Jumatano, 29 Oktoba 2014

Kama Si Bwana Israel na Aseme Sasa!


Zaburi ya 124;1-8.
Biblia inasema Hivi “   
 
1. Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, 2. Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia.       3. Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu 4. Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 5. Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. 6. Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. 7. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.             8. Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi”.

     Zaburi ni mojawapo ya vitabu vya kipekee sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano, inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana  na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa hisia za watu, utafiti wa kiroho unaonyesha kuwa wengi wenye kuzisoma kuzipenda na kuzikariri maisha yao huwa na mafanikio makubwa sana asante Bwana Mungu wangu Mungu wa baba zangu kwa kitabu hiki kizuri Zaburi 


·         Zaburi ziliandikwa kwa sababu mbalimbali za kihisia kama vile watu walipokuwa na furaha, huzuni, nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kama shwari  katika tenzi za rohoni aliimba wimbo huo kwa sababu ya ajali mbaya iliyokumba familia yake nay eye peke yake alipona na kutunga wimbo huo, kwa hiyo hata zaburi ziliandikwa kutokana na mapito mbalimbali waliyoyapitia wanadamu, kuna sababu nyingi zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1.       Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1
2.       Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingu huanza kwa kusema mshukuruni Bwana
3.       Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4.       Zaburi za kifalme au za kimasihi
5.       Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu
6.       Zaburi za kusifu au Halel Psalms ambazo huanza na neno Haleluya
7.       Zaburi za maombolezo
8.       Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano zaburi ya 351-8

Zaburi ya 124 ni zaburi ya kihistoria ni ya kukumbuka matukio na ni zaburi inayokisiwa kuwa imeimbwa na mfalme Daudi au mtu wa karibu na Daudi Kwani zaburi zimeandikwa na watu wengi akiwemo Musa, Sulemani wana wa Kora n.k na Daudi anazo zaburi kama 73 hivi na nyingine ni zaburi yatima yaani haijulikani nani aliandika, Zaburi hii ya 124 inakisiwa ndiyo iliyonukuliwa na Paulo katika Warumi 8;31 “Mungu akiwa upande wetu ni nani atakayekuwa juu yetu?” Inaonekana mwandishi wa zaburi hii alikuwa akitafakari kwa niaba yake na kwaniaba ya Taifa la Israel  jinsi hasira za adui shetani zilivyokuwa juu yao jinsi alivyokusudia kuiangamiza Israel kwa moto, maji mitego na mbinu mbalimbali, jinsi alivyokusudia kutumaliza lakini hatimaye  anaanza na hitimisho kuwa kama Bwana asingelikuwa pamoja nasi Tungeliangamia huku Israel wakiwa mashahidi ya wema wa Bwana na utetezi wa Mungu Hivyo kama si bwana Israel na aseme sasa Israel ni taifa linalotetewa na Mungu hata leo ni mara kadhaa wamepitia  misukosuko ambayo isingelikuwa rahisi kuiepuka kwa hali ya kawaida

*      1948 – wayahudi walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu wanawake na watoto Waarabu wakiwa milion 80 walikusudia kuwa futilia mbali lakini kwa uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya waarabu na kufanikiwa kupanua mipaka yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaka ukanda wa gaza, milima ya Golan, na kuuteka mji wa Yerusalem
*      1950 – Wafaransa walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa hivyo uhusiano na Israel kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha ndege hizo na zikatoa kichapo kikali
*      June 5 1967 – Israel kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na nyingine za Jordani na Syria  zilitandikwa vibaya na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba wa kudumu wa amani na Israel kuwa hawatapigana tena milele, mkataba huu uliwafanya Israel kuipa Misri Jangwa la mlima Sinai, kwa masharti kuwa hawatapigana milele
*      1969-1970 – Ndege 111 za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo waarabu waliaibika
*      Jeshi la anga la Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation mbalimbali waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo vilivyoweza kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali Mustafa, Ahmed Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea msikitini wakati wa ibada ya ijumaa
*      1976 walifanikiwa kuokoa  wayahudi kadhaa waliokuwa wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation iliyoitwa operation Entebe
*      1991 – Jeshi la anga la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko Ethiopia wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani Katika operation iliyoitwa operation Solomon
Sisi nasi tunapotafakari maswala ambayo adui ameyakusudia kwetu na kuona ushindi wa ajabu ni muhimu kufahamu kuwa kama si Mungu kuwa upande wetu tungelifutiliwa mbali kweli Kama si Bwana Israel na aseme sasa!

Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni