Jumapili, 31 Januari 2016

NIKAPATA SIMU KUITWA KITUO CHA POLISI


Naamini ya kuwa kisa hiki kilichonifundisha mimi somo muhimu kitakufundisha na wewe hususani kijana mwenzangu, Naitwa Didas Kibonye mkazi wa Yombo mjini Dar es Salaam, ilikuwa mwaka 2000 wakati huo ndio nikiwa nimeanza kujitegemea , nikiwa ninaishi nyumbani kwa mama yangu pamoja na dada zangu wawili  ambao walikuwa wanafanya kazi pia. 

Tamaa ya Maisha na kutokujikubali huwaponza wengi


Nilikuwa wakati huo nahaha sana na wanawake yaani mpenda wana wake sana , wakati huo nilikutana na msichana mmoja matata sana , Nikisema matata nina maana zote tu, alikuwa ni msichana mzuri kwa sura , mtanashatisana aliyependa kulka vizuri na pia kupenda vitu vizuri, kwa ufupi alikuwa ni wasichana ambao huitwa sista du, Hta hivyo kwa upande wangu mimi nilikuwa ni brazameni kwa hiyo nikisema Brazameni na sista du nina maana ya watu wanaopenda kujionyesha  kwa nje kwamba wana hali nzuri sana na mafanikio  makubwa sana  katika mambo mbalimbali wakati hali halisio siyo kweli, ni watu ambao wako tayari kuazima gari wakaonekane nalo mahali, au waazime simu ya bei mbaya sana wakaonekane nayo mahali mradi tu waonekane kwamba wanaweza kumiliki  vitu hivyo vya thamani kwa kifupi ni watu wasiojiamini kabisa , kwa hiyo mimi na huyu sista tulikuwa wa kada hiyo.

Tulianza uhusiano wetu kwa fujo na mkwara mzito sana  kwa kuwa nilikuwa nakula na kuoga na kupiga mswaki nyumbani basi kamshahara kangu kalikuwa hakana kazi kwa hiyo mtoto alijua kabisa kwamba amefika kwa mwenye mali name sikutaka kujivunjia heshima au kujishusha  kwa hiyo nilijitahidi kutoa. Tuliendelea kwa miezi kama mine hivi kabla binti hajkaanza kudai apate mkufu wa dhahabu nzito kidogo kwani ule wake ulikuwa ni wa gramu tano tu, kama ningepata walau wa gramu 15 ingekuwa nafuu sana Nilimwambia atulie tu atapata mkufu, nilijua mkufu aliokuwa anautaka kwa wakati ule ungegharimu kiasi cha shilingi 150,000, kwa kuwa nilikuwa na uhakika kuwa nisingeweza kuupoata hadi baada ya miezi saba labda baada ya kudunduliza, niliona labda niombe mkopo pale ofisini, lakini kumbe kutokana na muda wangu kazini sikuwa naruhusiwa kukopa, siku moja wakati niko nyumbani, dada yangu mkubwa alisahahu mkufu wake sebuleni, ulikuwa mkiufu wa nguvu hasa kama gramu ishirini au zaidi, Niliona Mungu akikupa hakugusi, bali hukuonyesha kinamna, Niliuchukua mkufu ule na kutokomea nao gizani.Dada alilalamika sana  alipobaini kuwa ameibiwa mkufu. Mkono wa lawama na tuhuma ulimwelekea hausigeli na mtoto wa mjomba wangu tuliyekuwa tukiishi naye pale nyumbani, nilijua nimeokoka, kwakweli mkufu ule ulifanya msichana wa kazi kupoteza kibarua chake.

Siku zilipita huku Yule hawara yangu akiamini kwamba simba au Dume lake limemnunulia mkufu ule na ilipita miezi sita. Siku hiyo nikiwa ofisini nikapigiwa simu kwamba niende kituo cha polisiMsimbazi, nilipouliza kulikoni niliambiwa kuwa Dada yangu mkubwa ana tatizo niliomba ruhusa ofisini  na kwenda kwenye tukio.Kufika nilimkuta dada pale kaunta na Yule hawara yangu, huku hawara yangu akilia , Nilipoona hiyo hali kumbukumbu za mkufu ilinijia haraka , kabla sijauliza ,dada aliniuliza  ulimpa huyu mwanamke mkufu wowote? Nilikuwa natetemeka, Maafande kadhaa na raia waliokuweko kaunta walinikodolea macho, kwani vipi mbona sielewi nasikia mkufu, wengine wanalia kuna kitu gani? Nlijifanya mtoto wa mjini afande mmoja aliingil;ia kati jibu swali bwana tuna kazi nyingine za maana , Nilinywea na kusema ndio kwani vipi! 

Dada yangu aliulizia uliutoa wapi mkufu huo? Niliona sina njia kama ninataka kutokuyakuza mambo Si ule mkufu wako ushasahau sista vipi? Dada yangu alikuwa na busara na alikuwa ananijia Pengine kwa kumtazama tu Yule msichana alijua kuwa nilikuwa naendeshwa puta, Afande naomba nipewe mkufu wangu tukayamalize nyumbani, Bila shaka afande Yule alikuwa anamfahamu dada kwani alimtaja kwa jina  na kumwambia sawa hakikisheni mnayamaliza yasirudi hapa,Halafu alicheka . Tulitoka kituoni kufika pale nje tu nilipokea matusi ya kumwaga kutoka kwa Yule hawara yangu matusi ya nguoni, kwenye kaptura, kwenye gagulo yangu ya mama na baba na ukoo mzima kwa ujumla. Kumbe mkufu ule ulikuwa na alama maalumu ya dada ambayo mgeni nao asingeweza kuijua, alimfuma Yule msichana akiwa saluni ndipo walipochukuana Polisi baada ya msichana Yule kuleta nyodo alipokuwa akihojiwa, wiki ileile ilibidi nihame kutoka nyumbani kutokana na aibu, ingawa hakuna aliyekuwa akinizonga, yake macho yao tu  yalivyokuwa yakinitazama ilikuwa kama vile wanapiga kamera kila kiungo changu cha mwili huko ndani, Watanzania bwana najua umekodoa mimacho ukitaka kujua tulimalizana vipi na Yule hawara yangu hiyo hainihusu mimi tena utajijua mwenyewe!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni