Ijumaa, 4 Machi 2016

Mbele ya Baba Mkwe Mtarajiwa akadaiwa Laki ya Bangi!



Maswahibu haya yalimkuta rafiki yangu mmoja kwa bahati mbaya kwa sasa jamaa ni marehemu na alifariki mwaka juzi ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu alipopatwa na fedheha ile, siandiki kisa hiki ili kwamba labda nataka kumuadhiri, hapana naandika kisa hiki kwa sababu tulijifunza jambo moja kubwa sana baada ya kufedheheka kule,

 Mmea Jamii ya Bangi ni mmea wenye utata Duniani

Ilikuwa ni mwaka 2001, nilikuwa wakati huo ndio kwanza nimeanza kibarua kwenye kampuni moja ya kuuza mafuta na nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa anafanya kazi katika kituo cha kuuza mafuta pia, lakini huyu rafiki yangu alikuwa ameanza kazi zamani kidogo ni miaka mine kabla yangu. Mwaka 2000 jamaa yangu alifikiria swala la kuoa na kuamua kutafuta mchumba, huyu mchumba alikuwa ni wa kutoka katika familia ya dini sana, wazazi wake walikuwa ni waislamu wale wanaoitwa waswalihina, ingawa nilikuwa najua kuwa rafiki yangu huyu alikuwa hana kitu, uchumba uliiva ilipofika januari 2001,Tulifanya mipango na taratibu ili ndoa ifungwe kabla ya mei lakini lilitokea tatizo kubwa februari. Yule jamaa alituhumiwa kwa upotevu wa fedha pale kazini kwake na hivyo alisimamishwa kazi, mtafaruku huu ulifanya kasi ya kuoa ipungue  ingwa ndugu wa jamaa yangu walishinikiza  mambo yaendelee kama yalivyokuwa yamekusudiwa, Jamaa yangu alijaribu kupinga  mawazo yao na kusema hawezi kuoa wakati hana kazi lakini ndugu zake walimzidi nguvu na alilazimika kukubaliana nao kwa hiyo ilipangwa ndoa ifanyike kabla ya Augosti tuliendelea na maandalizi ingawa jamaa yangu hakuwa na furaha kufuatia kufukuzwa kazi. 

Ilifika tarehe ya mahari ukweni na hivyo ilibidi wana ndugu maalumu wafanye kazi hiyo, miongoni mwa wanandugu wanne waliotumwa kupeleka mahari baada ya barua yetu kukubaliwa mimi nilikuwa mmoja wao, tulituma ujumbe kwanza kuwa tutafika saa sita mchana siku ya jumamosi pale kariakoo kwa wakwe watarajiwa, ni kweli tuliondoka saa 5;30 pale kwetu Kinondoni  na kufika hapo kariakoo saa 5;45  hivi tuliegesha gari tulilokodi  na kuanza kuelekea pale kwa wakwe. Lakini ghafla walitokea vijana kama sita hivi  ambao walikuwa wanaonyesha kila dalili ya kwamba  walikuwa wamevuta bangi na kubwia unga, walituzuia na wenyeji wetu walikuwa wameshatoka kuja kutulaki “Leo utatwambia  kama sisi ni Waisrael au Wayahudi  mmoja wa wale vijana sita alisema akiwa anamwangalia Yule jamaa yangu halafu ghafla walikuwa wamemzunguka na kutuacha sisi tukiwa tumeduwaa, tunaomba mkwanja wetu au tufanya kisichotarajiwa sasa hivi, mwingine ambaye ndiye aliyeonekana kuwa kiongozi  wao alisema  akionyesha ala ya kisu ambayo ilikuwa ikining’inia kiunoni  Yule jamaa yangu alibaki mdomo wazi kwa muda  Alipopata nguvu ya kusema alisema sasa, mbona tunataka kuadhiriana jamaa zangu? Kabla hawajajibu kaka wa jamaa yangu aliiingilia kati na kuuliza jamani hebu tumswalie mtumee ni jambo gani linaendelea hapo? Mmoja kati ya wale vijana walevi alisema labda tumesha mswalia  sana huyu jamaa yako ndiyo bado anataka kujifanya yeye Mpalestina  sana…’

Ilibidi wenyeji wetu nao kuingilia Baba mkwe aliwasogelea wale vijana na kumshika mmoja Ati vijana wangu kuna tatizo gani? tunaweza kuyamaliza haya mambo kiungwana bila mikwaruzano hebu tuliweke wazi….’ Kabla haja maliza mwingine kwenye kundi  la vijana wale alisema  hapo sasa umekuja penyewe, Huyu bwana anayejifanya leo kakwendea kipemba  kwa tarabushi tuna…’ Kabla hajamalizia Yule jamaa yangu aliingilia kati Sikiliza Bajalo tutayamaliza ngojeni  kwanza nimalize mambo yangu hapa halafu tutajadili baadaye  na nitafiksi kila kitu, kijana mwingine aliingilia kati  na kusema kila siku utafiksi utafiksi jana umetwambia kuwa umeacha  mzigo kwa demu wako, tukaenda patupu, tukaenda kwa Yule manzi wako wa huku kawe naye miyeyusho tu  mshikaji wangu sasa leo lazima kieleweke mkubwa wetu…’ 

Yule aliyeonekana kuwa mkubwa wa kikosi alimgeukia baba mkwe wetu mtarajiwa na kumwambia Sikiliza mkuu huyu jamaa tunamuuzia kitu yaani unajua huwa tunamuuzia bangi, mzee mwenzetu, hakutulipa ndo hivyo hadi kwanza ……..halafu zamani hakuwa hivi alikuwa freshi tu..”

Kwakweli hata mimi nilishituka kwa sababu sikuwa najua kwamba jamaa anavuta bangi ingawa nilikuwa na wasiwasi na jambo hilo mkwe mtarajiwa aling’aka na kuuliza bila kutarajia ni kweli haya mwanangu? Wale walevi wenzie walipaza sauti kwa pamoja mzee hiyo haina noma hapakaziwi mtu hapa mmoja aliendela kung’aka tunataka michome yetu Laki taslimu halafu wote tulishangaa kusikia deni la bangi la lakimoja Yule baba mkwe mtarajiwa  alirudia swali lake kama vile hakuwa akisikia kitu kingine  chochote pale jamaa yangu aliinama na kusema ndio mzee.

 Mzee Yule yaani baba mkwe mtarajiwa alisema astaghafirulah! Tulitulia kwa muda. Najua unataka niendelee kukusimulia kwa akili yako unadhani tuliruhusiwa kutoa mahari sawa kwa sababu unadhani wote wana njaa ya mahari  na sio nidhamu si ndio eee muangalie vile!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni