Jumanne, 26 Januari 2016

Nikaalikwa Kama Mtoto wa Waziri!



NIKAALIKWA KAMA MTOTO WA WAZIRI

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 34. Malezi na makuzi yangu yalikuwa ni ya wale wazazi ambao kwa siku hizi wangeitwa machekibobu, hawa ni wazazi ambao wanataka kujionyesha  kwa watu wengine kwamba  wao ni watu wenye fedha ,waliotoka kwenye familia bora, waliosoma sana  ingawa sio kweli kwa hiyo name nilikuwa mtu wa aina hiyo mpaka niulipofunzwa na dunia.

Kwa ujumla ni kama nilifundishwa kujikataa kwamba siyo mimi na nilimudu sana kujikataa kwani katika kukua kwangu name nimekuwa mtu wa kujikweza mwaka 2000 ni kiwa nimemaliza masomo katika chuo cha biashara nilipata kibarua kwenye ofisi binafsi katika eneo la viwanda vingunguti nilianza kazi hapo nikiwa kama karani wa kawaida tu wa kutumwa shughuli za hapa na pale kujaza fomu za hesabu za fedha na mengine ya aina hiyo

Wakati nikiwapo hapo kazini nilikutana na msichana mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi kampuni ya jirani, nilikutana na msichana huytu wakati wa chakula cha mchana Lunch hapo eneo la viwanda. Kwa keli nilimpenda sana ghafla, yaani jicho la kwanza. Lakini Mungu si Athumani naye alionekana kunipenda ghafla pia, tulijikuta tukiwa marafiki baada ya mimi kumuanza ingawa kiuoga uoga kwani alikuwa mzuri sana na pia alikuwa anamiliki usafiri aina ya Rav4 ya milango mitatu, nilipochokoza alikubali kirahisi tofauti na nilivyotarajia

 Rav4 ya Milango mitatu

Kama kawaida yangu katika kujitambulisha mimi nilijitambulisha kwa  kujilambisha ujiko wa ajabu sana, mimi ni mwenyeji wa Tanga  na baba yangu anajuana na mtu mmoja mkubwa serikalini ambaye hadi sasa ni waziri. Badala ya kusema ukweli kuhusu baba yangu ambaye kwa maisha ya kichekibobu kama yangu alikuwa amesha chalala sana nilimtaja mkubwa huyo

Yule binti aliniamini na huko nyumbani alitangaza bila shaka kwamba amepata mtu ampendaye ambaye baba yake ni mtu Fulani, siku hiyo binti alinialika niende nyumbani kwao kwaajili ya chakula cha mchana ilikuwa ni jumapili, nilijitahidi sana hadi nikamudu kukodi gari ya rafiki yangu kwa shilingi 40,000 ili niendenalo mwenyewe kule wajue kwamba nina gari unajua kitu gani kilitokea?

Nilipofika nyumbani kwao Yule binti nilimkuta mama yake, baba yake alikuwa amefariki zamani, lakini pia nilimkuta mtu mwengine, Hebu otea alikuwa nani? Alikuwa ni baba yangu, Nilibabaika sana  na kujiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu nilipigwa na butwaa kwa muda na baba baye pia, nilimsalimia mama wa binti yuile na baadaye kumsalimia baba na kumuuliza uko huku? Baba alisema nashangaa nawe unaijua familia hii Mama Lewisi tulikuwa naye kazini zamani. Siku nyingi sijamtembelea leo ndiyo nimeamua kuja kumwona….” Yuel mama mkwe wangu mtarajiwa aliuliza kwani mnajuana? Baba alisema huyu ni mwanangu wa kwanza” Halafu palizuka ukimya Yule mama kwaajili ya kuua soo alinikaribisha lakini ghafla Yule binti alikuwa amebadilika hakuwa na furaha tena.

Tulikula, lakini katika hali ya undavaundava tu, tulipomaliza  kula sikutaka kukaa zaidi kwani nilijua kuwa binti Yule na mama yake walikuwa wakinisanifu sana , du kutoka kuwa mtoto wa waziri hadi kuwa mtoto wa mzee aliyechezea maisha siku za nyuma, mbaya zaidi ni kuwa baba alikuwa amefika pale kwa nia  ya kuomba msaada, Niliaga nikimwacha baba akiendelea kupiga mabomu yake. Nilikuwa na uhakika kuwa baba aliambiwa ishu zangu zote, kwani jioni alinitembelea kwangu na kuniambia kwamba nimejisanifu sana kwa kujifanya mtoto wa waziri Unataka niendelee kukusimulia? Unataka kujua kuwa niliendelea na urafiki na Yule demu au La au nilitoa pua yangu kwa mama mkwe mtarajiwa? Hivi kichwa chako kiko sawasawa?

Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni