Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu wazi kwamba
tunaishi katika kizazi ambacho watu wanajaribu kujisahaulisha kuhusu kifo, watu
wanajaribu kusahau kuwa kifo kipo, na kwa namna fulani wanadamu wanajaribu kila
siku kubadili mtazamo wa kifo, kwa kuboresha Majeneza mazuri na kuyapamba kwa
maua kiasi ambacho kifo kinaonekana kama ni monawapo ya sherehe ya kumuaga mtu,
na sio hivyo tu hata makaburi yanapambwa kwa kujengewa vizuri kwa kiasi cha
kugeuka kuwa bustani na maeneo ya kutembelea, hii yote ni kujaribu kukifanya
kifo kionekane kuwa sio kibaya ! Laiki ukweli unabaki pale pale kuwa kifo ni
adui mkubwa sana wa Mwanadamu 1Wakoritho 15:25-26 “Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote
chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”
Kifo ni tamko la Mungu ambalo
limetamkwa kuwa kama mwandamu angemuasi Mungu basi kifo kigekuwa moja ya sababu
ya uharibifu mkubwawa mwanadamu, kwa hiyo tangu mwanadamu anapozaliwa adui
mkubwa anayefuata na kuanza kupambana naye ni mauti.
Yesu aliwajulisha wanafunzi wake
mapema kuwa nao watakufa, tena watakufa kwaajili ya imani katika yeye Yohana 21:18-23 “Akasema,
Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na
kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine
atakufunga na kukuchukua usikotaka. Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa
mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye
huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana,
ni nani akusalitiye?) Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu
je? Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe
unifuate mimi. Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi
yule hafi. Walakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu
akae hata nijapo, imekupasaje wewe?”
Yesu alikuwa amewatabiria wanafunzi wake namna watakavyokufa kwaajili ya imani, na sasa anamwambia Petro namna atakavyokufa kwa utukufu wa Mungu, Petro alimuuliza Yesu je vipi kuhusu Yohana Yesu alimjibu ikiwa nataka huyu akae hata nijapo imekuopasaje wewe? Yaani vyovyote ni takavyo kwamba afe au akae mpaka mimi nijapo wewe inakuhusu nini wewe nifuate! Petron aliuawa huko Roma kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu kama alivyotabiri masihi.
Yesu alikuwa amewatabiria wanafunzi wake namna watakavyokufa kwaajili ya imani, na sasa anamwambia Petro namna atakavyokufa kwa utukufu wa Mungu, Petro alimuuliza Yesu je vipi kuhusu Yohana Yesu alimjibu ikiwa nataka huyu akae hata nijapo imekuopasaje wewe? Yaani vyovyote ni takavyo kwamba afe au akae mpaka mimi nijapo wewe inakuhusu nini wewe nifuate! Petron aliuawa huko Roma kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu kama alivyotabiri masihi.
Hata hivyo historia ya Kanisa
inatuambia kuwa Yohana pekee ndie mtume ambaye hakuuawa bali alikufa kifo cha
kawaida, lakini vilevile kwa mujibu wa mwana historia maarufu wa kanisa
katoliki aitwae Jerome Mtume Yohana alipitia shida dhiki na mateso makubwa sana
kwani yeye aliishi karibu miaka 100, na hivyo alipitia vipindi vya mateso
makali sana, wakati wa utawala wa Tatulian aliweza kusokotwa kwenye majani na
akachomwa moto na alipoamka alijikungu’ta tu na nkuendelea na safari za injili,
wakati wa utawala wa Domitian alidumbukizwa kwenye pipa la mafuta ya lami na
kuchemshwa lakini alitoka akiwa hai, kutokana na kuwa na ugumu wa kifo
alipelekwa uhamishoni kwenye kisiwa kiitwacho patmo iali ateseke na kufia huko,
hata hivyo baada ya muda walikwenda kumchungulia na kukuta akiandika kitabu cha
ufunuo na walimkata mkono, waliporejea mara ya pili walimkuta akiwa na mikono
yake yote, Yohana aliishi maisha ya upweke lakini aliendelea kumuabudu Mungu,
hata siku ya bwana jumapili
aliiadhimisha akiwa katika roho, akiwa amechoka kwa mateso haya Ndipo Yesu
alimtokea na kumuagiza aandike kitabu hiki cha ufunuo, na jambo la kwanza Yesu
alilolifanya ilikuwa ni kumtia moyo, Yesu alitaka kumtia moyo Yohana na kila
mmoja wetu kuwa “Yeye anazo funguo za
mauti na kuzimu”
Yeye aliye na Funguo
za mauti na kuzimu.
Kuwa na funguo za mauti na za
kuzimu maana yake ni kuwa na mamlaka, au uwezo au mamlaka ya mwiho ya kuamua
kuhusu kifo, Yesu ana uwezo juu ya kifo, anauwezo wa kuamua ufe au usife, kama
uwezo huu angelipewa adui yetu angetufutilia mbali mara moja, Lakini ni Yesu
ndiye anayeamua ni yesu ndiye anyeruhusu yeye ndio mwenye mamlaka mwenye
udhibiti Hata maisha yake aliamua yeye mwenyewe kuyatoa na hakuna mtu
aliyaondoa maisha yake ilikuwa ni kwa hiyari yake mwenyewe
Yohana 10:17-18 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.”
Yohana 10:17-18 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.”
Yesu ana nguvu dhidi ya Mauti ana
mamlaka nayo na ni yeye anayeamua kuwa wale wanaomuamini watakufa lini, yaani
lini awachukue wakaungane naye na wakifa awapeleke wapi? Na ni yeye mwenye
mamlaka ya kufufua ni kama Yesu alikuwa
anamwambia Yohana kuwa usiogope Mimi nalikufa na sasa ni hai yaani huoni mfano
wangu? Mauti haina uwezo ndani yangu, kama jinsi ambavyo haikuwa na uwezo juu
yako,
Nisikilize watu wanaweza kujaribu
kukuua kwa maneno na matendo, wanaweza kusema ngoja tuone familia yake
itakuwaje, ngoja tuone mwisho wake utakuaje? Wanaweza kusema hapa amepatikana
hapa tumemuweza, huu ndio mwisho wake, hapa tumemkomesha, hapa hachomoki, hapa
tumemaliza, safari hii tumemuweza, hapa ndio mwisho wa kila kitu, tutaona watasomaje,
tutaona atakwepaje mtego huu, huduma yake itakufa, amekufa kiroho, ameishiwa
hana jipya, duka lake linakufa, biashara yake haiwezi kusimama, hawezi kuzaa
tena, jamaa kwishinei, zilikuwa kelele za bure tuna lolote wanaweza kusema
lakini Neno la Mungu linatuambia ye kuwa yukomwenye funguo, hatupaswi kuogopa
kelele za wasio na funguo, namuogopa mmoja tu mwenye funguo, mwenye mamlaka
ambaye yeye akifunga hakuna afunguaye na akifungua hakuna afunguaye
Ufunuo 3:7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.”
Nataka nikutie moyo leo kuwa usiogope yeye ndiye mwenye kufungua mlango na ndiye mwenye kufunga hakuna anyeweza kushindana naye kama ipo ipo tu, ana nguvu ya kuizuia mauti.
Ufunuo 3:7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.”
Nataka nikutie moyo leo kuwa usiogope yeye ndiye mwenye kufungua mlango na ndiye mwenye kufunga hakuna anyeweza kushindana naye kama ipo ipo tu, ana nguvu ya kuizuia mauti.
Alizuia mauti kwa shadrak, Meshak
na Abednego wakatembea kati kati ya moto, aidha alizuia makanwa ya simba kwa Daniel
aliyetupwa katika matundu ya simba Mungu akaifunga mauti, kumbuka wale simba
walikuwa na njaa , huyu ndiye aliyemsaidia Yohana akaangwe kwenye pipa la lami
na mauti isimuweze, yeye ndiye aliyakufa akafufuka changamka huna sababu ya
kuogopa adui huyu ni mdogo tu.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Amen ...
JibuFutaMungu akubariki kwa kazi hii ya kutufundisha na masomo yako nabarkiwa sana
JibuFuta