Jumanne, 26 Januari 2016

UJUMBE : MWENYEZI MUNGU ANAPOTUTENDA MAMBO MACHUNGU SANA!


Ruthu 1 : 19-22
Biblia inasema hivi:-
“19. Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20. Akawaambia, Msiniite Naomi niiteni Mara,kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.21. Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
     Nyakati za Biblia hususani nyakati za agano la kale watu wengi sana walipopatwa na mabaya walifikiri kuwa mabaya hayo yanatoka kwa Mungu, ni muhimu kufahamu kuwa mambo mabaya na machungu sana hutoka kwa Yule Muovu, lakini hata hivyo wakati mwingine ni kwa ruhusa ya Mungu, Mungu huweza kuruhusu mabaya yatupate kwaajli ya utukufu wake, na katika nyakati nyingine Mungu katika hekima yake huweza kuyatumia mambo mabaya ili kutuletea mambo mema!
Katika Mistari ile tuliyoisoma Ruthu 1:19-22 tumesoma habari za mwanamke aliyeitwa Naomi (mwenye kupendeza ndio maana ya Jina lake) akirudi Bethelehem na mkwewe wakiwa katika hali ngumu sana na wimbi la umasikini na kufilisika huku kila mmoja akiwa hajui maisha yake yatakuwaje mbeleni (No feature), Matumaini yake yote aliyokuwanayo yalitoweka, alikuwa na uchungu uliokuwa umemzunguka na ni uchungu wa mauti tu na hakukuwana tumaini la uhai, jumla ya mawazo yake ni kuwa Mwenyezi Mungu amemtenda mambo machungu sana
Ruthu 1-13 aliona ni kama mkono wa Bwana umeondoka juu yake ni kama vile Mungu hashughuliki naye tena
Alikuwa na Mume aliyeitwa Elimeleki Maana yake Mungu ndiye Mfalme au Mtawala
Alikuwa na mtoto wa kiume mkubwa aliyeitwa Maloni maana yake Magonjwa
Na wa kiume mdogo aliyeitwa Kilioni maana yake Kufilisika

Historia ya Familia hii inaonekana kama waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha yao kwa vile walikimbia njaa katika nchi ya Israel huko Bethelehem na kuelekea nchi ya Moabu Jordani ya leo kwaajili ya chakula lakini  familia hii ilikutana na wakati mgumu kwani ni wazi kuwa wakati Maloni anazaliwa ilikumbwa na magonjwa mazito na labda ndio maana  walimpa mtoto wao jina hilo na huenda walipokuwa huko moabu walifilisika kabisa na ndio maana walimuita mtoto wa pili kilioni yaani kufilisika na kama haitoshi ingawa kilioni na maloni walioa mara Baba yao alifariki, kisha Maloni na kisha kilioni bila kuacha watoto, na Naomi alijikuta maebaki na wakwe vijana Orpa na Ruthu, katika hali ya mashaka makubwa Naomi aliwasihi wakweze kurejea makwao katika hali ya ukwasi mkubwa Orpa alikubali huyu alikuwa mke wa Maloni na Ruthu alikazia kubakia na mkwewe huyu alikuwa mke wa kilioni
Hali ya Naomi ilikuwa ni ya kusikitisha nay a majonzi mno hakutamani tena kuitwa Naomi bali mara yaani machungu, mkwewe alifuatana naye katika hali hiyo ya umauti na kukosekana kwa matumaini, kazi kubwa aliyofanya ni kuokota ngano na masazo yaliyosazwa na waliovuna Ngono huko Bethelehemu
Mkwe wa naombi Ruthu aliyekuwa mwaminifu na kuendelea kumtunza mkwewe hatakatika hali ya umasikini na shida alipata mchumba na kuolewa sawa na desturi zao na Mchumba huyu aliitwa Boazi na baada ya kumuoa Ruthu walipata mtoto wa kiume na Kumuita Obedi yaani Kurejezewa Uhai! Huyu Obedi alimzaa Yese na Yese alimzaa Mfalme Daudi

Msomaji wangu mpendwa Mungu huweza kuruhusu mambo machungu yatupate, na wakati mwingine tukafikiri kuwa umefika mwisho wetu, hatuwezi kuinuka tena hata maadui zetu na wale wasiotutakia mema wanaweza kufikiri kuwa mwisho wetu umefika, lakini ninazo habari njema kwako leo kuwa Mungu amerejeza Uhai, haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia Mungu yuko Nyuma ya mambo ili kusababisha mambo mema yatokee Na  ndio maana njia zake hazichunguziki wala mawazo yake si kama  ya wanadamu njia zake ziko juu sana na hekima yake kwa wanadamu ni ujinda Lakini upumbavu wa Mungu una hekima kuliko Hekima ya wanadamu Hatupaswi kumlaumu Mungu kwa lolote tunalolipitia au linalotutokea, Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo

Na Rev. Innocent Kamote Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni