Jumanne, 22 Machi 2016

Ujumbe: Neema ya Mungu Haitendi Haki !


ONYO! “Kama hauna akili ujumbe huu haukufai, Usisome ujumbe huu kama hauna akili hutaelewa”acha!


1Wakoritho 1:26-31 Biblia inasema hivi:-
“26. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27. bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28. tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29. mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 31. kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.”

Ndugu zangu unapoyatafakari maisha kwa undani sana na hasa maisha ya kiroho unaweza kuchanganyikiwa na ukagundua kuwa kitu au jambo linaitwa neema ya Mungu ni gumu kupokelewa kuliko unavyofikiri, ni rahisi kutafakari mambo juujuu na ukasema ni kwa neema ya Mungu lakini neema sio jambo jepesi kama unavyofikiri, leo sitaki kabisa kufafanua nini maana ya neema kwa vile nafikiri tutazunguka tu lakini natka kukazia kuwa Neema ya Mungu haitendi Haki! Najua kuwa hii ndio lugha nyepesi itakayokusaidia leo kuelewa ninapotaka kuizungumzia neema ya Mungu.
Neema ya Mungu haitendi haki swala hili kwa asili sio sahihii lakini ndio litakalotusaidia leo kuelewa maana ya neema ya Mungu tukinena kiwazimu, kichwa hiki kinatusaidia kujua kuwa wewe na mimi sio Mungu na Mungu sio mimi na wewe, wakale walisema “ Mungu sio Athumani” hebu tufafanue kwa kina zaidi

Tunapoisoma biblia neno la Mungu mara nyingi tunasoma katika mtazamo wetu our own perspective, Hata ingawa tunafahamu kuwa hili ni neno la Mungu na kuwa njia zake sio njia zetu wala mawazo yake sio mawazo yetu, angalia tunapokosea akili zetu hutuambia kuwa tunahitaji kuadhibiwa kwa sababu ya makosa yetu ndio nah ii ndio Haki kabisa, tunajisikia kuwa tumemkosea Mungu na ni lazima tuadhibiwe ndio hiyo ndio haki, sio hivyo tu wanaotuzunguka wanaweza kuona kwamba tumemkosema Mungu na ni vema tukiadhibiwa na ni haki kabisa si tumekosea si amekosea ni haki akaadhibiwa ni haki tukasimamia aadhibiwe ni haki akione cha mtemakuni ni haki akome afundishwe asirudie tena ajutie kosa lake aipate fresh, ashughulikiwe  na ndio usahii wa mambo kwa mawazo yetu ya kibinadamu, Lakini shida au Tatizo la Mungu haangalii mambo kama tunavyoangalia sisi, sisis tunataka haki, tunatadhamia thawabu kwa mtu aliyetenda vizuri na mabaya kwa aliyefanya vibaya Mungu ni tofauti, haangalii kama tunavyoangalia sisi mtazamo wake sio sawa na wa kibinadamu “your perception is not always Gods reality” Mtazamo wako sio ukweli kuhusu Mungu wakati wote. Mungu aliweka mipango kabla sisi hatujazaliwa alijua kipi kitakuwa sahii na kipi hakitakuwa sahii katika maisha alijua wapi utakaa vema na wapi utakosea alijua kabla hajakuumba, na wakati wote huo mpango wake ni kutufanikisha, kuanguka kwetu sio jambo la kushangaza kwa Mungu sio habari hata its not a news yeye anaendelea na mpango wake wa kutufanikisha tu yuko busy kutufanikisha, sio lazima afungwe  na haki, anaangalia mpango wake yuko kwenye kutii mapenzi yake na makusudi aliyotuumba kwayo

Angalia kifungu cha maandiko tulichokisoma pale juu, ni mfano ulio wazi kuhusu neema, kama Paulo angesema Mungu anachagua watu maalumu, wenye akili, wenye cheo, wenye uwezo, waliowakamilifu, watenda mema anawatafuta watu wa aina hii duniani awabariki na kuwatumia kwa utukufu wake, hii ingekuwa ni sawa na inakubalika katika akili ya kawaida Logical na lingekuwa ni jambo jema na wote tungejitahidi sana kuwa wazuri kiasi ambacho Mungu angeshawishika kutuchagua, kama Mungu angekuwa anaagalia watu wa aina hiyo wachapa kazi, wenye bidiii, wasio na maswalimaswali hata katika maswala ya uadilifu, waungwana  kwa akili zetu za kawaida tusingeweza kulaumu chochote maana ni haki tu.

Paulo Mtume alichaguliwa na Mungu na kutumiwa kuandika karibu nusu na zaidi ya agano jipya, kamakuchaguliwa kwake kulitokana na kushinda mashindano ya mitume walio bora tusingelikuwa na maswali maana ni haki, amewashinda mitume wengine, lakini la kushangaza ni kuwa Mtume huyu hakuwa hata katika orodha ya mitume wale 12, wakati Yesu anapaa ndo kwanza huyu alikuwa upande wa pili akiwapiga vita wakristo na kuwatesa vibaya na kusimamia  mauaji yao, aliomba hata kibali cha kuwatesa na kuwaburuza wakristo kila waliko, cha kushangaza sasa Yesu anamchagua huyu na kumtumia kwa kiwango kikubwa kuliko mitume wote, hii inachanganya akili zetu za kawaida hii sio haki, huyu hafai, muuaji mtesi wa kanisa alitakiwa afe, hii ndio ilikuwa haki yake lakini anachaguliwa kuwa mtume hii sio haki kabisa hii ndio NEEMA YA MUNGU!

Sasa tunajifunza nini hapa?
1.       Neema ya Mungu haitendi haki. Unapofundishwa kwa kutishiwa kuwa kila upandacho utavuna au kuna kuvuna kile ulichopanda inakubalika akilini kuwa ni sawa logically unakubali na kuelewa kuwa utakachopanda utavuna, ni rahisi kuelewa kuwa apandacho mtu ndicho atakachovuna hii ni sawa hii ni haki, ni haki mtu mbaya kupatwa na mabaya na mtu mwema kupata mema ni sawa tunavuna kila tunachokistahili, lakini kama tunastahili mema kwa kutenda mema na mabaya kwa kutenda ubaya sasa hapo ni malipo na sio neema tena. Mungu hatendi haki hata kidogo Mungu hufanya mambo kwa sababu anatupenda, anakupenda na ananipenda

2.       Usijaribu kupigana na neema ya Mungu kwa akili za kibinadamu, wakati mwingine ni vigumu kuelewa kwa nini Mungu anafanya kitu Fulani kwako au kwangu, ni muhimu tu kukubali kuwa ni upendo wa Mungu na kupokea kila jambo kwa upendo, upendo wake ndio unaomshukuma afanye kitu katika maisha yetu, Mungu anaposema kuwa anataka kukubariki na kukutumia sana na akili yako inapopambana na kusema mbona sistahili unapigana na neema, Mungu anapombariki mwingine huku unafahamu kabisa udhaifu wake ukaanza kushangaa nankushutumu unapigana na neema ni lazima tukubali kuelemewa na Neema ya Mungu acha kupigana na neema acha




3.       Luka 15: 11- 32 Biblia inasema hivi “11. Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;   12. yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.        13. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. 14. Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; 19. sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.                 20.Akaondoka,akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. 25. Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.  26. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?  27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32. Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.” Yesu alitoa ujumbe huu hapo juu kwa sababu ya watu waliokuwa wkipigana na NEEMA YA MUNGU utawezaje kujua kuwa Yesu aliwaonya watu hao ili wasiingilie Kazi anazozifanya Mungu kwa kutumia akili zao logic angalia mistari hii ya awali katika Luka 15:1-2 Biblia inasema hivi  1. Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. 2. Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula naoAngalia maneno ya aya hizi kwa umakini na Mungu akusaidie Yesu alikuwa anajiwa na watu ambao kwa akili za kawaida walikuwa wabaya, waliitwa wenye dhambi, wahalifu kwa hiyo wale watakatifu wenye haki walinung’unika kwa nini mwokozi anatenda jambo kama hili, kwa akili za kawaida ilikuwa ni haki, Yesu ni Mungu na Mungu ni mwenye haki, rafiki zake ni wenye haki, anapaswa kuwahudumia na kuwajali na kukaa nao na kuwatendea mema., Mfano wa Yesu alioutoa kufuatia manung’uniko hayo unaonyesha tena Neema ya Mungu haitendi haki, kwa vipi?

Mwana mpotevu alikuwa tayari amepewa sehemu ya urithi wake na mali yake, alitaka kuishi mbali na baba alitaka kuwa huru, amelelewa vizuri hakuna alichokikosa kwa baba yake sasa anataka kuchukua kilicho chake akaishi maisha ya uhuru, Baba yake alimruhusu, alimuachia alimpa alichokiomba na kukidai, aliondoka na kila kilichochake, alivitumia kwa anasa na maisha ya ukahaba, Hakuna alichobakiza nyumbani. Alichezea mali yake na uhuru wake, alifanya anayoyataka , mwisho yakamkuta mabaya aliishiwa na kupigika sana, hakuna alichobakiza alipoteza uhuru wake akawa kibarua akawal mlisha nguruwe, kwa mtazamo wa kawaida mtoto huyu kibinadamu ungemfanya nini? Alistahili malipo yake angeachwa akione cha mtema kuni angetaharizwa kipi kinakurudisha nyumbani umesahau nini? Umebakiza nini hii ndio haki aliyopaswa kufanyiwa kibinadamu alitakiwa kufukuzwa, angeachwa aonje joto ya jiwe akione cha mtema kuni!
Kutokana na taabu aliyokutana nayo aliamua kurudi kwa baba, Jambo la kushangaza ni kile baba alimfanyia

 “Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.” 

 Hiki ndicho alichokifanya baba yake alimuonea huruma maana yake Rehema za baba yake na neema ya baba yake ilimsukuma kumtendea mwanawe sherehe kubwa na kumfanya mfalme Prince na watu wote wa nyumbani kwa babaye walifurahi, Baba alijua kuwa mwanaye sasa anaweza kutofautisha maisha ya uhuru na usalama aliokuwa ameupata kwa baba yake, ni mwanaye ulitegemea atamfanya nini? Mwenyewe alielewa wazi kuwa anapaswa kuwa mtumwa tu, baba akamfanya Prince kijana wa kifalme, tunapokosea sisi na wanaotuzunguka tunategemea kuwa Mungu hawezi kutukubali tena wala kutufanyia mema haya ni mawazo mabaya kwa Mungu wetu ni kuushushia hadhi upendo wake kumbuka kuwa mfano huu na fundisho hili halitii moyo hata kidogo kuishi maisha ya dhambi lakini pia halikubaliani hata kidogo na fikra za majivuno na kiburi cha kujifikiri kuwa wewe unastahili kwa vile ni mwema kuliko Fulani, kipimo cha wema anacho Mungu na kwa rehema zake na neema yake ana haki ya kumuona mmoja kuwa sawa na wewe au kumuona mmoja kuwa bora kuliko wewe hata kama kwa vipimo vyako wajiona kuwa uko sahii, hakuna kiburi kikubwa na kibaya duniani kama kujiona unastahili nje ya neema ya Mungu, kama utakuwa na mawazo hayo utaiona Neema ya Mungu kuwa Haikutendei haki.
Hukumu na aibu ilimkuta ndugu mkubwa badala ya furaha kwake ilikuwa huzuni majuto na mkususa na kukasirika na ilikuwa siku yake ya kuhubiriwa kwamba kwanini afurahii Baba kumpata mwanaye, kwa nini hafurahii baba kumfanyia hserehe mwanaye ni wazi kuwa kwa akili za kawaida kaka mkubwa alijiona ni mwenye haki na mwenye kustahili, lakini lisahau kuwa amejikweza kwa matedno yake ya haki, aka kiburi Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema. Haya ndio yaliyomkuta 

“Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.  26. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?  27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32. Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.”

Kama kazi ya baba huyu ingekuwa ni kuhukumu na kutokuhurumia kuacha kuutumia ukarimu wake basi angekuwa ametenda haki, kama baba angemfanyi sherehe mwana wake mkubwa na kumpongeza kwa kuwa mtoto mwaminifu angekuwa ametenda haki na wote tungekuwa na ujuzi na watu wote wangeelewa kuwa Baba ni mtenda haki amemlipa kila mmoja sawa na kutenda kwake sasa tatizo ni Moja Mungu ni wa rehema na neema hapa anaonyesha Upendo, rehema na neema na ndipo linapokuja swala lililowazi linaloacha vinywa vyetu wazi kuwa Neema ya Mungu Haitendi haki kwa nini haitendi haki ili ibaki kuwa Neema, Bila shaka nikisema ni kwa neema sasa kila mmoja atakuwa anaelewa maana ya neema.

Unataka haki unataka Neema? Mimi nachagua Neema ya Mungu.

Sala ya kuomba neema:-

Baba ninakushukuru sana nakushukuru kwa Neema yako, kadiri ninavyojifunza kuhusu neema nagundua mambo ya kushangaza sana, Unajua vema kuliko ninavyojua, na ninavyojijua, unajua mara ngapi nimekosa na mara ngapi nimekulazimisha uingie name hukumuni uniadhibu, na wakati mwingine nimejiadhibu na hata kuadhibiwa na wengine kwa makosa yangu, lakini nashukuru kwa Upendo wako na kwa msamaha wako, umeniita hata hivyo, unanitumia hata hivyo pamoja na kunijua nilivyo, sio kwa sababu ya akili nyingi sana, sio kwa sababu ya kutoka katika familia ya wenye hekima, wenye vyeo, watawala, si kwasababu nimestahili, bali ni kwa neema yako, Kwa neema yako tunawashangaza wengi, kwa neema yako nitakuabudu na kukusifu siku zote za maisha yangu, kwa neema yako Maadui zangu wataisoma namba, kwa neema yako wanaoniwazia mabaya watatahayari, kwa neema yako umewatetemesha na kuwaziba vinywa watesi,kwa neema yako umenipa mema ya umande wan chi, kwa neema yako mdogo atakuwa elfu, kwa neema yako, Kaka zangu na Ndugu zangu wataniinamia, hawataponyoka kamwe katika kongwa langu,kwa neema yako umenibariki, kwa neema yako umeniinua, kwa neema yako kila kinywa kitakachoinuka kinyuma name kitahukumiwa, kwa neema yako utabatilisha kila shauri lisiolo haki dhidi yangu, kwa neema yako, kwa neema yako kila dua mbaya itageuzwa kuwa Baraka kubwa sana kwangu, kwa neema yako utanyamazisha woote walioona hududa dhidi yangu, kwa neema yako kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, nipe kuhubiri, kwa neema, nipe kuimba kwa neema, nitumia kwa neema, weka moyoni mwangu jumbe mbalimbali kwa neema, Neema neema neema

Wimbo kuhusu Neema
Wimbo: Mungu amenihurumia

1. Mungu ametuhurumia, tendo hili kubwa sana,
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake

2. Nalistahili kupotea, lakini nahurumiwa,
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.

3. Mungu mwenye huruma nyingi, usininyime huruma,
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
Ubarikiwe!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni