Jumapili, 18 Machi 2018

Nguvu ya Pasaka!


Mstari wa Msingi: Kutoka 6:5-8Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya MIZIGO ya Wamisri, nami nitawaokoa na UTUMWA wao, nami NITAWAKOMBOA kwa mkono ulionyoshwa, na kwa HUKUMU KUBWA; nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA


Utangulizi:

Hivi karibuni wakristo nchini wataungana na wakristo wengine kote duniani kuadhimisha sikukuu ya pasaka, katika wakati huu ni muhimu kujikumbusha kuwa Pasaka inayoadhimishwa na wakristo, inaadhimishwa katika wakati ambapo Wayahudi nao huadhimisha Pasaka yao, wako wakikumbuka kuokolewa kwao Katika Inchi ya misri na sisi tukikumbuka na kuadhimisha kusulubiwa kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo pale Msalabani, Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa Pasaka zote kwa ujumla zinazungumzia Jambo moja la ukombozi na zote zinaashiria nguvu ya ukombozi kupitia damu ya mwana kondoo, na Damu hiyo ni ya Kondoo Halisi ambaye ni Yesu Kristo.

Kutoka 12;12-13Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.


Pasaka zote ile ya Wayahudi na ile ya Yesu Kristo zote zinauhusiano na Damu, Damu wakati wa agano la kale ilitumika kama ishara ya ukombozi na wakati wa agano jipya ni damu halisi ya Yesu Kristo damu hii ina nguvu ya ukombozi kama ilivyokuwa ile ya Mwana kondoo wa pasaka na nguvu hii ndio huitwa nguvu ya Pasaka kwa mujibu wa Rabbi Avraham Brandwein Damu ya Pasaka ina nguvu kuu nne za ukombozi zinazotajwa katika Kutoka 6:6-7 ambao ndio mstari wa Msingi

1.       Kutuondoa chini ya Mzigo – Mzigo ni kila aina ya usumbufu unaotuelemea wa Ulimwengu huu, ni maumivu na mateso ya kila aina ambayo yametusonga na kutosononesha ni kila aina ya kifungo cha ibilisi na nguvu za yule adui zinazo tuonea Yesu Kristo anataka kila mmoja anayelemewa na mizigo kumwendea yeye Mathayo 11:28Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”  
      
2.       Kutuokoa katika utumwa – Israel walikuwa utumwani Misri na wakristo walikuwa chini ya butumwa wa dhambi na Shetani Kazi ya Bwana Yesu Kristo ni kutuweka huru kutoka huko na kufanya kuwa wana wa Mungu, Kazi aliyoifanya Yesu Pale msalabani ilikuwa na kusudi la kutukomboa kutoka katika kila aina ya utumwa Wagalatia 4:4-7Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu

3.       Kutukomboa kwa Mkono ulioonyooshwa – kukomboa kitu maana yake ni kulipa gharama zinazohusika ili kukirejesha kwamuhusika halisia, kitaalamu Mungu alituumba kwa kusudi lake lakini Shetani alitutumikisha na kutuweka chini ya utumwa wa dhambi na chini yake yesu alikuja apate kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhambi Warumi 6:17-18 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.”

4.       Kutufanya kuwa watu wake urejesho  - Yeremia 30:122 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao. Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

 Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni