Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Nabii Yoel



A.     MWANDISHI WA KITABU CHA YOELI

Ø  Mwandishi ni Yoel baadhi ya wasomi wanaamini alikuwa mwana wa Samuel (Samuel 8;1-2.) lakini Maandiko yanamtaja kama mwana wa Pethuel yaani uaminifu wa Mungu ingawa hatuna taarifa alizaliwa wapi na historia yake si kubwa sana ingawa inaonekana ya kuwa alikuwa kuhani Yoel 1;13-14,2;1 na 14-17.
Ø  Jina lake maana yake ni Yehova ni Mungu wasomi wengi wanaamini kuwa alikuwa kuhani hii labda huenda inatokana na kujishughulisha kwake zaidi na maswala ya hekalu na kushughulikia na majukumu ya kikuhani  1;13-14, 2;1, 14-17.Na mkazo wake katika kitabu chake chote unawafanya wasomi kuamini hivyo.
Ø  Inaonekana pia kuwa alikuwa anaishi Yudea na ni maarufu sana kama Nabii wa Pentekoste.Kwa sababu ya kuzungumzia swala la ujio wa Roho Mtakatifu katika Yoel 2; 28.


B.     TAREHE YA UANDISHI.

Ø  Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Yoel Haijulikani hasa ni lini Baadhi wanaamini kuwa huenda kiliandikwa wakati wa baada ya Uhamisho wa Babel kwa sababu Yoel hajawataja waashuru wala wakaldayo wala maswala ya kuabudu sanamu.
Ø  Ingawaje baadhi ya wasomi wanaamini kuwa uchanganuzi wa wadudu kama tunutu, Madumadu n.k ni Lugha ya mafumbo inayohusiana na uvamizi wa majeshi ya kigeni hivyo kama hivyo ndivyo Basi tarehe ya uandishi inaweza kuwa ni kabla ya utumwa na moja ya jambo linalothibitisha kuwa hakikuandikwa wakati wa utumwa ni kwa sababu kinagusia maswala ya ukuhani na hekalu hivyo kunauwezekano kikawa kimeandikwa 830 k.k. kwani hekalu liliharibiwa mwaka wa 586 k.k.

C.      HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA YOEL 2Falme 11; 1-12;3.

Ø  Ukweli kuwa Yoeli anashughulika na makuhani zaidi na sio wafalme unashuhudia ya kuwa kitabu huenda kiliandikwa wakati wa Yehoiada kuhani mkuu ambaye ni mtu mkubwa aliyechaguliwa kusimamia maongozi kwa sababu mfalme alikuwa mtoto hivyo Yoel hajazungumzia maswala ya mfalme katika kitabu chake.
Ø  Malkia wa Yuda Athalia alikuwa amewaongoza watu katika kuabudu mabaali. Lakini Yehoiada aliwaongoza kurudi kwa Mungu Na huduma ya Nabii Yoel ilichangia kuwarudisha watu kwa Mungu
Ø  Athalia alikuwa mtoto wa mchawi malikia Yezebeli aliyeolewa na Ahabu na aliolewa na Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Athalia aliwaongoza Yehoramu na Yuda kuenda mbali na Mungu kuabudu baali na kufanya dhambi nyingine Yehoramu aliwaua nduguze 6 ili kujihakikishia anabaki kwenye kiti cha kifalme na alipokufa mwanae Ahazia akawa Mfalme Badala yake, Athalia alimchochea Ahazia katika kuabudu miungu na baada ya mwaka mmoja aliuawa na Athalia alitawala na kutoa amri kuuawa kwa watoto woote wa Ahazia yaani wajukuu wake na warithi wa kiti cha ufalme.
Ø  Dada wa Ahazia alikuwa ni mke wa kuhani mkuu Yehoiada na kwa neema ya Mungu aliweza kumuokoa moja ya wana wadogo aliyeitwa  Yoashi na kwa kuwa alikuwa na umri mdogo  miaka 7 Yehoiada aliongoza makuhani na wazee wa Yuda kisiasa kufanya mapinduzi na kumfanya Yoashi kuwa mfalme na Athalia akauawa.
Ø  Yehoiada aliendelea kusaidia kuongoza mpaka Yoashi alipofikia Umri wa kuweza kutawala.

D.     UPEKEE WA KITABU CHA YOEL NA UJUMBE WAKE

a.       Yoeli alisisitiza kuhusu Siku ya Bwana, majukumu ya makuhani ambao ni muhimili wa dini na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mapigo yanayohusiana na nzige ni vitu maalumu sana katika kitabu hiki.
b.       Kitabu chote kialenga katika siku ya Bwana, huku Yoeli akitumia mifano ya Nzige kuwaonya dhidi ya hukumu ya Mungu itakavyokua isipokuwa kama watatubu. Jambo hili ingawaje linaenda zaidi ya hali halisi ya siku hizo kwani pia inazungumzia juu ya dhiki ile kuu siku za mwisho ambapo hasira ya Mungu itashuka ulimwenguni.
                


Nzige (Locust) Moja ya wadudu waharibifu wakubwa wa mazao kwa mujibu wa Yoel ni miongoni mwa Majeshi ambayo Mungu angeyatumia kuwashambulia watu wasipotubu uovu wao Picha na Maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.

E.     MSTARI WA MSINGI AU MISTARI YA MUHIMU

Yoeli 2;1   - Siku ya Bwana inakuja
Yoel 2;13. -  Rarueni mioyo yenu
Yoel 2;28  - Nami nitawamwagia watu wangu Roho yangu
Yoel 3;10  - Yeye aliye dhaifu na aseme mimi ni Hodari

F.      MGAWANYO WA KITABU

Kitabu cha Yoeli kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
a.       Nabii anazungumza 1;2-2;17
b.       Mungu anazungumza 2;18-3;21

G.    MCHANGANUO WA KITABU CHA YOELI

·         Hukumu na toba Yoel 1;1-2;27
Yoeli anatoa kwanza sababu za ujumbe 1;1, Neno la Bwana lilimjia, mara nyingi kile ambacho Bwana aliwapa Manabii walitakiwa kuwaambia watu na Mungu alizungumza wazi kulingana na mazingira yao nini cha kukifanya  ili waepuke hukumu zake na kufurahia Baraka zake zaidi
·         Mapigo ya Nzige 1;2-0
Mapigo ya nzige kulikuwa kitu cha kawaida katika mazingira yale lakini nzige hawa anaozungumza Yoel ni wa Tofauti na hawajawahi kuonekana mstari 2-3 ilikuwa ni kitu ambacho wazazi wangewasimulia kizazi kijacho cha watoto wao, kule kuonyesha kuwa wazazi hawatasahahu ni wazi kuwa watu wanapomuacha Mungu kwa hakika hukumu ya Mungu huwa inakuja juu yao bila mzaha, 2-4, Mstari wanne unaashiria labda vipindi vinne vya uvamizi wa nzige au hatua zao za kukua
·         Baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa adhabu ya aina hii ya nzige inawakilisha falme nne zilizoigandamiza Yuda na Israel kwa miaka mingi
Ø  Tunutu – wanawakilisha Babeli
Ø  Nzige – wanawakilisha Waajemi na Waamedi
Ø  Parare - wanawakilisha Wayunani
Ø  Madumadu -   wanawakilisha Warumi.
Hata hivyo baadhi ya wanatheolojia wanasema hawa walikuwa ni wadudu halisi na hawakuwakilisha falme yoyote I; 4 na 2;25-26

H.    WITO WA KUTUBU 1;2-2;17

Ø  Yoeli aliwaita watu woote kutubu kuanzia na Viongozi 1;2,3,14, 2;15-16 na wote walioishi juu ya nchi 1;2,3,14, Watoto wachanga na wanyonyao 2;16, Walevi 1;5 wakulima na watunzaji wa mizabibu 1;11 makuhani 1;13,14,2;15,2;1,15,17.bwana harusi na bibi harusi 2;16,8 walitakiwa kuomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mume wa ujana wake, walitakiwa kufunga na kuomba na kuitakasa siku ya bwana  hili lilikuwa linadhihirisha nini watu wanatakiwa kukifanya ili kuepuka hukumu ya Mungu
Ø  Yoeli aliwahakikishia watu kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na huruma na neema na si mwepesi wa hasira  na  kuwa hughairi mabaya
Ø  Uamsho lazima uanze na Viongozi wa kidini  hivyo makuhani waliagizwa kuomboleza kati ya patakatifu na madhabahu

I.       KUREJESHWA KWA BARAKA ZA MUNGU 2;18-27

Ø  Yoeli 2;18-27 Inatoa majibu ya Mungu kwa maombi ya Nabii, makuhani na watu wote, toba ya kweli inapofanyika Mungu Huiheshimu na kuikubali, hivyo Mungu alihaidi kuwaondolea Mbali nzige na kuwa angerejesha mazao na mavuno yangepatikana, miti ya matunda ingezaa na mashamba yangezalisha mavuno mengi
Ø  Baadhi ya wasomi wanatafasiri kuwa Yoel 2;20  jeshi la kaskazini kuwa kama ni Ashuru lakini mstari wa 25 unaweka wazi kuwa Mungu anamaanisha ni nzige halisi
Ø  Ingawaje namna atakavyo wafukuza nzige hao kungewatia moyo  watu wake kumuamini kwa wokovu dhidi ya majeshi ya wageni
Ø  Yoeli 2;21-27 inakazia maswala ya kiroho na Baraka ambazo zingewajilia watu wa Mungu,Baraka hizo za kimwili na kiroho zingeipata Yuda kama wataamua kumgeukia Mungu na hii pia iliwakilisha Baraka ambazo zingewapata kwa kumuamini Yesu wakati wa miaka 1000 ya Utawala wake duniani.

J.      SIKU ZA MWISHO 2;28-3;21

Ø  Kwa Maneno Hata itakuwa baada ya hayo 2;28 Nabii alimaanisha kuhusu wakati ujao mbali kutakuwa na utembeleo maalumu na hukumu
A.      Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu 2;28-29
Ø  Watu woote wa Mungu wangejazwa Roho Mtakatifu na kuna makundi sita yanatajwa kama ambao wangetembelewa na Roho Mtakatifu Wana wenu, binti zenu, vijana, wazee wanaume na wanawake.
Ø  Hiki alicho kitabiri Yoeli kilitimia kuanzia siku ya Pentecost Matendo 2;17-18 Petro aliitumia tafasiri ya siku za mwisho na kuendelea kwa kawaida siku za mwisho zilianza na Kuzaliwa kwa kanisa  siku ya Pentecost na kuendelea katika kipindi chote cha kanisa, Mungu aliwajaza watu wa chache Roho wake kwa kusudi maalumu lakini sasa anasema kwa watu woote kila mtu atakuwa na sehemu katika utumishi wa kazi yake Sehemu hii pia ya unabii wa Yoeli unaeleza nini kitatokea kutokana na kumwagwa huko kwa Roho wa Mungu, watu watatabiri, wataota ndoto, na kuona maono
Ø  Ishara hizi zoote zinafunua ushahidi wa Agano la kale  Mungu angaeendelea katika namna kama hiyo iliyokuwa wazi wakati wa Agano la kale  kujifunua mwenyewe lakini kwa upana zaidi katika Agano jipya
B.      Dhiki kuu 2;30-32.
Ø  Ishara na maajabu yanayotajwa katika mstari wa 30-32 yatatukia mwisho wa  kipindi  cha kanisa, Danieli alisema kutakuwa na kipindi cha dhiki ambayo haijawahi kuweko tangu kuumbwa kwa ulimwengu  lakini katika wakati huo watu wako kila atakayeonekana jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima wataokolewa Daniel 12;1, Tunaona katika Ufunuo 6;12-14 kile ambacho Yoel alitabiri lakini kwa undani zaidi
Ø  Tetemeko kuu jua kutiwa Giza na kuwa jeusi mwezi kuwa mwekundu kama damu lakini wale watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.
C.      Hukumu ya Mataifa 3;1-16 Isaya 2.
Ø  Mwishoni mwa dhiki ile kuu kutakuwa na hukumu kubwa kwa kuanziwa na vita vya Armageddon watu wa Mungu watakapokuwa wamepatwa na maangamizo makubwa mwishoni wataliitia jina la Bwana kwa wokovu 5;15
Ø  Maombi ya Israel wakati huu yatakuwa  watelemshe mashujaa wako ee Bwana Yoel 3;11 na Isaya 64;1
Ø  Yesu atakuja na watakatifu wake na jeshi la malaika  na atamshughulikia mpinga Kristo na Israel watakapomuona watatubu na kumtambua kama Bwana na mwokozi wao, Kisha hukumu ya mataifa itachukua nafasi yake na mataifa yoote yatahukumiwa katika msingi wa namna wanavyoshughulika na Israel na kanisa.
D.      Utawala wa Yesu Kristo wa Miaka 1000. 3;17-21 Isaya 35
Ø  Ujumbe wa Yoeli unamalizikia na Baraka kubwa iliyohaidiwa kwa watu wa Mungu
o   Bwana atakuwa kimbilio lao na Ngome yao kuu sana 3;16
o   Bwana atakaa katika Sayuni 17,21
o   Yerusalemu watakuwa watakatifu na haitovamiwa tena mstari wa 17
o   Israel itapata chemuchemu za maji na nchi itakuwa yenye kuzalisha sana mstari wa 18 na Yuda itadumu milele mstari wa 20. Mungu atawasamehe Israel Mstari wa 21.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni