Jumanne, 26 Januari 2016

SI KILA MWANAMKE AMEKUJA KUCHEZEWA HAPA DUNIANI.



Siku hizi huwa nashindwa kujiuliza sana kuhusu maisha, najiuliza kuhusu watu kushindwa kuwajibika kwa matendo yao na maisha yao kwa ujumla, Maswali haya najiuliza baada ya kujifunza kupitia uzoefu mmoja  na ambao ningependa kuushiriki na wengine leo hii 

Ilikuwa mwaka 1995 nilikuwa nimepata uhamisho kutoka wilayani mpanda  kuja Dar ni lazima niwe mkweli kwamab siku hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza  kuja dar kuishi mara nyingine kama mbili tatu hivi nilikuwa napita  tu kiofisi, nakuja ofisini kwetu na siku ya pili narudi mkoani, Nilipofika nilitafuta nyumba na kupata katika maeneo ya mwenge,  sikuja na familia yangu kwa sababu ilinibidi kuja kutafuta nyumba kwanza  na kasha familia yangu  ifuate baada ya kuhakikisha kuwa nimepata nyumba , nikiwa bado mgeni wiki ya pili tu, niliotoka siku moja kwenda kutembea  na kunywa kidopgo, wakati huo tulisha kubaliana na familia yangu  kwamba wajiandae na kuja Dar baada ya wiki mbili.


Siku hiyo nilikwenda kutembea katika baa moja maarufu wakati ule pale Mwenge-Sinza najua unanielewa vema kama unaipata vilivyo mitaa na vitongoji vya Dar ilivyo na utata kubainisha , Basi wakati nakunywa akatokea  dada mmoja akanizoea palepale.Kule kwetu Mpanda mwanamke kukuzoea haraka ni lazima  awe anakupenda hasa kwa hiyo nilitafasiri kuwa huyu dada kanizimia haswa tulikunywa naye na kuzoeana usiku huo huo.

Hatimaye nilikwenda naye kwangu na kupitisha usiku naye kiibilisi, kosa namba moja likawa hili, nilimwambia kwamba sijaoa, kwa ushamba wangu nilidhania kumwambia msichana  wa Dar kwamba nimeoa ingekuwa ni kujiangusha sana kwa hiyo Yule changudoa ambaye mimi nilimuona kuwa mwanamke wa maana sana  baada ya kunidanganya kwamba anafanya kazi ubalozini na ametokea kunipenda, kusikia sijaoa nadhgani alijua amejipatia bwana, kwa sababu hiyo akawa amepata pa kulala , Zile pesa zangu za uhamisho nilianza kuzimwaga  kwa matumizi ya kijingakijinga. Nilikuwa sijui mambo ya bilicanas au FM, nikayajua kupitia kwake Ilibidi mke wangu anishitue akiwa ofisi ya basi pale Kariakoo, Nilikuwa nimekwisha sahau kabisa hata kuhusu kuja kwake, nilifanya utaratibu wa kwenda kumpokea, kwa habari ya yuel changudoa nilishindwa kumjulisha kuhusu ujio wa familia yangu, nilitaka nimfahamishe kwamba mke wa kaka yangu na watoto wamekuja na hivyo itabidi tusikutane nyumbani kwanza kwaajili ya kulinda heshima.

Lakini ningempata wapi? Mtu anakwambia anafanya ubalozini ukimwambia nipeleke anakwambia anafanya hazina , ukimwambia nipeleke ofisini kwako  anabadilika na kukwambia kuwa yuko Usalama wa Taifa, aha Niliamua kwenda kwanza kituoni  kuwachukua watu wangu, nilifika kituoni  na kukuta pamoja na mke wangu na watoto wawili alikuwemo mama mkwe wangu, niliwachukua na kuwapeleka nyumbani Mwenge muda ulikuwa ni kwenye saa tano asubuhi siku ya jumapili, Nilimwambia mke wangu kuwa ninaenda kazini, kuna kazi maalumu huko, niliondoka  kwenda  kumsaka Yule changudoa lakini sikuweza kumpata . Ilibidi nirejee nyumbani na kuamua kwamba , nikisikia hodi tu  nitakuwa wa kwanza  kwenda mlangoni ili kuuwa soo hukohuko,Ni kweli jioni  iliingia  na usiku ukaingia  kwenye saa mbili hivi wakati tunakula  ndiyo ikatokea  Mlango mkubwa ulikuwa umesindikwa tu kama unavyojua  watu wa Bushi kufunga milango kwao sio Issue, Ghafla tuliona mlango ukifunguliwa na mwanamke aliingia, Mwanamke Yule akiwa  amelewa alipiga kelele “Haroo daring izi faini yuu welikamu” Halafu alikuja pale mezani  na kuniinamia  na kunibusu. Kumbe una wageni daring wangu mbona hujasema ndiyo maana sikukuona sehemu sehemu…’ Ehee Hebu tulia bwana wewe unaona kuna wageni halafu unaanza kuleta fujoi zako, Huyu hapa ni mke wangu hawa ni watoto wangu na huyu ni mama mk…” Nilisema kwa kelele.

Alinikatisha karibu mke mwenzangu mimi pia ni mke wa huyu bwana tulikuwa hatujuani…” Niliinuka kutaka kuangusha kipigo lakini kabla sijarusha ngumi au kibao nilijikuta niko chini Mke wangu ni wale ambao hawakuja duniani kuchezewa na wanaume. Alimvaa  changudoa Yule  na kushughulika neye vilivyo kuna kupigwa na kusuuzwa, Yule changudoa alisuuzwahaswa, ilibidi mama mkwe aingilie kati na kumsihi mwanawe aache  vurugu, changudoa Yule alitumia nafasi hiyo kuiona njia  kwa kukurupuka kama guruwe pori  lililokoswakoswa mshale, huku akisema tutaonana, kasha ikafuata zamu yangu nakwambia mkioa muwe mnatazama vizuri kuna wanawake wengine bwana wakikasirika, wana kuwa kama nyati majeruhi, Kama isingekuwa kelele za ‘Mama unamuua baba‘ ya watoto na mama mkwe  kuingilia kati apigwe yeye badala yangu  huenda ningefikishwa Muhimbili kitengo cha kuunga mifupa MOI nikiwa unga wa dona.  Najua ungependa niendelee sawa si unapenda kuona wengine wakiadhirika ili upate nyuzi ehe! Ngoja yaje kukupata hutakuwa na hamu hata ya kusikiliza ya wenzio!.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev Innocent Kamote

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni