Jumatatu, 1 Februari 2016

SINA KITU SASA LAKINI NINA CHA KUKUMBUKA!


Ndugu wawili walipanga kuwa na safari, na siku moja jiono waliamua kujipumzisha katika moja ya misitu mikubwa, walipokuwa wakiangalia huko na huko humo waliona jiwe lililokuwa na maandishi yafuatayo;-




"Ulimwengu wa Mafanikio uko na wale wanaothubutu"

Yeyote atakayeliona jiwe hili” walilisoma “ na aingie moja kwa moja msituni wakati wa jua kupunga yaani jioni, Ndani ya msitu mto utatokea ogelea mto huo mpaka ufike upande wa pili, hapo utaona gari zuri na ufunguo wake endesha gari hilo mpaka kwenye kilele cha mlima bila kuangalia nyuma, utakapofika mlimani utaona nyumba na ndani ya nyumba niyo Utapata furaha kuu” walipomaliza kusoma habari hii katika jiwe Kaka mdogo akasema Kaka tafadhali twende….. tunaweza kuogelea na kuuvuka mto huu na kuchukua gari na kupata nyumba na huko mlimani tutaipata furaha kuu!

Sitakwenda sitaingia msituni na kuogelea sita vuka huko alisema Kaka mkubwa na kisha akamsahauri nduguye, “fikiria labda yaliyoandikwa humu ni fumbo, au labda tunaweza kuwa hatujasoma sawasawa, au tumesoma na hatukuelewa, na hata kama yaliyoandikwa hapa ni kweli jaribu kuwaza kama tutavuka na tusiuone mto au kama tunaweza kuuona na tukashindwa kuogelea  au kama tutaogelea na kuvuka nay ale yaliyoahidiwa upande wa pili yakawa hayako na badala ya kupata furaha kuu, tukajikuta tunaangamia, tutawezake kuupanda mlima bila kupumzika wala kugeuka nyuma inawezekana ile furaha kuu tunayoitazamia ikawa ni msiba mkuu sana kwetu

“Kwa maoni  yangu” alisema kaka mdogo “Hauko sahii” Yaliyoandikwa katika jiwe hili hayangelikuweko hapa pasipo sababu, Na ni wazi kwamba Hakuna madhara yanayoweza kutupata endapo tutajaribu kama tutajaribu, aidha kwa upande mwingine kama hatutalifanyia kazi hili kuna mtu mwingine atasoma na kulifanyia kazi yaani haya yaliyoandikwa kwenye jiwe na atapata furaha kuu, sisi tutapoteza na mimi sitaki tupoteze nafasi hii”

Kaka mmkubwa alijibuna kusema kuna mithali isemayo “ Mtaka cha uvunguni shurti ainame” yaani katika kutafuta furaha kuu tutapata majaribu na maumivu, na pia mithali nyingine inasema “Ndege aliye mkononi ni bora kuliko wawili walioko Porini” Kaka mdogo akajibu na kusema nimesikia Basi yeye anayeogopa asiingie msituni, Basi kaka mdogo akaingia msituni na kuanza safari na mkubwa akabaki nyuma, ndugu mdogo aliingia msituni usiku na akauona mto uliokuwa umeelezwa, akaogelea na kuvuka nga’mbo na akaiona gari na ufunguo wake na kuingia na kuiendesha  akapanda mlimani bila kuangalia nyuma alienda kwa muda mrefyu na hatimaye aliiona nyumba, kaka mkubwa alirudi nyumbani.

Aliingika katika nyumba ile na kuikuta iko vizuri sana imeandaliwa vema na alipoingia mara kundi kubwa sana la watu wakaja kumpokea kwa ujasiri, wakamkaribisha katika mji wao wakampaka mafuta na kumtawadha kuwa Mfalme wao akaishi kwa furaha kuu akitawala kwa miaka mitano, mwaka wa sita aliinuka mtawala mwingine wa mji mwingine mwenye nguvu na wakafanya vita na ufalme wake na katika vita ile mfalme huyu alishindwa na kila kitu kilitawaliwa na Yule mfalme mwenye nguvu, kwa kuwa hakuuawa aliamua kurudi kwa kaka yake

Kaka yake alikuwa akiishi kijijini na hakukuwana mabadiliko yoyote katika maisha yake hakuwa tajiri wala masikini aliishi kawaida tu, Kaka mkubwa alifurahi kumuona ndugu yake wakakumbatiana kwa furaha hasa kwa kuonana katika maongezi yao Kaka mkubwa alimwambie ndugu yake unaona nilikuambia nilikuwa sahii mimi nimeishi kwa raha mustarehe japo maisha yangu yalidumaa niko vilevile, wewe umerudi duni ingawa ulikuwa mfalme na umekutana na taabu kubwa sana na vita  kaka mdogo alijibu, “Sijutii niliyokutana nayo nimevuka mto na nimepanda mlima, nimekuwa mfalme na nimetawala inawezekana nimerudi nikiwa sina kitu sasa lakini nina cha kukumbuka na kuelezea watu wewe huna cha kuelezea wala cha kukumbuka” – wise man Leo Tolstoy interpreted by wise Master mason Rev. Innocent Kamote.

"Ulimwengu wa Mafanikio uko na wale wanaothubutu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni