ANDIKO LA MSINGI: 2WAFALME 6:15-16 “.Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule
mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi
na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana
wangu, tufanyeje? Akamjibu, Usiogope;
maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”
Utangulizi:
Ni muhimu kwa kila Mkristo kuwa
na ufahamu kwamba ulimwengu wa kiroho ni halisi, na kuwa kama tulivyojifunza,
kwamba kuna vita vya kiroho katika ulimwengu wa roho, kwamba ziko pande mbili
zinazoshindana, upande wa Mungu na Shetani na kuwa wakati mwingine vita hii
hujitokeza katika hali halisi ya mwilini.
Ili ushindi wetu uweze kuwa
Dhahiri,ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha namna na jinsi ambavyo ulimwengu
war oho unavyotenda kazi, ujuzi huu wakati wote utakufanya utembee katika
ushindi na kuwa mbali na hofu ya jambo lolote linalohsindana nawe.
Nabii Elisha alikuwa moja ya
manabii muhimu sana katika Israel, hii ilitokana na uwezo wake mkubwa sana
katika kuuona ulimwengu war oho na kujua kila kinachoendelea upande wa maadui
wa Israel, kutokana na umuhimu wake siku alipougua na kukaribia kufa, mfalme
alilia san asana na kusema “ Baba yangu baba yangu Gagari la Israel na Mpanda
farasi wake” 2 Wafalme 13:14 Biblia
inesema
“Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa
wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia
mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi
wake!”
Kilio hiki kilikuwa kina maanisha
mtu huyu anayekufa alikuwa ni wa muhimu kwa Israel kuliko jeshi zima, Elisha
alikuwa ametumiwa na Mungu sio tu kama Nabii lakini pia kama Mlinzi na mtetezi
wa Izrael na Mfalme pia, Mfalme alijua kuwa kufa kwa Elisha ni sawa na kutoweka
kwa Jeshi la Ulinzi la Israel kwa sababu kadhaa wa kadhaa.
·
Elisha alikuwa ni zaidi ya Idara ya Usalama wa
taifa kwa Marekani, tunaweza kusema alikuwa ni zaidi ya FBI au CIA, alikuwa na
uwezo wa kuona maadui na mipango yao zaidi ya rada kali sana katika Israel
inayoitwa “GREEN PINE” Rada hii ina
uwezo wa kuhisi hatari kwa zaidi ya KM 400, Elisha alikuwa ni zaidi ya Green
Pine”
Pichani ni Rada aina ya Green Pine ambayo imegunduliwa na kuundwa na Jeshi la Israel pekee
·
Ulinzi wa Elisha ulikuwa ni zaidi ya “IRON DOME” hii ni silaha nzito yenye
uwezo wa kuhisi mashambilizi ya adui na kufyatua makombora ya kudhoofisha
makombora ya adui kabla hayajaleta madhara
Pichani ni silaha aina ya Irone Dome ni silaha iliyogunduliwa Israel ina uwezo mkubwa sana wa kulinda na kuharibu mashambulizi dhidi ya silaha za adui na vituo vyao
·
Elisha alikuwa ni zaidi ya “DELILAH CRUISE MISSILE” yenye uwezo wa kupiga km 250 ikiwa na uzito
wa kg 187 au “PROTECTOR USV RAFAEL”
ambazo ni boti zenye uwezo wa kufanya kazi ya boti 9-11 za kijeshi na inauwzo
wa kutumiwa na watu sita na kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja, umuhimu wa
silaha hizo zote nzito zinazotumiwa na Jeshi la Israel kwa wakati wa sasa
zilikuwa sawa na Elisha mmoja tu umuhimu wake kwa ufahamu kuhusu silaha hizo
Google Top 10 Most Powerful weapons of Israel pia unaweza kupitia Defencyclopedia.com)
Pichani ni Israel Rafael Protector USV ni chombo chenye uwezo mkubwa sana na chenye kufanya kazi nyingi katika Jeshi la Israel
Kwa nini Elisha alikuwa wa Muhimu kiasi hicho?
2Wafalme 6:8-14 Biblia inasema “Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita
na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu
kitakuwapo mahali fulani. Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa
Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko
wanakoshukia Washami. Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale
alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si
mara moja, wala si mara mbili. Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana
kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je!
Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?, Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana
wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme
wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala. Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate
kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani. Kwa
hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku,
wakauzingira mji ule pande zote.”
Unaposona kifungu hicho utaweza
kuona umuhimu wa Elisha kwa Israel uwezo wake wa kuona mambo katika ulimwengu
war oho ulimpa ujasiri mkubwa kiasi cha kuliteka Jeshi zima la madui wa Shamu,
Kijana wake Elisha alikuwa haoini katika ulimwengu wa Kiroho na hiyo aliogopa
sana lakini Elisha alimtia moyo asiogope
Kuna watu wengi sana wanaogopa
tena wanaogopa nguvu za giza, au wanapoona mapambano ya vita za aina mbalimbali
kwa jinsi ya mwili wanaogopa sana woga wao ni kama wa mtumishi wa Elisha shida
yao ni kutokuujua ulimwengu wa Kiroho ulivyo
-
Mtu anaweza kuogopa Hirizi tu
-
Mtu anweza kuogopa kuwa ametumiwa njiwa
-
Mtu anwexza kuogopa milio ya Bundi tu wakati wa
usiku
-
Mtu anaweza kuogopa akisikia vitu vinatembea juu
ya dali au bati
-
Mtu anaweza kuogopa kusikia milio ya Mapaka
-
Mtu anaweza kuogopa kwa sababu tu ameota ndoto
mbaya
-
Mtu anaweza kuogopa kwa sababu tu ya nguvu za
giza au wachawi na wapiga madogoli
-
Mtu anaweza kuogopa kwa sababu ya vitisho vya
aina mbalimbali duniani
Ukijujua ulimwengu wa Roho kwamba
tunazungukwa na majeshi ya Malaika hutaweza kuogopa Elisha alikuwa anajua kuwa
analindwa na nguvu za kupita kawaida, Malaika wenye farasi za moto walikuwa
wamemzingira pande zote, ikiwa Elisha wa agano la kale alikuwa analindwa kiasi
hiki sisi nasi tunalindwa na nguvu za Mungu, Zaburi 3:5-6, 27:3 Waebrania 1:14
Roho watumikao kuwahudumia wale watakaourithi wokovu wapo kutuhudumia na
kutulinda hivyo hatupaswi kuogopa
2Wafalme 6; 16-17 “Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi
ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana,
nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule
mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari
ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”
Pichani ni silaha ya Mashambulizi iliyogunduliwa Israel iitwayo "Delilah Cruise Missile"
Mungu akikufungua macho ukaona
namna unavyolindwa na majeshi ya Malaika hutaweza kuogopa Daudi akasema Jeshi
lijapojipanga kupigana name Moyo wangu hautaogopa”
Mungu na akubariki kwa jumbe na mafundisho mazuri.
JibuFutaMungu akubariki sana nafurahia mafundisho yako na yanijenga sana.
JibuFutaBwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu. Asante kwa mafundisho, ukweli yanibadilisha sana. Naomba kuuliza pia je, una vitabu? Asante kwa huduma hii ya Ki-Ungu, Mungu akubariki sana.
JibuFutaBwana Yesu asifiwe sana. Asante kwa mafundisho mazuri, kwa kweli yananibadilisha sana. Asante na Mungu akubariki sana.
JibuFutaBwana Yesu asifiwe sana. Asante kwa mafundisho mazuri, kwa kweli yananibadilisha sana. Asante na Mungu akubariki sana.
JibuFutaBwana Yesu asifiwe sana. Mungu akubariki sana kwa mafundisho. Binafsi ninajengwa na ninabadilishwa sana na masomo haya. Asante sana Mtu wa Mungu.
JibuFuta