Yesu Kristo alifundisha katika
mafundisho yake umuhimu wa kujihadhari na Manabii wa uongo Mathayo 7;15 kwa
kukosa kuwa na ufahamu katika neno la Mungu tunaweza kujikuta tunachukuliwa na
uongo wa shetani kwa kuikimbia kweli na kwenda mbali kabisa na neno la Mungu
hata hivyo namna ya kuwatambua manabii wa uongo ni jambo linaloweza kukuchanganya
kama hutakuwa na ufahamu kuhusu Neno la Mungu ni kwa msingi huo sasa leo
tutachukua Muda kujifunza neno la Mungu
linasema nini uhusu manabii wa uongo ili tupate kujihadahri sawasawa na neno la
Mungu.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo;-
Muhubiri huyu hapaswi kugusa chini wakati wa mahubiri hushinda juu ya migongo ya washirika
§ Maana
ya neno Nabii
§ Jinsi
ya kuwatambua manabii wa uongo.
Maana ya neno Nabii.
Neno nabii lmejitokeza zaidi ya
mara mia 300 katika agano la kale na mara 100 katika agano jipya katika agano
la kale neno hili lilitumika kama Navi au Nabi ambalo maana yake mtu mwenye
uwezo wa kupokea neno la Mungu na kulifikisha kwa watu, walifanya kazi ya
kuzungumza mambo ya Mungu kwa wakati ulioko, uliopita na ujao, kwa ufupi leo
tunaweza kusema kuwa manabii ni wanenaji kwa niaba ya Mungu au watumishi wa Mungu wanaohubiri yale yaliyo
haki na yale ambayo sio haki mbele za Mungu hao ndio manabii wa kweli Waefeso
4;11 nabii wa kweli kwa kawaida anakuwa na sifa kuu mbili A. atafundisha maneno
ya kweli ya Mungu bila kuchuja kwa namna yoyote ile bila kujali cheo au sifa ya
mtu na atafundisha njia ya Mungu kwa Usahii bila upendeleo Yohana 3;34, Mathayo
22;16, Wagalatia 2;4-6.B. Maisha yake yataonyesha matunda ya Kristo na ya Roho
Mtakatifu maana Mungu anayemwakilisha ni Mtakatifu kwa hivyo maisha yake yataendana
na yale anayoyafundisha kila siku
Matendo 1;1 Warumi 2;21-25 Wagalatia 5;22-25 pale tunapoona sifa izi kuu na
nyinginezo sawasawa na neno la Mungu
ndipo tunapoweza kujua kuwa huyu ni nabii wa kweli tuliyoipokea.
Jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo.
Maandiko yanatupa mwanga wa
kutosha kuweza kuwatambua manabii wa uongo kama anavyo tufundisha Bwana wetu
Yesu Kristo. Katika Mathayo 7;15-20 anasema tutawatambua kwa MATUNDA yao matunda
ya manabii wa uongo kwa mujibu wa maandiko nikama ifuatavyo;-
a. Manabii
wa uongo hufundisha UONGO na katika maandiko wanaitwa mikia, Kufundisha uongo
ni kufundisha yale ambayo hayako kwenye Biblia au yale ambayo Biblia haikumaanisha
badala yeke watafundisha hadithi zilizotungwa na wanadamu na katiba zao hata
kama ziko kinyume na neno la Mungu linatuonya kuwa mbali nao katika jina
la Yesu, tujihadhari kabisa Isaya 9;15-16, 2Petro 2;1-4.
b. Manabii
wa uongo hukiri kwa vinywa vyao kuwa wanamjua Mungu lakini kwa Matendo yao
wanamkana ni wenye machukizo na uovu
wote Tito 1;16 watakuwa ni watu ambao wanashika Biblia au vitabu vya kidini na
kwenda huko na huko kuhubiri dini lakini ukiangalia maisha yao ni ya uasherati,
Uzinzi, usengenyaji, uongo, ushirikina, fitina, faraka na uadui haya ni baadhi ya matunda ya mwili Wagalatia 5;22
c. Manabii
wa uongo kamwe hawakiri kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ila wanasema ni mwanadamu tu
sawa na wengine 1Yohana 4;1-4
d. Manabii
wa uongo hukataa neema ya wokovu iliyokuja kwa mkono wa Yesu Kristo na
hufundisha na kuwaambia watu kuwa watafika mbinguni kwa matendo Fulani ya
sheria, Nyakati za leo hatuko chini ya sheria ya Musa ili tuko chini ya
sheria ya kifalme ya Yesu Kristo ambayo tunawezeshwa na Yesu mwenyewe Tito
2;11-12 Wagalatia 5;4 2;16 Yohana 1;16-17, 2Petro 2;1-2.
e. Manabii
wa uongo huwaambia watu amani tu hata kama yale waliyoyafanya yako kinyume na neno
la Mungu, manabii hao kusudi lao au mungu wao hasa ni tumbo Yeremia 23;16-17
Warumi 16;17-18 wafilipi 3;18-19. Fedha ndio lengo lau kuu wanatajirika kupitia washirika masikini ambao labda wangehitaji msaada kutoka kwao.
f.
Manabii wa uongo watasifiwa na watu wote na
kutakuwa hakuna upinzani wowote wa kunenwa vibaya au vinginevyo. Nabii wa kweli
kunakuwa na mchanganyo wa utukufu na aibu na kunenwa mabaya Luka 6;20-26 angalia sifa za nabii wa kweli
2Wakoritho 6;4-10,Yohana 7;20,8:48.
g. Manabii
wa uongo hawaongozi na neno la Mungu ila wanaongozwa na mapokeo ya kibinadamu tu
ndoto na maono ya uongo Wakolosai 2; 18-19, Marko 7;6-7,13. n.k.
Ni muhimu basi
kujihadhari na kutokuwakubali walete upuuzi wao au kuanza kubishana nao
2Timotheo 2; 14, 23-24, waefeso 5;4 Mungu atupe neema ya kutokukubali kupotea. Lazima watumishi wenye kudai kuwa wanaihubiri kweli waishi sawa na injili, tunafahamu kuwa yako matatizo ya kibinadamu na udhaifu wa kibinadamu lakini manabii wa uongo kwa makusudi kabisa lengo lao ni kujitajirisha wao wenyewe wengine kuwaona ni gharama kubwa sana kuliko kumuona Yesu, washirika wanateseka mpaka wakiponyoka katika kanisa lao wanajisikia Huru Mungu awasaidie watu wake walioteswa na kundi kubwa la manabii wenye kujikinai na kutabiri uongo
hakika blog hii imenisaidia
JibuFutaubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu
ushauri wangu: kama upo uwezekano wa kutengeneza APP,naomba unda....tutabarikiwa zaidi!