Apologetics ni nini?
Apologetics ni tawi la Theolojia
linalohusiana na elimu ya Utetezi wa imani ya kweli ya Kikristo, ni neno
linaltokana na asili ya kiyunani Apologia
ambalo maana yake ni kulinda au kutetea au kujitetea ni neno lenye asili ya
kimahakama sawa na utetezi unaotolewa mahakamani katika misingi ya Kisheria,
kwa msingi huo Mteteaji huitwa Apologist jina ambalo lilitolewa kwa waandishi
wa Karne chache za mwanzoni baada ya Kristo waliojitetea mbele ya Mtawala wa
Kirumi na jamii kuonyesha kuwa Ukristo ni Falsafa na Maadili yaliyo juu zaidi
ya Upagani ambao kwa asili ulikuwa ukiabudu asili wanautetezi wa Mwanzoni
kabisa ni kama Aristides, Anthenagoras, Saint Justin Martyr, Minucius Felix, Tatian
na Tertullian.
Ø
Tangu mwanzoni
kabisa mwa Karne ya Kwanza Kanisa
lilipatwa na tishio la kuweko kwa Imani potofu
Ø
Jibu kubwa la kanisa
lilikuwa ni kujibu hoja hizo kwa kuleta fundisho sahii na kushambulia fundisho
lisilo sahii jambo hili ndio linaitwa Apologetics
Ø
Yuda anazungumza
swala hilo la utetezi wa Imani katika Yuda 1;3 “Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii kuwaandikia habari
ya Wokovu ambao ni wetu sisi sote
naliona imenilazimu kuwaandikia ili niwaonye kwamba muishindanie
Imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”
Kwa kiingereza cha
kisasa inafikiriwa kuwa neno Apology
ni kuthibitisha ukweli pia inamaana ya kuitetea sheria au mtu ni utetezi wa
Imani ya Kikristo au kanuni za kuitetea imani ya Kikristo ni taaluma inayohusu
kupinga mawazo au imani hususani zilizo kinyume na Ukristo kwa hoja za Kikristo
zinazokubalika
Ni tawi la Theolojia
ya kikristo linalojihusisha na kuuthibitisha ukweli wa Imani ya Kikristo.
Tofauti ya Apologetics na Polemics.
Polemics ni neno la
Kiyunani lenye maana ya Vita au shambulizi dhidi mawazo ya mtu mwingine maana
nyingine ni pamoja na utetezi wa Imani dhidi ya upinzani kutoka ndani ya Kanisa
Wakati Apologetics ni utetezi wa Imani ya Kikristo dhidi ya upinzanikutoka nje
ya kanisa
Ufahamu kuhusu Maana
ya Maneno mbalimbali yatumikayo kwenye somo hili.
Uzushi (Heresy) – Ni Mawazo yasiyo sahii au
yasiyozingatia ukweli wa kimaandiko na ambao unapingana na misingi ya imani na
amafundisho ya Kikristo
Nyakati za kanisa la
Kati Medieveal Church Wazushi walikuwa wanatengwa na kanisa au kuuawa hata ingawaje mawazo
yaliyofikiriwa kuwa ni uzushi kwa sasa ni moja ya misingi muhimu ya Imani kwa
mfano Fundisho la Kuhesabiwa haki kwa Imani Justification by Faith ambalo ni
fundisho linaloaminiwa na makanisa jamii ya kiprotestant.
Dini za uongo (Cults) – Neno Cults limetokana na Neno
Cultus ambalo kwaasili maana yake ni ibada za uongo au ibada katika vitu
visivyo halisi kwa mfano kuabudu jua n.k. Dini za uongo pia inaweza kuwa imani
ya Kikristo na ambao wanakiri kuwa ni Wakristo lakini katika mafundisho yao
kuna Imani za Uzushi ingawa kwa nje wanaweza kuonekana kubeba alama za Kikristo
Linaweza kuwa kundi la watu wakristo lakini wanaoamini Mafundisho yanayotokana
na Tafasiri za mtu Fulani na kusababisha
kumeguka au kuondoka katika mafundisho ya Msingi.
-
Cult ni mfumo wa
kidini au imani ya Kiroho ambayo haiku sawa na misingi ya kweli ya imani , au
watu waliokengeuka au imani potofu ambayo inafuata mafundisho ya mtu Fulani
-
Ni kundi la dini au
watu wanaoshiriki imani Fulani za kiroho ambayo ni wazi kwa wengine kuwa ni
potofu
-
Ni kundi la watu
wenye Imani iliyopituka Extremist ambayo ina mlengo wa kumuamini mtu au kufuata
falsafa za mtu Fulani mtindo wa maisha na tabia pia inaweza kuwa ibada ya
sanamu au mashetani ibada za kichawi pia zaweza kuitwa Cults.
Dhehebu la uongo (Sect) – Kwa ujumla kuna tofauti ndogo
na Cults lakini sect ni dhehebu na
linakuwa kubwa kuliko Cults na linawezxa kuwa na miaka mingi lakini wao huziona imani kama za kipentekoste
kuwa kama madhehebu ya uongo mfano wa Sect ni kama SDA. (Wasabato).
Orthodox – Ni neno la
Kiyunani lenye maana ya wazo lililonyooka ni Imani ya asili na mafundisho ya
kweli ya Dini mfano ni Wayahudi wenye imani kali Orthodox Judaism.
Dogma – Ni mafundisho ya
Imani au Usemi wa kimaadili uliowekwa katika utaratibu maalumu ambao umetamkwa na kanisa au kundi Fulani
wakiamini kuwa ndio mafundisho yao ya Imani
- Ni utaratibu wa mafundisho ya Imani uliokusanywa naDini au
dhehebu Fulani wakiamini kuwa ndio kweli zao kuu. Mfano ni Imani ya Nikea au
mitume N.K.
- Ni itikadi au Falsafa au maadili au sera za kisiasa au
kundi la kidini zinazoaminika kuwa kweli.
Kwa mfano Mwaka 1850 ilitangazwa na Pope wa wakati huo kuwa
Mariamu alizaliwa pasipokuwa na dhambi kwa msingi huo hiyo imekuwa Dogma kwa
wakatoliki.
Kazi za Apologetics.
§
Nyakati za Karne ya
Pili kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa ni kuutetea na kuulinda Ukristo na kuondoa
madai
§
Kazi kubwa ya
apologetic ilikuja kupata nguvu baada ya miaka kadhaa iliyofuata
§
Jukumu la
kiapologetic kwa mfano lilidhihirishwa na Mtakatifu Agustino kwa kudhihirisha
kuwa kazi ya kuutetea Ukristo haikuwa tu kwaajili ya kushughulika na Madai bali
ni zaidi ya hapo
§
Dr. Ramm aliidhinisha
wazi kabisa kwa kuonyesha kuwa Apologetic ina kazi kuu tatu
-
Kuonyesha Imani ya
Ukristo jinsi ilivyo ya Kweli na kuwa imani nyinginezo nje ya Ukristo ni kama
Hadithi
-
Kuonyesha Nguvu ya
Ukristo katika tafasiri sahii za maandiko
-
Kukanusha fundisho
lolote ambalo liko kinyume na Ukristo
Matawi makuu ya Apologetic.
Tunaweza kuligawa
shamba la Utetezi katika maeneo makuu mawili
a.
Utetezi wa Kifalsafa
(Philosophical Apologetics) – hii ni
hali ya kuwasilisha mtazamo wa Kikristo kwa kutumia mawazo ya msingi na yaliyo
sahii ni sawa na kuonyesha uungwana wa Kikristo
b.
Utetezi wa kihistoria
(Historical Apologetics) – Hii kazi
yake kubwa ni kutoa Ushahidi kwa
kuonyesha jinsi Ukristo ulivyokumba na Vikwazo mbalimbali na jinsi walivyoweza
kujibizana navyo na kukabiliana navyo na kuwa matokeo yake yalikuwa nini
Katika somo letu hili tutakuwa tukiangalia kwa upana kuhusu
tawi lile la kwanza la utetezi wa Kifalsafa
Kazi kubwa ya Apologetic Elimu ya
Utetezi.
Ni muhimu kufahamu
kuwa kazi kubwa ya elimu ya utetezi sio kupinga tu bali ni pamoja na kujenga, kutoa
msaada, kutoa ujasiri na kupinga mawazo ya kuchukuliana na ybatili na
kuwasaidia wakristo katika swala zima la kuitetea imani yao.
Kwa hiyo kazi ya
utetezi sio kupinga tu ni kuwasilisha mawazo sahii kuhusu Kristo, kuilinda
imani kutoka katika ujinga, kutokueleweka,na mashambulizi ambayo yanaweza
kuharibu imani yetu
Kwa
msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa Elimu ya utetezi katika Ukristo kamwe haitii
moyo swala la Kumashjambulia mtu bali ni kushugfhulika na Mawazo au mafundisho
yasiyo sahii ndani ya mtu Waebrania 3;12 Biblia inasema
“Ndugu zangu, angalieni,
asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu
aliye hai.”
Kama watu wa ulimwengu watakuwa ni wenye kutafuta ukweli
Apologetic itakuwa hainakazi kwao lakini wanapoupinga Ukristo na kuiharibu
imani ni wazi kuwa apologetics itafanya kazi kwao.
CHIMBUKO LA ELIMU YA UTETEZI.
Kwa ujumla chimbuko la elimu ya utetezi linatokana na sababa
kubwa Tatu zifuatazo
1.
Mabadilio makuu matatu katika kanisa.
-
Kanisa katika hatua
za mwanzoni lilikuwa ni kanisa kama shirika lisilo na sheria au kanuni au
makusudi ya kimaadili au kimuuundo
-
Hakukuweko na Muundo
maalumu wa kimaongozo wala wa kitaratibu nabaadaye lilikumbwa na mabadiliko
hususani katika karne ya pili ambapo waamini walianza kufikiri kuhusu ushirika
na kuweka viwango vya kimaadili na mafundisho ya msingi sababu zilizopelekea
mabadiliko hayo ni pamoja na
a. Kufa kwa Mitume wa
Bwana.
Mwishoni
mwa Karne ya kwanza Mitume wote wa Bwana walikuwa wamekwisha kufa wao walikuwa
ni kama Mamlaka ya juu kabisa ya Kanisa na kila kulipotokea tatizo walikuwa
wakitoa suluhisho je nanai atakuwa mwenye mamlaka kama ile?
Je
kanisa lingewezaje kutunza umoja wake wa imani bila kuweko kwa Mitume? Ilikuwa
ni lazima na muhimu jibu lipatikane na zaidi sana Mchanganuo wa majibu ya
Misingi ya Imani ilikuwa lazima Isitawishwe.
b. Mateso dhidi ya
Kanisa.
Wafalme
wengi wa Kirumi makaisari walitaka kuabudiwa wao kama miungu, aidha wayahudi
walianza kuwaona wakristo kama dhehebu lililo kinyume na sheria ya Musa na kuwa
ni imani pinzani au tishio Kanisa lingeweza kukabili vipi dharula hizo
zilizojitokeza ndipo ilipoonekana haja ya kuwepo na Ushirika thabiti pamoja na
sauti kamili ya kimafundisho au mafundisho sahii ambayo ungekuwa ndio msingi wa
Imani ya wakristo wote.
c. Kuweko kwa mafundisho
ya uongo.
Mafundisho
ya Mitume yalikuwa yanakubalika na kuheshimika kama Mamlaka ya mwisho hususani
walipokuwa wakiwa hai, Lakini baada ya wao kufariki waalimu wa uongo wengi
walitokea je ni nani angesimama na kuzungumzia maswala ya imani na misingi ya
mafundisho ya kweli ya kanisa? Hapa ndipo tunapoiona elimu ya utetezi
ikihitajika
Tatizo
lilikuwa kubwa zaidi wakati jamii ya wakristo wa Mataifa walipoamini na kuingia
kanisani kulizuka mawazo tofautifalsafa tofauti na migogoro iliinuka
Na mkuu wa wajenzi mwenye hekima!
Rev. Innocent Kamote
Maoni 3 :
Nashukuru sana nimejifunza kitu hapa kwakweli kuhusu utetezi wa imani ya kikristo kutoka mashambulizi yatokayo nje ya kanisa la kristo.
Mafundisho mazuri sana. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu kwa elimu tunayopata hapa hasa sisi wanafunzi wa theolojia tunapata madini ya kutosha sana. Baba usiache kuchambua kitabu baada ya kitabu tafadhali Askofu. Nimefurahia sana uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo. Ubarikiwe
Ameni Mungu akubariki sana🙏🙏
Chapisha Maoni