Alhamisi, 20 Novemba 2014

SOMO: Kwa Nini Wakristo Tunavaa Viatu Wakati Wa Ibada?

Nachukua nafasi hii kwa unyenyekevu mkubwa kujibu swali kwa nini wakristo tunavaa viatu wakati wa Ibada? Hili ni swali muhimu sana kwa vile linaulizwa na wakristo na waislamu hivyo nitalijibu kwa faida ya jamii nzima, lakini naomba kutoa angalizo, kuwa mada hii isitumike kwa kusudi la kukashifiana au kutukanana kwa vile nimeingia huku kwa kuwa nataka kujibu swala na sio kwa makusudi ya kuamsha mabishano ya Kidini Mimi ni mjenzi wa jamii na sio mmbomoaji ni mwalimu wa falsafa na nafundisha imani zote kwa makusudi mema ya kujenga na sio ya kubomoa
Ndugu zetu waislamu huwa wana huwa wanatulaumu kuwa huwa hatumueshimu Mungu kwa vile tunavaa viatu wakati wa ibada tofauti na wao ambao huvua viatu hasa pale wanapoingia Msikitini, waislamu hudai hayo kwa kunukuu Biblia (Kutoka 3;3-6 na Yoshua 5;13-15).vifungu ambavyo huonyesha Musa na Yoshua wakiambiwa wavue viatu. Kutoka 3: 3-6 Inasema …


3. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. 4. BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5. Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu…..”
Kwa ufupi ni kuwa hakuna aya yoyote katika quran ambayo inaunga mkono swala zima la kuvua viatu wakati wa kuswali, zaidi ya aya hizi mbili zinazopatikana katika Biblia yaani upande wa agano la kale, waisalamu wanaovua viatu wamepata mila hii kutoka katika Biblia kwa vile Historia inaonyesha kuwa hata waislamu walioishi kipindi cha Muhamad na muhamad mwenyewe waliswali wakiwa na viatu. Na hakuna agizo lolote kutoka katika Quran linaloagiza kuvaa viatu!


Ni muhimu kufahamu kuwa kwa waislamu wanaoifahamu quran, quran haiingilii maswala ya ibada za watu wengine kila umma umejaaliwa kawaida ya ibada wanayoishika soma (Surat al-Hajj-I 22; 67) kwa mujibu wa Pamfleti moja ya huduma ya biblia ni jibu Tanzania imenukuu kitabu kimoja kiitwacho Uislamu katika Biblia uk.20-21 kuna maneno yasemayo.


“Waislam wanapoingia pahala popote patakatifu kama vile msikitini huvua viatu, kinyume na wakristo…”Mwandishi wa pamfelti hilo anadai waislamu ni lazima wajiulize kuwa Musa alipoambiwa avue viatu maana pale alipokuwepo ni mahali patakatifu je mahali pale palikuwa mahali pa ibada kama msikiti? Kama mahali pale palikuwa patakatifu kwa kuwa Mungu alikuwepo pale je ni lini huyo Mungu amehamia msikitini? Mungu yuko mahali kote je Musa alipoambiwa avue viatu aliviweka upande gani ambapo Mungu hayupo?na kama Musa alivishika mkononi je havikuwa najisi kwake? Biblia inatufundisha kuwa utukufu wa Mungu umeijaa dunia nzima (Isaya 6;3) ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hakuwa na maana inayodhaniwa na waislamu bali alikuwa anawataka watu hao Musa na Yoshua kuwa wanyenyekevu,watii,wenyekujishusha,wenye hofu ya Mungu Viatu pia ilikuwa iashara ya kuwa na mamlaka lakini mamlaka tuliyo nayo kwa Mungu si kitu, si kila kinachotamkwa katika Biblia ufasiriwa kama mtu apendavyo kwa mfano Mungu asemapo “Tahirini govi za mioyo yenu”(kumbu 10;16). Je, Mungu humaanisha moyo utahiriwe? Je moyo unaonekana?, Una govi? Itamfaa nini mtu kuvua viatu wakati wa ibada huku moyoni ni mchafu ?


Ni muhimu kufahamu kuwa waislamu wanapovua viatu hawamfuati Muhamad ambaye yeye ni Ruwaza nzuri sawa na (surat Al-ahzab 33;1). Muhamad mwenyewe anasema “Alaa Yuminu ahadukum hattaa Yakuna Hawaahu Tab’an lima jitubihi” yaani haamini yeyote (katika ninyi waislamu)hata matamanio yake yawe yenye kufuata kile nilichokuja nacho(yaani kuvaa viatu ibadani). Kwanini kwa sababu Muhamad mwenyewe alivaa viatu ibadani, angalia uthibitisho;-.


• Muhamad alikuwa anaswali, huku amevaa viatu, Al-Mughira alijaribu kumkumbusha Muhamad hasa alipomuona anatawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini Mughira akasema “Yaa Rasuwlala-hi Nasiyta”, (yaani ewe Mtume wa Allah Umesahau) Muhamad akajibu “Anta Nasityta Liannahuhadha Huwaamaratani rrabbu” (Yaani wewe ndiwe uliyesahau kwa maana hivi ndivyo alivyoniamuru Mungu) soma Miskat-al-Masabih,sura ya 10 sehemu ya III,Kitab-al-Wadhu) Kama Muhamad aliamuriwa asali na viatu je waislamu wametoa wapi swala la kuvua?


• Muhamad anaonekana tena akiswali na viatu katika (sahih-al-Muslim,I,hadith 555) hapa Saad bin Yazid (abu Maslama)alipokuwa anamuuliza Anas bin Maliki “Akana Rasula llaah (SAW) Yaswullay fiy l-Na’alay-hi?qala na’am” yaani Mtume wa Allah huswali huku amevaa viatu vyake? Anasi akajibu “Ndiyo”


• Sehemu nyinginezo nyingi ambazo Muhamad anaonekana akiswali na viatu na tena si kosa kufanya hivyo ni pale alipotawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini na kuswalisha (Muwata-Imam malik sura ya 16-hadithi 69) pia soma sahih al-Bukhari I,hadith 388.,Sahih-al-Muslim I,hadith 1129,1130,nk).Pia Mishkat-a;-Masabihi vol ii hadith 766,Sunnan Abuu Dawud – Juzuu ya 1-uk,36-40 (Tafasiri ya Profesa Ahmad Hassan)nk. Katika kitabu hicho Abuu Said amemkariri Muhamad akisema baada ya kuulizwa swali.


“Mtu akifika msikitini na huku amevaa viatu vyake afanye nini?” kwa kiarabu “Idhaa jaa-a ahadukum lmasijid,Fal-yaqalab na’alayhifal-Yandwur fiy-himaa” Fiq-us-sunnah juzuu 1 uk 32,na muhamad akajibu
“Fa idhaa raa Khabathan,Fal-ya Masahu bii l-ardhhwi,Thumma liyu swalla fiy-himaa” yaani amesema mtume “Kama mmoja wenu amekuja msikitini, basi ageuze miguu yake kuona chini ya soli.akikuta kuna uchafu katika soli basi avifute katika ardhi (yaani aviburuze chini)Kisha aingie msikitini aswali navyo”
Ukweli ni kuwa kwa matendo yetu ya nje hatuwezi kumpendeza Mungu ambaye ni mtakatifu sana (Ebrania 12;14) haki ya mtu mbele ya Mungu inapatikana kwa imani tu (Galatia 3;11)

Waislamu ni lazima Wajifunze kutoka kwetu.

Quran 6;90. “Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza basi Fuata Uongozi wao”. Allah amewaamuru waislamu na Muhamad afuate uongozi ulio ndani ya injili kwa kuwa humo mna uongozi kwa wacha Mngu wote (quran 5;46), Waislamu ni lazima waisome Biblia kwa umakini na kujifunzaa yaliyomo humu ili siku ya hukumu wasiseme walikuwa hawana Habari ya yale yanayosomwa na Wayahudi na Wakristo (Soma Quran 6;156 soma ufafanuzi yaani Torati na injili).hakuna Mwislamu yeyote mwenye haki ya kumpinga Kristo kwani quran imeelekeza kufata uongozi humo ni lazima tuchukuwe nafasi hii kuwakumbusha waislamu kuwa atakaekuja kuuhukumu ulimwengu wote ni Yesu Kristo kwani ndiye aliyepewa Idhini hiyo hivyo kupingana na Mafundisho yake ni sawa na kubishana na Jaji (Quran 43;61-62, 78;38, Matendo 17;31).Muhamad mwenyewe aliwaonya waislamu na kuwakemea Kuwa mtakuwa katika hali gani(waislamu)atakapoteremka mwana wa Maryam na kuwa Mtawala au kiongozi Miongoni Mwenu?(sahih-al-Muslim IV,Kitab-al-Swifat-hadith 72 uk.2169)
Jambo la mwisho ni kuwa kila mtu na amuabudu Mungu wake vile anavyojisikia Mungu ni Baba wa wote na ana watoto tofauti wa tamaduni tofauti na aliyafanya yote kwa utukufu wake, yeye anapendezwa na kila mtoto wake anavyomuabudu kama alivyo hatupaswi kuhukumiana nani ana ibada sahii kuliko mwingine ibada sahii ni Mungu kuukubali moyo wako kama alivyokubali wa Habil na kukataa wa Kaini ingawa wote walikuwa wakiabudu ni wazi kuwa ibada ni mkao wa moyo na sio mtindo gani unautumia katika kuabudu


Ninapotaka kuzungumzia swala la uwasilishaji ibada nataka nikuonyeshe kwanza stori ya mtumishi mmoja wa Mungu ambaye alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa yaan Birthday mtumishi huyu alikuwa na watoto wanne wote walikuja kumpongeza baba yao na kumpa zawadi wa kwanza ambaye alikuwa na miaka 26 wa kike, alimpa zawadi ya Fedha baba yake kwa ajili ya kutembea kokote atakako kisha akambusu baba yake na kumwangalia kwa upendo, wa pili ambaye alikuwa na miaka 23 wa kike Yeye alichora picha nzuri sana na alimkabidhi baba yake kisha akambusu na kumkumbatia na kumnong’oneza kwa sauti ndogo nakupenda baba, kisha mtoto wa tatu mwenye miaka 21 wa kiume yeye alileta shati zuri kisha akamvalisha baba yake mabegani na kumwambia wewe ni baba wa pekee duniani na wa mwisho mwenye miaka 16 wa kiume alimpa baba yake saa aliyokuwa amenunua safarini na kisha akamwambia Baba yake najivunia kuwa na baba kama wewe bila shaka utaipenda zawadi hii. Unajifunza nini katika mfano huu? Kila mtoto anayo namna yake ya kuonyesha upendo na shukurani kwa baba yake na kama ambavyo kila zawadi ilikuwa tofauti hali kadhalika namna walivyoonyesha upendo na maneno waliyoyatoa yalikuwa tofauti je unafikiri kuna aliyempendeza baba yake zaidi kuliko mwingine? Bila shaka hapana wote walimpendeza hivyo ndivyo Mungu anavyopendezwa na kila mtu anayeonyesha upendo wake kwake na kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa kila ibada kama imeelekezwa kwa Mungu katika hali ya kumpenda basi hata kama ni tofauti na ile uliyoizoea Mungu anapendezwa nayo Hata hivyo Kibiblia Lazima kila Ibada Ipitie kwa Yesu Kristo tu
Maana Msingi mwingine hakuna mtu anayeweza kuuweka, isipokuwa uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo. Wako mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Mkombozi Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni