UTANGULIZI
A.
Umuhimu wa Kozi ya Ushauri wa kichungaji
Itakusaidia kufahamu historia na Ufahamu kuhusu ushauri nasaha
Itakusaidia kufahamu mbinu za kishauri ili kwamba uanze kufanya
ushauri nasaha
B.
Maeneo muhimu ya kozi ya ushauri wa kichungaji
Katika kozi hii kuna mambo ya msingi makuu matatu ambayo yanahusu
Watu ambao tutawafanyia ushauri
Mbinu za kufanya ushauri
Aina za ushauri wa kichungaji
C.
Kwa ni nini ni muhimu kujifunza ushauri wa kichungaji?
Kwa sababu kuna watu ndani na nje ya Kanisa wanaokuzunguka ambao
wana matatizo wanayokumbana nayo
Watu wana shida katika
maeneo makuu manne
1.
Matatizo ya kihisia Emotional problems au matatizo ya kisaikolojia
Psychological Problems
2.
Matatizo ya kiroho Spiritual Problems
3.
Matatizo ya kiuchumi Economic Problems
4.
Matattizo ya kimwili Physical Problems
D.
Kazi yako au jukumu lako kama mchungaji ni pamoja na
Kutafuta njia za kuwasaidia watu kuchukuliana na matatizo yao na
kutafuta kuyatatua kwa mafanikio
Kuhakikisha kuwa hatimaye wanayaona matatizo yao madogo na
yasiyotishio.
Ushauri wa Kichungaji "Pastoral counseling"
SOMO LA KWANZA: UFAHAMU
KUHUSU USHAURI COUNCELING
A.
Ushauri Nasaha ni nini?
·
Usahauri ni
uhusiano baina ya pande mbili zenye mahusiano ambapo mmoja wa wenye mahusiano
hayo yaani mshauri (The counselor)
anatafyuta kutoa ushauri, kutia moyo na kumsaidia muathirika (The counselee) kukabiliana na tatizo
alilo nalo katika maisha yake kwa ufanisi.
·
Jambo la
msingi hapa ni kuwa Mshauri nasaha anapaswa kufahamu kuwa hatoi tu ushauri tu
na kutia moyo lakini pia unapaswa kuvaa kiatu cha Yule unaye msahuri yaani
kuumia pamoja naye ,
·
Jambo kuu la
msingi katika kushauri ni kutafuta wazo lenye uifanisi litakalosaidia katika
kumfanya msauriwa kufanya maamuzi na kumsaidia kurudi katika hali ya kawaida
kiakili na kisaikolojia
·
Kwa kawaida
kulingana na mtazamo huu hata kama mtu hana tatizo ambalo ni kubwa sana bado
anaweza kuja kutafuta wazo lenye busara litakalo msaidia kufanya maamuzi mazuri
na kupata mafanikio katika maisha kwa ujumla
B.
Mchungaji kama msahauri
·
Ushauri wa
kichungaji ni moja ya njia za hali ya juu ya njia za uponyaji na njia ya
kusaidia watu kubeba matatizo yao na magumu wanayaokutana nayo hivyo
kusababisha ukuaji ulio bora na uponyaji wa mioyo iliyovunjika, si kila wakati
mahubiri ya madhabahuni yanaweza kuyafikia matatizo ya ndani sana ya wanadamu
wakati mwingine inahitaji kuwasikiliza watu na ushauri nasaha ndio njia ya
uponyaji huo.
·
Huduma hii
pia ni hatua ya kuwafikia walio karibu na walio mbali kimisheni hasa kwa
kuwafikia wenye shida na taabu jambo
hili hujumuisha mbinu ya kuwafikia watu kwa kuitikia mahitaji yao ya kishauri
ndani ya kanisa na nje ya kanisa
C. Lengo la
ushauri wa kichungaji.
·
Lengo kuu la
ushauri wa kichungaji ni kuhakikisha kwamba muathirika yaani mwenye kuhitaji
ushauri anafikia kilele cha uponyaji wa kiroho na ukomavu
·
Mshauri
anakuwa ni njia ya kusaidia kukua kiroho kwa wahusika washauriwa anakuwa ni
mwezeshaji na njia ya uponyaji na mchakato mzima wa ukombozi.
·
Washirika wa
kanisa husika wafikie hatua ya kumuona mchungaji wao kuwa Baba mwenye kuaminika
, Mchungaji anapojishughulisha na
mahitaji ya kondoo anajiweka katika nafasi ya kuonekana kuwa ni muhusika
wa kundi na sio polisi katika kundi Matendo 20;28. Biblia ina sema hivi “
D.
Mbinu kuu mbili zinazohitajika katika ushauri
wa kichungaji
1.
Kijihusisha
(Relating) – Ili kutia moyo kwa
uwazio kabisa uponyaji na ukomavu
mshauri lazima akubali kuwa na na uhusiano na watu au kujihusisha na watu,
ushauri wa kichungaji ni njia nzuri ya
kupeleka habari njema katika lugha ya
mahusiano lugha itakayo ruhusu mshauri kuwasilisha ujumbe wa uponyaji kwa
mshirika mwenye kusumbuliwa na hatimaye
kuweza kumfanya aone mambo yako sawa.
2.
Mawasiliano
(Communicating) – Mchungaji
mshauri ni njia ya kupitisha taarifa na
njia ya kuhakikisha kwamba wazo lenye Busara litakalomfganya msauriwa kuchukua
uamuzi kwa msingi huo ni muhimu mchungaji kuwasiliana au kujifunza namna ya
kuwasiliana kwanza kwa kuonyesha upendo wake binafsi na upendo wa Mungu kwa
Mshauriwa.
UHUSIANO WA
USHAURI WA KICHUNGAJI NA UCHUNGAJI.
Uchungaji ni jukumu moja la muhimu na
pan asana kuliko tunavyoweza kufikiri na ni zaidi ya kuhubiri,Huduma ya
uponyaji na makuzi katika kanisa na jamii katika mzunguko wa maisha haya basi
ushauri wa kichungaji ni moja ya majukumu ya ndani nay a muhimu sana ya
kichungaji. Kwa ujumla kuna majukumu
makubwa muhimu kama matatno hivi katika shughuli za kichungaji
1.
UPONYAJI – Moja ya majukumu ya muhimu ya
kichungaji ni uponyaji ambapo mchungaji anafanya kazi ya kuweka malengo ya watu
wake au wateja wake kushinda matatizo ya aina mbalimbali kwa kupitia
a.
Kuhakikisha kuwa mtu anakombolewa kwa ujumla
b.
Kumuongoza katika malengo yaliyo zaidi ya mahitaji yake ya
mwanzoni
2.
KUWEZESHA – NI wajibu wa mchungaji
kumsaidia muathirika kuweza kuvumilia na kuchukuliana na Mazingira hata pale
inapoonekana kuwa kuna mazingira ya kutokuwezekana au pale ambapo uponyaji uko
katika mchakato au haiwezekani.
3.
KUONGOZA -
mchungaji atamsaidia muathirika ,kufanya uamuzi sahii kwa ujasiri
4.
KUPATANISHA – Ni wajibu wa mchungaji
kustawisha uhusiano ulio haribika kati ya mtu na mtu au kati ya mtu na Mungu hivyo wakati wa
kufanya ushauri wa kichungaji , Mchungaji pia atakuwa anaifanya kazi ya
kumpatanisha mtu husika na Mungu
5.
KUFANYA MALEZI – huu ni uwezeshaji wa kumtia
moyo mtu kuweza kuendeleza kipawa au karama aliyopewa na Mungu.
6.
Kumbuka kuwa kuna nafasi za kufanya mambo nmengi yahusianayo na
huduma za kichungaji endapo nafasi hiyo itatumika zaidi ya nafasi
zilizoorodheshwa hapo juu.
A. BIBLIA NA MASWALA YA USHAURI
Umuhimu wa kutumia maandiko wakati wa kufanya ushauri.
Biblia ni kitabu cha ushauri wa Kikristo ,
Kila msahuri wa kikristo hususani Mchungaji ni muhimu kukumbuka kuwasaidia watu
kuwa na uwezo wa kuchukuliana na maisha ya kila siku kupitia neno la Mungu,
ushauri wowote ambao hautaruhusu Biblia kufunuliwa huo sio ushauri wa
kichungaji au hauwezi kuwa ushauri wa kikristo
Kuna matatizo mengi ambayo yanaweza kutatuliwa au kutiwa moyo kupitia
vifungu Fulani vya kimaandiko, ndani ya hayo kuna majibu yaliyo wazi na yaliyo
elezewa vizuri, ingawaje inaweza kuwa ngumu kutafuta maandiko kwa ajili ya kila
aina ya tatizo lakini hutakosa muongozo au kanuni zinzoongoza ndani ya biblia
ambazo zinahusiana na maisha ya kila siku kwa ajili kujifunza namna ya
kuchukuliana na hali halisi.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA NA
UTUMIAJI WENYE MATOKEO MAZURI WAKATI WA USHAURI
·
Ni muhimu
uwe mtandaji wa neno Yakobo 1; 22-25,2Timotheo 2;15.
·
Soma biblia
kila mara kwa utaratibu maalumu ili uweze kuwa na ufahamu wa kutosha wa kanuni
hizo zenya kuongoza maswala Fulani ya maisha Wakolosai 3; 16-17,2Timotheo
3;16-17.
·
Hakikisha
kuwa unakariri baadhi ya maandiko, kwa mfano unajua kuwa utashauri watu katika
maeneo kadhaa ya kimaisha basi ni muhimu kuandaa maandiko yanayoendana na
tatizo husika utakalokuwa ukishugjhulika nalo weka orodha ya matatizo unayotaka
kuyashughulikia kwamfano
-
Woga andaa Zaburi
ya 34;4
-
Kukosa amani
andaa Yohana 14;27
-
Kutokusamehe
Mathayo 6;12
-
Zinaa andaa
Mathayo 15;19, 1Koritho 6;9-10 n.k.
-
Majaribu
andaa 1Petro 1; 6-7n.k.
-
Ulevi na
madawa ya kulevya andaa 1Koritho 6;15,19-20Luka 21;34
-
Utaweka
orodha ya matatizo unayokutana nayo katika jamii na majibu ya kimaandiko kwa
shida za aina mbalimbali
·
Tumia toleo
zuri la Biblia na itifaki ili kujaribu kusaidia kukusanya maandiko yanayohusiana
katika na matatizo husika
·
Muombe Roho
wa Mungu akupe maandiko yenye kufaa
ambayo yatavuvia utumiaji wako wa neno wakati wa kufanya ushauri wa kikristo
B. MASWALA YA USHAURI WAKATI WA AGANO LA KALE
Nyakati za agano la kale tunaona kuwa
kulikuwa na aina nyingi sana za maswala ya ushauri pamoja na kusaidia watu
kishauri, nyingine kati ya vifungu vya kishauri katika agano la kale vilikuwa
vilikuwa vikilenga tatizo moja kwa moja ili kulishughulikia na shauri nyingine
zilikuwa zenye kuzunguka
Maneno
yanayotumika kuonyesha ushuri katika agano la kale ni pamoja na
a. Mithali 12 ; 15 Yeye atafutaye ushauri ni
mwenye hakima
b. Mithali 11 ; 14 Katika wingi wa mashauri kuna
usalama
c. Zaburi 25 ; 9 Wanyenyekevu wataongoza
d. Zaburi 23 ; 2 Kando ya mito ya maji ya
utulivu huniongoza
e. Yeremia 23;3-4,Mwanzo 29;7, Isaya
40;11,1Nyakati 17;6 Mungu anatajwa kama mchungaji ambaye analisha kundi lake
Nabii Kama
Mshauri
Manabii wote wa agano la kale walikuwa ni
washauri,Hususani kwa wafalme na pale
ushauri unapokuwa ni wa taifa zima Mfalme angeutoa kwa watu wote mfano 2Falme
21; 1-14, Damuel 12;1-15.
Waamuzi kama
washauri
Kutoka 18;13-26 Musa alikuwa aki waamua watu na kuwashauri
kutoka aubuhi hata jioni,lakini kuna wakati nay eye alishauriwa namna ya
kuwaamua watu ili asichoke na watu wasichoke alishauriwa kuweka makuindi ya
viongozi kubeba kazi ile pamoja naye.
Debora alifanya kazi ya kiushauri waamuzi 4-5
Samueli alikuwa nabii na mwamuzi
Mifano
mingine ya kiushauri katika agano la kale
1. Mordekai
alikuwa akimsauri Esta Esta 4;1-14
2. Samuel
alikuwa akimsahuri Sauli 1Samuel 15;10-12
3. Suleimani
aliwashauri wanawake wawili 1Falme 3;16-28
4. Rehoboamu alikataa ushauri
mzuri na kuchukua mbaya 2 Wafalme 10;1-13.
C. MASWALA YA USHAURI WAKATI WA
AGANO JIPYA
- Neno ushauri
katika agano jipya lina asili ya kiyunani “Symboleuo”
ambalo maana yake kutoa wazo, kutoa au kuwaza kwa pamoja Matendo 20; 27
- Maandiko mengi
katika agano jipya yanayohusu wachungaji au uchungaji yana wazo lihusulo
ushauri Matendo 20; 28.
- Katika agano
jipya Neno la kiyunani Koinonia lilitumika kuonyesha uponyaji wa kikanisa
katika kuibadilisha jamii wakilenga maswala ya kiroho, Koinonia ilimaanisha
kustawisha ushirika miongoni mwa waamini kwa ajili ya kusaidia na kutia nguvu
Matendo 2; 42-47 kwa msingi huo mshauri anaweza kumjumuisha mwenye kuhitaji na
kupitia ushirika unaotolewa na waamini unaleta uponyaji na ushindi unajitokeza
- Injili zinazo
fanana zinaonyesha kuwa ingawa Yesu alihubiri injili kwa umati mkubwa wa watu
lakini pia alikuwa na muda na kutoa uthamani kwa mtu mmoja mmoja, mafano wake
wa kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea na ule wa mwana mpotevu unaonyesha
kielelezo chake cha kujihusisha na kujali maisha ya mtu mmojammoja na furaha
inayowakilishwa katika mifano hiyo inaonyesha mafanikio ya kujihusisha na mtu
mmojammoja mifano hiyo iko katika Luka 15.
- Katika injili ya
Yohana pia tunaona jinsi Bwana akijihusisha na maisha ya mtu mmoja mmoja
binafsi kama Nikodemo Yohana 3;1-17 na hatimaye kumshauri kuhusu kuzaliwa mara
ya pili,na Yohana 4;1-30 alijihusisha na mwanamke msamaria na kumuhubiri kuhusu
uzima wa milele na katika Yohana
20;27-28,alimshauri Thomasi kuhusu kuamini.
SOMO LA PILI: MBINUMBALIMBALI
ZA KUFANYA USHAURI.
Kuna njia mbalimbali za kufanya ushauri
hizi ni njia zinazowakilisha falsafa mbalimbali za kuelewa ipi ni njia ifaayo
katika kufanya ushauri (Theories of counseling).
A. PSYCHOANALYSIS
Falsafa ya njia hii ni imani kwamba kila
mtu ana baadhi ya maumivu aliyoyapitia mapema tangu utoto wake maumivu hayo kamwe
hayawezi kusahaulika isipokuwa yanakandamizwa tu chini sana katika ubongo wa
kumbukumbu bila kudhamiria, Ubongo unaitunza kumbukumbu hiyo isiyopendeza na
kutokutaka ikumbukwe na pale inapochochewa na kukumbukwa inasababisha matatizo
ya kihisia kwa hiyo kupitia njia hii ya Psychoanalysis tatizo lililokuwa
limekandamizwa linaweza kugunduliwa na likiisha kugundulika ndipo sasa muhusika
anapoweza kujisikia vizuri
Njia hiyo ya Psychoanalysis hufanywa na
Psychoanalyst ambapo mtaalamu huyu humruhusu muhusika kujieleza kwa uhuru kuhusu
historia yake ya huko nyuma, mambo aliyojihusisha nayo na kumbukumbu zake na
kadhalika. Theory hii au falsafa hii iligunduliwa na mtaalamu wa Psychology
Bwana Sigmund Freud daktari kutoka Austria.
Sigmund
Freud 1856-1939
Hili jamaa lilikuwa daktari
katika maswala ya madawa na utabibu alikuwa ni mtaalamu wa maswala ya akili
aliamini kuwa tabia ya binadamu inasukumwa na misukumo “Drives” isiyozuilika
kidhamiri au isiyokusudiwa kuelekea kwenye hitaji husika la kistarehe kama
tendo la ngono na endapo halitatimizwa basi linamuacha mwanadamu huyu katika
migogoro wa mtu na mazingira yake .
B. CLIENT
– CENTERED THERAPY
Falsafa hii inaamini kuwa kama muathirika
akipewa nafasi salama ambapo anaweza kuzungumza kwa uhuru kuhusu tatizo lake
anapata ahueni na hatimaye anaweza kupona ahueni hii inaletwa na upatikanaji wa
wazo jipya au ufahamu mpya kuhusiana na tatizo alilo nalo ufahamu huu huja
baada ya kuwa mgonjwa amepewa nafasi salama ya kuzungumza na kujadili nini kiko
moyoni mwake aina hii ya tiba iligunduliwa na kuendelezwa na mtaalamu Carl
Rogers ambaye alikuwa na shahada ya udaktari wa falsafa katika maswala ya
saikolojia huko U.S.A.
C. REALITY
THERAPY. (Dawa ya kweli)
Tiba hii inahusiana hasa na tatizo ambalo
limejitokeza hivi karibuni na sio nyakati zilizopita, aidha tiba hii hufanya
kazi katika maeneo ya mahusiano zaidi hususani pale mtu anapowajibika kitabia
kuliko maswala ya hisia
Kiini kikuu cha tiba hii ni kuwajibika
mara moja hapa au sasa hivi na sio kusubiria mpaka baadaye kabla ya kusubiri
muhusika azalishe hisia zenye kujirekebisha kitabia
Aidha lengo
linguine kubwa la tiba hii “Reality
therapy” Kumpa mtu vidonge vyake kwa lugha za mtaani au kumwambia mtu
ukweli ili aamue kupona au kufa hapohapo, na kumpa fundisho ili asiruydie tena
baadaye
Njia hii ina faia kwamba inampa mtu
kujitambua na kujielewa anapokosea kujua makosa yake anapofanya vema kujua
uwezo wake na hii itasaidia katika
kumfanya mtu kuwa na uwezo wa kujirekebisha mwenyewe, inamfundisha mtu
kutokukwepa kuwajibika na kujengeka mwenyewe kitabia njia hii iligunduliwa na
Dr.William Glasser.
D. MINIMUM
CHANGE THERAPY (hata badiliko dogo ni badiliko)
Tiba hii au falsafa hii inalalia katika
wazo la kuleta mabadiliko yaliyo mazuri hata kama ni kwa kiasi kidogo, bado
inasadikiwa kuwa ni muhimu, kwa hiyo muhusika anaachiwa ateseke kwa muda wowote
atakao uchukua kwani hatimaye atatulia na kupokea mabadiliko
Tiba hii
imegunduliwa na Bwana Leona Tyler ambaye alikuwa ni Professor wa chuo kikuu na
mtaalamu wa mambo ya ushauri
E.
BEHAVIORISM
Kwa mujibu wa tiba hii ambayo ni falsafa
ya bwana B.F.Skinner ambaye anaamini kuwa mwanadamu ni zaidi ya mbwa
asiyeeleweka na kwa ujumla anaathiriwa na mazingira yanayoamuliwa na shughuli
za kila siku na aina za mawazo, hisia, na matendo na hivyo anaweza kufundishwa
na kudhibitiwa kama mnyama mwengine yeyote kwa sababu ya kuharibu hali ya
mazingira yake.
Tiba hii inasema kwamba hakuna mtu muahalifu,
Bali kuna mazingira yanayopelekea uhalifu wakati bwana Freud anatafuta namna ya
kuufanya utu wa ndani wa binadamu ukae sawa bwana Skinner anataka kuboresgha
mazingira ambayo yatapelekea badiliko la kitabia katika muelekeo
utakaochaguliwa na mchongaji wa tabia yaani msahuri
Kwa hiyo kila kilichoko na mwanadamu ni
tabia na kwa haraka tunajifunza kuwa bora zaidi na sayansi ndio jibu la swala
hilo
F.
EXISTENTIALISM
Falsafa hii inaamini kuwa
mwanadamu ni kiumbe kisichotabirika na huwezi kuhusisha swala Fulani na ujuzi
kuhusu tabia Fulani hii ni kwa sababu maswala yake mengine hutokea kama ajali
na hakuna sababu inayokubalika kuweza kumzungumzia
Kwa msingi huo suluhisho pekee
ni kutokuhusisha hali yake na jambo lolote bali kujaribu kumfanya awe na
furaha, mfanya afurahi bila kutafuta sababu na anapopata furaha itatupilia
mbali matendo na tabia zilizokuwa zimejitokeza na jambo hili litaleta maana
kuliko kutafuta sababu
G.
GROWTH
COUNSELING APPROACH
Kulingana na falsafa hii
ushauri wenye matokeo ni moja ya njia ya kutafuta kumtia nguvu mashauriwa na
kumfanya Yeye kwa ujumla wake atiwe nguvu katika maeneo yote muhimu ya maisha
hii inaonekana kuwa mwanadamu anafunguka katika mfumo mzima na ukuaji unachukua
nafasi katika mahusiano ambayo yanalenga maeneo makuu sita ambayo ni
Uhusiano wake na Mungu unaimarika
Akili zake zinakaa sawa
Mwili wake unaponywa na kuwa na afya nzuri
Uhusiano wake katika ndoa unakomaa vema
Uhusiano wake na mazingira ya asili unastawi
Ukuaji wenye kuhusiaha umuhimu wa kujifunza maswala kadhaa katika maisha
Growth counseling approach ndiyo mbinu ya ushauri inayopendelewa sana na wasomi
wengi katika mpango mzima wa maswala ya ushauri wa kichungaji
SOMO LA TATU: MCHUNGAJI KAMA
MSHAURI
A.
Wachungaji wote ni washauri
Kila mtumishi hususani mchungaji ni
mshauri mara unapokuwa umeitwa kwa ajili ya kumtumikia Mungu basi wakati huohuo
umeongia katika kazi ya ushauri kwa msingi huo kushauri kwako linakuwa sio
swala la kuchagua kuwa nishauri au nisishauri, kwa sababu uwe umejifunza
ushauri au hukujifunza unakuwa umeingia katika kushauri hii ni kwa sababu
katika kila kanisa wako watu ambao wana maumivu ya ndani sana ya uhitaji
wanahitaji mchungaji awashauri ili kwamba wajue ni namna gani wanaweza
kuepukana na matatizo yao lakini sio kushauri tu kwani kuna nidhamu na mbinu za
stadi za kufanya ushauri hivyo kama kuna mchungaji atazikosa stadi hizo mtu
mwenye uhitaji anakuwa na moyo wa jiwe kwa kukata tama kwa kawaida ni mchungaji
pekee ambaye ana nafsi kubwa ya kuingia katika moyo wa maisha binafsi ya mtu na
ushauri ni sehemu muhimu ya kukutana na maswala ya aina hiyo
B.
Moja ya silaha za muhimu za ushauri kwa
mchungaji
Kuishi maisha yaliyo kielelezo ni moja ya
silaha yenye nguvu sana ya Ushauri wa kichungaji Mshauri hususani mchungaji
anawajibika kuwa na maisha yaliyo ya maadili ambayo yatakuwa ni kielelezo
katika jamii swala kama hili linamsaidia muathirika, kwa msingi huo unaweza
kufisha tabia ambazo zinawadhuru unaotaka kuwahudumia na kujijengea tabia
zitakazo wafanya wengine wakuamini.
Ni jambo gani tunapaswa kulifanya wote
tunajua kuwa Matendo yanasema kuliko maneno na ndivyo ilivyo kwa watu
wanaotuzunguka tabia zetu zinaleta athari, Biblia ina mafundisho mengi
yanayotukumbusha kuwa kielelezo kwa wengine kwa msingi huo maisha yako ni moja
ya mtaji mkubwa sana wa kufanya ushauri kumbuka
·
Ni maisha
Yesu aliyoyaishi yaliyoweza kuleta changamoto kubwa kwa wanafunzi wake maisha
yao yalibadilika kadiori walivyokuwa wakimkaribia na kuwa na muda naye soma
injili
·
Paulo mtume
aliishi maisha ambayo kwayo aliweza kuwahamasisha wafuasi wake kuufuata mfano
wake 2Thesalonike 3;7-9,Maisha ya Paulo yalikuwa yamejaa mafundisho yenye nguvu
kwaajili ya ushauri kwa msingi huo hata anapotoa ushauri kwa watumishi kama
Timotheo na Tito ushuri huo unaweza kufanya kazi kupitia mfumo wa maisha ya
mfano aliyoishi
C. Mipaka
na faida za ushauri wa kichungaji
Mipaka
1. Kila shughuli
itamgharimu mtumishi nguvu na muda, ukiachia mbali swala la kuandaa jumbe, kuna
maongozi ya kanisa zima kwa ujumla nah ii huwafanya wachungaji wengi kushauri
kati ya masaa 5-10 kwa wiki bila kuacha shughuli nyingine ziharibike
2. Mshauri ambaye
amesomea kitaalamu anatakiwa atumie miaka 8-10 ukiachia elimu ya sekondari kujifunza
swala zima la kufanya ushauri hivyo kwa mchungaji sio lazima atumie muda wote
huo kwa ajili ya mafunzo ya kushauri lakini anapaswa kufanya kila liwezekanalo
kujizoeza na kujifunza mbinu za kufanya ushauri
3. Wajibu wa
mchungaji mara nyingi umekuwa ukichanganya watu, Wengine humuona mchungaji kama
polisi na wengine huwaona wachungaji kama majaji wakali sana wasio na huruma kwa msingi huo ni muhimu sisi wachungaji
kuondoa upolisi na kukubali na kujaribu kuwasiliana na watu kwa sababu watu
ndio sehemu ya utumishi wetu inatupasa kuwapenda na kuwapa kipaumbele bila
kujali wako vipi
4. Wachungaji wengi
hawashiki malipo ya kazi zao za kiushauri lakini wataalamu wa maswala ya
ushauri Psychologists waligundua kuwa kuna watu ambao hawawezi kuithamini
huduma hii mpaka uwatoze fedha yaani inapowagharimu basi inaleta maana kwao
5. Majaribu wakati
mwingine hutokea kuwa mshauriwa akaweza kuendeleza hisia kali kwa mshauri na
hii inaweza kusababisha, hisia za upendo au chuki, hii inaweza kutokea hususani
katika ushauri unaochukua muda mrefu na maswala ya aina hii husababisha wakati
mwingine kashfa za ngono kwa wachungaji na chanzo kikiwa ni maswala ya ushauri
Faida za
ushauri wa kichungaji.
1. Kuaminika mara nyingi moja ya faida za
ushauri wa kichungaji ni pamoja na kuaminiwa na washirika na watu washauriwa
watakuja kwako.
2. Kustawisha uhusiano ukweli kuwa wewe ni
mchungaji ni rahisi kwa jamii na washirika kuwa na uhusiano na wewe kwa msingi
huo unaweza kustawisha uhusiano na jamii na familia katika kanisa na hivyo kuwa
na mahusiano yenye nguvu mahusiano haya yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
katika maswala ya kiushauri kuwa na mafanikio makubwa sana na hivyo kumfanya
mchungaji kuweza kutoa ushauri pale inapobidi.
3. Upatikanaji, Kwasababu ya upatikanaji
wa mchungaji inakuwa ni rahisi mwenye mahitaji kuja mara moja au mchungaji
kuwatembelea
4. Imani
moja ya faida kubwa ya mchungaji kama mshauri ni pamoja na watu kumuendea mara wanapokuwa na matatizo
kwa sababu ya maswala ya imani na kutoa uthamani kwa kiongozi wa kiroho.
5. upekee wa kuwa mshauri wa kichungaji ni
kuwa ni lazima angalau uwe na ujuzi wa kitheolojia na Saikolojia, kwani
mchungaji sio tu kuwa ni mshauri wa kawaida anaye shauri kwa kutumia mbinu za
kiushauri tu lakini anakuwa ni msomi mwenye ujuzi wa falsafa, elimu kuhusu
Mungu, maadili, ujuzi wa kibiblia, historia ya kanisa na dini za ulimwengu kwa
msingi huo ana elimu pana zaidi inayoweza kumpa uwezo mpana katika kushauri
7. Hali ya kutokuweko
kwa Malipo ushauri wa
kichungaji ni ushauri unaotolewa bure tu pasipo malipo faida yake ni kuwa
inaruhusu mtui awaye yote hata masikini asiye na uwezo anaweza kumuona
mchungaji hata bila ya kusubiri kwa siku kadhaa au wakati mwinguine hata pasipo
mapatano maalumu appointment
SOMO LA NNE:
WATU TUNAOWASHAURI
A. Maelezo;
Msingi mkubwa wa somo hili ni kukusaidia wewe
kufahamu zaidi watu kwa ujumla na hatimaye mtu utakayekuwa unamfanyia ushauri,
Lengo la ushauri ni kumfanya mtu awe katika hali yake ya kawaida na kuweza
kuchukuliana na mazingira yake katika hali iwayyo yote lengo la kushauri sio
kuwa fanya watu wote wafanane hapana lakini ni kutunza utu huku ukimsaidia mtu
huyo kuishi kwa ajili ya mungu kwa usahii zaidi.
Kuna mambo ambayo ni ya msingi yanayoweza
kuwafanya binadamu wote wafanane au wasifanane mmoja wa wanasaikolojia maarufu
alisema
·
Kila mtu ni
kama mtu mwingine
·
Kila mtu ni
kama watu wengine
·
Kila mtu si
kama kila mtu au watu wengine
Kwa sababu kila mtu kwa mfano ni mwanadamu na
kwamba Yesu alikufa kwa ajili yake kwa msingi huo tunaweza kuwa na kanuni
ambazo zinafanana na kanuni kwa watu wengine lakini si kila wakati, na tunaweza
kutatua matatizo kwa kutumia kanuni ya msingi inayolingana lakini pia sio kila
wakati, lakini wakati wote ni muhimu kujikumbusha wenyewe kwamba si kila watu
wawili wanaweza kuwa sawa kabisa na kuwa lazima tuheshimu kila mmoja kama mtu
tofauti.
B. Utu wa mtu
Binafsi
Kwa ujumla
utu wa mtu binafsi ndio unaomfanya kila mtu kuwa tofauti kutoka mtu mmoja na
mtu mwingine utu huo wa mtu unatofautiana katika mazingira yafuatayo
·
Tofauti ya
kiakili
·
Tofauti za
kimwili
·
Tofauti za
kitabia
Mambo hayo
matatu muhimu hapo juu ndio yanayoamua Kuweko kwa tofauti za msingi nne
zifuatazo
Tofauti za
msingi nne
1. Tofauti za kurithi
Kila
binadamu ana tofauti zake za kurithi ambazo kwa kawaida huanza mara tu baada ya
kutungwa mimba tofauti hizi huamuliwa na chromosomes
na genes yaani Kromoson na jins, hizi ndizo zinazoamua mtu awe mwanamume au
mwanamke awe na rangi gani na macho ya nmna gani, urefu gani na aina ya mwili, akili,
aina Fulani za uwezo na vipawahivi vyote huamuliwa na GENES
-
Hizi ndizo
tofauti za kurithi zinazoweza kusababisha kuweko kwa hisia tofauti kwa njia
tofauti kwa mfano
·
Kama kijana
mfupi sana aliandamana na marafiki ambao wana urefu wa kawaida anaweza
akajikuta anachekwa au kudharauliwa na kutaniwa
au kukataliwa
·
Na wakati
msichana anapoishi katika jamii ambayo wanawake ni wachache ni warefu nay eye
pakee ni mrefu sana anaweza kuepukwa na watu na akaonekana sio mwenye kuvutia
kwa vijana
2. Tofauti za
ukuaji
Ukuaji ni moja ya tofauti ambazo nazo ni
sehemu ya urithi ni maswala ya kuzaliwa yaani hili linahusu maeneo mbalimbali
ya ukomavu na makuzi hii ni kuanzia aina ya meno, utembeaji wetu wa upesi au
kuchelewa kutembea,usomaji,sauti ya kivulana wakati wa kukua, ukuaji wa
mwanamke na kubalehe kwao yote huamuliwa na tofauti za ukuaji zinazotokana na
kurithi
3. Tofauti za
kujifunza
Tabia ya mwanadamu piua huathiriwa na namna
anavyojifunza, kujifunza ni kubadilika na kunabadilisha tabia nba mwenendo
kulingana na namna tunavyoyafanyia kazi yale tuliyojifunza kuna falsafa mbili
za nman ya kujifunza
a.
Drive-Reduction
theory wazo hili linaamini kwamba kila tendo linalotokea la kitabia hasa
litokanalo na misukumo yaani maswala ya kiu ya maji, Chakula, na hewa yanaweza
kupungua au kutoshelezwa kwa tabia ya kujirudia rudia, yaani mambo haya mtu
anajifunza kupitia kurudiarudia tendo Fulani linalokamilisha hitaji hii ndio
maana mtoto hujifunza kunyonya tena na tena.
b.
Reinforcement
theory wazo hili ni imani ya kuwa kama tendo fulani linaambatana na hisia
nzuri basi muhusika ataendelea kulifanya tendo hilo hii inaitwa kuendeleza
tabia chanya
Lakini kama mtu huyo atafanya
tendo Fulani likaambatana na maumivu mtu huyo ataacha kufanya tendo hili hii
inaitwa kuendeleza tabia hasi
Kwa mfano;-
i.
Kama mtoto
anapochukua hatua ya kwanza akasifiwa kwa kujaribu kutembea na kuimbiwa basi
atajaribu tena na tena kutembea na kujenga tabia chanya katika kutembea
ii.
Kama mtoto
atagusa jiko la moto na akaungua basi ataogopa kugusa tena kwa sababu ameungua
na hivyo kuendeleza tabia hasi
4.
Mambo
mengine yanayoendeleza tabiia ni pamoja na
1.
Tabia
ya kuambukizwa INTERNALIZED VALUES hii ni hali inayotokea tunapoambatana na
mtu na kumpa uthamani Fulani bila kutumia akili tunaambukizwa tabia zake mambo
anayoyapa uthamani na anayo yapendelea
2.
Kuchukuliana
au kutokuchukuliana CONFORMITY AND NON-CONFORMITY halii hii hutokea kwa
mfano mtoto au kujana anapokuwa anakubalika au kutokukubalika katika jamii kwa
sababu kadhaa kwa mfano labda ni mbunifu na hufanya mambo vema kuliko jamii
anayoishi sasa ili akubalike na jamii ambayo inaishi chini ya kiwango anaanza
kufanya kama kila mtu wa eneo hilo anavyofanya ili akubalike na jamii au
anaweza kuiasi jamii hiyo na kutokuchukuliana nayo.
3.
Tatizo
la kutokujitambua IDENTITY CRISIS Baadhi ya watu wanashindwa kabisa
kujitambua kuwa wao ni nani kwa sababu ya tatizo la kushindwa kujitambua na kwa
sababu hiyo wanaweza kutumia miaka mingi wakibadilisha uthamani wa mambo hii
huwapata sana vijana anaweza kujiingiza katika makundi au kujiunga na kundi linguine tofauti
akijaribu kujijibu swali yeye ni nani na anapaswa kufanya nini ?
Mtu anastawisha utu wake vema baada ya
kujitambua na kujijua kuwa yeye ni nani na ni nini anapaswa kukifanya
Kanisani mara nyingi tatizo la kutojitambua
linaweza kubainika wakati mtu anapofikia hatua ya kuchagua mchumba, au wakati
wa kufanya uamuzi fulani, wakati wa kuhudumu na hata wakati wa kuamua namna ya
kumtumikia Mungu, wapi na jinsi gani wakati huu utaweza kuona kuwa huenda
wazazi wake walikuwa na mpango mwingine tofauti kabisa na ule aliouchagua
matatizo kama ya usagaji na ushoga wakati mwingine pia hutokana na hali ya
tatizo la kutojitambua.
4.
Ndoto
iliyovunjika BLOCKED MOTIVATION hakuna
mwanadamu awaye yote anayeweza kufanya
jambo bila kusukumwa na nguvu fulani ya uhitaji kuna nguvu za aina hizo mbili mahitaji
ya kimwili nay a kisaikolijia mahitaji ya kimwili hujumuisha hewa, chakula, maji,
na kwenda haja.
Mahitaji ya
kisaikolojia ni pamoja na
a.
Kuhitaji
muitikio mfano kama ukiwapenda watu unatarajia nao watarudisha upendo kwako
b.
Kuhitaji
kutambuliwa kila binadamu anahitajim kutambuliwa kama hujaliwi unajiona hufai
au mahali usipojaliwa hapakufai
c.
Kuhitaji
usalama hili ni hitaji la vyote kimwili na kisaikolojia kila mtu anahitaji
usalama hususani unaotokana na jamii husika unayoishi
Sasa inapotokea kuwa ndoto hizo za kimsukumo
zinavunjwa kunakuweko matokeo mfano kama mtu amepata pancha hamu yake itakuwa
ni kulikarabati tairi au kulibadilisha sasa wakati anajaribu kufanya hivyo na
vifaa vya kufanyia kazi hiyo vikawa havipo basi anakuwa na shauku au ndoto iliyovunjika
na hivyo kusababisha mgandamizo wa mawazo au msongo
5. Hali za
kujihami DEFENSE MECHANISMS
Katika hali ya kujaribu kuchukuliana na
hali ya kidhamiri hasa mwanadamu anapokuwa na ndoto iliyovunjwa au shauku
iliyokwazwa basi kutazaliwa hali za kujihami hali hizo za kujihami ni pamoja na
i.
Ndoto za mchana DAY DREAMING: mtu anapokuwa na ndoto ya mchana maana yake
ni kuwa akili zake au mawazo yake yana wayawaya anakuwa hayuko kanisani au
kazini au shuleni na anaanza kufikiria kuweko mahali pengine pasipokuwa na
shida ili kujipendezesha na kupata raha katika kufikiri kwake lakini tatizo
linakuja kuwa kufikiri kwake au kuwaza kwake hakuwezi kumsaidia kitu na
matatizo yake yanabakia kuwa kweli vilevile.
ii.
Hali ya kutafuta visingizio RATIONALIZATION: mtu anapokuwa na hali hii hutafuta
visingizio ili kujikidhi kisaikolojia kwa mfano mchungaji anaweza kuwa
anatamani kupewa kanisa Fulani kubwa ili aliongoze na anapokuwa hajateuliwa
yeye kuliongoza basi anaweza kusema “Ah! Hata hivyo hawako kiroho Pele”Hiki ni
kisingizio.
iii.
Kusukuma lawama kwa wengine PROJECTION; Mtu anweza kuwa na tatizo lakini akatafuta
kumsingizia mtu mwengine ili kukwepa kuwajibika kwa makosa yake mfano Mwanzo 3
adamu alilaumu kuwa Eva kuwa ndio chanzo cha tatizo na kasha Eva akamlaumu
Nyoka.
iv.
Kukandamiza wengine kwa ajili ya maslahi yako
COMPENSATION: hali hii hutokea
pale mwanadamu anapofanya jambo kwa ajili ya usalama wa maslahi yake tunaiyona
hali hii kwa Farisayo katika Luka 18;10-14 anajaribu kumponda mtoza ushuru na
kujiinua mwenyewe ili kujipendekeza kwa Mungu, watu wengi wenye tabia hii
hutaka kufanikiwa kwa kuumiza wengine kwa mfano meneja aliye mfupi anaweza kuwa
mkali sana,au mume asiye na elimu anaweza kuwa mkali samna kwa mkewe mwenye
elimu ili kuziba ufa wa tatizo lake
v.
Kujifichia au kujifananishia IDENTIFICATION: Hii ni tabia ya mwanadamu kukimbia hali
Fulani ya matatizo aliyo nayo kwa kukaa karibu na mtu mwenye hali nzuri au
maisha mazuri au cheo kizuri au tabia nzuri ili kufunika madhaifu aliyo nayo
anaweza kuwa yuko karibu sana na muhubiri mkubwa au mchungaji ili kuficha uovu
alionao au kuonyesha kuwa ni rafiki wa mkubwa Fulani au mtoto wa raisi
vi.
Kukanusha DENIAL; Katika hali hii mwanadamu anakanusha kabisa
kwamba ana tatizo au amekosea anakubali kujidanganya mwenyewe kuwa hakuna kitu
kilichotokea kwangu.
vii.
Kutafuta sifa ATTENTION-GETTING: Hii ni jamii ya watu wanaojaribu kutafuta
sifa na kuvuta hisia za watu kuwaelekea marko 12;38-40 mafarisayo walivaa
mavazi marefu sana , au kusalimia kwa upendo na kusali sala ndefu sana na kuketi katika masinagogi na masokoni ili
waonekane na watu kuwa ni watu wema sana kwa watoto ili aweze kusikika hutumia
njia ya kulia na kusagasaga miguu ili watu wahusike nay eye zaidi, wengine
huchelewa ibada na kuingia na kiatu kirefu sana chenye mlio ili watu waone
anavyoingia, makahaba huitumia hii kwa kuvaa nguo maalumu zenye mvuto wa
kuonyesha mapaja, makalio au mahips waliyo nayo kwa lengo la kuwapata wanaume
n,k
viii.
Kutafuta makosa na kukosoa NEGATIVISM: Ni hali ya kutafuta makosa kwa watu na
kuzungumza kwa hali ya kutafuta kuwadhuru au kuwakosoa kinyume na watu au vitu,
yaani hawa kila kitu kwao hakiko salama
ix.
Enzi ya zilipendwa REGRESSION: Hii ni hali ya watu kujaribu kurudi nyuma na
kukumbuka enzi hizo au wakati wa ujana au utoto katika maisha yao ambapo
walifurahia maisha kwa hivyo katika kanisa utawasikia watu wakisema “enzi zile
bwana” hili ni tatizo la kisaikolojia la
kujilinda kinyume na hali halisi ambayo kwayo inatutaka tusonge mbele kwa
maswala ya mkondo ulioko
x.
Kukandamiza
REPRESSION: Ni hali ya kukandamiza chini hasa hali zozote zenye kuumiza, za
huko nyuma au za karibuni hali hii hutokea bila kukusudia na ingawaje
kumbukumbu za jambo hilo zinabakia pale pale na bado zinatuudhi.kwa wahubiri
wengi hujikuta wakikemea hali hizo hata katika mahubiri yao kwa nguvu sana
kumbe wamekandamiza hali zao wenyewe wakati mwingine.
xi.
Kuhamisha matatizo kwa wengine DISPLACED
AGGRESSION: Hali hii
hutokea hata kwa kupiga au kudhuru mtu aliyekukosea na inapotokea kuwa hatuwezi
kumduru mtu huyo aliyetusababishia matatizo kama bosi au rafiki au wazazi basi
tatizo hilo linahamishiwa kwa mwengine, kama umekemewa kazini na Bosi basi
unamalizia hasira zako nyumbani kwa mkeo na mke naye anahamishia kwa mtoto na
mtoto anamalizia kwa paka na hivo paka anakuwa na wakati mgumu
C.
Hitimisho
1.
Ili kuwa wazi kabisa ni muhimu kufahamu
hususani sisi washauri kuwa wanadamu wanatofautiana kabisa katika hali na utu
kila tukio linaweza kutubadilisha katika hali Fulani kwa hiyo utu ni hali tete
inayoweza kubadilika wakati wowote
2.
Hali hizo hapo juu zinamsaidia mshauri
kujua kitu Fulani kuhusu Yule anayemsahuri na utu wake ili kumsaidia katika hali kubwa mbili
a.
Kufikia
hatima yaani kukupa mwanga kuwa mshauriwa anaweza kuwa anapitia hali ya namna
gani ili kwamba kwa msaada wa Mungu na maongozi haya kumfikisha panapohusika
b.
Kuchukuliana yaani kukupa mwanga jinsi gani mshauriwa
anaweza kuchukuliana na hali halisi iliyoytukia katika maisha , kwa mfano kifo
cha mpenzi aliye karibu na hivyo kumfanya hata kama amehuzunika sana bado aweze
kuchukuliana na ukweli kuwa mwenzi wake hayuko naye kimwili tu lakini ameenda
kukaa na Bwana 1Koritho 5;8 na hali hii ya kuweza kuchukuliana pia inaweza kuwa
tofauti kati ya mtu na mtu
SOMO LA
TANO: MBINU ZA KUFANYA USHAURI
1.
Stawisha uhusiano; ESTABLISHING A RELATIONSHIP.
-
Ushauri wa
kichungaji wenye mafanikio siku zote unategemea jambo moja kubwa ni kustawisha
uhusiano kati ya mashauri na mshauriwa lazima kuweko na upendo wa kimungu Agape
na kukubalika hzi ndio funguo za kifundi katika maswala ya ushauri na mbinu
zake.
-
Uhusiano
kati ya mshauri na watu wengine lazima uongozwe na upendo wa kimungu agape, ambao
ni upoendo unaotokana na nguvu za kimungu za kupenda hata kile kisichopendeka
bila sababu.
-
Mshauri pia
lazima awe mwenye kukubalika na
kuaminika kwa watu wengine akikubalika
pia kupitia tabia zake ni hiyari kumruhusu mtu kuwa tofauti kwa njia iwayo
yote, Kukubalika kunahusisha pia swala zima la kuheshimu kila mtu yaani kama
mtu amezaliwa mara ya pili tutamuhesabu kuwa ndugu katika Bwana, na kama
hajazaliwa mara ua pili tutamuhesabu kama mmoja wa watu ambao Yesu alikufa kwa
ajili yao
-
Ni muhimu
kufahamu kuwa kama humkubali mshauriwa wanakuwa na uwezo wa kujua au kuhisi
kuwa hakubaliki na atahisi kupwekeka na kutokujihusisha na kutokujaliwa na
mshauri kwa msingi huo kujali ni muhimu sana.
2.
Stawisha
mazingira yenye kufariji; ESTABLISHING RAPPORT.
-
Neno rapport
maana yake ni faraja, katika maswala ya ushauri ni lazima ustawishe mazingira
yanayoleta ujasiri na faraja kwa kawaida
mshauriwa hupenda mtu na eneo ambalo anajisikia amani na hivyo inamsaidia kuwa wazi na kujiamini
machoni pa mshauri
-
Amani hiyo
inapatikana kutokana na muda muafaka uliopangiliwa kwa maswala ya mashauri na
matumizi ya sauti hususani kwa mjadala wa mara ya kwanza mazingira hayo
yataamua ni namna gani utaweza kufanikiwa kulingana na mtu husika.
-
Baadhi ya
maswala yanayoweza kusaidia katika kustawisha mazingira mazuri ya ushauri ni
pamoja na ;-
Ø
Onyesha
uaminifu jambo ambalo linaweza kusomeka katika uso wako
Ø
Anza wakati
mwingine na mazungumzo ya taratibu yanayoweza kumfanya mshauriwa kujisikia
salama mfano unaweza kumsifia kuwa unaonekana smart sana leo, au unafikirije
kuhusu radii le ya usiku wa leo, na vinginevyo
Ø
Pia unaweza
kuzungumzia swala ambalo unajua kuwa linamvutia sana mshauriwa kama maswala ya
siasa na kadhalika.
-
Kumbuka
kuangalia alama bubu za mshauriwa non vebal cues yaani alama ya uso wa mshauriwa
kama anaonekana kuwa na huzuni,au mchangamfu,mkao wake katika kiti na pia kama
kuna ishara za kuumizwa
-
Wakati
mwingine unaweza kuanza na kile
unachofikiri kuwa ndio tatizo njia hii inaitwa “Shock approach” njia ya
kustukiza kwa mfano unaweza kumwambia
umekasirika sana leo,Hebu tuzungumze ni kwa nini unaonekana hivyo leo n.k.
Mifano ya kibiblia ya mazingira ya amani ya
kiushauri
Ø
Yesu
alistawisha mazingira ya amani ili kuzungumza na mwanamke msamaria Yohana
4;7-15 alianzia na swala la kutaka maji swala ambalo msahauriwa ndio alikuwa na
lengo nalo
3. Stawisha hali ya kuchukuliana; SUSTAINING
EMPATHY
-
Hali ya
kuchukuliana na tatizo Emphathy ni hali ya ndani sana ya kuliona tatizo la
muhusika kama tatizo lako, kuna usemi unaosema kuvaa kiatu cha mwingine au
o
kuona kama yeye anavyoona
o
Au ni hali
ya kuliona tatizo la muhusika kama tatizo lako ni hali ya
o
Kuhurumia na
kusukumwa na pendo la kweli kuhusu tatizo la mwingine
-
Mshauri
anayejali hujihusisha sana na tatizo la msahauriwa yaani anakuwa tayari kwa
muda kuyaachia maisha yake kwa ajili kufikiri maswala ya wengine na hii sio
hali ya kuigiza lazima uwe mkweli na mwaminifu kwani mshauriwa ataona mwanga
kupitia wewe, unatakiwa kutenda na kuhisi kana kwamba tatizo analolipitia
mwengine ni kana kwamba ni la kwako, usijaribu kuigiza jambo hili na usijali
matatizo yako.
-
Mwitikio wa
mshauri kivitendo kwa maneno na kwa ishara bubu vinawasilisha ujumbe kwa
unayemshauri iwe ni wenye kukubaliana naye au ulio kinyume naye na yote
yatakubaliana na hisia zake
-
Huruma za
Bwana yesu zilionekana alipokufa Lazaro Yohana 11; 33-36 na alipomuona mama
mjane aliyefiwa na mwanaye Luka 7; 11-17.
4. Stawisha hali ya kuuliza maswali; QUESTIONING
TECHNIQUES.
-
Moja ya njia za muhimu Sana za kumsaidia mshauri na mshsuriwa ni
kustawisha hali ya kuuliza maswali na ziko namna mbili kuu za kuuliza maswali
i.
Maswali mepesi kwa ajili ya kupata taarifa simple-Information question - mfano unatokea wapi,mumeo anaitwa nani, unafanya kazi wapi na kadhalika
ii.
Maswali ya kufungua yaliyofichika kwa ajili ya kutatua tatizo Open-end” question – Kwa mfano unafikiria nini
sasa juu ya hili, je unaweza kurudia tena namna ambavyo utamwambia? Kusudi
kubwa la maswali namba mbili ni kumfanya mshauriwa ajieleze mwenyewe ili kwamba
uweze kumfahamu vema au kumsaidia kufumua vitu na kujitambua
5.
Stawisha hali za kujadili pamoja ; THE INTERVIEW
-
Namna ya kustawisha mijadala
a. Mahali
(Location).Ushauru unaweza kufanyika mahali popote mahali pa siri ndipo pa
muhimu zaidi, ni muhimu kutafuta mahali ambapo kuna utulivu na ambapo
hapaytakuwa na mwingiliano, kiti pia ni lazima kiwe chenya kumfanya mshauriwa
kujisikia salama na mahali hapo pasiwe na picha zenye mvuto.
b. Tabia ya Mshauri au
mtazamo (Counselor’s Attitude) Mshauri
mwenyewe ni mtu wa muhimu sana na sehemu
muhimu sana ya ushauri,kama msahuri mwenyewe anajiweka katika hali ambazo
zinamfanya mshauriwa ajisikie kutokukubalika au kutokujaliwa mshauriwa anaweza
asijisikie vema
-
Vikwazo vya kustawisha mijadala.
1. Njia unayoitumia-
Unaposisitiza matumizi ya mbinu fulani zaidi itumike kuliko au kukazia mambo
fulani kunaweza kusababisha kutokuweko kwa usikivu na hatimaye kuvunja
mawasiliano, kwa msingi huo ni muhimu kukumbuka kuwa njia za mawasiliano ziko
kwa ajili ya kutusaidia tu katika maswala ya ushauri ili uweze kufanyika vema
na kwa sababu hiyo tunahitaji kujifunza kwa undani zaidi ili kwamba hatimaye
ziweze kuwemo ndani yetu kwa kusudi la kuwasaidia watu na sio kuonyesha kuwa
sasa ndo tunazitumia hususani wakati wa kufanya ushauri
2. Usijaribu kutafuta
suluhu mapema jambo hilin kitaalamu tunaliita Pre-mature seeking of solutions usijaribu kujionyesha kuwa una
majibu tayari ya tatizo la mtu hii ndio shida ya wachungaji wengi wanaposikia
shida ya mtu hujaribu kuyatumia maandiko mapema ili kusuluhisha tatizo kabla ya
kuwa amemsikiliza mshauriwa na kuhakikisha kuwa je anaweza kubeba hali yake na
kuchukuliana na hali yake.
3. Usionyeshe kushangaa hali hii inaweza
kusababisha mshauriwa kutokuwa makini kujisikilizia kihisia na hata wewe kumsikiliza
vizuri unayemshauri hali hii kwa kawaida inaweza kuondoa usikivu na hisia za
mshauri kujihusisha na hisia za mshauriwa kwa msingi huo ni muhimu sana
kusikiliza kwani ndiko kutakakokuongoza katika kuelewa vema.
4. Jihadhari na maneno au maswali kwanini aina
hii ya maswali katika mjadala inaweza kumfanya mshauriwa kujiondoa katika
kuelekea kujibu maswali kwa sababu inaweza kusababisha aijibu maswali ya aina
hiyo kwani swali kwanini limekuwa likitumika kwaajili ya kuhukumu kwa muda wote
wa maisha kwa hivyo mshauriwa anaweza kudhani kuwa anahukumiwa kwa msingi huo
ni muhimu sana kujihadhari na maswali
i.
Kwanini
ulimpiga mkeo?
ii.
Kwanini
hukukabidhi ile kazi?
iii.
Kwanini
hukufika kanisani kwa siku zote hizo tatu?
-
AINA ZA
MWITIKIO WA MSHAURI WAKATI WA KUFANYA MJADALA.(FATUKA)
Zifuatazo ni
aina tano za mwitikio ambazo zinaweza kuwakilishwa na msahuri wakati wa kazi ya
kushauri
i.
Fanya
tathimini - jaribu kuanza kumuonyesha unayemshauri kama ambaye unampeleka
katika kukubali hitimisho la shida yake kwa mfano unaweza kuanza kumshauri kwa
maneno kama Hili no wazo zuri sana, au huu ni mwanzo mzuri, au Biblia inasema
kuwa jambo hilo ni dhambi,au hivyo haikupaswa kufanyika au natarajia utaonyesha
mabadiliko
ii.
Anza
kutafasiri mambo - kwa mfano Mwitikio unaoonyesha kutaka kufundisha au mtu
kufafanua jambo kwa nguvu ili kubadilisha tabia Fulani badala ya kuuliza swali
kwanini unaweza kutengeneza sentesi isemayo Inaonekana unataka kusema kuwa…, au
Inaonekana unategemea kuwa…
iii.
Tumia uwezo
wa kutegemeza – Hapa mshauri anapaswa kuanza kumuinua mshauriwa, kwa kumtia
moyo ili ushauri uweze kueleweka na mshauriwa aweze kuwa na uhakika au
kuchochewa, hapa unaweza kutumia misemo kama Oh! Watu wengi hupatwa na mambo
kama hayo, au naamini watakuelewa, au mambo yatakuwa mazuri
iv.
Uliza maswali
yenye lengo la kufanya uchunguzi zaidi kwa mfano Je mkeo analichukuliaje hili?
Na ilikuwaje baada ya hapo? Ahaa! Ok! Sijui kama nimekuelewa vema, Hebu nifafanulie
zaidi swala hili.
v.
Kuwa na
uelewa hii ni hali ya kuwa na ufahamu unaotaka kuonyesha kuwa una mwitikio na
kuwa unamuhurumia mshauriwa na hapa unaweza kutumia misemo kama hii inaweza
kuwa ni ngumu sana …au kwa hiyo umesema , kwa kweli ulikuwa na wakati mgumu
sana mtu mmwingine asingeweza!.
vi.
Anza kutoa
ushauri hii hutokea baada ya kuwa umemsoma
na kumuelewa mshauriwa kuwa anafikiri ni jambo gani linaweza kujenga au
kuondoa tatizo kwa hiyo hapa utakuwa na semi kama mimi naona au hebu na mimi
nichangie kwa nini usijaribu kuzungumza
na mumeo kuhusu hisia zako n.k
Kwa msingi huo basi endapo
utakuwa umeitumia kanuni hiyo hapo juu (FATUKA).bsi utakuwa na nafasi nzuri ya
kuwa na uwezo wa kushauri kulingana na tatizo husika
-
Namna ya
kuandaa mjadala STRUCTURING INTERVIEWS
o Kuandaa mjadala
kunajumuisha
1. Jiandae kuwa na ujuzi
wa tatizo la mteja wako
2. Amua kama mshauriwa
anaweza kurudi kwa ajili ya ushauri
3. Amua namna ya
ratiba ya mjadala na muda utakaotumika
4. Weka mazingira
yenye uhakika kwa mshauriwa kuwa mazungumzo yenu yatakuwa siri yenu
5. Fafanua kanuni za
kuonyesha ushirikiano na ile kweli kuwa anawajibika kuwa muwazi kwa faida yake
6. Na mdhihirishie
kuwa hakuna tiba ya kichawi inayoweza kuleta suluhu ya matatizo yake isipokuwa
kuyakabili
6. Stawisha hali ya usalama wa kihisia EMOTIONAL CATHARSIS.
-
Usalama wa kihisia ni hali ya kumfanya mshuriwa kujiachia kuwa huru na
kuweza kuachilia hisia zake ili kusafisha akili inasemekana moja ya mambo
muhimu sana katika kufanya ushauri ni pamoja kumuachilia mtu kuwa wazi kimawazo
na kihisia kuzunguka tatizo alilo nalo hii inaponya kutoka katika shida binafsi
individual conflicts.
-
Hali ya mtu kujiachia kihisia inatokea tu pale kunapokuwa na mazingira
mazuri yanayoruhusu mshauriwa kujiachia kihisia na mshauri kuichochea hali ya
kumfanya ajiachie kihisia hili linaweza kufanyika mahali salama na hapa mtu
atajisikia huru kuzungumza na kujiachia kihisia Hapa mshauriwa anweza hata kulia machozi kwa sauti kubwa bila
kuhofia kusikiwa na watu na kujieleza kwa uhuru
Matokeo
mazuri ya ya usalama wa kihisia POSITIVE OUTCOMES OF EMOTIONAL CATHARSIS
-
Mtu
anapojiachia kihisia anaondoa sumu ya maumivu yaliyoumiza nafsi ya mtu hali ya
kujiachia kihisia inaondoa hali ya kupooza, kukata tama na inakuwa ni msaada wa
ndani wa kuondoa hukumu na matatizo ambayo hayangeweza kutibika
SOMO LA
SITA: AINA MBALIMBALI ZA USHAURI
1. Ushauri wenye kutia moyo; SUPPORTIVE COUNSELING
-
Lengo kuu , Lengo kuu la ushauri wenye kutia moyo ni pamoja na kumsaidia mshauriwa katika
maisha yake ya kila siku na hivyo
mchungaji atatumia njia inayoongoza ,inayolea inayotia nguvu hata wakati wa
matatizo
Ø
Kuongoza –
ni kumpeleka mtu katika uelekeo ulio sahii, ni kumuonyesha njia
Ø
Kulea – Ni
kuonyesha kujali na kujihusisha na maisha ya kila siku ya mshauriwa
Ø
Kutia nguvu
– ni kumfanya mtu aimarike
Ø
Kuhamasiha –
ni kumfanya mtu atende katika hali Fulani
Ø
Kuhakikishia
– ni kumuwekea mtu hali yenye usalama.
A.
Njia ya kufanya ushauri wenye kutia nguvu METHODS OF SUPPORTIVE COUNSELING
1.
Tengeneza mazingira ya kufariji, Gratifying Dependency Needs kutia
moyo kulisha, kuhamasisha kuongoza, kufundisha na kuweka mipaka
2. Tengeneza
mazingira ambayo mshauriwa atakuwa na uwezo wa kujieleza Emotional Catharsis kiasi cha
kuweka matatizo yake nje akiamini kuwa kuna usalama
3.
Ni muhimu
kiufahamu mtu huyo ameumizwa kiasi gani Objective Review of the stress
situation Mtu aliyeumizwa anakuwa
karibu sana na tatizo alilo nalo kuliko kawaida na hivyo anashindwa kuielewa
hali yake kuwa iko vipi na kujisahiisha kwani anaiona kwa ndani yeye
mwenyewe kwa hivyo mshauri yuko pale ili
kumsaidia kuona uhalisi wa mambo wazi na kuona uzito wake katika namna inayofaa
4.
Hudumia hali
ya kujilinda nafsi Aiding the Ego Defenses: mwanadamu anapokuwa anapitia
hali Fulani ngumu akili zake zinajiandaa kujilinda lakini kujilinda huko sio
sababu ya kupata suluhisho la kudumu baadhi ya hali za kujilinda huwa
zinahitajika kwa ajili ya kutatua matatizo ya ghafla na mchungaji anapaswa
kumsaidia muhusika kuchukuliana na
tatizo na kumpa muda wa kuondoka katika mshituko kisha kushughulika naye
baadaye badala ya kumshambulia mara nyingi watu wengi wanapokuwa wametoka
katika hali za kujilinda kwa sababu ya mshituko wanarudi katika hali ya
kawaida na kutambua tatizo lao na kisha
kukubali kuwajibika na kubeba hatia na hapa ndipo ambapo mchungaji sasa anaweza
kuwajibika kumjenga muhusika na kushughulikia tatizo lake
5.
Kubadilisha
hali halisi ya maisha Changing Life Situation msaada wa kivitendo
unaweza kutolewa na mchungaji kama sehemu ya ushauri ni pamoja na kumsaidia
muhusika, aidha kupata kazi au kusaidia kupatikana kwa makazi ya muhusika na
familia yake na kutoa msaada wenye kujenga.
6.
Tia moyo
hali ya kuchukua hatua mahususi Encouraging Appropriate Action: wakati
mwingine mtu anpopatwa na tatizo kunakuweko hali ya kupooza na kushindwa,kuanguka
na kujidhuru au kujiua ni wajibu wa mchungaji basi kuwapa baadhi ya watu jukumu
la kushughulika na muhusika ili kustawisha uhusiano na mtu huyo na kumfanya
asijisikie mpweke au aliyetengwa njia hii huitwa kitaalamu Action Therapy hapa
kinachofanyika ni kumfanya mshauriwa atende wakati njia ya kjuu inataka mshauri
atende
7.
Tumia vyanzo
vya kidini Using Religious/Spiritual Resources hapa inahusisha maswala
ya maombezi, kujitoa, kufundisha na vijarida au tracts maandiko njia za kutia
moyo na ushauri wa kichungaji.
B.
Aina za
ushauri wenye kutia nguvu TYPES OF SUPPORTIVE COUNSELING
Ø
Ushauri wa
kushughulika na mgogoro CRISIS COUNSELING
Hu ni ushauri wa kushughulika na
matatizo yanayojitokeza katika maisha ya kila siku kivitendo bila kutarajia au
katika namna isiyopendeza na ambayo hali zetu za kujilinda zinakuwa bado hazija
jiandaa na kama mgogoro au tatizo ni kubwa au baya sana hisia zinakuwa kali
sana na hali ya kukosa faraja kwa namna isiyotegemewa hujitokeza na wakati
mwingine hata tatizo la ugonjwa mkubwa unaweza kutokea.
Kuna aina kuu mbili za matatizo
ya Kimgogoro.
a. Mgogoro
endelevu DEVELOPMENTAL CRISES
Migogoro hii ni ya kawaida na hutokea kwa
mtu awaye yote kadiri tunavyokua, ni migogoro inayojumuisha namna tulivyozaliwa,
tunavyoishi nyumbani, tunavyokwenda masomoni, tunavyochumbia, maswala ya ndoa,
maswala ya ujauzito, namna ya malezi, miaka ya ujanani, kufiwa na wazazi,
kustaafu, kifo cha umpendaye, haya yote yanaweza kusababisha migogoro ambayo
inaweza kusababisha hali zetu za kuweza kubeba au kuchukuliana kuathiriwa
b. Migogoro
inayotokea kama ajali ACCIDENTAL CRISES
Hii ni
migogoro inayojitokeza katika hali isiyo ya kawaida na katika hali isiyoweza
kutegemewa na kwa kawaida hutokea pale
mtu anapopoteza kile ambacho kwake ni
cha muhimu sana au anaamini ni chanzo kwa utoshelevu wake, hii inaweza kuwa
kupoteza kazi, kupoteza fedha, kuvunjiwa heshima, au kupata ajali au matukio ya
vita na maswala ya ukimbizi
Mchungaji
kama mshauri ambaye yuko makini kwa mahitaji ya watu waqliosumbuka na matatizo
ya aina mbalimbali atachukua muda mwingi kushughulika na migogoro hii ya
kimaisha iliyojitokeza na kutoa ushauri
Njia zisizo za kiafya za kuchukuliana na
Migogoro ya kimaisha.
i.
Kukataa
tatizo lililojitokeza Denial that a problem exist
ii.
Kukataa au
kujaribu kufunika tatizo kwa nia mbadala kama vile kunywa sana Pombe
iii.
Kukataa
kutafuta au kukubali Kusaidiwa
iv.
Kushindwa
kujielezea au kuona kinyume cha hali halisi Inability to express or master
negative feelings
iv.
Kushindwa
kulifanyia au kulipitia au kutafuta chanzo cha tatizo
v.
Kushindwa
kutafuta suluhu
vi.
Kutafuta
visingizio, kukwepa kuwajibika au kumalizia hasira kwa wengine
vii.
Kujitenga na
marafiki aun kwenda mbali na familia
Mshauri anayeshughulika na
migogoro anapaswa kuwa makini na
kujihadhari na kudhuriwa au kuumuzwa kamamatokeo ya kushughulika na hali
halisiya muathirika kwa msingi huo ili kumsaidia unaweza kuwa mbali na muhusika
na kuanza kutumia njia bora za kuweza kuchukuliana na migogoro katika njia
zilizo za kiafya za kuchukuliana na mgogoro.
Njia zilizo za kiafya za kuchukuliana na
mgogoro ya kimaisha
i.
Kukubali
kukabiliana na tatizo
ii.
Kukubali
kupanua ufahamu wa mtu mwenye tatizo mfano 1Thesalonike 3;13-18
iii.
Kujieleza na
kuzifanyia kazi mawazo yaliyokinyume na ghisia kama njia ya kukubali hatia na
kujirekebisha
iv.
Kuwajibika
kuchukuliana na tatizo Daniel 9;4-11
v.
Kujaribu
kutafuta njia za kulibeba tatizo na kuchukuliana nalo
vi.
Kutenganisha
kinachobadilika na kisichobadilika
vii.
Kukubali
kuwa umeshindwa na kukubali kuchukuliana na mzigo huo na kujiona mwenyewe
kujichunguza
viii.
Kufungua
njia za kuwasiliana na wengine miongoni mwa ndugu jamaa au marafiki au watu
wanaoweza kutoa msaada wa kitaalamu Yakobo 5;14
ix.
Kuchukua
hatua hata kama ni ndogo katika kushughulika na tatizo kwa namna ya kuhakikisha
kuwa unajenga
Uzuri
wa nia bora za kushughulika na mgogoro
Ni muhimu kufahamu kuwa migogoro hii ya
kimaisha ni rahisi lakini ni hatari ina maumivu ina migandamizo,haibebeki na
lakini inabadilisha tabia zetu na utu wetu na inatusaidia kukua na kumpelekea
mtu kuwa na hatua kubwa za uvumilivu na nguvu yakobo 1;3-4,warumi 5;3-4.
Ø
Vunja kizuizi cha kufanya ushauri STOP GAP
COUNSELING
Jambo hili linahusiha swala zima la kutumia
njia za kumtia nguvu mshauriwa aliyesumbuliwa mpaka afikie hatua ya kukaa sawa,
Kwa bahati mbaya wachungaji wengi wanafikiri kuwa kumsaidia mtu ni mpaka
akubaliane na tatizo lakini ukweli ni kuwa wachungaji wengi hawana muda katika
huduma zao za kichungaji na kwa sababu hiyo wanasisitiza jambo lifanyike tu kwa
maslahi ya faida zao wanashidwa kuwa na muda wa kutafuta kujua matatizo ya
ndani sana ya jamii zao ili kwamba wajishughulishe kutatua au hata kujifunza
kutoka kwa wataalamu wa maswala ya ushauri na watumishi wenzao ambao wangeweza
kuwasaidian hata mawazon Fulani ni namna gani wanaweza kubeba mizigo na
kuwasaidian wahusika wanaopatwa na shida na hivyo hujikuta wakiwa mbali na
wanaowashauri na kutokujua matatizo yao kwa undani.
Ø
Ushauri wenye kutianguvu ulio endelevu SUSTAINING COUNSELING
§
Ni uhsuri
ambao kwamba unaendeleza ushirikiano na mshauriwa ambao utachukua muda mrefu
kabala ya kuzungumza neye
§
Aina hii ya
ushauri imekuwa ikitumika na mtu ambaye ana hisia zisizo kali sana ambaye
haumizwi kwa haraka au mwenye tatizo sugu au mzee
§
Lengo la
aina hii ya ushauri ni kumtia nguvu mshauriwa na kumpatia namna mbalimbali za
kufanyia kazi hata kufikia kuwa katika hali yake ya kawaida
Ø
Ushauri wenye kuchochea ukuaji. SUPPORTIVE
GROWTH COUNSELING
§
Ni ushauri
wenye kuchochea hali ya ukuaji kwa kutumia mbinu za kisaikolojia kulingana na
maeneo ambayo mtu huyo amekulia au anaishi
§
Kwa mafano
kama una kundi la watu waliokomaa ambao wana tatizo kama la kwake basi kuna
mambo makuu matatu amabayo yanaweza kufanyika
-
Hali ya mtu
kuweza kuchukuliana na tatizo lake inachochewa anapokuwa nao
-
Hali ya
kutiwa moyo na wengine inamsaidia mshauriwa kuvunja hali ya kukata tama na kuwa
na uwezo wa kuchukuliana
na tatizo alilo nalo
-
Inamsaidia
muhusika kuondoa upweke
2. Ushauri
wenye kuelimisha EDUCATIVE COUNSELING
A. Maelezo;
Ushauri wenye kuelimisha ni ushauri unaojumusha
mawasilianao yenye aina Fulani ya maarifa au imani na njia mbalimbali za stadi
za kiushauri ndani ya shughuli nzima ya kufanya ushauri kama sehemu ya mchakato
wa kufanya ushauri kwenyewe.
Ushauri elimishi ni tofauti na aina nyingine za
ushauri kwa sababu unathamani ya kutoa elimu na ujuzi mkubwa wa kugundua tatizo
kutimiza malengo kuwasiliana na kusaidia
C.
Malengo ya ushauri Elimishi .THE
GOALS OF EDUCATIVE COUNSELING.
§ Kumfanya mshauriwa agundue Kweli,
apate wazo aone uthamani, aamini aongozeke ashughurike aelewe mahitaji ya ya
mtu nini mtu napenda na namna gani mtu naweza kuchukuliana na hali ya halisi ya
matatizo yake.
§ Kuwasilisha kweli moja kwa moja ni
kumsaidia mshauriwa kugundua kweli anazopaswa kuzifahamu hata kama ni kwa
kupitia kusoma n.k.
§ Kumsaidia mtu kuwasilisha taarifa
ili kusaidia uelewa na hii inapanua ufahamu wake na kumpa kufanya uamuzi wenye busara kukabiliana
na hali ngumu na zenye kujenga
§ Kwa ufupi hatua hii ina mambo ya
msingi katika swala la kugundua na kuwasiliana
na kutoa maarifa yanayohitajika kwa mshauriwa kusaidika kwa hekima
Mambo matano
ya kuwasiliana kuhusu mahitaji ya mshauriwa
1.
Mpe kweli na taarifa zinazomuhusu
2.
Mpe mawazo au ushauri na namna ya kufanya uamuzi ibaki kwake
3.
Mshauri kutumia vyanzo vinavyoweza kutumika na kumuhusu kulingana
na hali yake
4.
Msaidie kukutana na hali halisi.
5.
Mpe shuhuda zinazoweza kumtia nguvu kulingana na hali zake
D.
Hatari ya ushauri Elimishi DANGERS
OF EDUCATIVE COUNSELING.
§ Hatari ya kukubali kushawishika
kwa mshauriwa
Unapotoa ushauri unaoelimisha ni rahisi sana kutoa msukumo kwa
mshauriwa na kumsababishia kuchukua mawazo yako yatokanayo na ushawishi wa
msukumo huo na hivyo kuweza kumfanya achukue uamuzi ulio kinyume na matakwa
yake
§ Kunakuweko hatari ya kuikosea
mamlaka
Hatari hii ni ile inayoweza kusababishwa na kutoka katika kuwa
mwenye mamlaka kuelekea katika kutumia mamlaka yaani unaacha sehemu yako kama
mshauri na kuiingilia hali ya mshauriwa na kumuamuru kidikteta kwa ajili ya
ushawishi wako Yesu aliwafundisha watu akiwa Kama yeye aliye na mamlaka lakini
hakuwa dikteta Marko 1;22.
§ Taarifa zenye kuhukumu vibaya
Kuna hatari ya kufikiri kuwa taarifa pekee inaweza kutosheleza
kumfanya mshauriwa kukubali kirahisi rahisi kwa kufikiri labda kwa sababu
nimesema basi iatasaidia bila kujali kuwa ni wazo gani tumelitumia haijalishi
wazo hilo likoje na lina hekima kiasi gani ni muhimu kufahamu kuwa si sehemu ya
mshauriwa mpaka amelikubali wazo baada ya kulichuja na hatimaye kulikubali kwa
ajili yake.
§ Kutia moyo utegemezi.
Katika aina hii ya ushauri kuna uwezekano wa kumfanya mshauriwa
kuwa tegemezi katika maisha,ni kweli unaweza kumsaidia kiushauri yaani ni
ushauri wenye kutia moyo sana na wenye kuonyesha kujali hususani kwa watu wenye
migandamizo na tunarizishwa na hali zao tegemezi lakini hili linapoongoza
katika hali kubwa tegemezi Mchungaji anapaswa kujitoa taratibu katika aina hii
ya ushauri kwa kutoa ushauri wa aina nyingine wenye kuongoza kwenye
kujitegemea.
§ Hatari ya kuhukumu vibaya mafunzo
Kuna hatari
hatari ya kupeleka mafunzo Fulani na taarifa Fulani ambazo ni wazi kuwa ni
njema kwa mshauriwa kwa sehemu, kunaweza kujitokeza ujifunzaji wa kweli kabisa
kuhusu wazo fulani kwa msingi huo ili mtu awe na wa kujifunza lazima kuna wazo
linguine litagongana na wazo jipya na kama uhitaji ni lazima basi mtu atahitaji
wazo jipya kama kuna kitu kipya kimejitokeza
3. Ushauri wenye kukabibliana CONFRONTATIONAL
COUNSELING
A.
Ushauri wenye kukabiliana ni nini?
Huu ni ushuri wa moja kwamoja wenye kumleta mshauriwa kukabiliana
na tatizo lake moja kwa moja
B.
Lengo la ushauri wenye
kukabiliana
i.
Ni ushauri unaomlazimisha mshauriwa kukabiliana na tatizo lake
kama ni dhambi au hali yoyote ngumu
ii.
Ni kumsaidia muhusika kuweza kuendeleza nguvu ya kimaadili na
kuepuka kufanya tatizo kama hiulo tena wakati mwingine baadaye ni kama
unakomesha kuwa muhusika akome kufanya aina hii ya kosa tena ni njia yenye
maumuvu haina kupaka mafuta
C.
Aina za matatizo yanayohitaji
ushauri wenye kukabiliana
i.
Tendo lolote lisilo la kimaadili au kitendo cha kikatili
ii.
Aina yoyote ya tendo ambalo mtu binafsi au jamii au kanisa la
mahali pamoja au kile ambacho maandiko yanafundisha kuwa si sahii.
iii.
Jambo lolote lile ambalo linasababisha hatia au hali ya kujisikia
hatia kihisia
iv.
Kukabiliana na mafarakano ya kundi au migawanyiko, au
kutokuelewana na migomo katika kanisa.
D. Ufunguo
wa Ushauri wa wenye Kukabiliana.
§
Ufunguo
mkubwa wa aina hii ya ushauri ni KIBALI
-
Hapa maana
yake ni kuwa Mshauri lazima awe ni mtu anayekubalika sana kwa mshauriwa ili
ieleweke kwamba kinachokataliwa ni tabia mbaya lakini mtu Yule bado tunampenda
vilevile
-
Mshauriwa ni
lazima akubali kuwajibika kwa ajili ya tatizo alilolifanya sio swala la kujua
tun bali aelewe kuwa amefanya makosa.
E.
Mbinu zinazotumika katika kufanya
ushauri wenye kukabiliana.
i.
Mkabili CONFRONTING
Hii ni njia mojawapo ya kushughulika na mtu mwenye tatizo na ni moja ya njia za kichungaji katika
ushauri wa kichungaji mara nyingi hujumuishwa uangalifu katika kutumia mamlaka
ya mtumishi ingawaje mchungaji anapaswa amkubali mahsuriwa na ikumkabili
ikiwezekana na mkabiliwa ni lazima akubali kukabiliwa.
ii.
Kuungama CONFESSION: Mchungaji ni lazima ahakikishe
kuwa muhusika anakubali kukiri makosa yake au ahatia yake.
iii.
Msamaha FORGIVENESS
Ni muhimu sana kumuhakikishia mshauriwa kwa habari ya msamaha
kutoka kwa mungu na kuwa pia ni lazima ajisamahehe mwenyewe.
iv.
Malipizi RESTITUTION:
Ni lazima mchungaji umsaidia muhusika kufanya uamuzi ulio sahii,
afanya mambo mema yenye kujenga ,aonyeshe wema kwa mtu aliyemkosea yaani kama
kunauwezekano wa kwenda kwa mtu aliyemkosea na kufanya mapatano na wahusika ni
muhimu wakikubali kwa vile walivyiokwazwa wao pamoja na wengine.
v.
Upatanishi RECONCILIATION: baada ya hatua kadhaa ni muhimu
sana kwa mchungaji kuhakikisha kuwa upatanishi unafanyika kati ya muhusika na
Mungu kisha muhusika na wale aliowakosea na kuhakikisha kuwa kama ni uarafiki
unarudia katika hali yake ya kawaida ,amani inakuwepo na mawasiliano
yanaendelea na kusababisha mtu huyo kukubalika au kujikabidhi tena kwa Mungu.
vi.
Ukuaji wa kiroho SPIRITUAL
GROWTH:
Ujenzi wa kiroho katika njia mbalimbali ikiwemo maombi, uisomaji
wa neno la Mungu Biblia na kumtegemea Roho mtakatifu kutachangia ukuaji wa
kiroho baada ya kutokea kwa amtatizo.
F.
MAANDIKO NA USHAURI WENYE
KUKABIBLIANA.
Kukabiliana katika agano jipya
kunazungumzwa kama kuelezana ukweli katika upendo sawa na Waefeso 4;15 kupeana
ukweli ni kuzuri sana kama kutafanyika kwa uangalifu na kwa njia ya upendo,
mshauri ambaye anazungumza ukweli asipokuwa anajali au kuonyesha upendo
atazalisha hisia za kukataliwa au hakli za kujitetea kutoka kwa mshauriwa
WAGALATIA 2:11 Tunaona Paulo
mtume akimkabilia Petro ambaye kwakweli alistahili kulaumiwa
2SAMUEL 12:1-12 Tunamuona nabii
Nathani akimkabili Daudi kuanzia na kuufunua ukweli kuhusu matendo ya Daudi na
kumafanya asikie hatia ya kile alichokifanya na hatimaye kukubali toba na
kukiri kisha kupokea mshamaha na badiliko huu ni mafano mzuri wa ushauri wenye
kukabiliana.
G.
HATARI WAKATI WA KUKABILI
Kukabili ni kama dawa kali sana inapotumika bara bara inaweza
kuleta uponyaji lakini pia kuna hatari kubwa sana inapotumika vibaya
i.
Hatari ya kutumia Udikteta - halii hii inapoptumika vibaya
hususani kwa wachungaji inaweza kupelekea hali ya wao kujisahau na kujiona kama
watu wengine ambao hufikiri kuwa wakati wote wao wako sawa na wengine tu ndio
wakati wote wanakosea, kwa ujumla watu namna hii ni wale wanaoamini kwamba
wakatui wote unapaswa uitii mamlaka na wanatarajia kuwa mshauriwa atafanya kila
wanachokitaka swan a jinsi wanavyotaka.
Udikteta hauwezi kuwa na matokeo endapo kutakosekana uvumilivu na
upendo na kumbuka kuwa funguo muhimu hapa ni kukubalika
ii.
Swala la maadili - Mtu anapoishi juu ya kiwango
cha maadili kule tu kuishi kwake ni hukumu kw2a watu wasio na maadili, kwa hiyo
unapotaka kufanya ushauri wenye kukabili ni muhimu sana kwako kuhakikisha kuwa
unaishi sawa na maadili ili uwe na mamlaka ya kuwambia wengine nini cha kufanya
utawezaje kuelekeza wengine wafanya kile ambacho wewe hukifanyi huo ujasiri
unautoa wapi, lengo kuu likiwa kumfanya mshuriwa kutambua makosa yake na
kugundua kuwa anawajibika juu ya hilo.
iii.
Mshambulizi mageni.
Baadhi ya
watumishi wanaweza kuwakabili watu kwa mashambulizi mageni kwa hiyo ni muhimu
kutofautisha kati ya ushauri wa kukabili na Hasira zako, kwa hiyo pale
unapokemea uovu usimwage hasira zako juu ya mshauriwa kwani matokeo yake
inaweza kuwa ni kudhuru badala ya matokeo kuwa mazuri au yanayokusudiwa.
4. USHAURI KATIKA MASWALA YA
NDOA NA FAMILIA.
A.
MAMBO YANAYOCHANGIA KUMFANYA MCHUNGAJI KUWA MSHAURI MZURI WA
MASWALA YA NDOA NA FAMILIA
1.
Mkao wenye faida STRATEGIC
POSITION
Wachungaji wana nafasi nzuri sana ya kuwa washauri wazuri wa
maswala ya ndoa na familia kuliko aina nyingine za washauri, ana nfasi kwa
maswala ya vijana, wanaojiandaa kwa aajili ya kuoana, wakati wa harusi, kwa
ajili ya kujihusihsha na maswal aya furaha na huzuni katika matukio mbalimbali
ya kifamilia na hivyo kumfanya mchungaji kuwa na nafasi nzuri za kuweza
kushauri familia na ndoa za jamii
2.
Mkao wa kimafundisho STRATEGIC
INSTITUTION
Wachungaji wana nafasi ya kuifundisha jamii katika mkakati wa
kimafundisho kwa sababu kimsingi wana nafasi ya kuzifikia familia kwani katika
ngazi hii ndiko watu wanako kulia, wanakoharibika na wanakoweza kubadilishwa,
Kupitia ndoa ambao ndio msingi wa kila familia, mchungaji ana nafasi ya
kuchangia kiakili, kiroho,na kimwili ukuaji wenye afya kuaznia na wanandoa
wenyewe na hata , wadhamini,watoto wao na hata wajukuu wao.
3.
Matatizo ya kindoa MARRIAGE
CRISIS:
Yafuatayo ni baadhi ya changamoto za ndoa na familia ambazo
hujitokeza kwa wingi katika nyakati za leo na kuonyesha wazi kuwa kweli ndoa
hiyo iko katika wakati mgumu au ina mgogoro.
·
Kutishiana ama kupeana talaka
·
Kutawanyika au kufarakana kwa familia
·
Uchungu wa kupita kawaida wa mke
·
Watoto kuwa na tabia mbaya au kubakwa
·
Tabia mbaya za kipindi cha mpito kwa watoto
·
Swala la mtu kutaka kujiua
·
Hali ya kutokufurahiana tendo la ndoa au kunyimana, maumivu au
kukosekana kwa furaha
·
Kuweko kwa ukimwi n.k.
·
4.
Kubadilishana wajibu ROLE CHANGES.
Katika
nykati za leo kumekuweko na wimbi kubwa la wanawake na wanaume kubadilisha na
wajibu na kufikia hqali ya kutokutambua wajibu wa kila mmoja na hivyo
kusababisha mtikisiko wa mahusiano na kutikisa misingi ya mahusiano katika ndoa
nyingi, hali ya wanawake kutaka au kudai kuwa wana haki sawa na wanaume na kuwa
wanaweza kushiriki sawa katika kila kitu ikiwemo hata kufanya maamuzi
kumepelekea familia nyingi na ndoa kuwa katika hali ya migogoro
B.
ASILI YA MIGOGORO KATIKA NDOA
Migogoro katika ndoa imejengeka katika msingi
wa mahitaji ya aina mbili ya kibinadamu, misingi inayomvutia mwanaume na ile
inayomvutia mwanamke katika kila aina ya mahitaji kwa ajili ya kujiridhisha,
kuridhika kimahitaji kunategemeana nguvu ya ndoa yenyewe na kutokuridhishwa
katika kila sehemu ya hitaji la kibinadamu la wana ndoa linaweza kupelekea kuweko
migogoro katika ndoa.
Aina kuu
mbili za mahitaji.
1.
Mahitaji ya kiutu PERSONALITY NEEDS.
i.
Hali ya kustahili
ii.
Uhuru wa ndani
iii.
Hali ya kumaanisha mambo
iv.
Uhusiano wenye uaminifu
v.
Hitaji la kupendwa
vi.
Jitaji la kiulinzi
Hali yoyote inayopelekea mahitaji
ya kiutu kuingia katika matatizo inaweza kusababisha migogoro.
2.
Hitaji la kingono SEXUAL NEEDS
Mahitaji ya kingono ya kike au ya kiume yana
aina zake za changamoto kisaikolojia, kuna uhitaji wa ndani sana uliofichika
unaohitaji kuridhishwa au kutoshelezwa na kama hautoshelezwi katika jinsia hizo
mbili zinapokutana pamoja katika ndoa basi kuna uwezekano wa mwanamke au
mwanaume kutafuta utoshelevu huo kwa mwingine na kwa kweli ni jambo
lisilokanushika kuwa kuna hitaji kubwa la kingono linalohitaji kutimizwa ambalo
hatuwezi kulikana.
C.
BAADHI YA VYANZO VYA MATATIZO KATIKA NDOA.
1.
MAWASILIANO MABAYA NEGATIVE INTERACTION:
Mawasiliano yanaweza kumaanisha ni kitu gani kila mmoja anakifanya katika
mchakato mzima wa kuonyesha mwitikio kwa mwenzake, wanasaikolojia wametumia
swali hili katika kujaribi kutafiti ni namna gani watu wanaingiliana katika
ndoa Je unakunywa kwa sababu mkeo ana kelele, au ana kelele kwa sababu wewe unakunywa?
2.
Mawasiliano mabaya huweza kusababishwa
na maswala kadhaa yakiwemo yafuatayo
a. Kukosekana
kwa mawasiliano au mawasiliano kuwa duni
b. Hali ya
kukataliwa
c. Hali ya
kutokuwa sawa na majibu ya mkato
d. Hali za
kushambuliana
e. Hali za
kukosoana kila wakati
Kazi kuu za mshauri hapa ni
·
Anapaswa kisimama kama mpatanishi
·
Anapaswa kuwa kama nguzo ya mawasiliano
Wajibu huo unaweza kumsaidia yeye
kuingiliana vema na watu waliokosana na kusaidia wao wanandoa kupatana na
kuacha kuumizana na kuacha kuchochea mgogoro unoweza kuwapeleka pabaya
NAMNA YA KUPANUA WIGO WA MAWASILIANO
Ili kuruhusu muingiliano
Mchungaji kama mshauri anapaswa kuhakikisha kuwa anapanua wigo wa kuvunjika kwa
mawasiliano,kuvunja hali za kuumizana kihisia,kuondoa hali za kukataana, na
mgogoro wa kihisia , kuachwa kwa majibu ya mkato na kukosoana
3.
KUANGALIWA WAJIBU WA NDANI INTERNALIZED ROLE IMAGES:
Kila mwanandoa ana aina ya mtazamo namna gani mwenzake anapaswa
kuwa mtazamo huu hauko nje uko ndani huu unajengeka kutokana na wazazi wa kila
mmoja walivyokua, na kile watu walichokiona mama yake akikifanya anatarajia mke
wake naye akifanye, na kile mke alichokiona baba yake akikifanya anatarajia
kukiona mume wake akikifanya , kazi ya mshauri itakuwa ni kupanua wigo wao wa
kimtazamo ili uweze kuwa matazamo wa hali halisi jambo hili linawezekana tu
pale inapotumika njia ya kuelimisha yaani ushauri elimishi kwa kuwafundisha
upekee alio nao kila mmoja na kuwa kama
wana ndoa wanapaswa kuchukuliana
4.
Kukosekana kwa maarifa LACK OF KNOWLEDGE.
Baadhi ya wana ndoa hawana maarifa na matatizo mengine katika ndoa
zao husababishwa na hali hiyo na maarifa hayo yamo katika maswala makuu matatu
hivi mfano
a.
Maswala ya fedha.
b.
Maswala ya tendo la ndoa
c.
Maswala ya malezi na mipango ya kifamilia.
Ni wajibu wa mshsuri kuwasilisha
ujuzi kulingana na eneo linalohusika au lenye tatizo.
5.
Dhambi. SIN
Hili ni moja ya Sababu ya matatizomakubwa sana katika ndoa na kwa
kawaida hujumuisha
·
Zinaa
·
Hali ya kinafiki
·
Kukosekana kwa uaminifu
·
Ubinafsi
Kwa msingi huo kukabiliana
kunakoongoza katika toba, Msamaha na upatanisho ni muhimu kunapokuweko na
matatizo makubwa na kujadili sababu muhimu za kuzitendea kazi baadaye
6.
Misukumo kutoka nje EXTERNAL PRESSURES.
Wakati mwingine maswala ya matatizo ya ndoa huweza kuwa mabaya au
husababishwa kuwa mabaya kwa sababu ya misukumo kutoka nje au kutokana na hali
za migandamizo hali hizi ni pamoja na
·
Wahusika kutoka nje yaani mawifi, n.k ambao huwa na matakwa kadhaa
dhidi ya wana ndoa
·
Watoto ambao mahitaji yao na kuweko kwao kunaleta mwingiliano wa
ndani kati ya mwanaume na mwanamke na wakati mwingine wanaweza kuwa ukuta kati
ya wana ndoa.
·
Marafiki ikiwa ni pamoja na marafiki wa jinsia tofauti ambao
huchukua muda kati ya wanandoa aidha mmoja wao au wote kwa pamoja au kwa
nyakati toafauti.
·
Kazi ambazo zinahitaji mume au mke kuchukua muda na kurudi akiwa
amechoka na hivyo kuwafanya wana ndoa wakiwa na muda usiotoshelezana
D.
JINSI YA KUDHIBITI MATATIZO YA KINDOA.
1.
Fundisha kanuni za Kibiblia
kuhusu ndoa
Mungu ndiye
mwanzilishi wa ndoa na ndiye aliyemuumba mwanaume na mwanamke na ametoa
muongozo wa kibiblia ni namna gani wanapaswa kuishi na majukumu waliyo nayo
kila mmoja, miongozo hiyo ni lazima ifundishwe kwa uwazi majumbani na
makanisani na kuonyeshwa mfano kutoka kwa kiongozi kanisani ni moja ya maswala
ya muhimu sana. Hivyo mshauri mchungaji anapaswa kuwa mfano huo wa kuigwa
vinginevyo itakuwa ngumu kushauri.
2.
Sisitiza umuhimu wa ndoa, utajiri
uliomo katika ndoa na kujitoa katika tendo la ndoa.
§ Ni muhimu kusisistiza umuhimu wa
ndoa kwa muda wakutosha na kuwa juhudi kubwa ionyeshwe katika kushughulika na
matatizo hayo aidha tia moyo watu kuipa ndoa uthamani wa hali ya juu na kuipa
kipaumbele zaidi ya kitu chochote
§ Watie moyo wana ndoa kujihusisha
na
-
Semina mbalimbali za ndoa
-
Kusoma vitabu mbalimbali vyenye kutoa msaada wa maswala mbalimbali
ya ndoa na kusikiliza kaseti zinazohuso maswala ya ndoa
-
Watie moyo kufanya mambo pamoja
na kwa ajili ya kila mmoja
-
Wasaidie kustawisha
kipaumbele chao katika maisha na kufanya kazi kuelekea katika kutimiza
malengo hayo
3.
Wafundishe kanuni za mawasiliano
na namna ya kutatua matatizo.
§ Wafundishe namna ya kuchukuliana
kila mmoja kwa madahaifu ya mwenzi wake.
§ Wafundishe umuhimu wa kila mmoja
kumsikiliza mwenzake na kujifunua kumkubali mwenzi wake na kumuelewa isha
kuchukuliana naye kama alivyo.
§ Wafundishe umuhimu wa kuhurumiana na
kuchukuliana kuwa wazi kwa kila mmoja na mwenzi wake
4.
Wafundishe kuhitaji ushauri pale
inapobidi.
§ Kwa baadhi ya wanandoa kutafuta
ushauri kwao inakuwa kama aibu na inaonekana kwao ni kama wameshindwa au
wanatoa nje maswala yao ya ndani, lakini inaweza kusisitizwa hata kupitia
madhabahuni kuwa kuna umuhimu wa kuwaona ashauri kama sehemu ya kutia nguvu hali
yao ya kindoa Mtu mmoja alisema hivi njia mojawapo ya kujua nguvu ya mtu ni
kujua udhaifu wako
§ Hata hivyo ushauri ni muhimu kama
utatolewa mapema kabla ya kusubiri matatizo yatokee na kurundikana na hatimeye
kushughulikiwa wakati hali ikiwa mbaya.
E.
BAADHI YA MASWALI MUHIMU UNAYOWEZA KUYAULIZA WAKATI WAUSHAURI WA
MASWALA YA NDOA
§ Kwanza jiulize kama wanandoa hao
wanaweza kuwa pamoja au kwanza kila mmoja peke yake?
-
Ndoa ni uhusiano na matatizo ya ndoa hujumuisha watu wawili kama
mijadala inaweza kufanyika pamoja basi
mapatano yatakuwa ni matokeo makubwa nay a haraka
-
Ingawaje wakati mwingine unaweza kugundua kuwa miongoni mwa hao
wanaohitaji ushauri mmoja anataka ushauri na mwingine hataki na kuna maeneo ambayo mmoja aun wote wana
matatizo ambayo ni ya siri na yanaweza kuwa faida kutatua tatizo endapo
watatsikilizwa tofauti tofauti.
-
Kumbuka kuwa hata kama unawaona labda mwanandoa mmoja ndiye tatizo
kubwa zaidi ni muhimu kuwa katikati usionyeshe kukosoa mmoja na kumkandamiza
mwingine
§
Je inakuwaje unapomshauri mtu wa jinsia
tofauti?
-
Kadiri
iwezekanavyo ni muhimu kufahamu kuwa kumshauri mtu wa jinsia tofauti na yako ni
swala la hatari sana hivyo hakikisha kuwa kunakuweko watu wengine hata kama ni
mbali kidogo lakini wawepo.
-
Kama n I muhimu
sana kufanya hivyo basi ni lazima uwe na maarifa ya kutosha, na maombi ya
kutosha au uwe na mkeo, ama kiongozi wa kanisa kwani nao wana wajibu mkubwa wa
kujua nani anamsaidia nani nini, hata kama hawajui kwa undani yale
mnayoshauriana lakini ni muhimu kwa usalama wenu wako na mshauriwa na kama kuna
uwezekanao basi aina hizo za ushauri zifanyike katika eneo lililo wazi ofisini
au maeneo mengine ambayo watu wanapita.
§
Je kuna haja ya kuwa na Muda maalumu kwa
ajili ya ushauri?
Kumekuwako na utafitu unaobainisha kuwa
ushauri unaofanyika ndani ya muda mfupi umekuwa na matokeo mazuri sana kuliko
ule unaochukua Muda mrefu hasa wa majuma kwa majuma.
§
Je kuna umuhimu wa kutunza siri za ushauri?
Kwa kweli
mshauriwa anahitaji kuwekewa uhakika kwamba kila kinachozungumzwa kitakuwa ni
siri na kuwa itabaki kuwa hivyo
Kama mshauri anamuhusisha mkewe
kwa undani sana maswala ya mshauriwa basi hilo linapaswa kuwa wazi sana kwa
muhusika kuwa maswala hayo yatakuwa bayana kwa mke/mume wa mshauri.
Maswala ya ndani ya ushuri hayapaswi kamwe kuchukuliwa
kwenye bomba yaani madhabahuni na kutolewa mifano katika mahubiri ama
vinginevyo usinukuu jina la mshauriwaa au dalili zinazoweza kudhihirisha
5.
Ushauri wa jumla au ushauri wa
kimakundi
A. Maana
ya ushauri wa kimakundi Group Counseling.
·
Ni ushauri
unaohusu kushirikishana ain a za hisia, mawazo na uzoefu katika hali ya heshima
na Ufahamu.
B.
Kikundi fulanmi katika kanisa
kinaweza kujihusisha na ushauri wa kimakundi
·
Kikundi kidogokatika kanisa kinaweza kikaandaliwa kushughulika na
watu wenye upweke na hatimaye wakafaidika kuona uzuri wa ukristo kupitia mahusiano yanayofanyika kupitia uhusiano huo
ulioundwa na hivyo kupitia wengine Mungu
anatumia kikundi kuleta uponyaji makundi ambayo Mungu huweza kuyatumia ni
pamoja na
o
Makanisa ya nyumbani
o
Makambi ya kanisa hisika
o
Makundi ya wazazi kwa ajili ya kuelimishana
o
Vyama vya vijana
o
Vikundi vya kujifunza Biblia
o
Familia rafiki
o
Kundi la wataalamu
o
Makundi ya waajiriwa
o
Vyama vya akina mama
o
Vikundi vya wasiooa na wajane. N. K.
C.
Shughuli za Vikundi hivyo ni pamoja na
§ Maombi ya pamoja
§ Usomaji wa Biblia wa pamoja
§ Kushirikiana kwenye kujali
§ Huduma kwa jamii.
-
Kama kundi linaloongozwa na Mchungaji au kiongozi mwingine aliyeteuliwa
waamini wanaelekeza utendaji wao katika maeneo makuu matatu
§ Juu Kumuabudu Mungu
§ Nje kuwafikia wasiofikiwa
§ Ndani kuwajenga washirika kupitia
kubebeana mizigo na mafundisho na ushirika.
D.
Maandiko na ushauri wa kimakundi.
1.
Wanafunzi wa Yesu (Katika injili)
-
Yesu alizungumza na mtu mmoja mmoja kuhusu mahitaji binafsi na
alikutana na vikundivikundi baadhi yao wakiwa ni wanafunzi wake ambao alikuwa
akiwandaa kwa ajili ya kufanya utumishi baada ya yeye kurudi Mbinguni.
-
Yesu aliweza kuwafundishwa wanafunzi wake alipokuwa akiingiliana
nao kimazungumzo kimaisha na kupitia mafundisho maalumu.
2.
Nyakati za kanisa la kwanza (Katika Matendo na Nyaraka)
-
Nyakati za kanisa la kwanza wakristo waliyaendeleza mafundisho ya
Kristo na huduma kwa kufundisha na kuhubiri, na kutoa ushauri Matendo 2
-
Maswala haya hayakuwa yanaonekana kama jukumu maalumu la mtu
maalumu au kiongozi wa kanisa ziliweza kufanyika kupitia wakristo wa kawaida tu
walifanya kazi,walishirikiana, na kujaliana kila mmoja na mwenzake na hakuna
mtu aliyetengwa nje ya kanisa
-
Kama utasoma kitabu cha matendo ya mitume ni wazi kuwa hawakuwa
wanaifanya kazi ya kuhubiri tu bali na kufundisha na kuitiisha jamii na
kushughulika na uponyaji wa jamii
E.
Faida zitokanazo na ushauri wa kimakundi.
§ Kunakuwa na uponyaji wa ujumla
kupitia mazingira ambayo watu wanakutana nayo katika familia, kazini, shuleni,
na mahusiano yatokanayo na jinsia zao na katika jamii na kupitia hali hiyo basi
kunatokea uponyaji na kupitia watu waliokutana na changamoto mbalimbali
kunakuweko uzima hivyo kunakuweko uponyaji kuna usemi usemao kwa makundi
walivunjika moyo na kwa makundi walitiwa moyo.
§ Kunakuweko na kuokoa Muda wakati
mwingine ni ngumu kumzungukia kila mtu na kumshauri na kukutana na mahitaji
yake lakini ushauri wa kimakundi unasaidia
kuokoa Muda na huku tunakuwa tumewafikia wengi walioumizwa kwa wakati
mmoja.
§ Kufundisha wasaidizi wengi watu
waliosumbuliwa watapata nafasi ya kujifunza na kusikia njia au mbinu mbalimbali
zinazotumiwa na wahusika katika kuwasaidia watu na hivyo baada ya muda unapata
wengine wenye uwezo wa kusaidia wengine.
§ Kuponya tatizo la upweke. Uzoefu
mmojawapo wa kufanya ushauri wa kimakundi ni pamoja na kuondoa upweke, haliza
kuvunjika moyo na kupata shuhuda kama Da nafikiri nilikuwa mtu mbaya sana,
lakini sasa naweza kuona shida yangu ilikuwa wapi au naona tatizo kumbe ni dogo
sana ukilinganisaha nay a wengine.
§ Kurudisha uaminifu, watu ambao
walipoteza uaminifu wanaweza kurudisha uaminifu sasa kupitia wale walio
walioponywa kwa ushauri wa kimakundi.
Kanuni ya
kuwa na ushauri wa kimakundi wenye mafanikio.
i.
Kuweko kwa vigezo vyote vyenye kuwavutia watu.
§ Unda kundi lenye malengo ya
kuyafikia matatizo ya kihisia ya mahitaji ya watu aumtu Fulani katika kundi.
§ Elezea wazi kwa kundi kusudi la
kundi hilo kwa jamii
§ Lipe kundi hilo jina lisilotishia
watu
§ Mchungaji anaweza kumuweka mtu
aliyemuamini au kiongozi wa kawaida au mtu Fulani anaweza kualikwa kwa ajili ya
mada Fulani
ii.
Hakikisha kuwa unaunda kundi dogo linaloweza kutosheleza na
kuruhusu muingiliano na uwezo wa kuonana uso kwa uso wakati wa mawasiliano na
wahusika wote
iii.
Katika wakati Fulani ni muhimu sana kwa kiongozi kuwauliza
washirika kueleza kile wanachokitazamia na kupata kutokana na uzoefu wao
iv.
Mnaweza kuandaa vitabu au mada au mistari ya muongozo ni namna
gani mijadala itaongozwa ili kuondoa hofu na kupata mtiririko unaokwenda kwa
mpango na utaratibu.
v.
Kiongozi anapaswa kutengeneza mazingira yanayokubalika na kutoa
nafasi ya kusikiliza kila mmoja anasema nini, kisha kutia moyo hali ya kuwa
wazi na kuwasiliana
vi.
Kiongozi ni muhimu kujaribu kupata mwangwi feed back na kujaribu
kulisaidia kundi kuwa waangalifu katika mchakato mzima wa muingiliano na
mawasiliano.
Jinsi hali ya mambo inavyopaswa kuwa.kwa
mfano wakati wa kushughulikia tatizo la ktokukubali kubadilika.
Luka 12; 16-19, na Yohana 5; 1-9.
§
Mada izungumzwe katika hali inayoashiria tatizo linashughulikiwa
sasa au tatizo lilioko leo
§
Au inaweza kupangiliwa katika hali inayoonyesha kuwa una tatizo
sasa na ukilijumuisha katika mtazamo wa kikristo leo na kuonyesha kama sababu
ni za kiroho au udhaifu wa wakristo na kuonyesha kama mkristo anaweza kukubali
mabadiliko au hapana.
Njia kuu mbili za kuonyesha hali ya mambo
katika maisha tuliyo nayo
1.
Kuridhika na hali hjalisi tulizo nazo leo mfano mafanikio Luka
12;16-19 tajiri huyu aliridhika na kila alichokipata na hakujua kuwa kulikuwa
na jambo muhimu zaidi ya hilo
2.
Kuna wakati tunaweza kuufikia tukadhani kuwa tumafika na
hatuhitaji kwenda zaidi ya hapo na hatufany bidii zaidi ya ile
Paulo alishinda tatizo kama hili kwa kuwa na tabia ya kutokukubali
kuwa amefika Wafilipi 3;12-14.
3.
Hali ya kutokuwa na matumaini ya kubadilika. Yohana 5;1-9.
-
Mlemavu huyu aliyepooza alikuwa amekwisha kupoteza tumaini la kuwa
angekuja apone
-
Kuna watu huwa wanasubiri mabadiliko mpaka wanakata tama ya kuweza
kutokea kwa mabadiliko
-
Kume njia za mabadiliko ziko na kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
3.
Mambo makuu matatu yanayosababisha watu kutokukubali mabadiliko au
kufikiri wamefika
1.
Kujilinganisha na wengine Luka 18;9-12 Farisayo na mtoza ushuru.
Ni muhimu kukumbuka kuwa“hatujaitwa kuwa bora kuliko wengine bali
tumeitwa ili tuwe bora kwa kadiri itakavyowezekana.”
2.
Kukosa imani Mwanzo 28;10-14 Mungu naweza kufanya zaidi ya
tunavyofikiri Waefeso 3;20.
3.
Kuwa na maonao madogo. Weka mawazo yako juu sana gfanya malengo
yako katika maisha kwa nguvu na kutumia uwezo wako ,uvumilivu wako na kujipa
moyo ili uyafikie na Anthony D’Souza
nashukuru kwa elimu hii muhimu. ongezeni material zaidi hasa kwa mapungufu katika kozi ya ushauri nasaha/nasihi
JibuFutaHongera kwa kazi nzuri hii ambayo imetukuka.Naomba kujua naweza kuwasiliana na wewe kwa njia ya simu?
JibuFutaMaana ninauhitaji na maarifa haya kwa undani zaidi.
Naitwa Selius mtumishi wa ktk kanisa katoliki.
Huwezi weka PDF
JibuFutaSasa nina ufahamu mkubwa kuhusu ushauri
JibuFutablessed
JibuFuta