Jumapili, 31 Januari 2016

BABU AKAOMBA NIBEBE!



Ilikuwa ni mwaka 2002 nilipokuwa bado niko nyumbani Moshi, nikiwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha  sita  wakati ule nilikuwa na kiburi na nyodo sana kwa kweli katika hangaika yangu nilikutana na  binti mmoja ambaye alikuwa mlokole, ili nimpate ilibidi na mimi nijifanye mlokole, kwa hiyo tukawa karibu sana na hata familia yake ikanifahamu  na kuniamini nikawa nahesabiwa kama kaka wa kiroho kwenye familia ile , hata hivyo mimi na yule binti tulisha zungumza kuwa hatimaye kuna siku tutakuja kuwa mwili mmoja, kwa hiyo nilikuwa naenda mara kwa mara na nikazoeleka pale, nilijua kuwa kwa ushawishi Fulani wa kimjini ni ngempata binti yule kwahiyo nikawa nikawa najitahidi kwenda kila wiki  kwao  na kumtoa out hata kwenda Cofee house kupata kahawa 


Siku hiyo ilikuwa jumamosi  niliamua kwenda kwao, mimi kwetu ni karibu na YMCA au tuseme majengo, nilikuwa naenda kwao hbuyu binti mara nyingi kwa miguu , walikuwa wakiishi bendeni mtaa wa Swahili, kwa wale wanaopajua moshi ni karibu na Brewries ni mbali kidogo kwa wale wa Dar ni sawa na kutoka ubungo hadi manzese, nilipenda kutembea kama sehemu ya mazoezi. Waklati nikiwa maeneo ya soko kuu nilimpitia Babu Fulani akiwa na mkba wake wa plastiki ngumu, Nilipompita Yule babu bila ya kusalimia aliniita na kunisalimia Kijana hujambo? Nilimwambia sijambo bila shikamoo, aliniomba kama naweza kumsaidia kamzigo kake kwani hakuwa akienda mbali, lakini alikuwa amechoka,nilimtazama  Yule babu na mwisho nilimwambia kwa kunionaje kwamba nimefanana na kuli au kitu gani, hunijui unanivaatu nikusaidie mkoba Je kama umeweka bangi humo ndani na uchawi…’ Niligeuka na kuendelea na safari yangu, Nilifika kwa rafiki yangu na kupokelewa vizuri  kama kawaida, wakati naletewa soda nikaona watoto wanakimbia kuelekea  nje halafu nikasikia babu, babu, babu!, sikujali, Yule rafiki yangu alisema babu naye mbishi alisema atakuja mwenyewe na kweli kaja  ametokea hapo Mwanga, mimi nilisema ni mzee shapu labda . Wakati namalizia kuzungumza yuele babu aliingia, akiwa amesindikizwa na wajukuu  wakionyesha furaha kubwa, inaonekana ni babu anayependwa sana ,halafu Yule rafiki yangu alienda na kumkumbatia, kabla hajamwambia akeye kitini, kweli wewe kijana yaani umefika mwenyewe siamini Yule rafiki yangu alisema. Halafu alinitambulisha kwa babu yake, Wakati huo nilikuwa kama nimepigwa na radi, nimeganda, alikuwa ni Yule babu niliyekataa kumpokea mkoba, Babu huyu ni rafiki ni kijana safi tunatarajia kuwa tutakuwa mwili mmoja, kabla hajamaliza utambulisho babu aliangua kicheko kikubwa sana Halafu alisema kwa kipare “Kweri wathia uo eput lila ijani” mimi nilisomea shule moja inaitwa suji huko juu mlimani upareni kwa hiyo kipare nakijua.

Huyu babu alinikumbuka na alikuwa anamwambia mjukuu wake kwamba amekwisha kwani ninavuta bangi, ni kweli nilikuwa navuta wakati ule, kusikia hivyo watu wote sebuleni walikaa kimya, kwanza walidhani ni utani, lakini baadaye ikaonekana  ni suala la dhati, Halafu babu alianza kuelezea kile kisa changu tena safari hii kwa Kiswahili

Nilijikuta nasimama na kutoka nje, Nilianza kuondoka kwa hatua ndefu, huku nyuma nilisikia maneno ya laana ya kidini yakirushwa kunielekea sikujali mwanaume ingawa ndo nilikuwa naaibika kwa kweli ilikuwa soo mbaya, je unataka kujua nini kiliendelea? Najua unapenda umbeya sana hata hivyo sikuonana tena na binti Yule wala sina haja ya kukutana naye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni