Jumapili, 31 Januari 2016

AKAOMBA AACHIWE MKEWE KWA MAGOTI!



Kisanga hiki hakikunikuta mimi  lakini niliguswa sana na jamaa mmoja ambeye alifehdeheka kupita kawaida, sikuwa namjua jamaa huyu lakini nilimfahamu  kwenye ofisi moja, huyu jamaa alikuwa amefika hapo ofisini  kwa shughuli zake na mwenye ofisi, nilipochungulia na kumwona mgeni huyo nilitaka kurudi  nyuma  yaani kuacha  kuingia ofisini. Lakini mwenye ofisi aliniita na kuniambia niingie tu kama vile hawakuwa na jambo la siri na Yule mgeni wake.

Niliingia na kuwasalimia wote, mwenye ofisi na Yule mgeni. Kabla sijaanza kuzungumza chochote Yule mgeni alianza kuzungumza kuhusu jambo ambalo nadhani walishaanza kuzungumza na Yule jamaa yangu yaani mwenye ofisi
 
Mapeniz ni Darasa kubwa sana Duniani!


“Kama hivyo nilivyokuambia naomba sana unilindie ndoa yangu tafadhali naomba sana , Najua una hela na mke wangu anakupenda lakini ona huruma basi nionee huruma “ alisema Yule mgeni kwa sauti ambayo haikuwa ya mzaha  hata kidogo, Yule mwenyeji wangu yaani mwenye ofisi aliingilia kati na kusema “ sikiliza wee mtu, mimi natembea na mkeo lakini siyo kosa langu Nataka nikuambie ukweli kwamba sikuwahi kumtongoza bali mwenyewe ndiye alinianza na hata jana nimemwambia aachane na mimi lakini haelewi, sijui nimempa kitu gani kimemnogea Yule mtoto’ alisema na kucheka kidogo, 

Awali nilidhani ni mzaha wanafanya au labda kuna watu wanawaiga, lakini baadaye nikajua kuwa haukuwa mzaha nilipomuona Yule mgeni akiwa anatokwa na machozi. Niliogoipa sana baada ya kubaini kwamba ule haukuwa mzaha ni ukweli halisi, najua hata wewe itakuwa ni vigumu kwako kuamini jambo hili lakini nakuomba uamini.

Ati ndugu yangu mke wa mtu anakufuata anakung’ang’ania ufanye naye mapenzi wewe kama rijali utafanya nini? Yule mwenyeji wangu aliniuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa rahisi kwangu. Lakini nisingeweza kulitoa. Nilitaka kumjibu kwamba ni kweli hata mama yako akikuambia ufanye naye mapenzi na kukung’ang’aniza inabidi ufanye kwa sababu anataka? Badala yake nilimwambia kama hujui kuwa ameolewa na yuko salama  unaweza kukubali Yule jamaa yangu alicheka  na kusema umemwona mke wa huyu jamaa bwana au unasema tu huyu jamaa ana mke sio wa kawaida  aisee ni mzuri sana . Nilijitahidi kukataa mwanzoni lakini nikashindwa, alisema akiwa hana wasiwasi, Yule mgeni aliporomoka kutoka kitini na kupiga magoti mbele ya meza ya yule mwenyeji wetu “Tafadhali bwana mkubwa niachie ndoa yangu mke wangu akiondoka si nimekuambia nitaona maisha hayana maana, kama mnafanya fanyeni lakini usiwe unamchukua usiku anawaacha watoto…’

Yule mwenyeji alimkatisha yuile jamaa ambaye kitendo chake cha kupiga magotio kwa mtu anayetembea na mkewe aliniingiza kwenye fedheha kubwa ajabu, nataka nikuambie kuwa nilijisikia kama nimevuliwa nguo na nina tembezwa mitaani, Nilikuwa natetemeka kidogo nilimuuliza Yule jamaa yangu hivi ni siriasi kweli au mnafanya mzaha? Yule jamaa yangu alisema nashangaa sana yaani mambo ya mapenzi yanakuja ofisini je mke wangu akitokea hapa sasa hivi akauliza sababu ya wewe kupiga magoti utasemaje? Yule mwenyeji alimuuliza mpiga magoti

Mpiga magoti aliinuka na kusema basi naomba uniachie mke wangu, halafu alinigeukia mimi na kuniambia braza mwambie ndugu yako namwomba sana aniachie ndoa yangu…’Ilibidi kwa kweli nisimame na kumuaga jamaa yangu kwa kumwambia nitapita baada ya dakika kumi malizaneni kwanza…’ jamaa yangu alitaka kunizuia nisiondoke Lakini kabla hajasema neno nilikuwa nimeshafika nje na kuondoka nani anataka kuona upuuzi kama huo duniani? Ambaye ni mstaarabu? Kwa ujumla niliumia sana sio siri najua utataka kujua walimalizana vipi na Yule jamaa mimi sio mbeya je angekuwa ndio mkeo? We ungefanyaje? Yesu alisema llolote usiotaka kufanyiwa na watu usiwafanyie na wewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni