Alhamisi, 27 Februari 2020

Neno la Mungu na umuhimu wa kuimba na mziki!



Kumbukumbu la Torati 31:19-22Basi sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli; kawatie vinywani mwao, ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa Israeli. Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu. Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa. Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo, akawafundisha wana wa Israeli.”


Utangulizi:
Moja ya urithi wa Muhimu sana ambao wanadamu wameurithi tokea enzi za baba zetu ni habari ya kuimba, Maswala ya uimbaji yanaonekana kabisa yalianzishwa na watu waliokuwa wametengwa na uso wa Mungu kwa sababu ya dhambi za wanadamu, hivyo watu hao walitumia nyimbo kama njia ya kujifariji wakiwa na matumaini kuwa Mungu atawarehemu


Mwanzo 4:17-22
Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama.  Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi.  Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama.”


Kwa hiyo Biblia inamtaja Yubal kama mwanzilishi wa wapiga kinubi na filimbi, wao ulikuwa ni uzao wa Kaini ambao walitengwa na uso wa Mungu na hivyo walitafuta faraja na rehema na unafuu wa mioyo kwa kuimba hapa duniani.

Mziki leo hii umekuwa ni Lugha ya kihisia ambayo inaunganisha watu kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa mpira wa Miguu, kwa Karne nyingi sana Mziki umekuwa faraja kubwa sana na njia ya kuwasilisha hisia kali za kibinadamu, kutuliza nafsi na kujitia nguvu katika roho zetu, Inaonekana kabisa katika maandiko kwamba moja ya njia kubwa sana ya kujijenga nafsi hasa kwa mtu aliyepitia mateso na magumu kuimba ni njia ya hali ya juu sana ya kujitia moyo hata katika Mungu, Biblia inashauri wazi kuwa mtu wa kwenu akipatikana na mabaya aombe na ana moyo wa kuchangamka na aimbe zaburi angalia katika

Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
 

Unaona andiko hili lina suluhu mbili maana yake hasa wakati mtu anapopatwa na maswala mazito, majaribu na kadhalika au mafanikio na furaha vyote hisia zote mbili zinaweza kupokelewa kwa kuomba na kuimba, Lakini vilevile wakati wa Mateso unaweza kuliitia jina la Bwana kwa maombi na anapokujibu unaweza kumuimbia kwaajili ya utukufu wake na Rehema zake alizotuonyesha kwa sauti

Zaburi 50:15 “Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”

Mziki uko karibu katika kila tamaduni za watu wa Duniani, na unatofautiana kutokana na mazingira, kwa sababu kila utamaduni una namna yake ya kutafasiri maana ya muziki na wimbo na kwa mujibu wa historia ya hiyo jamii, Utafiti mdogo pia usio wa kisayansi unaonyesha kuwa watu wa jamii iliyoteseka sana huwa wanaimba kwa hisia kali zaidi. Kwa hiyo mziki unawakilisha hisia za watu duniani na wakati mwingine hata bila ya kujua maneno yaliyomo kwenye wimbo husika kama umeimbwa kwa hisia unagusa hisia ya aina binadamu mwingine aliyepo popote. Paulo mtume aliweza kuwatia moyo Wefeso kuwa tunaweza kujengana na kusemezana kwa namna ya kipekee kwa njia Zaburi, tenzi na nyimbo za rohoni, kwa hiyo mziki na wimbo unaweza kabisa kuijenga jamii na kutunza mafundisho na maonyo na kuhekimisha watu na kutoa shukurani

Waefeso 5:19 -20“mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;” Kwa hiyo muziki una uwezo mkubwa sana wa kujenga maendeleo ya Kanisa na taifa kwa ujumla!

Katika kifungu cha Msingi kwa somo hili, Mungu anamwambia Musa aandike wimbo, bila shaka ulitungwa na Mungu mwenyewe na kuwa awape wana wa Israel ilikuweza kutunza historia ya matendo makuu ya Mungu, na kusudi jamii ijayo au kizazi kijacho kisiweze kusahau matendo makuu ya Mungu, hata baada ya Musa kumaliza kazi zake duniani, Mungu alijua wimbo utadumu na utaenda kizazi na kizazi na utawafunza watu na kuwakumbusha kuhusu matendo yake

Kumbukumbu 32:44-47 “Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki
.  

 
Kama uimbaji wa mziki ni swala linalokubalika kwa Mungu basi ni muhimu kwetu, kuangalia neno la Mungu linatuambia nini kuhusu Muziki na kuimba.

Neno la Mungu na umuhimu wa kuimba na mziki!

Maandiko matakatifu yaani agano la kale na agano jipya yanaunga mkono swala zima la kuimba na muziki kama mojawapo ya njia ya juu kabisa ya kuabudu, uwepo wa swala la Muziki na uimbaji katika maandiko unaonyesha wazi kuwa Mungu ameupa mziki na nyimbo umuhimu mkubwa sana na kuwa njia ya juu kabisa ya kuonyesha uwezo wetu wa kumuabudu Mungu ni pamoja na kumuimbia kabla ya wanadamu kugundua swala la muziki na uimbaji inasemekana huko Mbinguni nyimbo na muziki vilikuwa vinatumika na vinaendelea kutumika katika kumuabudu Mungu angalia

Isaya 14:11-15 “Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.  Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo

.
Maandiko haya yametumika sana na wanatheolojia kuyahusisha na anguko la Shetani aliyekuwa malaika mkuu na kiongozi mkubwa wa sifa nyota ya alfajiri au Lucifer yeye aliumbwa na uwezo mkubwa sana na kuimba na muziki akiwa moja ya maserafi wanaojua kusifu na kumuabudu Mungu kwa vinanda kama wazo hilimni kweli basi ninwazi kuwa uimbaji umetoka Mbinguni, na kama Mungu aliona umuhimu wa kumfundisha Musa wimbo kwaajili ya wana wa Israel ni wazi kuwa Mungu ndie mwanzilishi wa mziki na uimbaji, kwa hiyo ni wazi kuwa neno la Mungu linakubali kuwa uimbaji katika kusanyiko la watu wa Mungu yaani kanisa ni wa thamani kubwa sana katika kuonyesha namna na jinsi tunavyomuheshimu Mungu, kwa hiyo neno la Mungu linaruhusu matumizi ya vyombo vya muziki na aina flani ya mtindo wa kuabudu kwa vyombo hivyo wenye kufaa, na amri rahisi ni kumuimbia Mungu sawa na neno lake

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”


Unaona sasa Neno la Mungu linaagiza kwamba tujae neno, yaani tulijue neno, tujifunze neno la Mungu kwa kina na mapana na marefu kisha tunaweza kulitumia kwa mafundisho kwa  kuonyana, kwa kuliimba kama zaburi, tenzi na nyimbo kwa kadiri ya neema yake Mungu katika mioyo yetu! Kwa mtazamo wangu kuimba ndio ngazi ya juu zaidi ya maombi, naweza kusema kuwa mtu mwenye uwezo wa juu zaidi wa kuimba ndiyemwenye uwezo wa juu zaidi wa kukaribia uwepo wa Mungu au wa ibilisi, tunaweza kuonyesha kiwango chetu kikubwa sana cha kumpenda Mungu kupitia uwezo wetu mkubwa zaidi wa kuimba, mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu zaidi pia ndiye aliyekuwa muimbaji zaidi, na ndiyemwenye kitabu kirefu zaidi kuliko vyote katika agano la kale kitabu chenye zaidi ya asilimia saba ya agano la kale cha zaburi ni ushairi wa juu zaidi wa hisia za mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu, kadiri unavyoimba kwa hisia kali zaidi ndivyo unavyoweza kuugusa na kuufikia moyo wa Mungu na moyo wa mwanadamu hivyo uimbaji ni huduma kubwa sana ya upatanishi ni huduma ya kikuhani!.

a.       Biblia imeagiza watu waimbe

Mungu ametuumba ili tumuabudu, sisi ni vyombo vyake na ametuumba tukiwa na uwezo wa kuimba na kutengeneza muziki, wote tunajua sasa kwamba muziki ni wa muhumu sana katika kuabudu biblia imeamuru sisi tumuimbie watu wasiojua umuhimu wa kuimba hawatoi sauti zao wala hawajishughulishi kusikiliza maneno, kujumuisha hisia zao na kufuatilia au kuitikia uimbaji katika ibada ni muhimu kufahamu kuwa Mungu anataka tuimbe ni amri

i.                    Zaburi 95:1-3 “Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.”

ii.                  Zaburi 98:1-8 “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.  Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha.”

iii.                Zaburi 150:1-6 “Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;  Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

iv.                 Waebrania 2:12 “akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.”       

v.                   Waebrania 13:15 “Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

vi.                 Unaweza kuona maandiko yanaamuru sisi tumuimbie Mungu, Kama shauku yetu ni kuyatenda mapenzi ya Mungu, basi hakuna kitu cha ziada cha kukitafuta zaidi ya kile ambacho Mungu ameagiza katika neno lake jinsi na namna ya kumuabudu

b.      Watu wakubwa sana katika Biblia waliimba.

i.                     Yesu Kristo na wanafunzi wake waliimba angalia Mathayo 26:30Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.

ii.                   Mtume Paulo na Sila waliimba gerezani Matendo 16:25 “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.”


iii.                Mariam mama yake Yesu aliimba Luka 1:46-55 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele

iv.                 Malaika waliimba siku aliyozaliwa Masihi Luka 2:13-14 “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

v.                   Musa na wana wa Israel na Miriam walipovuka bahari ya shamu Kutoka 15:1-3 “Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.

Aidha Nabii Musa kabla ya kifo chake ama wakati anahitimisha maisha yake duniani alihitimisha kupitia nyimbo Kumbukumbu 32:1-43. Lakini pia inaaminika kuwa Zaburi ya 90 ni utunzi wa nabii Musa.

vi.                 Yoshua na Israel walipoukaribia Yeriko walipiga tarumbeta Yoshua 6:8-9 “Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana likawafuata. Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda.”

vii.               Deborah na Baraka waamuzi waliimba baada ya ushindi wao Waamuzi 5:1-3 “Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile, wakisema; Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini Bwana. Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli

viii.             Sulemani ni moja kati ya watu wakubwa sana ambao Mungu alipata kuwainua yeye naye alikuwa muimbaji biblia inasema alitunga nyimbo 1005 japo nyingi zilipotea 1Wafalme 4:29-34 “Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.”

ix.                  Daudi huyu ndiye mtu mkubwa zaidi katika maswala ya kuimba na muziki au tungeweza kusema huyu ndiye mwanamziki mkubwa zaidi kuliko wote katika maandiko, Katika Zaburi 150 zilizomo katika maandiko zaidi ya 75 hivi zimeandikwa na Daudi yeye anatajwa kama mtungaji wa nyimbo za Israel

2Samuel 23:1 “Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;”
alikuwa na uwezo wa kuimba kwa upako kiasi cha kutoa pepo 
1Samuel 16:14-23 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee. Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye.  Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo. Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake. Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu. Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”
Wakati wa utawala wake Daudi aliunda kwaya ya makuhani kwaajili ya kumuabudu Mungu kwa njia ya mziki 1Nyakati 15:16-19

Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha. Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi; na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu. Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;”

1Nyakati 23:1-5 “Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli. Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi; na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

Kwanini muziki nimuhimu kwa mujibu wa neno la Mungu!
a.       Hutumika kwaajili ya kuagana – Mwanzo 31:27 “Mbona umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi?

b.      Hutumika kuiimbia miungu – Kutoka 32:17-18 “Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita maragoni. Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi.”

c.       Hutumika wakati wa kusimika viongozi – 1Wafalme 1:39-40 “Na Sadoki, kuhani, akatwaa ile pembe ya mafuta katika Hema, akamtia Sulemani mafuta. Nao wakapiga panda; na watu wote wakasema, Mfalme Sulemani na aishi! Kisha watu wote wakapanda juu nyuma yake, watu wakapiga mazomari, wakafurahi furaha kubwa mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao.”

d.      Hutumika kufundishia - Kumbukumbu la Torati 31:19-22Basi sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli; kawatie vinywani mwao, ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa Israeli. Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu. Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa. Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo, akawafundisha wana wa Israeli.”

e.      Hutumika kuhamashisha – Muhubiri 2:7-9 “Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng'ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana. Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.” 

       
f.        Hutumika kujenga umoja – Mziki unafanya kazi muhimu sana ya kuwaleta watu pamoja, aidha katika huzuni au katika furaha au shereh, watu wanaweza kukusanyika pamoja na kuburudika Luka 15:25-27. “Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.  Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima.

g.       Hutumika kwaajili ya kujipa moyo –  Yesu na wanafunzi wake waliimba mara ya mwisho kabisa wakati Yesu anakaribia Marko 14:26 “Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni”. Zaburi 23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”

h.      Hutumika kwa maombolezo – Mathayo 9:23 “Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,” 

   
i.        Hutumika katika kutoa Pepo 1 Samuel 16:14-23 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee. Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye. Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo. Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake.Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu. Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.

j.        Unashusha uwepo wa Mungu 2Nyakati 5:12-14 “tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.”

Vyanzo vya muziki:-
Mziki kutoka kwa Mungu Zaburi 40:3 “Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana
Mziki kutoka kwa shetani- hii inakuwa na upako wa kishetani na huchochea na kuhamasisha na kukuza maswala ya uasi dhidi ya Mungu wa kweli.
Mziki kutoka kwa Mwanadamu Zaburi 57:7 “Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi,

  
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

0718990796/0784394550

Maoni 2 :

  1. If you're attempting to lose kilograms then you certainly need to start following this totally brand new custom keto meal plan.

    To create this keto diet service, certified nutritionists, fitness trainers, and cooks united to develop keto meal plans that are useful, convenient, economically-efficient, and fun.

    Since their first launch in early 2019, hundreds of clients have already completely transformed their body and well-being with the benefits a good keto meal plan can provide.

    Speaking of benefits: in this link, you'll discover 8 scientifically-tested ones given by the keto meal plan.

    JibuFuta
  2. Ahsante ndugu Mchungaji nimelielewa vizuri sana somo hili kwakweli umelifundisha kwa kina MUNGU wa Mbinguni may bless you

    JibuFuta