Jumapili, 31 Januari 2016

WIGI HILO LIKAPOTEA!



Ilikuwa ni mwaka juzi nilipopata kijana ambaye niliamini ndiye aliyenipenda, nilikutana naye siku moja katika harusi ya mtoto wa shangazi yangu, tukazoeana polepole tukajikuta tukiwa karibu zaidiHatimaye siku moja aliniomba kama niko tayari kwenda naye kupata chakula cha jioni. Nilikubali kwa haraka kwani nilijua anakwenda kunitamkia neno la upendo, nilishaamua kwamba ningekubaliana naye, Nilikuwa nampenda na nilijua kuwa naye ananipenda.

Maisha ni kujikubali! jeje wewe unategemea nini kukamilisha utu wako, Uasilia huwapendeza wengi


Tulikubaliana kukutana kwenye mgahawa fulani ambao uko maeneo ya kariakoo. Siku hiyo nilitoka kwelikweli, kawaida yangu mimi huwa navaa wigi, siyo kwa urembo bali kwa sababu ya ajali, nikiwa sekondari nilipata ajali ya moto na kuungua kichwani, kwahiyo sehemu kubwa ya kichwa changu hakioti nyelwe kwa hiyo sijaacha kuvaa wigi, nilikuwa nimejitahidi kwa kweli  kwani mawigi niliyokuwa navaa ni yale ya bei mbaya , siku hiyo tuliyokutana nilikuwa na wigi babu kubwa , tulifurahia sana kukutana kwetu , kwani ilikuwa mara ya kwanza kukutana kwa faragha,tulianza mazungumzo yetu huku tukila na Yule jamaa alikua anaelekea kuniambia kuwa ananipenda, lakini kabla ya kufanya hivyo niliomba radhi na kuinuka kwenda maliwatoni, kufika huko niligundua kuwa wigi langu halikuwa halijakaa vizuri,nililivua na kuliweka juu karibu na dirisha ili ninawe na kurekebisha nywele zangu chache kabla sijalivaa tena , lakini nataka kulichukua wigi mshituko ambao  nilikuwa sijawahi kuupata maishani  mwangu, wigi lilikuwa halipo, nilihangaika kulitafuta nikidhani limeanguka mle ndani lakini niligundua kuwa lilikuwa limeanguka nje au kuchukuliwa, kwani pale dirishani  dirisha lenyewe lilikuwa linaelekea mtaani nilibaki mle maliwatoni nikijiuliza ni nini cha kukifanya, ningetoka vipi nje na kwenda kwa Yule kijana  na kichwa cha kipara? Hatimaye niliamua kutoka sikuwa na njia isipokuwa kutoka. nilitoka na kwenda mezani, nilipokaa huku nikitabasamu Yule kijana aliniangalia kwa hasira, na kusema pana mtu hapo, nilijua kuwa alikuwa amenisahau Nilimwambia ni mimi wig…wig… langu limedondoka, nilisema nikiwa natetemeka, Yule kijana alionyesha mshangao ambao sijawahi kuuona tena kwenye maisha, hakujibu bali alimwita muhudumu na na kuomba bili, Alilipa na kuinuka na bila kusema neno, aliinuka hakunisemesha. 

Alipolipa aliondoka bila kusema neno, Sikumlaumu lakini nilikuwa katika maumivu makali ajabu nikajitia moyuo kuwa kumbe hakuwa ananipenda aliogopa nini kipara changu? Niulikaa hapo mezani na kufuta machozi, wateja wa meza ya jirani walikuwa wakinitazama na kunikodolea mimacho yao machozi yalizidi kunitiririka nilisimama na kutoka nje nilichukua teksi kurudi nyumbani kwa kweli ilikuwa siku yangu mbaya sana we cheka tu utakuja kupatikana nawewe muone misikio kwa taarifa yako sasa nimeolewa  mwaka jana tu  na mwanaume mwenye kujua kupenda  hakujali kipara changu wala nini  alinipenda kama nilivyo lakini siku ile sitaisahahu hasha!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni