Mmea aina ya zeri kama unavyoonekana katika Picha
Ni
muhimu kufahamu kwamba hapa duniani hakuna jambo lolote Gumu lisilo na
majibu, kila jambo na kila tatizo lina majibu yake na ufumbuzi wake,
Magonjwa hali kadhalika yanaweza kutibiwa kwa tiba za aina mbali mbali,
Mungu aliwapa wanadamu mimea ambayo ndani yake aliweka nguvu za uponyaji
kwaajili ya matibabu ya aina mbali mbali.
Nyakati za Biblia watu
walitumia pia madawa yatokanayo na mimea kutibu magonjwa na mateso ya
aina mbalimbali, kulikuwa na miti mingi sana iliyotumika kama tiba,
kabla ya kuanza kutumia zaidi kemikali ambazo nyingi zina uharibifu
mkubwa katika mwili wa wanadamu na hivyo kuchangia udhaifu mkubwa wa
aina binadamu walioko leo juu ya uso wa nchi. Moja ya miti maarufu sana
iliyotumika kwa tiba katika Israel na mashariki ya kati ulikuwa ni mmea
ujulikanao kama Zeri ambao ulikuwa unapatikana kanaani na katika mji wa
Gilead.
Zeri ni nini hasa?
Zeri kwa kiingereza (BALM)
ulikuwa ni mmea ambao ulikuwa maarufu sana nyakati za Biblia mmea huu
ulipatikana katika nchi ya milimamilima iliyokuwa nga’mbo ya Jordan
iliyojulikana kama milima ya Gilead, mmea huu uliuzwa kwa bei kubwa sana
na wafanya biashara wa zamani waliokuwa matajiri walitajirika kwa kuuza
zeri,
Mwanzo 37:25 “Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua
macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na
ngamia zao, wakichukua ubani na ZERI na manemane, wakisafiri kuvichukua
mpaka Misri.”
Unaweza kuona aidha katika nyakati za Biblia kama mtu
anakupenda sana na kukuheshimu sana moja ya zawadi ya ngazi ya juu
kabisa ambayo mtu anageweza kukupatia ilikuwa ni pamoja na ZERI angalia
Mwanzo 43:11 “Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni
hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo
zawadi, ZERI kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na
lozi”.
Kwa nini Zeri ilikuwa bidhaa ya thamani na zawadi kubwa
sana, Zeri ilikuwa na sifa ya kuponya majeraha yote ya mwili
“recovering” na vidonda mbalimbali pia vikiwemo vidonda vya kuumwa na
nyoka, aidha watu pia waliitumia zeri katika kuhifadhia mwili wa
mwanadamu aliyekufa usioze, Hivyo kama dawa nyingine zote zingeshindwa
kutibu jeraha la mtu ndipo sasa ili kuokoa maisha yake ilipaswa
kuitafuta Zeri kwa vile hii ilijulikana kama dawa isiyoshindwa hata
hivyo dawa hii ilikuwa ghali sana ingekugharimu kuuza vyote ulivyo navyo
ili kutibiwa na wataalamu wa Gilead upate kupona. Dawa hii likuwa
haishindwi kutibu jambo kama mtu anetibiwa na dawa zote na
ikashindikana watu walimshauri aende Gilead kwa wataalamu kataumie Zer.
Yeremia 46:11 “Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa
Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.”
Ni wazi kuwa
kama mtu angetumia dawa bila mafanikio dawa ya mwisho ingekuwa Zeri ni
zeri tu ndiyo ambayo ingeweza kutibu maumivu aliyoyapata mtu".
Yeremia 51:8 “Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa”
Katika namna ya kushangaza sana hata hivyo yalikuweko magonjwa ambayo
yalikuwa ahayasikii dawa yaani magonjwa sugu, ilipotokea kuwa mgonjwa
haonyeshi badiliko, kila mara alionekana yuko vilevile hapati kugangwa
lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kusikia Zeri imeshindwa au
wataalamu wa Gilead wameshindwa, katika mstari wa Msingi Yeremia alikuwa
anazungumzia tatizo la kiroho na tabia ya wana wa Israel ambao
walishindwa kutubu na kubadilika kiasi cha kufikia ngazi ya kuhukumiwa
na Mungu, Nabii alikuwa akiomboleza na kujiuliza kuwa dawa isiyoshindwa
imekosekana? Matabibu wa Gilead hawako, Yeremia alikuwa anamaanisha
kuweko kwa toba na manabii, Israel walishindwa kuwasikiliza manabii na
pia walikosa moyo wa toba nJe hapana zeri katika Gilead? Na Matabibu
maana naona afya ya watu wangu haijarejea?
Kimsingi zeri ya Gilead ilikuwa ghali sana na hata hivyo haikuweza kuponya majeraha mengine yaliyowasibu watu.
Marko 5:25-28 “Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi
na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa
vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi
kuwa mbaya, aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma,
akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu,
nitapona”
Zeri ulikuwa ni mti halisi lakini vilevile ulikuwa ni
picha ya Yesu Kristo, katika muujiza huu alioufanya Yesu ni dhahiri
biblia inatuonyesha zeri kutoka mbinguni, inatuonyesha mwanaume mwenye
uwezo wa kumfanya mtu akawa recovered akapona akawa kamili, unaweza
kuhangaika huko na kule kwaajili ya mahitaji yako, kwaajili ya afya yako
ya kimwili na kiroho, kwaajili ya majeraha ya moyo wako, kwaajili ya
majeraha ya adui zako, kwaajili ya majeraha ya ndoa na kazini na shuleni
na hata kanisani, unaweza kuangaika huku na kule kwaajili ya mahitaji
yako ya aina mbalimbali lakini lao ninakutangazia kuwa iko dawa
isiyoshindwa Dawa hii ni Yesu Kristo peke yake yeye anaweza yote kwake
hakuna linaloshindikana ni dawa ya waliokata tamaa, dawa ya
waliojeruhiwa na kudharaulika, ni dawa ya maisha yetu, feature yetu
haiku mikononi mwa wanadamu, iko mikononi mwa Yesu tu, huyu ndio wa
kumkimbilia, huyu ndio wa kumpapatikia, huyu ndio wa kumtazama kwa kila
unalokaboliana nalo katika maisha katika masomo, katika ndoa, kazini nk.
Mwangalie Yesu na utafanikiwa yeye ni zaidi ya zeri ya Gilead ni Zawadi
ya upendo wa hali ya juu kutoka kwa Mungu baba
Kwa maana jinsi
hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa Pekee ili kila
amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
Na. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Hongera sana na shukrani sana kwa naelezo mazuri kuhusu zeri. Ni jani ninalolifahamu ila sikujua kuwa ndio zeri. Asante sana. Geoffrey
JibuFutaHongera sana na shukrani sana kwa naelezo mazuri kuhusu zeri. Ni jani ninalolifahamu ila sikujua kuwa ndio zeri. Asante sana. Jeff
JibuFutaDah! Mwenyezi mungu akubaliki sana kwa kutoa dondoo za kibiblia nzuri
JibuFutaNahitaji mbegu za zeri.Namba ya simu 0658777269
JibuFutaAmeen
JibuFuta