Jumatatu, 7 Machi 2016

Mambo Muhimu ya kuyafahamu Katika uislamu



Ni muhimu kufahamu tafasiri na maana ya mambo kadhaa katika Uislamu ili kuweza kuyatambua kwa kina maana zake kama anavyochanganua Mchungaji Innocent kamote tafadhali fuatana nani.

·   Maana ya Uislamu na Muislam (Islam) & (Muslim).
     Neno uislam (Islam) ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo maana yake ni kutii “Submission” na muislamu maana yake aliyejisalimisha kwa allah na Muhamad “one who submits” au mtu aliyesilimu yako madai pia kuwa neno Islamu maana yake ni amani hatahivyo maana hii hutumika kama njia ya kuficha uhalisia wa uislam ambao hauna amani kama tutakavyoona huko mbele je uislam ni amani na je waislamu ni watu wa amani au la.

·   Maana ya neno Quran (Koran).
     Ni neno la kiarabu cha kikureshi ambalo maana yake ni “Recitation”maana yake “yaliyokaririwa” Hivyo quran ni mjumuisho wa makusanyo ya aya “wahy”au mafunuo aliyoyatoa Allah kwa Muhamad kupitia malaika jibril au kwa ndoto nk. Muhamad alipozitoa aya hizo watu waliokuwa karibu walizikariri na baadae alipofariki zilikusanywa na kuwa kitabu ambacho waislamu huamini kuwa ni kitabu kitakatifu.

·   Maana ya neno Imam.
     Ni jina linalotumika kwa kiongozi wa dini ya kiislamu, ambaye ana ujuzi wa quran, waislamu wasio na ujuzi wa quran huitwa “maa mumah” na mwalimu wa ngazi ya juu zaidi wa kiroho kwa washiha huitwa “ayatollah” yaani aliye karibu na allah, pia wale waliomrithi Muhamad baada yake huitwa khalifa au maswahaba neno ambalo ni sawa na neno naibu

·   Maana ya jina Muhamad.
     Hili ndilo jina la nabii wa waislamu, alikuwa ni mwarabu wa jamii ya Makuresh(Quirsh-yaani papa) alizaliwa katika mji wa Mecca mwaka wa 570 B.K. Baada ya Kristo, alikufa mwaka wa 632 katika mji wa Madina, hivyo aliishi miaka 62,  Jina hili Muhamad maana yake ni “praised” yaani aliyetukuzwa wenyewe hutumia neno la kiyunani “Periclutos”,habari zaidi kuhusu muhamad tutazizungumzia katika somo maisha ya Muhamad huko mbele na nakuhakikishia kuwa sitambakishia kitu katika maisha yake tangu kuzaliwa hata kifo, tutaelezea maisha yake wazi kabisa sawa na Quran yenyewe.

·   Maana ya jina “allah”.
     Hili ndilo jina la mungu wa Muhamad na waislamu wenyewe wanadai kuwa jina hili haliwezi kuelezeka kwa neno god la kiingereza, ni jina la pekee na la mola linalobeba ukamilifu wote na uzuri, wao hulinganisha jina hili na jina YHWHYHWH”   la Kiebrania yaani Yehova, Ingawaje sifa za Mungu hawa hazifanani kabisa kama tutakavyoona huko mbeleni,allah hana mshirika,ni mkali sana si wakike wala wa kiume ana kigeugeu na hafai kutegemewa ni muongo na mwenye hila hana nguvu au uwezo wa kufufua wakati kwetu sisi wakristo Mungu kwetu ni kimbilio na nguvu msaada uonekanao tele wakati wa mateso.

·   Mambo mengine ya kufahamu katika Uislamu ni pamoja na;-
§  Sunnah-Ni maisha na tabia za matendo yoote ya Muhamad, unapoigiza lolote ambalo Muhamad amelifanya ni sunnah yaani unafuata njia au kielelezo cha maisha ya nabii muhamad mjumbe wa mwenyezi Mungu
§  Quibla-Kibla ni muelekeo wa maombi, unapoomba unapaswa kuelekea katika msikiti mkuu wa Mecca  huko ndio kibla ya waislamu.Yaani muelekeo wakati wa sala
§  Hafiz-Mtu aliyekariri quran kwa moyo anaweza kuisema bila kusoma.
§  Sheikh-Kiongozi wa kiroho wa kiislamu.
§  Halaal-Mambo yoote safi yaliyoruhusiwa katika uislamu.
§  Haraam-Mambo yoote yasiyo safi yaliyokatazwa katika uislamu(yaliyo harimishwa)
§  Mishkat-Hadhithi au kitabu cha baadhi ya hadith zilizochaguliwa
§  Mansukh-Aya ambazo baadaye zilibatilishwa.
§  Nasikh-Aya ambazo zilishuka kuchukua nafasi ya aya zile zilizo harimishwa.
Mwishoni pia nitatoa tafasiri za maneno yoote ya kiarabu kama hayo tutakayoyatumia na hata yale ambayo hatutayatumia yatusaidie baadae tusomapo quran.

·   Ufahamu kuhusu jamii ya waarabu (Arabs).
    Waarabu tulionao leo kwa asili wanatokana na uzao wa Shemu maarufu kama Semites yaani jamii yenye asili ya shemu huyu alikuwa mojawapo ya watoto watatu wa Nuhu, Shemu alikuwa na  wajukuu  moja ya wajukuu hao ni Eber baba wa waeber (waebrania) ukoo ambao Ibrahimu alitokea,Eber alizaa watoto wawili,Pelegi-ambako ndiko Ibrahimu alitokea na Yoktani ambae ndiye baba wa waarabu wengi,ingawa waarabu wengi hudai kuwa wao ni wa uzao wa Ishimael si kweli, uarabu wa Ishimael ulitokana na mama yake Hajir aliyetokea Misri Hivyo waarabu walikuwepo hata kabla ya Ibrahimu mwebrania (Mwanzo 10:21-23-29,11;10-26) jina hili arabs limetokana na asili ya maneno mawili yaani “Nomads” na “ Bedouns”




Pichani jamii ya waarabu nomads na beduians wakiwa na kondoo zao nyikani Picha  na maelezo ni kwa Hisani ya maktaba ya mwandishi  wa Somo Mwalim Innocent Mkombozi Kamote Mwandishi wa somo.

 Au mabedui hii ni jamii ya watu waishio jangwani na wanaoongea kiarabu wako kwa wingi mashariki ya kati Arabia shamu na sehemu za kaskazini mwa Afrika ni jamii ya watu wenye pua kubwa, na walikuwa jamii ya watu wasiomjua Mungu na wapinzani wa Mungu wa waebrania kwa karne nyingi hata kabla ya Kristo soma (Nehemia 2:19) Ishimael alikuwa mwebrania na alimuabudu Mungu wa baba yake na baadae aliishi maisha yanayofanana na mabedui wa jangwani kwani ndiko alikokimbilia na kuishi Mwanzo 25;17 Maneno Ismael akakusanyika kwa watu wake ni wazi kuwa alimwanimi Mungu wa Baba Yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni