Jumatano, 8 Januari 2020

Mwenendo wangu na Mavazi yangu!



Mwanzo 3:21BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Mwanamke wa Kikristo Nchini Syria akiwa Katika mavazi nadhifu kwa mujibu ta tamaduni zao

Utangulizi:
Moja ya mada ambazo zinalitesa sana kanisa kwa miaka mingi ni pamoja na swala zima la Mavazi, swala hili limeleta mijadala mikubwa mno na hata kulifanya kanisa ama watu wa Mungu wakose nini cha kusimamia linapokuja swala la uvaaji, Kuna maswala mengi sana ya kujiuliza katika swala zima la uvaaji, Mwenendo wako na mavazi yako ni swala linalopaswa kujadiliwa kwa kina huku tukiliangalia neno la Mungu linasema nini? 


Mwenendo wangu ni upi linapokuja swala la mavazi, nina mawazo gani linapokuja swala la mavazi, Je ninakubaliana na Maelekezo ya kibiblia linapokuja swala la Mavazi, Je Mungu hivi kweli anajali namna ninavyovaa? Je ninatoa nafasi ya kutosha kwa uongozi wa Mungu katika kuvaa kwangu? Maswali kama haya yakipata majibu yanayojitosheleza ndipo tunapoweza kuona na kujua kuwa swala la mavazi kwa mtu wa Mungu ni swala nyeti sana, wengi tunapenda kuhitimisha kwa kusema tu aaaha swala la mavazi ni swala la fashion na kwa hiyo itategemea na mtindo na dhamiri aliyonayo mtu! 


Ilivyo ni kwamba Biblia ina namana ambavyo inaeleza kwa kina na mapana na marefu namna tunavyoweza kumpendeza Mungu katika mwenendo wetu wote, Neno la Mungu lina muongozo wa kutosha kwa wanadamu namna na jinsi wanavyopaswa kuenenda, swala la mwenendo wetu na kuvaa kwetu hakuhusiani tu na wanawake peke yao, kuna husiana na kila mmoja wetu, kwa sababu mstari wetu wa Msingi unaonyesha kuwa Mungu aliwafanyia mavazi ya Ngozi ADAMU na MKEWE na akawavika. 


Kusudi kubwa la somo hili ni kuchunguza kwa umakini Mafundisho ya kibiblia kuhusiana na mavazi, kwa ujumla kwa wanawake na wanaume na kwa watu maalumu, yaani kwa wanaume na pia kwa wanawake ili tufahamu ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu juu ya mwenendo wetu na kuvaa kwetu, ili kwamba tuishi sawa na mpango ambao Mungu ameukusudia kwetu tukimpendeza Yeye na wanadamu. 2Wakoritho 8:20-21 “Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.” Linapokuja swala la mwenendo wetu ni lazima tufikiri yaliyo mema sio mbele za Bwana tu ila na mbele za wanadamu, kila mtu aliyeokoka anapaswa kuhakikisha kuwa hana lawama katika mwenendo wake wote, kwa msingi huo ni muhimu kuhakikisha kuwa mwenendo wetu pia unaendana na kuvaa kwetu sawa na Mungu anavyotarajia mtu wake avae!.

Viwango vya Mungu katika mwenendo wa kuvaa kwetu!


1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.


Neno la Mungu linaonyesha kuwa kuna kiwango cha mwenendo ambao Mungu ameukusudia, ili kwamba wakristo tuweze kutembea katika mwenendo huo. Kwa msingi huo basi ni wazi kuwa kila kitu katika maisha yetu kuna namna ambavyo Mungu anakusudia tuishi kwa kusudi la Kumpendeza yeye, Biblia ina kitu cha kutuambia kuhusiana na mwenendo mzima tunaopaswa kuenenda, Biblia ina majibu ya maswali yote magumu na mepesi ambayo ni muongozo mwema katika maisha yetu na mwenendo wetu, Mungu anayo majibu vilevile namna tunavyoweza kuenenda katika tabia na mavazi yetu.


Swali la Msingi je Mungu ana viwango katika mwenendo wa kuvaa kwetu? Wengi wetu tunaweza kuwa na imani kuwa Mungu hana wala hajaweka msingi wa mwenendo wa namna ya kuvaa kwetu, au watu wake wavae vipi, tunaweza kufikiri tu kuwa ni vema kuvaa kwa heshima kulinga ana fasheni zilizoko, au tunaweza kusema wako watu hawavai kwa heshima kulinga na hali ya utandawazi na hivyo twaweza kudhani kuwa swala la mavazi ni swala huru hivyo kila mmoja anaweza kujivalia kama anavyotaka tu. Hivyo swala la mavazi ni swala la mtu binafsi na mazingira yake tu na kila mtu na ahukumu moyoni mwake namna impasavyo kuvaa!


Swala lingine la kujiuliza Je wadhani Mungu mwenye haki hakuwa na ujuzi kuwa kutakuwa na mavazi?, Yeye ambaye ni mwanzilishi wa mavazi; wadhani ya kuwa hakuelewa kuwa utafika wakati tutakutana na changamoto hizi tunazokutana nazo? Inawezekanaje Mungu mwenye haki akataka sisi tuwe watakatifu katika mwenendo wetu wote alafu kisha akaacha tujivalie kama tupendavyo? Angalia andiko hili 1Petro 1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Kwa msingi wa andiko hili utaweza kugundua kuwa Mungu anataka tuwe watakatifu katika mwenendo wetu wote yaani ikiwa ni pamoja na namna tunavyovaa! Haiwezekani uwe msomi wa maandiko kisha useme ahaaaa Mavazi sio ya kuyazungumzia! Ahaaa ni watu waliofilisika kiinjili tu ndio wanaoweza kuzungumzia mavazi, ahaaaa ni makanisa yaliyojaa sheria yanayobania watu uhuru ndio ambayo yanaweza kuzungumzia mavazi!  Ahhaaaa ni wachungaji wasiotembea ndio ambao wanaweza kuzungumzia mavazi, aaah ni watumishi washamba tu ndio wanaoweza kuzungumzia swala la mavazi, kama kuna theolojia ya maombi, kuna theolojia ya kuabudu, basi ni lazima tukubaliane wazi kuwa kuna theolojia ya mavazi na kama ulikuwa hujawahi kupitia darasa hilo basi ni vema sasa ukawa mpole ili wote kwa pamoja tuiangalie Biblia inasema nini juu ya mwenendo wetu na kuvaa kwetu. Ni lazima tukubali kuelewa kuwa Mungu ameweka viwango vya namna na jinsi inavyotupasa kuenenda! Kwa nini na ni viwango gani? Ikiwepo pamoja na kuvaa kwetu.


1.     Mwili ni hekalu la Mungu!

Mwili wa Mtu aliyeokoka ni hekalu la Mungu, ni hekalu la Roho Mtakatifu, kwa msingi huo ni lazima ujue wazi kuwa mwili wa mtu asiyeokoka ni hekalu la shetani na mapepo, kwa hiyo kuna tofauti kubwa kati ya mwili wa Mtu aliyeokoka na mwili wa mtu asiyeokoka sisi tunatajwa kuwa ni hekalu la Mungu yaani Mungu anakaa ndani yetu! 1Wakoritho 3:16 -17 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.” Sio hivyo tu Yesu mwenyewe alisema mtu akimpenda atayashika maneno yake na Baba atampenda na kuja kukaa ndani yake Yohana 14:23 “Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” Unaweza kuona sasa kuwa ni wazi kabisa mtu aliyeokoka mwili wake ni Hekalu la Mungu, ni mahali akaapo Mungu, Hekalu lilijengwa vipi maeneo yote nyeti katika hekalu la Mungu yalifunikwa kwa mapazia maalumu, hii ilikuwa ni muonekano wa nje wa hekalu, kutunza sehemu yenye uwepo wa Mungu. Wewe sio mtu baradhuli wewe sio wa hovyohovyo mwili wako ni makazi ya Mungu wewe ni ikulu, ikulu haiwezi kuwa mahali pa hovyo hovyo!  Wewe kama ni hekalu la Mungu basi hekalu haliwezi kuwa mahali pa hovyo hovyo, wewe ni makazi ya Mungu Baba na Mungu mwana na makazi ya Roho Mtakatifu Mungu yu atembea ndani yako je ni sawa ukakaa uchi? Ili hali ndani yako uko uwepo wa Mungu? Unaweza kuona! Kwa vyovyote vile hatuwezi kuachilia miili yetu hovyo!.

2.     Ole wake yeye asababishaye Makwazo!

Linapokuja swala la uhusiano wako na Mungu, wewe pekee ambaye ndio hekalu la Mungu kisha ukawa uchi, au unaoga, au ukawa unashiriki ngono na mumeo au mkeo au umelala uchi Mungu hana neno na wewe, yeye bado yuko pamoja nawe, uhusiano wake na Adamu katika Bustani ya Adeni haukujali hali ya Adamu kuwa uchi, yeye ndiye aliyetuumba, ni baba yetu mikononi mwake sisi ni tupu tu, japo kama unapiga magoti kuomba ni vema ukavaa nguo au ukajifunika Mungu ni baba yetu lazima tumuheshimu kupitia miili yetu. Nakazia tena unaweza kuvaa nguo au kujifunika iwapo umekusudia kupiga magoti na kusali.

Sasa ingawa Mungu hakuna la kumkwaza lakini katika neno lake ameonya kuwa ni ole wake yeye asababishaye makwazo! Hapa ni lazima tutangulie kufikiri yaliyo mema mbele za Mungu na wanadamu, Kwa mtu aliyeokoka ni lazima afahamu kuwa kuvaa kwetu kunamuwakilisha Yesu Kristo, watu waliomwamini Yesu wanaitwa wakristo kwa msingi huo maisha yetu ni lazima yamwakilishe Yesu Kristo, na kwa sababu hiyo tunapaswa kuwafikiri sana wanadamu tunapovaa ili kwamba tusiwakwaze na kuwafungia mlango au kuwatoa nje ya Mpango wa Mungu kupitia mwenendo wetu na kuvaa kwetu, Kama kuvaa kwetu kutasababisha makwazo kwa wengine ni lazima tujue kuwa tutakuwa na hatia kwa kukwaza wengine!

Marko 9:42Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini.

Hayo yalikuwa maneno ya Yesu mwenyewe kuhusu kuharibu mioyo ya wengine! Je Mafundisho ya mitume yanasemaje juu ya kukwaza wengine? Paulo anasema hivii!

1Wakoritho 8:13 “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.Ahaaaa unaweza kuona kumbe basi kama mavazi haya yanamkwaza ndugu yangu je?.  Sitayavaa hata milele nisije nikamkwaza Ndugu yangu. Mkristo wa kweli wakati wote hatafikiri mambo yake tu atafikiri na mambo ya wengine, hatupaswi kuwakwaza wengine katika jambo lolote na kwa msingi huo Mkristo ambaye amekomaa kiroho na anaweka upendo wa Mungu mbele hatakubali kuvaaa katika namna ambayo itawakwaza watu wengine na hivyo kufungiwa jiwe kubwa shingoni na kutupwa kilindini hakutamuhusu!

Tunaweza kudai kuwa katika Kristo tuko huru na tunaweza kujifanyia lolote tulipendalo lakini biblia inaonya kuwa uhuru wetu usiwe kikwazo kwa wale wenye imani dhaifu 1Wakoritho 8:9

Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.” Biblia ya kiingereza ya New Living Translation inasema “But you must be careful so that your freedom does not cause others with a weaker conscience to stumble” na biblia ya kiingereza ya NKJV inasema “But beware that lest somehow this liberty of yours become a stumbling block to those who are weak.Uhuru au haki tuliyo nayo katika Kristo haipaswi kutumiwa kijinga bali kwa tahadhari ili tusiwakwaze wengine. Kanuni hii inahusiano na mambo yote kukiwemo kuvaa kwetu.

3.     Wala msiifuatishe namna ya Dunia hii.

Warumi 12: 2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.Andiko hili linaweza kuunganishwa na lile la 1Yohana 2:15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Neno la Mungu lnasema “Wala msiifuatishe namna ya Dunia hii” kwa lugha ya kiingereza tunaweza kusema “And be not conformed to this world” tafasiri halisi ya neno comformed ambalo limetumika katika Biblia ya kiingereza ni  “Be similar in form or type or agree or behave according to socially acceptance convention acceptable or standards”

Hapa  Neno la Mungu lina maanisha wala msiifuatishe namna ya dunia hii yaani kwanza kabisa wakristo wasiishi sawa na watu walio chini ya sheria ya Musa, wala tusiwe kama wayahudi ambao waliishi chini ya sheria za kidini, lakini kwa nia njema sisi tusifanane nao, wala tusiishi sawa na kiwango chao, ambacho ni cha chini, wala tusiwafanye wao kuwa mfano wala kuwa na tabia kama zao au za jamii yao, lakini vile vile wakristo hawapaswi kuwa kama mataifa yale yasiyomjua Mungu wala tusifanane nao, wala kuishi kwa kiwango chao au kuwa na tabia kama zao, wala muonekano kama wao, hii maana yake ni kuwa Mungu anatutarajia sisi kuwa tofauti na Wayahudi walioshi chini ya sheria za Mungu lakini vile vile tuwe tofauti na mataifa yasiyomjua Mungu, Kwa msingi huo Basi Mungu anamtarajia Mkristo kuwa na kiwango cha juu cha kuigwa na watu wote, Kuanzia mtazamo wetu akili zetu, uwezo wetu na muonekano wetu, Mungu hakutokumboa katika sheria ya Musa ili tuishi kama Mataifa hapana, Mungu alitukomboa katika sheria ya Musa ili sisi tuwe kielelelezo kwa Wayahudi na Wayunani pia, sisi tuwe na mfumo mpya na mwenendo mpya ambao kila mtu atakayeuona atasema kweli hawa ni wanafunzi wa Yesu, Mwanafunzi wa Yesu ana mfumo mpya wa kuigwa na sio kuigiza

 1Petro 3:1-5 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.” 



Neno la Mungu linatutaka tuwe kielelezo kiasi ya kwamba wasioamini waweze kuvutiwa kuwa haya ndio maisha! Kanisa linapaswa kuelewa hili, haiwezekani sisi ndio tuwe tunavutiwa na dunia, Dunia inapaswa kuvutiwa na sisi hasa kwa kuonyesha mwenendo wetu ulio safi, swala hili ni katika kila eneo la Maisha yetu, Petro anakazia kuwa wanawake waliookoka wanaweza kuwavuta waume zao kupitia mwenendo wao mwema! Sasa kama mtu aliyeokoka ataendenda katika kuvaa kwake sawa na watu waliochoka wa dunia hii mbovu wale wanaoutazama mwenendo wetu watavutwaje kuja kwa Yesu?



Endapo sasa tutavaa na kuenenda kama watu wa ulimwengu huu ni wazi kuwa tunaupenda ulimwengu na ni wazi kuwa tunaifuatisha namna ya dunia hii na kwa sababu hiyo kumpenda Mungu hakumo ndani yetu, Kumbuka kuwa Kanisa ni chumvi ya ulimwengu tunapochanganyika na watu wa Dunia na kuwa kama wao tunapoteza ladha na ubora wa Ukristo wetu utakuwa wapi?



Mathayo 5:13 “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Kanisa lina wajibu wa kuwatunza Wayahudi na Mataifa mengine, lina wajibu wa kuwa kielelezo kama tukishindwa tutatupiliwa mbali kama walivyotupwa wayahudi, sisi ni kielelezo sisi ndio mfano wa kuigwa sisi ndio  Mungu anataka wale walio gizani watufate watuone 

Mathayo 5:14-16 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.  Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni

unaona Yesu anazungumza maneno mazito sana kwa Kanisa kwamba sisi ndio kielelezo sisi ndio mfano tunapaswa kuishi katika viwango vya juu mno kiasi ambacho watu watamtukuza Mungu kwa kwa kuyaona Matendo yetu ni ujinga na upuuzi wa hali ya juu kuvaa katika kiwango ambacho kila mtu atapata maswali kuhusu Mungu wako ni aibu kwamba duniani watu wanatembea uchi na kuutukuza uchi kisha sisi tukawa tunaunga mkono swala hili huku tukidai kuwa sisi ni wanafunzi wa Yesu, kuna wakati huitaji kutambua kuwa huyu ni mwanajeshi, au Polisi au Muuguzi kwa sababu mavazi yao yanawatambulisha sisi hatuwezi kuwa na uniform kama wao lakini tunaweza kuwa na mwenendo wetu na uvaaji wetu nadhifu utakaomfanya mtu asiyeokoka aweze kutufuata!, wakati dunia ikitusukuma kuliachia wazi Hekalu la Mungu na kufunua mapazia yake waziwazi sisi tunapaswa kuionyesha dunia kuwa Hatuwezi kuacha maumbile yetu nyeti yakaonekana hovyo, ni muhimu kanisa kuelewa kuwa Shetani ana mitindo yake ya Mavazi anayo ndio anayo, na wakristo wanapaswa kulitambua hili, ni lazima ufikie wakati tunaponunua nguo au kuijaribu tujiulize inamwakilisha nani, Je hufahamu kuwa nguo nyingi zina alama za kishetani, ama alama zinaashiria kuabudiwa kwa shetani lakini wakristo wa nyakati za leo wanavaa tu? Je unapovaa alama zinazoashiria kumtukuza shetani je hujafanyika sehemu ya muhubiri wa kishetani? Kwa sababu unapotembea unasaidia kutambulisha uwepo wake kwa sababu hiyo ni lazima tuwe kielelelzo wala msiifuatishe namna ya dunia hii!.. sisemi kuwa tusinunue nguo kutoka kwao viwanda ni vilevile lakini ni lazima tukangalia kama kuna maandishi maandishi hayo yanamaanisha nini na je yanaleta utukufu kwa Mungu au hapana na kama hapana ni kwa nini ninunue sasa?

4.     Mavazi ni ya kuficha uchi!

Mwanzo 3:9-10, 21 “BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha., BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.Msingi mwingine wa kibiblia kuhusu mwenendo wetu na kuvaa kwetu unaweza kuonekana katika maandiko haya, swala hili linaweza kutafasiriwa kimwili na kiroho vilevile, kama vile lilivyo neno la Mungu kuwa siku mtakayokula matunda ya mti huu hakika mtakufa, baada ya kula matunda Adamu na Hawa walikufa kiroho na baadaye kifo cha kimwili, pia kiroho walikuwa uchi na waliona aibu kwa vile dhambi ni aibu, hata hivyo ilikuwa wazi kimwili kuwa walikuwa uchi na hawakuona haya walipoumbwa, sasa walikuwa uchi na waliona haya, Kimsingi Hapa tunaona wazi kuwa Mungu ndiye mwanzilishi wa mavazi na kusudi lake kuu la kuwavika ilikuwa ni kuwaponya kimwili na kiroho, Damu ya mnyama ilifunika dhambi zao kiroho lakini kimwili ngozi ya mnyama ilifunika uchi wao, hivyo kusudi kuu la mavazi ni kufunika uchi!

Uchi ni nini ?

Uchi au kuwa uchi ni hali yoyote ya kutokuvaa nguo au kutokufunikwa kwa nguo maeneo yoyote yenye asili ya usiri. Hali hii ndio inayomtofautisha mwanadamu na mnyama, Mwanadamu ana akili lakini mnyama hana akili hivyo mwanadamu anaweza kujihifadhi lakini wanyama hawawezi, kwa msingi huo sasa uchi ni

Ni maeneo yote ambayo kihalali yanapaswa kuonwa na mumeo au mkeo tu kwa wanandoa na hayapaswi kuwekwa hadharani, mfano yafuatayo ni maeneo ambayo hayapaswi kuwa wazi kwa mwanamke

1.      Kifua (Maziwa au chuchu) Katika ufalme wa Mungu na katika ukristo kifua cha mwanamke na maeneo yake yote ni uchi na ni sehemu ya siri, hivyo inapaswa kuwa shemu ya siri na kufunikwa na Nguo  Mithali 5;16-17Je chemichemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako wala si ya wageni pamoja nawe” Neno la Mungu hapa linazungumza kwa hekima ya hali ya juu, kwamba uwazi wa mkeo au mumeo ni mali yako mwenyewe wala si wa wageni, sehemu za siri za mumeo au mkeo zinapaswa kuwa zako wewe mwenyewe na sio kila mtu ajichotee na kujionea, Je na kwanini uonyeshe Maziwa yako? Je unataka wanaume wote wayaone? Kisha … …unafanya dhambi


2.      Mapaja – Mapaja ya mwanamke ni siri yake na inapaswa kuwa sehemu yake ya siri, mapaja huanzia sehemu ya juu ya magoti kuelekea juu mpaka kwenye mazingira ya kiuno au kitovu, kwa msingi huo wanawake wanapaswa kuyahifadhi maeneno hayo, wanawake wa Kikristo ni wazi kuwa hawapaswi kuvaa mavazi yanayoishia juu ya goti na kuacha wazi maeneo hayo isipokuwa kwa mumeo unaweza kuacha maeneo hayo ni vema maeneo yote nyeti yakawa yanaonekana kwa mumeo tu na sio vinginevyo, lakini unawezaje kuyaacha maeneo hayo yenye kuvutia kwa kweli yakaonekana na watu wa mtaani lazima kuna kitu utakikaribisha.

3.     Kiuno – Mwanawake wa Kikristo ni muhimu kufunika kiuno chake, kiuno chako ni uchi na ni siri hivyo ni vema kikibakia kuwa siri


4.      Makalio au Nyuma kwako – Ni vema ukajisitiri vema nyuma kwako, sio vema kila mtu akaona zaidi ya mumeo, muonyeshe yeye kwaajili yan utoshelevu wa kingono na sio wengine, kwa ujumla haya ni maeneo yenye kuwavutia sana wanaume na kuwaletea fadhaa kubwa sana unapoachia Tako lako na umbile lake likaonekana je wadhani Mungu atasifiwa tu kwaa uumbaji wake? Ndio atasifiwa lakini utatamaniwa, utachochea hisia za kingono mno

5.      Nguo za Ndani – Hizi ni nguo zote za ndani ikiwa na maana ya chupi, sidiria, na kadhalika nguo hizi ni nguo za siri na hazipaswi kuonekana kwa namna yoyote na ndio maana zikaitwa nguo za ndani au nguo za siri.
Kwa upande wa wanaume vilevile ni muhimu kufahamu kuwa kisaikolojia wanadamu wote wanafanana, wanawake pia kuna maeneo wakiyaona kwa wanaume wanavutiwa kama ilivyo tu kwa wanaume wakiona baadhi ya maeneo ya wanawake wanavyovutiwa, hili ni swala la asili ya uumbwaji tu kwa hiyo wanaume pia yako maeneo ambayo kwa wanawake ni uchi, wote tuna paswa kulindana kwa kutokuyaonyesha maeneo hayo, najua wako watu wanaweza kuwa na hoja kwamba kama mimi nimevaa hivi yeye inamuhusu nini si tamaa zake mwenyewe? Jambo hili halipaswi kuwa hivi ytunao wajibu wa kulindana na kujiepusha kusababbisha makwazo!


Jinsi gani mwanaume Mkrito anapaswa kujihifadhi?


1.      Tunza kifua chako! – fiua chako hakipaswi kuonekana kwa wanawake ni kifua cha mke wako tu uliyepewa na Mungu hivyo si vema mwanaume akaonyesha kifua chake, wanawake wanavutiwa sana na mwanaume aliyejengaka vema katika mazingira ya kifua kwa msingi huo kwa mwanaume Mkristo ni muhimu kuyahifadhi mazingira hayo 

2.      Misuli ya Mikono yako – Misuli ya mikono yetu na ukakamavu tulio nao kwenye mikono ukionekana na wanawake unaamsha hisia za kingono kwa hiyo ni muhimu kwetu kuhakikisha pia tunayahifadhi maeneo hayo kwaajili ya wake zetu tu, wanawake kwa haraka sana huangalia misuli ya mikono yetu na wanapoona mishipa ya damu namna na jinsi iliyojengeka katika mikono yetu mawazo yao yanapaa, kwa hiyo ni vema ukajihifadhi.

3.      Nguo za Ndani – Nguo za ndani pia za mwanaume hazipaswi kuonekana wazi kwa Mwanamke asiye mke wako, ni vema kujihifadhi na wale wanaovaa mlegezo ni muhimu wakajua kuwa hii ni tabia mbaya sana, utafiti unaonyesha kuwa tabia ya kuvaa mlegezo ni tabia ya kishoga na sio vema kwa mtu mwanamume aliyeokoka kuachilia chupi yako ikaonekana je inapoonekana ni kwa utukufu wa nani?

Miili yetu haikuumbwa kwaajili ya kila mtu tu, mwili wa mwana mume umeumbwa kwaajili ya mke wake tu na mwili wa mwanamke umeumbwa kwaajili ya mume wake tu, hivyo wengine hawapaswi kuona kwa sababu zozote zile.

1Wakoritho 7:3-4Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.”  Neno la Mungu linadhihirisha wazi kuwa mwili wa mwanammme unamuhusu mkewe na mwili wa mwanamke unamuhusu mumewe na hakuna amri, wao wanapaswa kuachiana na kupeana miili yao na kutokuificha wanapokuwa faragha, huu ndio msimamo wa kimaandiko, mbele ya uwepo wa mkeo au umeo unaruhusiwa kuvaa vyovyote utakavyo hata kama ni kukaa uchi, kwa kusudi la kumfurahisha mwenzi wako na kutimiza hivyo mahitaji ya kingono ya mwenzi wako, vaeni vyovyote mpendavyo mbele ya kila mmoja wenu muwapo faraghani hapo sio tatizo.

Lakini nje yenu, hadharani mbele ya wazazi, kaka zako na dada zako, mashemeji na kadhalika lazima uvae kwa heshima, na kujifunika maeneo yote yenye kutafasirika kama uchi kwa jamii yako lazima yafunikwe.

Roho ya kutokujali kuwa itakuwaje kwa wengine kaka au dada zangu wakiingia majaribuni kwaajili yako haitokanani na Mungu, Mkristo wa kweli lazima ajali kwamba nisije ni kasababisha makwazo na kuangusha dhambini wengine, Uhuru wako usiwe sababu ya kusumbua wengine na kuwaingiza dhambini angalia 1Wakoritho 8:9 “Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.Toleo lingine la maandiko haya linasomeka Lakini angalieni huu uhuru wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu. Mkristo wa kweli ataishi sawa na viwango anavyovitaka Mungu, ataenenda kwa uadilifu na kuvaa kwa uadilifu akijali uwepo wa Mungu na sio dunia itakavyo.


Je ni halali kukaa uchi Hadharani?


Kama kuwa uchi hadharani ndio maendeleo na fasheni au ndio mtindo wa kisasa, na Mkristo akaamua kuwa kama watu wa dunia hii inavyotaka ukweli ni kuwa unatenda dhambi 

1Yohana 2:6 “Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.”

 
Wakrito ni wale wanaomfuata Yesu maana yake ni wale wanaoenedna kama yeye mwenyewe alivyoenenda kwa msingi huo lolote lile ambalo tutalifanya ikiwemo kupiga picha ambazo hazina uadilifu kama wa Kristo na kuzitupia katika mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, Instagram, google plus, whatssapp na kadhalika na zikaonekana hadharani ukweli ni kumvunjia Mungu heshima si jambo jema kabisa kwa Mkristo kueneza picha za utupu ama za kwakwe au za mtu mwingine, utupua ua uchi umekuwa ndio mvuto mkubwa sana wa aina binadamu na kuwafanya wengi kuzama katika mwenendo wa kishetani sisi sio wa ulimwengu huu na kama tutakubaliana na kila kitu cha ulimwengu huu nazungumzia mfumo wa utendaji wa ibilisi, maana yake kumpenda baba hakumo ndani yetu. 


1Yohana 2;15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.


Picha za wanaume au wanawake walioko uchi na nyinginezo zinawakilisha wazi kazi za ufalme wa shetani, ni kupitia picha hizi shetani na majeshi yake yaani mapepo wanafanya kazi ya kuwavuta watu katika tamaa na kuinua hisia za kingono zisizo halali, kwa hiyo ukiacha kuvaa tu ni vema na uadilifu kabisa kwa wakristo pia kuacha mara moja kusambaza picha zenye kuonyesha utupu wa wanadamu, au kuzitazama uchi ulileta laana kwa kizazi cha kanaani 


Mwanzo 9:20-27 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.  Mungu akamnafisishe Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.”


5. Wengine watatamani tu bila kujali umevaa nini?


Yakobo 1:14-15 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”. 

           
Ni muhimu kufahamu na ikaeleweka wazi kuwa ni kweli wako watu ambao wanateswa na tamaa tu bila kujali umevaaje watu wanateswa na roho ya tamaa wapo, watakutamani au watatamani bila kujali mtu amevaa nini, lakini ni muhimu vilevile ikaeleweka wazi na hata watu wa dunia hii wanajua wazi kuwa kuna muuunganiko wa kile mtu amekivaa na tamaa, na hili linaweza kuchangiwa na jinsi wanaume na wanawake wanavyovaa hasa katika mitindo ya kisasa.

Na ndio maana matangazo mengi ya bidhaa hapa duniani hayawezi kutangazika bila kuweko mwanamke mrembo au mwanaume mrembo wenye aina fulani ya mtindo wa kisasa wakihusishwa na kutangaza matangazo hayo, kwa nini kwa sababu Dunia inajua kuwa ukitaka mtu aangalie kitu au bidhaa au akitamani huna budi kuweka picha za aina hiyo ya watu sasa swali je na Wakristo tunapaswa kufanya hivyo? Hatupaswi kuichochea tamaa hata kama wako watu wenye tamaa, na tunapaswa kukumbuka kuwa tamaa huzaa dhambi na kisha huleta mauti hivyo ni vema tukaidhibiti, ndani yetu au sisi kuwa sababu ya watu wengine kutamani. Kila mtu anawajibika au atawajibika kwa tamaa aliyo nayo

Mathayo 5:27-30 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 

Mungu anamtaka kila mmoja awajibike kudhibiti tamaa ndani yake bila kujali kuwa mtu mwingine anavaaje

2Wakoritho 10;3-6Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;  (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia.

Ni lazima tuhakikishe kuwa fikra zetu zinamtii Kristo, mapambano ya kuushinda ulimwengu yako katika ufahamu wa mwanadamu, Hivyo kila mwanadamu anapaswa kupambana na tamaa itendayo kazi ndani yake bila kusahahu kuwa shetani hutumia watu katika kutekeleza majukumu yake

Mathayo 16:21-23. “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, Bali ya wanadamu.”  

Unaweza kuona kwa msingi huo basi ni ujinga kufikiri kuwa huwezi kujihifhadhi katika kiwango  ambacho kitamfanya mtu mwingine asitamani eti kwa sababu wako watu wanatamaa hapana ni muhimu kufahamu kuwa neno la Mungu halitaki sisi tuwe kikwazo kwa wengine na hivyo ni muhimu kujihifadhi, Warumi 14 inafundisha namna na jinsi tunavyopaswa kuepuka kuwa kikwazo kwa wengine, ni ujinga kufikiri kuwa unaweza kufanya mambo kuwa rahisi au magumu kutokana na kuvaa kwako la msingi usiwe sababu ya mwakwazo kwa wengine warumi 14 iko wazi kuhusu hilo.



Wanawake wa Kikristo Nchini Syria wakiwa katika ibada


6.      Kila mtu aliyeokolewa ni Balozi wa Mungu. 

2Wakoritho 5:20 “Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.” Neno hili la muhimu katika lugha ya kiingereza linasomeka “Now then we are ambassadors for Christ” Neno hili linatumika kwa sifa sawa na Waefeso 6:20 “ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.” Neno hilo mjumbe maana yake ni balozi “I am an ambassador in bonds”Kwa asilineno hilo limetokana na neno la Kilatini “Ambasciator” na likapata umaarufu katika lugha ya kirumi na ufaransa na uingereza, Likimaanisha mjumbe au balozi ambalo kwa lugha nzuri na nyepezi nimwalikishi, kila mtu aliyeokoka ni mwakilishi wa Yesu Kristo, balozi ni mtu anayewakilisha badala ya hivyo sisis tunamuwakilisha Kristo ni mabalozi wa Yesu Kristo ni mabalozi wa serikali ya Mungu, ni mabalozi wa ufalme wa Mungu, vile alivyo balozi na heshima aliyo nayo ndivyo ilivyo na serikali anayoiwakilisha, Miaka kadhaa iliyopita uingereza ilitaka kuleta balozi shoga hapa Tanzania na Rais aliyekuweko madarakani alikataa, tulikataa kumpokea, kwa sababu kwetu hatujahalalisha na kukubaliana na tabia hizo, awaye yote anayemwakilisha Kristo anapaswa kuenenda kama Kristo mwenyewe alivyo, muonekano wako na mtazamo wako unamwakilisha Kristo na hivyo ni muhimu kwako kujihoji na kujiuliza kuwa namna unavyovaa je inaaakisi maana nzima ya kuwa wewe ni balozi wa masihi? Je unamwakilisha vipi Yesu katika muonekano wako, Kama ilivyo ni kweli Yesu ni mfalme wa wafalme katika Serikali yake je angekuchagua uwe balozi wake je angechagua mtu wa namna gani? Na kama Yesu anaweza kumchagua kila mtu kwa kuwa ni Mungu je wewe kwa Heshima aliyonayo Yesu Kristo ungeamua kumuwakilisha namna gani? Kule kuvaa kwako, mwenendo wako na muonekano wako  unapeleka ujumbe kuwa unatokea serikali ya namna gani je unamwakilisha Mungu au unamwakilisha shetani?

7.  Mavazi yako ni utambulisho wako.

2Wafalme 1:7-8Akawaambia, Je! Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa namna gani? Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.”


Nabii Eliya nyakati za agano la kale alitambulika kwa namna na jinsi alivyokua anavaa, mavazi yana sehemu kubwa sana ya kukutambulisha, Tunaona katika maandiko wakati Musa alipokuwa amekimbia Misri kuelekea Midian wale walimuona kwa vile alikuwa amekulia kwa Farao walimtambua kama Mmisri kutokana na uvaaji wake angalia Kutoka 3:16-19 “Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.

Kutokana na kukulia katika mazingira ya nyumba ya Farao na utamaduniwa Misri Japo Musa alikuwa Muebrania alionekana kama Mmisri, Sababu kubwa ilikuwa ni Mavazi yake kumbe mavazi yana uwezo mkuwa sana wa kumtambulisha mtu, aina yake haiba yake tabia yake na mwenendo wake lakini hata utaifa wake na wakati mwingine kazi yake, kwa msingi huo hata wale wanaojiuza au makahaba utambulika kirahisi kuwa makahaba kutokana na mavazi yao na ukatongozwa, wakati Fulami mwanamke mmoja aliyeitwa Tamari alivaa mavazi ya kikahaba na Yuda mwana wa Israel alimtongoza na kuingia kwake kwa kudhani kuwa alikuwa kahaba na kumbe alikuwa mkwewe ona katika

Mwanzo 38:15 “ Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.”

Kuvaa kwetu kunaweza kuonyesha wazi kama sisi ni watu wa Mungu au wasiomjua Mungu, watu wema au waovu, lazima ujihoji na kujiuliza kuwa unapovaa unamuwakilisha nani na unapeleka ujumbe gani?!Ikiwa yako mavazi ambayo yanaweza kueplekea wewe kutafasirika kama kitu kingine ni muhimu kwetu tukazingatia aina ya ujumbe tunaoupeleka.

8.  Ukristo ni kiasi 


Tito 2:11-12Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;”

Biblia inakazia kuwa wakristo ni watu wanaopaswa kuishi kwa kiasi neno kiasi , haki na utauwa katika biblia ya kiingereza yanasomeka hivi we should live soberly, righteously, and godly,  soberly maana yake kwa Hekima, na nidhamu, tukijidhibiti wenyewe self control  na kwa haki maana yake kwa heshima tukizingatia sana namna wenzetu wanavyotufikiria na kwa utawauwa godly kama vile tuko ndani ya uzima wa milele au tuko mbinguni au tuko na Mungu au kwa utukufu wa Mungu, hii ina maana vyovyote vile tunavyofikiri ni muhimu kwetu wakristo kuvaa kwa nidhamu tukimfikiri Mungu na majirani zetu walio nje hii ni kanuni muhimu sana katika maisha yetu ya ukristo chochote kikizidi ni mno, wakristo wanapaswa kulikumbuka hili siku zote za maisha yao.


Kanuni saba za Mavazi ya Mkristo:-


1.      Yamwakilishe Yesu kuwa ameniokoa na kunibadilisha  na kuwa sasa ninaishi maisha matakatifu ya kumpendeza Yeye Warumi 12:1,Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Tito 2:11-12, Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;” 1Timotheo 2;9-10, Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.” 


2.      Kuvaa vema huwa haimaanishi kuwa mtu huyu ndio yuko sawa na Mungu lakini Mungu huangalia moyo na mwili pia. Kwamba nimechagua nguo yangu kwaajili ya utukufu wa Mungu ama kwa sababu ya kuiangalia dunia  ISamuel 16:7” Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.” Mithali 31:30 “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.”

 
3.      Ninachagua mavazi yangu kama mtu mwenye badiliko aliyebadilishwa na Mungu, Warumi 6:12-13, “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.”         Waefeso 2;10, “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”  Tito 2;14 “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.


4.      Je ninaishi kwa kuridhika na kwa kiasi Mathayo 6:28-30 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?” – Mungu atakutana na mahitaji yetu na sio yote tuyatakayo, kama tutachukuliwa na mfumo wa kujijali tunaweza kusahahu kuwajali wengine


5.      Je ninafuata muongozo wa Mungu ninapovaa  na je ninafuata matakwa ya wazazi ninapovaa je ninavaa kwa kuzingatia unyenyekevu? 1Petro5:5bVivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”  kuvaa vema haimaanishi kuwa kinyume na mitindo, maana yake kubwa ni kuvaa kwa makusudi ya kumpendeza Mungu 1Timotheo 2:8Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu.” waamini ni lazima wajiweke katika nafasi iliyo njema na ya kuvutia watu kwa Mungu wanapovaa  na sio kuvaa kama makahaba Mithali 7:10Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;“


6.      Zingatia utamaduni wako, Paulo mtume alipozungumzia mavazi alizungumza kwa mujibu wa tamaduni za warumi za wakti ule na alipokuwa akiwataka wakristo wasiifuatishe mana ya dunia hii ilikuwa dunia ya wakati ule hii ina maana gani? Yaani tuhakikishe kuwa kwanza hatuko kinyume na utamaduni  na mazingira yanayotuzunguka, lakini vilevile tusivae sawa na jambo au namna inayooenakana katika jamii yako kuwa sio sawa.


7.      Je unavaa kwa Heshima Na Uchaji wa Mungu? Mithali 31:25 “Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.”  Maisha yetu ni lazima yajawe na kumuheshimu Mungu, lakini vilevile yajenge heshima yetu, ni lazima tujihoji kama hiki tunachikivaa kina mpa Mungu utukufu 1Wakoritho 6:19-20, 19. “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”    10:31,Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” sisi sio mali yetu wenyewe ni mali ya Mungu., lazima tulizingatie hili na kulikumbuka!


Hitimisho!


Kwa ujumla Biblia iko wazi sana kuhusu swala la mavazi, ni swala la utamaduni na mkao wa Moyo lakini kwa makusudi muhimu yaliyotajwa hapo juu, Kwa mfano Biblia inatambua tofauti iliyoko kwa kimaumbile Mwanzo 1:27Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”, na inataka kila mmoja avae kwa mujibu wa maumbile yake yaani mwanaume mavazi ya kiume na mwanamke mavazi ya kike Kumbukumbu la torati 22:5Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.  baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa neno hili lilihusu jamii ya watu waliokuwa wanavaa kama wanawake kwa kusudi la kujificha na kushiriki zinaa kwa hiyo kwa makusudi ya kuepusha zinaa andiko hili liliandikwa, swala hili limeinua mijadala mingi sana ya kitheolojia sasa watu wavaeje lazima pia dhamiri ikishuhudie sawa na Neema ya Mungu iliyoko juu yako namna unavyopaswa kuvaa Warumi 14:23,Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.” Wagalatia 2:20 “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.“


Ni muhimu kufahamu kuwa kuna baadhi ya vitu vilikatazwa katika Agano la kale kutokana na tamaduni zao kwa mfano wayahudi walikatazwa kuvaa nguo mchanganyiko kwa wakati mmoja Kumbukumbu 22:11” Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.”  hata hivyo wataalamu wanakubali kuwa andiko hili lilimaanisha katika halia ya kiroho kutokumshirikisha Mungu na miungu au kuwa mshirikina ingawa hakuna anayejua kwa hakika maana ya andiko hili


Jambo moja lilillo wazi ni kuwa agano la kale limekamilishwa na agano jipya na kuwa wakristo wako huru mbali na sheria ya Musa iliyotolewa kwa wayahudi Warumi 8:1-2 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” na Wagalatia 5:13-14 “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.” Paulo anatoa ushauri huu kwa wanawake akimsihi Timotheo kuwaelekeza 1Timotheo 2:9-10,Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. Petro pia anatoa hoja mfano wa hiyo katika1Petro 3:2-5 “wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.   

        
Ukiangalia kwa makini aya hizo ni kama vile mitume walikuwa wanakwepa swala zima la kuzungumzia mavazi huku wakisisitiza utu wa ndani ambao kwa kawaida ukiwa safi na mtu nje yake atakuwa safi tu, hali ya kimavazi kwa kweli inabadilika miaka na miaka huku kanisa nyakati zote likipambana kupata uhakika kuwa ni mfumo gani wa kuvaa unapaswa kufuatwa, Mungu ataokoa watu kutoka katika mkila taifa na jamii na utamaduni kwa hivyo ni vigumu kulinganisha viwango gani kanisa limnapaswa kusimamia zaidi ya kuzingatia isingi na dhamira ya kibiblia iliyoainishwa hapo juu, Mungu amelikusudia kanisa lake liwe na umoja 1Wakoritho 11:20-22, 20. “Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.” Wagalatia 3:28 “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.”   

   
Biblia imeonya kuwa tuache kuwahukumu watu, au kuwapendelea watu fulani na kuwadharau wa aina fulani kutokana na kuvaa kwao Yakobo 2:1-9 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa? Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.”     

      
Jambo kubwa la msingi kila Mkristo anapaswa kujifunza tu na kujiuliza swali kunbwa la msingi ni kitu gani ninataka kukisema na ujumbe gani ninataka kuupeleka kwa kile ninachochagua kuvaa

Dua

Baba Mungu mpendwa katika jina la Yesu, umeniumba kwa sura na mfano wako, nataka nikuheshimu wewe kwa kila kitu ikiwemomwenendo wangu na kuvaa kwangu, tafadhali nipe hekima na ufahamu nauwezo wa kuopambanua moyoni mwangu ili kwamba maisha yangu yakupendeze wewe na kuwa ushuhuda na yenye kuwavutia walimwengu watakaonitazama Duniani amen!

Mwenendo wangu na Mavazi yangu kwa mujibu wa Quran

Kwa vile inawezekana kuwa ngumu kujifunza na kuelewa kutoka kwa Biblia kutokana na tafasiri tofauti za namna ya kuvaa ni muhimu kufuatana nami kama mkuu wa wajenzi na kujifunza somo hili kwa upande wa pili yaani wana wa Ishmael wao wanaesemaje kuhusu mwenedno wetu na kuvaa kwetu kwa mujibu wa Quran fuatana nami


Mwenendo wangu na kuvaa Kwangu “2”
Mstari wa Msingi:  Surat Al- Ahzaab 33: 35 “Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake na waumini wanaume na waumini wanawake na watiifu wanaume na watiifu wanawake na wasemao kweli wanaume na wanawake  na wanaosubiriwanaume na wanawake na wanaofunga wanaume na wanawake na watoao sadaka wanaume na wanawake na na WANAOJIHIFADHI TUPU ZAO wanaume na wanawake wanao Mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake Mwenyezi Mungu amewaandalia Msamaha na ujira mkubwa

Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Quran inazungumza kwa uwazi na upana sana kuhusu tabia na mwenendo ambao watu wa Mungu wanapaswa kuuenenda, na ahadi kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa wale watakaoenenda  sawa na njia za mwenyezi Mungu au wenye kujitia nia katika kutenda matendo mema na mojawapo la Msingi ikiwa ni pamoja na WANAOJIHIFADHI TUPU ZAO yaani wanawake kwa wanaume wanaojihifadhi wanaovaa kwa nidhamu hawa wana ahadi ya msamaha na thawabu kubwa sana kwa Mungu.

Maandiko yanamtaka kila mtu Mcha Mungu kutilia maanani swala zima la mavazi, usafi na nidhamu wakati wote tunapijihusisha na watu wengine na pia wakati wa ibada Quran inasema katika Surat Al-‘Araaf 7:31 “Enyi wana wa Adamu Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada , na kueleni na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu kwa hakika yeye hapendi wanaofanya israfu

Mungu anataka watu wavae vizuri kwa heshima na nidhamu tena wavae mavazi nadhifu yanayowapendeza na yenye muonekano mzuri kwa kufanya hivi waamini watakuwa wanampendeza mwenyezi Mungu na kutii neno lake Surat Al-‘Araaf 7:32 “ Sema Ni nani aliyeharimisha PAMBO la mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki, Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani na siku ya kiyama vitakuwa vyao wao tu,. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanaojua.”

Kwa lugha Nyepesi qurani inazungumza katika eneo hili kuwa ni nani amewakataza PAMBO yaani nguo nzuri nadhifu ambazo Mungu amewabarikia watu wake au vitu vilivyo vizuri katika riziki yaani chakula, ni wale wanaoamini kuwa wataendelea kuwepo duniani hata baada ya siku yamwisho ili vitu hivyo view vyao. Mungu anataka kama una mavazi mazuri yaliyo nadhifu uyatumie sasa na katika ibada na zaidi sana kama kuna chakula kizuri ukitumie sasa hii ndio ishara nya watu wanaojua yaani watu wanaojua kuwa duniani tuko leo na kesho hatuko

Kwa nini maneno ya Mwenyezi mungu yanasisitiza kuvaa kwa unadhifu tena kuvaa vizuri na tena kwamba kuna dhawabu kubwa kwa watu wanaojihifadhi yaani wanaovaa kwa kuzingatia kuficha tupu zao jambo ambalo lilianzishwa na mwenyezi Mungu. Ilivyo ni kwamba kuna faidha kadhaa ambazo muumini anafaidika nazo kwa kuvaa kwa nidhamu na unadhifi

Makusudi ya kuvaa kwa nidhamu:-

1.      Mavazi ni kwa kusudi la kujihifadhi hasa unapokuwa hadharani, Maandiko yanaeleza wazi kuwa Mungu ndiye anayetupa mavazi na anatupa kwa sababu anataka tujihifadhi angalia tena Surat Al-‘Araaf 7:26Enyi wanadamu tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu na nguo za Pambo na nguo za uchaMungu ndio Bora , Hayo ni katika ishara za mwenyezi Mungu mpate kukumbuka” Unaona maandiko yanaoinyesha ya kuwa Nguo zinatoka kwa Mungu ni Mungu ndiye aliyetupa mavazi kama vile alivyompa Adamu na Hawa walipokuwa wakali uchi, Mungu anatuvika, na anatuvika kwa kusudi la kuficha uchi na kwa kusudi la kumuabudu yeye hivyo mavazi ni ibada.

2.      Mwenyezi Mungu pia ametupa mavazi kwa kusudi la kuupa mwili joto na kujikinga na madhara ya baridi, wote tunafahamu kuwa joto na baridi ni hali zinzoweza kuleta madhara kwa binadamu, hivyo Mwenyezi Mungu pia ametupa mavazi kwa kusudi la kudhibiti hali hizo za hewa angalia Surat An- Nahl,16:81 “Na mwenyezi Mungu amekufanyieni vivuli katika vitu alivyoviumba na amekufanyieni Maskani milimali na amekufanyieni Nguo za kukukingeni na joto na nguo za kukukingeni katika vita vyenu, Ndio atakutimizieni neema zake ili mpate kutiiKumbe ni dhahiri na ni wazi kuwa mavazi ni thawabu inayotoka kwa mwenyezi Mungu na iko pale kwaajili ya kutukinga na joto au baridi

Linapokuja swala la Mavazi ni dhahiri kuwa watu wengine wanapinga sana na wanapingana mno kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuzungumzia mavazi katika njia ya uwazi sana kama ilivyo katika Tourat na injili kama anavyozungumzia katikia Quran

Ni qurani pekee yenye nguvu na utukufu mkubwa ambayo imesisitiza kwa namna ya uwazi na bayana swala la mavazi kuliko katika imani za dini nyingine, Mwenyezi Mungu ameweka sheria na utaratibu ulio wazi kabisa na ulioonyooka na wenye sababu zinazokubalika wazi kwa nini watu wavae kwa nidhamu na uadilifu.

Sheria na kanuni zinzooongoza katika mwenendo wetu na kuvaa kwetu.

Ni muhimu kufahamu kuwa katika imani ya kiislamu sheria ya jumla kuhusu mavazi inaruhusu mtu kuvaa chochote akitakacho, na wala sheria ya jumla haimkatazi muumini wa kiislamu kuvaa ajisikiavyo nguo za aina zote ni halali isipokuwa tu kama hazikiuki makusudi yanayohitajika ya mwenendo wa kuvaa kwetu, sheria inakataza aina yoyote ya mavazi yatakayovaliwa yakazidi vile viwango na mipaka ya uislamu na kuuvunjia heshima.

Mitume walivaa mavazi yaleyale ambayo waliikuta jamii yao inavaa na wala hawajawahi kuwapangia namna na jinsi ya kuvaa, lakini walitoa maonyo na muongozo wa namna na jinsi inavyowapasa waamini wao kuvaa

Kanuni ya uvaaji katika uislamu inamtaka kila mmoja avae vyovyote apendavyo endapo tu ziko sababu za msingi za kumfanya avae hivyo, hii maana yake ni kwamba hakuna kinachodhaniwa kuwa ni haramu katika kuvaa endapo tu kutakuwa na sababu zilizowazi zinazopelekea mvaaji akavaa alivyovaa hii ina maana gani kama uko chumbani vaa mavazi ya huko chumbani au jiachie wewe na mumeo au wewe na mkeo, au kama mko ndani basi hakuna sababu ya kuficha tena yale maungo ambayo mwanamke au mwanamme anayafunika kwaajili ya kuonyesha heshima kwa mwenza wake anapokuwa nje, lakini wawapo faragha hakuwa cha kuwazuia na mavazi au ukaaji wa hasara baina yenu wana ndoa sio haramu!

Qurana pamoja na sunnah zinasema  Sunan An-Nasaa’ee 2559 “kuleni,Kunyweni, Vaeni na fanyeni ukarimu bila kubughudhi watu wala kufanya Majivuni” hii maana yake nje ya nyumba yako kama utavaa kikahaba au bila kujali uislamu ama dini ya haki ya mwenyezi Mungu basi utawabughudi watu na ucha Mungu wako utaingia dosari kubwa na Mwenyezi Mungu atakukataa.

Kwa msingi huo Muumini wa Mwenyezi Mungu anaweza kuvaa nguo zilezile wanazovaa katika inchi aliyojaaliwa kuwepo kwa kuzingatia mwenendo na kuvaa sawa na sheria za kiislamu zinavyotaka au kupendekeza

Kanuni za mwenendo wa mavazi katika uislamu.

1.      Usivae mavazi yanayoonyesha utupu  hii ni kwa wote wanaume na wanawake Surat Al-Arraf 1:26. “Enyi wanadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo zap ambo, na nguo za uchamungu ndio bora , Hayo ni katika ishara za mwenyezi Mungu mpate kukumbuka” Nguo za kumcha Mungu ndio bora zaidi

2.      Vaa kulingana na aina yako ya jinsia, Katika uislam ni mauruku kama wewe mwanaume kuvaa mavazi ya kike na kama wewe ni mwanamke kuvaa mavazi ya kiume hata kwa kuigiza hairuhusiwi soma khadithi 4098 ya sunan Abu Daawood wamelaani wa wanaume wanaojifanya wanawake kwa kuvaa kama wao na wanawake wanaojifanya wanaume kwa kuvaa kama wao’ pia Khadithi 5546 Saheeh Al- Bukharee inawaelekeza wanawake kuvaa swwa na jinsia zao, Uislamu unawataka watu kuvaa kulinga ana jinsia zao ili kukidhi haja ya uhalisia wa uumbaji wa Mungu kulinga na jinsia zao.

3.      Hiruhusiwi kuvaa mavazi yanavyovaliwa na wasiokuwa waislamu kwa mfano hairuhusiwi kuvaa kama Mapadre, au makuhani wa kiyahudi, au kuvaa msalaba au mavazi yoyote yanayoashiria utamaduni wa dini nyingine isiyokuwa islam. Sawa na khadithi ya Sunan Abu-Daawood 4031

4.       Mavazi yanayovaliwa kwaa ujeuri inaelezwa katika khadithi Saheeh Muslim 91 kwamba hakuna mtu mwenye kiburi moyoni mwake atakayeingia peponi kwa maana hiyo muislamu hapaswi kuvaa kwa kiburi mwenyezi Mungu sio tu hatawaruhusu nkuingia peponi lakini hatawaangalia kabisa katika siki ya kiyama wanaovaa mavazi kwa misingi ya kiburi utasoma katika Saheeh Al-Bukhaare 3465 na Saheeh Muslim 2085

5.      Usilamu pia umeonya kufaa mavazi yoyote yale yenye kuvutia hisia za watu yanaitwa kwa kiarabu Libaas ash – shuhrah yaani mavazi yatakayofanya uonekane wa tofauti au kila mtu akuangalie wewe mavazi yanayochota hisia za watu yaani lolote lile litakalokufanya unateka hisia za watu Muhamad anasema awaye yote anayevaa SHUHRAH katika ulimwengu huu Mungu atamvika mavazi ya aibu na kumnynyekesha mno wakatai wa kiyama siku ya hukumu soma Musnad Ahmad 5664 na Sunan ibn Maajah 3607

6.      Mavazi ya thamani kubwa mno ya kupita kawaida  yanayozidi kipato cha kawaida cha mtu hayo pia yameharimishwa, Mavazi yakichanganywa na dhahabu na vito vya thamani kubwa na urembo urembo haya yameruhusiwa kwa wanawake na yamakatwazwa kwa wanaume  Sunan ibin Majaa 3595 na Sunan Abu Daawood 4057

Kuleni na vaeni na toeni kwa ukarimu na kila mmoja ajihadhari ni kiburi na majivuno na kamwe katika hayo yote msichanganye na kiburi na majivuno Sunan An- Nasaa’ee 2559 kwa mba mpango mzima wa kuvaa kwa mtu unategemeana na kipato chake, uchumi wake anavyowajali masikini akiwa mbali na kiburi na majivuno bila kujali utajiri wake wala kuwadharau masikini
Hii ndio misingi ya mwenendo wetu na kuvaa kwetu katika uislamu

Sasa kwanini nimeliweka somo hili? Uili kwamba usipoelewa misingi ya kuvaa kibiblia basi uelewe misingi ya kuvaa kwa mujibu wa uislamu na usipoelewa misingi ya kuvaa katika uislamu basi uelewe missing ya kuvaa katika Ukristo

Duah
Baba Mungu mpendwa katika jina la Yesu, umeniumba kwa sura na mfano wako, nataka nikuheshimu wewe kwa kila kitu ikiwemomwenendo wangu na kuvaa kwangu, tafadhali nipe hekima na ufahamu nauwezo wa kuopambanua moyoni mwangu ili kwamba maisha yangu yakupendeze wewe na kuwa ushuhuda na yenye kuwavutia walimwengu watakaonitazama Duniani amen!

Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!

0718990796

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni