Jumanne, 26 Januari 2016

Wakurugenzi wakaniita!



WAKURUGENZI WAKANIITA
Sikumbuki tarehe wala mwezi lakini ilikuwa mwaka wa 1990 wakati huo nilikuwa nimeachishwa kazi katika kiwanda kimoja cha viatu, kilichokuwa barabara ya Pugu siku hizi Nyerere, nilikuwa nafanya kazi pale kama mlinzi mwaka huo ndio nilipata skendo na kuachishwa kazi 

 Kiwanda cha Viatu Pugu

Nikawa nahangaika kutafuta kazi mjini, Nilifanikiwa mwaka huohuo kukutana na mtu ambaye alisoma na ndugu yangu, huyu Bwana aliamua kunisaidia kupata kazi mahali, aliponiuliza kuhusu elimu yangu nilimwambia nimemaliza kidato cha sita, ingawa ukweli ni kwamba nimesihia darasa la saba, Alinifanyia mpango nikapata kazi kwenye kiwanda kimoja hapohapo barabara ya Nyerere.Nilitafuta vyeti vya bandia  kutoka kwa rafiki yangu ambaye wakati huo alikuwa chuo kikuu, niliajiriwa kama karani waupokeaji wa mali ghafi na udhiinishaji wa  utokaji wa bidhaa, ilikuwa ni nafasi kubwa sana hata kwa mtu wa kidato cha sita, hata hivyo kwa sababu ilikuwa ni kazi yenye kuhitaji tu maelekezoili mtu kumudu kuifanya  niliielewa  kwa kiasi.


Bahati mbaya mwezi wa kwanza tu wa kazi , nikaanza kwa unoko sana, nilikuwa najifanya najua na nikawa nawazibia watu riziki zao, ili nipendwe na wenye kampuni, Kumbe katika unoko huo huo ,taarifa za kwamba mimi ni darasa la saba  na niliwahi kupata skendo zilifika pale kazini, Siku  hiyo nafika kazini kama kawaida , nikaitwa kwa mkurugenzi. Nikajua kuwa ninaenda kumwagiwa misifa kutokana na utendaji wangu wa kazi, kufika mkurugenzi akaniambaia, “tulikuajiri tukiamini kwamba kila ulilolisema kwetu lina ukweli, Hebu hasa jina lako na kiwango chako cha elimu na wapi uliwahi kufanya kazi kabla ya kuja hapa”

Nilihisi moyo ukianza kudunda kwa kasi na kwa nguvu, Nilijikaza na kusema  sijafanya kazi popote, tangu nimemaliza masomo ya kidato cha sita mwaka juzi, na jina langu ndilo hili ninalotumia, Wakurugenzi waliokuwa wamenizunguka walitabasamu kwa dharau hadi nikaogopa “Sasa bwana kuna mawili ama tukupeleke polisi sasa hivi kwa kudanganya na kufoji vyeti na jina la mtu  ambalo si lako au uondoke sasa hivi bila hata kipande cha karatasi yaani kama ulivyokuja , Hatuna haja ya kubishana nawe kwa sababu unaujua ukweli wote kuliko sisi”  Mkurugenzi mkuu alisema, Yule jamaa aliyenifanyia mpango wa kazi naye alikuwepo kwenye kikao kile , “Umeniangusha sana sikutegemea kabisa, kumbe hata sekondari hujakanyaga unakwenda kujipachika ufomu six wa bure! Kwa kweli hata tukionana njiani usinisalimie kabisa, Ungenisababishia kuharibu kazi yangu bure” Aliniambia.

Nilimwambia nimekosa nitaondoka sasa hivi na sitaki chochote, Nilijivuta polepole na kuanza kutoka nje, huko nje kumbe wafanya kazi wengine  walishapata  taarifa, kwa hiyo nilipokuwa nikikatiza mitaa walikuwa wakinicheka  na kunizomea , sikujibu chochote  kwa kweli ilikuwa fedheha  ya mwaka  unataka kujua nini kiliendelea we bwege nini? Mbona unapenda sana umbeya kwa taarifa yako sasa tukio hili lilinifanya niende kujisomea kwa machungu nikamaliza kidato cha sita na sasa nina stashahada ya uhasibu. Ilikuwa fedheha ambayo ililipa!.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni