Alhamisi, 20 Julai 2017

Jinsi ya Kuwashinda Pepo!



Mstari wa Msingi  Waefeso 6:12Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” 


 
Utangulizi:-

Ni muhimu kufahamu wazi kuwa kila mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu awe ameokoka au hajaokoka yuko katika vita na mapambano na shetani pamoja na majeshi yake katika ulimwengu wa roho, Kwa wale waliookoka vita hii huwa kali zaidi. Biblia inatufundisha wazi kuwa shetani ni adui  yetu mkuu Mathayo 13:38-39, “lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika”. Yesu anamtaja shetani kuwa ni adui ni adui wa Mungu na ni adui wa wana wa Mungu, Kama shetani hakusumbui na kukupiga vita wewe unapaswa kujiangalia sana kwamba uko upande gani. Yesu anamtaja tena shetani kuwa ni adui katika Luka 10:17-19 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”. Kwa msingi huo katika somo hili tutachukua muda kuchambua na kujifunza kwa undani kuhusu mapepo na jinsi ya kuwashinda kwa kuzingatia maswala ya msingi yafuatayo:-   
  
·         Ufahamu kuhusu Ulimwengu wa roho
·         Ufahamu kuhusu asili ya Mapepo na nyadhifa zao
·         Ufahamu kuhusu vita vya kiroho.
·         Jinsi ya kuwashinda Pepo.

Ufahamu kuhusu Ulimwengu wa roho.
Ni muhimu kufahamu kwamba nguvu za Mungu ziko; lakini vilevile nguvu za giza zipo, na nimuhimu kufahamu kuwa nguvu hizo zinatenda kazi katika ulimwengu usioonekana, ulimwengu huu usioonekana ndio unaitwa ulimwengu wa roho Waefeso 6:12Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, Pale in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Kwa msingi huo basi maandiko yanatufunulia wazi kuwa uko ulimwengu huu wa asili unaoonekana na uko ulimwengu war oho usioonekana, ni katika ulimwengu huu usioonekana ndiko aliko Mungu, lakini vilevile ndiko aliko shetani, ulimwengu huu tunaouona ni wa muda tu, na ule usioonekana ni wa milele 2Wakoritho 4:18tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele” kwa msingi huo tunao ulimwengu huu unaoonekana ulimwengu ambao tunaweza kuona kila kitu kwa macho,tunaweza kuhisi, tunaweza kusikia, tunaweza kunusa na kuonja huu ndio ulimwengu tunaoishi siku zote, Lakini vilevile kuna ulimwengu war oho, ulimwengu huu una Mungu na Malaika zake, ulimwengu huu una shetani na malaika zake waovu ambao ndio tunawaita pepo, Na biblia imetaja hivyo nasi tunaamini, Biblia tunayoitumia yenye vitabu 66 imewataja malaika mara 300, imemtaja shetani mara 40, na imewataja pepo mara 50 na neno roho chafu mara 40 pia limetajwa likimaanisha pepo. Kwa msingi huo tunapozungumzia vita katika ulimwengu wa roho maana yake tunapambana na malaika waovu yaani pepo ambao wanafanya kazi nyingi sana za kuwapinga wanadamu katika ulimwengu huu unaoonekana kwa vyanzo kutoka ulimwengu usiioonekana.

Ufahamu kuhusu asili ya Mapepo na nyadhifa zao
Ni muhimu kujiuliza sasa hawa pepo wanatokea wapi? Wakoje na wanatendaje kazi, Pepo kama wanavyotajwa katika biblia vilevile ndio Majini kama wanavyotajwa katika quran hawa kwa asli walikuwa Malaika

Malaika ni nani?
Neno au jina malaika lina asili ya kiyunani  ambayo ina maana pana kadhaa jina hilo kwa kiingereza ni Angel ambalo limetokana na jina la kiyunani Angelos (Angelos)ambalo lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) kwa Kiarabu Malakat au Malik ambalo pia maana yake ni mjumbe(Messenger) wa Mungu, Hawa ni roho watumishi wanaotumwa na Mungu kuwahudumia watu wake  Waebrania 2:14Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa kumaanisha maswala kadhaa yafuatayo;-

·         Neno hili angelos lilitumika pia kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa” na matumizi kama hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika Matendo 12;15 ambapo wanafunzi walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga mlango hii ni kwa sababu kimsingi wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na isingeliwezekana kutoka gerezani na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama vile hii ni kwa sababu walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa Yakobo pamoja na kuwa waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro kuweza kuwa hai. Jambo lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa kama malaika kwa msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia ilimaanisha wazi kutumiwa kama neno malaika.

·         Neno malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe wa Mungu aliye mwanadamu” mfano katika Ufunuo 2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu inakisiwa kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani  wajumbe ambao wanabeba gombo la chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa ambayo Yohana alikuwa akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa na  Ufunuo 1;11, ambapo agizo linaonyesha kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo ukayapeleke kwa hayo makanisa saba  Efeso, na Simirna,  na Pergamo na Thiatira, na Sard na Filadelfia na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano wale waliopeleka magombo hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa inamaanisha  viongozi wa kila kanisa ambao husimamia makanisa  na huwasomea watu maandiko kama ilivyokuwa wakati wa matumizi ya masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza kazi ya kiongozi ilikuwa ni kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo walikuwa ni watu wanaowajibika kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo viongozi hao pia waliitwa malaika yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha viumbe wa kiroho wa Mungu ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa yale na imani hii ina mzizi katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa malaika wa kila eneo, na pia kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya mbinguni hapa duniani.

·         Malaika ambao tunajifunza habari zao ni viumbe wa kiroho  wenye maadili na uwezo mkubwa wa Ufahamu ambao hawana miili ya kibinadamu na wale wa aina hiyo lakini wakaasi na kuitwa mashetani kwa msingi huo somo hili halitahusu aina nyingine za malaika zile ambazo zimetwajwa hapo juu kama roho ya waliokufa, wanadamu, wasomaji maandiko , wasimamizi wa kanisa au sinagogi au wachungaji ama kanisa lenyewe ambalo humwakilisha Mungu duniani

·  Malaika pia wana majina kadhaa katika maandiko kama vile Wana wa Mungu Ayubu 1;6,2;1,Watakatifu Zaburi 89;5,7. Roho Waebrania 1;14, Walinzi Daniel 4;13,17,23,Enzi, Falme, mamlaka na usultani Wakolosai 1;16 na nguvu Waefeso 1;21.

Pepo ni Nani?
Neno hilo pepo (Demons evil spirit) maana yake ni roho chafu au malaika walioasi, malaika wabaya majini, au malaika waliofanya dhambi.

Asili yake ni nini?
Mungu alipouumba ulimwengu aliumba kwanza ulimwengu wa roho, katika ulimwengu huo Mungu aliwaumba malaika, hatuambiwi kuwa ni wakati gani malaika waliumbwa lakini bila shaka ni miaka milioni nyingi sana, Mungu alipowaumba malaika aliwaumba wakiwa na uhuru wa kuchagua mema au mabaya, la kusikitisha ni kwamba Mungu alipowaumba wanadamu ndipo ilipofunuliwa kwetu kwamba kundi kubwa la Malaika walichagua uovu, walimuasi Mungu wakiongozwa na Shetani ambaye alijulikana kama LUCIFER yaani nyota ya alfajiri Isaya 14:12-14Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” Ezekiel 28: 13 -18Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.” Baada ya anguko hili la shetani theluthi moja ya malaika walijiunga naye na kupoteza nafasi yao mbinguni kwa Mungu Baba na hawa ndio Mashetani, majini au mapepo au roho chafu au majeshi ya pepo katika ulimwengu wa roho sasa basi kazi yao kubwa ni ipi?

Yohana 8:44Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa MWUAJI tangu mwanzo; wala HAKUSIMAMA KATIKA KWELI, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu YEYE NI MWONGO, na baba wa huo.”  
          
Yohana 10:10Mwivi haji ila AIBE na KUCHINJA na KUHARIBU; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

Ufunuo 12:10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini MSHITAKI wa ndugu zetu, yeye AWASHITAKIYE mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.” 

Hizo ni kazi kuu za shetani na sifa zake, katika somo langu hili tutajadili pia kazi azifanyazo shetani na malaika zake au mapepo.

1.      Kuongoza ulimwengu katika uasi “Misleading the Entire Inhabited Earth”
Ni muhimu kufahamu kuwa shetani  pamoja na mapepo wana nguvu ya ushawishi katika akili na maisha ya watu, shetani na mapepo yake wanamamlaka ya kuuongoza ulimwengu katika kuasi au kufanya maasi Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”

 Ziko njia nyingi sana ambazo ibilisi huzitumia katika kufanikisha njia zake pamoja na mapepo yake na moja ya silaha yake kubwa ni kutumia UONGO, atatumia mafundisho ya uongo na dini za uongo 1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;” 

unaweza kuona kwamba kumbe shetani na mapepo wanaweza kutumia mafundisho na ushawishi usio wa kiungu kuupotosha ulimwengu, wakitumia dini za uongo pia Mashetani wamefanikiwa kuzipofusha fikra za watu wengi ili isiwazukie Nuru ya injili 2Wakoritho 4: 3-4 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu

a.       Mafundisho kuhusu mawasiliano na wafu “The teaching that the dead are still alive and you can communicate with them” Shetani anaweza kutumia sauti na uwezo wa kichawi kupitia mapepo kuwadanganya watu kuwa unaweza kuwasiliana na wafu, Biblia inatufundisha kuwa baada ya kifo ni hukumu na kuwa hakuna mawasiliano na wala tusiwasiliane na watu waliokufa Kumbukumbu 18:9-13 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.  Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.”
Mungu alikataza maswala hayo kwa sababu alijua kuwa mashetani yanatumia njia hizo hapo juu, kuharibu uhusiano wetu na Mungu na kujikuta tukipoteza ibada, wote tunakumbuka Jinsi Sauli alivyowaendea waaguzi na kupiga bao hii ilikuwa kinyume na Torati na hivyo alikufa
1Samuel 28:1-25,
Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako. Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima. Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?
Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha. Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia. Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako. Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda. Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo; kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.”
1Nyakati 10:13-14
Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.”
Mtu awaye yoye anayekwenda kwa waganga na kutaka shauri, kupiga ramli anafanya kosa kwani Neno la Mungu liko kinyume na ibada za kishetani

b.      Mmomonyoko wa Maadili “Anything-goes morality”
Ulimwengu mzima uko chini ya yule mwovu 1Yohana 5:19 “Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.” Shetani na mapepo yake wanatumia nguvu zao katika vyombo vya taarifa Media na njia nyingine zote kuinua kiwango cha uovu, ili kwamba wanadamu waone ni sahii na kufuata tamaa za dunia na kusababisha mmomonyoko mkubwa wa uadilifu Waefeso 2:1-3 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine”. Kwa sababu hiyo leo tunashuhudia mmommonyoko mkubwa wa uadilifu, ushoga, tamaa, na kila aina ya uharibifu huku viwango vya utakatifu na uadilifu vilivyowekwa na Neno la Mungu vikionekana kuwa ni ushamba.

c.       Kuinuka kwa roho za uaguzi (Uganga) “The promotion of spiritism.”
Maandiko yanaonyesha jinsi Paulo mtume alivyokutana na mwanamke mwenye roho ya uaguzi au pepo wa auaguzi, na aliyekuwa akijipatia fedha au faida nyingi kwa sababu yanuaguzi Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.” Watu wengi hudhani kuwa waganga wako kwaajili ya kutoa msaada lakini waganga wote ni maajenti wa shetani na wanakuwa na pepo wa uaguzi kwaajili ya kuwasaidia kuagua na kutafuta dawa kwa nguvu za kipepo na hivyo kuwapotoshwa watu wa Mungu katika ushirikina, Paulo akitambua kuwa ni dhahiri chanzo cha uaguzi ni pepo au shetani alikataa kusikiliza sifa za kishetani na kulikemea pepo hilo na likaondoka 

d.      Kuinua watu wenye kufanya Uchawi “The promotion of witchcraft”
Wachawi ni njia nyingine ya utendaji kazi wa kishetani na kipepo, Mungu alikataza uchawi na alitaka wachawi wauawe Kutoka 22:18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” Wachawi walikuwa ni maadui wakubwa wa kazi ya Mungu wakati Mungu alipomtuma Musa na Haruni, wachawi wa Farao huko Misri walipingana na Musa na Haruni wachawi hao walijulikana kama Yane na Yambre 2Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.” Kutoka 7: 10-13 “Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Ni kazi za wachawi ambao pia ni maajenti wa shetani kuwafanya watu wasiokoke, wasiiamini injili na wawe na mioyo migumu kama ilivyokuwa kwa farao, wachawi hufanya kazi za shetani na ndio maana Paulo alimkemea Mchawi
Matendo 13:8-12 “Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana
Unaweza kuona hizi ni baadhi ya kazi za waziwazi za kimapepo, ni kazi za shetani na majeshi yake, yako na mambo mengine mengi ambayo mapepo huyafanya na ni vigumu kuorodhesha moja baada ya jingine lakini hata hapo umepata picha dhidi ya utendaji wa Ibilisi.
2.      Tabia za pepo.
Pepo kwa vile ni roho wachafu waasi ambao walikuwa malaika wana tabia zinazofanana na za malaika na pia kwa kiwango Fulani wana tabia zinazofanana na wanadamu, popo wana nafsi kwa sababu hiyo wana sifa kadhaa vilevile ambazo tunaweza kuzipata katika maandiko matakatifu
a.      Pepo wana Hisia
Pepo wana hisia na utambuzi, Yesu alipokutana na mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo mengi sana katika inchi ya wagerasi pepo waliweza kuonyesha hisia zao na utambuzi wao kuhusu Yesu, walimuogopa Mathayo 8:28-29 “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?”
b.      Pepo wana uwezo wa kufundisha.
Kwa ujumla wataalamu wote wa uganga na uchawi na wapunga pepo huwa wanafundishwa na mapepo, Hali kadhalika pepo huweza kupotosha ukweli na kusababisha ukengeufu, wanauwezo wa kutumia watumishi wa uongo na kufundisha mafundisho yao, biblia inasema wazi kwamba roho hizi zidanganyazo zaweza kutoa mafundisho, ambayo biblia inayataja kama mafundisho ya Mashetani 1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”
c.       Pepo wana vurugu na wanapiga.
Wakati mwingine ni muhimu kuwa na ufahamu hususani endapo utajihusisha na kazi za kutoa pepo, kwamba pepo wanavurugu wanafanya fujo na wanaweza kupiga, Matendo 19: 13-16. “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa
d.      Pepo hupokea ibada.
Katika namna ya kijanja sana shetani na mapepo hupenda na hutamani kuabudiwa, hivyo kila mtu anapaswa kuwa na ufahamu ni namna gani na jinsi gani atajilinda na utendaji wa mapepo asije akayaabudu, wanao hujificha nyuma ya sanamu, wakipokea ibada, hujificha nyuma ya waganga wa kienyeji na wachawi wakipokea ibada na hujificha nyuma ya dini za uongo wakipokea ibada uwezo wote na nguvu zote za waganga na wachawi na makuhani wa dini za uongo hutegemea nguvu hizi za kimapepo nyuma yake ni muhimu kujihadhari tusiwasujudie mashetani Ufunuo 9:20-21 “Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.”
e.       Pepo wana uwezo wa kufanya ishara na miujiza
Tuliona tangu wakati wa Musa na Haruni jinsi walivyofanya ishara na wachawi wakaigiza sihara zile, Biblia iko wazi kuwa pepo nao huweza kufanya ishara lengo lao likiwa ni kupotosha watu kupitia siashara zao Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”
f.        Pepo wanawajua watu wa Mungu na wokovu.
Kama unamtumikia Mungu kwa dhati na kuhubiri njia sahii ya wokovu pepo wanafahamu, ingawa wakati wmingine wao ni waongo lakini wakati mwingine husema ukweli. Tunapaswa kuwa makini na kuwa na karama ya kupambanua hasa wakati unapotoa nafasi ya kuwasikiliza Pepo Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.”
g.      Pepo wanaamini kuwa yuko Mungu mmoja na wanatetemeka.
Pepo wanafahamu ukweli kuhusu Mungu na wanajua wazi kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, wanatambua kuwa anapaswa kuabudiwa na wanatetemeka, na ndio maana tunapowakemea kupitia jina la Yesu, kwa ufahamu walio nao kuhusu Mamlaka hiyo wanatii na kuondoka. Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka
h.      Pepo wanaweza kuwapagaa wanyama
Biblia inatuonyesha kuwa uko uwezekano wa pepo kuwapagaa wanyama, na hii inatupa ushahidi ulio wazi kuwa wachawi na waganga wanaweza kufanya mambo ya kichawi na kusumbua watu kupitia wanyama mbalimbali Mathayo 8:28-31. “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.          Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe
i.        Pepo wanaweza kuwa wengi ndani ya mtu mmoja.
Biblia inatufundisha kuwa tabia ya pepo katika kuwatesa wanadamu kwamba pia wanauwezo wa kupagaa mtu mmoja huku wao wakiwa wengi na kusababisha madhara makubwa zaidi Luka 11:24-26 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.    Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.      
3.      Nyadhifa na mamlaka za mapepo.
Biblia inaonyesha wazi kuweko kwa mamlaka za kipepo kama zilivyo mamlaka za Malaika kwamba mapepo kuanzia na shetani yana protokali zake Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu”Wakolosai 2:15 Biblia inaonyesha kuwa ziko enzi na mamlaka “akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.” Kwa msingi huo unaweza kuona kuwa biblia inagusia kuwepo kwa enzi na mamlaka za kipepo katika namna isiyokuwa ya kawaida Nabii Daniel pia anasaidia kujua namna na jinsi mamlaka za kipepo zilivyojipanga kwamba kuna pepo linalotawala kwa kila Taifa au ufalme na uko wezekano mkubwa kuwa pepo hao wakawa wamejipanga mpaka katika kiwango cha mkoa, wilaya, tarafa kata, kijiji, kitongozi na hata kifamilia (Family spirit) kwa msingi huo unaweza kuona kuwa katika mpangilio wa Mapepo na utawala wa shetani hali hii inawezaikawa inafanana na mpangilio wa uongozi wa shetani.,Daniel 10:13,20-21

1.      SHETANI
(Mungu wa Dunia hii, na Mfalme wa Uweza wa Anga, Mkuu wa ulimwengu huu)
2Wakoritho 4:4,Yohana 12:31
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru” ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.”
2.      WAKUU WA NCHI FALME AU MAMLAKA
Waefeso 6:12, Daniel 10:13,20
Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT) kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.
3.      MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Waefeso 6:12,
Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
4.      MAAJENTI WA SHETANI NA MAPEPO
Waefeso 6:12 c “juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Hawa ni binadamu ambao wanafanya kazi kwa niaba ya shetani, kundi hili ni pamoja na waganga, wachawi, wanga na wengineo
Majeshi haya ya Pepo hufanya kazi mbalimbali za uharibifu na wamejipanga vema katika kuhakikisha utaratibu wao wa uharibifu unafanikiwa
5.      MAPEPO WALIOFUNGWA
Yuda 1:6
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.”
Mungu Katika hekina yake amewaweka kifungoni baadhi ya Mapepo kutokana na uwezo wao mkubwa wa uharibifu, aidha baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa aina hii ya mapepo inaweza kuruhusiwa wakati wa dhiki kuu na watahusika kipekee katika kuleta mateso na uharibifu mkubwa kwa binadamu wakati wa dhiki kuu.
Majina ya Mapepo na kazi zao
Mapepo yana majina mengi tofauti tofauti kutokana na tabia, vyeo na kazi zao, waislamu wanasema kuna majina yapatayo 99 ya majini, Katika ukristo Shetani ametajwa kwa majina kadhaamachache kulingana na tafasiri ya kazi zake lakini kwa mujibu wa Mtandao wa unexplained-mysteries.com ambao unafundisha kuhusu Mapepo na vyeo vyao tunafunuliwa kazi kadhaa za mapepo kupitia majina yanayotumika katika jamii mbalimbali
Apollyon (Abaddon) : King of Demons- Mfalme wa Mapepo
Abigor: Horseman with a scepter and lance, commanding 60 legions, Kiongozi wa kikosi cha farasi anayeongoza Majeshi 60 ya mapepo, kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000
Adremelech: Chancellor and High Council of Demonds – Kiongozi mkuu wa halimashauri kuu ya Mapepo
Aguares : Grand Duke of Eastern region, commanding 30 legions- Mtawala wa Mashariki anayeongoza Majeshi 30 ya mapepo kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000
Alocer : Grand Duke , commanding 36 legions - Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36 ya mapepo
Amduscius : Grand Duke, commanding 29 legions, -Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 29 ya mapepo
Andras : Marquis , commanding 30 legions- Mtawala anayeongoza Majeshi 30 ya mapepo
Asmodeus (Asmoday) : Head of Casinos, Mkuu wa anasa za Makasino na Majumba ya Starehe
Astaroth : Grand Duke of Western region, Lord Treasurer, Mtawala wa Magharibi na Mtunza hazina wa mapepo
Aym : Grand Duke , commanding 26 legions, Mtawala wa kati anayeongoza majeshi 26
Ayperos : Prince, commanding 36 legions- Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36
Azazel : Standard Bearer of Armies, also known as Satanael.Mpambe wa Majeshi
Baal : Commanding General of the Infernal Armies, Mkuu wa Majeshi ya Mapepo yanye makelele sana ya kuzimu
Baalberith : Chief Secretary and Archivist (second order demon, Berith)Katibu mkuu wa mipango ya kipepo
Balan : Prince, Mfalme
Bearded Demon : Remains nameless to avoid his use in search of the Philosopher's Stone (King Solomon)Mfalme wa maswala ya ujenzi wa kutumia mawe
Beelzebub (Beelzebuth) : Prince of the Demons, Lord of the Flies, second only to Satan
Mfalme wa Mapepo, Mungu wa mainzi ni mamlaka ya pili kutoka kwa Shetani
Belial : Prince of Trickery, Demon of Sodomy- Mfalme wa Hila na mtawala wa maswala ya ulawiti na ufiraji na mapenzi ya jinsia moja
Belphegor : Demon of Ingenious discoveries and wealth, Pepo la maarifa na ugunduzi na utajiri
Buer : Second order demon but commands 50 legionsMamlaka ya kipepo inaongoza vikosi vya majeshi ya pepo 50 kumbuka kila jeshi au kikosi ni pepo 6000
Caym : Grand President of the Infernal Rais wa kuzimu
Charon : Boatman who ferries souls across the river Styx-Pepo la maji na mito
Chax : Grand Duke- Pepo dume mkuu
Cresil : Demon of Impurity and slovinliness- Pepo la uchafu na kutokujali, uvivu na uhovyohovyo
Dagon : Baker and member of the House, Pepo la mapishi na nyumbani
Eurynomus : Prince who feeds on corpses,
Furfur : Count , commanding 26 legions
Geryon : Giant centaur, guards hell
Jezebeth : Demon of Falsehoods
Kasdeya : According to the "Book of Enoch", the fifth Satan
Kobal : Entertainment Director, patron of Comedy
Leonard : Inspector General of Black Magic and Sorcery
Leviathan : Grand Admiral: androgynous ( Christian myth says he seduced both Adam and Eve)
Lilith : Princess of Hell. ( Hebrew myth is that she is a succubus)
Malphas : Grand President, commanding 40 legions
Mammon : Demon of Avarice
Mastema : Leader of the offspring of fallen angels by humans
Melchom : Treasurer of the House
Mephistopheles : Some versions a servant of Lucifer, others Satan himself
Merihim : Prince of Pestilence
Moloch : Another demon of Hebrew lore
Mullin : Servant of the House of Princes, Lieutenant to Leonard
Murmur : Count, Demon of Music
Naburus : Marquis, connected with Cerberus
Nergal : Chief of Secret Police, second order demon
Nybras : Grand Publisist of Pleasures, inferior
Nysrogh : Chief of the House of Princes, second order demon
Orias : Marquis, Demon of Diabolic Astologers and Diviners
Paymon : Master of Ceremonies
Philatanus : Demon assisting Belial in furthering sodomy and pedophile behaviors
Proserpine : Princess of Hell ( some say, close to Persephone of Pagan traditions)
Pyro : Prince of Falsehoods
Raum : Count, commanding 30 legions
Rimmon : Ambassador from hell to Russia, also known as Damas
Ronwe : Inferior, yet commands 19 legions
Samael : Angel of Death, Prince of Air
Semiazas : Chief of Fallen Angels
Shalbriri : Demon that strikes people blind
Sonneillon : Demon of Hate (Michaelis )
Succorbenoth : Chief Eunuch of the House of Princes, Demon of Gates and Jealousy
Thamuz : Ambassador of hell, Creator of the Holy Inquisition, Inventor of Artillery
Ukobach : Stationary Engineer
Uphir : Demon physician
Valafar : Grand Duke
Verdelet : Master of Ceremonies of the House of Princes
Verin : Demon of Impatience
Vetis : demon who specializes in corrupting and tempting the holy
Xaphan : Stokes the furnace of hell, second order demon
Zaebros : Animal - human combination
Zagan : Demon of Deceit and counterfeiting
Ufahamu kuhusu vita vya kiroho.

Ni muhimu kufahamu kuwa katika nyakati za agano jipya biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba kila mtu aliyemwamini Yesuyuko katika mapambano, tunapambana wazi kabisa na nguvu za yule muovu Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.       Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba tuko katika mapambano yasiyoonekana, ni mapambano dhahiri kati ya ufalme wa giza na ufalme wa Nuru, ufalme wa shetani na ufalme wa Mungu.

 Linaendelea.....................................................................

Jinsi ya kuwashinda Pepo.
1.      Lazima uwe Hodari Yoshua 1:6  Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.” Biblia inazungumzia Uhodari, kwa kuwa kuwashinda Pepo ni vita vya kiroho basi jambo la kwanza ni kuwa Hodari, kuwa hodari maana yake ni kuwa na uzoefu wa vita mbalimbali za kiroho, uwe mpambanaji, kama unaytaka kuwa huru au kuweka wengine huru kutoka katika nguvu za giza basi huwezi kuepuka kuepuka agizo la kuwa Hodari, popote biblia inapozungumzia vita inazungumzia UHODARI, Angalia Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.     Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Mashujaa wote wa Imani katika Biblia wanatajwa kuwa walikuwa Hodari katika vita angalia Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;           ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Unapotaka kuwashinda maadui na kufukuza majeshi ya wageni unapaswa kuwa hodari, neno Uhodari katika kiibrania linatajwa kama neno “Mashal” ambalo maana yake ni kufanya zaidi ya jinsi ulivyofundishwa, ni weledi katika kupambana na maadui, lazia kila anayetaka kupambana na shetani ajue kuwa anapaswa kuwa na ujuzi na ukomavu katika imani, ni lazima uwe na mamlaka na ujuzi wa mamlaka ya kupambana na majeshi ya mapepo na uhodari huu unafichwa katika uzoefu wa vita na imani.
2.      Ni lazima uwe na Mafuta ya Roho Mtakatifu. Luka 4:18- 19 “Yesu alisema maneno haya muhimu sana Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”. Yesu Kristo anaonyesha wazi kuwa ili kuweka watu huru tunahitaji Upako yaani tunahitaji kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu, Roho wa Bwana akiwa juu yetu na kutupaka mafuta tuaweza kuwafungua waliofungwa, tutaweza kuwaweka watu huru kutoka katika upofu,tutaweza kuwaweka huru waliosetwa yaani wanaoonewa wote hao ni kutoka katika vifungo mbalimbali na uonevu wa Ibiblisi, Nabii Isaya anaonyesha wazi kuwa njia ya kuwashinda maadui na kujilipiza kisasi na kuondoka katika mizigo yao ni kwa kupitia mafuta angalia Isaya 10:24-27 24. Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri. Maana bado kitambo kidogo tu ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza.Na Bwana wa majeshi ataamsha mjeledi juu yake, kama vile alivyopiga Midiani karibu na jabali la Orebu; na fimbo yake itakuwa juu ya bahari, naye ataiinua kwa namna ya Kimisri. Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta”.
3.      Ni lazima umfunge kwanza yule mwenye nguvu. Mathayo 12:28-29 “Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.    Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.” Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu alizungumza nini katika eneo hili, kwa uwazi wote tunajua kuwa miili yetu ni nyumba Biblia inasema kwa wale waliookoka kuwa waoa ni Hekalu la Roho Mtakatifu 1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;” Kama mwili wa mtu aliyeokoka ni Hekalu au nyumba ya roho Mtakatifu ni wazi kuwa mtu asiyeokoka ni nyumba ya pepo angalia Mathayo 12:43-45 “43. Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.” Kumfunga yule mwenye Nguvu basi kwa maana ya Yesu ni kushughulika na mwenye nyumba zaidi yaani ni kumshughulikia Shetani na kupindua ufalme wake na kumuingiza mmiliki mwingine yaani Yesu Kristo ili atawale maisha ya mtu huyo, ili pepo wasiweze kummiliki mtu ni lazima shetani afungiwe kabisa na kutupwa nje, ni rahisi sana mapepo kuondoka yenyewe ikiwa ufalme wake umepinduliwa, mapepo hufanya kazi chini ya utawala wa shetani, mtu akimpokea Yesu anapewa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu na hivyo ufalme wa giza hupinduliwa na Yesu huchukua nafasi yake na hivyo wajumbe wa shetani yaani mapepo huondoka bila shida Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
4.      Shugulikia kiti cha enzi cha Shetani Ufunuo 2:12-13 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI CHA SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, HAPO AKAAPO SHETANI”. Ni muhimu kufahamu kile anachokizungumza Yesu hapa Pergamo, Pagamo ndio ulikuwa mji mkuu wa kisiasa katika ugiriki ya zamani nyakati za leo ni uturuki, mjii huu ulikuwa na hadhi ya kipekee kwa kuwa hali ya ushawishi wote ilianzia hapo katika asia ndogo ya zamani, ulikuwa ni mji wenye wagunduzi na waanzilishi wa maswala ya mambo mbalimbali, lakini hata mauaji ya wakristo yalianzia kwa kasi katika mjii huu, Lugha anayoitumia Yesu kutaja kiti cha Enzi cha shetani ilikuwa inamaana kuwa wakati huu ushawishi mkuu wa ibilisi ulikuwa unatokea katika eneo hilo, hivyo Pagamo palikuwa ni makazi ya Ibilisi, hii inatupeleka mbali zaidi kuwa shetani anaweza kufanya makao ndani ya mtu, ndani ya familia, ndani ya ukoo, ndani ya kijiji, ndani ya kitongoji, ndani ya kata, nadani ya tarafa, ndani ya wilaya ndani ya mkoa na ndani ya taifa, bara na kadhalika, ni muhimu kumfunga na kuharibu kila kinachoonekana kuwa ni utawala wa ibilishi na kusimamisha utawala wa Mungu kama ilivyo katika kipengele kilichopita

Angalia shuhuda hizi kutoka kwa Joseph Ntandu alipokuwa akifundisha kuhusu umiliki na kuwashinda wakuu wa giza Nanukuu..
Mchungaji Yonggi Cho
apambane kwa maombi na mkuu yule giza. alipomshinda kwa maombi kupitia jina la YESU ndipo huduma yake ilistawi na huduma hiyo imefikia hatua ya sadaka zinahesabiwa kwa zaidi ya siku 2 na sadaka hiyo kuipeleka bank ni kwa msafara mkubwa kukiwa na ulinzi mkubwa wa Polisi wengi.
Ndugu, ukishinda katika ulimwengu wa roho hata katika ulimwengu wa mwili utashinda pia.
#Askofu Moses Kulola kabla ya kuanza kuhubiri injili ya mafanikio makubwa katika Tanzania aliingia katika maombi ya kufunga siku 4 mlimani. Katika maombi hayo akiwa katika siku ya mwisho ya maombi aliona jitu kubwa la kutisha likija alipo na lilipokaribia lilimwambia kwanini anataka kulichukua eneo lake huyo mkuu wa giza, yaani
Tanganyika kwenye ulimwengu wa roho wa giza kulikuwa na mtawala wake ambaye ndiyo huyo roho ya kuzimu, kwa maombi Askofu Moses Kulola alimshinda yule mtoto wa shetani ndio maana akaanza kuhubiri injili ya mafanikio sana. Kila Eneo huwa lina utawala wa aina tatu. Kuna utawala wa kibinadamu, kuna utawala kutoka ulimwengu wa roho wa giza na utawala wa MUNGU hutawala pote na una mamlaka ya mwisho.
Kumbe ili ulipate eneo fulani kwa ajili ya kitu fulani chako chema inabidi kwa maombi umpige mkuu wa giza wa eneo husika. Mwisho wa kunukuu.
Kumbe basi ili kuweza kuyashinda mapepo hatuna budi kuhusika kipekee katika kushughulikia viti vyao vya enzi na kuvisambaratisha.
5.      Tumia jina la Yesu. Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.” Pepo wanaweza kutii pale unapolitumia jina la Yesu, kumbuka kuwa ni Yesu ndiye aliyetoa amri na agizo la kutoa pepo, hivyo huwezi kutoa pepo kwa namna nyingine yoyote kanuni ni lazima ulitumie jina la Yesu Marko 16:15-18 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;         watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya
6.      Hakikisha kuwa unamtii Mungu na kumpinga shetani Yakobo 4:7 Biblia inasema “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Utii kwa Mungu unaongeza Mamlaka yetu dhidi ya pepo waovu na maasi mengine yote ya ibilisi, Utii wetu na uchaji wetu kwa Mungu hutupa nafasi na kibali cha juu sana cha kusikilizwa na Mungu, Waebrania 5:7-9. Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtiiNi kutokana na utii aliokuwa nao Yesu alisikilizwa sana na Mungu, Yesu mwenyewe alishuhudia kuwa Mungu anamsikia siku zote yaani mara zote Yohana 11:41-42 “Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenitumaUtii na ushirika na Mungu utakufanya usikilizwe siku zote na shetani akukimbie tunaona jinsi maisha ya Yesu yalivyojaa utii na unyenyekevu jambo lililopelekea kuadhimishwa mno na kila kitu kuwekwa chini yake Jina lake limekuwa juu ya majina yote na ameadhimishwa sana kama maandiko yasemavyo lakini sababu kuu ikiwa ni utii Wafilipi 2:8-11 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” Biblia inaonyesha wazi kuwa kuna viwango tofautitofauti vya kusikiwa na Mungu na si kila mtu anaweza kusikilizwa tu ziko ngazi ambazo unaweza kuzifikia kwa utii na Mungu akakusikiliza na katika kiwango hichohicho cha utii mamlaka yako dhidi ya Ibilisi ikawa kuu mno Yeremia 15:1 “Ndipo Bwana akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu MUSA NA SAMWELI, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.” Unaona Kumbe biblia inaonyesha wazi kuwa Musa na Samuel walikuwa na ushawishi mkubwa kwa Mungu hii ina maana Mungu aliwasikiliza sana watu hao, Katika Ezekiel Mungu anawataja watu wengine ambao yeye huwasikiliza Ezekiel 14:14 “ wajapokuwa watu hawa watatu, NUHU, NA DANIELI, NA AYUBU, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU  Biblia pia imewataja Nuhu, Daniel na Ayubu kwamba ni watu ambao Mungu angeweza kuwasilikiza Kama utajongea katika kujiongeza kutii ndivyo ulimwengu war oho unavyoweza kukusikiliza na kutii na ndivyo mamlaka yako inavyoweza kuongezeka juu zaidi.
7.      Isipokuwa kwa kufunga na Kuomba
Ni muhimu kufahamu kuwa kutokana na ngazi na mamlaka walizonazo pepo ambazo ni sawa na mamlaka za kijeshi, kila mtoa pepo anapaswa kukumbuka kuongeza mamlaka yake kwa kutii, lakini kama Yesu anavyotufundisha ni wazi kuwa aina nyingine za pepo hawatoki kwa mtu anayeomba maombi ya kawaida tu, wakati mwingine ziko aina nyingine za Pepo watatoka kwa kujumuisha maombi na kufunga angalia mfano wa aina hizo za pepo kama pepo wanaohusika kuleta kifafa  Mathayo 17:14-21Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Unaweza kuona pia katika Marko 9:17-29Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu.  Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu.  Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.  Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.”
8.      Ni lazima kuharibu kazi zake 1Yohana 3:8atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi” Ilikuwa mbali na nguvu za giza ni lazima kazi zote za ibilisi zivunjwe na kuharibiwa hapa kuna jambo pana sana la kujifunza, Kazi ya kwanza ya ibilisi ni kuhakikisha watu wanafanya dhambi, kuishi katika dhambi ni kuishi katika uharibifu, ni ugonjwa mkubwa wa kiroho unaoweza kuruhusu magonjwa mengine ya mwili naya kipepo pia Marko 2:17Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” Kusudi kuu la Yesu Kristo kuja ni kuleta uzima na sio hukumu Yohana 3:17Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”.          Tunaposhughulika na kuharibu kazi za ibilisi maana kuu ni pamoja na kuhakikisha watu wanaondolka katika dhambi, ama tunaacha dhambi ili tuwe mbali na utendaji wa shetani, lakini vilevile kuharibu kazi nyingine za ibilisi ni pamoja na kuhakikisha kuwa tunajiepusha na shughuli zote za utendaji wa ibilisi au kazi zile ambazo nyuma yake shetani anaweza kujificha na kuzitumia kuleta madhara ya kiroho
-          Ushishiriki ibada za kimila/kimapepo/kishetani 1Wakoritho10:20-21 “. Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani
-          Ikimbieni ibada ya sanamu 1Wakoritho 10:14Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.” Ni wazi kuwa ibada ya sanamu ni kazi nyingina ya ibilisi, biblia ilikwisha kukataza kuabudu au kutengeneza au kuzitumikia sanamu za aina yoyote ile Kutoka 20:2-6 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”. Vijana kama Shedrak, Meshack na Abednego wanaotajwa katika Daniel walikuwa tayari hata kuangamiza maisha yao kuliko kuabudu sanamu hii ilitokana na msimamo ulio wazi kwao kwamba kuabudu sanamu kungemaanisha wazi kuwa wanaabudu miungu mingine na kuabudu miungu mingene ni uhalisia ulio wazi kuwa ni kuabudu mashetani hivyo walimtumaini Mungu naye akawaokoa Daniel 3:1-18Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,  wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.  Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi.    Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza, Ee mfalme, uishi milele. Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto uwakao. Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha” Ni lazima watu wakatae kuabudu sanamu kwa gharama yoyote nyuma ya sananu yako mashetani yakitafuta kuabudiwa, yako mapepo, Vijana hawa alikataa kazi hizi za ibilisi kuabudu sanamu kungeweza kuleta laana ya Mungu kwa kizazi cha wanadamu hata cha tatu na cha nne, lakini Rehema za Mungu yaani kama tutamcha zinaweza kudumu pia kwa vizazi vyetu
-          Choma moto vifaa vyote vya uganga na uchawi Matendo19:18-20 18. “Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu.    
Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu”Unaweza kuona Biblia inasema watu wa Efeso walidhihirisha matendo yao, yaani walionyesha wazi kuwa wao na kazi za ibilisi basin a hivyo waliamua kuziharibu kabisa ona kwamba vitabu hivyo viligharimu fedha 50,000/- yaani sawa na shilinga 34,000/- ya mwaka 1952, Mji wa Efeso walikuwa wakiabudu sanamu na miungu na walishiriki uchawi na uganga lakini walipoiamini injili walaiharibu kabisa kazi za ibilisi, ni muhimu kwa kila mtu anayetaka kuwa huru kuharibu kabisa, Hirizi, kuharibu tunguli, kuharibu na kuchoma mapembe na kuacha kabisa ushirikina, achana na wapunga pepo na wapiga madogoli na ibada zote za mizimu na kishetani, achana na misa za wafu kabisa, achana na ubashiri wa nyota, kupiga bao na ramli, ngoma za mashetani,kujizindika, kuchanjia muku, kupandisha mapepo, sadaka za kuchinja, makafara ya watoto au ndugu,kunuiza, namba za kichawi, kwenda kwa waganga wa kienyeji, ulaji wa nyama za binadamu,kushiriki bahati nasibu, kucheza kamari, maswala ya kuondoa nuksi na mambo yanayofanana na hayo hizi zote ni kazi za shetani ambazo zinapaswa kuharibiwa.
9.      Usiwaruhusu peo kuzungumza Marko 1:34Biblia inasema  Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.” Yesu hakuwaruhusu pepo kuzungumza biblia inasema kwa sababu walimjua, hata hivyo ziko sababu nyingi ambazo zinaweza kujumuishwa hapa kwanini Yesu hakuwaruhusu Pepo kuzungumza Luka 4:41Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo”. Kama tulivyosema awali kuwa ziko sababu kadhaa kwanini Yesu hakuwaruhusu Pepo kuzungumza
a.       Shetani anaitwa baba wa uongo angalia katika Yohana 8:44 na Mwanzo 3:4 ni wazi kuwa Mashetani au mapepo yana tabia sawa na ile ya shetani hakuna kweli ndani yake hata siku moja Yohana 8:44Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Kama shetani ni muongo asemapo uongo hujihakikishia tabia yake hivyo hakuna pepo mkweli, pepo wanaweza kusema kweli mara kadhaa lakini hatuhitaji ukweli wao hata kidogo, Mapepo yalikuwa yanamjua Yesu kuwa ndio Masihi lakini Kristo hakukubali kudhihirishwa na Mapepo watu wapinzani walishamsema kuwa anatoa pepo kwa mkuu wa pepo, na hivyo kuyaruhusu mapepo kuzungumza hata kama yangesema kweli, ilikuwa ni kutia mafuta ya petrol katika moto, lakini tukijifunza kutoka kwa Yesu Kristo hii inamaanisha wazi kuwa hatupaswi kuwasikiliza Mapepo, wako watumishi mbalimbali hasa wenye karama za kinabii huchukua mud asana kuwahoji pepo, kufanya hivi wakati mwingine kunaweza kuruhusu fitina na mafarakano miongoni mwa watu
b.      Kuwaachia pepo kuzungumza kungemaanisha kuwa huna mamlaka dhidi ya pepo, pepo wameumbwa kijeshi, jeshini hakuna mazungumzo na muhalifu ni amri, hatujapewa nafasi ya kuzungumza na pepo tumepewa amri ya kutoa pepo, kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuwafunga na kuwaamuru kutoka tu Marko 8:33Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” Yesu hakutoa muda hata kusikiliza mawazo ya shetani, kuwanyima pepo kuzungumza kunaonyesha jinsi ambavyo pepo hao wanatii mamlaka iliyokuu kwa jina la Yesu Luka 10:17Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.”
c.       Kuwahoji pepo ni kupoteza Muda, angalia huduma zifanywazo na wanaotoa pepo katika mtindo huo huku wakiwa na umati mkubwa wa watu wanaohitaji huduma kumbuka Yesu alikuwa na watu wengi sana aliokuwa akiwahudumia angalia biblia inavyosema Marko 1:34Biblia inasema  Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.” Je watu wengine wanaohitaji huduma watafunguliwa saa ngapi kama bwana yesu angehusika kuhoji waliopagawa mmoja mmoja  nafahamu kuwa kuna wakati Yesu aliliuliza pepo jina lako nani Luka 8:30Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”Katika kifungu hiki Yesu aliuliza jina la pepo kwa kusudi la kutufundisha kuwa pepo wanaweza kuwa wengi katika mtu mmoja katika mstari wa habari hii hii katika injili nyingine neno Jeshi limatajwa kama neno Legion angalia Marko 5:9Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.”jina hilo la kilatini Legion lilikuwa na maana ya kikosi cha askari wapatao 6000 kusudi kuu la Yesu ni kuonyesha jinsi ambavyo mapepo hao wakiokuwa juu nya mtu mmoja walivyokuwa wengi na kwa kusudi hilohilo aliwaruhusu kwa nguruwe 2000 kumaanisha au kuonyesha mateso makubwa alivyokuwa nayo mtu yule, hivyo pepo wanaweza kuulizwa swali kwa kusudi tu lakini si kila wakati
d.      Yesu hali kadhalika hakutaka kudhihirishwa kuwa yeye ni Masihi kupitia roho wa uongo hata kama walisema kweli, Miujiza aliyoitenda Kristo pekee ilikuwa inatosha kuonyesha wazi kuwa yeye ni masihi Mathayo 11:4-6, Luka 7:21-23 na miujiza yake yote ilitabiriwa katika Isaya 29:18, 35:4-6 kwa sababu hiyo hakupenda kudhihirishwa na mapepo, ni jambo kama hili ndilo lililomuudhi Paulo, hatupaswi kuthibitishwa ubora wa utumishi wetu kupitia mapepo, tusifurahi kwa sababu pepo wanatutii bali kwa sababu tunajulikana mbinguni yaani majina yetu yameandikwa mbinguni.
10.  Watu wengi wasikemee pepo mmoja au kwa pamoja
Kumekuweko na tatizo kubwa sana kwa jamii ya wapentekoste au watu wenye kuhusika na kuwafungua wenye pepo, kumbuka pepo wameumbwa katika mfumo wa kijeshi na hivyo hupokea amri kijeshi, unapokuwa jeshini kisha ukaamriwa na kila kamanda kufanya jambo Fulani unaweza kujikuta unachukua muda mwingi kutafuta yupi wa kumtii kwanza, Pepo hawatatii kwa haraka watu amabao hawajajipanga katika utoaji wa pepo, tunatofautiana viwango vya amri na mamlaka na utii ni muhimu mtu mmoja anapokemea pepo wengine wakawa kimya kinyume na hilo itawachukua muda mrefu sana kumfungua mtu anayeteswa na Mapepo.

Jinsi ya kutoa Pepo
Kazi ya kanisa ni kuhubiri injili, kazi hii ya ufalme wa Mungu katika agizoa lake kwa ujumla pia inahusisha kutoa pepo, Marko 1:21-27, Kutoa pepo pia ni ishara ya kila mtu anayelitimiza agizo kuu na aliyemwamini Yesu Kristo Marko 16:17
Lengo kuu la Mapepo ni kutimiza Mapenzi ya kiongozi wao amabaye ni ibilisi, kama ilivyo kwa wakristo wanapenda kutimiza mapenzi ya Mungu, mashetani hutimiza mapenzi ya baba yao ibilisi, wakijua wazi kuwa hawamwezi Mungu wanataka kumuuzi Mungu kwa kuwaonea wanadamu ambao Mungu anawapenda upeo
Wanataka mkuiba ibada 1Wakoritho 10:19-21
Wanataka kuwaweka wanadamu katika utumwa wa hofu magonjwa na tabia mbaya ili kuharibu sura ya Mungu ndani yao.
Wanawapiga watu upofu ili wasiikubali injili Matendo 10:38, 2Wakoritho 4:4, 2Timotheo 2:25 na Waebrania 2:14
Mapepo hudanganya Yohana 8:44, 1Timotheo 4:1 2Patro 2:21
Mapepo yanaua na kusababisha machafuko na kudhuru wanadamu Yohana 8:44
Mapepo yanatesa Mathayo 12:22, Luka 13:11-17,Ayubu 12:22
Mapepo yanatia watu ukichaa Luka 8:27-29
Mapepo yanaongoza katika uchafu wa kingono  Mathayo 10:1, Marko 1:23,3;11
Mapepo huzuia kazi ya injili 1Thesalonike 2:18
Mapepo yanafundisha uchawi Torati 32:16-17 ISamuel 15:23
Mapepo yanaongoza kuabudu Mizimu 1Wakoritho 10:19-20

Mapepo hupagaa watu
Kupagaa ni kitendo cha kudhuru na kutawala kwa namna mbalimbali, Mapepo yanapokuwa yamempagaa mtu maana yake huingia ndani ya mtu na kutawala maisha yake kwa sehemu au yote, hii inaweza kutokea pia mtu huyo akawa anafanya vitu nje ya akili zake za kawaida, mtu anapokuwa amepagawa kunaweza kuwekokwa dalili zifuatazo
1.      Mabadiliko ya mtu huyo Marko 9:26
2.      Nguvu za kupita kawaida Luka 8:29
3.      Ufahamu usioweza kuelezeka Matendo 16:16-17
4.      Mateso ya kupita kawaida ikiwemo upofu, uziwi au ububu  Marko 1:26, Mathayo 12:22-30, 9:32-34
5.      Kujichukia kujiua na kujifanyia vitendo vya ukatili Marko 9:22,5:5
6.      Kuogopa jina la Yesu au kumuogopa Yesu mwenyewe Marko 1:24
Mapepo hayawezi kumpagaa Mkristo wa kweli
Inagawa mapepo hayawezi kumpagaa mkristo wa kweli bado mapepo yanaweza kumjaribu, au kumtia majaribuni, kumdanganya, kumshambulia, na kumtesa kutokea nje lakini ni vigumu kumpagaa kupagaa ni kudhibiti kabisa ufahamu na maamuzi ya mtu hivyo kwa mkristo aliyezaliwa mara ya pili yaani aliyeokoka ni vigumu na haijawahi kuthibitika kuwa anaweza kuwaliwa na Mapepo, lakini uwezekano wa Mkristo kupagawa na pepo unaweza kutokea kwa Mkristo aliyerudi nyuma au kukengeuka

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Rev. Innocent Kamote.

Still underconstructions / bado linamatengenezo!

Maoni 2 :

  1. Nimepokea maarifa katika utendaji wa kazi ya Mungu.

    JibuFuta
  2. Ubarikiwe kwa mafundisho haya.

    JibuFuta