Jumanne, 28 Oktoba 2014

Shule Maalumu Ya Uongozi Wa Kiroho




Shule Maalumu ya Uongozi somo namba moja
      Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
       Somo; Wito wa kuwaongoza Kondoo.
  Leo Tunaanza kujifunza mfululizo wa masomo yahusuyo shule ya uongozi kwa kujifunza somo hili la msingi “Wito wa kuwaongoza kondoo”Tutajifunza Somo hili kwa kuligawa katika vipengele vitano vifuatavyo;-
·         Watu waliookoka huitwa Kondoo
·         Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo
·         Wachungaji wanadamu
·         Jinsi isivyowezekana Mchungaji kuongoza kondoo peke yake
·         Wito wa kuwaongoza kondoo.

 * Watu waliookoka Huitwa Kondoo.

Watu waliookoka huitwa kondoo (zaburi 79;13;100;3;Yohana10;27-28) Kwanini wanaitwa kondoo,Kondoo ni wanyama wasioweza kufanya lolote bila kuongozwa au kupewa msaada wa Kiroho,wao hutembea wakitazama chini na kuiangalia miguu ya kiongozi wao yaani Mchungaji wao Kondoo wanahitaji Malisho na kunyweshwa maji (Mwanzo 29;7,Yohana 10;2-4).Kondoo watatulia mahali Fulani wakingoja Maelekezo ya Kiongozi wao tofauti na Mbuzi au wanyama wengine  na kutafuta Malisho wenyewe nk.Siyo hilo tu kondoo ni rahisi sana kuvamiwa na wanyama wengine wakali na kuuawa bila kujitetea kwa lolote  hawana mbio kama wengine wala viungo vya kujitetea kama pembe kali nk.hivyo maisha ya kondoo  yanahitaji sana Mchungaji au kiongozi Kadiri mchungaji  wao alivyo shujaa ndivyo wanavyo faidika, mchungaji akiwa mtu mbaya nao pia Hudhurika (1Samuel 17;34-35, Yohana 10;11-12)Hivyo maisha ya watu waliookoka yanatutegemea sana sisi viongozi Tukiwa wema kondoo wataishi maisha Mazuri ya kupendeza(Yeremia 50;6;Ezekiel 34;5-6)
   Kilio cha kondoo wakati woote ni  kupata kiongozi wa kuwaongoza wao hulia wakati wote wakisema ni nani atakayeniongoza hata Edom(zaburi108;10)Bila kiongozi  watu waliookoka wanaweza kufanya yaliyo mema machoni pao wenyewe na kumhuzunisha Mungu. (waamuzi 21;25).

 * Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa Kondoo.

      Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo ambao pia ndio kanisa ni kondoo zake kanisa ni mali yake (Waebrania 13;20;1Petro 5;4;Zaburi 23;1-3).Mungu kama mchungaji mkuu wa kondoo,Yeye ndie Kiongozi mkuu wa kondoo wake na maongozi yoote ya Kondoo hutokana na neno lake(Kutoka 13;17;Yohana8;47;Zaburi 119;9)hata hivyo ingawa Mungu ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo katika mpango wake wa Uongozi ameweka wachungaji wanadamu ambao hufanya kazi pamoja na Mungu(1Koritho 3;9).

* Wachungaji wanadamu.

Katika mpango wake Mungu anawaongoza kondoo wake kwa kuwatumia wachungaji wanadamu(zaburi 78;70-72;2Samuel 5;1-2, Zaburi 77;20 Kutoka 15;22 Hesabu 27;15-21 Yohana 21;15-17).Mungu huwatumia wachungaji wanadamu hawa kufanya kazi ya kuwaongoza kondoo kwa maelekezo ya neno lake(Kutoka 32;34)Hata hivyo uongozi wa wachungaji hao  wanadamu wanadamu hufikia mpaka wanapokuwa na kundi kubwa la kondoo nao huitaji wanadamu hawa wengine wengi wa kutenda kazi pamoja nao

*  Jinsi isivyowezekana Mchungaji kuongoza kondoo Peke yake.

Kadiri kanisa linavyoongezeka kunakuwa na kundi kubwa la kondoo wanahohitaji uongozi.kiongozi mmoja  hata angekuwa na uwezo Mkubwa namna gani huelemewa na kushindwa kukidhi mahitaji ya uongozi wa kondoo wengi, matokeo yake kondoo wengi hujisikia upweke kwa kukosa msaada wa uongozi na matokeo yake hutawanyika na kuliacha kanisa hilo na kutafuta mahali Pengine wanapoweza kupata uongozi wa maisha yao lakini wengine kwa kukosa uongozi  hurudi nyuma na kuacha wokovu(Waamuzi 18;1,30-31). Kiongozi Musa alipokuwa amewaacha kondoo bila kiongozi ,pale alipopanda mlimani Sinai kupokea amri kumi  za Mungu huku nyuma kondoo walipoona  hawana kiongozi maana kiongozi wao amekawia kurudi walirudi nyuma na kuacha wokovu  na kufanya machukizo makubwa mbele za Mungu.(Kutoka 32;1-8,15-24).Ufumbuzi wa Tatizo la watu waliookoka kurudi nyuma na kuacha wokovu ni  kuwa na viongozi wengi wanaomsaidia Mchungaji.Kadiri tunavyokusudia kanisa letu kuwa na watu wengi zaidi ndivyo inavyotupasa kuwa na viongozi wengi zaidi wa kumsaidia Mchungaji kuliongoza kanisa,Viongozi hawa watakuwa wanashughulikia matatizo madogomadogo ya kondoo na kuyapatia ufumbuzi na yale makubwa tu ndiyo yatakuwa yanapelekwa kwa Mchungaji, Bila kufuata mpango huu Kanisa litadumaa na haliwezi kuongezeka kiimani na kiidadi, Hata kama watu wengi watakuwa wanakata shauri,hawataendelea katika zizi la kondoo kwa kukosa uongozi.Musa na watu wake waliukubali na kuufuata mpango huu wa Mungu na matokeo yake walifanikiwa (Kutoka 18;13-26)   Bwana amusaidie kila mmoja wetu ili tusiwe kwazo la kukua na kuongezeka kwa kanisa. 


*Wito wa Kuwaongoza kondoo.

     Kilio cha watu wa Mungu humfikia Mungu (Kutoka 2;23;Mwanzo 18;20-21,Yakobo 5;4) Kondoo wa Mungu  wanaohitaji uongozi wanapolia  wakisema nina atakayetupeleka hata mji wenye Boma?ni nani atakaye tuongoza hata edomu (Zaburi 108;10).Kilio hiki humfikia Mungu,Kondoo hawa wana wasi wasi wa kulala Porini na kuwa katika hali ya kushambuliwa na mbwa mwitu au simba wanataka kiongozi atakaye wapeleka kwenye mji wenye Boma (yaani zizi la kondoo).Kondoo hawa pia wanalia wakihitaji mtu  wa kuwaongoza hata wafike Edomu nchi yenye malisho mengi na maji mengi(Hesabu 20;14-19).Ndivyo kondoo wa Mungu wanavyolia pia,wanahitaji viongozi watakaohakikisha wokovu wao unadumu na hawawezwi na shetani samba aungurumaye na tena wanahitaji viongozi  wa kuwahakikishia wanapata malisho na kuangaliwa na kutunzwa ili wafurahie raha ya Wokovu. Kilio hiki cha kondoo kikimfikia Mungu ,Mungu nae anatoa wito kwa watu wake akitaka wajitoe kuwaongoza Kondoo yaani kiongozi wa kanisa,Mungu anauliza Hapana hata mmoja wa Kumshika mkono? Miongoni mwa wana wote aliowalea(Isaya 51;18) Kwa sababu hiyo mungu anauliza ni nani atakaye kwenda   kwa ajili yetu?-Isaya 6;8 Isaya alisema Mimi hapa, sisi nasi hatupaswi kumuachia mchungaji pekee kuifanya kazi hii peke yake na hivyo tunapaswa kushirikiana nae katika kulitunza Kundi.                   

                    Shule maalumu ya uongozi somo la Pili
                              Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
 Somo; Faida ya kuwa kiongozi wa kanisa.

        Wanafunzi wa Yesu waliitikia wito wa Mungu na wakawa tayari kuwaongoza kondoo,na wakawa tayari kuacha vyoote walivyokuwa navyo ili kutekeleza wito huo Hata hivyo waliuliza Tutapata nini Basi (Mathayo 19;27).Kila mmoja wetu angependa kuwa kiongozi wa kaniasa kama angefahamu faida za kuwa kiongozi wa kanisa kwa sababu hii somo letu la pili katika mfululizo wa masomo ya shule ya uongozi ni Faida za kuwa kiongozi wa kanisa,tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-
                    *Gharama za kuwa kiongozi wa kanisa
                    *Kukwepa uongozi wa kanisa
                    *Faida za kuwa kiongozi wa kanisa

*Gharama za kuwa kiongozi wa kanisa

1.Gharama za kuchukua udhia,Mizigo na mateso ya kondoo.

Kuwa kiongozi wa kanisa  ni tofauti kabisa na kuwa kiongozi wa mataifa yaani  kuwa kiongozi wa serikali au shirika la umma au kampuni Fulani,mtu anapokuwa kiongozi katika shirika,au kampuni Fulani au serikalini uongozi huo kwa kawaida huambatana na maslahi Fulani heshima na marupurupu au maslahi makubwa na kupata raha au kustarehe zaidi,Uongozi wa kanisa ni tofauti kabisa,huu ni uongozi wa kitumishi ni kuwatumikia kondoo wa mungu kwa kuchukua udhia na mizigo yao na kukubali mateso ya aina yoyote ile nyakati za biblia mtu aliyekuwa kiongozi alikuwa akikabiliwa na kuuawa wakati wowote (1Timotheo 3;1…) Lengo la uongozi huu ni kurahisisha matatizo ya kondoo wa bwana ili waweze kuingia mbinguni.hivyo hatupaswi kutumaini maslahi yoyote hapa duniani isipokuwa kutazamia malipo yetu mbinguni,Yesu kristo alikuwa ni kiongozi atumikaye ,kiongozi wa kanisa naye anapaswa kutumika bila kutegemea faida za kidunia kama ilivyo kwa viongozi wa kawaida wa duniani (luka 22;24-27).Kuwa kiongozi wa kanisa ni kukubali kubeba mizigo ya watu na kuwafanya wapumzike (Mathayo 11;28) kubeba mizigo ni kubeba huzuni zao,na masumbufu ya aina yoyote ile ili waone raha katika safari yao ya kwenda mbinguni (Kutoka 18;21-22) ni kuwa kama mama au baba anaye beba mizigo na udhia wa watoto wanaohitaji malezi ni kama mtumwa anayebeba mzigo wa bwana wake ili yeye atembee kwa raha,kazi ya maongozi ya kiroho si kazi nyepesi ni nzito ina lawama huwezi kuwapendeza woote na hawawezi kuridhika na lolote utakalowafanyia, watakuteta, watasema kuwa huwajali, watakulalamikia na kukulaumu, watakupiga mawe na wakati mwingine watakukataa na itakupasa kuendelea kuwatumikia bila kujali haya yaliwapata wengi wa viongozi waliokuwa viongozi wakubwa akiwemo Musa (Hesabu 11;11-15;kumbukumbu 1;9-18).

     Kiongozi katika kanisa hapaswi kuwaza juu ya malipo ya kazi anayoifanya  ni viongozi wachache sana wa kanisa ndiyo watapaswa kutunzwa na kanisa kwa mapato ya kanisa hawa ni wale tu wanaokuwa wameacha shughuli nyingine ili wapate muda wa kulihudumia neno kama ilivyokuwa pia wakati wa kanisa la kwanza (Matendo 6;2-4). Ingawaje  hata Paulo na barnaba kwa kipindi Fulani ilibidi wafanye kazi  ili kupata mahitaji yao na ya wale waliokuwa wakiwaongoza (Matendo 20;33-35;!Thesalonike 2;9) mtume pauilo alifanya hivi ili kupata mahitaji ya wale aliokuwa akiwaongoza hivyo viongozi woote ambao wanamsaidia mchungaji inawalazimu kufanya kazi kama zile za kaisari ili kupata mahitaji yao na kukulisaidia kanisa aidha ni muhimu kukumbuka kuwa Paulo alifanya vile ili kutoa kielelezo kwa Wathesalonike ambao walikuwa hawataki kufanya kazi (2thersalonike 3;6-9).

2 Gharama za kujikana nafsi zaidi kwa ajili ya kondoo.

    Viwango vya mungu kwa kiongozi wa kanisa ni vya juu zaidi kuliko vile vya kondoo wa kawaida,yako mambo ambayo yatakuwa halali kwa kondoo wa kawaida kuyafanya lakini yasiwe halali kwa kiongozi wa kanisa kuyafanya, Kwa mfano nyakati za agano la kale ilikuwa ni halali kwa watu wa kawaida kunyoa nywele zao,Kurarua mavazi yao na kuomboleza walipopatwa na misiba (2samuel 1;11-12,ayubu 1;18-20). Hata hivyo kuhani au kiongozi  wa kanisa wa nyakati hizo yeye hakuruhusiwa  kufanya hivyo au kufanya mambo mengine kadhaa wa kadhaa ambayo wengine walikuwa wameruhusiwa kuyafanya (Walawi 21;10-15) Hata wanawe Haruni; Nadabu na Abihu walipokufa Haruni kiongozi wa kiroho hakuruhusiwa, kuomboleza,kuwazikana kunyoa nywele zake (Walawi 10;1-7) Kwa msingi huu kiongozi wa kiroho kwakweli anapaswa kujikana nafsi yake  kwa ajili ya wengine (Yohana 10;11;Marko 8;35)Wakati mwingine itakugharimu kuwa wa mwisho kuondoka kanisani wakati viongozi wengine wako majumbani (Mathayo 14;22-23)Wakati mwingine inaweza kukugharimu kutokwenda likizo endapo kufanya hivyo kunaonekana kutaathiri utendaji wa kazi ya Mungu.

 Kukwepa uongozi wa kanisa

   Baada ya kuwa tumefahamu  mzigo huu mkubwa wa kuwa kiongozi wa kanisa watu wengine waliookoka ,hutafuta visingizio mbalimbali vya kukwepa uongozi wa kanisa na kuona bora wawe kondoo wa kawaida katika kanisa (Kutoka 4;10;13;Yeremia 1;4-6) Hawa watakuwa ni watu wasiofahamu faida za milele zinazoambatana na kuwa kiongozi wa kanisa,hii ni sawa na mtoto anayetoroka shuleni kwa madai eti kuwa masomo ni magumu,mwanafunzi wa jinsi hii atakuwa hajui faida zinazoambatana na kusoma,mkulima  anayekubali taabu ya kilimo huwa wa kwanza kufurahia apatapo chakula tele,wale wanaokwepa mzigo wa kilimo  hupata shida baadaye .(2Timotheo2;6;Mithali 28;19).

Faida za kuwa kiongozi wa kanisa

   Isaya alipomwambia na Mungu  “MimI hapa nitume mimi” nakuanza  kufanya kazi ya Mungu kama kiongozi wa Kiroho,hatimaye alifikiri kuwa anajitaabisha bure na kutumia nguvu zake bure bila ya faida,lakini baadae akakumbuka faida au thawabu  zinazoambatana  na kuwa kiongozi wa kiroho hivyo aliendelea kumtumikia mungu  mpaka mwisho alipouawa kwa kukatwa misumeno (Isaya 49;4,Ebrania 11;37).sisi nasi ni muhimu kufahamu kuwa kuna faida za kuwa kiongozi wa kiroho katika kanisa na hili litatutia moyo kumtumikia Mungu kwa gharama yoyote Faida hizi ziko katika makundi makuu mawili

1. Faida za Duniani.

 Ziko ahadi nyingi za Mungu alizozitoa kwa kiongozi wa kiroho yeyote anayemtumikia Mungu ni wajibu wetu kumkumbusha Mungu wakati woote wa utumishi wetu (Isaya 43;26);-
  • Kuheshimiwa na Mungu(Yohana,12;26) Mungu anapokuheshimu hukupa kipaumbele
  • Kuna kula na kushiba (Kumbukumbu 11;13-15;Isaya 65;13).
  • Atabariki chakula chako na maji yako, atakuponya, hapatakuwa na aliyetasa wala mwenye kuharibu mimba na hesabu ya siku zako ataitimiza (Kutoka 23; 25-26).
  • Mungu atakuponya katika hatari yoyote kubwa itakayokuja au inayokukabili (Daniel 6;16,20-22)
  • Mungu atakuwa pamoja nawe katika kazi yote ya utumishi mpaka kazi yake itakapomalizika (1Nyakati 28;20).
2. Faida za Milele
  • Kung’aa kama nyota milele na milele (Daniel 12;3)
  • Atakuwa na daraja njema (1Timotheo 3;1,12-13 na Ufunuo 21;14)na katika utawala wa Kristo miaka elfu duniani watapewa utawala (Luka 19;15-19).
  • Kuna taji ya utukufu isiyokauka (1Petro 5;1-4)
  • Kuna taji isiyoharibika(1 Koritho 9;23-25)
  • Atakuwa miongoni mwa wale waliobarikiwa (Mathayo 25;34-40)
  • Atalipwa mshahara mkubwa mbinguni na kujaa furaha tele (Yohana 4;35-36).


             Shule maalumu ya uongozi somo la Tatu
                          Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
            Somo; Kuigwa kwa kiongozi wa Kanisa
     Hakuna furaha kubwa kwa baba yetu wa Mbinguni anayoipata  kuliko anayoipata anapowaona watoto wake wanaitikia wito wa kuwaongoza kondoo wake.kuitikia wito wa kuwaongoza kondoo ni moja ya hatua zinazodhihirisha kukua kwa mtu aliyeokoka.katika hali ya asili Mzazi asingependa kumuona mtoto wake anabaki mchanga tu siku zote na hakui, Furaha ya mzazi hutimia anapoona moja ya watoto wake akiwaongoza wadogo zake na kusaidia kufanya majukumu ya mzazi katika hali kama hiyo Mungu hufurahi anapoona mtu aliyeokoka anakua na kuifikia hatua ya kuwaongoza wengine Lakini ni muhimu kuufahamu mapema kuwa wale ambao tumekubali kuwaongoza huwa wanaiga sana Tabia zetu hivyo ni muhimu kujifunza somo hili “kuigwa kwa kiongozi wa kanisa” tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu;-

*      Jinsi kondoo wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa.
*      Wajibu wa kiongozi wa kanisa kuwa kielelezo
*      Kiongozi wa kanisa ni mwakilishi wa Mchungaji

Jinsi kondoo wanavyomuiga Kiongozi wa Kanisa.

     Watoto wa kike huwaangalia kwa makini mama zao wanapopika chakula katika hali ambayo wakati mwingine ni vigumu hata mama kujua kinachoendelea na hatimaye utaona nao wanatafuta vyombo vya kitoto vinavyofanana na kuanza kuwaiga jinsi ya kupika kumbe watoto ndivyo walivyo ni kwa msingi huu watoto wakiroho huwaiga wale wanaowaongoza au waliowatangulia katika wokovu kwa jambo lolote lile liwe jema au baya. Kuna usemi mmoja unaosema “ukitaka kufahamu tabia ya kiongozi waangalie wale anaowaongoza” Kiongozi kamwe hapaswi kuwaambia watu fuateni yale ninayosema na si yale ninayotenda kiongozi huyo hajui analolisema, Kuigwa kwa kiongozi katika Matendo yao ni kanuni iliyoandikwa mioyoni mwa watu  na haiwezi kuepukika  Biblia ina mifano mingi ya jinsi watu wanaooongozwa wanavyowaiga wale waliowaongoza angalia mifano hiyo katika 1Falme 22;51-53, 2Nyakati 22;1-4, Yeremia 9;14, Amosi 2;4, 2 Nyakati 17;3-4,26;3-4, 2Tomotheo 1;5.Biblia inaonyesha kuwa Simeon Petro aliandaliwa mapema kuwa kiongozi wa kanisa Luka 22;31-32,Matendo 1;15,2;14. Simeon Petro wakati mmoja kama kiongozi wa kanisa aliamua kuacha majukumu yake ya kiutumishi na kuamua kwenda kuvua samaki wanafunzi wengine walipomuona waliamua kujiunga na kiongozi wao kuvua samaki Yohana 21;7.Yesu alipowakuta wao Baharini Petro alifahamu kuwa ameonyesha mfano mbaya hususani kwa wanafunzi wale wengine akajuta na kujitupa baharini Yohana 21;7 sisi na si kama Viongozi tunawajibu mkubwa wa kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kufahamu kuwa kuishi maisha ambayo si kielelezo ni sawa na kuisaidia kazi ya shetani, Viongozi wataigwa na wale wanaokuja nyuma yao kwa kila kitu kama tunawahi ibada, ni waombaji, tuna bidii,tunatii neno la Mungu na kulitetemekea tunatii wachungaji n.k watu wanaoongozwa humtazama kiongozi wao kwa kila jambo hata kama ni baya kama uvivu, ulegevu, uzembe n.k kwa msingi huo ni muhimu kuwa makini tunapokuwa tumeingia katika ngazio ya maongozi.

      Petro alimwangaluia sana kiongozi wake Yesu jinsi alivyokuwa anafanya maombi ya kufufuka wafu naye akaiga vilevile kabla ya kufanya maombi ya kufufuka wafu  kumbuka kuwa Yesu aliwatoa watu nje  na Petro akaiga vilevile Linganisha Marko 5;39-42 na Matendo 9;39-41 sisi nasi tukiwa kama Viongozi wa kanisa tunaangaliwa katika kila jambo. Waebrania 13;7 Nyakati za kanisa la kwanza waliwaiga Viongozi wao katika kila jambo walichofanya Viongozi ni kuwasihi wauchunguze mwisho wa mwenendo wa Viongozi wao. 

Wajibu wa kiongozi wa kanisa kuwa kielelezo

     Mpaka hapo tumeona jinsi kiongozi wa kanisa anavyoweza kujenga ufalme wa Mungu au kuubomoa,kiongozi wa kanisa akafanya vema atawafanya wanaomuongoza nao kufanya vema ni kwa sababu hii ndio maana Mungu huwaheshimu sana Viongozi wa kanisa na ndio maana anataka Viongozi wa kanisa wawe vielelezo Neno la Mungu linatoa wito na wajibu kwa Viongozi wa kanisa kuwa vielelezo 1Timotheo4;12,16 Tito 2;7;1Petro 5;2-4.Viongozi Nyakati za kanisa la kwanza walijitahidi sana kuwa vielelezo na ndio maana ufalme wa Mungu ulijengeka kwa kasi sana na kwa namna ya kipekee katika wakati wao 1Koritho 11;1, 4;16,Wafilipi 3;17,4;9,1Thesalonike 2;10,2Thesalonike 3;7,9, Mungu hana upendeleo Neema ya Mungu iko kwa kila kiongozi  kutusaidia kuwa kielelezo kwa ajili ya kujenga ufalme wake Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa kielelezo katika jina la Yesu Kristo.

Kiongozi wa kanisa ni mwakilishi wa Mchungaji.

     Ni muhimu kuufahamu kuwa mtu anapoteuliwa kuwa kiongozi katika sehemu yoyote iwe kanisa au cell au makanisa ya nyumbani au vijana au kina mama au maombi au kikundi chochote yeye ni  ana kuwa ni mwakilishi wa Mchungaji katika eneo husika ina maana ya kuwa kiongozi huyo huongoza eneo lake hilo kwa niaba ya Mchungaji hivyo unafanya kile ambacho Mchungaji angekifanya  katika sehemu hiyo Luka 10;1, hivyo anayemsikiliza kiongozi anamsikiliza Mchungaji anayekataa hamkatai Mchungaji tu bali na yeye aliyewatuma Luka 10;16,Kwa msingi huo ingawa Viongozi hawa hawaitwi wachungaji Lakini ni wachungaji wa maeneo yao waliyopewa kuyasimamia hivyo kila unapofanya jambo jiulize kuwa hiki ninachikifanya je Mchungaji angekifanya? Kwa msingi huo wewe kama kiongozi ni muhimu kukumbuka kuwa uko karibu na watu kusaidia huduma ya kichungaji na hivyo maisha yako kama kielelezo yatasaidia kujenga au kubomoa ufalme wa Mungu na kanisa lake kwa nia moja kabisa tukatae kutumiwa na ibilisi kuliharibu kanisa la Mungu na chini ya neema ya Mungu tuseme kama Paulo mtume “MNIFUATE MIMI, KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO”

       Shule maalumu ya uongozi somo la Nne
                  Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
   Somo;     Sifa za kiongozi wa kanisa
Somo letu la nne katika Mfululizo wa Masomo ya shule hii maalumu ya Viongozi ni somo sifa za kiongozi wa kanisa tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vikuu viwili vifuatavyo;-

*      Sifa za kiongozi wa kanisa
*      Kiwango cha kuanzia tunapoitwa kuwa Viongozi wa kanisa.

Sifa za kiongozi wa kanisa
     Neno la Mungu linaeleza waziwazi sifa za kuwa kiongozi wa kanisa na tutakapokuwa tunaichambua sifa moja baada ya nyingine itakuwa ni rahisi kwa kila mmoja wetu kujipima na kuangalia pale palipopungua kisha kumuomba Mungu neema ya kuzifikia sifa hizi za maongozi katika kanisa kama apendavyo Mungu.
  1. Awe Mwanafunzi wa Yesu;-
Neno la Mungu linaelekeza kuwa Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu ambaye ameokoka hivi karibuni 1Timotheo 3; 6 Baada ya mtu kuokolewa anapaswa Kwanza kujifunza Neno la Mungu na kulitendea kazi hata kufikia ngazi ya kuwa Mwanafunzi wa Yesu. Mwanafunzi wa Yesu ni mtu aliyeokoka ambaye analitendea kazi Neno la Mungu bila ubishi au kulijadili na kukaa katika neno Yohana 8;31 wao wanakuwa watii si kwa neno tu Lakini wanaelewa pia faida za utii kwa Viongozi wake utii uhuu unafananishwa na ule wa kijeshi Wafilipi 2;5-8 askari hujifunza kutii amri za Viongozi wao hata kama amri hiyo itamsababishia kifo Mwanafunzi wa Yesu hali kadhalika ni askari wa Yesu 2Timotheo 2;3,Filemoni 1;2 , hivyo Mwanafunzi wa Yesu ni mtu aliyeokoka ambaye analitii neno la Mungu na Viongozi wake wa kiroho kama askari kwani watumishi wa Mungu ni wajumbe wa Bwana wa majeshi Malaki 2;7,Filemoni1;21 Yesu Kristo aliwatuma wale thenashara kwenda kwa niaba yake  baada ya kufikia kiwango cha utii kama wa askari wa kijeshi Mathayo 11;1 Makanisa mengi hayafanikiwi kwa sababu watu hawajafunzwa kuwa kama askari hivyo kunakila aina za uasi na majadiliano kuhusu maagizo yanayotoka kwa Viongozi wao, Mtu aliyeokoka hivi karibuni ataona ni ngumu kuyatii maagizo ya kiongozi wake kama askari hivyo hafai kuwa kiongozi akiambiwakama Anania “Simama Enenda” atafanya hivyo mara moja Matendo 16;1-3.

  1. Awe mume wa mke mmoja au Mke wa mume mmoja;-
1Timotheo 3; 2, 12 Mwanamume yeyote ambaye ana mke zaidi ya mmoja au mwanamke aliyeolewa na mume mwingine wakati mumewa kwanza bado yuko hai watu wa jinsi hiyo huwa hawapewi uongozi kibiblia Kristo ni mmoja na ni kichwa cha kanisa mwili ni mmoja vivyo hivyo mume mmoja kichwa na mke mmoja mwili.

  1. Awe anayaamini mafundisho yote.
2Koritho 4;15 Kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa ni mtu anayeshika na kuyaamini mafundisho ya imani yetu kama vilevile anavyofundishwa Tito 1;9, 2Wathesalonike 2;15 ni muhimu kwa kiongozi wa kanisa kuwa anayeamini mafundisho yoote ya kanisa lake na sio sehemu tu fulanifulani Mafundisho hayo ni pamoja na Wokovu, ujazo wa Roho Mtakatifu, Ubatizo wa maji mengi, mafundisho ya toba na Malipizi, unyenyekevu na utii, kujitenga na dunia, uponyaji na miujiza kiongozi anapokuwa anapinga baadhi ya mafundisho kama hayo ya muhimu basi huyu  ni kiongozi wa watu waliomkamata Yesu kama Yuda Matendo 1;15-17,.

  1. Awe anaisimamia Nyumba yake vema.
Kama kiongozi wa kanisa ni Mwanamume basi kama kichwa anapaswa kuwa na msimamo mkali na thabiti utakaomfanya mkewe na watoto kufuata maagizo yake kama mwili unavyotekeleza maagizo yote ya kichwa kutoka katika ubongo aidha lazima awatiishe watoto wake katika ustahivu woote yaani watoto wake wawe katika hali ya kumtii na kumuheshimu mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe moja je atawezaje kulisimamia kanisa lenye nyumba nyingi? 1Timotheo 3;4-5,12.Kama watoto wa kiongozi ni wakaidi jeuri na wasiotaka kutii ni lazima ithibitike kuwa amechukua hatua kali na thabiti katika kuwazuia kufanya wanayoyafanya na sio kuzungumzia nao kwa kuwadekeza 1Samuel 2;12, 22-25, 3;12-14. Mtu ambaye atawaona watoto wake hawafuati njia za Bwana kisha akawachekea tu bila kuchukua hatua kadhaa huyo hafai kuwa kiongozi wa kanisa

  1. Awe analifahamu neno la Mungu na kujua kulifundisha kwa uhakika akionyesha tabia na Matendo yanayolingana na neno analolifuindisha.
Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa na bidii katika kulisoma neno la Mungu kulisikia Kupitia ibada na njia za kaseti, tv, Vitabu n.k na kujifunza ili alifahamu kwa uthabiti na kumudu kulifundisha 1Timotheo 1;7;3, 2, 4;13 Tabia na Matendo yanayoendana na neno analolifuindisha hayana budi kuwa yenye kuonekana katika maisha yake Kutoka 18;21, 1Timotheo 3;1-12, Tito 1;5-8

  1. Awe na moyo wa msamaria.
Kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mtu aliye tayari kuchukua mizigo ya waaminio na awe tayari kufanya hivyo kwa wakati unao faa na usio faa Luka 10; 30-35, 2Timotheo 4;2.

  1. Awe Mtu asiye na upendeleo.
Mtu awaye yote anayekuwa kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu wa upendeleo kwa namna yoyote ile wako Viongozi ambao hufanya upendeleo kwa watu wa kabila lake tu au kwa wasomi na matajiri kwa ajili ya mafungu au kuipokea uso wa mwanadamu mtu wa namna hii hafai kuwa kiongozi wa kanisa Kumbukumbu 1;17, Yakobo 2;1-9.

  1. Awe mtu wa kweli na mwenye kuchukia mapato ya udhalimu
Shetani ni baba wa uongo, kiongozi wa kanisa anamwakilisha Yesu ambaye ni kweli hivyo anapaswa kuwa mkweli wakati woote Mtu mwongo hafai kuwa kiongozi wa kanisa, aidha kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mtu anayechukia mapato ya udhalimu Kutoka 18;21. Aidha anapaswa kuwa mbali na mizaha na tabia zozote za kuchukiza Mithali 26;18-19; 19;29.

  1. Awe mtu ambaye uasherati au uzinzi haitajwi kwake
Uasherati au zinaa ni mwiko kutajwa kwa mtu yeyote anayedai kuwa ameokoka na ni zaidi sana kwa kiongozi wa kanisa Waefeso 5;3 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa Mithali 6;32 Kumbukumbu 1;13.

  1. Awe mtu aliyejaa imani, anayeishi maisha matakatifu na aliyejaa Roho Mtakatifu na Hekima Matendo 6;3-6
 Aidha kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mtu mwenye Hekima anayeishi maisha matakatifu na aliyevikwa uwezo utokao juu yaani Roho Mtakatifu Luka 24;49 Anapaswa kuwa mstari wa mbele katika imani akiamini kwamba kwa Mungu yote yawezekana.

Kiwango cha kuanzia tunapoitwa kuwa Viongozi wa kanisa.

     Baada ya kujifunza sifa hizi ni rahisi kwa kila mtu mmoja mmoja kujihisi kuwa huenda Hastahili na ana upungufu katika eneo Fulani. Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hatuiti katika uongozi tukiwa wakamilifu mia kwa mia Mungu hakuwaita kina Petro wakiwa kama watu maalumu wala Yakobo na Yohana hawakuwa wakamilifu kulikuwa na mapungufu kadhaa wa kadhaa katika maisha yao Hivyo si ajabu kwetu kujikuta tukiwa na mapungufu Fulani na ndio maana Mungu hutufundisha hatua kwa hatua hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo Waefeso 4;11-13 jambo la msingi kwetu ni kumuomba Mungu atujazilize katika kile ambacho kimepungua katika maisha yetu na kufanya sehemu yetu ya kuipokea kwa imani na kulifanyia kazi neno Yakobo 1;5-7.          

              Shule maalumu ya uongozi somo la Tano
             Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
                    Somo ; Wito wa kumtumikia Mungu
      Somo tunalojifunza sasa katika Mfululizo wa Masomo maalumu ya shule ya uongozi ni Wito wa kumtumikia Mungu hili ni moja ya Masomo muhimu sana na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitano vifuatavyo;-

*      Mafundisho ya msingi kuhusu wito wa kumtumikia Mungu
*      Aina tatu za wito wa kumtumikia Mungu
*      Njia Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
*      Aina ya watu wanaoitwa na Mungu
*      Neema ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu

Mafundisho ya msingi kuhusui wito wa kumtumikia Mungu

Wako watu wengine katika kanisa la Mungu ambao kwa kukosa Ufahamu husema hawawezi kukubali kumtumikia Mungu au kukubali nafasi yoyote ya uongozi katika kanisa kwa madai kuwa eti mpaka wasikie Sauti halisi ya Mungu ikiwaita katika utumishi huo, huku ni kukosa Hekima na sio sahihi Wito wa kumtumikia Mungu sio lazima uambatane na kuisikia sauti halisi ya Mungu Elisha hakusikia sauti ya Mungu alipoitwa ni Eliya alipita karibu naye na kumtupia vazi 1Falme 19;19-21 pamoja na hayo Mungu alikuwa pamoja naye na alimtumia kwa upako maradufu kuliko Eliya, Yoshua hakusikia pia sauti ya Mungu  bali alitwaliwa na Musa na kuwekewa mikono Hesabu 27;22-23 pamoja na hayo Yoshua alikuwa mtumishi wa Mungu wa kipekee, upande mwingine pia wako watu ambao hujipachika majina makubwa kama Mwinjilisti, Mwalimu, Mchungaji n.k bila ya kuwa na wito maalumu wa kuwafanya wawe na nafasi hizo watu wa jinsi hii hufanya makosa na wanapojaribu kufanya kazi hizo kamwe hawawezi kupata matokeo mazuri mfano wa kibiblia ni kwa AHIMAASI mwana wa Sadoki na mkushi mmoja  Ahimaasi alikuwa na moto wa kijipachika cheo cha kuwa mchukuwa habari na kufikiria kuwa ni swala la kuwa na ubingwa wa kupiga mbio na ni kweli alikuwa wa kwanza kufika kwa mfalme  Lakini alipofika na kuulizwa habari alibabaika tu na hakuwa na ujumbe maalumu kama ilivyokuwa kwa mkushi aliyekuwa na wito maalumu wa mchukua habari 2Samuel 18;19-33. Awaye yote anayetaka kumtumikia Mungu ni muhimu kuwa na wito.

Aina tatu za wito wa kumtumikia Mungu

Ziko aina kuu tatu za wito kuelekea katika kumtumikia Mungu
1. Wito wa jumla katika wokovu- huu ni wito ambao mtu huitwa kutoka dhambini na kusamehewa dhambi ili apate kumuabudu Mungu  na ili kuurithi uzima wa milele hata hivyo wito huu huambatana na wito wa jumla wa kumtumikia Mungu yaani Mungu anapokuwa amekuokoa anataka pia umtumikie

2. Wito wa jumla wa kumtumikia Mungu- Mtu hawezi kuingia katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hajaokoka, Lakini punde mtu huyo anapokuwa ameokolewa anakuwa ameitwa katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu na wito wa kuyaishi maisha matakatifu Waefeso 4; 1,1Petro 1; 15-16 kila mtu aliyeokoka amepewa wito wa kuenenda ulimwenguni mwote na kuihubiri injili kwa kila kiumbe Mathayo 28;19-20 Marko 16;15 wito huu ni kwa jinsia zote, Nyakati za kanisa la kwanza watu woote waliitikia wito huu pale walipotawa nyika na kwenda huko na huko wakiwaacha mitume pale Yerusalem Matendo 8;1,4. Hivyo kila mtu aliyeokoka bila hata ya kungojea sauti ameitwa katika wito huu wa kumtumuikia Mungu

3.Wito maalumu wa kumtumikia Mungu- wito huu hutolewa na Mungu kwa Mtu maalumu  ili kufanya utumishi Fulani wa kimaongozi katika kanisa  wakati mwingine wito huu utaambatana na karama maalumu zitakazomwezesha mtu huyo kulitimiza Jukumu alilopewa kwa ufanisi .Yusufu alipewa wito maalumu wa kuhifadhi roho za watu na maisha yao wasife kwa njaa na alipewa karama maalumu za kutafasiri ndoto Mwanzo 45;5-8 wito huu ulioambatana na karama hizo maalumu  ulimuwezesha kuwa waziri mkuu katika inchi ya Misri, Esta 4;15-16 alikuwa na wito maalumu wa kuliokoa taifa la kiyahudi lisiangamizwe na aliwezeshwa kuwa tayari kuangamia  au kukutana na magumu ya aina yoyote ile hivyo ili mtu awe Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu lazima wito wake uambatane na neema maalumu itakayomwezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi wa kipekee, aidha wito maalumu pia huambatana na mtu kuwa mwaminifu katika kutekeleza wito wa jumla wa utumishi kabla ya kuingia katika wito maalumu wa kumtumikia Mungu Matendo 13;1-3 Barnaba na Sauli walikuwa waaminifu sana katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hawajaitwa katika wito maalumu wa kumtumikia Mungu baada ya kupewa wito maalumu huduma zao zilibadilika kabisa.  

Njia Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa

  1. Kujipachika mwenyewe uongozi
Hii ni sawa na ule mfano wa Ahimaasi mwana wa Sadoki 2Samuel 18;19-33 na tuliona kuwa matokeo yake haya kuwa mazuri, Uzia alijipachika kufanya ukuhani na matokeo yake alipatwa na ukoma na kufa 2Nyakati 26;16-23 kora na wenzake hawakuwa tayari kuwa chini yza Musa yeye na wenzake wakataka na ukuhani matokeo yake walipoteza hata nafasi ile waliyokuwa nayo wakafa kifomcha aibu Hesabu 16;1-35 ni hatari kubwa mtu kijipachika uongozi katika kanisa.

  1. Kuchaguliwa na wanadamu bila kufuata uongozi wa Roho mtakatifu.
Kiongozi wa kiroho kamwe hachaguliwi kwa kupigiwa kura au baada ya kufanya kampeni nyingi kama za kisiasa,tunaweza tukampigia kura mwanadamu Fulani na ikawa Bwana hakumchagua huyo Baada ya Mathiya kupigiwa kura na kushindwa kwa kura katika Matendo 1;23-26 hatuoni  jina lake likitajwa tena katika Biblia najua kuwa Vitabu vya kihistoria vinaeleza kazi alizozifanya  Lakini hatuoni tendo la upigaji kura likirudiwa tena katika agano jipya Mungu ndiye anayechagua Viongozi katika 1samuel 16;6-7 Samuel alimchagua Eliabu Lakini Bwana hakuwa amemchagua huyo, Ni marufuku kuchagua kiongozi wa kanisa kwa kumpigia kura swala hili limeleta migogoro mingi katika makanisa Kiongozi wa juu wa kiroho ndiye anayechagua  Viongozi walio chini yake  kwa kuongozwa na Roho wa Mungu Luka 6;12-16 Matendo 15;40-41;14;23;Toto 1;4-5 au Mungu kusema Kupitia Roho Mtakatifu Matendo 13;1-3.

  1. Kuchaguliwa na Mungu Mwenyewe.
Mungu anaweza kuchagua mwenyewe Viongozi mbalimbali wa kanisa Yeremia 1;15 Hata hivyo Mungu anapochagua mwenyewe huduma ya mtu huyo itakuwa dhahiri katika kanisa na kutakuwa na udhihirisho wa wazi wazi  unaothibitisha kuwa huduma ya mtu huyo imetoka kwa Mungu.

  1. Kuchaguliwa na Mungu Kupitia watumishi wake.
Yoshua alichaguliwa na Mungu Kupitia mtumishi wake Musa Hesabu 27;16-18.elisha alichaguliwa na Mungu Kupitia Eliya 1Falme 19;15-16 Paulo mtume alimchagua Silla  kwa uongozi wa Mungu Matendo 15;40 halikadhalika Viongozi wengi wa Nyakati za kanisa la kwanza walichaguliwa na watumishi wa Mungu kwa uongozi wa Mungu Matendo 14;23,Tito 1;4-5 kwa msingi huu basi Mchungaji akimchagua mtu kuwa kiongozi wa kanisa la nyumbani sehemu au zone au kuongoza idara nyingine yoyote hufanya hivyo kwa uongozi wa Mungu na hivyo mtu huyo aliyechaguliwa hakujitwalia mwenyewe heshima hiyo Waebrania 5;4 na anakuwa ameitwa na Mungu. 

Aina ya watu wanaoitwa na Mungu

     Mungu katika Hekima yake huwaita watu wengi wasio na Hekima ya mwilini au wasio na nguvu wasio na cheo au wanaoonekana kuwa wapumbavu na dhaifu wanyonge na wanaodharauliwa ili adhama na sifa kuu ya uwezo wa iwe ya Mungu mwenyewe na sio ya mtu yule dhaifu 1Koritho 1;26-29, 2Koritho 4;7 hivyo hatupaswi kujiona kuwa hatufai Kuchaguliwa . Musa alikuwa na kigugumizi, Yeremia alikuwa mtoto n.k sisi nasi tunaweza kujiona kuwa tuna mapungufu Fulani wakati Mungu anapotuita kwenye utumishi hayo yasikukatishe tamaa kwani yeye ndiye atakaye tuwezesha si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho wangu asema Bwana wa majeshi Zekaria 4;6 Warumi 9;16.

Neema ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu.

     Tunapochaguliwa kuwa Viongozi wa kanisa na kuwekewa mikono na yule aliyetuchagua kuwa Viongozi kwa uongozi wa Mungu Sehemu ya heshima yake na uwezo wake aliopewa hutushukia Hesabu 27;18-23. Yoshua baada ya kuwekewa mikono na Musa  alibadilishwa kabisa na watu wakamuheshimu Kumbukumbu 34;9.Kuwekewa mikono namna hiyo huchochea karama zilizofichika ndani yetu na kizifanya zijitokeze 2timotheo 1;6 Kwa msingi huo Mchungaji anapotuwekea mikono ili tuwe Viongozi wa Makanisa na idara na sehemu nyinginezo sehemu ya uwezo aliopewa huja kwetu na kutusaidia kikamilifu

   Shule maalumu ya uongozi somo la sita
 Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
                  Somo; Jinsi ya kuliongoza kanisa
Tunaendelea kujifunza Mfululizo huu wa Masomo maalumu yahusuyo uongozi na sasa tunajifunza somo hili Jinsi ya kuliongoza kanisa la Mungu tutajifunza somo hili pia kwa kuzingatia vipengele viwili

*      Hatari ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa
*      Jinsi ya kuliongoza kanisa.

Hatari ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa

     Ni hatari kubwa kama tutakuwa na Viongozi vipofu katika kanisa. kipofu alimuongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni wote wawili Luka 6;39 kwa kukosa akili au Ufahamu wa jinsi ya kuliongoza kanisa sisi nasi tunaweza Kuhesabiwa miongoni mwa vipofu Mathayo 15;14-16 ilitupate Ufahamu wa kutosha kuhusu kuliongoza kanisa tutachukua muda mwingi katika somo hili kujifunza mambo kadhaa wakadhaa yahusuyo jinsi ya kuliongoza kanisa.
Jinsi ya kuliongoza Kanisa.
      Yako mambo kadhaa ambayo ni muhimu kuyaangalia na kuyazingatia kwa makini ili tupate mafanikio yanayokusudiwa katika kuliongoza kanisa

  1. Kujiamini.
Mungu anapokuwa ametuchagua kuliongoza kanisa tunaweza kujikuta kuwa tuna umri mdogo kuliko wale tunaowaongoza, hii sio ajabu Musa alikuwa mdogo kuliko kaka yake Haruni Lakini ni Mungu aliyemchagua Musa aliye mdogo kumuongoza kaka yake Kutoka 7;7 sio hilo tu Mungu aliwachagua Viongozi waliokuwa na umri mdogo mno  na Biblia inaonyesha kuwa wengi kati ya hao waliongoza vizuri na kwa mafanikio makubwa  Mfano ni Yoashi aliyeongoza akiwa na miaka saba 2Nyakati 24;1-2 Yosia alinza kuwa kiongozi akiwa na umri wa miaka nane 2 Nyakati 34;1-2 Uzia alikuwa na umri wa miaka 16 2Nyakati 26;3-4 Yothamu na Hezekia woote walikuwa na umri wa miaka 25, 2Nyakati 27;1-2,29;1-2. Timotheo naye alikuwa kijana mdogo tu kama Yeremia alipoanza kuongoza 1Timotheo 4;11-12,Yeremia 1;4-7 tunaweza kuwa sio tu na umri mdogo Lakini pia Elimu ndogo kuliko wale tunaowaongoza hii pia sio ajabu Viongozi wakubwa wa kanisa, Petro na Yohana  walikuwa ni watu ambao walikuwa hawana Elimu wala maarifa  Matendo 4;13 lakini waliifanya kazi ya Mungu kwa ujasiri na kuliongoza kanisa. Hatupaswi kamwe kujidharau wala kubabaika  kutokana na vigezo hivyo vya kibinadamu tunapaswa Kujiamini na Mungu atawatiisha chini yako wazee na wasomi nao watakusikiliza  kumbuka kuwa si sisi tuliojichagua wenyewe na kuwa ni Mungu ndiye aliyetuchagua hivyo yu aweza kutupa uwezo wa kuongoza na kulisimamia kanisa lake Yohana 15;16,Zekaria 4;6;Wafilipi 4;13 kwa sababu hiyo yeye aliye dhaifu na aseme mimi ni Hodari maana uhodari wetu uko katika Bwana  aliye tuwezesha maana amesema atakuwa pamoja nasikatika utumishi wetu woote Yoel 3;10, 1Nyakati 28;20, Mathayo 28;19-20. 

  1. Kuwa na utii uliotimia kwa Viongozi wetu wa juu.
    Uasi wa namna yoyote kwa kiongozi wetu wa juu unamfanya Roho Mtakatifu atuache, wakati wowote ni muhimu kwa Viongozi wa kanisa kuhakikisha kuwa wanawatii Viongozi wao wa juu na wajuu wanawatii wale wa juu, utii huu ni kama ule utii wa jeshini  ni utii usio na ubishi wala majadiliano  hata kama moyoni unadhani kuwa agizo hilo lina dosari, mradi sio agizo la kufanya dhambi  ni muhimu kulitii kwanza  tukijiona kuwa tuna kitu chochote cha ziada kuliko kiongozi wetu wa juu  na kuacha kumtii basi Roho Mtakatifu anatuacha Barnaba alipoacha kumtii kiongozi wake Paulo na kushindana naye kuanzia hapo Roho wa Mungu aliacha kutupa historia yake akiwa na Marko Bali Roho anatupa ripoti ya Paulo na wale aliofuatana nao katika utumishi yaani Silla na Timotheo Matendo 15;36-41,16;1-3 kama Viongozi wa kanisa tunataka kuona Roho wa Mungu akiwa pamoja nasi na kututumia katika viwango vya kupita kawaida basi siri ni utii uliotimia 2Koritho 10;4-6.na tatizo la Viongozi wengi katika makanisa ya kiroho shida yao kuu ni kukosa utii na hasa utii uliotimia, Viongozi wengi watataka kufanya kazi kwa kusukumwa sukumwa tu na kwa msingi huo utendaji wa Mungu na karama za Roho Mtakatifu hufifia Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mtii na kuzidi katika  Yesu.

  1. Kuwaongoza watu kwa kutumia maombi
    Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa mtu muombaji siku zote akiwaombea wale anaowaongoza kwa kuwataja  majina na kuwaombea juu ya udhaifu walio nao, tukiwa tunapenda kufoka tu bila maombi ya kutosha  pamoja na kufoka kwetu sana tutaona mambo hayatendi kama inavyokusudiwa Yeremia 31;9 kuomba ni kumhudumia bwana inatupasa kumhudumia bwana zaidi kabla ya kuwahudumia watu tunao waongoza ili tuone mafanikio maombi ni kama mafuta yanayolainisha msuguano au ugumu wa mioyo ya watu tunaowaongoza bila maombi ya kutosha kanisa letu haliwezi kukua kiidadi na pia wale tunaowaongoza hawawezi kukua kiroho na watadumaa  kadiri mtu anavyopewa majukumu makubwa ndivyo anavyopaswa kuomba zaidi maombi husaidia kunyonya kiburi cha kibinadamu tukipenda kuwahudumia watu bila maombi ya kutosha ni rahisi kujidhuru  kiroho sisi wenyewe

  1. Kuacha kuongoza pale tunapokuwa vipofu.
     Katika sheria za usalama barabarani  dereva anashauriwa kusimamia ikiwa haoni vizuri mbele kutokana na ukungu au moshi n.k vilevile dereva anashauriwa kuegesha gari pembeni  na kulala ikiwa anaona usingizi  Dereva akipuuzia ushauri huo ni rahisi kupoteza maisha  vivyo hivyo kama Viongozi wa kanisa hatupaswi kumshauri mtu kitu ambacho hatuna uhakika nacho tukiwashauri watu makosa tutapata adhabu iliyo kubwa zaidi  Yakobo 3;1,Mathayo 18;6-7 lolote lile tusilokuwa na uhakika nalo ni vema kuulizwa kwa uongozi wa juu zaidi kisha kutoa majibu yapasayo  hivyo ni muhimu kuacha kufanya jambo lolote tusilolifahamu vema.

  1. Kuongoza kwa neno la Mungu
      Tukiona lolote kwa wale tunaowaongoza lisilofaa inatupasa kutumia neno la Mungu  kulirekebisha kwa upendo na sio Maneno matupu ya kibinadamu Neno la Mungu lina uwezo mkubwa wa kumbadilisha mtu wala sio adhabu zetu au Maneno yetu ya kuumiza mwanadamu huwezwa na Mungu tu Maneno ya kibinadamu husukumia tatizo kuzidi Mithali 6;21-23; 2timotheo 3;16-17,4;2.

  1. Kutokubali kuvunjika moyo.
      Adui Ibilisi humwandama kiongozi wa kanisa na kutumia kila aina ya mbinu ili kumvunja moyo, iwe ni kwa matatizo ya kikazi, kifamilia au kibiashara, kusengenywa, kunenewa vibaya kwa kila aina ya Maneno, n.k  na wakati mwingine atatuonyesha hali za kutokufanikiwa kwa njia mbalimbali hata kukuonyesha jinsi kanisa lako lisivyokua  na atakushauri ni afadhali uache  yamekushinda  kamwe hatupaswi kusikiliza ujinga huo na kukubali kuvunjika moyo kwa lolote hata kama tuna watu waili au mmoja katika kanisa Endelea kuwalisha kwa uaminifu na tudumu katika kazi ya bwana kwa uaminifu kwani kuna majira ya kupenda na kuvuna Matendo 21;9-14 Zaburi 126;5-6 Muhubiri 3;1-2 marufuku kukata tamaa tusikubali kuvunjika moyo kwa namna yoyote.

  1. Kuongoza kwa Hekima.
     Ni vigumu kuongoza kanisa la Mungu huku hatuna Hekima Hekima inatusaidia kujua kuwa tuseme nini, tujibu nini au tufanye nini na kwa wakati gani  Hekima ya Mungu ndio ufumbuzi wa tatizo hilo na hufumbua kwa amani Hekima humfanya mtu ajue neno la kuzungumzia wakati Fulani na sio kuropoka tu na kusababisha matatizo zaidi Mithali 25;11-12 kwa Hekima tunaweza kuwapa watu Elimu ya Mungu Mithali 16;21 hekima hutupa kujua jinsi ya kuwashughulikia wazee Tofauti na vijana n.k 1Timotheo 5;1 kwa sababu hii Suleimani alipofanywa kuwa mfalme   jambo la kwanza lilikuwa ni kuomba Hekima sisi na si ni muhimu kumuomba mungu atupe Hekima  kila siku katika shughuli zetu za maongozi 2Nyakati 1;7-10,Yakobo 1;5.

  1. Kufanya kazi ya Mungu kwa bidii.
     Hatuwezi kuwa na mafanikio makubwa katika kazi yoyote ya Bwana kama sisi wenyewe ni watu wavivu au walegevu inahitajika bidii kubwa ili kufanikiwa Yeremia 48;10 Warumi 12;11 hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa na vipindi vya mapumziko na kukumbuka kula chakula vizuri ili tusimpe ibilisi nafasi Marko 6;31-33.

  1. Kumbuka kuwaita moyo wale tunaowaongoza.
     Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu wa kuchokonoa mabaya tu ya kondoo wake na kutaja mapungufu yao tu inatubidi pia kutafuta yale yaliyo meme hata madogo na kuyainua hayo na kuwaita moyo na kuwapongeza kwa kawaida pongezi humtia mtu moyo wa kufanya vizuri zaidi na husaidia kuondoa makosa makubwa ya mtu na kufanya bidii zaidi 2samuel 11;22-25,Kumbukumbu 3;28.

  1. Kutangulia mbele ya Kondoo
     Mchungaji hutangulia mbele ya kondoo wake kuongoza , hii maana yake ni kuongoza kwa mfano huku ndio kuongoza kunakoleta mafanikio makubwa kiongozi anayechelewa kufika mahali pa ibada na kuonyesha udhaifu Fulani Fulani  huyo sio kiongozi anayewatangulia kondoo Yohana 10;4 Waamuzi 5;2 Marko 10;22-25 Kumbukumbu 3;28.

  1. Kuwa na utayari wa kuwapa wengine majukumu
     Kiongozi aliye botra hafanyi kazi yeye mwenyewe bali huwa tayari kuwapa wengine majukumuhususani wale anaowaongoza na wakati mwingine hata wale wachanga Kutoka 18;13-17.

  1. Kuheshimu mipaka ya madaraka uliyo nayo.
     Mithali 22;28 ni muhimu kutakuwa na kimbelembele kwa mambo yasiyohusiana na madaraka uliyo nayo fanaya kazi ndani ya mipaka yako mfano kama wewe sio msomaji wa kanisa usipendelee kuzungumzia lolote kuhusu kanisa acha wenye mamlaka kuu zaidi wazungumzie.

Shule maalumu ya uongozi somo la saba 
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
             Somo; Majukumu ya kiongozi wa kanisa
Kufahamu majukumu ya kazi za kiongozi katika kanisa ni mojawapo ya Jukumu muhimu kwa kiongozi wa kanisa, Mara nyingi imetokea Viongozi wengi wa makanisa ya kiroho hawajui majukumu yao na hii inachangia kwa kiasi Fulani kutokuyafikia malengo. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia mambo mawili yafuatayo

*      Viongozi wa kanisa ni wachungaji.
*      Majukumu ya kichungaji ya kiongozi wa kanisa

Viongozi wa kanisa ni wachungaji.

     Viongozi wa makanisa ya nyumbani au cells na Viongozi wengine woote na wasaidizi wao woote ni wachungaji wa kondoo wa Mungu, Hawa ni wachungaji wanaotenda kazi chini ya Mchungaji hata ingawa hawaitwi kwa jina hili, lakini majukumu yao wanayoyafanya ni ya kichungaji, katika mpango wa Mungu kila mtu ana husika katika utendaji kama makuhani wa Mungu Ufunuo 1;5-6, 1Petro 2;5,9 kama ikiwa kila mtu aliyeokoka Maandiko yanamuita kuhani ni zaidi sana mtu anapokuwa kiongozi katika kanisa Viongozi katika kanisa ni wachungaji wanaotenda kazi chini ya Mchungaji na kumsaidia katika huduma za kichungaji

Majukumu ya kichungaji ya kiongozi wa kanisa.

    Viongozi wa kanisa kama ilivyo kwa Mchungaji wana wajibika kufanya kazi ya uiunjilisti uchungaji na ualimu katika eneo lao walilopewa na Mungu leo tutachukua Muda kujifunza majukumu  mbalimbali ya kiongozi wa  yanayohusiana na uinjilisti na ualimu na uongozi kwa ujumla wake

  1. Kuwafahamu Kondoo kwa sura na majina Yohana 10; 2-3.
Ni wajibu wa kiongozi katika kanisa kuwafahamu kondoo wake kwa majina na sura, kadiri kanisa linavyokua na kuongezeka lazima kanisa liwe na mfumo unaoruhusu watu kujulikana kama kuwa na makanisa ya nyumbani ambapo kiongozi anapaswa kuwatambua kwa sura na majina ,watu hupenda kutambulika na hujisikia salama pale  anapokuwa anatambukiwa Kanisani hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwatambua watu wake, na kutokana na kuwafahamu kwa majina na sura  inakuwa rahisi kuwaombea kwa kuwataja majina yao Viongozi wanapaswa kuwafahamu wale Viongozi wengine walio chini yao  pia tunapaswa kujua mahudhurio yao katika ibada zote za mafundisho siku ya bwana na kadhalika 

  1. Kuhubiri na kufanya uinjilisti Marko 1;38-39;Matendo 20;27.
Kiongozi yeyote wa kanisa kwa ngazi yoyote ni lazima awe muhubiri  na anawajibika kuwahamasisha watu walio chini yake kuwa na furaha ya kuona watu wakiokolewa na kuongezeka katika kanisa  tuhakikishe kuwa tunawahubiri watu na wageni wanaokuja katika kanisa letu na kuwaaalika katika ibada mbalimbali za kanisa ,aidha kama ni kuiongozi wa cell au kanisa la nyumbani hakikisha kuwa unalihubiri eneo lote linalokuzunguka na kuhamasisha watu kuhudhuria ibada zote  aidha tunapofahamu kuwa Fulani na Fulani hawakuhudhuria ibada ni muhimu kuwatembelea na kujua ni kwanini hakuhudhuria  na kutoa msaada unao hitajika kwa  pia kufanya ufuatiliaji kwa washirika wachanga kiroho na kuwalisha kwa neno na mafundisho,kiongozi anapaswa kukumbuka kuwa mfano au kielelezo kwa watu aliopewa kuwaongoza.

  1. Kufundisha au kulilisha kanisa. Matendo 20;28.
   Lisha kondoo zangu huu ni wito kwa kila kiongozi wa kanisa kwa msingi huo ni wajibu wa kiongozi wa kanisa la nyumbani n.k kujiandaa na kujitayarisha mapema kwa habari ya somo atakalolifundisha  kila siku ya ibada za makanisa ya nyumbani au katika vipindi vya ibada za idara n.k. Masomo yanayopaswa kufundishwa ni yale yaliyo maalumu kwa ajili hiyo au yale yanayofundishwa Kanisani ni hatia kuleta mafundisho mageni 2Yohana 1;9-11,Tito 1;9 kufundisha kwetu hakuna budi kuwe na malengo ya kuondoa au kurekebisha  matatizo yaliyopo katika sehemu zetu za maongozi tabia kama masengenyo, kuchelewa ibada au kutohudhuria n.k kumbuyjka kuwa inahitaji maombi na maandalizi ya kutosha  kabla ya kufundisha somo au siyo kondoo watajkuwa  hawashibi na matokeo yake hawatavutiwa kuendelea kuja katika  katika kipindi husika.

  1. Kuwatunza kondoo.
Ni wajibu wa kiongozi kufanya kazi ya msamaria katika kutunza kondoo wake Luka 10;30-37 ni lazima kuwatafuta waliopetea na kujua kuwa ni kwanini hawaji katika ibada,lazima tumuombe Mungu atupe karama na vipawa  ili kuwahudumia watu wake kuomba kwa ajili ya uponyaji kwa ajili ya wote wenye shida za magonjwa na kuwafungua waliovunjika moyo kwa kuwapa neno la Mungu la kuwaita moyo Ezekiel 34;1-2,4-6.

  1. Kuwatembelea washirika na kujua hali zao za kimwili na kiroho.
    Yeremia 23;1-2 matendo 15;36.  Kiongozi yeyote wa kanisa anatakiwa kuifahamu kila nyumbay a mshirika wake  na kuwatembelea mara kwa mara na waqkati mwingine kwa kushtukiza ili ajue hali ya kimwili na kiroho ya washirika, bila matembezi ya jinsi hii  ni rahisi kumkuta kondoo amejerihiwa  iwapo kuna taarifa ya tabia mbaya ya mshirika awaye yoote  zifanyiwe uchunguzi wa kina na wa haki kisha zitafutwe njia za kumsaidia kiroho endapo liko juu ya uwezo wako likabidhio kwa Mchungaji kumbuka katika kuwatembelea washirika pia ni muhimu kuweka kipaumbele kwa wale walio wachanga ,wageni na wenye kuugua au waliopatwa na misiba na matatizo mbalimbali haita kuwa busara sana kwa mshirika aliyekomaa kiriho kuwa na madai ya kutembelewa na badala yake wao nao washirikiane na Viongozi katika kuifanya kazi ya kuwatenbelea washirika na kuwaita moyo.

  1. Kutoa ushauri kwa kondoo. Mithali 20;18;12;15.
Mengi tunayoletewa na kondoo kutaka ushauri mara nyingi ni yale yaliyo mepesi kuyatolea ushauri hata hivyo Mengine huwa magumu na mtu unapoletewa tu ni rahisi kuona moyoni kuwa hili limenizidi kimo  katika mazingira kama hayo hilo lipeleke kwa kiongozi wako wa juu na katika kanuni za kutoa ushauri ni vizuri uwe mwepesi wa kusikia kuliko kusema Yakobo 1;19 Roho wa Mungu hudondosha ushauri kwetu tunapokuwa watu wa kusikia au katika hali hii ya utulivu,  na wakati huo huo zingatia kuwa ni Kinyume na mapenzi ya Mungu kutoa siri za matatizo ya mtu aliyekuomba umpe ushauri Mithali 25;2,9.

  1. Kumlinda Mchungaji 1 Samuel 26;16
Viongozi katika kanisa  ni wawakilishi wa Mchungaji na wana wajibu wa kumlinda Mchungaji na kuhakikisha kuwa kila roho ya uasi  inayoinuka kinyume na Mchungaji inashughulikiwa ipaswavyo na kuitolea taarifa lazima kiongozi wa kanisa awe na moyo wa kiuchungaji Isaya 40;11,1Thesalonike 2;7 Bila moyo huu utendaji wetu wa kazi utaingia dosari.lolote linalopungua katika karama hii ya kumtumikia Mungu tumuombe Mungu atupe karama hizo za kutuwezesha kuifanya kazi yake  aidha sivibaya kuwatumia wale ambao Mungu amewapa karama hizo kutusaidia  katika kuwahudumia wale tunao waongoza.

 Shule maalumu ya uongozi somo la nane.
      Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
      Somo:Umuhimu wa kuwa na maono
Tunaingia katika somo muhimu sana katika Mfululizo wa Masomo haya ya shule maalumu ya uongozi na kama livyo kwa Masomo mengine somo hili umuhimu wa kuwa na maono kwa Viongozi ni somo la muhimu na tutajifunza somo hli kwa kuzingatia vipengele  vitano vifuatavyo.

*      Umuhimu wa kuwa na maono
*      Maana ya maono.
*      Makusudi ya Kuchaguliwa kuwa kiongozi katika kanisa
*      Faida za kuwa wengi katika kanisa
*      Umuhimu wa kuwa na maono kivitendo.

Umuhimu wa kuwa na maono.

    Katika Mithali 29;18 maneno pasipo maono watu huacha kujizuia  katika Biblia ya kiingereza ya KJV (King James Version) yanasomeka “Where there is no vision ,the people Perish” tungesema kwa usahii kwamba pasipo maono watu  huangamia au huacha kujizuia kuangamia.Watu wanapokosa la kufanya kuhusiana na mapenzi ya Mungu  hawana budi kuangamia kutokana na kutokuyafanya mapenzi ya Mungu. Kiongozi wa kanisa akiwa ni mtu asiye na maono yoyote  watu anaowaongoza hawataacha kujizuia kufanya yasiyo mpendeza mungu na wanaweza tu kuyafanya yanayo mpendeza mungu  kwa kufanya mapenzi yake ikiwa kiongozi ana maono.

Maana ya maono

Neno maono linalozungumzwa katika Mithali 29;18 maana yake ni “mawazo ya jinsi ya kutekeleza mipango na makusudi ya Mungu “kiongozi mwenye maono maana yake nui mtu aliyejaa mawazo ya mipango mbalimbali inayoweza kufanya makusudi ya Mungu yakatimilika ni muhuimu kwa kila kiongozi kuwa na maono hayo.

Makusuidi ya Kuchaguliwa kuwa Kiongozi katika kanisa

Mungu anamchagua kiongozi katika kanisa kwa makusudi ya kulifanya kanisa liweze kukua kuzaa matunda na kuongezeka Yohana 15;16 mungu anapendezwa na tawi linalozaa matunda hivyo ni wajibu wa kiongozi katika idara au kanisa la nyumbani au eneo lolote la maongozi ya kikanisa kuhakikisha kuwa anayafanya hayo mapenzi ya Mungu na kuufanya ufalme mzima wa mungu kukua na kuongezeka endapo tunashindwa kufanya hivyo tawi hilo litakatwa Yohana 15;2  mungu anafurahi wakati woote anapoona kuwa kiongozi katika kanisa anasababisha kanisa kukua kiroho na kiidadi na kanisa kuwa kubwa hata kufikia kiasi cha kugawanywa ikiwezekana Viongozi wa jinsi hii  ndio wanao mtukuza mungu Yohana 15;8 ni muhimu kwa kiongozi kuhakikisha kuwa nafanya jitihada mbadala ili mti huo aliokabidhiwa uzae matunda Luka 13; 6-9 mungu huonyesha furaha kuu kwa mtunzaji wa shamba la mzabibu ambaye shamba lake linazaa na kuongezeka Yohana 15;16 kiongozi wa jinsi hiii  maombi yake huwa na matokeo makubwa sana na mungu hujibu hujibu maobi ya kiongozi hyo kwa ufanisi Yohana 15;16 Hivi ndivyo ilivyo ulimwenguni kote leo Viongozi ambao makanisa yao yanaongezeka na kukua kwa kasi kubwa maombi yao huwa na nguvu kubwa ya kuleta majibu kutoka kwa Mungu Viongozi Nyakatiza kanisa la kwanza maombi yao yalikuwa na matokeo makubwa sana kwa sababu tu makanisa yao yalikuwa kwa kasi sana  bwana atupe neema ya kuwa na maono na mipango ya kanisa kubwa katika Kristo.

Faida za kuwa wengi katika kanisa

     Kiongozi yeyote wa kanisa nanpaswa kuwa na mawazo ya kukua na kuongezeka kwa kanisa lake usiku na mchana Ndiyo maana utaweza kuona kuwa Nyakati za kanisa la kwanza  walizingatia wakati woote kuhesabu idadi ya watu katika kanisa ili waone kama wanaongezeka ? Matendo 2;41,4;4,5;14,6;1,7, 9;31,11; 24,16;5. Kwa ujumla hesabu yao iliongezeka kila siku  huu ndio mukhtasari wa Nyakati za kanisa la kwanza walivyokuwa wakitenda kila siku kila kiongozi wa kanisa anao wajibu wa kuhakikisha kuwa anawapandikizia moyo washirika woote kuwa na mzigo wa kuliona kanisa linaongezeka  bila kufikia kiwango cha kuridhika na idai yeyote ni lazima tulisisitize hili tena na tena  hata lizame katika mioyo yao  pia ni muhimu kuwaelezea watu umuhimu wa kuwa wengi kwamba sio tu kunamfurahisha Mungu na kumtukuza  na kutekeleza agizo la mungu 1koritho 10;31,Lakini kukua kwa kanisa pia ni kwa faida yetu, Kanisa linapokuwa kubwa tunaweza kushirikiana na watu wengi katika matukio kama Misiba,harusi,furaha za kujifungua mtoto  n.k kunakuwa na watu wengi sana na wa namna mbalimbali wa kushirikiana nasi  na kutupa msaada sio hilo tu tuankuwa na watu wengi wa kutuombea kwani kanisa ni lazima watu wawe wanaombeana wao kwa wao
Umuhimu wa kuwa na maono kivitendo.

     Ni muhimu kwa kila kiongozi wa kanisa kujua kuwa ni mapenzi ya Mungu na ni ahadi ya Mungu kutuongeza kiroho na kiidadi katika makanisa Yetu Mwanzo 28; 3, 35; 11, Kutoka 1;7, Kumbukumbu 12;20, Zaburi115;14, Zekaria 10;7-8 ni muhimu kufahamu kuwa kiongozi wa kanisa ana nafasi kubwa ya kufanya kanisa lake likuwe na kuongezeka lakini ili kanisa likue na kuongezeka kiongozi katika ikanisa hana budi kufanya mbao ya msingi yafuatayo

  1. Kuhamasisha anao waongoza
Kwa kawaida watu tunaowaongoza huwa wanangoja tuwambie nini cha kufanya kwa kuwahamasisha ndipo wapambe moto,kwani tukikaa kimya nao hufanya hivyo ni wajibu wetu kufungua zizi la kondoo na kuwaacha watoke nje  tukilifunga tu nao wataendelea kukaa humo Yohana 10;4 Mungu hutupa kondoo ili tuwatumie na sio kuwafurahia kuona wanakaa humo ni muhimu kuwatumia kondoo kuongoza idadi ya kanisa  hivyo kukua na kuongezeka kwa kanisa ni muhimu kuwa wimbo wa kanisa letu mpaka kieleweke

  1. Kuhakikisha watu wanawaalika wageni.Zekaria 3;10.
   Ni muhimu kuhakikisha kuwa watu au wageni wanaalikwa kwa wingi katika kuhudhuria ibada zetu, watu wenye uwezo mkubwa wa kuwaalika wageni sio wale walio na muda mrefu katika wokovu hii hufanya kazi kwa kiwango kizuri kwa wale waliookoka hivi karibuni yaani wachanga wao ni rahisi kuwaalika marafiki zake, wa zamani kabla hawajamkimbia kwa sababu ya wokovu mtu aliyeokoka karibuni maisha yake hayatofautiani sana na wasiookoka  na hivyo ni rahisi kwao kuwa wenye kupatana kwa urahisi  hivyo ni muhmu kuwahamasisha wale wachanga kufanya kazi ya kuwaalika wengine  na kuacha kupiga kelele hizi kwa wale wa zamani tuwafahamishe kuwa wanapowaleta wageni watatoa taarifa kwa Viongozi ili wapenyeze ujumbe wa wokovu kwa wageni hao na kuwaleta kwa Yesu

  1. Kushuhudia Yohana 4;28-30,39;Marko 16;15. Wale waliookoka zamani tuwahamasishe zaidi katika maswala ya kushuhudia hata kama hawajapitia katika shule maalumu ya uinjilisti tuwafundishe namna wanavyoweza kushuhudia au kuambatana nao katika shughuli ya ushuhudiaji.
  2. Kuwafuatilia watoto wachanga Waebrania 5;13,1Petro 2;2. Tusi wangojee watu kufikia hatua ya kupitia shukle ya uinjilisti ili wajifunze ufuatiliaji ni lazima tuwafundishe sisi wenyewe na kuwakomaza katika kuifanya kazi nzima ya ufuatiliaji tukafanya hivi kwa upendo tutaweza kuona matokeo mazuri bila haja ya kukemea na kukaripia hasa kama ni watoto wachanga
  3. Kuhakikisha kuwa wanapata neno la Mungu Mathayo 4;4 Neno la Mungu ni muhimu  na lina uzito mkubwa hasa katika ibada za kanisa kuu hivyo tuwasisistize watu kuja ibadani na kulisikiliza neno la mungu wakati mwingine ghata kama ni kwa njia ya kaseti.
  4. Kufanya maombi kwa ajili ya kukua kwa eneo lako au kanisa lako. Kukua kwa kanisa hakuwezi kutokea bila kuwako kwa maombi ni muhimu kuwa na maombi ya aina mbalimbali kama ya kufunga au kufanya maombi ya mapatano  na kuwa na maombi maalumu pia kwa ajili ya ukuaji wa kanisa Zaburi 2;8.
  5.  Hakikisha ya kuwa unawajali kondoo.
Imani hutenda kazi kwa upendo Wagalatia 5;6  Ni muhimu kutilia mkazo kwa uzito mno kuhusika na wagonjwa na wenye shida ,misiba wasio na nauli za kuja ibadani wanaojifungua n.k ng’ombe anayetunzwa vizuri mara nyingi hutoqa maziwa mengi na mbwa mkali ni tule anayejaliwa na kutunzwa tukipunguza matedno ya ukarimu na upendo tunashusha chini kiwango cha ukuaji wa kanisa letu na kutoa mwanya wa kwenda mahali wanakoona kuwa wanajaliwa zaidi tukipungua katika eneo hili nqa kuwataka watu watende kazi tu tutaona upungufu mkubwa upendo ndio ufunguo mkubwa wa kukua kwa kanisa

  1. Washrikishe watu malengo
Eleza juu ya mahudhurio toa ripoti za aina mbalimbali ikiwemo maswala ya fedha na matumizi waeleze juu ya ongezeko la kanisa waeleze furaha ya Mungu ya kuona wakiongezeka  kama ni kanisa la nyumbani likifika idadi ya watu 250 ni muhimu luikigawanywa na kuendelea kuwa na matawi mengi zaidi ya nmakanisa ya nyumbani au cells  hii itakuwa nifuraha kubwa kwa Mungu Ezekiel 19;10;Marko 4;30-32,.

  1. Panga mipango mwingine ya kuongezeka kwa kanisa lako.
Kiongozi mzuri ni yule mwenye ubunifu mkubwa hata zaidi ya ule tulio jifunza katika mbinu za kijeshi kiongozi wa kijeshi anatakiwa kuwa Hodari yaani Mashal huyu ni mtu mwenye uwezo wa kuwa na mbinu ambazo ni zaidi ya zile alizijifunza  hizi unakutana nazo huku huko katika uwanja wa vita  jaribu na usiogope kukosea mtu anayeogopa kukosea hawezi kuwa kiongozi mzuri Petro alikuwa mwenye kujkosea sana na Yesu alimfanya kuwa kiongozi wa kanisa ukikosea utarekebishwa na utaendelea Mbele, Mungu akubariki sana

Shule maalumu ya uongozi somo la Tisa.
      Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
       Somo: Maelekezo kwa kiongozi wa kanisa la nyumbani
Somo tunalojifunza sasa ni miongoni mwa Masomo ya mwisho kabisa katika awamu hii ya kwanza ya Masomo maalum ya shule ya uongozi somo hili ni muhimu endapo kanisa husika litakuwa na mfumo huu wa makanisa ya nyumbani au cells na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-
*      Jinsi ya kufanya ili kondoo watupende, kututii na kutuheshimu.
*      Jinsi ya kuongoza ibada ya makanisa ya nyumbani
*      Umuhimu wa kutoa ripoti za makanisa ya nyumbani
*      Tahadhari kabla ya hatari.
Jinsi ya kufanya ili kondoo watupende, kututii na kutuheshimu.
     Wengi wetu hususani Viongozi tunapenda kuona watu wanatupenda kututii na kutuheshimu, lakini hatujui ni jinsi gani tunaweza kuona hayo yakitimia kwa ukamilifu watumishi wengi wa Mungu na Viongozi wengi wa kanisa wanapenda kuona kondoo walio chini yao wakiwapenda na wakiwapenda kuwatii na kuwaheshimu  lakini siri kubwa ya kupendwa na Kuheshimiwa kwanza ni kujitoa kivitendo kuwapenda na kuwahudumia kwa upendo wa kweli na sio wa Maneno tu au ulimi 1Yohana 3;18 uhusiano wa kondoo na kiongozi wao unafanana na uhusiano wa mke(anyeongozwa) na mumewe (kiongozi)Mume ana wajibu wa kumpenda mkewe kama nafsi yake mwenyewe ili ategemee Kuheshimiwa na kuipokea utii  kutoka kwa mkewe Waefeso 5;24-25,28,33. Vivyo hivyo siri ya kiongozi kupendwa na wale anaowaongoza na wakamtii na kumuheshimu ni kuwapenda kondoo walio chini ya uangalizi wake Yohana 11;5,19;26,20;2 21; 7,13;34,15;12. Yesu Kristo aliwapenda kondoo wake kivitendo alishughulika na matatizo yao  na kuonyesha kuwajali na kuwa karibu nao  katika matatizo makubwa na madogo kwa mfano Petro alipouguliwa na mkwewe kiongozi wake wa kanisa Yesu alihusika mara moja na tatizo hilo Marko 1;30-31 alihusika pia na matatizo ya kondoo wake Mariamu na Martha  walipokuwa wamefiwa na ndugu yao Lazaro Yohana 11;1-44 Yesu kama kiongozi na kielelezo aliugua nafsini mwake na kulia machozi  alipowaona kondoo zake katika matatizo,hii ndio ilikuwa siri kubwa ya kondoo zake kumpenda kumtii na kumuheshimu,hatuwezi kamwe kuipokea heshima na utii toka kwa kondoo hawa kama tunawapiga nyundo na kuwasema kuwa wana kiburi tunawalaumu na kuwasema kuwa ni kiburi au jeuri n.k kumbe tatizo letu tumeshindwa kuwaonyesha kuwa tunawapenda  kwa vitendo  unapokwepa kuyafanya hayo usitarajie watu watakuogopa na kukupenda na kukuheshimu never! Kupendwa na washirika kunahitaji jitihada na juhudi nyingi kutoka kwa kiongozi 1Petro 1;22,4;8 ni lazima tuonyeshe bidii na kufanya juhudi kutoka moyoni  kuonyesha kuwa tunawajali na kuhusika nao katika jambo lolote ambalo linawapata iwe la furaha au la huzuni hata kama kondoo ankwenda au kurudi kutoka likizo unaweza kupanga namna ya kumpokea au kumsindikiza kwa kuhusika sisi wenyewe au kutuma wawakilishi  tukafanya hayo na kuzidi lazima kondoo watatupenda kutuheshimu na kututii na hapo ndipo tutakapoiona kazi yetu na kifurahia sana kinume cha hapo tutakuwa na kondoo jeuri na wakaidi na watatuletea shida kubwa sana.
Jinsi ya kuongoza ibada ya makanisa ya nyumbani
    Ibada za kanisa la nyumbani inaweza kufanyika kila jumamosi au siku ifaayo kulingana na mazingira husika  na twaweza kifanya kuanzia saa 9 kamili mpaka saa 11 jioni ibada iaongoza na kiongozi wa kanisa la nyumbani au msaidizi wake  au kiongozi mwingine  ufuatao unaweza kuwa utaratibu unaofaa katika kuliongoza kanisa la nyumbani kiibada

Kipindi
Muda
dakika
Maombi ya kufungua ibada
            9;00 - 9;03
Dakika 3 tu
Kukaribisha wageni kwa ma
            9;03 - 9;05
Dakika 2 tu
Pambio na kuabudu
            9;05 - 9;10
Dakika 5 tu
Shuhuda
            9;10 - 9;20
Dakika 10 tu
Neno la Mungu
            9;20 - 10;00
Dakika 40-45 tu.
Maombi kwa ajili ya kanisa
           10;00 -10;15
Dakika 15 tu
Kuombea wenye uhitaji
           10;15-10;35
Dakika 20 tu
Matangazo kuhusu ibada
           10;35-10;45
Dakika 10 tu
Kuombeana
         10;45 - 10; 55
Dakika 10 tu
Maombi ya kufunga
         10;55 - 11;00
Dakika 5 tu


Ibada za makanisa ya nyumbani hazipaswi kuwa ndefu zaidi ya muda uluiokusudiwa acha watu warudi nyumbani mapema kweupe nuruni na sio usiku gizani
Umuhimu wa kutoa ripoti za makanisa ya nyumbani
   Ni muhimu kwa kiongozi wa kanisa la nyumbani kutoa ripoti kwa Viongozi husika katika kanisa  kila wiki au kulingana na utaratibu mtakaojiwekea katika kanisa , hili ni la muhimu kwani litamsaidia mchungaji kuwa na Ufahamu kuhusu kanisa na kushughulikia matatizo husika ni dhambi kutokutoa ripoti ni sawa na kujenga ufalme wako mwenyewe Marko 6;30;
Tahadhari kabla ya hatari
1.      Ni muhimu kufahamu kuwa unapokuwa kiongozi wa kanisa kwamba shetani atakutafuta kwa viwango vikubwa ili yamkini akurudishe nyuma hakuna furaha kubwa sana kwa shetani na ufalme wake kama anapofanikiwa kumrudisha nyuma kiongozi wa kanisa  kwake huo ni ushindi mkubwa sana kuliko ule wa kuangusha mshirika wa kawaida kiongozi akianguka maadui wa injili hufurahia sana na shetani hufurahi kwani linachangia kuwafanya walio wachanga wengi kuanguka pamioja na kiongozi wao yaani inachangia sana wachanga kuacha wokovu hii huwafurahisha maadui wa wokovu wafilisti  2Samuel 1;17-20;12;7-14 siku zote unapoukata mti mkubwa unapoanguka unaangukia na miti mwingine midogo na kuiua na hili linakuwa ni sababu ya kuwakosesha watu wa Mungu walio wadogo, Mathayo 18;6-7 Bwana ampe neema kila moja wetu amabye ni kiongozi wa kanisa kuendelea kuitegemea neema ili  tatizo litakalotufanya turudi duniani Mathayo 26;31-35,56,69-75.Mathayo 26;21-22.
2.      Mbinu nyingine ya shetani kuvunja heshima ya kiongozui ni kuleta mafarakano mafarakano hayo huweza kuletwa na washirika wetu wakitumiwa na shetani,kila kiongozi anapaswa kuwa upande wa kiongozi wake au mwenzake wanapokuwa mbele ya kondoo,maswala ya Viongozi kwa Viongozi shughulikieni wenyewe pembeni 1timotheo 5;17,19,21, 1 Samuel 9;26-27. Viongozi ni muhimu kuchukuana faraghani na kuambizana mambo yenu usipoheshimu mafuta mungu ni rahisi kukuacha mafuta ni lazima yaheshimiwe wako watu wanawafanyia watumishi wenzao mambo ya kuwaaibisha mbele za washirika huko ni kudharau upako na utavuna kudharauliwa hata na wewe mwenyewe kwa washirika Viongozi lazima washikamane kama askari tukiifanya kazi ya Mungu kwa pamoja
3.      Ni muhimu kuiongozi kujilinda na kiburi majivuna humaliza kabisa huduma nzuri ya kiongozi awayeyote na kutuingiza hukumuni Mithali 11;2,16;18 Yeremia 50;31-32 1Timotheo 3;6 Kiburi ni hali inayoinuka ndani ya mtu na kujiona yeye ni yeye kama ni kiroho mtu huweza kujifikiri kuwa Yuko juu kuliko watu wote Hapo tayari kichwa kimekuwa puto na kupasuka ni rahisi,watu wenye kiburi wamejiharibia huduma au wameharibu huduma za watu wengine Kiburi! Hali ya kujiona Bora kuliko wengine, kuhukumu wengine kuhitaji kuheshimiwa na kuabudiwa kama miungu wadogo hii nishida kubwa Mtu akiwa na kiburi Mungu humuacha polepole hii ndio dhambi iliyomfanya shetani akatupwa toka Mbinguni juu na kushushwa chini kuzimu Bwana atupe neema kila mmoja wetu kuwa wanyenyekevu katika jina la Yesu amen.


Shule maalumu ya uongozi somo la Kumi.
Mchungaji Innocent Kamote.
******************************************************
                                   Somo ;Wajibu wa msaidizi
Somo hili ni somo muhimu katika Mfululizo wa Masomo maalumu ya uongozi wa kanisa,kukosa Ufahamu katika somo hili kutalifanya kanisa kuwa bduni na dhaifu na kuwa katika nafasi ya kushambuliwa na iblilisi na kutekeleza mipango yake iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu ufalme wa Mungu hauwezi kustawi kama ikiwa Viongozi wa kanisa watakosa maarifa yatokanayo na kujifunza somo hili kwa msingi huhuu itakuwa sio rahisi kwa kanisa kukua na kuongezeka na kuwa kanisa la maelfu ,malaki au  mamilioni ya watu,kuwa na mafanikio makubwa katika kanisa kutategemeana na jinsi gani Viongozi watalitendea kazi somo hili Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuipokea maarifa yatokanayo na somo hili katika jina la Yesu Amen.Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vingele sita vifuatavyo;-

*      Umuhimu wa kuwepo kwa wasaidizi wa kiongozi mkuu
*      Viongozi wa kanisa kama wasaidiszi wa kiongozi mkuu
*      Sifa za msaidizi
*      Wajibu wa msaidizi
*      Madhara ya msaidizi anayewasaidia waovu badala ya kumsaidia kiongozi mkuu
*      Mbinu kubwa anayoitumia shetani kuharibu huduma ya kiongozi mkuu na jinsi ya kuikabili.

Umuhimu wa kuwepo kwa wasaidizi wa kiongozi mkuu

     Hapo mwanzoni Mungu alimuumba Adamu Mwanamume wa kwanza kuishi duiniani na kumkusudia kutawala peke yake .Hata hivyo muda usio mrefu baada ya kuumbwa kwa Adamu Bwana Mungu alisema si vema huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi Mwanzo 2;18. Kumbe mume anahitaji msaidizi Ni muhimu kufahamu kuwa katika mambo mengi ya kifamilia yana fanana sana na kanisa Waefeso 5;22-32 Kwa msingi huo si vema kiongozi mkuukatika kanisa kufanya kazi peke yake hivyo ni muhimu kuwa na msaidizi.

Viongozi wa kanisa kama wasaidizi wa kiongozi mkuu.

     Maelekezo ya Mungu kupitia kwa mkwewe Musa yalikuwa kama hayo Si vema  Musa kiongozi mkuu kuwa peke yake bila wasaidizi, kutokana na maelekezo hayo Musa alikuwa na wasaidizi waliokuwa Viongozi wa Maelfu na mamia na wa hamsini na wa makumi,hawa walimsaidia musa kuchukua mzigo wa kuwaongoza wana wa Israel au kanisa la jangwani kutoka 18;13-26,Matendo 7;37-38. Hivyo ni muhimukuwa na mgawanyo wa wasaidizi ili kuifanikisha kazi ya Mungu Mfumo huu umefanya kazi nzuri katika kanisa la Full Gospel of Yoido Seoul Korea kwa Dr David Yonng choi na Full gospel Bible Fellowship Tanzania kwa askofu Zachary Kakobe na Yaoundé Cameroun .

Sifa za Msaidizi

Kila kiongozi msaidizi wa kiongozi anapaswa kuwa na sifa zifuatazo na kupaswa kuhakikisha anakua nazo katika maisha yake ni sifa za muhimu na za kibiblia;-

  1. Kufanana na kiongozi wake mkuu.
     Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye (Mwanzo 2;18) Yeyote asiyefanana na kiongozi wake mkuu hawezi kuwa msaidizi anayefaa Mwanzo 2;19-20, Kufanana na kiongozi wako mkuu ni kuwa na nia moja naye kama ilivyokuwa kwa Timotheo kwa kiongozi wake Paulo Wafilipi 2l;19-20 kuwa na nia moja ni pamoja na kuwa na maono mamoja na kiongozi wako, yaani yale anayoyaona, anayoyataka yawe, yote hayana budi kuonekana vilevile kwa msaidizi mipango na maono ya kiongozi mkuu hayana budi kuwa ya msaidizi pia.

  1. Msaidizi ana paswa kuwa mwili mmoja na kiongozi wake  Mwanzo 2;18-24 lazima uhakikishe kuwa unakuwa upande wakiongozi wako mkuu kwa gharama yoyote ile 2samuel 5;1-4 Nyakati 12;1,17-18 hivi ndivyo masaidizi anavyopaswa kuwa tumika pamoja naye katika mswala ya injili katika utii kwake kama mwana na baba yake Wafilipi 2;19-22 Msaidizi anayefaa hatakuwa mfuasi wa Bwana Yesu tu bali na wa kiongozi wake 1Thesalonike 1;6 msaidizi anayefaa ni yule anayekuwa tayari kuwa mfuasi wa Kristo na wa kiongozi wake mkuu.
Wajibu wa msaidizi

      Jukumu kubwa la msaidizi kwa ujumla wake ni kusaidia na sio kuwa kinyume na kiongozi wake utamsaidia kiongozi wako mkuu kushinda maadui zake kutekeleza majukumu yote pamoja naye mipango na maazimio yakewasaidizi wanapojitoa hivi kuwasaidia Viongozi wao siku zote ndipo kanisa linapoweza kuwa Jeshi kubwa kama jeshi la Mungu, Kutoka 2;16-17, Yoshua 10;6, 2Nyakati 26;1, 15 2Samuel 21;15-17 1Nyakati 12;1, 14-18, 22.
Madhara ya msaidizi anayewasaidia waovu badala ya kumsaidia kiongozi mkuu
     Msaidizi anapoamua kuwa upande ulio kinyume na mipango ya kiongozi wake mkuu mtu huyo anakuwa anawasaidia waasi na waovu na kufanya hivi ni kutafuta adhabu ya Mungu 2Nyakati 19;2 Hatuna budi kuwa waangalifu tunapokuwa Viongozi Maneno ya washirika na hata wasio washirika yatatushawishi tusiwe upande wa kiongozi wetu mkuu na hivyio kuweko na usaliti na kumsaidia shetani kazi yake jambo hili linaharibu sana kazi ya Mungu ni vizuri kuwa upande wa Nabii na utapokea thawabu ya Nabii Mathayo 10;40-41.
Mbinu kubwa anayoitumia shetani kuharibu huduma ya kiongozi mkuu na jinsi ya kuikabili
 Tangu Mwanzo shetani amekuwa akiwatumia wasaidizi kuharibu huduma za Viongozi wao wakuu,alimtumia hawa kumsaidia shetani badala ya Adamu,pale alipompa tunda mumewe ale na hivyo kuharibu huduma ya adamu Mwanzo 3;4-6,Shetani alimtumia Sipora mkewe Musa msaidizi na hivyo ilibidi Musa aambatane na Haruni badala ya Sipora Kutoka 4;18-29 Shetani alimtumia mkewe Ayubu msaidizi kujaribu kuiua huduma na maisha ya Ayubu Ayubu 2;9 alimtumia Yuda mmoja wa Viongozi wasaidizi wa Yesu kumsaliti Yesu,na hii ndio maana Yesu alimuita Yuda Shetani Yohana 6;70 kwa sababu aliifanya kzi ya Shetani Hata leo shetani huwatumia  Viongozi wa kanisa katika kuharibu mipango ya mungu kwa kanisa Ni muhimu kuwa waangalifu kuhakikisha wakati woote tunakuwa upande wa Viongozi wetu na kuwalinda na kuwatia moyo na kufanya kazi pamoja nao Sehemu nyingi duniani ziko shuhuda za kutosha zinazoonyesha jinsi Viongozi wasaidizi walivyotumika kuharibu kanisa la mungu tuwe makini kwani Viongozi katika kanisa ni Nguzo Tunapo tetereka jingo yaani kanisa linakuwa katika wakati mgumu sana Wagalatia 2;9 Bwana atupe neema Tunapochaguliwa kuwa wasaidizi kutokukubali kutumiwa na Shetani katika Jina la Yesu amen.


Shukurani maalumu

   Masomo haya Mwandishi alijifunza alipokuwa mshirika wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Mwenge Dar-es-Salaam kwa msingi huo ni muhimu kwako kuwa na Ufahamu kuwa kanisa hilo ni sehemu ya mwili wa Kristo kama ilivyo kwa makanisa mengine , mimi bnimejifunza Mambo mengi sana nilipokuwa mshirika katika kanisa Hilo chini ya Mchungaji wangu Zachary Kakobe hivyo nachukua nafasi hii kutambua mchango wake kwangu na kwa kanisa la Tanzania ni Muhimu kulizingatia hili na kukubali kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu Endapo utakuwa unapiga vita huduma ya kanisa hilo basi hata mafundisho haya yanaweza yasitende kazi utakapoyatumia katika kanisa lako sisi tu viungo katika Kristo Nyakati hizi hatuwezi kuendelea kung’ang’ania udhehebu bali tunapofahamu kuwa mahali Fulani inahitajika kweli au pana mambo mazuri ya kujifunza basi ni muhimu kujifunza kutoka kwa watu hao. Hivyo nachukua nafasi hii kuitambua huduma ya Zachary Kakobe na kitabu hiki ni wakfu kwa ajili yake Mungu ambariki na namtakia huduma njema amen

Rev. Innocent Mkombozi Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
ikamote@yahoo.com
0718990796
0784394550
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni