SOMO
namba 1; NGUVU YA KUFUNGA
Muhubiri ;Mchungaji
Innocent Kamote
Katika Mathayo 17;14-21 tunajifunza juu ya
nguvu itokanayo na kufunga, Biblia inatufundisha kuwa yako mambi ambayo
hayawezekani kama kuomba hakutaambatanishwa na kufunga ni kwwa sababu hii basi
ni muhimu kwa kila mkristo kuchukua muda
na kutoa kipaumbela na uzito mkubwa sana
katika mfululizo wa masomo haya yahusuyo kufunga na tutajifunza somo hili nguvu ya kufunga kwa
kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-
·
Maana ya kufunga
·
Umuhimu wa kufunga
·
Mifano ya watatkatifu waliokuwa wanafunga
·
Nguvu ya kufunga
Maana ya kufunga
Neno kufunga
limetokana na neno la asili la kiyunani “Nestevo”
ambalo nalo limetokana na muunganiko
wa maneno mawili ya kiyunani “Ne” na
“Esthio”. Neno “Ne”maana yake ni bila au pasipo kwa kiingereza ni “No” au “Without”na Esthio maana yake ni kula chakula au kinywaji kwa
kiingereza “To eat solid or liquid food”Kwa
msingi huo Neno Nestevo sasa linaunganisha maneno hayo mawili ya kiyunani Ne na Esthio na lina maana ya Bila kukla
chakula au kunywa kinywaji chochote kwa msingi huo basi maana kamili ya neno
kufunga ni Bila kula au kunywa chochote. Without eating solid or liquid food
Hiyo ndiyo maana ya kufunga kufunga sio
kuacha kusoma magazeti tuliyoyazoea,au kuacha kuchana nywele n.k ni kuacha
kabisa kula na kunywa maana hii ya kufunga inathibitishwa na maandiko kadhaa
yafuatayo Ezra 10;6,Yona 3;7,2Samuel 3;35,Esta 4;16 Kumbukumbu 9;9 Matendo 9;9
ni muhimu kufahamu pia kuwa kufunga sio kuacha kula aina fulani ya vyakula na
kula aina nyingine ya vyakula kwa mfano
labda mtu aache kula ugali au wali lakini anakunywa maji au kunywa soda,au
maziwa au uji na matunda n.k kufunga maana yake ni kuacha kula chochote, wako
watu wanaofundisha funga ambayo sio ya kibiblia Partial Fasting na hutumia
andiko la Daniel 10;2-3 katika kuhalalisha fundisho hilo katika andiko hili
kuna maneno “Sikula chakula kitamu” chakula kitamu ni Dessert kwa kiingereza au Pudding
yaani ndizi ,nanasi,papai ,machungwa
jamii za matunda n.k Daniel anachokisema hapo ni mkuwa hakula kabisa
chakula chochote ikiwemo na hivyo hakula kabisa na hata kama ingekuwa ndivyo ni
muhimu kufahamu kuwa huwezi kufanya fundisho kupitia mstari mmoja tu kwa kanuni
za matumizi halali ya maandiko hivyo fundisho hilo sio halali
Umuhimu wa kufunga
Mathayo 6;16-18, Yesu
Kristo anamtazamia kila mtu aliyeokoka kuwa na maisha ya kufunga hili liko wazi
kupitia lugha inayotumika katika maandiko
“Tena mfungapo”au “Bali wewe ufungapo”hii maana yake Yesu anamtazamia
kila mtu aliyeokoka kuwa na wakati wa kufunga katika msingi uleule wa wakati
tunapoomba Tena wewe usalipo Mathayo 6;5-6, katika mistari hii tunajifunza kuwa
Mungu huwajazi wale wafungao , maana yake huwapa thawabu au huwapa zawadi au
kuwajazi pale palipopungua kwa msingi huo
Mungu hutuongeza imani inayopungua kwetu tunapofunga ,wanafunzi
hawakuweza kumtoa pepo kwa sababu ya upungufu wa imani yao na wakaelezwa kwamba
hawana budi kufunga na kuomba ili wawe na imani hiyo Mathayo 17;14-21 hivyo
kufunga hutuongezea imani.
Mifano ya watakatifu waliokuwa wanafunga
·
Yesu Kristo
- mara baada ya kujazwa na Roho alifunga siku arobaini baada ya mfungo
alirudi akiwa kwa nguvu za Roho Luka 4;1,14.
·
Musa – Kutoka 34;28
·
Ezra – Ezra 10;6
·
Eliya – 1Falme 19;8
·
Daudi – Zaburi 109; 24
·
Paulo na Barnaba Matendo 14;23
·
Kanisa la kwanza Matendo 13;1-3
Ikiwa watakatifu wengi tunaowaona katika
Biblia walifunga na tunaona jinsi mambo yalivyobadlika baada ya kufunga sisi
nasi hatuwezi kupuuzia kufunga na tukadai kuwa ni wakristo kibiblia, kupuuuzia
kufunga kutatufanya tuwe dhaifu kiimani tukilinganishwa na watakatifu wa zamani
Nguvu ya kufunga
Sehemu nyingi sana katika Biblia
tunaona jinsi ambavyo mambo yalivyobadilika baada ya kufunga na kuomba ,
Mifano mitano ifuatayo inatufundisha juu
ya nguvu ya kufunga
·
Wana wa Israel
walipigwa mfululizo katika vita na wana wa Benjamini na baada ya kupigwa
mfululizo wakaamua kufunga na kuomba
Waamuzi 20;20-22,24-26baada ya kufunga na kuomba matokeo tyalibadilika
,Benjamini wakapigwa sana na wana wa
Israel wakashinda kwa kuiteketeza miji
ya maadui zao kwa moto waamuzi 20;34-35,41-45,48 tunaweza kuitia moto miji yote
ya shetani katika ulimwengu wa kiroho kama tukiwa wafungaji
·
Ezra hakutaka kumtegemea Mfalme na badala yake
walifunga na mkono wa bwana ukawa pamoja
naye nay eye na wenzake wakaokolewa na
mikono ya adui Ezra 8;31-32 ikiwa
tunahitaji kuokolewa katika mikono ya adui kama kanisa ni muhimu kuzingatia
swala la kufunga
·
Yehishafati alipata taarifa za kuwako kwa jeshi
kombainia ya maadui waliotaka kumpiga akatangaza kufunga na kuomba
2nyakati 20;1-4 matokeo yake wakashinda vita kirahisi kwa kuimba sifa tu
2Nyakati 20;22-25
·
Nehemia alivyopata taarifa za kubomolewa kwa
ukuta wa Yerusalem na malango yake
kuteketezwa kwa moto alifunga na kuomba nehemia 1;3-4 na matokeo yake
ukuta ulijengwa tena kwa muujiza mkubwa Nehemia 6;15-16
·
Hasira ya Bwana inapowaka kwaajili ya taifa au
kanisa kutokana na uovu wa watu inaweza kufanywa kuwa amani kwa kufunga na
kuomba 1Falme 21;27-29,Yona 3;7-10,Ezra 10;6
Namna hii
haitoki ila kwa kufunga na kuomba mathayo 17;21
Yesu alifunga siku 40 akiongozwa na Roho Mtakatifu Nyikani
SABABU ZA KUFUNGA somo na 2
Muhubiri ; Mchungaji
Innocent Kamote
Tunaendelea na mfululizo wa
masomo yahusuyo kufunga na sasa au leo tunaingia katika somo la pili
linalozungumzia sababu za kufunga tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele vitatu vifuatavyo;-
·
Kufunga ni mapenzi ya Mungu
·
Kila mtu aliyeokoka anaweza kufunga
·
Sababu za kufunga
Kufunga ni mapenzi ya Mungu
Katika mathayo 6;16-18 tuliona Yesu akitumia neno tena mfungapo na
Bali wewe ufungapo hasemi kama wewe ukipenda kufunga au tena mkipenda kufunga
hii maana yake ni kuwa Yesu anatarajia
kuwa kila mtu aliyeokoka awe na maisha yaliyojawa na kufunga ,kuna wakatui
mungu hufurahia kutuona tumemfungia yeye ,tunapokula na kunywa tunafanya hivyo
kwa ajili ya nafsi zetu na tunapoacha kula na kunywa tunakuwa tumeacha kwa
ajili ya Mungu yaani tunafanya hivyo kwa ajili ya nafsi yake Mungu Zekaria
7;4-6 yako mambo kadhaa ambayo hatuwezi kuyapokea kwa Mungu ikiwa hatumwendei
kwa kufunga Yoel 2;14 kwa nini inakuwa hivyo tutapata majibu ya maswali hayo
tutakapoangalia sababu za kufunga
Kila mtu aliyeokoka naweza kufunga
Mtu yeyote aliyeokoka mwenye afya timamu
anaweza kabisa kufunga, kwa msingi huo hatupaswi kujiona kuwa hatuwezi na
kuruhusu woga, ikiwa wafuatao katika biblia walifunga ni wazi kuwa kila mmoja wetu anaweza kufunga
a.
Ana Bint Fanuel – Huyu alikuwa mjane mwenye umri
wa miaka 84 hata hivyo alikuwa mfungaji mkubwa sana ,ikiwa mzee wa jinsi hii
aliweza kufunga ni muhimu kufahamu kuwa
sisi nasi tunaweza kufunga luka 2;36-37.
b.
Watu ambao hawajaokoka – watu ambao hawajaokoka
waliweza kumsikiliza Yesu akiwafundisha bila kula wala kunywa kwa siku tatu
Mathayo 15;32 ikiwa hawa waliweza bila shaka sisi nasi tunaweza
c.
Ng’ombe na kondoo – wanyama kama ng’ombe na
kondoo waliweza kufunga wakati wa Yona ona katika Yona 3;7 ikiwa hawa waliweza
sisi hatuna udhuru kabisa
Watu wanaoweza kuepuka swala la
kufunga ni wale ambao wana afya mbaya au wajawazito wao sio vema kufunga katika
halui kama hizo na pia ni muhimu kuzingatia kutokuwalazimisha watoto wetu
kufunga bila hiyari yao Ni muhimu kukumbuka kuwa kufunga ni kuacha kula na
kunywa hivyo tunapopiga mswaki na maji
yakaingia kinywani au wakati wa kuoga matone yakakudondokea kinywani bila
kukusudia huko sio kula na kunywa kwa hiyo kufunga kuko palepale Mume na mke
watazingatia kupatana ili kuwa na kiasi katika swala hili 1Koritho 7;5 biblia inasema hivi “Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana
kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena
ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na
kiasi.” Hii ni kwa sababu mmoja wa wanandoa asipokuwa radhi na mfungo
wako hususani Mume ambaye ni kichwa basi mfungo huo unaweza kuwa batili. Ni
muhimu pia kila mfungaji kuzingatia
kumuomba Mungu neema ya kumwezesha kufunga kabla ya kuanza kufanya hivyo
kwa kufanya hivyo Mungu anatupa neema ya kutuwezesha kufanya yale tuliyokuwa
hatuwezi kuyafanya zamani neema hii
itatuwezesha kufunga Yohana 15;5,Wafilipi 4;13,Yohana 1;16-17 Wakolosai 1;10-11
Sababu za kufunga
Kuna sabau kadhaa za kutufanya sisi
kufunga
1. Kutokufunga ni sawa na kuabudu sanamu au
miungu mingine
Biblia inatufundisha kujilinda nafsi zetu
na ibada za sanamu na kuikimbia ibada ya sanamu 1Yohana 5;21,1Koritho 10;14
sanamu katika Biblia ni zaidi ya vinyago vya kuchonga vya miti na fedha
n.k lakini pia ni kitu chochote au jambo
lolote au mtu yeyote ambaye umempa moyo wako
wote , akili zako zote na roho yako yote
na kuruhusu ichukue nafasi ya Mungu kwa msingi huo sanamu inaweza kuwa
Elimu, Mkeo, akili zako,cheo , kazi au kutamani chochote au kukitumikia kuliko Yesu Kristo hiyo ndiyo ibada ya sanamu
Kwa msingi huo kama mtu atakuwa anaendekeza kula basi mungu wake ni tumbo
Wafilipi 3; 17-19 mtu wa namna hii
anawekeza nguvu zake katika maswala ya lishe na fedha na akili kwa ajili ya
kula inasemekana ya kuwa mtu a anayetumia dakika 30 kunywa chai na dakika 45 kwa chakula cha mchana ,dakika
20 chai ya jioni,dakika 45 chakula cha usiku na dakika 40 nyingine katika kunywa soda ,juice,kutafuna karanga au machungwa njiani .n.k mtu wa namna hiyo
muda anaoutumia kula kwa siku ni dakika 180 sawa na masaa matatu hivyo kwa
mwezi mtu huyo anatumia saa 90 au 93 ambazo ni karibu siku nne nzima kwa hiyo kwa mwaka mmoja anatumia siku 48 kula tu kama mtu huyu ataishi miaka 75 atakuwa
ametumia siku 3600 au miaka kumi 10
mchana na usiku kula tu kwa
msingi huo mtu huyo atakuwa anajaribu kuishi kwa mkate tu na analisujudia tumbo
Yesu alisema mtu hataishi kwa mkate tu .
2.
Kufunga
ni kushinda jaribu la kwanza la shetani lililoleta maafa kwa mwanadamu
Adamu wa kwanza alijaribiwa na shetani kwa
chakula Yaani kwa kula lile tunda na akaanguka
dhambini Adamu wa mwisho yaani Yesu Kristo alipojaribiwa na ibilisi
jaribu la kwanza lilikuwa ni chakula pia
Mathayo 4;3-4, nguvu za Roho wa Mungu zinapatikana kwa mtu ambaye hatiwi chini
ya chakula 1 Koritho 6;12 Luka 4;1-2,14 chakula nmdicho kinachoweza kumfanya
mtu aibe, afanye uasherati ,atoe au kupokea rushwa na kufanya dhambi nyinginezo kwa msingi huo
kushinda jaribu la kula ni kuwa kama Yesu
na ni kumshinda shetani na kupata
nguvu za Roho wa Mungu Yesu hakutiwa
chini ya uwezo wa chakula ,Pamoja na kuletewa chakula na wanafunzi wake
aliendelea kuifanya kazi ya Mungu bila
kula Yohana 4;6-8,31-34
3.
Kufunga
ni kuomboleza mathayo 9;14-15
Mtu huomboleza baada ya kuondokewa na
mtu ampendaye na huwezi kufurahia
kunywa na kula 2samuel
1;11-12,3;31-35,37-38 Yesu tumpendaye hayuko nasi kimwili ,tunaomboleza kwa
kumkosa na kumtafuta katika maombi, na tunapompata katika maombi ndipo furaha
yetu inapotimilika , aidha pia kwa sababu yaq maangamizo yatakayowapata ndugu
zetu au sisi kama tumefanya dhambi
tunaomboleza na kutamani kuwa huru kumbukumbu 9;18-19
4.
Kufunga
ni kujinyenyekeza mbela za Mungu
1Falme
21;27-29,Ezara 8;21.luka 14;11 na yakobo 4;9-10 kufunga ni ibada kwa Mungu ni
ishara ya kutafuta kunyenyekea na ni kujinyenyekeza kwa Mungu hii ni kwa
sababu kula na kunywa ndiko kunakoleta
kiburi cha uzima hata awe mbali na mungu
na kuwasahahu hata watu wengine , kushiba na kusaza kunamfanya mtu aone kwamba hana haja ya kumtafuta Mungu
kumbukumbu 32;13-15 Isaya 22;13 mtu anapokuwa amefunga kiburi cha uzima
kinanyonywa na anajifunza kumtumainia
Mungu katika udhaifu wa mwili.
5.
Kufunga
ni kwa ajili ya afya zetu
Maandiko na
kitaalamu inashauriwa na kupendekezwa kuwa ni muhimu sana kufunga pia kwa ajili
ya afya zetu Mungu alipoweka mpango wa kufunga na kukataza mambo kadhaa wa
kadhaa hakufanya hayo kwa ajili yetu lakini zaidi sana kwa ajili yetu
SOMO
namba 3; MUDA WA KUFUNGA
Tunaendelea na mafululizo wa masomo yahusuyo kufunga na sasa tunaliangalia somo namba tatu ambalo
tutalichambua kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo
·
Aina
mbili za wito wa kufunga
·
Muda wa
kufunga
·
Vizuizi
vya nguvu ya kufunga
Aina mbili za wito wa
kufunga
Kuna aina mbili za wito wa kufunga
ambazo mtu aliyeokoka anapaswa kuzishiriki
1. Kufunga
kunakotokana na mbiu ya kufunga
2Nyakati
20;3-4,Yona 3;7-8 na Ezra 8;21 Huku ni kufunga kunakotokana na mbiu inayoweza
kulatwa kwetu na kiongozi wetu wa
kanisa au taifa n.k kiongozi
anapolieleza kanisa kwamba lifunge kwa
siku kadhaa kwa ajili ya jambo fulani na kisha kukutana mahali fulani kwa ajili
ya kilele cha maombi hiyo ni mbiu ya kufunga
na inaweza kutanga zwa aidha na kiongozi wa kundi la maombi au shemasi
wqa eneo husika viongozi wa zone au section
kwaya ,vijana ,wamama n.k.kiongozi atatelezea sababu ya kuitisha mbiu
hiyo ya kufunga na kama watu wana shiriki inaleta baraka kwa jinsi ambavyo
inajumuisha watu wengi kwa pamoja kwani Biblia inasema wawili wenu ama watatu
wakipatana katika jambo lolote watakalomuomba Baba wa mbinguni watatendewa Mathayo
18;18-20
2.
Kufunga
kunakotokana na uamuzi Binafsi
Katika maisha
binafsi ya mtu aliyeokoka ni muhimu kujipangioa muda wa kuwa na vipindi vya
kufunga na kuomba ili kujichotea baraka mbalimbali kutoka kwa Bwana ,kama kila
mmoja anavyoweza kujipangia muda wake binafsi wa kuomba bila kungojea maombi ya
kikanisa basio hali kadhalika ni muhimu kujipangia siku za kufunga na kuomba
binafsi , na tutaweza kuiomba kwa ajili nya mahitaji BINAFSI na mahitaji ya
kifamilia kanisa na kazi ya Mungu
Muda wa kufunga
Je ni muda gani unaofaa kwa kufunga? Biblia
haiweki muda maalumu wala sheria juu ya siku za kufunga kwamba ziwe ngapi
lakini tunapoangalia vipindi vinavyotajwa katika Biblia kuhusu kufunga basi
tutajifunza mambo kadhaa ya msingi , mifungo mingi inayotajwa katika Biblia
haiweki siku za kufunga lakini
tutaangalia hapa ile inayotaja siku za mfungo na sababu za kufunga
MUHUSIKA KUFUNGA
|
KIPINDI CHA KUFUNGA
|
SABABU ZA KUFUNGA
|
MAANDIKO
|
1.Daudi
|
Siku 1
|
Kuomboleza
kwa ajili ya aliyekufa
|
2samuel 3;35
|
2. Israel
|
Siku 1
|
Kumuuliza
bwana kwa ajili ya kushindwa vita
|
Waamuzi 20;24-27
|
3.Daudi
|
Siku 1
|
Kumlilia
aliyekufa
|
2samuel 1;12
|
4.Yuda
|
Siku 1
|
Kuutafuta uso
wa Bwana
|
Nehemia 9;1-4
|
5.Yuda
|
Siku 1
|
Kuutafuta uso
wa Bwana
|
Yeremia 36;6
|
6.Farisayo
|
Siku 2 kwa kila juma
|
Sababu za
haki za kudini
|
Luka 18;9-12
|
7.Israel
|
Siku 1
|
Kumlilia Bwana
waokolewe na wafilisti
|
1samuel 7;6-14
|
8.Esta/Mordekai
|
Siku 3
|
Kumuomba
Mungu kwa ajili ya taifa la kiyahudi huko uhamishoni wasiuawe
|
Esta 4;13-16
|
9.watu wengi
|
Siku 3
|
Siku tatu
kusikiliza mafundisho ya Yesu
|
Mathayo 15;32
|
10.Paulo
|
Siku 3
|
Wokovu na
wito wa paulo
|
Matendo 9;9
|
11.Daudi
|
Siku 7
|
Kumuombea
uhai mtoto wake
|
2samuel 12;16-18
|
12.Israel
|
Siku 7
|
Kuomboleza
kifo cha sauli na wanae
|
1samuel 31;13
|
13. Paulo na watu 276
|
Siku 14
|
Kwa ajili ya
safari iliyojaa misukosuko
|
Matendo 27;33,37
|
14.Daniel
|
Siku 21
|
Kumuomba
Mungu kwa ajili ya Taifa baada ya
kufunuliwa neno
|
Daniel 10;1-3
|
15.Musa
|
Siku 40
|
Kuketi
mlimani mbele za Mungu na kuombea Israel
|
K/Torati 9;9.18.25-29.10;10
|
16.Yoshua
|
Siku 40
|
Kuketi
mlimani mbele za Mungu
|
Kutoka 24;12-15
|
17.Eliya
|
Siku 40
|
Safari ndefu
baada ya chakula maalumu
|
1falme 19;5-8
|
18. Yesu
|
Siku 40
|
Kuongozwa na
Roho ili kujaribiwa nyikani
|
Mathayo 4;1-2
|
Kutokana na Jedwali hilo hapo juu
tunajifunza mambo ya msingi yafuatayo;-
1. Kipindi
cha kufunga katika kumtafuta Bwana kwa maombi kinapaswa kiwe sio chini ya siku
moja yaani saa 24
2. Kipindi
cha kawaida cha mfungo kinapaswa kuwa siku tatu nzima ni katika hali ya uzito usiokuwa wa
kawaida ndipo tunazidisha hapo tena kwa
muongozo wa Roho Mtakatifu na hata ikiwa
hivyo basi hazitazidi siku saba
3. Kufunga
siku zaidi ya saba ni lazima kuambatane
na kufunuliwa Neno,Daniel,Musa ,Yoshua ,Yesu na Eliya walikuwa katika hali ya
kupokea ufunuo wa Neno la Mungu na kwa ajili ya taifa na ulimwengu kwa msingi
huo mtu hawezi kufunga siku 40 bila kula na kunywa kama hakuna muongozo maalumu
wa Roho Mtakatifu yeye anapoongoza ndipo
inapotokea neema maalumu kukuwezesha kufanya hivyo 1falme 19;8
Vizuizi vya nguvu ya kufunga
1. Nia
ya kufunga Warumi 12;2 Nia yako ya kufunga ni ya muhimu sana kuliko hata
kufunga kwenyewe ikiwa nia yako haiku sawa na neno la Mungu itazuia upatikanaji
wa nguvu itokanayo na kufunga
2. Kufunga
katika dhambi Yeremia 14;10-12,Isaya 58;3-5 dhambi huzuia maombi na nguvu
itokanayo na kufunga kwa msingi huo toba ni ya muhimu sana kabla ya kuingia
katika mifungo
3. Kufunga
Bila kuomba 2Nyakati 20;3-4,Ezra
8;21,Mathayo 17;21 Kufunga mara nyingi ni lazima kuambatane na
kuomba kama unafunga kisha unapoteza
muda katika shughuli nyinginezo basi nguvu itokanayo na kufunga hutaiona
4. Kufunga
hakupaswi kuchukua nafasi ya imani. Ni muhimu kufahamu kuwa kufunga ni ibada
kwa Mungu na huchiochea imani lakini hatupaswi kufikiri kuwa kila jambo
jhaliwezekani mpaka tufunge kwanza pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu
waebrania 11;6,yakobo 1;6 kufunga kunachochea imani tu na sio sababu ya
kumlazimisha Mungu kufanya jambo.
Ahsante
JibuFutaTuendelee kujifunza neno la Mungu ili tukue kiimani
JibuFutaAsante sana , nimebarikiwa sana
JibuFutaUbarikiwe sana๐๐
JibuFutaNimeona mafindisho Mazurie
JibuFutaNimebalikiwa sana
JibuFuta