Ijumaa, 8 Desemba 2017

Huyu ndiye Rais Halali wa Kenya!




Uhuru Muigai Kenyatta.

Uhuru Kenyata alizaliwa tarehe 26 October 1961 ni moja ya wanasiasa mahiri na raisi  wa awamu ya nne wa jamhuri ya Kenya.

Mheshimiwa Kenyatta amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Gatundu ya kusini kati ya mwaka 2002 mpaka 2013, Kenyatta ni mtu aliyejaa upendo, imani, na mwenye kuheshimu utu, ni mpole na mnyenyekevu, ni mpenda maendeleo na ni mtu anayeipenda Afrika kwa dhati na mwenye moyo wa Kumcha Mungu.

Kabla ya kuwa raisi wa awamu ya nne wa Kenya ndugu Kenyata amewahi kuwa mwanachama wa Kenya African National Union, chama ambacho kilihusika kudai Uhuru wa Kenya chini ya baba yake Mzee Jomo Kenyatta. Kwa sasa Kenyatta ameingia madarakani kwa tiketi ya chama cha “Jubilee” jina ambalo kwa asili ni la kibiblia lenye kuzungumzia mwaka wa Bwana wa kuwaweka huru watu wake sawa na Luka 4:18-19. “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”  Neno mwaka wa Bwana uliokubaliwa kibiblia ndio ulijulikana kama Jubilee.

Uhuru Kenyatta ni moja ya watoto wa kiume wa aliyekuwa rais wa Kwanza wa jamhuri ya Kenya na mama yake Mama Ngina Kenyatta ambaye kwa bahati nzuri bado yu hai, Mheshimiwa Uhuru alishinda Uchaguzi  kwa mara ya pili August 2017 katika uchaguzi mkuu na kupata ushindi kwa asililia 54% kupitia kura za wakenya wote waliokuwa wamejiandikisha, Hata hivyo ushindi huu uliokuwa umetangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi wa nchi hiyo “Independent Electoral and Boundaries Commission” Ndugu Wafula Chebukati. Ushindi huu ulipingwa kisheria na mahakama kuu nchini humo baada ya kuzingatia madai ya muungano wa vyama pinzani unaojulikana kwa ufupi kama NASA uonaoongozwa na “Raila Odinga” kwa kuzingatia madai kadhaa tarehe 1 September 2017 Mahakama kuu ilibatilisha matokeo hayo na kuamuru kuwa uchanguzi urudiwe tena tarehe 26 October 2017 yaani ndani ya siku 60 tangu kutanguliwa kwake, hata nhivyo katika namna ya kushangaza uchaguzi huu wa marudio ulipingwa na kukosolewa vibaya  na wapinzani na watu wa maswala ya haki za binadamu, Huku mpinzani mku Raila Amolo Odinga akisusia uchaguzi huo.

Maswala kadhaa ya ya uvunjifu wa amani yalijitokeza kwaajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliorudiwa kwa mara ya pili, huku wafuasi wa raila wakiandamana katika mitaa kama Kawangware,  Nairobi na maeneo mengine wakipinga vikali na kuchoma moto maduka na kuchoma matairi, watu kadhaa walijeruhiwa na wengine kufariki dunia, waandamanaji walikuwa wakimtaka Raila kuchukua hatua, kabla ya kura kurudiwa tena,  Huku yeye mwenyewe akiwachochea wafanye fujo na kupinga uchaguzi huo kwa madai kuwa hakukuwa na uwanja huru na wa haki wa ufanyikaji wa uchaguzi huo, Na baadaya bwana Odinga alijitoa katika kinyanganyiro hicho cha uchaguzi wa mara ya pili, kutokana na tukio hilo Muheshimiwa Kenyatta alipata nafasi ya kushinda uchaguzi wa Marudio kwa njia iliyo laini zaidi na hivyo kumpa nafasi ya kuiongoza Kenya kwa miaka mitano ijayo.

Katika uchaguzi huo wa Marudia muheshimiwa Uhuru Kenyatta alipata ushindi mkubwa wa kishindo kwa asilimia 98% ya kura zote zilizopigwa, Wakati akiapishwa Rais Kenyata aliahidi kuwa daraja la maendeleo lenye kuwaunganisha wakenya kuwa kitu kimoja na kusonga mbele huku akiweka moyo wake wote, katika Hutuba yake iliyojawa na utukufu wa Mungu Mheshimiwa Kenyata alisoma andiko na Nabii Isaya  akihusisha tukio la kuapishwa kwake tarehe 28/11/2017 kuwa bila Mungu haikuwa rahisi namnukuu 
Today is yet another historic day for our great motherland.  First and foremost, our gratitude is to our Almighty God. The Prophet Isaiah proclaimed: When you pass through the waters, I shall be with you. When you pass through the rivers, they shall not overwhelm you. When you walk through fire, the flames will not consume you, Our God is faithful.  He heard our voices when we cried out to Him.  He listened, and answered our prayers.  He has brought us thus far, and He will take us even further.This is the testimony of our country today; and for this we thank Him
Tafasiri isiyo rasmi Leo ni siku nyingine ya kihistoria katika ardhi mama yetu, Kwanza ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Nabii Isaya alisema, “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.” Mungu wetu ni mwaminifu, amesikia sauti zetu tulipomlilia na kuhitaji msaada wake. Amesikia na kuyajibu maombi yetu, ametufikisha hapa leo na atatuvusha zaidi ya hapa na huu ni suhahidi ulio wazi leo na kwaajili ya hili tunamshukuru mwisho wa kumnukuu
Maandiko yaliyotumiwa na Mheshimiwa Kenyatta ni Isaya 43:2, Ni wazi kuwa Kenyatta hakunukuu maandiko haya hivihivi tu Kenyata pamoja na willium Rutto ambaye siku ile Kenyata alimuita Pastor ni wazi kuwa walimtegemea Mungu, ni wazi kuwa walimtanguliza Mungu mbele, ni wazi kuwa walikuwa na timu kubwa ya watu walioomba pamoja nao na kwaajili yao mapema waimbaji kadhaa walisikika katika uwanja ule wakiimba kuwa sio uchawi ni Maombi, hii ilikuwa ni ushahidi wazi kuwa kuna watu walikuwa wakiomba kwaajili ya wakenya.
Kwanini naandika makala haya, ? wanafunzi wangu wote waliosoma Living Stone Boys’ Seminary ni mashahidi kuwa kwa neema aliyonipa Mungu niliweza kuwatabiria maraisi kadhaa na wakawa katika nafasi nilizowatabiria, akiwepo Rais John Pombe Magufuli, Rais Trump na Kenyatta, Niliwaambia wazi wanafunzi wangukwa vile tulikuwa tunaomba pamoja mara kadhaa nilitaka wayajue mapenzi ya Mungu niliwaambia kuhusu ujio wa maraisi hao madarakani na ikawa kama nilivyowaambia, niliwaambia kuwa mimi sio Muhubiri mkubwa sana kwa maana ya umarufu, wala sijiiti nabii lakini nilimsikia nabii mmoja mkubwa mwenye kituo kikubwa cha tv huko Dar es Salaam akisema wazi kuwa anamuona Raila Ikulu, mimi hapohapo nmilimwambia mke wangu hapana mimi namuona Kenyetta Ikulu, na jiono nilipokwenda kuomba niliwaambia wanafunzi waziwazi kuwa yuko nabii mwenye kituo cha TV huko Dar es Salaam amesema kuwa amemuona Raila akiwa ikulu mimi naomba nieleze wazi kwamba tuiombee Kenya kwani nimeona Moto katikati ya mji, na moshi mkubwa karibu na jengo moja refu sana nchini humo, na tukiomba vema moto huo unaweza kuzimishwa lakini mimi simuoni Raila Ikulu namuona Kenyatta.
Leo ninapoandika naandika mambo haya yakiwa yametimia lakini kwa nini nataka kuandika hili leo nataka kukiri Mbele za Mungu kuwa Kenyatta yuko Kihalali madarakani, si kwa sababu ya uchaguzi kurudiwa, si kwa sababu, ameapishwa lakini kwa sababu Mungu amemchagua na kukusudia awepo na nataka kuitumia nafasi hii kutoa maonyo kwa raila Odinga, kuwa ajihadharina jaribio la kutaka kujiapisha kuwa Rais kwani tukio hili licha ya kuwa na madhara kwa wafuasi wake kadhaa lina madhara makubwa sana kwake mwenyewe, huu ndio utakuwa mwisho wa Raila, kisiasa, kiimani na kwa heshima aliyonayo, litakuwa tukio la aibu kubwa sana kwake na lenye kufedhehesha, kwani licha ya kuwa kinyume cha sheria liko kinyume na Mungu, Mungu hakukuchagua Raila, wala hatakuchagua tena kuwa Rais wa Kenya wakati wowote na nataka kuweka wazi wazi wazi kuwa Rais ajaye wa Kenya mara baada ya Kenyata atakuwa Mcha Mungu zaidi mara mbili ya Kenyatta atalitaja jina la Mungu maradufu zaidi na atatokea Jubelee tena na  Raila hataonekana tena. Katika Historia ya mageuzi nchini Kenya.
Wito kwa wakenya wote tusikubali kamwe kumwaga Damu, tusikubali kushawishiwa na wapinga maendeleo na wapinzani na maadui wa Kenya walioko ndani na nje, Kenyatta anaweza asiwe mkali kama Magufuli, watu hawafanani, lakini moyo wake una mapenzi mema kwa wakenya na Afrika kwa ujumla, Mimi ni Mtanzania sina asili yoyote ya Kenya, lakini nabii hana mipaka kwa vile Mungu ni wa watu wote, lakini Kenya ikiendelea ni Afrika imeendelea, uchumi wa Kenya ukikua ni uchumi wa Afrika umekua,
Naitakia Kenya wakati wa utulivu na wakati wa kufanya kazi na kuachana na aina yoyote ya ushawishi ulio na nia ovu wa kutokuitambua serikali halali iliyoko Madarakani, niwaonye wakenya wote kutokujitokeza tarehe 12 kwaajili ya kuapisha mtu asiyehusika na  wamuache mwenyewe aidha serikali ya Kenya iliyoko madarakani ichukue hatua stahiki na kali za kisheria kwa jaribio hilo la kipumbavu litakalojaribiwa kufanya na uongozi wa Nasa.
Mungu Ibariki Kenya
Mungu Ibariki Afrika
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni