Jumanne, 28 Oktoba 2014

Jinsi Ya Kutunza Uwepo Wa Roho Mtakatifu



Mambo yanakwenda shaghala baghala kinaweza kuwa kilio cha watu wengi waliookoka katika nyakati tulizonazo, kila kitu katika maisha kinachoachwa chenyewe bila kushughulikiwa kinasambaratika kama ni katika maswala ya kisayansi tungweweza kusema kuwa mambo ynajiendea kiasili bila utaratibu

   Hivi ndivyo inavyokuwa katika ulimwengu wa kiroho kadhalika mambo yasipokuwa na usimamizi madhubuti hatimaye yanaparaganyika, karama isipochochewa inakufa 2Timotheo 1;6 Paulo alimuandikia Timotheo kusudi kwamba aichochee karama iliyo ndani yake, Maisha ya kiroho wakati wote  yatahitaji kuendenda kwa roho ili kuweza kuyatunza Wagalatia 5;25, Ni muhimu kukumbuka kuwa tunayaanza maisha yetu ya kiroho kwa kuzaliwa mara a pili baada ya kuzaliwa kiroho kutokana na Roho wa Mungu, na baada ya kuzaliwa huko kunakotokana na Roho wa Mungu tunahitajika kujazwa na Roho Mtakatifu mara moja  na ujazo huo unafungua mlango wa kukutana na aina nyingne za Baraka za Mungu.

   Kila mtu anayekuwa amepitia hatua hiyo analazimika sasa kutokuridhika na kiwango hicho na kubweteka kwa sababu tu eti amebatizwa katika Roho hatua hiyo sio mwisho hata kidogo kwa ujumla ndio mwanzo wa safari ya kiroho, na wala mtu asifanye makosa kusema kwakuwa sasa amejazwa kwa Roho anaweza kustarehe na kujishughulisha na maswala mengine zaidi, ni muhimu kuzingatia kuwa maisha ya kuendelea kuwa na ufahamu zaidi na kutembea na Roho Mtakatifu yanapaswa kuunzwa na kuendelezwa  zaidi katika kijitabu hiki tunataka kujadili jinsi ambavyo mtu aliyejazwa kwa Roho Mtakatifu anavyoweza  kuendelea kutembea na Roho Matakatifu  na katika kuiyatimiza hayo tutajadili maswala makuu mawili yaani Umuhimu wa kutunza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu na muongozo wa namna ya kuendeleza maisha ya ujazo wa Roho Mtakatifu na kwa kufanya hayo maisha ya kiroho hayataweza kuparaganyika kiasi cha kutokupata kibali mbele za mfalme na kutokukataliwa wakati wa kuja kwake au kuwamfano wa wale wanawali wapumbavu watato ambao Bwana Harusi alipokuja alikuta taa zao hazina mafuta Bwana ampe neema kila mmoja wetu anayepitia kijitabu hiki kutokupoteza Nguvu za Roho Mtakatifu na kuyaona mambo akiparaganyika katika jina la Yesu Kristo Amen!


 SOMO LA KWANZA: UMUHIMU WA KUTUNZA HALI YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.

Mara baada ya mwamini kumpokea Roho Mtakatifu swala la kuhusu kutunza na kuendeleza ujazo wa Roho Mtakatifu huwa halitiliwi mkazo wala halina maundisho na itakuwa ni uzembe wa hali ya juu kudhani kuwa hakuna la ziada la kufanya kwani hali ya ujazo wa Roho Inapaswa kutunzwa siku zote za maisha yako.

§  Uzoefu wa ujazo ni lazima utunzwe.

Haijalishi mtu ana upako kiasi gani au alifurika kiasi gani wakati wa kujazwa Roho Mtakatifu ana weza akawa amejazwa kwa nguvu kubwa sana lakini kama mwamini huyo hatunzi kile alchokipokea katika maisha yake kupitia maisha ya maombi, kushuhudia,na kuishi maisha matakatifu ukweli ni kuwa mtu huyo atapoa haraka sana na haribiko litafuata ni muhimu kufahamu kuwa Ujazo wa Roho Mtakatifu unamleta mwamini katika uhusiano na Roho ambao unapaswa kudumishwa kwa  kiutunza na kuuendeleza kila wakati.

§  Wajibu wa kila Mwamini.

Kila mwamini katika Kristo anapaswa kukubali kwamba anawajibika katika kutunza maisha yake ya Kiroho, Ingawa Mchungaji na washirika wengine jamaa na marafiki katika Bwana wanaweza kukutia moyo na kukuchochea katika swala zima la kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ni muhimu kufahamu kuwa jukumu la mwisho ni lako mwenyewe kwa msingi huo ni lazima ujifunze kujitia nguvu mwenyewe katika Bwana 1Samuel 30;6.

Kushindwa kulisimamia hilo matokeo yake yatakuwa ni kurudi nyuma na kupoteza nguvu, na kwa bahati mbaya mtu anaweza hata kupoteza wokovu na ni kwa kusudi hilo Paulo alimuhimiza Timotheo kichochea Karama  iliyokuwa ndani yake 2Timotheo 1;6 kama jinsi tanuru la moto linavyohitaji kuchochewa kupitia kuni ndivyo na maisha yetu ya kiroho yanavyopaswa kuchochewa na kama tukilala usingizi moto huo na utazimia  kwa msing huo ni muhimu kwetu kuhakikisha kuwa tunawajibika kikamilifu  katika kutunza maisha yetu ya kiroho.

SOMO LA PILI: MUONGOZO WA KUTUNZA HALI YA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.

Moto unahitaji kuchochewa ili uweze kuendelea kuwaka  na mafita yanahitaji kuongezwa  ili kuongezea mwanga kuwaka zaidi katika namna kama hiyo ni muhimu kuendelea kuwa na wakati wa kujisimamaia na kujichunguza na kuyalinda maisha yetu ya kiroho  kwa kujiangalia kila wakati ili kutunza hali ya ujazo wa Roho Mtakatifu, Paulo mtume aliwafundisha wakoritho kuwa na tabia ya kujihoji wenyewe  ili kujiona kuwa uko kaika kiwango gani cha kiimani 2Wakoritho 13;5 kila mwamini anao wajibu na anapaswa kukubali wajibu wa kujisimamia kiroho na kama mkristo akiharibika kiroho chake hana mwingine wa kumlaumu isipokuwa ajilaumu yeye mwenyewe

Mtu anaweza kujiuliza Kama ninawajibika kujisimamia kiroho changu mwenyewe je ninapaswa kufanya nini? Na ni hatua gani ninaweza kuchukua katika kuhakikisha kuwa ninadumu katka kutembea na Roho katika maisha yangu? Yako maswala ya msingi nane ambayo tutayaangalia kama mbinu za kuhakikisha kuwa unajisimamia kiroho na unatuza maisha yenye kujawa na Roho wa Mungu.

§  Tafuta kujazwa upya kila wakati.

Kama mkristo anataka kubakia akiwa amejaa Roho Mtakatifu ni lazima atafute kujazwa na Roho Mtakatifu kila wakati kama ilivyoainishwa kuwa kila mwamini ni lazima abatizwe katika Roho Mtakatifu mara tu anapokuwa ameokoka Matendo 1;4-5, 8:14-17 ubatizo huo wa Roho Makatifu ni neema ya ajabu katika maisha yetu. Ingawa mwamini anapaswa kutambua kuwa kubatizwa katika Roho Mtakatifu sio mwisho wa kuendelea kujaa tena na tena na kila mwamini ni lazima atafute kujazwa tena na tena siku zote za maisha yake

Tunaweza kuona ushahidi katika maandko kwamba wanafunzi wa bwana walijaa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste katika Matendo 2;4 lakini huo haukuwa mwisho kwani wakati Fulani tena walijazwa tena Matendo 4;8,31, Paulo alijaa Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza huko Dameski Matendo 9;17-18 lakini alijazwa tena huko Kipro Matendo 13;9 Wanafunzi huko Efeso walikuwa wamejazwa Roho walipoammini na Paulo alipoweka mikono juu yao  Matendo 19;6 lakini alipowaandikia Waefeso aliwasihi wajae Roho Waefeso 5;18, Kila mwamini anapaswa kujazwa kwa Roho Mtakatifu lakini anapaswa kujazwa upya kila wakati  katika maisha yake ya Ukristo.

Unaposoma kwa makini jinsi na namna Paulo anavyowaasa waefeso kujazwa na Roho katika Waefeso 5;18 pia utaweza kugundua kuwa kanuni ya kukazia kujazwa na Roho inakaziwa kama kanuni ya kanuni ya nguvu za kiroho na tena neno hilo katika Biblia ya kiyunani mjezwe Roho liko katika wakati uliopo na unaoendelea , hii ikiwa na maana basi mjazwe Roho ni tendo endelevu kwa lugha rahisi tungeweza kusema muwe mnajazwa Roho. Dr Stanley Horton alichangia hivi kuhusu andiko hilo la Waefeso 5;18 “Tunapaswa kutunza kuendelea  kujazwa Roho Mtakatifu” na hii ndio maana halisi ya adniko hilo katika kiyunani kwa hivyo sio swala la kujazwa mara moja tu hapana! Ni swala endelevu kama kitabu cha matendo ya mitume kinavyoweza kuonyesha.

Mkristo aliyejaa Roho anapaswa kujua kwamba anapaswa kuendelea kutunza hali ya kuendelea kujazwa Roho kila siku ya maisha yake , Yesu alipokuwa akizungumza kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu alisema hivi Nami nawaambia Ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtaona bisheni nayi mtafunguliwa”  Luka 11;9 baadaye alisisistiza hili katika mstari 13  “basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema  je Baba aliye mbinunihatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamuombao” unaweza kuona Dr. Horton  Mtaalamu na mwalimu wa maswala ya Roho Mtakatifu Duniani anasema hivi  swala la kuomba kutafuta na kubisha  ni swala endelevu na sio la mara moja  kwa msingi huo nikama Yesu anasema endeleeni kuomba, endeleeni kutafuta na endeleeni kugonga kwa maana kila anayeendelea kufanya hayo atapokea, Ili kuendelea kujaa Roho Mkristo anapaswa kuendelea kutafuta kujaa Roho kwa hiyo swala la kupokea au kujaa Roho ni swala endelevu.

§  Omba bila kukoma.
Moja ya maswala a msingi ambayo yanaweza kumuweka mwamini kaika hali ya kujaa Roho ni kuomba  kuomba bila kukoma ni maombi endelevu 1Thesalonike 5;17 maombi ni muhimu sana kwakla mkristo ni kama kujitia nidhamu kwa msingi huo mkristo anapaswa kuishi maisha hayo ya kujitia nidhamu na kujitia nidhamu ni kutembea katika Roho,Paulo anawaambia wathesalonike  kuendelea kuomba kila wakati na kushukuru katika mazingira ya aina yoyote na kwamba wasimzimishe Roho angalia mstari ule wa 17-19 kumbuka na angalia kwa makini hapa ni kama Paulo anasema kama Mwamini akiendelea kuomba hatafanya makosa ya kumzimisha Roho mstari wa 19 kwa msing huo msiatari hii inapaswa kutafasiriwa kivitendo tusiache kuomba, Paulo aliwafundisha waefeso kwamba mwamini ana vita vya kiroho Waefeso 6;10-18 na alikamilisha maelekezo yake kwa kuwataka waombe katika Roho mstari wa 18  somo liko wazio hapa kwamba ili kuyatunza maisha yetu kiroho  na kuwa tayari kwa vita ya kiroho tunapaswa kuomba katika Roho katika mazingira yote  maana yake ni kuwa kila siku tunapaswa pia kuomba kujazwa kwa upya na Roho na kuhitaji muongozo wake katika maisha yetu, au maombi yetu kila siku yanapaswa kuwa ni pamoja na kuomba kwa kunena kwa lugha kila siku na Paulo alisema maombi ya jinsi hii humjenga yaya anenaye kwa lugha 1Koritho 14;4 na ndo maana akasema  napenda kila mmoja anene kwa lugha au aombe kwa kunena kwa lugha  mstari 5 na kasha namshukuru Mungu kwama nanena au naomba kwa lugha kuliko wote matsri 18 na tunapoomba kwa lugha tunadumisha nguvu nza roho ndani yetu kwa kuwasiliana na Mungu.

§  Kuwa mtu wa kujituma katika kuabudu.

Njia nyingine ya mkristo kutunza uwepo wa Roho Mtakatifu  ni kujituma katika kuabudu, kuabudu kunabeba umuhimu mkubwa sana wa maisha ya kiroho hususani katika maisha ya mtu aliyejazwa Roho ni kwa njia ya  kuabudu roho tunaketishwa katika ulimwengu wa roho na Yesu kristo Waefeso 2;6 aina hii ya kuabudu kwa roho ndiyo inayotupa nyakati za kuburudishwa Matendo 3;19. Ili kuyalinda maisha yetu na kuyadumisha kiroho ni lazima tutafute nafasi ya kujituma katika kuabudu nafasi hii tunaitumia kama nafasi pekee ya aina kubwa ya kujitoa kiroho na kuimarisha maisha yetu binafsi kiroho nguvu kubwa ya kiroho itakuja kupitia kujituma katika kuabudu binafsi Isaya 40;31, lakini wakati huo huo ni muhimu kukumbuka kujiunga na waamini wengine katika matukio ya kuabudu Biblia inakazia kwamba wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine Waebrania 10; 25.

Kila nafasi inapopatikana ya kuabudu ni muhimu kujituma na kujiingiza na kujimwaga katika kuabudu kwa moyo wetu wote Zaburi 100;4 Daudi aliomba eenafsi yangu Umuhimidi Bwana  na vyote vlivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu  103;1 Paulo anazungumzia moja ya njia kuu za kuendelea kuyatunza maisha yetu ya kiroho kuwa ni pamoja na kujaa Roho Waefeso 5;18 anasisitiza mjazwe Roho na kisha katika mistari inayofuata anaeleza ni namna gani tunaweza kujazwa Roho Mstari wa 19-20 kwa zaburi, kwa  tenzi na kuimba nyimbo za rohoni mtu anapoabudu kutoka moyoni kwa kudhamiria katika kuabudu na kumwaga moyo wake kwa Bwana anajiweka katika hali ya kuendelea kujaa Roho Mtakatifu.Paulo pia anaweka wazi kwamba  kuabudu ni moja ya nia yenye nguvu sana ya kutunza uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha  mtu anapoabudu  roho yake inafanywa upya, imani yake inajengeka na nafsi yake inaburudishwa  na zaidi ya yote anatiwa nguvu kwa makusudi ya vita vya kiroho.

§  Tafakari neno la Mungu.

 Kila siku tunapaswa kulitafakari neno la Mungu kama tunataka kuendelea kutunza uwepo wa Roho mtakatifu katika maisha yetu Yesu alisema Roho  hutia uzima na mwili si kitu Maneno haya niliyowaambia ni Roho na uzima Yohana 6;36 Kile Kristo anachokisema kuhusu maneno yake  kinayahusu maandiko yaani neno la Mungu neno la Mungu ni roho tena ni uzima, tunapoisoma biblia na kuitafakari  Roho wa Mungu anazungumza nasi na kutuhuisha katika maisha mapya  na kama tunataka kudumisha maisha yetu kiroho tunapaswa kuendelea kuyatoa maisha yetu kila siku katika kujisomea na kulitafakari neno la Mungu neno la Mungu ni chakula cha kiroho kwa mtu wetu wa ndani na ni kupitia kulisoma neno la Mungu ndipo roho zetu zinapokea maisha mapya na kutiwa nguvu Zaburi 119:92-93. Ni muimu kufahamu kuwa haitoshi tu kujisomea Biblia na kasha kutokufanya lolote kuhusu, lakini inatupa sa kulitii na kuitumia ile kweli yake katika maisha yetu Yakobo alisema tusiwe wasikiaji tu bali tuwe watendaji wa neno Yakobo 1;22 Yesu alisema kila ayasikiaye maneno yangu asiatende atafananishwa na mtu mpumbaqvu aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga Mathayo 7;26 majaribu yajapo  na kuipiga nyumba ile anguko lake litakuwa baya na haita weza kusimama , maisha yetu ya kiroho yanatunzwa sio tu kwa kusoma neno la Mungu lakini kwa kulitii katika yale linayoagiza.

§  Tembea kwa imani.
Mbinu nyingine ya kutunza maisha yetu ya kiroho ni kutembea kwa imani, kwa maana nyingine kutembea kwa Roho ni kutembea kwa imani na maswala haya yanakwenda sambamba Paulo anaunganisha swala la kutembea kwa imani na kutembea kw Roho alipoandika hivi “sisi kwa njia ya Roho kwa imani tunasubiri katika matumaini ya haki Wagalatia 5;5, ni kwa imani watu humpokea Roho Wagalatia 3;2,14 na kwaimani vilevile anatunzwa Wagalatia 3;3. Ndio kwa imani vile vile tunapata karama za Roho na miujiza hali kadhalika mstari wa 5 kwa msisitizo huo wa Paulo ni wazi kuwa upatikanaji wa Roho Mtakatifu na utendwaji wa miujiza vinapatikana kwa imani na kwa sababu hiyo tunaenenda kwa imani wala si kwa kuona 1Koritho 5:5-7 kwa msingi huo yeye anayetamani kuishi katika Roho anapaswa kuishi kwa imani na sio kwa kuona

§  Ishi maisha ya kujitoa.

Kuna jambo la sita ambalo mtu anapaswa kulifanya ili kuendelea kuwa rohoni na hili ni kwamba lazima ujifunze maisha ya kujitoa hii ikimaaniska kijikabidhi kwa Roho Mtakatifu na mapenzi yake  nah ii inajumuisha kuanzia na mtazamo, tabia , uwazi na kutamani kuishi siku zote akiwa na utayari wa kumtii Roho Mtakatifu na sauti yake, Yesu aliishi maisha ya kujitoa alishuhudia kujihusu hakutenda jambo lolote kwa nafsi yake na kwa jinsi hiiyo baba alimpenda Yohana 5;19-20 Yesu alijitoa moja kwa moja katika kuyafanya mapenzi ya Mungu. Hii ilijumuisha pia swala zima la kujikabidhi kufa msalabani. Yohana 8;28-29.

 Katika mazingira kama haya  mitume pia waliishi maisha ya kujitoa na kumtii Roho Mtakatifu lolote walilolifanya  kama ni kuomba au Luka 24;53, Matendo 1;14, 3;1, 4;31 Kuabudu Matendo 11;15, 13;1-4 kushuhudia 1;8, 4;8, 31 kuhudumu 6;8, 16;6-10 au hata kuendesha mikutano a kanisa 15;28 walifanya yote chini ya uongozi wa  mamlaka ya Roho Mtakatifu, kama tunataka kutembea tukiwa na uwepo wa Roho Mtakatifu wakati wote  ni laizma tujifunze kumtii Roho Mtakatifu na kujifunza kutenda mapenzi ya Mungu na makusudi yake.

§  Uwe makini katika maswala ya kiroho.

 Jambo linguine la muhimu kwa kuishi maisha yaliyojaa Roho ni kuwa makini kiroho “spiritualsensitivity” yaani uwezo wa kuwa na hisia kali dhidim ya maswala ya kiroho au kuwa makini katika kutaka kujua Roho mtakatifu anataka ufanye nini? Na kasha kufanya hali hiyo ya uamkini wa kiroho ni ya muhimu kwa kila mtu anayetaka kweli kumfuata Roho wa Mungu lazima uwe makini kuisikiliza sauti yake  na uwe mwenye kutekeleza kwa haraka kile anachokisema na kuwa mtu wa toba ikibidi. Mara ntyingi tunapowasha redio zetu huwa tunasikiliza kuwa ni radio gani tunaitune ili kwamba tuweze kupata usikivu mzuri wa kile tunachokiaka hali kadhalika katka ulimwenu wa Roho  ni lazima tujifunze kuweka masikio yetu kwa Roho wa Mungu  Biblia inasema leo kama mtaisikia sauti yake msiifanye mioyo yenu kuwa migumu waebrania 3;8,15,4:7, moja ya namna ya kuifanya mioyo yetu kuwa migumu ni kutokuisikiliza vema sauti ya Roho wa Mungu hii ni sawa ni kile alichokisema Paulo msitweze unabii 1Thesalonike 5;19-20 msimzimishe Roho, kwa kuifanya mioyo yetu uwa migumu tunaweza kuuzima moto wa Mungu katika maisha yetu kwa msingi huo kamwe tusikubali fanya jambo lakijinga kisi hiki.kwa kuwa kinyume na Roho.

§  Tembea kwa utii.

Kutembea kwa utii na maisha matakatifu ni swala lingine la kutunza uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu, tumajifunza kuwa tnaweza kumzimisha Roho na kisha maisha yetu ya kiroho yakawa mashakani na kashatukaishi maisha yasiyofaa kitu katika Waefeso 4;29-31  Paulo aliorodhesha baadhi ya dhambi ambazo zinamzimisha Roho Mtakatifu kuwa ni pamoja na
§  Mazungumzo mabaya/Marafki wabaya

  • §  Uchungu,
  • §  Hasira/Ghadhabu,
  • §  Kelele na matukano
  • §  Kila namna ya ubaya
  • §  Kutokusamehe
  • §  Kutaka kulipiza kisasi

Matukio a jinsi hiyo yasio ya kitakatifu na tabia za aina hiyo zinamuhuzunisha Roho Mtakatifu na kumzimisha kutembea kwa wepesi katika maisha yetu na kama tukimuhuzunisha hatimaye anaondoka

Kwa maana nyingine tunapomtiii na kuisikiliza su\auti yake uwepo wake unakuwa mkubwa katika maisha yetu na wakati huo huo tunajifunza kumfuata vema Waebrania 5;14 na Roho wa Mungu ataachilia vipawa vyake na karama zake na roho ya kuomba na tukitii kwa haraka  tunakuwa na nguvu zaidi katika roho zetu.

Hitimisho.
Mambo yameparaganyika ili kuyajenga maisha yetu ya kiroho au kama hayako sawa sawa kama hatujali, kama tutakjali na kuyafanyia kazi yaliyomo humu hakika yake utakuwa na uhusiano mzuri na Roho wa Mungu na ukiendelea kuyatunza maisha yako kuwa katika hali ya buujik na Roho wa Mungu tutapiga hjatua kwa namna yoyote na kamwe hatutakuwa kama tulivyo Bwana ampe neema kla mmoja wetu kutunza uhusiano wake na Mungu na kuzidi kaika jina la Yesu amen!

Rev. Innocent Mkombozi Kamote
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550

Maoni 13 :

  1. MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA MTUMISHI NIMEJIFUNZA MENGI SANA LEO

    JibuFuta
  2. MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA MTUMISHI NIMEJIFUNZA MENGI SANA LEO

    JibuFuta
  3. Nimebarikiwa sana mtumishi wa MUNGU aliye juu

    JibuFuta
  4. Kwa kwel umezungumza na mm MUNGU aendelee kukutumia kwa viwango vya juu zaid

    JibuFuta
  5. Ameni nimebarikiwa sana

    JibuFuta
  6. Barikiwa,kwa kazi njema ya ufalme wa MUNGU.

    JibuFuta
  7. Somo zuri sana Mungu anitie nguvu niliweke rohoni

    JibuFuta
  8. Amen saana mtumishi nimepata vitu vya kunisaidia pia vya kuwasaidia na wengine Barikiwa na Yeah kristo

    JibuFuta
  9. Jina langu ni Mt. Edma mgaya nipo daresalam

    JibuFuta
  10. Mungu akubariki mtumishi nimebarikiwa sana na mafundisho Yako,Mungu anisaidie niyaweke moyoni na niyafanyie kazi

    JibuFuta
  11. BWANA YESU AKUBARIKI BABA MIMI MWANAO MCH JOSEPH GENGE MUHEZA

    JibuFuta