Jumanne, 26 Aprili 2016

Bikira na umuhimu wa ubikira katika Imani.



Utangulizi

Siku za hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa sana kuhusu umuhimu wa ubikira katika imani, wote tunafahamu kuwa Maandiko katika Agano la kale na Agano jipya kwa ujumla yalisisitiza sana umuhimu wa kuoa mwanamke bikira!, Mila nyingi na tamaduni nyingi pia zinathamini sana umuhimu wa mume kuoa au kupata mwanamke Bikira, Bikira ni nini na ina umuhimu gani kiimani? Je kuna ulazima wa kuoa mwanamke Bikira? Kwa nini Mungu aliiweka bikira na kwa nini alisisitiza mwanamwali kuolewa bikira kuna jambo gani katika ulimwengu wa kiroho kuhusu ubikira, je kuoa mwanamke ambaye hakuwa na bikira kuna faida gani au hasara gani? Maswala haya yote yote yanatufikisha mahali hapa ambapo tunapaswa kuliangalia swala hili kwa kina na mapana na marefu.

 Mabinti Bikira Uko Afrika ya Kusini hupewa uthamani mkubwa sana katika tamaduni zao

Maana ya Neno Bikira kimaandiko!
Kwa mujibu wa tafasiri za Agano la kale neno bikira lilitumika kumaanisha Mwanamwali yaani mwanamke kijana asiyejua Mume au ambaye hajawahi kushiriki tendo la Ndoa, na kuna maneno kadhaa ya kiebrania yaliyotumika kuwataja wanawake hao, yaani BETULAH mwanamwali bikira asiyejua mwanaume au ambaye hajaingiliwa na uume bado kwa kiarabu BATULI, na BAHUR mwanamke au mwanamwali kijana na ALMAH mwanamwali bikira aliyetolewa mahari au ambaye yuko karibu kuolewa, Almah pia ilitumika kumaanisha mwanamke safi ambaye hakuna maswali katika kuthibitisha usafi wake, Neno hili ALMAH ndilo analolitumia Isaya Nabii katika Unabii unaohusu Mwanamwali atakayemzaa Masihi Isaya 7: 14. “Tazama Bikira (ALMAH) atachukua Mimba!.” Kwa hiyo kibiblia hii ilikuwa ndio maana ya neno Bikira. Hata hivyo Neno la Mungu lilikuwa na maana ya ndani zaidi kama tutakavyoiona baadaye.

Umuhimu wa Ubikira katika Ndoa.
Ni ukweli usiopingika kabisa kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya kibiblia yaani Agano la kale na Agano jipya na katika mtazamo wa Mungu, Ndoa ilithibitika kuwa ni halali na takatifu endapo alama za ubikira zingeonekana katika tendo la kwanza la ndoa, Damu ambayo ingemwagika kwa mara ya kwanza ingeweza kuthibitisha kuwa mwanamke huyu ameingiliwa kwa mara ya kwanza, Damu hii ilihusianishwa kama damu ya agano lililo wazi kabisa kuwa ndoa hiyo ni ya halali na ni safi na kwa mume na kwa sababu hiyo huyo ndio angekuwa mkeo halali na mwenye kumuingilia ndio mmiliki halali wa Mume huyo:-

Walawi 21: 1,7 Biblia inasema hivi “ Kisha Bwana akamwambia Musa Nena na hao makuhani wana wa Haruni kuwaambia, Mtu ASIJINAJISI……. Wasimumwoe mwanamke aliye Kahaba, au huyo aliye mwenye UNAJISI, wala wasimuoe mwanamke aliyeachwa na mumewe: kwa kuwa yeye ni kuhani ni mtakatifu kwa bwana Mungu wake” ni wazi kuwa hapa BIBLIA iliwakatza Makuhani kuoa wanawake wenye UNAJISI yaani ambao sio safi yaani ambao wameshabikiriwa hivyo kwa ufupi walitakiwa kuoa mwanamke Bikira! Yaani ASIYENAJISIWA!

Ubikira katika agano la kale na wakati wa sheria uliinua sana thamani ya mwanamke, licha ya kuweko kwa mahari maalumu (Waebrania waliita Mohar Betulot) kiarabu (Mahar al Batul) sawa na “bride price for virgin”  Mahari maalumu ya Ubikira, kwa sababu ya kukutwa Bikira, heshima kwa wazazi kwa matunzo mazuri ya binti yao, heshima kwa binti kwa kujitunza lakini pia ilithibitisha uwezo na kiwango cha juu cha uadilifu.

Katika Torati ya Musa mwanaume alipolala na mwanamwali aliyeposwa “ALMAH” na kuharibu uanawali wake alitakiwa kumuoa yeye, na kama Baba yake angekataa asimuoze binti yake kwa mtu aliyembikiri, mwanaume huyo alipaswa kulipa mahari sawa tu na ile ya muoaji wa mwanamke Bikira “Kutoka 22:16-17

Kama mwanamume angembaka mwanamke Bikira alipaswa kwa mujibu wa torati kulipa shekel 50 sawa na mahari ya mwanamwali bikira na alilazimika kumuoa na hakupaswa kumuacha maisha yake yote Kumbukumbu 22:28-29

Kumbukumbu 22: 13-22 Biblia inasema hivi “13.Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, 14. kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; 15. ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; 16. na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; 17. angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. 18. Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, 19. wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote. 20. Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira; 21. na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kupoteza ubikira kungegharimu adhabu ya kifo kwa kijana wa kike na, kuondoa bikira ya mwanamwali kulilazimu kulipa mahari na kumuao hii ilikuwa sheria nzima ya uanawali au ubikira katika agano la kale au torati ya Musa

Katika agano jipya pia mwanzoni Ubikira ulichukuliwa kuwa ni sehemu ya Maisha ya kujitoa na kumtumikia Mungu, mtu alipaswa kuishi maisha ya uanawali siku zote za maisha yake ni hii ingekuwa ni sadaka Sacrifice kuwa ameyatoa maisha yake kwa Yesu na hataki kuruhusu Unajisi katika maisha yake hivyo wazee wengi nyakati za Kanisa la kwanza waliwatunza binti zao, wasiolewe waishi maisha ya kumtumikia Mungu, jambo hili lilifanywa kwa usimamizi wa mzazi vilevile kama ilivyokuwa katika agano la Kale kwa vile kama binti angenajisiwa au kubikiriwa aibu ingekuwa kwa familia nzima, lakini ingekuwaje sasa kama binti anajisikia kutaka kuolewa Paulo mtume akashauri
1Wakoritho 7: 8-9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane Ni heri wakae Kama mimi nilivyo, Lakini kama hawawezi kujizuia na waoe; maana ni afhadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”
1Wakoritho 7: 25-28 “ Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
Wanawali wanaotajwa hapo ni vijana wa kike walio bikira kwamba kwa mujibu wa Paulo kama wanaamua kujitoa na kuishi maisha hayo ya utawa ni vema na kama wanaamua kuolewa hawana hatia yaani sio dhambi

Kwa hiyo katika falsafa za agano jipya kuishi maisha ya ubikira ilikuwa ni aina ya sadaka Sacrifice ambayo madada wengi wanaishi maisha ya utawa hulazimika kuwa bikira na hawasumbuki katika maisha yao kwa vile hawajui lolote HAWAJANAJISIKA!.

Umuhimu wa Ubikira kwa mujibu wa Tamaduni za kiyahudi.

Kwa mujibu wa tamaduni za Kiyahudi na katika vitabu vya tamaduni zao vijulikanavyo kama Talmud, Halakhah na Hagadah  Marabi wakuu kama Gamaliel na Eliezer na Joshua bin Hananiah  wanatoa maoni yao kuwa kulikuweko na utata kadhaa katika kuziangalia alama za ubikira kwani wakati mwingine alama za Damu hazikuonekana kabisa katika harusi kadhaa huku kikiwa na uhakika kuwa mabinti hao walikuwa safi na hawakuwa wamenajisiwa ugumu wa uume kuingia katika uke ulionekana na ulisumbua katika hatua za awali za ndoa au tendo la ndoa hii ilipelekea kuondoa umuhimu wa Damu katika kuthibitisha ubikira wa mwanamke hata ingawa damu ya ubikira ina kiherehere na humwagika kwa wingi tu katika mtindo ulio wazi kuwa mwanamke huyu ni bikira lakini sio wote wanakuwa na alama hiyo na hivyo labda kungekuweko uwezekano wa kuhukumiwa kwa mabinti wasio na hatia ambao ubikira wao uliweza kutokuthibitika katika mazingira mengine
Mkazo mkubwa wa ubikira unapochunguzwa vyema Katika maandiko ulimaanisha KUTOKUNAJISIKA, ASIYENAJISIKA, UNAJISI ni lazima kujiuliza unajisi ni nini kunajisika kunakozungumzwa hapo ni nini? Neno unajisi kwa urahisi ni kuchafuka, kuchafuliwa n.k. kuingiliwa kwa mwanamke katika tendo la ndoa kungepeleka taarifa ya uzuri au ubaya wa tendo hilo katika Ubongo na ungerekodiwa mara moja, taarifa ya utamu wa tendo la ndoa ingekuwa imeingizwa kwa mwanamwali ambaye hakuna mtu wa kumuoa bado, uhitaji wa tendo ungeingizwa mapema kwa binti katika ubongo wake, angeanza kuwakwa tamaa ya kutaka mume huku hakuna wa kumuoa na hivyo roho ya ukahaba ingeingia kichwani na hivyo kumbikiri mwanamke kungeitwa kumnajisi au kumfanya kuwa kahaba, na kama binti aneshindwa kujitunza angeitwa mpumbavu kwa hiyo maana kubwa ya kiroho kuhusu UBIKIRA ni KUTOKUNAJISIKA.

Mwanamke anaweza kuwa Bikira lakini akawa amenajisika

Kama maana ya kiroho ya Ubikira ni kunajisika uko uwezekano wa mwanamke kuwa na ubongo au nafsi iliyonajisika na huku akaendelea kuwa Bikira!, Katika Tamaduni za kiarabu ambako hukazia sana maswala ya Ubikira huku wanawake wakiwa ni adimu sana ziko shuhuda kuwa baadhi ya wanawake Uarabuni, na Jordani na mataifa mengine yenye tamaduni hizi, wanawali walionajisika bongo zao kimapenzi walikuwa auwamekuwa tayari kutunza heshima ya ubikira wana na heshina ya familia zao kwa kutunza ubikira wa uke huku wakitoa maumbile yao ya Nyuma na kuwafurahisha wanaume waliowahitaji kwa nyuma eti ili kutunza mbele je kuna umuhimu gani wa kuoa mwanamke ambaye ametunza bikira ya mbele huku bikira ya kichwani imeharibiwa? Amenajisika
Biblia inaonyesha wazi kuwa Binti wawili wa LUTU walikuwa Bikira yaani walikuwa wanawali lakini kutokana na historia ya kuishi katika mazingira ya Sodoma na Gomora mabinti wa Lutu walibaki na bikira za uke wao lakini walikuwa wamebikiriwa akili zao na uchafu wa Sodoma na Gomora na hivyo hatima yake hawakuona tija kulala na Baba yao baada ya kumlevya na kupokea ujauzito, kwa nini walimlevya kwa sababu walielewa wazi kuwa baba yao katika akili nza kawaida hangelikubali kuzaa na binti zake Angalia Mwanzo 19: 8 “Tazama ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume nawasihi nitawalotea kwenu…” andiko hilo lathibitisha wazi kuwa mabinti wa Lutu walikuwa Bikira hawakujua Mume, lakini pamoja na haya binti za Lutu walikuwa waovu mioyoni mwao Mwanzo 19:30-38 Biblia inasema hivi “
Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.  Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.
Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.    Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.

Unaweza kuona je ulimwengu tulionao leo unaruhusu watu kuendelea kuwa Bikira? Je watu wamenajisika au la? Leo hii kuna vifaa maalumu ambavyo vinawawezesha watu kushiriki ngono hata bila mwanamke au mwanaume “sex toys” zimeenea kila mahali duniani, maendeleo ya sayansi na teknolojia yenye kuruhusu watu kunajisika yameenea kila mahali unaweza kumpata bikira katika dunia ya sasa ambaye hajabikiriwa uke lakini amebikiriwa Ubongo! Lipi lilolo jema ASIYENAJISIKA, kama unataka bikira maana yake tafuta mtu ambaye ubongo wake umetakaswa na kusafishwa na damu ya Yesu asomaye na afahamu

Ubikira na uhalali wa Ndoa.

Biblia inapozungumzia ubikira haizungumzii sehemu moja ya kiungo cha mwili inazungumzia usafi wa nafsi, mwili na roho. Ndio maana kanisa huitwa bikira mbele za Mungu, hivyo neno ALMAH alilolitumia Isaya kuhusu Mariam ndio neno zuri lenye kufaa kwa mtu mwenye sifa ya kumbeba masihim Mariamu hakuwa bikira wa uke tu, mabikira wa uke tu katika Israel walikuwa wengi, Mariam alikuwa safi Mwili nafsi na Roho na hakukuwa na maswali katika habari ya maisha yake”
Hakuna mwalimu yeyote wa ndoa Duniani ambaye amewahi kufafanua kuwa uhalali wa ndoa unasababishwa na bikira hata kidogo, ilivyo ni kwamba hata Biblia haisemi kuwa ubikira unaifanya ndoa iwe halali, biblia inaonya kuwa TENDO LA NDOA lenyewe ndio linaloifanya ndoa iwe halali kuwe na damu ya ubikira au isiweko, yaani katika Ulimwengu wa kiroho unaunganishwa na mwanamke au mwanamume hata kama ni kahaba hana bikira kuwa mwili mmoja kwa tendo la ndoa
1Wakoritho 6:16 “ Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema wale wawili watakuwa mwili mmoja”
Chunguza andiko hilo hapo juu nini kinaunganisha ndoa? Sio bikira ni tendo la ndoa hata kama utalifanya na kahaba unakuwa mwili mmoja naye
Hivyo bikira haijawahi kutumika na wanatheolojia wa aina yoyote kama sehemu halali ya kuunganisha ndoa

Je ni mambo gani yanayoifanya ndoa kuwa halali?

Ndoa halali haimaanishi kuwa ni ile iliyofungwa kanisani tu ndoa inaweza kufungwa kanisani nabado ikawa si halali au batili, Cheti cha ndoa si ndicho kinachoifanya ndoa kuwa halali, Machoni pa Mungu, Adamu na Hawa babu na bibi zetu walizaliwa zamani kabla ya kuwepo kwa vyeti, lakini ndoa zao zilikuwa halali na zilidumu kwa Muda wa kutosha Je nini basi kinaifanya ndoa iwe halali? Maswala yafuatayo huifanya ndoa kuwa halali;-

RUHUSA YA WAZAZI.

Ndoa inakua halali kwanza pale ambapo wazazi hasa wa mwanamke (Mwanamwali),wanapokuwa wametoa ruhusa ya binti yao kuolewa na kijana, Baada ya kijana kuomba  kibali hicho na kuruhusiwa aidha kwa kupitia yeye au mshenga wake, (Mwanzo 34;8,11-12, Samuel 13;11-13,1Koritho 7;36) baada ya Ruhusa hiyo hata kama kuna taratibu nyingine zitafuata  kama mahari, kitakachofuata hapo hakiifanyi ndoa kutokua halali iwe ni taratibu za kimila au desturi, dini au dhehebu, Fulani, Mchungaji, shekhe, Padree au ofisi ya DC. Machoni pa Mungu hiyo ndoa ni halali na haitenganishwi (Malaki 2;13-16).Hivyo ni lazima ndoa hizo ziheshimike na talaka si ruksa (Ebrania 13;4,Math 19;3-4,6) Kumbuka kuwa Mungu huzieshimu ndoa zote hizi hivyo watu wa namna hii wanapookoka kuja kanisani kama wameyazingatia haya watapokelewa kama wanandoa halali isipokuwa kama ana mke zaidi ya mmoja mkewe halali atakuwa ni yule wa kwanza katika kuwaoa hivyo atabakia na yule mkewe  wa kwanza kama mke halali na jambo hili litafanyika kwa hiyari baada ya kujifunza Biblia na kuielewa wala si kwa shinikizo la kichungaji.

SWALA LA KISHERIA

       Swala lingine linaloifanya ndoa iwe halali ni swala la kisheria  au swala la kiserekali kwa mfano hapa Tanzania Unapokaa na mwanamke au mwanamume kinyumba kwa Muda unaozidi miezi mitatu mfululizo na kuzidi, Kisheria serikali inawatambua kama mke na mume walio halali hata kama mahari haijatolewa. Kwa sheria hii mwanamume anapo pokonywa mke kwa sababu yoyote ile ana haki ya kufungua kesi mahakamani na kudai haki ya kurejeshewa mkewe na endapo mwanamke atafukuzwa bila sababu za msingi ana haki ya kudai mahakamani yaliyo haki yake  jambo la msingi au ushauri wa bure kwa wanandoa wa jinsi hii ni kuzisajili ndoa zao serikalini hii itasaidia ndoa kutambuliwa rasmi na kuepuka usumbufu wakati yanapotokea Matatizo kama kuachana, madai ya mirathi au kifo, hili litawafanya watu hao kuwa salama, Wanapookolewa watu wa namna hii ni muhimu mkwa watumishi wa Mungu kuwasaidia watu hao kujisajili na kutokutia moyo ndoa hizi kuvunjika hii ni kwa sababu kanisa ni msimamizi wa utaratibu duniani na serikali pia hivyo ni muhimu kwa kanisa kusaidiana na serikali katika kuhakikisha watu wanaishi kwa utaratibu na si vinginevyo (Warumi 13;1

SWALA LA UZIMA WA VIA AU VIUNGO VYA UZAZI (MITAMBO).

      Hili ni mojawapo ya  swala gumu na lenye utata sana  na huwa lina leta  maaamuzi magumu endapo linatokea hususani katika ndoa zetu za kikristo katika swala hili wako wale wanaounga mkono  kuwa endapo ndoa  itafungwa na baada ya kufungwa ikabainika kuwa  mmoja wa wanandoa hana uwezo  wa kufanya tendo la ndoa  yaani mitambo yake ya kike au kiume haifanyi kazi basi ndoa hiyo ni batili na hasa pale itakapo bainika kuwa mmoja hawezi kabisa kufanya hivyo tangu walipooana ndoa hiyo inabatilishwa swala hili linategemea na mtazamo wa kichungaji na mazingira. Wengine huliona jambo hili kuwa ni halali na wengine huliona kuwa si halali lakini kwa mujibu wa serikali watu wa namna hii hutenganishawa na mahakama.

SWALA LA AGANO (KIAPO) CHA NDOA.

Ndoa ni swala nyeti linalogusa jamii, Dini, Serikali na Mungu, pia hugusa Maisha ya kiroho ya  Wahusika, Hivyo ni muhimu kuelewa kuwa Mungu ni muhusika mkuu hasa pale  wanandoa wanapoapa kwa Mungu humuhusisha yeye Moja kwa moja  na kule kumhusisha Mungu huifanya ndoa kuwa AGANO, Agano ni nini? Neno agano kwa ufupi ni Patano, Ahadi au nadhiri inayofanywa baina ya pande mbili huku zikimuhusisha Mungu, Patano linapofanywa bila kumuhusisha Mungu huitwa  “Mkataba” na Mungu anapinga vikali sana Ndoa za mkataba  ndoa za mkataba  zinazo ibuka duniani hivi karibuni ni kinyume na mapenzi ya Mungu, Mkataba unaweza kuvunjika, lakini sivyo lilivyo Agano, Agano linapokuwa limefanyika huwa limefanyika  (Yoshua 9;14, Kumbukumbu 20;10,Samuel 21;1-9)  Agano huwa halivunjiki hata kama mmojawapo atakuwa amedanganya kwa namna yoyote hiwezi kubatilisha Agano.Kwa mtazamo huu basi sababu ya via vya uzazi kutokufanya kazi inaweza isikubalike kibiblia.

Ubikira haujawahi kutajwa kokote kule kama jambo linaloifanya ndoa kuwa halali, kwa sababu hiyo binti napobikiriwa yuile aliyembikiri anakuwa ameinajisi akili ya binti na hivyo alipaswa amchukue asimuache kwa vile kufanya hivyo kungeharibu maisha ya binti na kumfanya aishai maisha yasiyo yenye kujitunza, Mke wa mtu pia aweza kunajisiwa, kama mtu aliolewa na hajawahi kutoka nje ya ndoa yake pia anakuwa safi na mwaminifu kwa mumewe, anapojaribu kufanya tendo la ndoa na mwanamume mwingine kinachotokea ni uwezekano wa kunajisika kiakili, kwa vila wanawake na wanaume hutofautiana katika utendaji wao washughuli za kimapenzi kila mmoja ana namna yake na hivyo kujaribu sehemu nyingine kunaweza kukuumbia ulevi mwingine wa kimapenzi nakukufanya uhesabike kuwa kahaba au Malaya jambo hili pia hutokea kwa wanaume wanawake hutofautiana miitikio yao kimapenzi na kimahaba na maumbile yao na kadhalika huweza kukufanya uonje tofauti na hivyo kujikuta unaharibu maisha yako ya uadilifu na hivyo kuharibu ubikira wako hata sasa
Ubikira ilikuwa ni alama kivuli ya kibiblia yenye kuzungumzia maswala yafuatayo

1.      Mungu hakutuita katika uchafu (UNAJISI)
Biblia inasema hivi 1Thesalonike 4: 3-7 “3. Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.

2.      Zinaa inakaa katika akili inakamata akili
Ikimbieni zinaa 1 Wakorotho 6: 18-20 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Biblia ya kiingereza haisemi ikimbieni zinaa inasema flee from from sexual immorality yaani kukimbia uchafu wa kingono hii ni zaidi ya zinaa na inahusu kujinajisi na sehemu nyingine muhimu inasema “yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake” ni muhimu kupafahamu mahali hapa muhimu ambapo pamesumbua wanatheolojia wengi kwa miaka kutotafasiri kwa usahii eneo hilo neno juu ya mwili wake “against their own body” kiibrania ni neno NEPHES ambalo maana yake NAFSI ambayo tafasiri yake AKILI au UBONGO dhambi ya zinaa au uchafu wa kingono unatawala mawazo sana kuliko dhambi nyingine zambi nyingine zote hazikai akilini Ni nje ya mwili wake lakini dhambi za kingono zinakamata akili Juu ya mwili wake hii ndio tafasiri kwamba zinaa inatia UNAJISI

3.      Uhusiano wa Mungu na watu wake Efeso 5:31 wawili kuwa mwili mmoja kisaikolojia ni kuunganisha nafsi na hisia, si vema kuunagnisha nafsi na hisia na mtu ambaye hujaamua kuwa naye, Mungu nanapenda watu committed na wanaume wameumbwa kwa mafano wa Mungu pia wanawake hivyo kila mmoja anapenda uaminifu, Mungu anataka kanisa aminifu mume anataka mke mwaminifu na mke anataka mume mwaminifu hili ndo swala la msingi katika uhusiano Damu aliyoimwaga Yesu kwaajili yetu ilikuwa ni uthibitisho wa upendo na kujitoa kwake kwetu, damu ya ubikira ni uthibitisho wa uvumilivu uaminifu na upendo kwa Yule atakayekuwa mwenzi wako lakini kwa sasa damu hii haina msingi tena si kwa maana kuwa watu wasijitunze bali kwa maana ya kufanya uhalali wa ndoa uaminifu ni msingi na kutokuruhusu akili yetu kunajisika

4.      Kila mmoja anapaswa kufanya kila aliwezalo kuhakikisha kuwa anamfurahisha mwenzi wake kisaikolojia ili kumjenga awe wake, kama hujaolewa unaporuhusu chuchu zako kunyonywa na makalio kupapaswa na mdomo wako kuliwa denda mwanamume huyo anakuteka kisaikolojia na kukufanya umtegemee na kumuhitaji, miitikio yako kama unalegea ua unatoa milio au unalegeza macho nk inamnfanya mwanamme huyu kukukumbuka na kutekwa kisaikolojia na ndoo maana kumfikisha mtu kileleni katika mapenzi kunaweza kuwa hatua ya juu kabisa ya kuunganisha nafsi kuliko kuondoa bikira na ndio maana ndoa huwa halali kwa tendo la ndoa zaidi kuliko Ubikira

Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda
Makala na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Maoni 9 :

  1. kwanini watu hawayapati masomo haya? naona wanakosa mengi sana

    JibuFuta
  2. Ubarikiwe na Mungu, Kiukweli kuna Jambo lililo niathiri kisaikolojia, nilikua na Mchumba wangu tulie juana akiwa bado ni bikra, nilikua nipo katk imani skupenda kabsa kumwingilia, lakini nilimwacha nyumbani kwa ahadi kali,,
    ''Nakuomba uzidi kua katka uaminifu kama ulio nao" alinipa ahadi za kutosha,
    Nilielekea Masomoni Chuoni Dodoma (UDOM) Nilipo rudi nilihitaj kuanza nae maisha, lakn alionekana know badilika kimaumbile kama ameharibiwa,
    Siku moja nililazmika kubunja ukimya na kumbana hapo ndipo alip nambia ukweli, niliumia sana, Kiukweli nimeshindwa kumwacha ila naumia hasa napo mwon na kumkumbuka mtu alie mharibu, nimemwoa lakn hamu hutoeka gafla nkikumbuka kua ameharibiwa na kidume fulani,,
    Napata wakati mgumu sana, naomba msaada wako nifanye nn sioni umuhm wake, namwona kana kwamba hana utam wowote inaniuma
    Unaweza tumia simu 0759021034
    Email danielzachason25@gmail.com
    Naomba ushauri

    JibuFuta
    Majibu
    1. kwa ninavyo ona ndoa na mahusiano mengi huvunjika kutokana kwamba watu wengi hususani wanawake kwenye mahusiano wamekua na wanazidi kuwa watumwa wa wanaume waobwa zamani hvyo hata ukiwa nae kama mke ni sawa na kuwa unaishi ma mke wa watu tu kwa sababu akitafutwa na mwanaume wake wa zamani hawezi kukataa kutokana na agano la damu aliotoka kipindi anatolewa bikira..na hii ni kwa wasichana ambao hawajaokolewa yaani kuzaliwa mara ya pili kiroho nandio maana shetani anatumia huo mwanya kuharibu ndoa za watu kwa kuwakumbushaa mambo ya zamani

      Futa
    2. kwa ninavyo ona ndoa na mahusiano mengi huvunjika kutokana kwamba watu wengi hususani wanawake kwenye mahusiano wamekua na wanazidi kuwa watumwa wa wanaume waobwa zamani hvyo hata ukiwa nae kama mke ni sawa na kuwa unaishi ma mke wa watu tu kwa sababu akitafutwa na mwanaume wake wa zamani hawezi kukataa kutokana na agano la damu aliotoka kipindi anatolewa bikira..na hii ni kwa wasichana ambao hawajaokolewa yaani kuzaliwa mara ya pili kiroho nandio maana shetani anatumia huo mwanya kuharibu ndoa za watu kwa kuwakumbushaa mambo ya zamani

      Futa
  3. Ingiza maoni yako...yatulazimu tuoe bikira ili tusihishi kwa wasiwasi maana anakuwa wa kwako peke yako

    JibuFuta
  4. Ni kweli kabisa ni tatizo tunaloishi nalo kwa sasa wanawake wengi wapo hivyo na ndio maana kumekua na ile misemo kama mtalaka hatongozwi! msemo huu hutumika hata kama mwanamke hakuolewa ila tu kama alishakutana na mwanaume sababu akikutana nae basi mwanaume hatumii nguvu nyingi kumshawishi tena huenda akaanza yeye! kiukweli tunaishi na wake za watu! Kungelua na uwezekano taratibu hizi zirudi na zikaziwe zingesaidia sana hata mimba zisizo na baba zisinge kuwepo

    JibuFuta
  5. hili jambo ni la muhimu sana ndugu zangu oa mwanamke bikira utapunguza matatizo kwenye familia yako hata watoto wako utaweza kuwalea kwa mfano wa mama yao.

    JibuFuta
  6. (a) Kukosa Hofu na Kutii Sheria ya Mungu
    (b) Kuacha Mira na Tamaduni za Mababu

    (c) Elimu na Utandawazi wa Kishetwani ndio chanzo cha ngono zembe

    JibuFuta
  7. hili andiko ni zuri na limejitosheleza vyema kwa kugusia maeneo yote muhimu.

    JibuFuta