Jumatatu, 17 Novemba 2014

Ujumbe: Tatizo La Yule Mwana Mkubwa!

Katika Luka 15: 11- 24,25-32.


KWA NINI YESU ALIFUNDISHA KWA MIFANO.


Ziko sababu kadhaa zilizopelekea Yesu kufundisha kwa mifano hii ni njia nzuri na kubwa aliyoitumia Mungu na Manabii na pia marabi lakini kwa Yesu kulikuwa na sababu kadhaa zilizopelekea kunena kwa mifano

1.       Alitumia mifano ili kukwepa mitego ya watu waliomwendea ili kumnasa kwa Maneno Marko 12;1-12.

2.       Alimtumia mifano ili kutofautisha watu walioitafuta kweli na waliofuata miujiza na mikate na pia kama hukumu kwa watu wenye mioyo migumu, Mathayo 13;10-17

3.       Alitumia mifano ili kukwepa au kuufikisha ukweli kwa waalimu wa torati waliofuatilia mafundisho yake (Mfano wanafunzi wa vyuo vya Biblia)

4.       Kupunguza ukali wa ujumbe ili kukwepa kupigwa mawe au kuuawa kabla ya wakati 2Samuel 12;1-6. Mungu huwapa Hekima Manabii wake namna ya kupeleka jumbe bila kupata madhara

5.       Kusaidia watu kuelewa kwa urahisi habari za ufalme wa Mungu


KANUNI YA KUTAFASIRI MIFANO


  Ni muhimu kufahamu kuwa mifano ya kibiblia hubeba maana moja tu na ambayo ndio kweli ya kiroho kwa hivyo ni marufuku kufasiri mstari mmoja mmoja ulio na mfano na kufafanua kwa maana za kiroho hii sio kanuni ya kutafasiri mifano na kwa kufanya hivyo huwezi kupata kweli iliyokusudiwa unapaswa kusoma mfano mzima na kuangalia unabeba nini Principle of Contents kisha uweze kuelezea kile kinachosemwa mfano Kwa mfano wa Msamaria Yesu alikuwa akifundisha Jirani wa kweli ni yupi.

Baba wa Mwenye Upendo akikimbia kumpokea mwanae aliyepotea kwa Furaha kwa vile amerudi Nyumbani

 TATIZO LA MWANA MKUBWA.



Tunaona hasara za mwana mpotevu jinsi alivyofanya mambo mabaya ya kusikitisha na jinsi alivyokosa amani na kurudi kwa Baba yake, na jinsi Baba yake alivyompokea lakini kwa namna ya kushangaza Yule mwana  mkubwa alipokea mambo kwa mtazamo wa tofauti.

Jinsi Mwana huyu mkubwa alivyopokea inatufundisha mambo ya msingi yafuatayo (Luka 15: 25- 32)



I.  ALIKUWA NI MTU WA KUJIHESABIA HAKI ( 29-30)


Huyu mwana  mkubwa alikuwa na tatizo kubwa sana lililohitaji msaada wa Mungu, Alikasirika alisusia, na alijiona kuwa ni mwema kuliko ndugu yake na kuwa yeye pekee ndiye mwenye haki ya kufanyiwa sherehe kuliko mwingine na  kuhukumu, hii ni tabia ya  Kifarisayo ambayo Mungu anapiga vita, ( Luka 18: 9- 14) Utoaji na  Baraka za  Mungu haziko katika wema au ubaya wa mtu ( Math 5: 45) Baraka za Mungu ziko kama  Mungu anavyoamua kwa yeye anayetaka kumrehemu  humrejeza ( Warumi 9: 11-16) Mungu angekuwaanabariki kwa matendo ya haki basi Yakobo  hangebarikiwa  kwani alikuwa mwenye  hila na muongo, lakini alibarikiwa kwa rehema za Mungu tu. Ni ukarimu na rehema za Yule baba aliamua afanye hivyo kwa mwana mpotevu ndugu mkubwa – Alijifanya ni  mtii zaidi kwa babaye, Alimhukumu nduguye.



II.  ALIKUWA HANA UPENDO BALI  CHUKI.(28- 30)


Mwana mkubwa alikuwa na tatizo la ubinafsi na chuki, mafundisho ya kristo  kupita  mitume  wake  yanpingana sana na tabia ya chuki yakitaka  tuwe na upendo,  watoto halisi  wa  Mungu wanajulikana kwa tabia ya upendo kwa wanzao.

(1 Yohana 3: 10- 12, 4: 20)


III.  ALIKUWA MTU WA KUTAFUTA MAKOSA (25- 38)


Huyu ndugu mkubwa anaonekana kuwa na tabia ya  mafarisayo, tabia ya kuhukumu au kuona kosa la Mwingine hii nayo ni tabia ambayo Yesu alikemea hadharani. (Luka 6: 41-42) Ndugu yake mkubwa alipaswa kwanza kushughulikia tatizo lake la ndani kabla ya kutoa shutuma na lawama  kwa mwenzie, yeye alihukumu na aliona kuwa hata baba yake  wa mbinguni ana  kosa.


IV. HAKURIDHIKA; ALIKUWA NA CHOYO NA ALIKOSA FURAHA. ( 31-32)


Mwana huyu mkubwa alikuwa na vyote, na  katika uaminifu wake ; angeweza kufanya karamu aifanyayo na rafiki zake na hangezuiwa, kwa kweli hakuridhika na  alihukumu  huruma ya baba yake kwa wengine, dhidi ya yote alikuwa na  choyo na  alitaka yeye awe yeye tu, choyo ilimkosesha  furaha,  babae alimtaka afurahi tu, Mungu anapobariki anataka tufurahi anapobariki wengine pia.

Mifano ya Yesu pia ilikuwa inatoa mwanga namna Mungu atakavyo hukumu kwa haki wale wanaojikinai na kufikiri kuwa ni wema na wamestahili kuliko wengine watakataliwa katika Ufalme wa Mungu uwe mwangalifu

Somo Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni