kwanza kuwa na Ufahamu kuwa Amemkosea Mungu, ama hata kwa kuzaliwa kwetu sisi ni wenye dhambi mbele za Mungu, hii ikiwa na maana kuwa sisi ni wenye dhambi kwa kuzaliwa, kutenda, kuwaza kwa namna iwayoyote tumekuwa kinyume na Mungu Hivyo kabla mtu hajafikia toba ni lazima awe na ujuzi kamili kuwa amemkosea Mungu yeye mwenyewe, anapaswa kufahamu kuwa dhambi ni makosa mbele za Mungu zaidi ya kufahamu tu kuwa dhambi ina matokeo mabaya yanayoambatana nayo anatakiwa kujua tu kwamba dhambi inamuhuzunisha Mungu aliyemtakatifu, Daudi alifahamu kuwa alipofanya dhambi na mke wa Uria na alipomuua Uria alikuwa amefanya uhalifu kinyume na jamii, lakini alipotubu alikuwa naufahamu kamili kuwa alikuwa amefanya dhambi kinyume na Mungu Zaburi 51;4 “Nimekutenda dhambi wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako,Wewe ujulikane kuwa na haki unenapo. Utambuzi ya kuwa umemkosea Mungu ndio unaoleta huzuni inayotupelekea kwenye toba. Angalia mfano wa mwana mpotevu na toba yake katika Luka 15;21 Biblia inasema hivi Yule mwana akamwambia Baba nimekosa juu ya mbingu (Mungu) na mbele yako sistahili kuitwa mwana wako tena. Toba inapokuwa kama utambuzi kamili kuwa umemkosea Mungu inaweza kuleta matokeo, wako watu wanaojiona kuwa ni watakatifu sana na wenye kujihesabia haki Mungu anachukizwa sana na roho hii ya kiburi, Mbele za Mungu mtu anayetubu lazima akubali kuwa ametenda dhambi bila kujali kuwa anaishi katika haki kiasi gani Paulo mtume alikuwa ni Farisayo aliyeishi sawa kabisa na sheria ya Musa na wala hakuvunja hata kidogo kila alilolifanya kwa sheria lilikuwa ni haki kabisa hakuwa na hatia  hata pale alipokuwa akiwaua wakristo kwa sheria ilikuwa ni sahii soma Wafilipi 3;6  anasema “Kwa habari ya juhudi mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo na sheria sikuwa na hatia “ unaweza kuona Kwamba kwa Ufahamu wake Paulo alikuwa akimpendeza Mungu lakini siku moja Mungu alimwambia Sauli Sauli mbona waniudhi? Matendo 9;4 alikuwa akifikiri kuwa anampendeza Mungu kumbe anamchukiza na alitakiwa kujihoji na kuchukua hatua ya kuacha dhambi zake mara moja na maisha yake yalibadilika mara baada ya toba ya kweli Mungu amekwisha kusema kwenye neno lake kuwa wote tumefanya dhambi na tumepungukiwa na utukufu wake Warumi 3;23 awaye yote anayekuja mbele za Mungu kwaajili ya kutubu lazima akubali kuwa yeye ni mwenye dhambi mbele zake na neema ya Mungu itabadilisha kabisa mfumo wako wa maisha na kuyafanya kuwa safi kabisa.


Hisia. (Emotional aspect)
Mtu akiisha kuwa ametambua kuwa amemkosea Mungu kwa Ufahamu wake wakati huohuo anakuwa na huzuni kwaajili ya dhambi zake kinyume na Mungu, anasikitishwa na dhambi zake Zaburi ya 38;18 inasema “kwa maana nitaungama uovu wangu Na kusikitika kwa dhambi zangu” Kama mtu anajigundua kuwa amemtenda Mungu dhambi pia atasikitishwa atajutia ataombolezea dhambi zake atajuta Paulo mtume alipokuwa akiokolewa siku tatu aliomboleza akiwa ameacha kula na kunywa Matendo 9;9, hali kadhalika mwana mpotevu alizingatia moyoni mwake na kufanya mageuzi makubwa hali hizi ndizo zinampelekea mtu kuwa na toba kamili Paulo baada ya hapo alikuwa mwenye wivu mkubwa sana wa kumtumikia Kristo na alianza kumuhubiri Matendo 9;17-20

Uamuzi./ukiri (Volitional aspect)
Hatimaye baada ya kuhuzunika kunakuwa na utashi ambao Mungu ametuumba nao hapa ndipo mwanadamu huamua kuchukua uamuzi tunapochukua uamuzi ndipo toba inapokuwa imekamilika kufahamu kuwa umetenda dhambi kwa Mungu na kuhuzunika bila kuchukua uamuzi wa kuacha njia zako mbaya basi au njia zetu mbaya Toba inakuwa haijakamilika  lazima uchukue uamuzi wa kuacha  Mithali 28;13 Biblia inasema “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mtu anapofanya uamuzi wa kuacha njia zake ndipo sasa Msamaha wa Mungu unapopatikana Isaya 55: 7 “Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake  Na amrudie bwana Naye atamrehemu na arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa” .Uamuzi wa mtu una nguvu unapoungwa na Ufahamu kuwa amemkosea Mungu, huzuni ya moyo na uamuzi wa kuacha dhambi unaifanya toba iwe imekamilika na hapo tunakuwa tumesamehewa dhambi na kuupokea wokovu Luka 1;77 “Uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao”
Toba na malipizi.
Baada ya toba wakati mwingine toba inapokuwa imekamilika unaweza kuchukua hatua  za kurudisha mali au vitu vilivyochukuliwa kwa namna ambayo sio halali, hali hiyo ndio huitwa malipizi  ni ushahidi wanje kimaisha na kivitendo kuwa mtu huyo ameamua kubadilika au ametubu kweli  ni moja ya sehemu ya matunda yapasayo toba  Luka 3;8 Zakayo aliwarudishia mara nne wale aliokuwa amewadhulumu  Luka 19; 8 Malipizi yanaonyesha uzito wa toba lakini sio kwa Mungu bali kwa wanadamu, kwa msingi huo malipizi hayaokoi, kwani tunaokolewa kwa neema  lakini malipizi yanatangaza kwa wanadamu kuwa sisi sasa tumeokoka tumeacha njia mbovu za zamani na sasa tunafuata njia mpya  ni pokeo la kivitendo la toba malipizi sio njia ya wokovu lakini ni njia ya kuonyesha kuwa tumeokolewa. Si kila malipizi yanaweza kufanyika, Kristo hakumuagiza Zakayo kufanya, lakini alifurahia Zakayo alivyofanya kufanya malipizi kwa zakayo kulitokana na uamuzi uliosababishwa na Roho wa Mungu mwenyewe endapo wahubiri watakazia malipizi kama jambo la lazima kufanyika wokovu utakuwa ni kitu kizito na cha kuiogopesha sana kwa msingi huo inahitajika hekima sana na kumuacha mtu na moyo wake kuamua nini cha kukifanya na sio kuwashinikiza watu kufanya malipizi endapo utashinikiza Wokovu unaugeuza kuwa Kongwa zito na lisilo bebeka, Amani ya Kristo iamue ndani ya mtu mwenyewe kufanya malipizo.Hili pia lilikuwa fundisho la Agano la kale Kutoka 22;1 na Walawi 6;5,Hesabu 5;6-7 na tendo la Kristo kukaa kimya na kufurahia kilichofanywa na Zakayo sawa na sheria  ni wazi kuwa Yesu amekubali fundisho kuhusu malipizi katika maana ya kuwa ni ushahidi ulio wazi wa kuwa mtu huyo ametubu.

Mafundisho ya Agano jipya kuhusu Toba.
Agano jipya limejaa mafundisho yenye kuwaita watu katika toba mahubiri kuhusu toba yalikuwa ndio kiini kikuu cha mahubiri ya Kristo na Yohana mbatizaji Mathayo 3; 2, 4; 17. Kristo katika huduma yake alihubiri kuhusu toba aidha aliwaamuru mitume kuhubiri kuhusu toba katika jina lake Luka 24;47, Petro alihubiri kuhusu toba siku ya pentekoste Matendo 2;38, Paulo alihubiri kuwa Mungu ameamuru watu wote watubu Matendo 17;30,20;21 Patro alikazia kuwa Mungu anataka kila mtu atubu kwa ujumla neno toba au kutubu limetajwa mara 36 katika agano jipya,  Toba ni ya muhimu sana katika kutuletea neema ya wokovu Luka 13;3,5.
Kila mtu anaitwa katika wito wa kutubu hii inajumuisha wote wale wasio wakristo, kwa kuwa dhambi ni tatizo la ulimwengu mzima kila mmoja anaitwa katika toba, Wakristo pia wanapaswa kutubu makanisa katika kitabu cha ufunuo yanaitwa kutubu Ufunuo 2;5, 3;19 toba ndio njia pekee ya kumrudia Mungu mara tunapokuwa tumemtenda Mungu dhambi,  Mungu anathamini sana toba ya kweli  hivyo hata wale waliookolewa wanaitwa kutubu pale wanapokuwa wamekosea 1Yohana 1;9 Biblia inasema “Tukiziungama dhambi zetu,Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote
Kwa nini watu wanaitwa kutubu jibu ni kwa sababu tumefanya dhambi swala hili linamjumuisha kila mmoja wote tuna hatia kwa sababu ya dhambi, inawezekana tukawa tumefanya dhambi kwa makusudi au kwa kutokujua zote hizo ni dhambi, dhambi ya kutokukusudia au kutokujua huitwa sin of Omission na dhambi za makusudi huitwa sin of Commission Yakobo 4;17 Yeye ajuaye kutenda mema kisha asitende kwake huyo ni dhambi, 1Yohana 3;4 Dhambi ni uasi, vyovyote iwavyo mwanadamu anawajibika kuwa mwenye dhambi na kwa sababu hiyo kila mmoja anapaswa kutubu kwani iko dhambi lakini tunapotubu Mungu huleta msamaha na rehema.

Toba ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa pamoja na mafundishio hayo muhimu kuhusu hatua za toba zinazotupelekea kupokea wokovu ni vema kukumbuka kuwa wokovu hauwezi kuwa neema kama kuna hatua tu za kufuata ni muhimu kufahamu kuwa hatua hii ya kutubu yenyewe ni zawadi kutoka kwa Mungu  Biblia inaonyesha kuwa toba ni zawadi kamili kutoka kwa Mungu angalia 2Timotheo 2;25 Biblia inasema “ akiwaonywa kwa upole wao washindanao naye ili kama ikiwezekana Mungu awape kutubu na kuijua kweli” kumbe toba tunapewa na Mungu mpaka mwanadamu anatubu bado ni muhimu kufahamu kuwa ni wema wa Mungu unaotuvuta kufikia toba Warumi 2;4 Biblia inasema “Au waudharau wingi wa wema wake na usathimili wake na uvumilivu wake usijue kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Neno la Mungu pia linapohubiriwa pia linauwezo wa kusababisha watu kutubu watu wa ninawi walitubu baada ya mahubiri ya Yona ambao ulikuwa ni ujumbe aliopewa na Mungu Yona 3;8, wapinzani wanaweza kutubu kutokana na mafundisho ya neno la Mungu  2Timotheo 2;25, kazi iliyofanyika msalabani ya Kristio Yesu inapohubiriwa na upendo wake kufunuliwa pia husababisha toba Kristo alikuja kuwaita wenye dhambi kusudi watubu Mathayo 9;132, Marko 2;17 na Luka 5;32 aidha maono kuhusu Mungu pia huweza kusababisha toba Ayubu 42;5,6.

Matokeo ya kutubu.
Toba kwa kawaida inaambatana na Furaha kubwa miongoni mwa malaika huko mbinguni Luka 15;7,10 “kuna furaha mbinguni kwaajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”mtu anapokuwa amekubali kutubu na kumgeukia Kristo ni kama anavuta kengele za furaha za mbinguni na kusababisha shangwe.
Toba na imani ni kama mapacha kwa kawaida huenda pamoja wakati mwingine ni vigumu hata kuchanganua kuwa ni kipi kinatangulia kati ya imani na toba lakini  ni kama vinakwenda pamoja
Toba inaongoza katika kupokea msamaha,tunapoziungama dhambi zetu  na kumgeukia Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo Mungu hutusamehe kabisa 1Yohana 1;9 “Tukiziungama dhambi zetu Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” kwa msingi huo toba, imani na kusamehewa vyote viko katika mnyororo mmoja wa mtu kuokoka, kila moja inajitegemea lakini kila moja ina makusudi ya kusaidiana na nyingine  na hakuna hata moja inaweza kurukwa kwani kila moja ina thamani yake katika swala zima la mtu kuokolewa.

2.      Imani ni Muhimu kwaajili ya kupokea Neema ya wokovu.
Kama tulivyoona kuwa neema ile ya wokovu inapatikana kwa toba ambayo nayo ni zawadi ya Mungu, lakini pia kama ilivyo Nyanja hizi zinategemeana sana toba haiwezi kuwa kamili kama hakuna imani ndani yake Biblia inaweka wazi kabisa kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa msingi huo ni wazi kuwa mwanadamu anaokolewa kwa imani Matendo 16;31 na Yohana 3;16  kwa msingi huo hatuwezi kabisa kuzungumzia wokovu bila kuzungumzia maswala ya kuamini kwani ndivyo Biblia inavyofundisha ona

Matendo 16;31“Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako”
Yohana 3;16-18 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili ahukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye Amwaminiye yeye haukumiwi asiyeamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.

Kwa msingi huo imani ya mtu itamuamulia hatima yake katika kuupokea wokovu na kupata uzima wa milele au kutokuamini na kujikuta katika hukumu, Kumjua Mungu kwenyewe ni swala la imani Mtu amwendeaye Mungu ni lazima aamini kuwa yeye yuko na kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao Waebrania 11;6 ni wazi kuwa  imani ni ya muhimu kwaajili ya kumpendeza Mungu angalia mfano mtu anazungumza habari zako kwa mtu mwingine kisha mtu huyo hataki kuziamini je utapendezwa naye? Mungu amekuwa akijifunua kwa wanadamu kuhusu yeye na njia za kumfikia yeye kama mtu haamini katika njia hizo je anawezaje kumpendeza Mungu?
Imani ni kuamini na kutegemea, kama ilivyokuwa kwa toba imani nayo ina pembe tatu yaani  kujua, kuamini na kutegemea.


  Imani
                                                                                   Ufahamu
 

Kuamini                                                 Kutegemea
Imani ni nini?
Imani ni tendo la kujitoa kwa hiyari kimaneno na kivitendo ambapo mtu anaweka uzito mkubwa wa mahitaji yake na uongozi wa matendo yake kwa kile anachokiamini. Kwa mujibu wa Biblia imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.kwa msingi huo Hatumuoni Mungu, na habari za Kristo tunazisikia tu, na tunaamua kuamini kana kwamba sisi tu mashahidi kuwa Mungu yupo na kuwa ametupa thawabu hii ya zawadi njema ya Kristo Kuja kusulubiwa kufa na kufufuka kwaajili yetu, Kwa hiyo imani hii hujengeka kwa kusikia Neno la Mungu imani hiyo nayo ina sifa zake
Imani sio kuamini kuhusu Kristo bali ni kumuamini Kristo,wala imani sio kuamini sehemu Fulani ya mafundisho ya injili bali kweli yote ya injili, Haianzishwi na matakwa ya mtu bali neno la Mungu,Sio matumaini bali inafanana na matumaini, Bila tumaini maisha ya ukristo ni bure lakini bila imani maisha ya ukristo hayako, Tumaini ni kutazamia uzuri ujao kwa uaminifu, lakini imani inaleta uzuri huo pale tulipo, tumaini linatufanya tuwe na mwanga kuhusu ahadi za Mungu kuwa zitakuja kutimia, lakini imani inazifanya ahadi za Mungu kuwa halisi imani sio hisia au mawazo yanayotembea  ni uamuzi. Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa imani hii katika Kristo haiishii katika kuamini kwaajili ya wokovu bali inatakiwa kukua na kuendelezwa ndani ya maisha ya Ukristo, mtu anaweza kuwa na ujuzi kuhusu ndoa, anaweza kuwa amejifunza mengi kuhusu ndoa na hatimaye akatamani na kuamua kuoa lakini kama hajaishi katika ndoa Bado haijatosha kusema kuwa anaujuzi  wa kutosha kuhusu ndoa. Ndivyo ilivyo na imani baada ya kuokolewa ni lazima tuhakikishe kuwa tunaikulia imani na tunaishi kwa imani.

Kuongoka
Tukio la kuamini linatupelekea kuongoka “Conversion” Kwa asili neno kuongoka kwa kiyunani ni Proselytos  kwa kiingereza tunapata neno proselyte ambalo lilitumika kumaanisha mtu wa mataifa aliyejiunga na dini ya kiyahudi, baadaye pia lilitumiwa na wakristo kumaanisha mtu aliyejiunga na Kristo au mtu anayemfuata Kristo, au mtu aliyebadilika kuwa mtu mwingine kitabia, mfano 1Samuel 10;6, Pia Bwana Yesu alilitumia katika kufundisha maamuzi thabiti ya badiliko,mfano kunyenyekea na kuamini kama mtoto mdogo n.k, lilitumika pia kumaanisha mtu anayerejea au aliyeimarika kiimani, haliko mbali na neno ambalo tumelizoea siku hizi kuokoka, napenda sana kutumia neno kuokoka kuliko kuongoka, Tendo hili la kuongoka hutokea pale sasa mtu anapokuwa amemgeukia Yesu Kristo kutoka katika maisha ya dhambi na kupokea msamaha wa dhambi na hasira ya Mungu na adhabu juu ya dhambi kufutwa kabisa mtu huyu sasa anarejea kutoka katika njia ya dhambi kuelekea katika njia ya haki hivyo kwa ufupi kuongoka ni kurejea Matendo 3;19 Biblia inasema “Tubuni basi, mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana Yesu. Neno kuongoka limetumiwa na Kristo pia katika Mathayo 18;3 ambapo Biblia inasema Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mungu, Luka 22;32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako” Kwa ujumla kuongoka ni kama kukamilika kwa tendo kamili la kutubu, kuamini na kurudi kwa ujumla wake wote kumuelekea Kristo hii maana yeke ni kuwa kama mtu atatubu ataamini kisha haendelei katika njia ya Bwana maana yake tendo la kuongoka halijakamilika ndani yeke mtu aliyeongoka sasa anaishi ndani ya upande wa pili wa imani aliyoipokea kuikiri na badiliko lililotokana na toba yake. Mtu ambaye hajaongoka sasa anafananishwa na mbwa aliyeoshwa kisha kurudi kugaagaa matopeni 2Petro 2;22, Baada ya tukio hili la kuongoka yaani kuendelea katika imani ya bwana Yesu Kristo sasa ndipo kunafuata marupurupu yanayoambatana na wokovu wa mtu huyo.
3.      Mungu anamfanya mtu aliyeokoka kuwa kiumbe kipya. (Kuzaliwa mara ya Pili) Regeneration.

Bila shaka kama ni mwanafunzi wa maandiko utakuwa na Ufahamu wa karibu kuhusu neno Kuzaliwa mara ya pili lililotumiwa na Kristo kwa mwalimu mkubwa sana wa kiyahudi aliyeitwa Nikodemo Yohana 3;1-8 Yesu alimwambia ni lazima uzaliwe mara ya pili hapa ndipo linapokuja fundisho la kuzaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili au kufanywa kiumbe kipya Regeneretion kuzaliwa mara ya pili ni nini?
    Kuzaliwa mara ya pili ni tendo la Mungu kumbadilisha mtu aliyeokoka palepale kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, hii ni hali ya kukarabatiwa kwa nia au nafsi ya mwanadamu ambayo kabla ya wokovu wakati wote nia yake ilisukumwa kutenda dhambi kwa mawazo, maneno na matendo kila alilolikusudia mwanadamu kabla ya wokovu ilikuwa ni uasi mbele za Mungu sasa basi mtu anapoamini na kutubu na kuongoka nafsi yake inazaliwa upya inakuwa iko tayari sasa kutenda mapenzi ya Mungu, Mwalimu wa Kiyahudi kama Nikodemo alipaswa kuwa na Ufahamu kuhusu swala hili kwani wayahudi walikuwa wakipokea watu kutoka katika mataifa waliokuwa wakiongoka kujiunga na dini ya kiyahudi na watu hao walihesabiwa kama watoto wa changa  waliaozaliwa sasa penginepo  Nikodemo alisha ngaa kwa sababu Yesu alilitumia neno kuzaliwa mara ya pili kwake huku yeye ni Myahudi penginepo Nikodemo alifikiri kuwa swala hili linahusu kuzaliwa upya katika tumbo la mwanamke kwa kuingia tena tumboni kwani alifikiri kule kuwa myahudi hakumfanyi yeye kuhitaji kuzaliwa Mara ya pili, Jambo hili linatukumbusha kuwa hata kama u kiongozi wa kidini kama hujachukua hatua madhubuti za kutubu na kuamini na kuongoka si rahisi kuzaliwa mata ya pili, kuzaliwa mara ya pili kunawakilishwa katika lugha kadhaa za kimaandiko kama
Ø  Kuzaliwa na Mungu Yohana 1;13
Ø  Kuzaliwa mara ya pili Yohana 3;3
Ø  Kuzaliwa kwa maji na Roho Yohana 3;5
Ø  Kuzaliwa Mara ya pili Yohana 3;7
Ø  Kuzaliwa kwa Roho Yohana 3;8
Ø  Kuzaliwa kwa upya 1Petro 1;3
Ø  Kuzaliwa tena Petro 3;23
Ø  Kuzaliwa na Yeye  1Yohana 2;29
Ø  Kuzaliwa na Mungu 1Yohana 3;9
Ø  Kuzaliwa na Mungu 1Yohana 4;7
Ø  Kuzaliwa na Mungu 1Yohana 5;1
Ø  Kuzaliwa na Mungu 1Yohana 5;18.
Kuzaliwa mara ya pili ni swala la kimuujiza linalofanyika mara mtu anapokubali kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, ni swala la kimapinduzi na sio uumbaji mpya  mtu wa aina hii anapita kutoka mautini na kuingia katika uzima wa milele Yohana 5;24, na hivyo mytu katika Kristo ni kiumbe kipya 2Wakoritho 5;17 Wagalatia 6;15, hii sio kiumbe kipya kwa maana ya kuwa nje mtu huyu ataendelea kuonekana kama vilevile alivyokuwa isipokuwa ndani nia yake inaumbiwa shauku mpya ya kutaka kuishi maisha yanayompendeza Mungu kwa msaada wake wala si kwa nguvu zake, hivyo haya sio mapinduzi ya kibinadamu bali ni  bali uweza wa kimungu ndani ya mwanadamu.
Neno hili kuzaliwa mara ya pili Regeneration kwa kiyunani ni Paliggenesia ambalo maana yake ni kuzaliwa upya, au kufanywa upya au kurejeza au kukarabati “re-creation” Tito 3;4-5 Biblia inasema “Lakini wema wake mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa  si kwa sababau ya matendo yetu ya haki tuliyoyatenda sisi bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu”

Ni nini umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili?
Umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili ni tukio muhimu kufanyika kwa mwanadamu, ingawa wanadamu wanaweza kuzaliwa wakiwa na maadili tofauti tofauti wengine wanazaliwa wakiwa  na maadili mabovu kabisa wengine katikati na wengine wema kabisa , wengine wasomo na wengine wana uwezo mkubwa na wengine mdogo  lakini pamoja na hayo mwanadamu ameharibika katika ujumla wake  kiroho, kimwili na kiakili yaani Mwili nafsi na roho kwa sababu ya dhambi Warumi 5;12 na kwa sababu hiyo hakuna mwenye hakli hata mmoja Warumi 3;10 kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu Warumi 3;23, hii maana yake ni kuwa sumu ikidondokea kwenye glasi ya maji maji yote yana sumu, au kirusi kikiingia katika damu ya mtu safi mtu huyo ataathirika kila eneo hivyo na mwanadamu alipoanguka dhambini kila eneo la utu wake liliharibiwa roho yake inakufa akili zinaathiriwa na mwili pia kiroho kuna kuwa hakuna mawasiliano na Mungu unapookolewa sasa Mungu ainaifanya roho yako kuwa na mawasiliano naye  unakuwa umefufuka Luka 15;36 ndani yetu kunakuwa hakuna jambo jema Warumi 7;14 tunakuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi Warumi 7;18 na Efeso 2;1-3, unapookoka unafufuliwa , pia unajaliwa kuelewa mambo ya kiroho kwani akili zako zilikuwa hazielewi mambo ya Rohoni 1Koritho 2;14 na miili yetu inakuwa na uponyaji , kwa msingi huo hata kama mtu ana akili kiasi gani kama hajaokoka akili zake haziwezi kupambanua mabo ya kiroho 1Koritho 2;14 na ndio maana Nikodemo alikuwa mwalimu mkubwa sana katika Isarael lakini alishindwa kuelewa jambo dogo kuhusu kuzaliwa mara ya pili kwa kuzaliwa mara ya pili sasa tunapewa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.kuzaliwa mara ya pili ni wazi kuwa hakuji kwa matendo mema, wala hakusababishwi na ubatizo, wala sherehe za kidini  bali kwa kumuamini Mungu  kupitia neno lake , Tangu wakatu huu ndipo mtu anakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu 1Yohana 5;4 “Yeye aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu” pia kunakuwezesha kuishi kwa kutenda haki 1Yohana 2;29b “Kila asiyetenda haki hakuzaliwa na yeye” kwa hiyo tabia za kale zinatawaliwa na tabia mpya utampenda Mungu na ndugu zako katika Mungu !Yohana 5;2,4;20,3;14 hii haimaanishi kuwa mtu huyo hatatenda dhambi kabisa lakini haishi maisha ya dhambi kwa sababu anaye mwombezi atatubia na dhambi itamsumbua nitalizungumzia huko mbele zaidi swala hili 1Yohana 2;1,-2,1;9.
Kilele cha kuzaliwa mara ya pili tuwapo duniani ni kumuelekea Kristo na kuwa kama yeye lakini atakapokuja tutafanana naye na kuwa kama yeye 1Yohana 3;2 kwa hiyo hata kuzaliwa kwetu mara ya pili kutakuwa kamili atakapofunuliwa kwetu Bwana  na wakati huo tutakuwa na utukufu mkubwa Warumi 8;29-30 hivyo kazi ya kuzaliwa mara ya pili ni ya Mungu inaanzishwa nayeye na itakamilishwa na yeye sisi tunatakiwa kuendelea kuitikia neema hii ya Mungu kwa kuyatii yele atakayo

4.      Kuhesabiwa haki.Justification.
Ni moja ya Nyanja muhimu sana za wokovu kuhesabiwa haki kwa kawaida katika kiingereza hutumika neno Justification ni neno linalofanana na lile linaloweza kutamkwa mahakamani na hakimu au jaji mwenye haki  kwa mtu muhalifu kumtangaza kuwa hana hatia ni tendo la kukubalika kuwa huna hatia “you are Innocent” Mwenye hatia anasimama mbele za Mungu mwenye haki ili ahukumiwe na badala ya kuhukumiwa anatamkiwa haki kukubalika  na Mungu jambo hili pia hufanyika kwa imani na hutolewa kama zawadi ya Bure na Mungu  kupitia kumuamini Bwana Yesu, kwa hiyo tunaweza kusema kwa uwazi kuwa  kuhesabiwa haki ni tendo la neema ya Mungu  ambapo Mungu humtangaza mtu huyu mwenye hatia kuwa hana hatia kwa sababu tu mtu huyo ameweka imani yake kwa bwana Yesu hii ni tofauti na kusamehewa dhambi na ni zaidi ya kumtangaza mtu kuwa hana hatia  kwa sababu ukweli unabaki kuwa tuna hatia  lakini ni ile hali ya Mungu kutuchukulia kuwa ni kama hatujawahi kufanya dhambi kwa sababu ya haki ya mwanae Yesu Kristo kuwa haki yake inawekwa juu yetu na anafanyika kuwa haki yetu 1Wakoritho 1;30, tofauti na kuzaliwa mara ya pili ambalo ni tendo linalofanyika ndani yetu baada ya kuamini kuhesabiwa haki ni tendo la muonekano wa nje wakati Mungu anapokuwa ametusamehe. Kuhesabiwa haki kunabadilisha mtazamo wetu na mahusiano yetu na Mungu badala ya Mungu kututazama kama chombo cha hasira zake kwa sababu ya dhambi, sasa tunatazamwa kama chombo kipya chenye kufaa mbele za Mungu  kama ilivyo kwa kuzaliwa upya tendo hili pia hutokea wakati mmoja tunapokuwa tumekubali kumpokea Bwana Yesu na kwa sababu hiyo Yule mshitaki wetu Shetani anakuwa hana uwezo wa kutushitaki kuwa tuna hatia mbele za Mungu Warumi 8;33-34 Biblia inasema “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye awahesabiaye haki, ni nani atakaye wahukumia adhabu? Kristo ndiye aliyekufa, naam na zaidi ya hayo ndiye anayetuombea” kwa hiyo swala la kuhesabiwa haki ndugu yangu kimsingi ni zaidi ya kusamehewa dhambi na hukumu ya hasira au ghadhabu ya Mungu, Mungu anapotuhesabia haki anatuweka katika nafasi ya mtu anayestahili kwa hivyo kama Mungu angekuwa anawahesabia haki watu walio wema na wazuri kwa matendo injili isingelikuwa habari njema kwa watu wenye dhambi hivyo tunasema kuwa mtu aliyeokoka ni “mwenye dhambi aliyeuchinja
Hata hivyo tofauti na swala la kutangazwa kuwa huna hatia kimahakama ambayo kwa kawaida hufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria  kuhesabiwa haki katika Mungu ni tofauti na uhesabiwaji haki wa kimahakama kwanini kwa sababu sheria haiwezi kumuhesabia haki mtu mwenye hatia hata kidogo Sheria haiwezi kumuacha muhalifu hata kidogo ni lazima itamuhukumu kwa hiyo sasa basi kuhesabiwa haki kunakozungumzwa kibiblia ni tendo la neema ya Mungu lililokamilishwa kupitia kazi aliyoifanya Bwana Yesu pale msalabani hivyo haki yetu si haki yetu wenyewe ni haki kupitia kuamini kazi alizofanya Kristo pale Msalabani kwa hiyo basi mtu anapookolewa anakuwa huru anatangazwa kuwa na haki ya kuwa hana hatia na hastahili kuhukumiwa adhabu ni tofauti na msamaha unaoweza kutolewa na gavana anapomsamehe muhalifu muhalifu huyo yu awezxa kuwa huru toka gerezani lakini hawezi kuwa huru kutoka kwenye hatia na ile hatia ndani yake inapiga kelele na kumnyima uhuru kwa sababu ukweli unabaki wazi kuwa mtyu huyu ni mwenye hatia ambaye alifungwa na inagwa amefunguliwa alistahili adhabu na kwa sababu ana kumbukumbu ya swala hilo hivyo anabaki na hatia
Kuhesabiwa haki pia ni zaidi ya kutangazwa kuwa huna hatia “You are Innocent” kwani tangazo kama hilo kwa mtu mwenye hatia kwakweli litabakia kuwa uongo, Mungu anatuhesabu kuwa hatuna hatia kabisa kupitia haki ya mwanae Yesu aliyekubali kuteseka kwa ajili yetu na hivyo Mungu anaridhishwa na Neema yake inatukuzwa na mwenye dhambi anafaidika
Tofauti ya kuhesabiwa haki na sheria.
Sheria kamwe haiwezi kumfanya mwanadamu akahesabiwa haki na kuna sababu kama tatu hivi kwanini haiwezi kufanya hayo kwanza sheria ni dhaifu kwa sababu ya mwili Warumi 8;3 Biblia inasema hivi “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi na kwa sababu ya dhambi aliihukumu dhambi katika mwili” sheria ina nguvu moja tu ya kutuonyesha ugonjwa wetu yaani dhambi lakini haina uwezo wa kuponya au kuiondoa dhambi ni kama kioo ina uwezo wa kutuonyesha kuwa sisi tua uchafu lakini kioo hakiwezi kuondoa uchafu hata kama utakuwa na vioo vingi kiasi gani vioo hivyo haviwezi kuosha au kuondaoa uchafu ulio nao  sheria ni kama kuhani au mlawi aliyempita mtu aliyepigwa na majambazi wakamuacha bila msaada kumbe anahitajika msamaria mwema anayeweza kututibu na kushughulika na tatizo letu.
    Sababu ya pili kwa nini sheria haiwezi kutuhesabia haki ni kuwa sheria haina rehema ni kama msumeno ili mtu aweze kuhesabiwa haki kwa sheria analazimika kuyitimiza yote kwa ukamilifu na mtu anayefikiri kuwa anaweza kuishika yote huyu yuko sawa na mlevi anayejaribu kutembea juu ya kamba iliyofungwa toka ghorofa moja hadi jingine chini kukiwa na maji, kwa asili yetu ya kibinadamu yenye anguko hakuna anayeweza kufanya hayo na unaposoma historia yote ya mwanadamu katika Biblia haionyeshi kuwa kuna mtu aliweza na kwa kuwa sheria ilikuwa ikitangaza Baraka kwa watakaoitii na laana kwa watakaovunja hata moja kwa hiyo wote walioandikiwa kuyatii yote katika kitabu cha torati wasiyafanye wamelaaniwa ndio soma Wagalatia 3;10b Biblia inasema hivi  “…Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa  katika kitabu cha torati asiyafanye”
Sababu ya tatu ni kuwa sheria haiwezi kufuta historia yetu kuwa sisi ni wenye dhambi na haiwezi kuosha asili yetu ya dhambi ambayo kila mtoto wa Adamu anayo kwa msingi huo basi hata kama mtu angeweza kuishika sheria yote kwa ukamilifu bado ndani yake angejikuta ni mwenye dhambi kwa kulke kuzaliwa na mwanadamu mwenye asili ya dhambi Zaburi 51;10 ni damu ya bwana Yesu tu inayoweza kutusafisha na udhalimu wetu. Kwa ujumla sheria haikutolewa ili kumkamilisha awaye yote bali kuihukumu dhambi ili dhambi ionekane kuwa ni dhambi na izidi kuwa mbaya mno soma Warumi 7;13.Sheria yenyewe haina shida ni takatifu  na ni njema  lakini ilikuja ili kuonyesha mwanadamu alivyo na hatia Warumi 7;12 ,Warumi 7;17-20 sasa mwanadamu ategemee nini? Sheria ilikuja kwa mkono wa Musa bali neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Kwa hiyo basi sheria ni maarifa yanayotufundisha kuwa sisi tu wenye dhambi warumi 3;20, na kamwe haiwezi kutupa au kutuletea wokovu lakini inatuongoza kuona kuwa tunamuhitaji mwokozi Wagalatia 3;24 Biblia inasema wazi hivi “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo ili tuhesabiwe haki kwa imani” moja ya faida kubwa ya kuhesabiwa haki ni kuwa  tumeokolewa  mbali na hasira ya mungu Warumi 5;9 hakuna hukumu ya adhabu juu yetu kwa sababu Mungu ndiye anayetuhesabia haki Warumi 8;33, tunaingia katika kundi la waliobarikiwa hatuko chini yalaana Zaburi ya 32;1 yasema hivi “Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake” mtu awaye yote aliyemwamini bwana yesu amebarikiwa hayuko chini ya laana, faida nyingine ni kuwa tuna amani na Mungu warumi 5;1 badala ya kujificha kamna Adamu tunamkaribia  na mwisho tunakuwa warithi na sio watumwa tena bali wana wa Mungu warumi 8;17,Tito 3;7.
5.      Kufanywa kuwa wana wa Mungu Adaption
Yohana 1;12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake” Adaption au kufanywa wana wa Mungu ni tendo  la neema ya Mungu ambalo linatokea kwa wale wanaomuamini Yesu Kristo kufanywa kuwa watoto wa Mungu wenye haki sawa na marupurupu sawa na watoyo wa Mungu, mtu mmoja alisema hivi
Ø  Kuzaliwa mara ya pili ni kubadilishwa kwa asili yetu ya dhambi
Ø  Kuhesabiwa haki  ni kubadilika kwa mtazamo wa  Mungu kutuhusu baada ya kuamini
Ø  Kufanywa wana ni kupoandishwa cheo kutoka kuwa watumwa kuwa watoto na warithi
Kwa msingi huo tunapokuwa tumefanyika watoto wa Mungu Mungu hatuchukulii sisi kama watumwa au watoto walio chini ya mwanagalizi bali kama warithi na wana kamili wa Mungu wagalatia 4;1-5, wajibu wetu ni kuamini tu  na kwa njia hiyo tunazaliwa si kwa mapenzi ya mwili bali kwa MunguYohana 1;12-13, Anapokuwa amemtuma Roho wake  wa uana tunamlilia baba Warumi 8;15Wagalatia 4;6 kilio cha kuita baba kamwe hakiwezi kutamkwa na mtumwa  sasa kila aliyeokolewa ni mwana wa familia ya kifalme ya Mbinguni, umeondolewa kutoka utumwani wewe sio mtumwa wa sheria kwa sababu sasa tunapendezwa kufanya mapenzi ya Baba, hatuko tena chini ya utumwa wa hofu ya dhambi Mungu anazifutilia mbali kupitia damu ya Yesu 1Yohana 4;18 Biblia inasema hivi  “Katika Pendo hamna hofu lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hukamilishwa katika pendo, kufanywa wana kunatuweka katika ushirika usio wa kawaida na Mungu kwani watu wote n I viumbe wa Mungu lakini si kila mtu ni Mwana wa Mungu ni wale waliompokea Kristo tu wanaweza kuwa na uhusiano wa pekee  na wa kweli na Mungu na mwanae wa Pekee Kristo 1Yohana 1;3
6.      Kutakaswa “Santification”
Neno Utakaso limetokana na neno la asili la kiebrania ambalo kwa kiyunani linatumika neno “Hagiazo”ambalo lina uhusiano mkubwa na maswala ya utakaso ya agano la kale  hususani katika sherehe za kidini za kumfanya mtu  awe na uwezo wa kuukaribia uwepo wa Mungu au awe na hali zinazo mlazimu kuweze kumfikia au kumkaribia Mungu kwa hiyo utakaso kwa kiebrania maana yake ni kufanywa kuwa mtakatifu au kuhesabiwa haki mbele za macho ya Mungu na kwa hiyo kuweza kukubalika na kumuabudu kwa hiyo kwa kiibrania kutakaswa ni sawa na kuhesabiwa haki unaweza kuhisi mitazamo hii kwa kuangalia mistari ifuatayo Waebrania 9;13-14 Biblia inasema hivi “Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe walionyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili basi si zaidi sana Damu yake Kristo ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha  dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumuabudu    Mungu aliye hai?” ndugu yangu msomaji utakaso huu pia ni neema ya Mungu
      Utakaso ni kazi ya neema ya Mungu ambapo muumini  anatengwa  yeye mwenyewe na hali ya dhambi iliyoko ndani yake na kwa kujazwa Roho Mtakatifu anatengwa kuwa mtakatifu kwaajili ya utumishi, utakaso maana yake kwa ufupi ni kufanywa kuwa mtakatifu katika kulihakikisha hilo linafanyika Roho Mtakatifu ni nyenzo muhimu na kupitia kazi ya Kristo aliyoifanya ndani yetu 1Koritho 1;30.
     Utakaso ni hali ya kukua na kukomaa kuelekea kuwa na tabia za Kristo, ni mabadiliko ya kitabia na maisha  na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu kuelekea kuwa na tabia za kiungu Tito 3;5 maana yake ni kuwa mtu anapokuwa ameokoka hawezi kuendelea kuishi maisha ya ndhambi 1Yohana 3;9 kwa sababu nguvu ya maisha mapya ya kiroho inakuweka mbali katika kuishi maisha ya ufanyaji dhambi hali hiyo ya kubadilishwa katika hatua ya mwanzoni  huitw2a kutakaswa kwa hiyo mtu anapokuwa ameokoka anakuwa ameoshwa ametakaswa 1Koritho 6;11 na Pia Matendo 20;32 Paulo anajumuisha wakristo wote kuwa watu waliotakaswa
     Kazi ya utakaso ni kufunja nguvu ya dhambi kututawala Warumi 6 ; 14 Biblia inasema hivi “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi kwa sababu hamuwi chini ya sheria bali chini ya neema” tunapokuwa tumetakaswa tunakuwa huru kutoka dhambini na kuwa watumwa wa haki
Kwa muhktasari tunaweza kusema kuwa utakaso ni -;-
a.      Kutengwa
Kuwa mtakatifu kwa asili ni neno la kiungu ambalo kwa asili ni kutengwa kwa hiyo kimsingi utakaso unawakilisha ile hali ya Mungu kuwa na kila hali ya kidunia na kibinadamu na hivyo kuwa na hivyo kuwa mkamilifu kimaadili na kwa utukufu wake Mungu na anapotaka kukitumia kitu au mtu huyu aliye mtakatifu hukitenga au humtenga mtu huyo kutoka katika matumizi ya kawaida na kutumika kwa makusudi yake tendo hilo pekee hukifanya kitu au mtu kuwa mtakatifu.
b.      Kuwekwa wakfu
Utakaso hujumuisha pia swala la kutengwa lakini pia swala la kuwekwa wakfu, au kujiweka wakfu hii ni hali ya kukubali neema ya Mungu kwa muitikio wa kukubali kujitenga na dhambi na maswala ya anasa za kidunia  na kukubali kushiriki tabia za uungu na asili ya uungu na kujitoa au kujiingiza katika ushirika  na Mungu kupitia neema katika Kristo, kuwa mtakatifu ni neno linalotumika pia katika mswala ya ibada na alinapotumika kwa mtu  humaanisha pia kutumika kwaajili ya huduma za kiungu, kwa mfano Israel liliitwa Taifa Takatifu kwa sababu waliwekwa wakfu kwa kusudi la kimungu pia makuhani Walawi waliitwa watakatifu kwa sababu ya kuwekwa wakfu ili wamtumikie Mungu na hata si ku au sikukuu zilizowekwa kwa ajili ya Mungu ziliitwa siku takatifu
c.       Kusafishwa
Utakaso pamoja na kujumuisha kutenga au kuweka wakfu pia Mungu Yehova anapokuwa amemtenga mtu au kitu kwaajili ya makusudi yake hukisafisha vyombo vilivyotumika kwa kazi vilitakaswa kwa kunyunyiziwa mafuta Kutoka 40;9-11, Israel walisafishwa kwa damu ya agano Kutoka 24;8 Waebrania 10;29 Makuhani walitakaswa kuwa mawakili wa Yehova kwa kuoshwa kwa maji na kupakwa mafuta na kunyunyiziwa  damu na hivyo kuwa wakfu Walawi sura ya 8 watu waliookolewa leo tunatakaswa kwa damu ya Yesu Waebrania 13;12
d.      Kuishi maisha ya utakatifu na haki
Kusihi kwa haki maana yake ni kubadilishwa kwa neema ya Mungu na kuishi sawa na maagizo ya kiungu na kuishi kwa utakatifu ni kubadilishwa kwa neema kutoka katika asili yetu na kupokea asili ya uungu Mungu alipokuwa amewateua Israel kuwa taifa lake alielekeza pia ni namna gani wataishi na hivyo Israel walijitoa kuishi maisha sawa na maagizo ya Mungu na hivyo kila anayeokolewa sasa anapaswa kujitoa mwenyewe kuishi sawa na maagizo ya Mungu
e.       Huduma
Agano ni hali ya uhusiano ulioko kati ya Mungu na mwanadamu, mtu napoingia katika huduma maana yake ni kuwa ameingia katika uhusiano wa Mungu na watu wake mtu anayeingia katika huduma anaingia katika agano na kumtumikia Mungu kunamaanisha kuwa umeingia katika huduma ya kikuhani na uchafu wowote ule unaweza kuharibu uhusiano huo na hivyo ni lazima maji au damu itumike kusafisha na kurejesha uhusiano kwa msingi huo kila mtu aliyeokoka ni Mtakatifu, kupitia damu na maji aliyoyatoa Kristo Yesu pale msalabani kwa msingi huo tunafanyika kuwa taifa takatifu kama ilivyokuwa kwa taifa takatifu la Israel Kutoka 19;6,1Petro 2;9,5 kwa msingi huo kumtumikia Mungu kuna uhusiano wa Karibu sana na utakaso na utakatifu na hivyo Mungu anatumiliki na sisi tunakuwa wake Matendo 27;23.
Utakaso unatokea wakati gani?
Ni muhimu kufahamu kuwa utakaso umegawanyika katika maeneo makuu mawili
1.      Mtazamo wa Mungu kwetu na unatokea mara moja tunapokuwa tumeokolewa kwa kuamini
2.      Kwa kuishi na kuendelea kukubaliana na neema na mpango wa Mungu katika maisha yetu mpaka kufa
     Utakaso kama mtazamo wa Mungu na unaotokea mara moja tunapokuwa tumeokolewa kwa kuamini,(Position & Instantaneous) ni kusafishwa kwa asili ya dhambi kwa damu ya Yesu kupitia imani katika Yeye ni kazi ya neema ya Mungu kutuhesabia kuwa tumekwisha kuwa safi mara baada ya kuamini kazi aliyoifanya Kristo Msalabani kwaajili yetu hivyo katika macho ya Mungu tayari unakuwa mtakatifu na saa ileile unapoamini tayari unakuwa mtakatifu kwa hiyo waamini wote ni watakatifu 1Wakoritho 1;2,6;11 “Kwa kanisa la Mungu lilioko Koritho wale waliotakaswa katika Kristo Yesu walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.” “Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.” Pamoja na kuwa Paulo Mtume hapa anawaita wakoritho watakatifu jambo la kushangaza katika waraka huo huo aliwaandikia kurekebisha matatizo kadhaa ya wakristo ya kimwili na dhambi zilizo wazi angalia 1Koritho 3;1, 5;1,2,7,8 walikuwa watakatifu waliooshwa kwa damu ya Yesu  lakini baadhi yao walikuwa mbali na maisha ya kila siku waliyotakiwa kuyaishi kwaajili ya Mungu angalia msomaji wangu walikuwa wameitwa kuwa watakatifu lakini baadhi yao walikuwa hawaenendi sawa na huo utakatifu walioitiwa kwa ujumla utakaso una tofauti ndogo sana na kuhesabiwa haki katika mtazamo mzima wa agano jipya
     Utakaso katika mtazamo wa kuishi na kuendelea kukubaliana na neema na mpango wa Mungu katika maisha yetu mpaka kufa (Practical &Progressive) Utakaso sio tu swala la mtazamo wa Mungu kwetu kutuhusu mara baada ya kuokolewa  lakini ni pamoja na kuendelea kuishi maisha ya utakatifu au kuendelea kutakaswa mpaka kufa  baada ya kuwa umemfuata Kristo kwa kumuamini ni lazima uendelee kumfuata kila siku na kuendelea kumuamini na kukubali kutengwa kwaajili ya kusudi lake na kuendelea kumfanania yeye Yesu Kristo katika maisha yetu ya kila siku, kwa hiyo utakaso ni kazi ya Mungu inayotolea kwa neema bure ambapo tunabadilishwa maisha yetu kuwa na mwelekeo wa kuwa kama Mungu na tunaendelea kuwezeshwa tena na tena  mpaka kufa  kwa hiyo hii haimaanishi tunaukulia utakaso la tuna endelea katika utakaso kwa hiyo tunakuwa nao kabisa na huku tunaendelea kutakaswa Waebrania 10;14 kuendelea kwetu kunategemeana na kukubali kwetu kuendelea kukua katika Kristo Waebrania 12;14 na ni lazima tujishughulishe kwa kujitakasa sisi wenyewe kwa kuweka mbali uchafu wote wa mwili na Roho 2Wakoritho 7;1.
Kwa ujumla sasa tumeona upana na urefu wa wokovu msomaji wangu mpenzi bila shaka mpaka hapa utakuwa umeona wazi kuwa wokovu sio kazi ya mwanadamu ni kazi ya mungu na kuwa katika kila marupurupu yanayohusiana na wokovu mwanadamu anasehemu ndogo sana yaani kukubali neema ya Mungu kufanya kazi ndani yake lakini mimi nasema hata huko kukubali kwenyewe ni zawadi ya Mungu wala si kwa kadiri ya kutaka kwetu.Hata hivyo kabla sijamalizia katika eneo hili ni muhimu sasa nikukuelezea njia kuu za utakaso ili mwanadamu aweze kutakaswa kuna njia kuu tatu ambazo zinahusika na utakaso

1.      Kazi ya Yesu Kristo Msalabani.
Kazi aliyoifanya Bwana Yesu pale msalabani ni kazi kubwa sana ya ukombozi ambayo waaminio wanatakaswa kupitia kazi yake kuu ya umwagaji Damu kwa hiyo Damu ya Yesu inatakasa na kuondoa dhambi na uchafu wote kumbuka kuwa wakati wa agano la kale ili mtu aweze kusamehewa dhambi alitoa dhabihu ya wanyama kama Mbuzi na ndama wa ng’ombe walionona na wanyama hao walimwaga damu kwa niaba ya watu waliotoa dhabihu hizo, lakini ilipaswa kuwa jambo lenye kujirudiarudia,Kristo alijitoa mara moja tu kwa kusudi la sisi kusamehewa dhambi mwandishi wa kitabu  cha waebrania anaweka wazi swala hili Waebrania  9;11-14 Biblia inasema hivi;-

 “Lakini Kristo akiisha kuja aliye kuhani mkuu wa mambo mema  yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa  na kamilifu zaidi isiyofanyika kwa mikono , maana yake isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama  bali kwa damu yake mwenyewe  aliingia mara moja tu katika patakatifu akiisha kupata ukombozi wa milele, kwa maana ikiwa damu ya Mbuzi na mafahali  na majivu ya ndama ya ng’ombe walionyunyiziwa wenye uchafu  hutakasa hata  kuusafisha mwili  basi si zaidi swana damu yake  Kristo ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha  dhamiri zenu na matendo  mafu mpate kumuabudu Mungu aliye hai.”

Unaona ndugu yangu kuwa katika damu ya Bwana Yesu kuna ukombozi wa milele, Kazi kubwa aliyoifanya Kristo msalabani inatuhakikishia ukombozi milele hii haina maana kuwa mtu aliyeokolewa hawezi kufanya dhambi anaweza kwani kwaasili sio mkamilifu lakini anaporudi kwa Kristo ambaye ndie kuhani mkuu yaani mpatanishi na mwombezi na kuamini katika kazi iliyofanyika msalabani mtu huyo husamehewa Neno la Mungu lasema hivi katika !Yohana 2;2  andiko ambalo halipendwi sana  na wahubiri wenye misimamo mikali ya kichanga  andiko hili lasema “Watoto wangu wadogo nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba Yesu Kristo mwenye haki naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu, wala si kwa dhambi zetu tu bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” ni muhimu kufahamu kuwa ukombozi huu wa milele kupitia Damu ya bwana Yesu ni kuwa kila wakati mtu anaweza kukaribia kiti cha rehema cha Mungu kwa ujasiri na kupokea msamaha wa dhambi, Kristo ni Yeye Yule jana Leo na hata milele Kwa msingi huo Msamaha wake unapatikana kila sekunde na kila dakika na kila saaa na kila siku hii ni neema ya milele Maandiko mengine ambayo unaweza kujisomea kuhusu kazi ya damu ya Yesu ni pamoja na Waebrania 13;12,10;10, 10;14 na 1Yohana 1;7

2.      Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ndiye mwanzilishi wa kazi ya Mungu katika mioyo ya wanadamu  ndiye anayewaongoza  katika maarifa kamili yanayopelekea kupokea wokovu na kuhesabiwa haki kwa msingi huo ni moja ya njia zinazotumika kutuletea utakaso 1Wakoritho 6;11,2Wathesalonike 2;13 1Petro 1;1-2 na warumi 15;16

3.      Neno la Mungu.
Neno la Mungu linahusika katika kazi nzima ya utakaso wa mwanadamu kama Kristo alivyosema yeye mwenyewe Yohana 17;17 Uwatakase kwa ile kweli Neno lako ndio kweli , tunaona pia katika Waefeso 5;26, Yohana 15;3,Zaburi 119;9 Yakobo 1;23-25 Kwa ujumla wakristo wanaitwa watu waliozaliwa kwa neno la Mungu 1Petro 1;23,Neno la Mungu hufanya kazi ya kutuamsha na kutukumbusha na kutuonyesha makosa yetu na tunapotambua uzoefu wetu na kuliitikia katika kile kinachosemwa  na kutubu  tunaoshwa kwa neno hilo na kuanzia tulipoliamini na kuokolewa na tunapoendelea kulitiii linaendelea kufanya kazi ya kutusafisha na kututakasa Yakobo 1;22-25

Mawazo yasiyo sahii kuhusu utakaso na Wokovu.
Watu wengi waliookolewa watakuwa wanafahamu kuwa kizuizi kukubwa cha watu kuishi maisha ya utakatifu ni mwili na ndio unaokuwa kizuizi kukibwa katika maendeleo yao ya kuelekea kwenye ukamilifu je mtu anawezaje kuushinda mwili? Hapa ziko dhana kama tatu hivi ambazo sio sahii kuhusu namna tunavyoweza kutakaswa
1.      Imani iitwayo Eradification au “inbred” hiii ni imani ya kuwa dhambi inarithiwa kutoka kwa wazazi, imani hii iliandikwa na Lewis Sperry Chaefer ambaye anafikiri kuwa kama asili ya dhambi ingekomeshwa kamwe kusingekuweko kifo kwa sababu kifo ni matokea  asili ya dhambi wanatumia Warumi 5;12-21. Kwa hiyo wanaamini kuwa kwa kuwa wazazi wetu waliishi katika dhambi ni lazima tutaendelea kuzaliwa wenye dhambi, Je hali ya mwili kutupinga ikikomeshwa je kutakuwa na ukombozi kwa aina binadamu kuwawezesha kuishi maisha matakatifu? Jibu ni sio kweli kwani Bado mwanadamu angepambana na dunia  na hali kadhalika ukiiacha asili ya dhambi yuko shetani ambaye angeendelea kufanya kazi zake kutupinga
2.      imani iitwayo legalism hii ni jamii ya watu wanao amini katika kushika sheria Fulani na kuishi kwa sheria kali kunaweza kumsaoidia mtu kuwa mkamilifu Paulo anaeleza wazi kuwa sheria haiwezi kamwe kumtakasa mtu warumi 6 ukweli unawekwa wazi katika sura ya 3 ya Wagalatia kwa ujumla mtu anayetaka kutakasika kwa kujikana na kujiminya katika sheria kamwe hawezi kuwa mtakatifu hali ya wokovu wa mwanadamu inategemea nguvu kutoka nje yake na sio ndani yake mwenyewe wewe huwezi kujitakasa ni sawa na mfano wa kipima joto cha daktari ambacho kinaaaua kuwa leo nitapanda hadi kufikia nyuzi joto 80 Bila hali joto ya nje kipima joto kitabaki vilele ndivyo ilivyo kwa mtyu anayetaka kujiokoa mwenyewe utakaso na wokovu ni msaada kutoka kwa Mungu mwenyewe na sio kwa mwanadamu kwa kukazana kujipendelkeza kwa Mungu kwa Kushika Sheria
3.      imani iitwayo Asceticism hii  ni jamii ya watu walioamini au wanaoamini kuwa mwili ni muovu hivyo unapaswa kuutumikisha na kuutesa  ili uweze kuwa mtakatifu njia hizi hushikwa sana na Wakatoliki na wahindu na watawa wa kibudha, Imani hii ilijengeka tangu zamani sana  kutokana na watu waliaamini kuwa kila kitu ni kiovu ukiwamo mwili na mwili unaipinga sana roho hivyo ili roho iweze kuwa na nguvu unautesa sana mwili ili roho iweze kuwa takatifu, hii ni kinyume na maandiko Mungu alifanya kila kitu kuwa chema  ni Nafsi ya mwanadamu ndio yenye shida na sio kila kitu kuwa ni kiovu kwa hiyo wanaojaribu kujitesa ili kumpandeza Mungu maaana yake wanajaribu kuzitesa nafsi zao wanajaribu kujiokoa kupitia nafsi zao na nafsi haiwezi kuokoa nafsi wokovu na utakaso ni kazi ya Roho wa Mungu.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
0718990796

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni