Ujumbe: Chapa za Yesu
Wagalatia 6:17 “
Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake
Yesu”
Leo nataka
tutafakari kwa pamoja mstari huu muhimu sana katika maisha yetu ya utumishi
pamoja na kumfuata Yesu, yaani ukristo ni swala la kuchukua chapa za Yesu nini
maana yake? Kuchukua chapa za Yesu?
Biblia ya
kiingereza ya NIV inasomeka hivi “Finally, let no one cause me trouble, for I
bear on my body the marks of Jesus”
Biblia ya
kiingereza ya New Anerican Standard Bible inatafasiri msatri huo namna hii
we are arrested
by the words “ I bear on my body the brand-marks of Jesus” neon hilo Brand ni
kama “label” na Marks ni “alama” au
chapa maana yake hii ni alama ya kudumu katika mwili wa mnyama au mwanadamu
aliye mtumwa
Nyakati za
Biblia mtu alipokuwa na wanyama aliwaweka alama kwa kupasha chuma chenye moto
na kumbadika mnyama huyo ili kuonyesha kuwa ni wake, swala hili pia lilifanywa
kwa watumwa, mtu aliponunua watumwa na kuwamiliki watumwa pia waliwekwa alma
kwa chuma cha moto katika mwili wao na kovu la kudumu lingebaki mwilini mwa
mtumwa huyo kuonyesha uhalali wa kumilikiwa watumwa hao waliitwa Doulos kwa
lugha ya kiyunani, hakuwa na uwezo wa kutoroka na anemtumikia bwana wake milele
hata kufa
Paulo
anazungumzia maisha ya kujitoa kwa Yesu moja kwa moja ya kuwa kila anayeamua
kuwa mkristo hapaswa kuingiza mguu nusunusu kila mtu anayemtumikia Yesu
anapaswa kutambua kuwa
1.
Yeye ni mtumwa ni lazima akubali kuwekwa alama
na Yesu ya kuwa yeye ni bwana na kuwa ni lazima kumtumikia hata kufa 1Wakoritho
6:19-20 na Warumi 1:1
2.
Kila anayeamua kumfuata Kristo ni lazima akubali
kuwa amekubali kujiandikisha jeshi yeye ni askari na yuko tayari kutumika
akikabiliana na mazingira magumu 2Timotheo 2:3, 2Wakoritho 5:15
3.
Kila anayeamua kufuata Yesu ni lazima ajitoe
kumuabudu Wafilipi 1:20, 2Wakoritho 4:5
Hakika tumepigwa chapa zake Yesu Kristo
JibuFuta