Jumanne, 8 Machi 2016

Uhusiano wa Uislamu na Majini !



           Katika  moja ya mambo yenye kutushangaza sana sisi Wakristo hatuchangamani kabisa na majini au Mashetani wala hatuna uhusiano nayo, Kinyume na hilo Waislamu wana uhusiano mkubwa na wakaribu na majini na mashetani na kwa ujumla Masheikh na Maalimu wanaotumia quran kutibu au kulaani watu (al-Badir) hutumia nguvu za majini ambazo ni nguvu za giza, Muhamad pia alitumia nguvu hizo za giza, Kuna wakati ambapo wakristo kutoka Narjan kusini mwa Arabia walimtembelea Muhamad kujadili mambo ya dini kwa siku kadhaa baada ya kuwa wakristo wamekataa kusilimu,Muhamad akasema “njooni hadharani tukusanyike pamoja wana wetu na wana wenu,wanawake zetu na wanawake zenu,sisi na ninyi kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana kwa Mungu iwashukie waongo! (surat al Imran 3:61).Muhamad alitaka kuwalaani wakristo kwa jina la allah na wakristo walaani kwa jina la Yesu kuona nani wenye nguvu,Wakristo walikataa kwani hawakuitwa kulaani bali kubariki tu.



     Kuna hadithi pia kuwa Muhamad alikwenda Yerusalem akafika pale lilipokuwa Hekalu la wayahudi wenyewe waislamu hupaita Baittil maqdis kwa usiku mmoja  kwa kutumia mnyama aitwae “Buraq” Mnyama huyu ni jinni lenye sura ya mwanamke mzuri na mwili wa Farasi (Soma kitabu Maisha ya nabii muhamad uk 28 kifungu cha mwisho) jambo hili lilimfanya akataliwe zaidi na watu wa makka wakisema ni mchawi mkubwa na hawako tayari kumuamini mchawi,Hizi ni khadithi chache tu ambazo zinatudhihirishia kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya Uislamu na Majini, Mashetani na mambo ya uchawi au ushirikina katika uislamu tutachambua mtazamo wa quran kuhusu viumbe hao ikiwa ni pamoja na mashetani,malaika na majini.

 Mtazamo wa Quran kuhusu Mashetani, Majini na Malaika   
    Waislamu wanaamini kuwa kuna viumbe walioumbwa na Mungu ambao hawaonekani kwa macho ya kibinadamu viumbe hawa wamegawanyika katika makundi makuu matatu.

  • Shetani
    Shetani ambae hutambulika pia kama ibilisi “iblis” ameitwa hivyo kwa sababu alilaaniwa na Allah  kwa kukataa kumtii allah alipomuamuru kumsujudia Adamu mara baada ya kuwa amemuumba (Surat al-baqara 2;28-38 na al aaraf 7;10 na al khaf 18:50) kutokana na laana hiyo alipewa muda na Allah ili awapoteze watu kwa kuwakalia pande zoote na alipewa ruhusa baada ya kujiombea kufanya hivyo(al-aaraf 7;16-17)Allah alitoa nafasi ya kuingia motoni kwa yeyote atakayemfuata shetani,Hivyo kwa waislamu shetani ni adui mkubwa na hulaaniwa kila mwislamu anapotaka kufanya jambo lolote hujikinga na muovu huyu kwa dua hii “ aaudhubiiIlah mina shaytwaani rajiim” yaani najikinga kwa allah na shetani apigwae mawe,ameitwa apigwae mawe kwa kuwa Ibrahimu na mwanawe Ismael walimpiga mawe Punde alipotaka kuwadanganya wasiitii amri ya Allah ya kutaka kumtoa Ismail dhabihu,Mashetani ni kundi kubwa sana na baba yao majini ni shetani.Vitabu maarufu vya kiislamu vinathibitisha soma (Itqaan fiy’uluwmi al-juzuu 4 uk 374,hadith 5,553).

·         Majini
    Kumbuka shetani alikuwa miongoni mwa majini(al-kahf 18;50) hivyo shetani ni jinni na jinni ni shetani,quran inafundisha kuwa viumbe hawa waliumbwa kwa ndimi za moto(al-Hijir 15;26-27,ar –Rahman 55:14-15) woote wanaofanana na shetani woote wamezaliwa na shetani woote kazi zao zinafanana,Hivyo majini yana nafasi kubwa sana katika uislamu kujaribu kuwatenga majini na mashetani  ni kiini macho tu kwani majini yalisilimu (surat 72;1-14)ingawa kuna kundi lingine halikuslimu,Hata hivyo Allah aliwatumia woote katika kazi mbalimbali  mfano kumsaidia Sulemani katika kazi zake mbalimbali za ujenzi,kumletea johari na vito vya thamani toka baharini,kumjengea nk.Soma (Surat al anbiyaa 21;81-82)Allah alikuwa mlinzi yaani msimamizi,Allah pia huwatumia majini kufarikisha watu aliwatumia huko Babeli na kufundisha watu uchawi hawa mashetani huitwa Haruta na Maruta soma (al-Baqara 2;102) aidha katika namna ya kushangaza Allah alimletea kila nabii maadui aliowatuma mwenyewe yaani majini na Mashetani (surat al anam 6;112 na al-Hajj 22;52).Baadhi ya Madhehebu kama ahmadiyya walipogundua kuwa majini ni mashetani na mashetani ni majini walianza kukataa dhana hii na shehk Farsiy anawakanusha vikali katika ufafanuzi chini,Waislamu wanatambua kuwa majini ni ndugu zao na ndio maana moja ya mashart ya swala katika kumalizia kikao cha mwisho kiitwacho (atahiyat) lazima kwa kila Muislamu asalimie pande zoote mbili yaani kwa kugeukia kushoto na kulia,kushoto ni kusalimia muislamu mwenzako na kulia ni kusalimia kundi kubwa la majini ambao hujumuika na waislamu katika swala (arshad-alMuslim) hii ni lazima hata kama mwislamu atakuwa pekeyake wakati wa swala kwani majini hujumuika nae.Aidha muhamad anasema kila muislamu anapozaliwa anapata ulinzi toka kwa majini na mashetani (soma al-muslim,Miskat), Majini yana ufahamu mkubwa sana wa quran na uislamu, yameslimu Muhamad alipokwenda kwa majini na kuanza kuwauliza mambo ya uislamu majini yalijibu vizuri kuliko wanadamu soma (surat al ahqaf 46;29-30) soma pia ufafanuzi wa aya hiyo chini katika quran ya Farsiy.Kwa ujumla hutakutana na jinni ambalo lina jina la kikristo majini yoote yana majina ya kiislamu anaeleza Desmon Mkumbo moja ya wataalamu wa huduma ya biblia ni jibu Tanzania.Majini pia huhubiri Uislamu  kwa nguvu na huhusika kusilimisha watu ukiwa na ugonjwa au pepo limekupagaa ukipelekwa kwa sheikh au maalim akusomee duwa utapewa masharti ya kubadili dini,jina, kusilimu au kuswali haya ni maagizo ya majini Mwenye masikio na asikie!.

·         Malaika (malaikat)
   Hili ni kundi la tatu katika imani ya kiislamu kuhusu viumbe wasioonekana kumbuka waislamu huamini malaika na inasemekana kuwa Allah aliwaumba viumbe hao kwa nuru,Idadi yao haijulikani,kazi yao ni kumsifu Allah wako malaika wa muhimu watano nao ni jibril huyu ndiye malaika mkuu Allah humtuma kuwasiliana na manabii wake Quran humuita Roho mtakatifu (surat an nahl 16:102). Ni Roho wa mafunuo na Nguvu Laylatul-Qadr (surat al qadr 97;1-4)Mikail huyu yuko chini ya jibril (al baqara 2;98),Israfiil ni malaika anayeaminika sana,anasifika sana hatajwi katika quran lakini anaaminika kuwa ndiye atakaye puliza parapanda siku ya mwisho,  Izrail pia hatajwi katika quran lakini anaaminika kuwa ndiye mtoa roho za watu (al anam 6:61),Hamalat al arsh hawa wako nane inaaminiwa kuwa watabeba kiti cha Allah siku ya hukumu  (al- haqqah 69;17), Waislamu huamini pia wako malaika wengine watano ambao hujulikana kwa kazi zao hao ni hafadhan hulinda binadamu kutoka katika mikosi na balaa kwa mujibu wa Muhamad katika hadithi zake anadai wako kumi.Katibun hawa huandika habari za mtu wako wawili mmoja huandika habari za matendo mabaya na mmoja mema, wa mabaya hukaa kushoto wa mema hukaa kulia kila mtu anao wawili (az-zukhuf 43;80 na qaf 50;17-18),Malik ni mlinzi wa moto wa Jehanam(az-zukhuf 43;77),Ridhiwan hulinda pepo (paradiso),Munkar na Nakir  hawa ni wakali sana huuliza maswali kaburini mtu anaezikwa huulizwa maswali juu ya uislam, hivyo muislamu anapozikwa Masheikh humfundisha namna ya kujibu maswali hayo mtu aliyezikwa ili kumuepusha na adhabu ya malaika hao.

Maoni 10 :

  1. Nuru ya mungu ndio huangaza kweli, hakika ya mungu ni Hekhima na maarifa atujazayo.

    Ushukuriwe kwa tafiti ulizo sifanya, ni kwasababu Mungu amekupulizia pumzj kamili na utambusi wa yale ya sirini.

    Nimefurahishwa na uandishi wako, japo sijafwata mistr elekezi ili nijiridishe, sina shaka juu ya hayo.

    Nataka nikuambie kitu ndugu yangu, kunakazi katika taifa hili, Mungu muumba wa mbingu na nchi amekuzudia kuthibitisha utiisho wake mkuu hapa, tafadali nisaidie tukamilishe kazi ya mungu. Ninaagizo la muhimu kwa taifa hili please

    JibuFuta
  2. Tutafutie hivi vitabu ili nasi tuvisome

    JibuFuta
  3. Nafkiri page hii ina lengo la kuleta chuki za kidini na sio kuelimisha

    JibuFuta
  4. ww ulioandika hii page muongo na ni mtoto wa shetani

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kwamba yalioandikwa hapo hayapo au?

      Futa
    2. Ukiwa unakanusha unatakiwa utupe ukweli

      Futa
  5. Nijuze namna ya kitabu Cha maisha ya nabii muhammad

    JibuFuta
  6. Nijuze namna ya kupata kitabu Cha maisha ya nabii muhammad

    JibuFuta
  7. Hatari sana
    tuzidi kumuomba Yehova atujazie nguvu ya kiroho na imani tuweze kujiepusha na izo nguvu za kishetani na majini

    JibuFuta