Mstari wa Msingi:- 1Wakorithio 12:4-6 “4.Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5. Tena pana
tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6. Kisha pana tofauti za kutenda
kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.”
Utangulizi:
Leo tutachukua Muda kuzungumzia kwa
kina na upana na urefu, ufahamu kuhusu vipawa vya Mungu, ambapo katika maandiko
zinaitwa karama, Nyakati za Kanisa la kwanza vipawa au karama zilifanya kazi
katika viwango vya juu sana na hivyo Mitume waliweza kuzungumzia ufahamu kuhusu
karama au vipawa akiwemo mtume Paulo alipokuwa akiwandikia kanisa la Korintho
ambalo lilikuwa na vipawa au karama vyingi sana ona 1Wakoritho 12:1 “Basi, ndugu zangu, kwa
habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.” Paulo mtume
alitaka watu wawe na ujuzi kuhusu vipawa vya Mungu au karama za rohoni, kwa
msingi huo sisi nasi tunaishi katika nyakati ambapo karama na vipawa vya Mungu
vinatenda kazi sana katika kanisa na hivyo ni muhimu kwetu kujua namna na jinsi
vinavyotenda kazi: tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipendele kadhaa
vifuatavyo:-
·
Tofauti ya
neno vipawa na Karama
·
Makundi
makuu matatu ya Karama
·
Karama za
Roho Mtakatifu
·
Matumizi
sahihi ya vipawa na karama:-
Tofauti
ya neno vipawa na Karama.
Kwa kawaida neno vipawa na karama yote
yana maana moja na yote hutolewa na Mungu, lakini neno kipoawa hutumika zaidi
kwa uwezo wa asili na Karama hutumika zaidi kwa uwezo unaotokana na neema ya
Mungu, kwa msingi huo katika kanisa na katika neno la Mungu, neema ya utendaji
inayotokana na Mungu inaitwa karama neno hili limetokana na tafasiri ya neno la
kiyunani CHARISMATA (KARAMA) NA VIPAWA
vimetokana na neno la Kiingereza TALENT sasa karama na vipawa hutofautiana katika
namna ifuatayo
1. Kipawa ni
kipaji kinachiowekwa na Mungu ndani ya mtu Tangu siku ya kuzaliwa
Karama ni
kipaji kinachowekwa na Mungu mara baada ya mtu kumuamini Yesu
2. Kipawa
kinaweza kurithiwa kutoka katika ukoo au wazazi
Karama
inatolewa kwa neema ya Mungu kama apendavyo Mungu mwenyewe
3. Kipawa
kinapokelewa kwa kuzaliwa na kinakuja kwa asili
Karama
inakuja kwa neema ya Mungu
4. Vipawa
vinaweza kutolewa kwa watu wote, waamini na wasioamini
Karama
zinatolewa kwa mtu aliyemuamini Yesu tu
5. Kipawa
kinaweza kumpatia mtu faida kubwa sana, umarufu, fedha na kadhalika
Karama
ziko kwaajili ya kumpa Mungu utukufu na kulijenga kanisa
6. Kipawa
kinaweza kuchochewa kwa mazoezi, kusomea na kujituma zaidi
Karama
zinachochewa na hali ya mkao wa kiroho, maombi, kusoma neno la Mungu,ibada
ushirika na kukua kiroho na mzigo wa kuwahudumia wengine
7.
Vipawa ni uweza wa Mungu ndani ya wanadamu bila kujali wanaamini nini au
kama wanamuamini Yesu au la Mungu humpa yeyote tu kama apendavyo inaweza
ikapitia katika vizalia Genetics vya kifamilia na kadhalika:- Mfano
a.
Yabali- Mwanzilishi wa kukaa katika Mahema na kufuga Mwanzo 4:20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika
hema na kufuga wanyama.
b.
Yubali – Mwanzilishi wa kupiga vinubi na vinanda na filimbi Mwanzo 4:
21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao
kinubi na filimbi.
c.
Tubal –Kaini Mfua vyuma na vyombo vya kukatia na shaba, Mwanzo 4:22
. Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila
chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa
Naama.
Karama zinapatikana kwa kuomba na vilevile kama Mungu mwenyewe atakavyo
kwa kadiri ya wingi wa neema yake .
Kwa msingi huo tunapozungumzia vipawa
vya Mungu, maana yake tunazungumzia Karama za Mungu, ni vipawa ambavyo asili
yake sio uwezo wa kibinadamu bali asili yake ni Neema ya Mungu kwa makusudi ya
kuujenga mwili wa Yesu Kristo yaani Kanisa lake ona
Warumi
12:6-8 “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo
mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa
kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha,
katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu,
kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”
Karama hizi zote hutolewa kwa kusudi
la kuujenga mwili wa Kristo, au kwa kufaidiana
kwa maana nyingine ni kuwa Mungu hutoa vipawa
na Karama kwa makusudi ya kusaidia wengine na si kwaajili yetu Binafsi 1Corithians
12:7 Biblia inasema “Lakini kila mmoja
hupewa….Kwa kufaidiana”
Makundi
Makuu matatu ya Karama:
Tunapozungumzia sasa kuhusu Karama katika maandiko
kuna Makundi makuu matatu ya karamaambazo hizi zinatoka kwa Mungu katika utatu
wake yaani Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kuna
Karama mbalimbali katika kanisa kama zilivyoainishwa katika maandiko ona
1Wakoritho 12: 4-6 “4. Basi pana tofauti za karama;
bali Roho ni yeye yule. 5. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi
zote katika wote.” Unaona unapochunguza maandiko hayo utaweza kuona
kuwa kuna tofauti za karama kwa maneno mengine kuna karama mbalimbali, kuna
zinazotoka kwa Mungu Roho Mtakatifu, Kuna zinazotoka kwa Bwana yaani Yesu
Mungungu mwana na kuna zinazotoka kwa Mungu yaani Mungu baba hivyo ni wazi kuwa
kuna makundi makuu matatu ya karama
1.
Karama kutoka kwa Mungu Baba hizi zinaitwa
karama za Masaidiano ambazo pia huitwa tofauti za kutenda kazi kwa kiyunani ni “DIAKONAI” GIFTS hizi ni karama za
utendaji wa kazi mbali mbali katika kanisa zinaweza kuwa kwa waamini mbalimbali
katama hizi zimetajwa katika Warumi
12:6-8 “6. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo
mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa
kadiri ya imani; 7. ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha,
katika kufundisha kwake; 8. mwenye
kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia
kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”
2. Karama
kutoka kwa Mungu mwana hizi zinaitwa Karama za huduma au tofauti za huduma hizi
zinahusika pia na maongozi ya kanisa Administration Gifts kwa kiyunani zinaitwa “ENERGEMATA”
GIFTS hizi ni karama za maongozi na ujenzi wa kanisa zinatajwa katika Waefeso 4:11-12 “11. Naye alitoa wengine kuwa mitume, na
wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na
waalimu; 12. kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma
itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;”
3. Karama
kutoka kwa Mungu Roho Mtakatifu, hizi ndio maarufu sana duniani kama karama za
roho ambazo zenyewe huusika na kuhudumia watu, karama hizi hutoa msaada mkubwa
katika maisha ya kanisa nan je ya kanisa hizi huitwa kwa kiyunani CHARISMATA zinatajwa hivyo katika 1Wakoritho 12:8-11 “Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na
mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho
yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine
matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine
aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;”
Karama za
Roho Mtakatifu:
Karama za Roho zinagawanyika katika makundi
makuu matatu na ziko tisa
a. Karama za Uwezo (the gifts of Power)
i.
Karama ya Imani au Neno la Mamlaka – faith or word of Authority
ii.
Karama za Uponyaji – Healings Gifts
iii.
Karama za Matendo ya Miujiza – “the work of Miracles”
b. Karama za Ufahamu (Revelations Gifts)
i.
Karama ya Neno la Hekima – The word (Message) of wisdom
ii.
Karama ya neno la Maarifa – The word (Message) of Knowledge
iii.
Karama ya kupambanua Roho – Discerning of the spirits
c. Karama za Usemi (Saying Gifts)
i.
Karama ya Unabii – Prophecy
ii.
Karama ya aina za Lugha- Diferrents Tongue
iii.
Karama ya tafasiri za Lugha – Interpreting of Language
Uchambuzi
wa Makundi makuu matatu ya Karama za Roho Mtakatizu:-
Karama
za Uweza
i.
Karama ya
Imani au Neno la mamlaka hii ni karama ya Roho Mtakatifu kwa mtu
aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kunena maneno yenye Mamlaka na
maneno hayo yakatimizwa au kusababisha muujiza
a. Mfano Musa
alisema Kutoka 14:13-14 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone
wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo
hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya”
b. Elisha 2Wafalme 4:16-17 “Akasema,
Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe
mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo. Yule mwanamke akachukua
mimba, akazaa mtoto mume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia”
c. Eliya 1Wafalme 17:1 “Basi
Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa
Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua
miaka hii, ila kwa neno langu.”
d. Nabii Yoshua Katika Yoshua 10:12-13 “Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo
Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya
Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika
bonde la Aiyaloni. Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa
lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao”
e. Petro katika Mlango Mzuri Matendo 3:1-10 “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda
hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni
mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa
hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu
huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na
Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia,
akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala
dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na
vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza
kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu
Mungu”
f.
Yesu
alipousemea Mtini Marko 11:12-14 “Hata asubuhi yake
walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda
ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana
si wakati wa tini. Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda
kwako. Wanafunzi wake wakasikia.” Kisha Marko 11:20-22 “Na
asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro
akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.
Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.”
ii.
Karama za
Uponyaji: Ni karama za Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu
huyo kuwa na uwezo wa kumuombea mtu mwenye ugonjwa au homa na kumuwezesha mtu
huyo kupona kwa neema ya Mungu.
a. Mfano Yesu aliponya wengi Mathayo 4:23-24 “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha
katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa
na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu
yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na
mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.”
b. Wanafunzi wa Yesu wote Mathayo 10:1 “Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu
ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.”
c. Petro alimponya ainea Matendo 9:33-34 “Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo
amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia,
Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.”
iii.
Karama za
Matendo ya Miujiza – Ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu
huyo kwa uweza wa Roho Mtakatifu kuwa na Neema na uweza wa Mungu kumuombea mtu
au mfu na kusababisha muujiza wa kupita kawaida kutokea mfano
a. Paulo Mtume alitumiwa mno katika karama za
matendo ya Miujiza Matendo ya Mitume
19:11-12 “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo
miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka
mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.”
b. Yesu Kristo mwenyewe kwa Kulisha watu wengi kwa
mikate michache Luka 9:13-17 “Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu
zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa
wote vyakula. Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia
wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini. Wakafanya
hivyo, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili,
akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili
wawaandikie mkutano. Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia
walikusanya vikapu kumi na viwili”
c. Yesu Kumfufua Mfu Luka 7:11-15 “Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na
wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.Na alipolikaribia
lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye
ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. Bwana alipomwona
alimwonea huruma akamwambia, Usilie. Akakaribia, akaligusa jeneza; wale
waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. Yule maiti
akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake”
Karama
za Ufahamu. (Revelations Gifts)
Hili ni kundi la Karama za Roho kwa
Mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa neema ya ufahamu wa ndani na wa kina
kuhusu mambo, au maswala ya mtu kwa kusudi la kuleta suluhu inayokusudiwa,
Karama hizi zaweza kuwa za kudumu, lakini pia zaweza kumjia mtu wakati wa
kutatua tatizo
i.
Karama ya
neno la Hekima 1Wakoritho 12:8 “Maana mtu mmoja
kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye
yule;” – Nikarama kwa mtu
aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kutatua matatizo
yanayojitokeza kwa mtu au katika jamii kwa kusudi la kuleta suluhu, Ni karama
ya neema kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo wa kwenda nyuma ya
tatizo au mbele ya tatizo na kunga’mua na kuweza kuleta suluhu au kuondoa utata
Karama hii
inasaidia kushughulikia maswala kadhaa yafuatayo:-
·
Kufunua Makusudi ya Mungu – Purposes
·
Kufunua Mpango wa Mungu - Plan
·
Kufunua Mapenzi ya Mungu - will
·
Kufunua Mashauri ya Mungu - council
a.
Uwezo wa Kufasiri Ndoto Mwanzo 41:1-36 “Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto;
na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono,
walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine
wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale
ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale
ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya
pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa
na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba
yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni
ndoto tu. Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga
wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto
yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.
Basi mkuu wa
wanyweshaji akamwambia Farao akisema, Nayakumbuka makosa yangu leo. Farao
aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari,
mimi na mkuu wa waokaji. Tukaota ndoto usiku mmoja, mimi na yeye; kila mtu kwa
tafsiri ya ndoto yake tukaota.Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana;
Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto
zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. Ikawa, kama vile alivyotufasiria
ndivyo ilivyotokea; mimi nalirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa.
Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani.
Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. Farao akamwambia Yusufu,
Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya
kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri.
Yusufu akamjibu
Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani. Farao akamwambia
Yusufu, Katika ndoto yangu nalikuwa nikisimama ukingoni mwa mto; na tazama,
ng'ombe saba wanatoka mtoni, wanono, wazuri, wakajilisha manyasini.Kisha,
tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya sana,
wamekonda; katika nchi yote ya Misri sijaona kama hao kwa udhaifu. Na hao
ng'ombe waliokonda, wabaya, wakawala wale ng'ombe saba wa kwanza, wale wanono.
Na walipokwisha kuwala haikutambulikana ya kwamba wamewala, bali wakaonekana
wabaya kama kwanza. Basi nikaamka. Kisha nikaona katika ndoto yangu, na tazama,
masuke saba yanatokeza katika bua moja, mema, yamejaa. Na tazama, masuke saba
membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Na
hayo masuke dhaifu yakameza yale masuke saba mema. Nami nikawaambia hao
waganga, wala hakuna aliyeweza kunionyesha maana yake.Yusufu akamwambia Farao,
Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.
Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba.
Ndoto ni moja.
Na wale ng'ombe
saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba
matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo
nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi
karibu.Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. Kisha
kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika
nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. Wala shibe ile haitajulikana katika
nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana. Na ndoto
ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu
amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Basi, Farao na ajitafutie mtu wa
akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke
wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika
miaka hii saba ya kushiba.Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo,
wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika
miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya
njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.kwa” Yusuphu, Kupitia ndoto ya Farao
Yusufu aliweza kutatua tatizo ambalo lingeikumba dunia ya wakati ule kwa njaa.”
b. Uwezo wa kujua uovu uliofichika 2Wafalme 5:20-27 “Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema,
Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake
vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu
kwake. Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio
anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? Akasema,
Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka
milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta
ya fedha, na mavazi mawili. Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili.
Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na
mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.
Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha
wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya
bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako
hakuenda mahali. Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka
yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na
kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe,
na watumwa, na wajakazi? Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako
hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.” Eliya
aliweza kuona nuovu uliokuwa ukifanya na Mtumishi wake Gehazi
c. Uwezo wa kujua Mapenzi na Mpango
wa Mungu kuhusu Mambo yajayo Daniel 2:1-47, Daniel alitumiwa na Mungu Kufasiri Ndoto ya
Nebuchadneza iliyohusu maswala yajayo.
d. Uwezo wa kujua tukio lililoko
mbele ya upeo wa Macho ya kibinadamu Marko 14:12-15 “Hata
siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake
wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka? Akatuma wawili
katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini;atakutana nanyi mwanamume
amechukua mtungi wa maji; mfuateni; na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye
nyumba, Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo,
pamoja na wanafunzi wangu?Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa
tayari; humo tuandalieni.” Yesu
aliweza kuwaambia wanafunzi wake kuhusu mtu atakayewapatia Chumba cha
Maandalizi kwaajili ya Pasaka
e. Uwezo wa kujua mipango ya adui na
kuidhibiti mapema kabla ya kupata madhara 2Nyakati 20:12-23 Elisha aliweza
kumtahadharisha mfalme wake kuhusu mipango ya adui ya majeshi ya Washami.
ii.
Karama ya Neno la Maarifa 1Wakoritho 12:8 “Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la
hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;” Karama
ya neno la Maarifa Neno “Logos” the
spoken word Neno linalosemwa, Maarifa ni “Gnosis”
Knowing Kujua au kuvumbua, Hivyo Karama ya neno la Maarifa ni karama inayowekwa
na Mungu Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uweza
wa kiungu wa kuweza kujua Mazingira ya matatizo yanayowazunguka watu kwa kusudi
la kuleta suluhu, Mfano:-
a. Yohana 4:16-19 “Yesu
akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. Yule mwanamke akajibu, akasema,
Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; kwa maana umekuwa na waume
watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. Yule mwanamke
akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!”
b. Matendo 5:1-10 “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira
mkewe, aliuza mali,akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua
haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania,
kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia
kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na
kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje
hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote
walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje,
wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya
hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo?
Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana
kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao
watakuchukua nje wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana
wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.”
c. Mungu alimfunulia Nuhu namna ya kujenga Safina Mwanzo 6:12-13 Na kuonya juu ya hatari
itakayokuja kwa dunia
d. Mungu alimfunulia Abrahamu kuhus Israel kwenda utumwani Misri Mwanzo 15:13-14
e. Mungu alimfunulia Yusufu kwa Njia ya ndoto kuhusu kuwatawala Ndugu
zake Mwanzo 37:5-9
f.
Mungu alimfunulia Yoshua Dhambi
iliyofanyika kambini Yoshua 7:10-15
g. Samuel aliweza kujua Punda waliopotea kuwa wamepatikana 1Samuel 9:20
h. Nathan aliweza kuijua dhambi ya Daudi 2Samuel 12:1-7
i.
Mikaya aliona kushindwa na kuawa
kwa Ahabu vitani 2Nyakati 1-47
j.
Mungu alimuonya Yusufu kuhusu
mpango wa Herode dhidi ya Mtoto Yesu Mathayo
2:13
k. Mungu alimfunulia Simeoni kuwa hatakufa mpaka atakapomuona Masihi Luka 2:26
l.
Mungu alimfunulia Anna kuwa Yesu
ni Masihi Luka 2:38
m. Yesu alizungumza habari za Nathanael Tangu alipokuwa ameketi chini ya Mtini Yohana 1:45-51
n. Nabii Agabo aliona njaa itakayoikumba Yerusalem Matendo 11:28
o. Nabii Agabo aliona Mateso na kifungo cha Paulo Mtume yatakayompata huko Yerusalem Matendo 21:10-11
p. Paulo Mtume aliweza kuona hatari iliyoko safarini Matendo 27:10
iii.
Karama ya kupambanua roho 1Wakoritho 12:10 “na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine
unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine
tafsiri za lugha;” Ni karama kwa
mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kwa neema ya roho Mtakatifu kuwa na uwezo
wa kujua ni roho ya aina gani inatenda kazi katik ya Roho wa Mungu, roho ya
binadamu nay a shetani
a. Yesu alijua roho iliyotenda kazi nyuma ya maneno ya Petro Mathayo 16:22-23 “ Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo
hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo
kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
b. Yesu alijua roho iliyokuwa ikitenda kazi nyuma ya Yakobo na Yohana
Luka 9:54-55 “Wanafunzi
wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto
ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]”
c. Petro aliweza kumtambua Simon Mchawi kuwa yu katika uchungu Matendo 8:18-23 ” Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho
Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Nipeni
na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho
Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe,
kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala
huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira
hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u
katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu.”
d. Paulo Mtume alimtambua Elima yule Mchawi na kumdhibiti Matendo 13:6-12” Walipokwisha
kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa
uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio
Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake,
akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri
ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile
imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia
macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa
haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa
Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi
kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na
kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini,
akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.”
e. Paulo Mtume alimtambua Pepo aliyekuwa ndani ya kijakazi kule Efeso
Matendo 16:16-18 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi
mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida
nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa
ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya
hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo,
Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.”
f.
Karama ya kupambanua Roho
inatusaidia kujua ni roho gani inatenda kazi, sio kila roho inayotoa unabii au
kufanya ishara na miujiza au hata kuzungumza unabii wa kweli inatokana na
Mungu, maandiko yanatutaka tuzipime 1Yohana
4:1 “Wapenzi,
msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa
sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.”
Kwa nini kuna umuhimu wa kuzipima roho kwa sababu ziko roho za
uongo, yako mafundisho ya uongo, wako manabii wa uongo na kama kanisa tunapaswa
kujua namna roho hizo zinavyotenda kazi na kuzipambanua ili kuweza kupata
uhakiki wa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu
1Wafalme 22:19-24 “Mikaya
akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake
cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na
wa kushoto. Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee
Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana,
akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka,
na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na
kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo
kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako”
Ni muhimu kupima roho kwani siku za mwisho maandiko yanatuonya
kuwa yako mafundisho ya mashetani, na fundisho pia au maneno katika maandiko
huitwa roho Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo
niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Unaweza kuona kumbe kama
maneno ni roho hatuna budi kuwa na karama ya kupambanua roho ili kujua ni roho
gani inatenda kazi kati ya roho ya kibinadamu, ya shetani na ya Mungu, Mungu
haoni shani kuulizwa, mwanatheolojia aliyekamilika haoni shaka kuuliza sauti
anayoisikia kama ni ya Mungu au ya mwanadamu tunahitaji karama ya kupambanua
roho hususani katika nyakati hizi za mwisho
Paulo mtume alipotokewa na maono alihoji ni nani wewe Bwana
ninayekuudhi na Yesu alijibu kuwa ni Mimi Yesu unayeniudhi, kumbuka alisikia
sauti na mwanga mkali ulimulika na Mungu akasema naye Paulo alitaka kujua ni
roho gani inasema naye ni maono gani anayaona yanatoka kwa Bwana yupi Matendo
ya Mitume 9:1-5 “Lakini Sauli,
akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona
watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. Hata
alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote
nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini,
akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe,
Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.”
Kwa msingi huo Kanisa ililiweze kujilinda na mafundisho ya
mashetani na roho zidanganyazo hatuna budi kuhakikisha kuwa tunamuomba Mungu
atupe kupambanua roho, katika kazi ya nabii karama ya kupambanua roho ni ya
muhimu sana.
Karama za Usemi:-
Karama za Usemi ni karama kwa mtu
aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na neema ya Mungu kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu, kutoa ujumbe wa kinabii, kuzungumza lugha asiyoifahamu na kutafasiri
Lugha asiyoifahamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu bila kutumia akili ya
kibinadamu. Karama hizi zinatajwa katika
1Wakoritho 12:10. “na mwingine matendo ya miujiza;
na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na
mwingine tafsiri za lugha;”
Karama
hizi zinawekwa katika fungu moja kwa sababu zinahusisha kinywa
i.
Karama ya Unabii – Prophecy
ii.
Karama ya aina za Lugha- Diferrents Tongue
iii.
Karama ya tafasiri za Lugha – Interpreting of Language
Karama ya Unabii – Prophecy 1Wakoritho 12:10
Krama ya
unabii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa
kutangaza au kuzungumza mapenzi ya Mungu, au kutafasiri makusudi ya Mungu, na
kuyafanya yajulikane kwa wahusika kwa kusudi la kuwajenga watu au kuwatia moyo,
Karama hii haimfanyo mtu awe nabii, inngawa nabii anapaswa kuwa na karama hii,
Karama hii pia sio lazima izungumzie maswala yajayo ingawa kuzungumzia mambo
yajayo ni sehemu ya karama hii, kwa ufupi karama hii inahusu kuwajenga watu
kuwatia moyo na kuwaelekeza katika mapenzi ya Mungu hususani katika wakati
uliopo
Unabii
kamwe haupaswi kutolewa kwa Mapenzi ya kibinadamu, bali unatoka kwa Mungu kwa
kadiri ya neema ya Roho Mtakatifu anavojalia na kusukuma hilo kutendeka, 2Petro1:21 “Maana
unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena
yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” Ujumbe wa
kinabii wakati wote utajihusisha na kujenga, kufariji, kutia moyo na kuelekeza
mapenzi ya Mungu kwa watu wake na kanisa
1Wakoritho 14:3 “Bali yeye ahutubuye, asema na watu
maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.” Mifano ya
karama za unabii
a.
Matendo
13:1-3 “Na
huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni
Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa
ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia
Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa
kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao
juu yao, wakawaacha waende zao” Tunawezaje kujua hapa kuwa Roho
Mtakatifu alisema? Ni wazi kuwa kanisa lilikuwa na manabii kama inavyoelezwa
katika Mstari wa Kwanza na hivyo kupitia karama ya unabii Roho Mtakatifu
alikuwa ameweka wazi Mapenzi yake kwa kanisa la Antiokia
b.
Mtumishi wa Mungu kama Timotheo alitambuaje
kuwa amitwa katika utumishi ilikuwa ni kupitia unabii 1Timotheo 4:13-14 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya
na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa
unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.”
c.
Kusudi kuu la Karama ya unabii ni kujenga watu
na sio kuwaumbua au kuwadhalilisha 1Wakoritho
14:4 “Yeye
anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.”
Karama ya aina za Lugha – Ni
karama ya neema ya Mungu kwa Mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu
kumuwezesha mtu huyo kunena kwa lugha za wanadamu au malaika bila ya kutumia
akili
a. Mfano ni Katika Matendo 2:1-12 “Hata ilipotimia
siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi
kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa
wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia
kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi
wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii
iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja
aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu
wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi
kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Warparthi na Wamedi na Waelami,
nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia,
Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na
waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo
makuu ya Mungu. Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake
nini mambo haya?”
b. Biblia inathibitisha kuwepo kwa Lugha za
wanadamu na malaika 1wakoritho 13:1 “Nijaposema kwa
lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na
upatu uvumao.” Hata hivyo matukio ya kuzungumza lugha za
wanadamu kwa uweza wa Roho Mtakatifu yameendelea kuwa nadra katika miaka ya
kizazi chetu.
Karama ya tafasiri za Lugha – Ni
karama ya neema inayowekwa na Mungu Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka
kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kuzungumza au kutafasiri lugha za
wanadamu au malaika asizozijua au kujifunza bila kutumia akili
a. Mfano ni
Nabii Daniel aliweza kutafasiri Lugha ngeni iliyosumbua wengi Daniel 5:1-30 “Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake
elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao. Belshaza, alipokuwa akionja
ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba
yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba
mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.Basi
wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya
Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na
masuria wake, wakavinywea. Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya
fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe. Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa
mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme,
mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono
ulioandika. Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha;
viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana. Mfalme akalia kwa
sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme
akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko
haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na
kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika
ufalme.
Basi
wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale
maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake. Ndipo mfalme Belshaza
akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa. Basi
malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba
ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako
zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike. Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye
roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru
na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako,
naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na
Wakaldayo, na wanajimu; kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na
ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua
mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza.
Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri. Ndipo Danieli akaletwa mbele
ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Je! Wewe ndiwe Danieli yule,
aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta
huku toka Yerusalemu? Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani
yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako. Basi sasa,
watu wenye hekima na wachawi wameletwa mbele yangu, wapate kulisoma andiko
hili, na kunijulisha tafsiri yake; lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri ya
jambo hili.
Lakini
nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya!
Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi
ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa
mtu wa tatu katika ufalme. Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme;
Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini
nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.
Kwa
habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme,
na ukuu, na fahari, na utukufu; na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa
kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake;
aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka
kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.Lakini moyo wake
ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa
katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na
wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa
pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji
kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala
katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye
yote. Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua
hayo yote.
Bali
umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele
yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe
umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na
ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye
pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza. Ndipo kile
kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya
yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.
Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na
kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.
PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. Ndipo
Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau,
wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake,
ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa
Wakaldayo, akauawa.”
Matumizi
sahihi ya vipawa na karama:-
Karama
hazinunuliwi – wala haziuziwi – Mathayo
10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye
ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.” Matendo 8:18-20 “18. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho
Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, 19.
Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho
Mtakatifu. 20. Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja
nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.”
Karama
hazipaswi kutumiwa kwa kudhalilisha watu wa Mungu – Karama
za Mungu ni neema ya Mungu juu ya mwamini, hatupaswi kuzitumia Karama kwa
kuzalilisha watu, mfano sio vema kumkanyaga mtu unapomuombea huko ni kukosa
nidhamu biblia imeelekeza sehemu za kuombea Marko 16:17-18 “17. Na ishara hizi
zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya; 18. watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru
kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Karama
hazipaswi kutumika kwa chuki na kuligawa kanisa – Karama
zinapaswa kutumika kwa upendo na sio kwaajili ya majivuno au kuligawa kanisa
ukuaji wa kiroho wa mtu haupimwi kwa namna anavyotumiwa na Mungu unapimwa kwa
upendo 1Wakoritho 12: 1-3. “1Nijaposema
kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na
upatu uvumao. 2. Tena nijapokuwa na
unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi
cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3. Tena nikitoa
mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto,
kama sina upendo, hainifaidii kitu.”
Karama
hazipaswi kutumika kwa kiburi na majivuno – Lucifer alikuwa ni malaika mwenye
kipaji kikubwa sana lakini alikataliwa na kutupwa kutoka mbinguni kwa sababu ya
kiburi, Kanisa la nyakati za leo limepitia changamoto nyingi kwa sababu watu
hawataki kuonywa na kuelekezwa kuwa na karama hakumaanishi kuwa hatupaswi
kupokea ushauri na maonyo kutoka kwa
wengine au kujivuna kama ilivyokuwa kwa shetani tukiwa na kiburi Mungu
ataruhusu aibu kubwa sana Ezekiel 28:14
-19 “14. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta
afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu,
umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15. Ulikuwa mkamilifu katika njia
zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. 16. Kwa
wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda
dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu
kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe
hayo ya moto. 17. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu
hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya
wafalme, wapate kukutazama. 18. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi
wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako,
nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu
wote wakutazamao. 19. Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia;
umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.”
Kadiri
tunavyokuwa na vipawa vikubwa sana ndivyo tunavyotakiwa kuwa wanyenyekevu kwa
kiwango kikubwa ili Mungu atukuzwe na kukututumia zaidi Wafilipi 2:3-9 “ Msitende neno lo lote kwa kushindana wala
kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora
kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu
aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo
pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali
alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa
mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
”
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
MUNGU akubariki Sana mtumishi kwa ufafanuzi wako hakika nimejifunza kitu kupitia darasa hili. MUNGU azidi kukupa maarifa mengi zaidi.
JibuFutaNENO LA NGUVU ZAIDI NA WINGI WA UTUKUFU WA MUNGU!
JibuFutaHakika mungu akubariki Sana kwa huduma yako
JibuFutaMungu akupe neema kuu yenye mamlaka ya ki Mungu ndani yake
JibuFutaUmebarikiwa mtu wa Mungu, nimejifunza mengi kupitia post hii
JibuFutaMungu akubariki kwa ujumbe mzuri
JibuFutaMungu akubariki
JibuFuta